USIACHE KUSOMA KAMA UNA MIAKA 20 MPAKA 45!
1. Kama una umri huu hakikisha unatengeneza mahusiano yako mazuri na Mungu!
Kwanini? Kwasababu umri huu ndiyo umri ambao SHETANI atayavuruga maisha yako kiuchumi na kimahusiano. Pasipo Mungu,katika umri huu uchumi wako na mahusiano yako yatavurugwa vibaya sana na SHETANI.
2. Kama una umri huu hakikisha hauamini kila MTU!
Kwenye umri huu utakutana na matapeli wengi wa mahusiano lakini pia utakutana na watu ambao wanakuja kwenye maisha yako ili tu kuyavuruga. Kuwa makini sana!
3. Kama una umri huu hakikisha umefahamu ni kitu gani unakihitaji kwenye haya MAISHA!
KWASABABU.
Hautaweza kufanya kila kazi,
Hautaweza kutafuta kila kitu,lazima uchague vitu (vipaumbele) unavyovihitaji uweze kuvipambania.
4. Kama una umri huu hakikisha unaishi pasipo KUIGA MAISHA YA WATU WENGINE.
Wapo ambao watajenga katika umri huu, wapo ambao watafunga ndoa kwenye umri huu, wapo ambao watanunua magari na kumiliki biashara kubwa katika umri huu lakini wapo ambao hawatakuwa na chochote kwenye umri huu. Hivyo basi, kuepuka msongo wa mawazo na kupoteza mwelekeo wa maisha yako jifunze kuishi pasipo KUIGA MAISHA ya watu wengine bali ishi ukitambua kuwa kila mtu kapangiwa na Mungu kutimiza malengo na ndoto zake kwa wakati ambao ameupanga Mungu mwenyewe. Usijikatie tamaa!