MASTAA 5 WALIOLELEWA NA MACHANGUDOA
1. LOUIS HAMSTRONG
Huyu alikuwa mwanamuziki mwenye jina kubwa miaka ya 1960. Alikuwa mpigaji mzuri wa tarumbeta na pia mtu wa voko. Alitamba na muziki wake wa Jazz.
Huyu mwamba alizaliwa huko New Orleans. Mama yake na dada yake waligeukia biashara ya kujiuza ili kupata pesa ya kutumiana familia. Walikamatwa mara kwa mara na kuna wakati mama yake alikamatwa, akatozwa dola 2.50 akashindwa kulipa na hivyo kufungwa gerezani kwa siku 30.
2. CHARLIE CHAPLIN
Mama yake Charlie aliyeitwa Hannah aliondoka na mpenzi wake kwenda Afrika Kusini ambapo huko akalazimishwa kufanya biashara ya kuuza mwili wake.
Akiwa kwenye biashara hiyo mara kwa mara aliugua magonjwa ya kaswende. Baadaye aliugua magonjwa ya akili. Akiwa na miaka 35 tu alichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo cha kulelea watu wasio na akili hivyo kumuacha Charlie akiendelea kukua na kuwa mtoto wa mitaani.
3. DICK ‘NIGHT TRAIN LANE’
Huyu jamaa alikuwa mcheza mpira uitwao Football ‘NFL’. Alizaliwa katika familia ya mwanamke aliyekuwa akiuuzamwili wake kwa wanaume. Alipokuwa na miezi mitatu, akatelekezwa.
Aliokotwa na mwanamke mmoja kwenye jalala akiwa amezungushiwa gazeti. Mwanamke huyo aliitwa Ella Lane.
4. EDITH PIAF
Huyu alikuwa mwanamuziki wa Kifaransa aliyevuma kwa aina ya muziki aliokuwa akiuimba na hata uandishi wake mzuri.
Huyu alitelekezwa na mama yake alipokuwa mdogo kabisa. Bibi yake mzaa mama pia alimpuuza sana hivyo kuchukuliwa na bibi mzaa baba na kulelewa. Edith alilelewa huko na machangudoa kwenye danguro mpaka alipofikisha umri wa miaka 8.
5. RICHARD PRYOR
Huyu alikuwa mchekeshaji na muigizaji wa muvi mbalimbali. Alilelewa na bibi yake kwenye danguro moja huko Marekani. Mama yake alikuwa akifanya kazi kwenye danguro hilo ila alimuacha akiwa na miaka 10.
Bibi yake alimlea lakini alikuwa mkali kwake, hakutaka aharibikiwe hivyo mara kwa mara alikuwa akimchapa pale alipokuwa akikosa nidhamu.