KENGELE YA KIFO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 1
Ilisikika taarifa ya habari katika kituo cha habari hapa nchi. taarifa hiyo ilielezea kuhusu binti mmoja aliyezikwa miaka 50 hiliyopita…binti huyo alifufuka na kuanza kuonekana sehemu mbalimbali huku macho yake yakionekana kuwa na machozi ya damu iliyoganda…inasemekana kuwa binti huyo anajitokeza kila unaposikika mlio wa kengere yoyote ile…..anabadilika sura na kufuata mlio wa kengere ulipotokea,,na akifika eneo hilo anafanya mauwaji ya kikatiri kwa kunyonga shongo kwa kutumia kamba aliyokuwa anatembeanayo muda wote.kila anapobadilika….hakuna aliyekuwa akifahamu kuwa binti huyo alifufuka na anaishi katika maisha ya binadamu wa kawaida,lakini huwa anabadilika na nacho yake hutoa machozi ya damu kila inaposikika sauti ya kengere…
Usiku wa leo,binti huyo aitwae Tina..alionekana akiwa ndani ya clubu akiwa na mpenzi wake Domy….walikuwa wameketi kaunta huku wakinywa
karinya(pombe)Domy alikuwa hajui kuwa Tina alishakufa miaka hamsini (50)iliyopita akazikwa huko,Nigeria lakini alifufuka Tanzania..Domy aliishi na Tina miaka mitano lakini hakuwahi kuwajua wazazi wala ndugu wa tina..pia hakuwahi kumjua rafiki wa tina hata mmoja..hata simu ya tina ilikuwa na namba moja tu ya Domy.
waliendelea kunywa pombe…Tina akanyanyuka ili aende chooni kujisaidia haja ndogo..alipoingia chooni ikasikika kwa mbali sauti ya kengere ikitokea upande wa nje ya club..uso wa Tina ukaanza kubadilika macho yake yaanza kutoa machozi ya damu….akatoweka kimiujiza na kuelekea kule ulipotokea mlio wa kengere….
akajitokeza nje ya nyumba moja akaanza kuzipiga hatua..
kwa mbali kidogo walionekana wanafamilia wakiwa wamesimama mlangoni wakisubiri mlango ufunguliwe…walipo ona kijakazi wa ndani anachelewa kufungua mlango baba wa familia hiyo akabofya tena kitufe cha kengere ili yule kijakazi kama amelala basi aisikie kengere hiyo…
wakastuka kunamwanamke kasimama nyuma yao
akamkamata baba wa familia hiyo na kumnyonga kwa kamba aliyokuwa ameishikilia mpaka akafa.
mkewe akaamua kutimua mbio huku amewashika mikono watoto wake wawili wa kike… tina akajitokeza mbele yao na kuwanyonga wakafa papohapo…kisha akaingia uoande wa ndani na kumuuwa kijakazi wa nyumba hiyo….akatoka upande wa nje na kutoweka kimiujiza…..akajitokeza ndani ya choo cha cha wanawake ndani ya ile club aliyomuacha Domy…akarudi katika hali yake ya kawaida akatoka chooni na kurudi kule kaunta.. wakaendelea kuzitandika karinya(kunywa pombe)
ilipofika majira ya saa saba za usiku Domy alisema waondoke wakalale….wakatoka nje na kuingia ndani ya gari wakaianza safari ya kurudi nyumbani…
*****************
asubuhi palipokucha alidamka na kuandaa chai..
alipomaliza kuandaa chai wakaanza kunywa huku wakitaza Runinga…ikaoneshwa taarifa ya habari ikisema kunafamilia imeuwa na mtu asiyejulikana.
kisha wakainesha ile nyumba ya wanafamilia hao.
Tina alichukia akakaza macho kuitazama runinga ghafla ikavunjika kioo.. na kuanza kutoa moshi…
Domy alistuka sana lakini hakujua kuwa Tina ndiye kavunja Runinga hiyo kimiujiza..Domy akaanza kulalamika kwa kusem,,”Yani hili shirika la tanesco hawapo makini na kazi yao,ona sasa Runinga yangu imeeungua….Domy alikasirika sana akahairisha kunywa chai akaondoka na kuelekea kazini….kabla hajafika mbali aliamua kwenda nyumbani kwa rafiki yake…hakuna umbali mrefu kutoka nyumbani kwake…alipofika alipaki gari na kuufuata mlango akagonga hodi..akasubiri kwa sekunde kadhaa alipo ona hakuna mtu anayekuja kufungua mlango,,akahisi huenda hawajasikia akigonga mlango akaamua kubofya kengere iliyokuwepo kando ya mlango kwenye ukuta.
****************
Kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akiendela kufanya usafi wa nyumba…ghafla ukasikika mlio wa kengere akili ya tina ikabadilika pamoja na uso wake…macho yake yakaanza kutoa mchozi ya damu…akatuoa kitambaa alichokuwa anakitumia kuduta vumbi kwenye kabati la sebuleni……akatoweka kimiujiza na kuufuata mlio wa kengere…….
Domy akabofya kitufe cha kengere, akasubiri kwa sekunde kadhaa kumbe rafiki ake alikua dukani anaoga, domy alitazama saa yake mkononi ilikua ni saa tatu kasoro za asubuhi, akaingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuelekea kazini. Domy alipoondoka Tina kajitokeza kimiujiza akasimama nje ya mlango huo, wakati huo huo rafiki yake Domy alionekana akitoka bafuni huku akizipiga hatua za haraka haraka……alipofungua mlango akakutana uso kwa uso na Tina alistaajabu kuona macho ya Tina yakitoa machozi ya damu akafunga mlango kwa haraka. . alipogeuka alistuka kumkuta Tina ndani ya nyumba, Tina alimnasa alimnyonga kwa kamba mpka akafa…. kisha akatoweka kimiujiza, akajitokeza nyumbani kwake, baada ya sekunde kadhaa akarudi katika hali yake ya kawaida…akajishangaa sana…hali hiyo humtokea pasipo yeye kujua. akakimbia na kuelekea bafuni akanawa uso huku akijitazama kwenye kioo kilichokuwa ukutani…..kumbukumbu ikamjia akahisi kaona tukio la mauwaji ya mtu akinyingwa kwa kamba….
akatoka bafuni akaingia jikoni akaendelea kufanya usafi…alipomaliza…akatoka na kuelekea sokoni kwa ajili ya manunuzi ya chakula cha jioni…
alipofika sokoni alinunua vitu mbalimbali..kisha akaelekea super market kununua vitu vingine alivyokuwa amepanga kununua……
akiwa ndani ya super market….alionekana mama mmoja akiwa na mtoto wake mdogo..mama huyo alikuwa akinunua midoli kwa ajili ya mtoto..
katika midoli hiyo kunamdoli mmoja ulikuwa na kegere ndogo iliyofungwa shingoni mwa mdoli huyo…..yule mama alipoutikisa mdoli…kengere ikatoa mlio…
Tina akastuka…ghafla akaanza kubadilika…macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu hata uso wake ukaonekana kutisha….akatuoa kikapu alichokuwa amekishikilia na kuanza kuzipiga hatua kuufuata ule mlio wa kengere….
ghafla kuna mtoto mdogo aliyekuwemo ndani ya super market hiyo alikuwa na kamera ya kitoto(toy) alipomuona Tina,,mtoto huyo aliamua kumpiga picha….camera ile ikawaka mwanga(flash) Tina akajiziba uso huku akipiga kelele akabadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida…..akastuka huku akijishangaa….. hata watu waliokuwemo ndani ya super market hiyo,,walishtushwa na kelele za Tina wakageuka na kumtazama……Tina aliakota kikapu chake akazipiga hatua za haraka kutoka upande wa nje..
hakuna aliyemuona Tina kipindi alipobadilika zaidi ya yule mtoto aliyempiga picha…kumbe mwanga wa kamera unauwezo wa kumzuia Tina kipindi anapobadilika…..mwanga huo akiuona unamchoma kama kamwagiwa maji ya moto….sekunde hiyo hiyo anarudi katika hali yake ya kawaida..
******************
Alizipiga hatua huku akijiuliza kwa nini hali hiyo hujitokeza bila yeye kujua..akawa anajiuliza,”mimi ni nani???alijiuliza maswali mengi bila kupata jibu
baada ya nusu saa kupita alifika nyumbani..akaanza kuandaa chakula…tayari kwa kukipika jikoni.
****************
upande mwingine alionekana mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la SULE mzee huyo alikuwa anaishi porini familia yake mke na watoto wawili wa kiume…..ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na njia ya siri iliyopita chini kwa chini. nakutokezea kwenye jiko la mgahawa mmoja uliokuwa ukiuza supu na nyama choma….watu wengi walijazana kwenye mgahawa huo…kwa ajili ya kujipatia supu na nyama choma…
mgahawa huo ulikuwa nje kidogo ya Mji…na ulikuwa wazi na huduma inapatikana masaa 24..
mgahawa huo ulikuwa na siri nzito ambayo hakuna mtu aliyekuwa anafahamu zaidi ya Mzee Sule na mke wake pamoja na Watoto wake wawili wa kiume..ambao ndio walikuwa wapishi katika mgahawa huo……
***************
upande mwingine watu walionekana mtaani wakijiuliza kwa nini mtu akikutwa amenyongwa baada ya muda maiti yake inapotea na hakuna anayejua nani muuwaji……hata vyombo vya dola vilipata wakati mgumu sana kumtafuta muuwaji lakini mpaka sasa bado hawajafanikiwa kumjua wala kumpata…
***************
ilipofika majira ya jioni Alionekana Domy akiwa ndani ya gari lake baada ya kutoka kazini..aliliendesha gari kwa mwendo wa taratibu..
akaelekea nyumbani kwa rafiki yake….alipofika alipiga honi ya gari lakini hakuona mtu akija kufungua mlango akahisi huenda rafiki yake bado hajarudi…..Domy hakujua kuwa rafiki yake ameuwawa asubuhi ya leo….na muuwaji ni Tina ambaye ni mpenzi wake. Domy akaamua kuondoka zake na kuelekea nyumbani kwake.alipofika alikuta tayari Tina kamaliza kuandaa chakula cha jioni……..Tina alimpokea Domy kwa mabusu kama kawaida yake huwa anamfanyia hivyo kila siku….
ilipofika majira ya saa mbili za usiku Tina alipakua chakula wakaanza kula…
**************
upande mwingine alionekana mzee sule akiwa ndani ya gari lake aina ya TOYOTA PICK UP..
iliyokuwa wazi upande wa nyuma…..kulionekana kuwa na furushi refu kiasi…..Mzee Sule aliliendesha gari mpaka kule porini ilipokuwepo nyumba yake…alipofika alishuka kutoka ndani ya gari kisha akalivuta furushi lile na kuliweka begani
akazioiga hatua kuingia ndani ya nyumba yake…akapitiliza mpaka ndani ya chumba kilichokuwa kimejitenga peke yake…akalitupia juu ya meza lile furushi…akachukua kusu pamoja na shoka na Upanga mkali sana….akachana furushi lile na kutoa lile turubai alilokuwa amelifunga…alipo litoa turubai hilo,,ndani yake ilikuwemo maiti ya yule rafiki yake Domy……Sule akachukua shoka na kuanza kuikata kata maiti ile..na kukata nyama isiyokuwa na mifupa na kuiweka ndani ya ndoo..
akakata viganja na miguu na kuviweka kwenye mashine ya kusagia nyama unayotumia umeme…mzee sule alikuwa na mtambo maalumu unaofua umeme kwa kuakisi mionzi ya jua.mashine hiyo ilikuwa na nguvu..inauwezo wa kusaga mpaka mifupa ikawa unga mlaini kabisa…
viganja pamoja na miguu iliyosagwa aliitumia kutengenezea soseji pamoja na sambusa…..
alipomaliza kukata kata nyama hiyo alichukua shoka akakipasua kichwa na kutoa ubongo akauweka pembeni vilipokuwepo utumbo pamoja na maini na figo….ambavyo huvichanganya kwenye supu matata…
alipomaliza alichukua ndoo iliyojaa maji na kiisafisha meza kwa kufuta damu zilizomwagika….kisha akabeba ile ndoo iliyokuwa imejaa nyama pamoja na ndoo nyingine iliyokuwa na utumbo pamoja na maini,,figo na ubongo…akazipiga hatua kuelekea kwenye chumba chake cha kulala aka vuta kochi kulisogeza kando…akafungua mlango mdogo uliokuwa kwenye sakafu..mlango huo ulitengenezwa kwa mbao ngumu…… akaingia uoande wa ndani kisha akazichukua ndoo hizo mbili akaanza kuzioiga hatua kwa kupitia nja hiyo ya chini kwa chini kuelekea kuke kwenye mgahawa…
*****************
upande mwingine alionekana Domy akiingia nyumbani kwake….Tina alimpokea mumewe wakazipiga hatua kuelekea chumbani..walipoingia Domy alisema anahisi uchovu..hivyo anahitaji kupumzika…..akapanda kitandani akajipumzisha
Tina akatoka na kuelekea jikoni…..akaandaa chakula cha jioni…
*****************
upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee sule ilisikika sauti ikisema,,””Niongezee supu nalafu ongeza sambusa mbili….
wakati huohuo alionekana mzee sule akitokezea jikoni kutoka kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini ya aridhi….mke wake alichuku ile ndoo iliyokuwa na nyama akaiweka kwenye sufulia kubwa akaweka maji na kuliweka juu ya jiko….
kisha akachukua sufulia lingine akaanza kuosha utumbo kisha akaubandika jikoni huku akisema,,” mme wangu leo umechelewa yani supu ilikuwa imekaribia kuisha alafu leo wateja ni wengi sana si unajua ni weekend(siku ya mapumziko)
*****************
Upande mwingine alionekana muuza maziwa akiwa amebeba mitungi iliyokuwa na maziwa ndani yake….mitungi hiyo iliyotengenezwa kwa bati la aluminiamu…alikuwa kaifunga vyema kwenye kiti cha nyuma……..huku akiendesha baiskeli…..akapiga kengere huku akipaza sauti,,”MAZIWA MAZIWA MAZIWA….mtu huyo hakuwa mbali na nyumbani kwa Tina..
wakati huo huo Domy alionekana akinyanyuka kitandani ili akamwambie tina kuwa yeye anajisikia kula mboga kavu isiyokuwa na mchuzi..
Wakati huo huo Tina alionekana akiendelea kuandaa chakula..ghafla akastuka baada ya kusikia sauti ya kengere akaanza kubadilika,,macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu……ghafla kisu alichokuwa amekishikilia mkononi kikadondoka chini kutoka mkononi…..akanyanyuka na kusimama wima akazipiga hatua za taratibu ghafla akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya yule muuza maziwa….
yule muuza maziwa akastuka akashika breki ya ghafla baiskeli ikaserereka na kuanguka chini….Tina akamkamata na kunyinga kwa kutumia kamba yake….kisha akatoweka kimiujiza…..akajitokeza nyumbani kwake…..baada ya sekunde kadhaa akarudi katika hali yake ya kawaida…akawa anajishangaa ghafla Domy aliingia jikoni akamkuta Tina kasimama huku anaonekana kuushangaa mwili wake..
Domy akauliza,,,”umepatwa na nini mbona unainekana kujitazama mwili wako????
Tina hakujibu kitu alibaki kimya…ghafla fahamu zikarudi akastuka sana nusu akimbie….
***************
upande mwingine kule aliponyongwa muuza maziwa……kwa mbali lilionekana gari la Mzee sule likiishirizi kwenye kona huku limebeba baiskeli upande wa nyuma ya gari…..
Kule nyumbani kwa Domy….Tina aliamua kumdanganya Domy kuwa kichwa kinamuuma..huku akijishika usoni..Domy aliogopa akaamua ampeleke hospitali haraka..akamchukua Tina huku ameuweka mkono wa Tina Begani kwake wakazipiga hatua kuelekea kwenye gari ili waende hospitali….Domy aliliwasha gari na kuliondosha kwa kasi.
wakiwa njiani karibia kwenye mataa…walikuta foleni ikawalazimu wasubiri foleni…
pembeni kulikuwa na gari jingine limesimama..ndani ya gari hilo kulikuwa na familia alikuwemo Mwanamke Mtoto pamoja na baba wa mtoto ambaye aliyekuwa akiliendesha gari hilo….kulikuwa na vitu vingi vya kuchezea mtoto wao ndani ua gari hilo ghafla yule mtoto akachukua kengere ya kuchezea watoto…….mtoto hiyo aliitingisha kengere ile kwa kuigonga gonga kwenye kiti cha gari….ghafla Tina akasikia mlio wa kengere hiyo…..akastuka
Domy alitoa simu yake aina ya SAMSUNG NOTE 4
akampiga picha Tina…kitendo cha mwanga wa flash kuwaka kikazuia hali ya tina kubadilika…ghafla taa za alama za barabarani zikaruhusu magari yaliyokuwa uoande wa kushoto kuendelea na safari…kabla hawajafika mbali tina akasema,,” turudi nyumbani najisikia nafuu…Domy hakutaka kumpinga Tina…akakatisha kona na kuingia kwenye barabara nyingine…akiiacha ile barabara iliyokuwa ikielekea hospitali….Domy aliendelea kuzipanga gia huku akiliendesha gari lake kwa mwendo wa wastani…..
wakiwa njiani Tina akasema,,”Tupitie kariakoo kuna duka fulani hivi nikaangalie kama wameshaleta mapazia mapya….Domy akajibu,,”Sawa mke wangu kilenzi kisha akaliendesha gari mpaka kariakoo…..kutokana na msongamano wa magari kuwa mengi..Domy aliamua kulipaki gari kwenye hotel moja….ili Tina asguke aende dukani kwa sababu hapakuwa na umbali…….
wakati huo huo alionekana muhudumu wa hotel kwa upande wa jikoni akifunika chakula na kuzipiga hatua huku amekibeba chakula hicho kuelekea kwenye ngazi ya umeme(Lift) akaingia upande wa ndani mlango ukajifunga,,akabonyeza kitufe kilichoandikwa namba (6) lift ikaanza kupanda kuelekea juu….alipofika ghorofa namba sita akazipiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba (113) akabofya kengere iliyokuwa pembeni ya mlango huo..
Sehemu Ya 2
kule upande wa nje alionekana tina akizipiga hatua kuelrekea dukani..mara ghafla akastuka…akasita kuendelea kutembea akasimama…akaanza kubadilika macho yake yakaanza kutoa machozi…ghafla akatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere…..akajitokeza kwenye ile hotel juu ghorofa ya sita…..akazioiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba(113) alipofika akaingia upande wa ndani kimiujiza…..akamnyonga yule muhudumu pamoja na Mwanaume aliyekuja Hotelini humo kupumzika na mpenzi wake….baada ya Tina kufanya mauwaji hayo akatoweka kimiujiza na kujitokeza pale alipokuwa amesimama….Tina alionekana kujishangaa sana…..akahairisha kwenda dukani akazioiga hatua za harakaharaka kurudi kule lilipokuwepo gari la Domy…
wakati huohuo kabla Tina hajafika…alionekana Domy akiongea na simu,,ghafla salio likakakata akifungua mlango wa gari na kutoka upande wa nje …akazipiga hatua kuelekea madukani kununua vocha….
baada ya Domy kutoka Tina akafika akafungua mlango haraka na kuingia ndani ya gari…..akabaki humo akimsubiri Domy…
**************
Upande mwingine kule kwenye Mgahawa wa Mzee Sule walionekana wateja wakiingia na kutoka huku upande wa nje yakionekana magari mengi na Bodaboda zimepaki nje ya mgahawa huo……watu walifurahia supu iliyokuwa inapikwa kwenye mgahawa huo…..pamoja na ugali nyama choma…mishkaki ,,soseji na sambusa…kwa mbali alionekana mteja mmoja akinyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi na kumfuata mke wa Mzee sule……mtu huyo alifoka huku akisema….,,”yani tangu nimefika hamjaja kunisikiliza!!!haya nataka ugali nyama choma…nichomee uenye mafutamafuta kiasi usikaushe sana…weka pilipili nyingi….kisha akarudi kuketi pale alipokuwa ameketi mwanzo…
Upande mwingine kule kwenye Mgahawa wa Mzee Sule walionekana wateja wakiingia na kutoka huku upande wa nje yakionekana magari mengi na Bodaboda zimepaki nje ya mgahawa huo……watu walifurahia supu iliyokuwa inapikwa kwenye mgahawa huo…..pamoja na ugali nyama choma…mishkaki ,,soseji na sambusa…kwa mbali alionekana mteja mmoja akinyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi na kumfuata mke wa Mzee sule……mtu huyo alifoka huku akisema….,,”yani tangu nimefika hamjaja kunisikiliza!!!haya nataka ugali nyama choma…nichomee uenye mafutamafuta kiasi usikaushe sana…weka pilipili nyingi….kisha akarudi kuketi pale alipokuwa ameketi mwanzo…
Upande mwingine alionekana Mzee Sule….akitika nje ya nyumba yake iliyokuwa katikati ya pori kubwa huku amebeba matulubai matatu yaliyotengenezwa kama gunia,,akayarusha upande nyuma ya gari lake..akaingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake……
wakati huhuo kule lilipokuwa limepaki gari la Domy, alionekana Tina kujishangaa huku akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu!!!!!!
kwa mbali alionekana Domy akizioiga hatua kuja pale lilipokuwepo gari lake huku akiongea na simu..alipofika alifungua mlango na kuingia ndani ya gari….akaendelea kuongea na simu hiyi kwa dakika kadhaa,,alipomaliza akambusu Tina shavuni huku akisema,,”samahani mke wangu,, nilikwenda kununua vocha. Tina alibaki kimya akatabasamu…Domy akaliwasha gari wakaondoka kuelekea nyumbani….
walipotoka tu wakapishana na gari la Mzee Sule.likiingia ndani ya hoteli hiyo…Tina akastuka akamtazama kwa mshangao Mzee Sule…huku akijiuliza moyoni,”Mbona kama namfananisha huyu Mzee!!!sijui nishamuona wapi????Tina akabaki na mshangao kichwani mwake…huku Domy akiendelea kuzipanga gia kuelekea nyumbani…….
*****************
alionekana Mzee Sule akishuka kutika ndani ya gari lake na kuelekea ndani kabisa ya Hotel hiyo….akaimgia ndani ya ngazi ya umeme(lift)akabofya kitufe kilichoandikwa namba(6) alipofika ghorofa ya sita akazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba namba(113)huku ameshikilia ile mifuko mitatu mikubwa iliyotengenezwa kwa kutumia tulubai……akafungua mlango na kuingia upande wa nadani…..
baada ya Mzee sule kuingia ndani ya chumba hicho kwa mabali alionekana kijana mmoja akizipiga hatua za harakaharaka kumfuata Mzee Sule…..kumbe kijana huyo ni muhudumu wa Usafi upande wa vyumbani….akanyata mpaka mlangoni akachungulia upande wa ndani kwa kupitia tundu la ufunguo…..akastuka hofu ikamjaa alipogeuka ili akimbie mara ghafla……ikasikika sauti….
WEWE UNAFANYA NINI HAPO??? yule kijana alistuka kumuina Bosi wake…akazipiga hatua kuelekea upande mwingine…bosi akamuita kijana huyo……akazipiga hatua kumfuata bosi wake..alipomkaribia,, Bosi akauliza,,”tabia gani hiyo kuchungulia kwenye vyumba…wakati wateja wamepumzika??? kijana yule akajitetea kwa kusema,,”Bosi nahisi kuna mtu anafanya mauwaji ndani ya chumba hicho.!!!
wakati huohuo alionekana mzee sule mule ndani ya chumba akimalizia kuiweka maiti ya yule muhudumu wa kike,ndani ya ule mfuko mmoja uliobaki…kisha akatoa kichupa kilichokuwa na maji yaliyo onekana na rangi nyeusi..akamimina maji hayo kwenye kiganja na kujipaka mwilini….kumbe mzee sule akifanya hivyo,,hakuna binadamu wa kawaida atakayeweza kumuona yeye pamoja namaiti atakazokuwa amezibebe…
akabeba furushi la kwanza akatokanalo mpanje ya hoteli akaliweka nyuma ya gari lake……alipishana na watu lakini hawakuweza kumuona!!! kwa sababu alikuwa yupo katika hali ya kichawi…
akazipiga hatua kidudi kule ndani ya chumba namba(113) akachukua maiti ya pili akatokanayo na uitupia nyuma ya gari…akarudi tena..akachukua maiti ya yule muhudumu wa kike akatokanayo na kuitupia ndani ya gari…kisha akafungua mlango wa gari akaingia na kuliwasha akaondoka zake…watu waliokuwepo jirani na gari hilo walistahajabu kuina gari linaondoka wakati hawakumuina dereva akiingia ndani ya gari hilo….
******************
upande mwingine walionekana Seba na Tina wakiwa ndani ya gari wakielekea nyumbani,, wakapitia sehemu kununua Matunda…Seba akasema,,”Ebu nenda kaangalie maparachichi mazuri pia kama utapata ndizi mbivu chukua…akatoa noti ya elfu kumi na kumpa Tina…
Tina akafungua mlango wa gari na kuelekea ule ulande palipokuwa pakiuzwa matunda…
Seba alitoa simu yake ili abadilishe picha kwenye Facebook na kuweka ile picha aliyompiga Tina Tina…Seba alistahajabu kutokuiona picha ile ndani ya simu yake,,akajisemea moyoni,,”au sikuihifadhi??(save) nitampiga picha nyingine….
********************
Upande mwingine kule hotelini alionekana yule kijana muhudumu..akirudi kule ghorofa ya sita…ili akahakikishe kile alichokiona mara ya kwanza akazipiga hata kwa kunyatia alipoufikia mlango akacgungulia kwenye tundu la ufunguo lililokuwa kwenye kitasa….akastahajabu hakuona mtu yeyote yule….ikabidi afungue mlango ili ahakikishe…alipoingia upande wa ndani hakukuta mtu…akajisemea moyoni,,”mbona sijaona mteja yeyote akishuka kutika ghorofani!!!!! akaamua kutoka nje ya chumba hicho na kuendelea na shughuri zake nyingine..
*******************
upande mwingine kule alilipokuwepo gari la Seba alionekana akibofya bofya simu yake….kwa mbali akamuona Tina anakuja huku amebeba mduko uliokuwa na matunda ndani yake…Seba alimtazama Tina kwa macho ya matamanio…..na kwa jinsi Tina alivyokuwa amevaa kapendeza….Seba aliamua kumpiga picha Tina wakati tina akitembea…lakini Seba alishangaa kila anapompiga Tina picha,,haionekani kwenye simu..
Tina aliendelea kuzipiga hatua akafungua mlango na kuingia ndani ya gari…..Seba akamuoba Tina wapige picha ya pamoja kisha akamsogelea na kupiga picha kwa kutumia kamera ya mbele(Selfie) lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kupiga picha….Tina hakuonekana kwenye picha hiyo!!! alionekana Seba peke yake…kitendo hicho kilimfanya Seba astuke akawa na masha na mkewe Tina….Seba akaliwasha gari,,wakaondoka zao kuelekea nyumbani…
Tina alionekana kuwa na wasiwasi,,”alijiuliza maswali wa na majibu…..kunamatukio yakawa inazunguka kwenye ubongo wa Tina akawa anaona mauwaji ya kikatiri ya binadamu wakinyongwa kwa kutumia kamba…ghafla Tina akapiga kelele…..baada ya kumuona Mzee mmoja katika hayo matukio yaliyokuwa yakizunguka kwenye ubongo wake!!!! akageuza shingo yake na kutazama upande wa nyuma…kumbukumbu ikamjia kuwa yule mzee waliepishana nae akiingia hotelini huku anaendesha gari aina ya TOYOTA PICK UP……….kipindi wanatoka kule kwenye hotel…Tina alionekana kushangaa kisha akasema kwa sauti ya taratibu kwa kutaja jina,,”SULE…akakumbuka Tukio la miaka Hamsini (50)iliyopita.
Seba alistuka sana kwa kile kitendo cha Tina kupiga kelele….akauliza,,”unatatizo gani??
Tina hakujibu kitu,
baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani..
**************
Upande mwingine alionekana Mzee Sule akiwa ndani ya gari lake akiliendesha huku akionekana kuwa na furaha….
baada ya dakika chache akafika nyumbani kwake akashusha maiti zile tatu na kuziingiza ndani ya kile chumba chake alichokitumia kukatakata nyama….kisha akatoka upande wa nje akaliwasha gari lake na kuelekea kule kwenye Mgahawa wake.
alipofika alilipaki gari na kuingia ndani ya mgahawa…akapitiliza mpaka uoande wa jikoni
Watu waliendelea kunywa Supu matata na nyama choma iliyokuwa na utamu wa aina yake…..akainekana mtu mmoja akiingia ndani ya mgahawa huo…akaketi kwenye kiti..akaagiza supu….baada ya sekunde kadhaa kupita supu ikaletwa…..yule mtu alipoitazama supu ile aliina kuna kipande cha pua ya binadamu…akastuka akaacha kunywa supu na kuzipiga hatua kutoka nje ya mgahawa huo..
kijana mkubwa ambaye ni mtoto wa Mzeee Sule
alimuona mtu huyo ameondoka na kuiacha supu mezani..akazipiga hatua mpaka pale mezani..alipoitazama supu ile alikiona kipande ya pua…ndani ya supu ile akaichukua na kurudi jikoni haraka akamueleza baba yake…
Mzee Sule akatoka jikoni huku akizipiga hatua za haraka kutoka upande wa nje…akamuona yule mtu..akiondoka zake..
Mzee Sule akaingia ndani ua gari lake….na kuliwasha akaliendesha kwa mwendo wa taratibu kumfuata mtu huyo kwa nyuma…..alipo mkaribia
akapunguza mwendo wa gari..yule mtu alipogeuka kutazama nyuma ili aone ni nani anaye endesha gari nyuma yake…ghafla mzee Sule aliongeza mwendo akamgonga na gari mtu yule o chini kisha akarudisha gari nyuma haraka akamkanyaga kwa magurudumu….
mtu yule akapasuka kichwa ubongo ukamwagika chini…mzee sule akashuka haraka kutoka ndani ya gari akachukua maiti ile huku akilalamika kwa kusema,,”yani ubongo wote umemwagika siwezi kuuacha huu ukichanganya kwenye supu inakuwa amazing (supu tamu ya kushangaza) akauzoa ubongo uliokuwa umemwagika chini.akauweka ndani ya mfuko wa plastiki kisha akauweka juu ya maiti ile aliyoiweka nyuma ya gari lake akaimwagia ile dawa iliyokuwa kwenye kichupa kisha na yeye akajipaka mwilini ili asionekane kama kabeba maiti…..akaliwasha gari na kuondoka zake kuelekea kule mstuni,,ilipokuwepo nyumba yake….
***************
Upande mwingine alionekana Domy pamoja na Tina wakiwa chumbani mwao…lakini Domy alioneka kuwa na wasiwasi juu ya Tina..alijiuliza kwa nini Tina akipigwa picha haonekani kwenye picha!!!
Tina aliona kuwa Domy hayupo sawa…yupo katika hali tofauti na alivyozoea kumuona akiwa mchangamfu muda wote..Tina akauliza,,”mbona leo nakuona kama unamawazo!!! nini kinakusumbua???
Domy hakujibu kitu alibaki kimya huku akimtazama Tina…Tina alianza kuhisi huenda kuna jambo baya ambalo yeye kalifanya halijampendeza Domy…..Tina akaanza kuomba msamaha huku akilia…….Domy akauliza mbona nikikupiga picha hauonekani kwenye picha inakuwa kivuli??? Tina akastahajabu sana…..akasema,,”mmh! embu nipige picha tena…
wakati huohuo upande mwingine walionekana watu wawili wakitembea barabarani wakiwa wamelewa…wakakatisha kona na kubofya kengere iliyokuwepo pembeni ya geti…..wakaendelea kubofya kengere hiyo huku wakifoka kuwa,,kwanini watu waliopo ndani wanachelewa kufungua geti..
****************
kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akimwambia Domy ampige picha ili ahakikishe je? ni kweli akipigwa picha haionekani…
wakati huohuo walionekana wale walevi wakiendelea kubofya kengere…ghafla Tina akastuka akainama kutazama chini alipoinua uso wake macho yake yalikuwa yanatoa machozi ya damu…wakati Tina anainua uso wake ndio wakati Domy alikuwa kabofyaa kitufe cha kupigia picha.mwanga ukawaka(flash) mwanga ule uliizuia ile hali ya tina kuendelea kubadilika akarudi katika hali yake ya kawaida….akaonekana kujishangaa…..Domy alipoangalia simu yake ile picha ilionekana kivuli tu…..akastuka sana akamtazama tina akamuona Tina akijishangaa kwa kujitazama mwili wake..
***************
upande mwingine kule kwenye mgahaw wa Mzee sule..wateja walionekana kulalamika kwamba supu matata leo imekwisha mapema….walitoa lawama hizo kwa mke wa mzee sule…..ikabidi mke wa mzee Sule amwamvie mwanae mkubwa kuwa aende nyumbani akaangalie kama Mzee Sule kaleta nyama…ye kijana akafungua na kuingia kwenye ule mlango wa siri,,,akapitia njia ya chini kwa chini ya aridhi kuelekea nyumbani kufata nyama,,ailete ili supu ibandikwe jikini haraka..
baada ya dakika kadhaa kijana huyo alitokezea nyumbani akafungua mlango wa siri na kuingia ndani ya nyumba..akamkuta mzee Sule akiwa anakatakata na kutenganisha viungo vya maiti…akasema,,”baba fanya haraka wateja wanasubiri supu..alafu pia miskaki imekwisha ugali umebaki mwingi….
mzee Sule akacheka na kusema,,”kunaubongo nimeuweka ndani ya ndoo ebu usafishe kwa kuuosha ili mchanga utoke….kijana yule akafanya kama alivyoagizwa na baba yake….
baada ya dakika tano mzee Sule alikuwa tayari ameshamaliza kukatakata nyama….akaiweka kwenye ndoo na kumpa kijana wake apeleke haraka nyama hiyo kule kwenye mgahawa…
yule kijana aliondoka na kuelekea kule kwenye mgahawa kwa kupitia ile njia ya chini kwa chini ya aridhi…alipofika akaiosha ile myama huku akisaidiana na mama yake pamoja na mdogo wake kisha akachukua nyama kiasi akaiweka kwenye jiko kwa ajili ya kuichoma…….
ghafla kunamteja akaja na kusema nikatie nyama ya elfu kumi isiyokuwa na mifupa…kisha ikaushe usiikatekate…. niletee pamoja na ugali…kijana yule aliichoma nyama na ilipoiva akaiweka kwenye sahani pamoja na ugali…kumbe nyama ile ilikuwa ni sehemu ya kifua,,,yule mtu aliyeuwawa alikuwa kajichora tatuu(mchoro wa rangi usiofutika)….kutokana na harakaharaka ya mtoto wa mzee Sule ili awaishe nyama kwa mteja hakuweza kuona tatuu hiyo…yeye aliweka nyama kwenye sahani akapeleka moja kwa moja mpaka mezani kwa ye mteja aliyeagiza nyama hiyo…
wakati huo huo kule nyumbani kwa Domy…Tina alikosa amani kwa maswali aliyokuwa akiuliza Domy…Tina alishindwa kujibu kutokana yeye hafahamu chochote….haijui siri nzito iliyopandikizwa mwilini mwake……
wakati huohuo walionekana wale walevi wakigonga geti kwa nguvu….ye mle mmojawapo akabonyeza kengere kwa mara nyingine tena…
Domy akiwa anamuuliza Tina maswali mara ghafla Tina akastuka….akainamisha uso wake chini……Dimy alikasirika sana aliona kama Tina kamdharau kuwa yeye anamuongelesha alafu Tina kainamisha uso wake chini….Domy akaamua kumsogelea Tina huku amenyanyua mkono ampige kofi….
Tina alipoinua uso wake, Domy alishtuka macho yakamtoka alistaajabu kumuona tina amebadilika huku macho yake yanayotokwa na machozi ya damu,Domy akatimua mbio kuelekea chumbani wakati huo huo wale walevi waliendea kubofya kitufe cha kengele,Tina akatoweka kimiuzija kuufuata mlio wa kengere.
Sehemu Ya 3
wakati huohuo ule upande mwingine walionekana wale walevi wawili..kisha mmojawapo akazipiga hatua kadhaa akasimama kando na kuanza kujisaidia haja ndogo…ghafa akajitokeTina akiwa kwa mbali kidogo kutoka hapo walipo walevi hao…..akazipiga hatua kuwafuata…..yule mlevi aliyekuwa akijisaidia haja ndogo akamuona Mwanamke akija upande wao huku ameinamisha uso wake chini…..yule mlevi akaingiwa Tamaa ya kutaka kumtongoza Tina…akafunga zipu haraka haraka.akasimama huku anayumba yumba kwa ulevi…Tina alipomkaribia yule mlevi akamfuata..ghafla Tina akainua uso wake…ye mlevi akastuka akaogopa sana Tina akamkamata na kunyonga kwa kutumia ile kamba yake….wakati huohuo yule mlevi mwingine akageuka akaogopa sana kumuona mwenzake ananyongwa….pombe zikamruka,,akaanza kutimua mbio..alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea..Tina akajitokeza mbele yake…akamkamata akamnyonga kwa kutumia ile kamba…….kisha akazipiga hatua kadhaa akatoweka kimiujiza…..baada ya sekunde kadhaa akajitikeza nyumbani..akawa anajishangaa..
********************
wakati huohuo Domy alionekana akiwa kajifungia chumbani huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu…jasho lilimtoka mfululizo…akaona chumbani hapakaliki,,akaamua kufungua mlango wa chumbani akachungulia kule upande wa sebuleni..akamuina Tina yupo katika hali yake ya kawaida huku akionekana kujishangaa….Domy akatoka chumbani huku akizipiga hatua za tahadhari..alitembea huku macho yake yakimtazama Tina…alipomkaribia akamuita Tina kwa sauti ya chini,,Tina…Tinaaaa
Tina akastuka akamtazama Domy…hali yake ya ufahamu ikarudi akaitika,” Abee mume wangu.
Domy hakutaka kuuliza kitu chochote akaogopa hata kumsogelea…..Tina alijisikia vibaya,,alitamani kujua ni nini kimetokea lakini alishindwa jinsi ya kumuuliza Domy….Tina akaamua kuzipiga hatua kuelekea chumbani…akamuacha Domy kasimama palepale sebuleni,,Domy akajiuliza,,”yawezekana Tina ni jini…au niliona vibaya…mmh!! lakini sidhani kama macho yangu yalinidanganya….
***************
Upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee Sule…..alionekana yule mtu aliyeafiza ugali nyama choma akiendelea kula ugali pamoja na nyama hiyo matata….akapaza sauti,,”niletee chumvi na ndimu….pia niongezee pilipili..aliyasema maneno hayo huku akiendelea kutafuna minofu ya nyama……baada ya sekunde kadhaa kupita aliletewa vitu alivyoagiza…akachukua ndimu akakamulia kwenye nyama ile..kisha akaweka na pilipili..akachukua mnofu mwingine akala pamoja na tinge la ugali….ghala kunakipande cha nyama(mnofu) aliuona kama haujaiva vizuri ulikuwa haujakauka…akastuka akakitazama kwa makini akaona mchoro….akajisemea moyoni,,”mmh!!! mbona kama inaonekana ni tatoo! ng’ombe gani huyu alichorwa mchoro wa tatuu ambayo huchorwa kwenye mwili wa binadamu??
kutokana nyama ile ilikuwa imeshachomwa alafu imekatwakawa vipande…mchoro ule haukuonekana wote..ulionekana nusu tena kwa mbali sana…mtu yule akajipa moyo kuwa hiyo ni nyama ya ng’ombe..hakuwa na shaka kuwa kwenye mgahawa huo awawezi kupika nyama ya binadamu…….akajisemea moyoni,,”yawezekana mmiliki wa mgahawa huu ni mfugaji…itakuwa anang’ombe nyingi sana…..hata hivyo wanachoma nyama vizuri tamu sana..ndio maana watu wanajazana kula kwenye mgahawa huu usiku na mchana..
wakati huohuo alionekana mzee sule akiwa barani anaendesha gari lake…akakatisha kona na kutokezea kwenye ile nyumba ambayo wale walevi wawili walinyongwa na Tina..akachukua maiti zao na kuzirusha nyuma ya gari…kisha akaingia ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake…..
******************
Upande mwingine alionekana Domy akizipiga hatua za taratibu kuelekea chumbani…lakini alikuwa na hofu na wasiwasi kuhusu Tina huenda akamdhuru….akafungua mlango na kuingia chumbani akamkuta Tina amevua nguo kabaki mtupu(uchi) kajilaza kitandani……pia Domy akapanda kitandani,,kutokana na umbile la Tina kuwa na mvuto wa aina yake Domy akapata hamasa ya kuanza kumpapasa Tina…..akasahau yale yote aliyotoka kuyaona muda mchache uliopita…..Tina hakutambua wala kujua chochote kilichotokea kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kujitambua na kujizuia anaposikia mlio wa kengere…….
***************
upande mwingine walionekana maaskari wakiwa katika gari la polisi wakifanya doria kwenye mitaa usiku huo.wakakatisha kona na kuliegesha gari lao kando ya barabara kisha wakashuka kutoka ndani ya gari wakasimama barabarani kuhakikisha kila gari inayopita lazima ikaguliwe…..kumbe kunatukio la ujambazi limefanyika muda mchache uliopita ala majambazi wakakimbia na kuondika enei la tukio wakiwa na gari aina ya TOYOTA PICK UP.
wakati huohuo alionekana mzee sule akikatisha kona kuifuata barabara hiyo ambayo wale maaskari walikuwepo…aliliendesha gari lake bila wasiwasi akaingia kabisa kwenye barabara..
pande mwingine walionekana maaskari wakiwa katika gari la polisi wakifanya doria kwenye mitaa usiku huo.wakakatisha kona na kuliegesha gari lao kando ya barabara kisha wakashuka kutoka ndani ya gari wakasimama barabarani kuhakikisha kila gari inayopita lazima ikaguliwe…..kumbe kunatukio la ujambazi limefanyika muda mchache uliopita ala majambazi wakakimbia na kuondika enei la tukio wakiwa na gari aina ya TOYOTA PICK UP.
wakati huohuo alionekana mzee sule akikatisha kona kuifuata barabara hiyo ambayo wale maaskari walikuwepo…aliliendesha gari lake bila wasiwasi akaingia kabisa kwenye barabara.
akaliendesha gari mara ghafla akasimamishwa na maaskari waliokuwa kwenye doria..Mzee Sule akastuka…akajisemea moyoni,,”nimefanya ujinga sijajipaka dawa…akaonekana askari mmoja akizipiga hatua pale lilipokuwepo gari la mzee Sule……mzee sule akafungua mlango na kutoka nje ya gari akajifanya anajisaidia haja ndogo nyuma ya gari akatoa haraka ile dawa iliyokuwa ndani ya kichupa kidogo akaimwaga kiasi kwenye zile maiti mbili za wale walevi kisha akajipaka dawa hiyo mwilini haraka..yule askari alipolikaribia gari la mzee Sule,,,,akastahajabu kutomuona mzee Sule wakati kamuona sekunde kadhaa zilizopita akitoka ndani ya gari na kuelekea upande wa nyuma ya gari….yule askari akaanza kuingiwa wasiwasi akawa na mashaka na mzee Sule….akaiweka bunduki yake mkao wa tahadhari…akazipiga hatua za taratibu huku kaielekezea bunduki yake lilipokuwepo gari la mzee Sule……alipotazama kwa makini hakuweza kumuona mzee Sule kwa sababu mzee Sule alikuwa amejipaka ile dawa yake ya kichawi ili asionekane…..
wakati huo mzee Sule alikuwa akimtazama yule askari huku akimcheka kwa kejeri…lakini askari hakuwa na uwezo wa kumuona mzee Sule…ghafla akaona gari linawashwa bila kumuona dereva anayewasha gari hilo….mzee Sule akaweka gia na kuliondosha gari kwa mwendo wa wastani….
yule askari alipo ona hivyo akaogopa sana akajiuliza,,”yawezekana vipi gari kujiendesha lenyewe pasipo dereva!!!! akaamua kutimua mbio kuelekea kule walipokuwepo wenzake…alipowakaribia akapaza sauti kwa kusema,,”jamani jiniii……
wale maaskari wenzake wakatimua mbio wakasahau kama walikuja na gari…..walikimbia na kutokomea kusikojulikana…..mzee Sule akacheka sana kisha akapiga mluzi huku akiliendesha gari lake na kuelekea kule mstuni ilipokuwepo nyumba yake…aliendesha gari kwa mwendo wa nusu saa akaanza kuingia kwenye msitu…..baada ya dakika kadhaa alifika nyumbani kwake….akazishusha zile maiti mbili kutoka ndani ya gari na kuziingiza ndani ya nyumba,,akazivuruta mpaka kwenye kile chumba anachokitumia kuandaa nyama kwa ajili ya mishkaki na soseji,,,sambusa pamoja na supu flani hivi amazing(supu matata) akachukua maiti moja akaibeba na kuilaza juu ya mweza….akachukua shoka akaanza kukata miguu na mikono…..akaweka kando,, kisha akachukua upanga akakata shingo na kukitoa kichwa akakiweka pembeni…akachukua kisu akatoboa tumbo akatoa utumbo huku akisema,,”huyu mtu inaonekana alikuwa mlevi sana..kinyesi chake kinanuka pombe tupu….kisha akauweka utumbo kwenye ndoo…akachukua shoka akapasua kichwa akatoa ubongo na kuuweka kenye sufuria..kisha akaanza kukatakata kata maiti ile vipande vipande kwa kutumia uoanga mkali..huku akijisemea moyoni..,,”huyu mlevi alikuwa hali vizuri nyama yake kavu haina mafuta mafuta……alisema maneno hayo huku akikatakata nyama na kuiweka ndani ya ndoo.
***************
upande mwingine kule kwenye mgahawa walionekana watu wengi wakipata huduma ya chakula..wengine wakila ugali nyama choma,,wengine wakila soseji..na wengine walila sambusa na supu matata….watu walikuwa wengi sana,,hakuna kiti kilicho onekana kipo tupu..watu wengine walikuwa wakinywa supu huku wamesimama….sauti za watu zilisikika wakiisifia supu na nyama choma walisema chakula kinachopikwa kwenye mgahawa huo ni kitamu sana…..
*********************
Asubuhi palipokucha Tina alidamka amechelewa kuliko siku zote..akanyanyuka kitandani akaingia bafuni kuoga…akamuacha Domy bado kalala..kwa sababu siku ya leo ilikuwa ni jumamosi hivyo Domy hakwenda kazini kwa ajili ya mapumziko..
wakati huohuo nyumba iliyopo kando kando ya nyumba ya Domy alionekana jirani aingia nyumbani kwake akiwa na fundi umeme…siku ya leo jirani huyo aliamua kuweka kengere mlangoni kwake….fundi akatoka nje na kuanza kuifunga kengere ile kwenye ukuta kando kidogo ya mlango.
kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akitoka bafuni nakuanza kujifuta maji..akavaa nguo na kutoka akaelekea jikoni kuandaa chai….
wakati huohuo ule upande mwingine alionekana
yule fundi akimalizia kuifunga kengere ile pale ukutani….kisha akajaribu kubofya kitufe cha kengere aone kama itatoa mlio….alipobofya kengere ile haikutoa mlio wowote,,akahisi huenda atakuwa amegeuza nyaya..akaamua kuifungua na kuanza kuifunga upya..
wakati huohuo alionekanna Domy akiamka kutoka usingizini…akazipiga hatua kuingia bafuni kuoga…
wakati huohuo kule jikoni alionekana Tina akiendelea kuandaa chai…..
kule nje akaonekana yule fundi akimalizia kuifunga ile kangere..kisha akabofya kitufe cha kengere..ikatoa mlio……yule fundi akakusanya vifaa vyake na kumuita yule jirani ili amlipe pesa ya ufundi aondoke zake….
kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina kustuka
akainamisha uso wake chini akaanza kubadilika..macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu..akaatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere….akajitokeza mbele ya yule fundi
wakati huohuo alionekana Domy akitokea upande wa chumbani na kuelekea upande wa jikoni ili amuage Tina…alipofika alishangaa kutomuona Tina…akaamua kupaza sauti huku akimuita Tina…alipo ona Tina haitiki akaamua kutoka upande wa nje huenda Tina akawa huko…alipotoka upande wa nje..akaangaza angaza macho…mara ghafla akasikia sauti ya mtu akikoroma kama amekosa hewa au pumzi….akageuza shingo yake ukutazama ule upande ilipokuwa ikitokea sauti hiyo….
Tina akatoweka kimiujiza kabla Domy hajageuka akajitokeza sebuleni…..Domy alipotazama akastuka kumuona fundi anadondoka chini…akaogopa sana akaamua kurudi ndani haraka..hakutaka kuwa shuhuda kabisa…alipoingia upande wa ndani akastuka kumuona Tina anajishangaa mwili wake…Domy akafoka kwa kusema,,”Leo nataka uniambie kwa nini huwa unajishangaa mwili wako!!!unamatatizo gani???
Tina alibaki kimya bila kujibu kitu chochote..Domy akauliza tena,,,kwa sauti ya ukali zaidi..,,”Hivi Tina mbona umeanza kuwa na kiburi? yani nakusemesha alafu wewe unakaa kimya unamaana gani???kama umechoka kuishi na mimi ni bora uondoke..na sio kunifanyia Dharau…UMENISIKIA??
Tina akastuka hali yake ya ufahamu ikarudi..akastuka kumuona Domy akifoka kwa sauti ya ukali..
*********************
Upande mwingine kule kwenye nyumba iliyopo kando ya nyumba ya Domy…alionekana yule jirani akitokea ndani kuja upande wa nje…alipofungua mlango.akastuka akaogopa sana kumuina fundi amelala chini huku ulimi wake uko nje..na macho yamemtoka kama anatazama kitu kwa mshangao.
jirani akaingiwa na hofu akaamua kurudi upande wa ndani ili apige simu kwenye vyombo vya dora..wakati anaingia ndani kwa pupa akatereza kwenye marumaru/vigae nusu adondoke akawahi kushika ukuta..akabofya kitufe cha kengere bila yeye kujua…kengere ikatoa mlio….
wakati huohuo kule ndani ya nyumba ya Domy alionekana Domy kuendelea kufoka mara ghafla Tina akastuka..baada ya kusikia mlio wa kengere.
akainamisha uso wake..akaanza kubadilika,macho yake yakaanza kutoa machozi ya Damu..aliponyanyua uso wake Domy alistuka akapata uwoga wa hali ya juu..hakuwahi kumuona Tina akiwa hivyo katika sura ya kutisha..ghafla Tina akatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere….Domy akatimua mbio …… tangu azaliwe hakuwahi kuona binadamu akitoweka katika mzingira ya kutatanisha ndani ya sekunde moja….alihisi kuchanganyikiwa akasahau mlango wa kutokea upande wa nje akakimbilia chumbani.
akajifungia..
wakati huohuo alionekana Tina kujitokeza nje ya nyumba ya jirani…akazipiga hatua mpaka mlangoni..akatoweka kimiuhiza akajitokeza upande wa ndani ya nyumba…akamkamata yule jirani akamnyonga kwa kutumia ile kamba…
*****************
upande mwingine alionekana mzee Sule akiwa ndani ya gari lake akiliendesha kwa kasi ya ajabu utadhani anaendesha gari la kubeba wagonjwa mahututi(AMBULANCE),,,akakatisha kona kuelekea kwenye barabara inayokwenda kwenye mtaa anaoishi Domy….
wakati huohuo alionekana Domy akiwa chumbani kwake kasimama..huku akitazama huku na kule..kwa kuhofia huenda Tina ataingia chumbani na kumdhuru…akaona ndani hapakaliki akaamua kutoka chumbani akatembea hatua za kunyatia..huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa…mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi ya ajabu….hofu ikazidi kuongezeka..alipoukaribia mlango akafungua haraka akatoka upande wa nje na kuanza kutimua mbio…Domy alikimbia kwa kasi,utadhani anakimbia kwenye mashindano ya mita mia(100)
akaliparamia geti akafungua harakaharaka..akatoka upande wa nje…akaendelea kukimbia kwa kasi huku akitazama upande wa nyuma..mara kwa mara huenda Tina akawa anamfatilia…..wakati huohuo alionekana mzee Sule akiliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu….Domy aliendelea kukimbia huku akigeuza sgingi yake upande wa nyuma…alipofika kwenye kona..ndio wakati mzee Sule alikuwa anakatisha kona kuelekea uoande aliotokea Domy..ghafla akamgonga na gari!!Domy akarushwa juu kutokana gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi…alipotua chini alidondoka na kuangukia kichwa akavunjika shingo pamoja na uti wa mgongo..Domy akafa palepale…
****************
upande mwingine alionekana Tina akijitokeza ndani ya nyumba ya Domy…na baada ya sekunde kadhaa akaanza kujishangaa huku akiutazama mwili wake…..
wakati huo huo kule barabarani alionekana Mzee Sule akishuka kutoka ndani ya gari..huku akijisemea moyoni,,”mungu mkubwa yani kitoweo kimejileta chenyewe bila kutafutwa..akaichukua maiti ya Domy na kuirusha upande wa nyuma ya gari..kisha akaingia ndani ya gari..akaliwasha na kuendelea na safari yake…..akaonekana akilipaki gari nje ya nyumba ya jirani yake Domy….akashuka na kuichukua maiti ya fundi pale nje ya mlango..akaipeleka kwenye gari lake na kuirusha upande wa nyuma….akazipiga hatua mpaka kwenye mlango wa jirani yake Domy..akaufungua akaingia upande wa ndani..
baada ya sekunde kadhaa kupita akatika na maiti huku ameibeba begani..akazipiga hatua kulifuata gari lake…akairusha maiti ile nyuma ya gari….
wakati huohuo alionekana Tina amerudi katika hali yake ya ufahamu…akakumbuka kuwa mume wake Domy alikuwa akimfokea akagisi huenda amemkosea akaamua kuingia chumbani kwenda kumuomba msamaha….akastahajabu hakumuona Domy mule chumbani..akaamua kutoka upande wa nje huenda Domy yupo nje ili amuombe msamaha..alipotoka nje akaangaza angaza macho huku na kule ghafla akamuina mzee Sule…
akili ya Tina ikaanza kuzungukwa na kumbumbumbu ya ya tukio la miaka Hamsini (50)
iliyopita…..katika mawazo hayo yaliyokuwa yakizunguka kwenye ubongo wake akamuona mze Sule!!! ndani ya fikra hizo akasema kwa sauti ya chini chini Sule!!!!..Tina akastuka…..alipotazama tena ule upande lilipokuwepo gari la mzee Sule ili aende amuulize kitu…akamuona analiwasha gari na kuliondosha kwa kasi….Tina alipojaribu kuita..akasita macho yakamtoka alipomuona mumewe Domy akiwa amelala nyuma ya gari huku akionekana kutapakaa Damu…..Tina aliweza kumtambua Domy kutokana na nguo alizokuwa amezivaa siku hiyo…Tina akapiga kele kwa sauti kali akisema,,”simamisha gari…..
mzee sule aliliendesha gari bila kusimama akatokomea kusikojulikana…….Tina akarudi upande wa ndani huku akilia kwa uchungu..ghafla akasita akanyamaza kulia…kumbe Tina hatakiwi kuwa na hali ya mshtuko wa ghafla…hali hiyo ya mshtuko ikamfanya akaanza kubadilika..na kuwa kiumbe wa kutisha zaidi… akazipiga hatua kadhaa akatoweka kimiujiza…
Upande mwingine alionekana mzee Sule akiliendesha gari lake kwa kasi..kabla hajafika mbali…akapunguza mwendo akalipaki kando ya barabara..akashuka kutoka ndani ya gari akatoka nje haraka akatazama kushoto kulia,,ili aone kama kuna mtu anamuona…alipogundua eneo hilo hakuna mtu yeyote anayeshuhudia..akatoa kile kichupa kidogo akanyunyizia zile maiti kisha akajipaka mwilini mwake….akafunga mfuniko wa kichupa hicho akaingia ndani ya gari na kuondoka zake……akaelekea kule mstuni ilipokuwepo nyumba yake….
baada ya nusu saa kupita Mzee Sule alifika nyumbani kwake akachukua zile maiti na kuziingiza ndani ya nyumba yake moja kwa moja kwenye kile chumba chake anachokitumia kama bucha ( butcher) akaanza kukatakata nyama…..akatoa utumbo maini moyo na ubongo akaviweka pembeni kwa ajili ya supu matata..
akilpomaliza alichukua toroli dogo akaliingiza kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini…akachukua nyama na kuiweka kwenue toroli,,akaianza safari ya kuelekea kwenye mgahawa wake kwa kupitia njia hiyo ya siri..
INAENDELEA

