HAUJUI UCHUKUE MAAMUZI GANI? ZIFUATAZO NI ISHARA SABA ZA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI!
1. Zingatia mapigo yako ya moyo.
Kama unataka kufanya maamuzi basi zingatia mapigo yako ya moyo, kama unataka kufanya jambo ambalo sio sahihi mapigo yako ya moyo yatakuwa yanaenda haraka sana. Achana na jambo hilo sio sahihi linaweza kukuletea madhara! Kama unataka kuchepuka, kufanya uzinzi, kuiba, kuua lazima hali hii utakumbana nayo kwasababu sio maamuzi yako sio sahihi. ACHA!
2. Zingatia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Your gut feeling!)
Kama unataka kufanya jambo ambalo sio sahihi, hamu ya chakula itapotea hata kama una njaa ile hamu ya kula itapotea kabisa. Kama ulikuwa tayari umekula basi tumbo linaweza kujaa gesi kwasababu ya msongo wako wa mawazo kwa jambo unalotaka kulifanya. Ukiona dalili hiyo, achana na jambo hilo!
3. Zingatia hisia zako za FURAHA!
Ukitaka kufanya jambo baya, litakukosesha furaha utakuwa na huzuni na mambo niliyoorodhesha hapo juu yatatokea kwenye mwili wako. Lakini ukiataka kubadili maamuzi ya kuachana na jambo hilo baya unalotaka kufanya, hisia za furaha zitakuja ghafla. Ukihisi hali hiyo ya furaha baada ya kubadili maamuzi basi tambua umechagua jambo sahihi.
4. Fikiria kuhusu madhara ya maamuzi unayotaka kuchukua.
Kama maamuzi unayotaka kuchukua yanaweza kusababisha kifo chako,afya yako kuwa mbaya(kupata magonjwa hatari) au kupoteza pesa nyingi basi maamuzi hayo sio sahihi achana nayo. Siku zote maamuzi mabaya yana faida chache sana na hasara ni nyingi!
5. Zingatia kigezo cha jamii yako inayokuzunguka.
Iwapo unataka kufanya maamuzi yeyote, basi zingatia jamii yako je iwapo maamuzi yako yakiwekwa wazi mbele za watu(sio siri) je ni idadi ya watu wengi watakuunga mkono?au watakupinga.a
Maamuzi mengi sahihi yanaungwa mkono na watu wengi. Ukiona unachotaka kukifanya kinapigwa vita na jamii(kinyume na maadili ya jamii) basi tambua sio sahihi. Acha!
6. Sikiliza amani ya moyo wako!
Maamuzi sahihi yanaiacha roho yako ikiwa nyeupeee, pasipo kinyongo yaani unahisi amani kwenye moyo wako isiyo ya kawaida mithili ya mtu aliyeshusha mzigo kichwani mwake. Hivyo basi, kama unataka kufanya maamuzi na moyo wako ukawa na amani basi maamuzi hayo ni sahihi. Kitu ambacho unataka kufanya kikiwa sahihi basi mapigo yako ya moyo yatakuwa kawaida, Kwanini? Kwasababu moyo wako una amani tele!
7. Sikiliza roho yako, nafsi!
Hii ni hatua ya mwisho ambayo inakinzana na hatua ya tano. Mfanya maamuzi ni wewe na mnufaika wa maamuzi mabaya au mazuri ni wewe. Fanya maamuzi kwa kuzingatia roho yako itakuwa na furaha na amani na utakuwa tayari kuhimili matokeo ya maamuzi yako. Kama uko tayari, basi sikiliza nafsi yako inataka nini maana siku zote maamuzi kutoka kwa mtu mwenyewe yanakuwa sahihi kwasababu hatajutia wala kumbebesha mzigo wa lawama yeyote yule. Kuna watu hawafanyi mambo fulani kwasababu ni kinyume na imani zao,hicho ndicho nakizungumzia hapa! Sikiliza nafsi na imani yako inataka nini.