Kuwa Mbunge Kilwa, Uuujue Kwanza Uchawi
Ni kweli na haya ni ya kawaida sana jimboni kwangu Kilwa, na hasa Kilwa Kaskazini:
Baada ya Kingunge Ngombali Mwiru kuacha kugombea, trend ya wagombea kufa au kupatwa na madhila imekuwa hivi:👇🏾
1. Aligombea bwana Chubi na bwana Mtumbuka kwenye kura za maoni CCM, Mtumbuka akapata wenge akiwa anaendesha gari kuelekea bandarini Kilwa Masoko, akapitiliza na kutumbukia baharini. Hivyo Chubi akawa mbunge.
2. Baada ya miaka mitano, Chubi alitetea kiti chake na Dkt. Mpanda ndani ya CCM, Chubi akafa, Dkt. Mpanda akawa mbunge (ingawa siku ya kuapishwa alipata na upofu, akawa bungeni akiwa kipofu), na hakuwania awamu ya pili maana alifariki.
3. Mtanange uliofuata ukawa wa Balozi Ali Mchumo na Mangungu (wa Simba). Balozi Mchumo akafa, Mangungu akawa mbunge.
4. Awamu iliyofuata wakanyukana watatu: Mangungu (akitetea kiti chake), Dkt. Lugongo (alikuwa Mhadhiri wa Ardhi University) na Ndulane (mbunge wa sasa). Mangungu akashindwa, Dkt. Lugongo akaugua mguu ghafla na akafa, Ndulane akashinda. Hata hivyo, Ndulane alipoteuliwa na JPM kuwa naibu waziri, akashindwa kuapa/kusoma kiapo, akatenguliwa. Inasemekana alikuwa anaona matusi kwenye hati ya kiapo akasita kuyatamka.
5. Mwaka huu Ndulane anatetea kiti chake na watu kadhaa, akiwemo huyo mwalimu. Mwalimu kapata ajali kafa, Ndulane kavunjika mguu vibaya mno, yupo MOI…
*Halafu mtu eti anidanganye nikagombee? Wee! 😂😂😂*