KWA NINI MATAIFA YA KIARABU HAYAMSAIDII PALESTINA?
Unakumbuka kwamba Mfalme Faisal wa Saudi Arabia aliuawa mwaka 1975 kwa sababu ya hili. Hebu tusome wote tujifunze hapa.
Si kuhusu mafuta tu.
Ni deni la kitumwa.
DENI LA KITUMWA
Utawala wa Kiarabu si kwamba umepewa rushwa tu bali hata kutawaliwa.
Kila taifa linahitaji dola ya Marekani kufanya biashara lakini hizo dola zinakuja kutoka dola zinatoka kwa Hifadhi ya Shirikisho ambayo si sehemu ya serikali ya Marekani.
Hizo ni benki binafasi ambayo inaongozwa na benki 12. Hazijachaguliwa wala hazipo wazi kwa kila mtu, na kubwa zaidi si za Kiislamu.
Hawa majamaa wanaprinti pesa bandia, wanakopesha mataifa mbalimbali. Maana ya bandia ni kwamba wanachapa pesa ambazo hazipelekwi kwenye mzunguko, mnapewa nyie. Yaani mfano Tanzania inahitaji dola bilioni 10, wanaingia kiwandani, wanawachapia halafu wanawapeni. Hawataki uwarudishie pesa bali wanataka mali. Mali hizo ni kama mafuta, ardhi, utii na ukimya.
Saudi Arabia vipi?
Asilimia 80 ya deni lake anadaiwa na nchi za Magharibi. Hizo nchi ndipo zilipo hizo benki.
Na nadhani ushajua hizo benki zipo chini ya nchi gani. So hawa watu huwa wanatoa kauli moja. Kaa kimya kwenye suala la Palestina ama upoteze kila kitu. Viongozi wa Kiarabu wanatingisha vichwa na kutii.
Kama hawatotii kile wanachoambiwa basi hiki ndicho kinachokwenda kutokea katika nchi zao zenye mamilioni ya Waarabu.
Hawatoingiziwa chakula. Kumbuka nchi nyingi za Kiarabu hazilimi, wanaagiza vyakula.
Hawatengenezi dawa bali huagiza dawa kutoka huko Magharibi. Pia watakosa haki ya kufanya biashara kimataifa, so watapoteza vitu vingi, hawana jinsi zaidi ya kutii.
Mfalme Faisal wa Saudi Arabia alipojaribu kuuza mafuta bila dola ya Mmarekani miaka ya sabini, kilichomkuta, watu wakammaliza. Huo ukawa mfano kwa viongozi wengine kutokuthubutu kufanya hivyo.
MAFUTA
Nchi za Kiarabu zinategemea sana biashara ya mafuta. Sasa hii biashara imekuwa na mtego mkubwa sana.
Hizi nchi za Kiislamu haziwezi kuuza mafuta kwa kutumia pesa zao. Wanalazimishwa kufanya biashara hizo kwa kutumia dola. Hii inaitwa Petrodollars.
Hii system ililazimishwa kwa Saudi Arabia miaka ya sabini.
“Unauza mafuta kwa pesa ya Kimarekani, tutaulinda utawala wako.”
Hii inawafanya Marekani kuprinti pesa zao bure kabisa na wakati Waarabu wanafanya kazi kwa bidii, wanatokwa na jasho, na wanatii kuipata hiyo dola.
Libya walijaribu kuvunja suala hilo.
Iraqi nao walijaribu kwenda kinyume.
Nadhani unajua kilichotokea.
So utawala wa Kiarabu si kwamba wapo kimya juu ya Palestina kwa kupenda, wapo controlled, wapo utumwani. Hawawezi kuiokoa Palestina kwa sababu wao wenyewe wameshindwa kujiokoa.