“SITAKI KUOLEWA, NITAENDA MBINGUNI MOJA KWA MOJA” – BIBI BIKRA MWENYE MIAKA 93 AFUNGUKA
Chanzo: RAYNEWS
Useja si safari rahisi na kwa kawaida ni vigumu kwa idadi kubwa ya wanadamu kukaa miaka bila kujamiiana. Huu ni uamuzi wa kibinafsi unaohitaji kujitolea na lazima mtu awe tayari kushughulikia shinikizo na ukosoaji unaokuja pamoja na Useja.
Fatuma Mali sasa anaibuka kama bikira mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Mwanamke huyo anayetokea Afrika alikuwa na mahojiano na Afrimax English. Fatuma alisema kuwa ana miaka 93 na hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yeyote. Alisema hata kuolewa haijawahi kuwa chaguo kwake.
Alipokuwa bado mdogo alikuwa akikataa wanaume, aliishi na wazazi wake hadi wote walipofariki na yeye kubaki nyumbani kwao. Alijitolea wakati wake kumtumikia Mungu na kujiboresha tu. Fatuma alisema kuwa amekuwa akikosolewa sana, wengine hata kumwita mchawi lakini hii haijawahi kuathiri maisha yake.
Alisema hatawahi kuolewa na hata hana hamu ya kuwa mke wa mtu. Ana furaha tu na bado ana nguvu za kutosha kujitegemea. Atasisitiza useja hadi kifo.
TAZAMA VIDEO

