FAHAMU MAMBO YAFUATAYO KABLA HAUJACHELEWA NA KUHARIBU MAISHA YAKO!!
1. Kuwa na URAFIKI (ukaribu) sanaaaa na mtu fulani tambua ipo siku atakuvunjia heshima, kwasababu mmezoeana na anajua hauwezi kumfanya chochote!
2. Vitu vinaisha, watu wanabadilika,maisha yanabadilika na kusonga mbele!
Usiwekeze sana muda wako kwenye vitu kwasababu havidumu lakini pia maisha nayo hayadumu. Usijisahau na kuwa na kiburi!
3. Mwisho wa yote, utabakia wewe kama wewe!
Kwanini? Kwasababu utazikwa peke yako(mwenyewe), kama ni ugonjwa utakutesa mwenyewe,kama ni furaha itakuwa ya kwako. Hivyo basi,heshimu kila kitu kinachohusu maisha yako. Jifunze kufanya maamuzi mwenyewe yanayohusu maisha yako kwa faida yako!
4. Hakuna kitu chochote kinachopatikana BURE Duniani. Lazima ugharamie!
Kwenye Dini(Imani) hakuna cha bure, lazima utoe sadaka na zaka. Kwenye elimu lazima ulipie ADA ya masomo, kwenye biashara lazima uwe na mtaji,muda lakini ukubali wakati mwingine kupata hasara. Mahakamani, kwenye siasa na mahali popote pale, lazima utoe pesa kupata unachokihitaji!
UKIONA MTU ANAKUVUTA KWENYE KITU CHA BURE, TAMBUA KINA MADHARA AU KUNA MAHALI YEYE ANANUFAIKA.
5. Punguza au kuwa na kiasi na kiwango chako cha HURUMA, kinakuharibia maisha yako!
Duniani, kuwa na huruma sanaaa hakuwafanyi watu wakupende bali wakutumie. Watu wakijua kuwa wewe unahuruma, watataka kila shida waliyonayo uwasaidie au uwatatulie Jambo ambalo halitawezekana wewe kusaidia watu wote.
LAKINI PIA,
Kuna watu wengi sasa hivi wameshatambua kuwa HURUMA ni mtaji, ndiyo maana wako tayari kuigiza matatizo ya uongo ili waweze kusaidiwa. Sio wote wanao omba na kuhitaji msaada wana matatizo kweli japokuwa wapo wengi pia hawaigizi MATATIZO. Ushauri wangu kwako, saidia kwa kiasi chako usijiumize sanaaa!