YAFUATAYO NI MAMBO AMBAYO PESA HAIWEZI KUNUNUA!
Pesa haiwezi kununua tabia nzuri au mbaya. Tabia hujengwa na mtu mwenyewe na sio kwa kutumia pesa japokuwa pesa inaweza kuathiri tabia ya mtu na sio kumbadilisha utu wake asilia wa rohoni!
2. Maadili.
Pesa haiwezi kununua maadili. Kama maadili ya mtu ni mazuri au mabaya hayawezi kubadilishwa kwa kutumia pesa. Haiwezekani kabisa kulazimisha maadili mabaya ya mtu fulani yawe mazuri kwa kuyanunua.Never! Maadili ni utu wa ndani ambao huanzwa kujengwa tangu utotoni, japokuwa ukubwani maadili ya mtu yanaweza kuathiriwa kwa kubadilika kwa muda tu kutokana na kile anachokimiliki lakini sio hali ya kudumu hutokea kwa muda mfupi tu.
3. Hekima.
Hekima hainunuliwi kwa pesa. Hekima ni uzoefu alionao mtu katika kutatua matatizo ya Kimaisha kulingana na mapito yake. Hivyo basi, yeyote yule anaweza kumiliki hekima kwa kadri ya namna ambavyo anatatua matatizo yake na ya wanajamii wanaomzunguka pasipo kujali hali yake ya kiuchumi.
4. Uaminifu.
Uaminifu ni kiwango cha ukweli alichonacho mtu. Mtu anaweza kuwa mkweli au muongo PASIPO KUJALI UCHUMI WAKE. Pesa haiwezi kukufanya uwe mwaminifu(mkweli) lakini inaweza kuwadanganya watu na kuwafanya wakuamini au wasikuamini kutokana na mazingira. Mfano, mwenye gari, cheo kikubwa, ardhi na majumba(mwenye pesa) anaweza kuaminika kukopesheka Benki,yaani watu wanamwamini kumkopesha kwasababu anaonekana ana pesa. Lakini, mtu akifa kwenye familia au mtaani katika mazingira tatanishi, huyo huyo mwenye pesa watu watakuwa wa kwanza kupoteza uaminifu kwake( wengine watasema amemtoa kafara). Pesa ina athiri uaminifu lakini haiwezi kuununua!
5.Upendo.
Pesa hainunui upendo wa kweli, kwasababu suala la upendo hutegemea utu wa ndani(nafsi). Lakini, pesa inaweza kukudanganya ukaamini kuwa watu wanakupenda kumbe hawakupendi. Kuna watu watakuchukia kwasababu una pesa lakini pia wapo ambao watakupenda kwasababu ya PESA ZAKO.
6. Uvumilivu.
Uvumilivu ni tabia ya kustahimili matatizo pasipo kukata tamaa. Pesa haiwezi kukufanya uwe na kiwango kikubwa cha kustahimili matatizo kuliko watu wengine. Hata wenye pesa wanajiua kwasababu ya changamoto za Kimaisha, hivyo basi pesa hainunui UVUMILIVU.