MAMA UNATAKA WATOTO WAKO WAKUPENDE NA WASIKUSAHAU MILELE FANYA YAFUATAYO!
1. Waambie ukweli kuhusu baba yao!
Kama ni single mother unalea mwenyewe, baba yao amefariki waambie ukweli! Kama yuko hai lakini mahusiano yenu yalivunjika,angalia namna ya kuwaambia ukweli! Unaweza kufikiri unajenga kumbe unabomoa,siku wakianza kumtafuta baba yao au kufuatilia kuufahamu ukweli wao wenyewe na wakatambua kuwa ulikuwa unawadanganya hata kama ulikuwa unafanya kwa nia njema. Watoto wako watapoteza imani na wewe! Hawatakupenda tena.
2. Usiingize mwanaume chumbani na kulala pamoja naye Kama sio baba yao wanayemjua!
Wakikufumania au kushuhudia ukifanya hivyo watakuuliza maswali magumu ambayo utashindwa kuwajibu ukweli na utawadanganya. Lakini, tambua kuwa ipo siku watajua ukweli na hapo ndipo watakapokushusha thamani, hawatakuamini tena!
Hebu soma mkasa huu…Kijana mmoja wa kiume alikuwa akitazama filamu wakati akiwa chuo kikuu. Wakati wote huo, alikuwa ana mapenzi makubwa sana na mama yake mzazi(single mother) kila siku alikuwa akiwasiliana maye kwa simu kumjulia hali anaendeleaje lakini baada ya kuona kisa kimoja wakati akitazama filamu hiyo ya Kinaijeria,mambo yalibadilika unajua ni kitu gani kilitokea? KIJANA HUYO WA MIAKA 22 ALIMCHUKIA MAMA YAKE NA KUMUONA KAMA SHETANI. Alipunguza kumpigia simu mama yake,hapo awali alizungumza naye kila siku lakini sasa wiki ilipita. Hatimaye alianza kupiga simu baada ya mwezi,baadaye aliacha kabisa kupiga simu!
Ilikuwa hivi,
Wakati akitazama filamu hiyo, mama mjane(katika filamu) mwenye watoto wanne alianza kuuza mwili wake kupata pesa za kuendesha familia baada ya mume wake kufariki.Mama huyu mali zote za mume wake zilitaifishwa na ndugu wa mume wake na yeye kufukuzwa kwenye nyumba aliyojenga naye. Kwasababu ya ugumu wa maisha, alipanga chumba kimoja ambacho ndicho kilichotumika kama sehemu ya kuingiza wanaume kwa malipo.
MCHANA,alipopata mwanaume aliwaambia watoto tokeni nje au aliwatuma sokoni ilimradi tu ahudumie mteja wake. Vivyo hivyo,wakati wa usiku mambo yalikuwa hayo hayo watoto walidanganywa hivi wakadanganywa vile ilimradi waondoke chumbani mama yao afanye kazi yake ili wapate pesa ya kula.
Filamu hii ilimfanya kijana huyu wa chuo kikuu(Nampatia jina la Kendrick uwe mfano tu wa jina lake) kudondosha machozi mengi sana kwasababu ndiyo ilikuwa picha halisi ya maisha yake na mama yake mzazi wakati alipokuwa mtoto wa chekechea,yaani ni kama vile filamu hiyo ilikuwa ikizungumzia maisha yake ya utotoni.
Wakati akiwa chekechea,alikuwa akiambiwa na mama yake wakati wa mchana toka nje niongee na anko wako kisha mlango ungefungwa paa!. Usiku pia hivyo hivyo,hali hii ilimfanya Kendrick kutambulishwa kwa ma anko wengi sana maana kila alipoulizwa huyu ni nani mama yake alimjibu ni anko wako. Kendrick alikuwa akiletewa zawadi na wakati mwingine alipatiwa pesa na hao ma anko zake feki!
Katika umri huu wa chuo kikuu, Kendrick akiwa anatazama filamu hii ya Kinaijeria kumbukumbu zinamrudia na kugundua kuwa kumbe hata mama yake alikuwa akijiuza wakati yeye alipokua mtoto kama ambavyo mama huyu katika filamu anauza mwili wake ili apate pesa za kuitunza familia yake.
“Mama kulikuwa hakuna njia nyingine zaidi ya hii?Nakuchukia! nakuchukia sana mama!”. Kendrick alizungumza huku akilia kwa huzuni.
Dada au mama,
Hao watoto unao waona ni wadogo hawajui chochote, siku wakiwa wakubwa omba wasikumbuke chochote kama ambavyo Kendrick alikumbuka Mikasa ya utotoni kumuhusu mama yake. Watakuchukia sana!
Lakini pia, kama una watoto kuanzia miaka Saba na kuendelea,kuwa makini sana kuwatambulisha baba mpya kila siku. Watakuchukia!
3. Hata kama wamekukosea kwa kiasi gani. Usiwapatie adhabu ya kuwanyima chakula!
Binadamu hawezi kuishi PASIPO KULA. Kumnyima mtoto wako chakula kama adhabu ni kukosa utu, BAHATI MBAYA SANA unamnyima chakula halafu wewe mzazi unakula chakula ili usife. Dada, mwanao atakuchukia kwasababu ya ujinga wako! Adhabu ziko nyingi sana lakini si ya kumnyima mtoto chakula. Unaweza kumfanyia hivyo, kesho ukaona anafanya kazi kwa bidii ukafikiri amebadilika kumbe unajidanganya anaogopa usimfanyie ukatiri wa kumnyima chakula tena kama ulivyomfanyia siku zilizopita lakini pia unakuwa unamfundisha mtoto wako roho mbaya kuwa kuwanyima watu chakula ni jambo la kawaida!
4. Hata kama wamekukosea kiasi gani. Usiwapatie adhabu kali inayoacha alama au kovu kwenye MIILI YAO!
Watoto wanapokukosea, nakushauri usiwapige au kuwapatia adhabu kali kwa kiasi ambacho alama ya kovu inabakia kwenye MIILI YAO. Wapo wazazi huenda mbali zaidi kwa kuwapatia adhabu isiyo na UTU watoto kwa kuwachoma vidole vyao kwa Moto wanapofanya makosa. Mama, nakushauri usimfanyie hivyo mtoto wako kwasababu kila atakapoona makovu ya Moto au fimbo kwenye mwili wake ataona ukatiri wako na sio upendo wako. Anaweza kuonyesha kukupenda lakini ikawa upendo wa woga na hofu kwasababu anaogopa usimpe makovu mengine mwilini na sio mapenzi ya dhati kwa mama yake!
5. Kamwe usimkataze mtoto KUCHEZA!
Mama. Inawezekana mtoto wako anajichafua sana kiasi kwamba nguo zake zinakuchosha kufua kila siku. Lakini pia, inawezekana unaogopa ataumia.
NAOMBA NIKWAMBIE KWAMBA, UTOTO ni hatua muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu. Furaha ya maisha ya utoto ni KUCHEZA,tena sio kucheza peke yake, NA WATOTO WENZAKE! Kamwe usimkataze mtoto KUCHEZA au KUCHEZA NA WATOTO WENZAKE, atakuchukia kwasababu ni sawa na kumshangaa kwanini yeye ni mtoto aruke steji na kuwa mtu mzima! Ni sawa kumchukia jinsi alivyo.
Kama unampenda, mruhusu acheze! Kama unaogopa asijichafue, mtengenezee mazingira safi ya kucheza yasiyo ya kujichafua. Kama unaogopa atajifunza tabia mbaya za marafiki zake basi mchagulie marafiki wazuri wa kucheza naye. Kuendelea kumkataza kucheza ni kumfanya akuchukie DAIMA!