Yafuatayo achana nayo yanakurudisha nyuma kimaendeleo kwenye maisha yako!
Epuka kujihukumu kwa maisha yako na mienendo iliyopita. Jisamehe na wekeza nguvu zako katika maisha yako ya sasa na ya baadae. Wahenga walisema yaliyopita si ndwele tugange yajayo”. Kuwaza yaliyopita kutakusababishia msongo wa mawazo ambao hauna faida za kiafya na kiuchumi maishani mwako!
2. Uvivu
Epuka kuendekeza uvivu. Uvivu ni hali ya kutumia muda mwingi katika kustarehe na sio shughuli za kimaendeleo maishani mwako. Uvivu ni chanzo cha umasikini wa kiroho,kiuchumi na kijamii. Mafanikio yeyote yale,hayataki uvivu bali kuwekeza muda wako na jitihada au juhudi zako kutafuta unachokitaka kwenye maisha yako. Utafanikiwa na kufika mbali sana!
3. Kughailisha mambo
Acha kupanga kitu kile kile siku baada ya siku pasipo utekelezaji(Kughailisha mambo). Hakikisha unakuwa mtu wa matendo na sio maneno, ukipanga kitu unakitekeleza, utafika mbali sana.
4. Uraibu wa mambo hasi(Negative addictions)
Hakikisha hauendekezi mazoea ya kuamini katika vitu hasi ( kutowezekana kwa vitu, mipango kwenda hovyo,kutokea mabaya kwenye maisha yako). Hakikisha akili yako inaamini kuwa kila jambo linawezekana, utafika mbali sana.
5. Ushauri hasi kutoka kwa watu.
Hakikisha unakataa kukaribisha mawazo ya watu ambao wanakushauri kuwa mipango yako na malengo yako mazuri uliyonayo haiwezi kufanikiwa, wakwepe. Karibisha watu kwenye maisha yako au kuwa karibu na watu ambao wana amini katika MAFANIKIO na sio KUSHINDWA.
6. Marafiki wa uongo(Fake friends).
Hakikisha unajitenga mbali na watu ambao wanajifanya marafiki zako kumbe ni maadui zako(nyuma ya pazia wanapanga mipango ya siri kukutumia na kukuharibia taswira yako katika maisha yako.
7. Kuwaza kupita kiasi(Overthinking).
Hakikisha haukaribishi mawazo ya aina fulani kichwani mwako pasipo kuchukua hatua. Acha kukiwaza kitu kwa muda mrefu pasipo kuchukua hatua au kufanya vitendo kulifanyia utatuzi. Mara nyingi, kuwaza kupita kiasi hupunguza uwezo wa akili yako kufanya maamuzi, unaweza jikuta ukifanya maamuzi yasiyo sahihi.
8. Hofu ya kushindwa.
Haupaswi kuogopa kushindwa. Kushindwa ni sehemu ya maisha ya binadamu na ni sehemu ya kujifunza na kuongeza ujuzi na uzoefu. Kushindwa kusikufanye kukata tamaa ya kusonga mbele kupigania ndoto zako!