ALINISAIDIA KUPATA KAZI, TULIPOACHANA AKANIFUKUZISHA
Kuna Dada nilikutana nae, Nilimpenda tukajikuta tumezama katika penzi zito.Alinikuta msela tu sina kitu, life ngum basi Bidada akapambana nipate kazi. Kuna kampuni ya rafiki yake akaniunganisha hadi nikafanikiwa kupata Ajira.
✓Ajira ilikua nzuri kifupi maisha yalibadilika sana, nikambeba tukawa tunaishi pamoja. kabla Ya Kukutana nae, Kuna binti nilikua nae katika mahusiano na nilimzalisha mtoto tukaachana hivyo mtoto wangu alikua kwa bibi yake.
✓Baada ya kuona life imekaa sawa, ikabidi nimuambie bibie kua sasa ni mda sahihi nikamchukue mtoto nije tumlee hapa ikiwezekana aanze kusomea shule huku, mana alikua na miaka 5, Nazani hapo labda ndio kosa langu lilipo anza, Dada akasema mie siwez kulea mtoto wa mtu muache aendelee kukaa kwa mama
✓Nilifikiria sana, Na nikaangalia maisha na mazingira alipo mtoto, nikaona hapana siwezi ruhusu damu yangu ikahangaika wakati baba nipo hapa na Maisha sasa yapo sawa. Nikafosi nikaenda kumchukua mtoto na kumleta hapa tunapokaa na bibie.
✓Mwanamke kurudi anakuta mtoto, vita ikaanza ndani, kelele na kauli za Kuachana zikaanza hapo. mwisho nikaona haina haja ya kuwa na Mwanamke ambae anatesa damu yangu na hataki hata kumuona mtoto, Nikamuambia basi tuachanae kama unavyo taka wewe.
✓Miezi 2 baada ya kuachana, nafika Ofisini nakuta barua mezani ya kusimamishwa kazi, nakuja kuchunguza ni huyu mwanamke kuna maneno ya sumu kaenda kumlisha boss wangu ili niondolewe kazini. Nikaishiwa pozi lakini kwakua kuna bajeti nilikua nayo kidogo, basi nikaamua kufungua genge la matunda nipo nasongesha maisha mdogo mdogo hadi sasa
✓Nimeleta hiki kisa kwenu kama funzo na zingatio juu ya aina ya watu tunao kutana nao katika maisha. Au kuna sehem nimekosea juu ya maamuzi Yangu? kama Ipo Naomba ushauri ili nami nijifunze pia

