ALIKATAA MIMBA AKAENDA KUOA MWANAMKE ASIYE NA KIZAZI
Mimi ni binti wa miaka 23 mama wa mtoto mmoja niliianza kuitwa mama nikiwa na miaka 20 kwenye harakati za kuitwa mama nikiwa na mwenzangu alikuwa na miaka 27 nilikuwa naye kwenye mahusiano na kukubaliana kuoana ila bahati mbaya nilikuwa mwanafunzi ikabidi tuwe tunaiba, kwenye kuiba nikabeba mimba nilivobeba mimba mwenzangu alinikataa na kuwa ananiambia maneno ya kejeli
Baada ya kujifungua mtoto akamfanana aliniambia nimpe mtoto wake ila nilikataa sana kumbuka alivo nikataa alioa mwanamke mwingine akasema kuwa yule ni mzuri zaidi yangu ila MUNGU alivo wa ajabu haangalii uzuri wa mtu yule dada aliye olewa na huyo baba wa mtoto wangu alikuwa hana kizazi baada ya yule mwanamme kuona mke wake mzuri hazai ndio akaanza kudai mtoto na kwangu ni ngumu sana siwezi kumpa mtoto anadai turudiane ili tuweze kumlea mtoto pamoja ila kwangu ni ngumu sana kwa sababu aliniacha pindi namhitaji alinitelekeza nikiwa sina chochote nikiwa nahitaji msaada wake ila kwa sasa hivi namshukuru MUNGU nimepata zawadi ya mtoto pia nina biashara yangu namlea vizuri mwanangu na sina uhitaji wa kurudiana na huyo mwanamme kwasababu ya alichonifanyia
Jamani wanawake nwenzangu tusiwe wepesi wa kukubali ahadi za uongo na maneno matamu ya wanaume

