Maeneo Saba Ambayo Ni Lazima Utasemwa Tu
1. Kama hauna uwezo wa kufanya tendo la ndoa hautazuia kusemwa vibaya, LAKINI pia kama unafanya tendo la ndoa na kila mtu( WEWE NI MALAYA) watakusema vibaya pia.
2. Kama wewe ni tasa(hauwezi kupata watoto) hautazuia kusemwa vibaya. LAKINI pia, kama wewe umezaa watoto wengi sana WATAKUSEMA vibaya pia.
3. Kama ukifunga ndoa ya gharama kubwa sana ( ya kitajiri) wapo ambao watakusema vibaya na hautaweza kuwazuia, lakini pia ukifunga ndoa ya bei rahisi sana (ya kimasikini) utasemwa vibaya pia. Sio HIVYO tu, ukiamua usifunge ndoa, mkachukuana sogea tuishi na mwenzi wako bado utasemwa vibaya pia kuwa wewe ni mhuni, huna maadili ya kiroho(KIDINI) n.k.
4. Ukiwa tajiri sana hautazuia kusemwa vibaya(Pesa za kishirikina na kadhalika), LAKINI ukiwa masikini pia utasemwa vibaya.
5. Kama wewe ni Mfanyabiashara unauza sana, hauwezi kuzuia kusemwa vibaya kuwa unatumia ushirikina kwenye biashara yako. Lakini pia, kama hauuzi, utasemwa pia vibaya!
6. Ndugu akifa, mkigharamia msiba na kumuheshimisha Marehemu, kuna wakati mnaweza kusemwa vibaya kuwa nyie ndiyo mmehusika na kifo chake. Mmemuua, lakini pia iwapo ndugu akifariki msipojitoa kwenye msiba huo na kuugharamia, mtasemwa vibaya kuwa mna roho mbaya!
7. Ukiwa na elimu sana utasemwa vibaya sana ( niliwahi kuonyeshwa mtu mmoja nikaambiwa kuwa yuko kama mjinga mjinga kimuonekano kwasababu kasoma sana, ana phd). Lakini, pia kama hauna elimu utasemwa vibaya pia. KWENYE MAISHA, HAUWEZI KUZUIA KUSEMWA VIBAYA KAMWE!
Narudia tena! Rafiki, kama Binadamu ambaye bado uko hai hauwezi kuzuia kusemwa vibaya, anayesemwa vizuri ni marehemu tu!
LAKINI. JIONI YA LEO, NAKUOMBEA KWA MUNGU USEMWE VIBAYA KATIKA MAMBO YALIYO MEMA YASIYO LETA MADHARA KWAKO NA KWA WENGINE. UBARIKIWE SANA.
Maisha yana nyakati zinazoumiza na kusikitisha sana.
Je, wewe unasemwa vibaya kwenye maeneo gani hapo ulipo?
1 Comment
Utamu