MPENDE MKEO, MCHEPUKO HANA SHUKRANI
Hiki ni kisa chenye mafundisho makubwa sana kwetu sisi wanaume
Kuna rafiki yangu mmoja hivi alikuwa na mkewe mzuri tu na mungu aliwajalia watoto na kipato chao kilikuwa cha kati.
Sasa kama unavyojua sisi wanaume tunapopita mitaani macho kodo kudele warembo
Basi katika pita pita za mitaani jamaa akanasa kwenye penzi matata sana la mtoto wa kimwera kama unavyowajua wamwera hawanaga kazi mbovu show show ukiwa bwege unaisahau familia
Basi jamaa akazama mazima kwenye penzi la mtoto wa kimwera ikawa siku anarudi nyumbani siku harudi. Mapenzi nyumbani yakapungua na furaha ikatoweka
Mkewe akawa mtu wa mawazo sana na kujiuliza ni nini kilichompata mumewe.
Mara siku sio nyingi mke akaanza kuumwa na mume ndio kabisa akapata chance ya kuwa anaenda kabisa kwa mchepuko wake wa kimwera pasipo kuijali afya ya mkewe
Siku moja jamaa akatoka safari ya kwa mchepuko wake kufika kule mchepuko wake wa kimwera haupo jamaa kulizia akambiwa ameenda ruvuma kufuata samaki
Jamaa kwa kuwa alishazama kwenye penzi la mmwera wivu ukamshika nae akafunga safari kumfuata mchepuko wake ruvuma
Jamaa alivyotoka tu huku nyuma mkewe ugonjwa ukamzidia wasamalia wema wakampeleka hospital mumewe akipigiwa simu muda wote haipatikani.
Haikupita muda mke anafariki. Jamaa akipigiwa simu bado haipatikani
Ndugu wakachukua mwili wa ndugu yao wakaufanyia mazishi pasipo mume kuwepo wala kujua
Basi mazishi yalipopita siku sio nyingi mumewe akarudi kufika wanapoishi kila mtu anamuangalia yeye kwa macho mabaya, ndipo wazee wakamueka chini kumuhoji na kumpa tarifa za msiba wa mkewe jamaa akanza kulia na wengine wenye hasira wakataka kumpiga
Jamaa ikawa kwake hakukaliki akaona isiwe tabu kwa kupata faraja wapi ni kwa mchepuko wake kufika kule anambiwa mchepuko ushapanda Maning Nice upo dar kwa mumewe, penzi limerudi upya.
Jamaa akapagawa siku hizi kawa ni mtu wa Tungi (pombe)
Tuwaheshimu sana wake zetu
Chanzo: Jamii Forums

