MAMBO SITA AMBAYO WAAFRIKA TUNAYAPUUZIA LAKINI WAZUNGU WANAYATUMIA KUFANYA MAMBO YA AJABU DUNIANI.
Kwasababu mambo haya wao wanayachukulia kama sehemu ya kuongeza ufanisi wa akili zao na kuongeza uwezo wao wa kufikiri na kujiamini.
Inawezekana itakushangaza, lakini mambo haya ambayo haujawahi kufundishwa na yeyote yule lakini unayafahamu na umekuwa ukiyapuuzia. Leo hii nakufundisha mambo sita bure kabisa ambayo yatakusaidia kuwa mtu mwingine kabisa smart sana na kuanzia sasa haupaswi kuyapuuzia tena kwasababu yatakufanya uwe mtu wa KUJIKUBALI(KUJIAMINI),HODARI, SHUPAVU na usiye na MSONGO WA MAWAZO…
1. Kujifunza kupika na kupenda kula chakula cha kujipikia mwenyewe.
Kwasababu chakula cha kujipikia mwenyewe ni kitamu sana kuliko chakula cha kupikiwa. Hata kama umeoa,siku moja jaribu kuingia jikoni na kupika. Kupika ni sehemu ya starehe na kuiliwaza akili yako. Lakini pia, kila mtu ana tabia ya kujivunia kuunda kitu kizuri. Iwapo utapika kadri unavyotaka wewe na kujiandalia chakula kitamu kwa kutumia akili, juhudi, ubunifu na uwezo wako, basi utajiongezea uwezo wa kujiamini kwa kutambua kuwa kila jambo linawezekana! Wazungu, wanapenda kula vyakula vya kujiandalia wenyewe kulinda afya zao lakini pia kupika ni sehemu ya starehe kwao. Sisi, kupika ni adhabu. Yaani mtoto wa kike au kiume aliye katika umri wa kuoa au kuolewa hata kujiandalia kahawa HAJUI.
2. Kujifunza kuendesha gari.
Kuendesha gari ni ujasiri. Sio vyepesi kupishana na magari makubwa kama wewe sio jasiri,shupavu na hodari. Lakini pia,kuendesha gari lazima utumie akili ndiyo maana matumizi ya madawa ya Kulevya kwa madereva sio salama kwasababu ni chanzo cha ajari nyingi zilizoripotiwa Duniani kote. Hivyo basi, katika kipindi cha maisha yako usiache KUJIFUNZA KUENDESHA GARI. Kuendesha gari ni sehemu ya sterehe,lakini pia ni sehemu ya kuifanyisha kazi akili yako. Kama utaweza kuendesha gari kwenye miji mikubwa yenye msongamano kama Dar es salaam basi tambua kwamba kiwango cha akili yako kinafanya kazi vizuri. Unaweza kufanya mambo makubwa kwa ustadi mkubwa! USIJIDHARAU.
Hivyo basi, kuendesha gari ni njia mojawapo ya kujiongezea ujasiri kwa wewe ambaye ni muoga na mwenye hofu sana kwenye maisha yako!
Hapo awali nilisema kuendesha gari ni starehe. Ndiyo, kuendesha gari ni njia mojawapo ya kujiliwaza lakini pia huleta furaha kwa wewe unayeendesha kuliko wewe uliyeketi kama abiria.
3. Kujifunza kuendesha Baiskeli.
Mara nyingi watu wakubwa Duniani hutumia uendeshaji wa Baiskeli kama sehemu ya mazoezi. Lakini pia, inahitaji ujasiri kujifunza kuendesha Baiskeli na iwapo utafanikiwa baada ya kuanguka mara kadhaa,utahisi furaha ya ajabu kwa mafanikio hayo ya kuweza kuendesha Baiskeli kwasababu utakumbuka namna ambavyo ulianguka na kupata majeraha kadhaa. Kujifunza kuendesha Baiskeli kutakufundisha uvumilivu kwenye maisha, kujifunza kuendesha Baiskeli kutakufundisha kuwa maisha yana tabia ya kupitia changamoto ili uweze kufikia mafanikio. Kama unajihisi umekata tamaa, nenda kajifunze kuendesha Baiskeli! UTAJIFUNZA KITU.
Kama unafahamu kuendesha Baiskeli, lakini unajihisi akili imechoka na kichwa chako kimelemewa na msongo wa mawazo. Chukua Baiskeli yako endesha kilometa kadhaa, utanishukuru!
4. Jifunze serekasi kama inawezekana!
Serekasi ni mojawapo ya vitu ambavyo ukijifunza na kuvifahamu basi utaweza kujivunia. Lakini pia, iwapo ulikuwa haujui serekasi na baada ya kujifunza kwa jitihada zako pamoja na akili zako kisha ukaweza basi kiwango cha kujiamini kwako kitaongezeka.
Kwanini? Kwasababu serekasi ni vitu ambavyo vinafanywa na watu wachache, siku zote vitu vinavyofanywa na wachache ndivyo ambavyo huibua watu hodari,mashujaa na wenye uwezo mkubwa. Kama unajua serekasi, naomba nikwambie kwamba acha kujidharau,unaweza kufanya mambo makubwa sanaa!USIKATE TAMAA.
5. Kujifunza kuogelea.
Kuogelea ni njia mojawapo ya kujistarehesha, wazungu wengi sana wanatumia njia hii kujiondolea msongo wa mawazo na kuboresha uwezo wa kufanya kazi wa akili zao. Kuwa muogeleaji mzuri lazima uwe na juhudi katika kujifunza lakini pia inahitaji uhodari na kutokuwa muoga. Kama unataka kuwa jasiri kwenye maisha usiyeogopa maisha, nenda kajifunze kuogelea. Kadri ambavyo utastahimili mawimbi ndivyo ambavyo utakuwa hodari katika kustahimili mawimbi(vikwazo) vya maisha. Hizi ndizo starehe za wazungu, achana na ngono na madawa ya Kulevya. Chagua starehe hii uwe unastopable!
6. Jifunze kujenga urafiki na “Mazingira yako”.
Jifunze kupenda kuishi kwenye mazingira mazuri, ikiwezekana nyumbani kwako panda maua na bustani yako nzuri. Jifunze kuishi Kama binadamu na sio mnyama. Penda kuishi maisha mazuri, hivyo ndivyo utakavyoushinda umasikini. Mazingira mazuri yanaanza na kupenda kuishi mazingira yaliyo Safi nyumbani. Hivyo hivyo palivyo, papendezeshe usisubili mpaka siku utakapo miliki ghorofa. Anza leo kuwa rafiki na mazingira yako. Wazungu, hupenda kutembelea mbuga za wanyama lakini pia hupenda kuwa na bustani za maua nyumbani kwao,hiyo ni kama sehemu ya kujiliwaza na kuongeza uwezo wa akili zao kufanya kazi ipasavyo. Ndiyo maana, Waafrika tunapaswa kubadilisha mitazamo yetu kuboresha maisha yetu.
Hayo ni machache jioni ya leo ambayo yatakusaidia kujistarehesha,kuondoa msongo wa mawazo kwenye maisha yako lakini pia vitakusaidia kukuongezea uwezo wa kujiamini kwenye maisha yako.
Je, ulikuwa unajua kwamba kupika,kuendesha gari,baiskeli na kuruka serekasi ni Mambo ambayo yanaweza kutumika kama starehe na kukuongezea uwezo wa kujiamini iwapo utajifunza na kufahamu Mambo hayo?KAMA ULIKUWA HAUJUI, BASI NIMEKUFAHAMISHA.