BOSS ALIINGIA BAFUNI KIMAKOSA, AKAMKUTA DADA WA KAZI ANAOGA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 2
Baada ya Chakula, Eliza Alitoa nguo za ndani za mume wake pamoja na zake kisha akamuambia Dada wa kazi akafue, Moris aliweza kuona tukio lile na kuanza kumsema mke wake, Eliza hakuonesha kujuta na akatoa lugha chafu kwamba hawezi kumlipa mtu mshahara halafu akamchagulia nguo za kufua, Kitendo hiki kilimkera sana Mume wake Moris hivyo akaamua kumkataza nina Asifanye kazi ile..
Mke wake Eliza, Alishikwa na wivu na hasira nzito juu ya maamuzi ya mume wake, baadae moris Alipotoka nyumbani, Eliza akamuambia Nina leo itakua mwisho wa maringo yako, Nina akawa anashangaa huku akimuomba msamaha Eliza, Kwa ajabu kabisa Eliza akaenda kuchukua mafuta yalio kua yanachemka jikoni akaja kumwagia Nina…
Nina akapiga kelele za maumivu makali huku asipatikane wa kumsaidia..robo saa baadae Moris akarudi nyumbani, Akashangaa kuona tukio lile, Nina alikua analia bila kupata msaada wowote..
Moris alisikitika sana, na akambeba Nina haraka kisha akamuwahisha hospital, Bahati njema Aliweza pata huduma, na sehem alizo ungua alipata dawa ya kuweka.. Baada ya tukio hili, Moris akaona Eliza hafai tena kuwa mke na mama wa watoto wake, alichokifanya akamfukuza kwa kumpa talaka na hivyo wakaachana rasmi…
Nina aliweza kupona, na zile sehem alizo ungua zilianza kurudi katika usawa na ngozi ya sehem nyengine za mwili japo zilimuachia makovu, Moris akapeleka barua ya Posa kwa wazazi wa Nina, Barua ikajibiwa na hivyo Moris Akapewa kibari cha Kumuoa Nina na awe mke wa maisha yake
Ndoa ilipita, .na hivyo Nina Dada wa kazi akawa mke rasmi wa kijana Moris, Huku Eliza akibaki na majuto ya kumpoteza Mume wake kwa roho yake mbaya.
FUNZO
Jitahidi Kuwa Mwema Kwa kila Mmoja Unae kutana nae au kuishi nae, Malipo Ya Ubaya ni fedheha na Aibu


2 Comments
Hadithi zako ni nzuri sana ila naomba kama itakupendeza zifanye kuwa ndefu Kwa kila kipande unachoweka, Asante
Hadithi ndefu mbona zipo nyingi tu, ila ndio hivyo kuna baadhi ya hadithi ni fupi. Kwahiyo zote tunakwenda nazo kikubwa ziwe na ujumbe