ALINIAMBIA YEYE NI BIKRA, TUSIFANYE MAPENZI HADI NDOA – KUMBE KUNA JAMAA ALIKUWA ANAICHAPA
Nikiwa Chuo Mwaka wa Tatu, Kuna Binti nilikua nae katika mahusiano, Nilimpenda sana nae alionesha kunipenda.
✓Penzi lilikua zito, tukaweka malengo ya ndoa baada ya mimi kumaliza chuo, Kila ninapokutana nae alikua ni binti wa kunihusia mambo ya Ucha Mungu Na Nikigusia suala la kufanya mapenzi huwa ananitazama nakuambia usiwe na haraka, tusubiri ndoa, mimi bado bikra kabisa una wasiwasi gani.
✓Basi kwakua nilikua nampenda sana, ikabidi nijipe moyo kwamba kesho itakua nzuri zaidi wacha nimuache..Baada ya chuo kuisha nikarudi home
✓Nikakuta washikaji kitaa, nikawasanua bwana yule binti nataka kuoa, Na Wakati Huo bi dada alikua ananifosi sana niwahi kutoa barua ya posa ndoa ipite haraka, lakini washikaji wakaniambia mbona huyo Dada anamtu wake, na inavyosemekana ana mimba yake.
✓Kichwa Nikapata moto, nikaja kumbana binti aiseee akasema kweli, ..toka siku hio aisee nilichukia mapenzi na sitawahi kumuamini tena mwanamke.
Huyu binti alizaa mtoto, na yule jamaa akasepa zake. Saizi yule mwanamke yupo kwa wazazi wake kabaki kuwa singo Mama. hivi kwanini huwa mnatudanganya kina dada?

