DOCTOR NIKUNE NA HUKU KUNAWASHA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 16
Shemu alinambia hayo maneno nami nikayaandika ,, zilipita sec kumi tu ujumbe ukaingia (safii kumbe huwa unaakili sana,, upo wapi) shemu akausoma akajibu (naelekea kwangu)
(Upo na nani??)
(Peke yangu kwani vipi) haikujibiwa hiyo sms ila simu iliita shemu akanambia nipokee nami nikapokea sauti ilikuwa ile ile ya kila siku
“Sikia Nasra, sihitaji chochote kutoka kwako zaidi ya penzi tu , najua jamaa yako sa hivi yupo kazini kama utawasiliana nae chochote kile nitajua afu ndio utajiharibia zaidi nina hadi ushahidi kuwa hiyo mimba ni yanguu ” moyo ulipaa juu mjinga huyuu nilipatwa hasira yaan nilisema nikimshika walah namkata kende zake mbwa huyuuš„š„
Shemu akanituliza nitulie kwanza niache hasira afu akaniandikia maneno ya kuongea “Mpago wako ni upii hakuna muda wa kutishana sa hivi kama nitakupa hilo penzi utaniacha kwa amani au utatumia hiyo kama njia ya kunitesa??”
.”nasra mimi ninaakili zangu timamu nipe huo utam bwana”
“Tunakutana wapi nije??”
“Nataka nyumbani kwako najua muda wa jamaa yako kutoka kazini kwahiyo hawezi kutukuta”
“Una uhakika??”
“Niamini mimi”
.”poa Njoo haraka nakusubiri ” nilikata simu fasta tukaondoka, shemu alikuwa anaendesha gari kwa speed ili tu tufike kabla yake , baada ya kufika mitaa michache shemu alinambia nichukue bajaji nikamuuliza kwahiyo wewe akanambia inatakiwa uingie peke yako sa ingine yupo getini anakutazama akiona wawili dili itaharibika we nenda mi nakuja nyuma nikasema poa ….
Nikafika om wakati nafungua geti msg ikaingia acha geti wazi kutoka kwa huyo mpuuzi nilitukana bonge wa tusi afu nikasonya ni kweli alikuwa tayari maeneo hayo kama shemeji alivyodhani. Nafika sebleni nashangaa nakumbatiwa kwa nyuma kugeuka sura niliyoiona mungu wangu ni yule kaka alinitea box ile siku daah
“Njoo basi tufanye fastaa” akanivuta kwenye kochi akawa anavua nguo yaan yupo haraka haraka kama vile mtu alietoka gelezani .
Nikiangalia dakika zinaenda shemu haji mmh moyo ukanambia sasa hapa akija abbas si ndio basi nakufa miee š„š„ nikawa naangalia geti kupitia dirishani akajua kuwa natizama getini , akanambia geti nimefunga kuwa na amani nipe basi chap chap nikamuuliza “we ni nani na unataka nini haswa”
“Nasra sitaki maswali nipe kama tulivyokubaliana basi nikiondoka hutanipata tena na huu ndo utakuwa mwisho wako”
“Nani anakupa taarifa zangu anakulipa au??” Niliamua kuwa mkali maana kama geti limefungwa shemu hawezi kupita kuingia ndani tena na hapo nitakuwa mimi nimecheza lafu
“Oyaaa unanipa hunipiii???” Nikajifikiria hapa nifanye nini nikainua simu yangu ili nimpigie shemu akaipiga ikaanguka chini, wakati bado nastaajabu alisukuma nikaanguka kwenye kochi akaja kuanza kunivua nguo zangu kwa hasra huku ananipiga makofi ilikuwa kukuru kakara vuta nikuvute ,huku naomba mungu mbona wazo la shemeji linakuja kuniangamiza kabisa jamani nilikuwa nalia naomba mungu aniokoe hapo …
Gafla mlango ulifunguliwa akaingia shemu jamani kama nilie kwa sautiiš nilikuwa nimebaki na tait ya ndani tu maziwa wazi shemu akanitupia nguo yangu nikajifunga haraka hata sikuvaa ilikuwa gauni yule kaka akataka kutoka mbio alimbananisha pale mlangoni , alimpiga ngumi za haraka haraka ndani ya sec tu uso haueleweki akamburuza akamtoa nje ,nikamwabia shemu Asante alifunga geti huyu mpuuzi nikajua nimeisha Akanambia usijali nimeruka ukuta ndo nikagundua nilimuona mguu anachechea ule mda anaingia ..
Aliniagiza kamba ndani akaniekeza zilipo nikaenda kuleta shemu wangu ananguvu aisee , Alimuweka kule nyuma kwenye mtu akamfunga kama mwizi afu akachua waya ulikuwa mrefuu alianza kumchapa ,,yule kaka analia hatoi sauti maana mdomo wake ulikuwa umefungwa na gundi , alimchapa zaidi ya masaa mawili bila kupumzika wala kuongea kitu hata swali moja hakuuliza alimchapa mgongo wotee ukawa na vidonda shati ikachanika aii mpaka nikawa naogopa kutazama moyoni nasema hawa wasudani wakatili mnoo sijui kwao damu kawaida , baada ya hapo ndo akamtoa ile gundi mdomoni afu akampa maji ya kunywa ,,, yule kaka alifakamia yale maji mpaka nikamuonea huruma
“Kaka naomba unisamehe,dadaa Nisameheni mimi mtoto wa mitaani tu ” alianza kuomba moyoni nikasema nyoo leo unaniita dada ulitaka huyu mtoto mi nikalee wapii??
Aidani alikuwa kimyaaa ,huyu kaka leo ndo nilijua kuwa ni mkatili aisee ,hakumjibu yule kaka aliomba na kuomba ,Aidan alichukua praizi alamshika mguu wake aliibana kuchaa ya dole gumbaa akaaanza kuivuta uchungu niliouhisi mimi nilitaka kuzimia š alipiga kelele moja kubwaaa
Nikasikia anasema “kaka sio mimi alinipa tu hela kaka maisha yangu ya mtaani tu nikakubali hela kaka lakini mi nilitumwa tuuu” yaan alijielezea bila hata kuulizwa kitu hapo aidani akaacha afu akamsogelea akamkenua meno et atoe jinoo walai mkono ulinipita nilijikuta namuogopa hata mimi
“Nani??? Nani alikuambia uje umsumbue huyu mwanamke???”
“Yule dada nesi simjui hata jina lakini anafanya kazi na mume wa huyu ndo alinipa akanambia kama nitafanya nitapata pesa na huwa ananlipia hakiamungu kaka angu mimi sio simjui huyu dada achukuaga tu maelezo kutoka kwa huyo nesi”
“Ndio anajua na alinambia kama nikija nipige picha nmtumie atanipa pesa nyingi “
“Kwahiyi na wewe ukapenda kubaka si ndio mgoja kwanza nikufunze adabu wewe afu ndo nimalize kwa huyo maraya “
“Kaka angu kaka angu walai naapa siwezi tena kurudia nisaidie niache kaka angu nitakufa mimi”
“Mpigie simu huyo mtu mwambie ushamaliza kazi na picha unazo fanya haraka na ole wako agundue kitu “
“Sa hivi yupo kazini huyu namtext tu “
“Fanya hivyoo” huyo kaka alichomoa simu anatetemeka mwili wotee damu kila kona yaan nilikuwa naogopa lakini baada ya kusikia Martha mpuuuzi huyo kwanini sasa ananifanyia mimi
Yule kaka alituma sms baada ya muda Martha akapiga ,aidani alipokea akaweka sauti “that’s Why nakupenda jembe langu fanya kunitumia hizo picha pesa yako ipo sawa”
“Sawa nakutumia ngoja nisogee mbali kidogo “
.”poa poa”
Baada ya kukata simu aidani alimpigia simu abbas
“Abbas unatoka sangp??”
“Nakaribia vipi kwan””
.”fanya ufanyavyo njoo nyumbani kwako na Martha kama marafiki mshawishi “
“Aah kaka siwezi kufanya hiyo kazi huyu mjinga sitaki mazoea nae”
“Abbas ninashida ya muhimu sana na huyu mwanamke please mdanganye hata wewe na mkeo hamna maelewano ” abbas alimuwa mbishi kweli lakini aidani alimshawishi mpaka akakubali kishingo upande
Lilipita lisaa tu shemu wakati huo akanipikia mwenyewe jamani sema anaroho ngumu mi mpaka alinitisha kweli ila wanajua mno kumjali mtu nikala zangu nikashiba wakat namalizia kula aliingia Martha akiwa na Abbas pale sebleni
Martha kidogo alishtuka kuniona hata sijui kwa nini ,aidani alimuwahi mkono Martha akamwambia abbas tufuate ,abbas hata haelewi huyo Martha ndo kabisa nilitamani hata kucheka mtu anavyoenda kudhalilika leo,aidan alimpeleka kule nyuma Martha alishtuka wala hakuficha mshtuko wake baada ya kumuona yule kakaaa…..
Chapter 17 & 18
MarthaĀ alishtuka mpaka simu yake ikaanguka chini wakati anainama kuichukua Aidan alimpiga bonge wa kofi la chogo alaanguka chini yaani mpaka nilicheka kwanza sikuwa nimetegemea hilo tukio nahivi alikuwa kavaa ki sistaa duu
Alipiga magoti chini akawa kama vile anataka kutambaa ,Alimkanyaga teke la mgongo akalala kabisa chini ,abbas alimvuta kaka ake pembeni kwanza
” kwani kuna nini mbona sielewi???” Abbas aliuliza kwa panick
“Utamwambia au mimi ndo nimwambie ??” Aidan alimuuliza Martha wakati huo abbas alikuwa anamuinua huku anamfuta futa ,nilichogundua ni kuwa abbas hana roho ngumu kama kaka ake abbas anahuruma sana
“Mi sijui hata kwanini nap…” kilikuwa kinajibia chenyewe sauti ya puani alikatizwa na bonge wa kofiii la mdomo mpaka damu afu akatoa simu ile ya yule jamaaa akapray ile voice ambayo Martha alikuwa akimpa maelezo yule jamaaa
Ndipo yule kaka aliongea mbele ya abbas mwanzo mwisho tangu Martha alivyomtafuta ili kuharibu mahusiano yetu , maskini nilimuonea huruma abbas hakuongea kitu akaja mbele yangu akapiga magoti tena machozi yanamtoka
“Nasra kipenzi changu naomba unipe nafasi nyingine hii ya mwanzo nimeiharibu sikuweza kukuamini hata kidogo hata ujauzito niliutilia mashaka, Nasra mama angu naomba unisamehe kwa kushindwa kusimama na wewe mimi pia nilichangia wewe kuwa na msongo wa mawazo nakuomba kwa dhati sintarudia huu upumbavu siwezi kurudia tenaa ” abbas alikuwa anaongea huku analia nilimuinua nikamkumbatia
“Nakupenda abbas nilijua naenda kukukosa nashkuru sana kila kitu kipo wazi sio leo tu hata milele siwezi kukusaliti abbas siweziii”
“Ukweli nakupenda sana Mke wangu that’s Why niliumia sanaaa kwa haya yaliyokuwa yanaendelea Nisamehe sanaaa”
Aidani alimpiga sana Martha sana sana mpaka abbas alimuambia awaache waende , akachukua gari lake akawapeleka wote wawili hospital na akagaramia kila kitu huduma zotee huku akimpa onyo kalii Martha asije kunikera hata kwa bahati mbaya…
Abbas akananbia kuwa kaka ake anamoyo mdogo sana hapendi yeye akelwe na mtu huwa anaweza hata kumuuwa mtu atakae tishia kunidhuru hata kwa bahati mbaya hiyo ndio sababu mimi huwa simuambii kama nina shida na mtu mana hapendi kabisa alinilea hivyo tulipo kuwa kwenye kituo cha watoto yatima tulikuwa tunaonewa sana kwahiyo alisimama kunitetea kila sehemu tangu huko nyuma”
Duh mwenyewe nilisisimkwa sana kwa habari zile …
Aidani alirudi usiku nyumbani akamfokea kweli Abbas kwa kushindwa kuwa pamoja na mimi yaan abbas ni mpole sana jaman alikuwa akiomba tu msamaha
“Inatakiwa umuoe Nasra haraka anaenda kuwa mama wa watoto wako sio vizuri mnakaa mnazini zini tu humu ndani wakati sheria za dini unazijua”
Weuweeeš„°š„°š„° kamoyo kangu kusikia ndoa kakadunda puuuhā¤š nikameza matee ..
“Sawa kaka nimekuelewa,, nasra upo tayari” aaawee sa nitasemaje sipo tayari auuuš š Nikasema “muda wowote unakaribishwa ” tena kwa mapozi hatari wee hakuna raha kama kuwaanzishia watu ukoo yaan hawa wasudani mimi ndo nawaanzishia familia badae unakuja kuwa ukoo wa Sultani aaaweeeš„°š„°š„° Raha kweliii ,kweliii, mimi ndio nitakuwa Bibi mkubwa wa ukoooš š ššš Nyie rahaaa …
Aidan akamwambia abbas tutoke mara moja baby akanambia mama k nikuletee niniii?? Aaaah weuweeeš„° et mama k nyie Rahaaa nikasema , basi hapo nikajidekeza na mimi et uwahi tu kurudiiiš “sawa mama k wangu” akanikiss wakatoka nikafunga geti yaan sitaki kabisa mgeni kwangu sitakiii wakome huko hukoš
Siku inayofata tuliondoka mimi aidani na abbas wangu mpaka nyumbani kwa mdogo wangu mbagala , nikawatambulisha Rasmi maana huwa namuhadithia tu mdogo wangu
Tulikaa siku mbili tukasafiri taboraaaššš„° unyamwezini kwetu nikawapeleka wasudan wangu basi watu vijichoo kila mtu anawatizama mnoo mimi na wasudani wangu huku abbas huku aidaniš¤š¤ nilikuwa najiona mimi mwanamke peke yanguuuš
Hapo mambo yakawa mwake tukafunga ndoa huko huko tabora , huku dar mdogo wangu nae hakutaka papoee mana tabora tulifunga ndoa isiyo na mambo mengi ..
Chapter 19
Tulikaa siku tatu nyumbani ndo tukasafiri kurudi Dar nikafikia kwenye nyumba ingine maana alinambia abbas pale tuhame nyumba ishakuwa na mkosi hiyo tukaamia kwa kaka ake yye alikuwa na bonge wa jumba mbezi beach huko tena Kanunua , Aidani na mdogo wangu wakaungana et wafanye sherehe kubwa , walialikwa watu mbali mbalii ..
Nami nikasema hata sipitwi nikachukua , kadi zangu tena kadi zangu ni VIP , mpaka bondeni kwetu kulee Vingugwe.
Nilimkuta Emmy yupo nje anafua na kitumbo cha mbalii nikajua shoga anamimba nikasalimia pale kulikuwa na wengine kibao basi wakanipokea pale unajua ile za siku nyingi eeh wakaniwao paleee .
Nami nilivyowaka nyiee nimengaa nimekuwa mzuriiiš„° ka mimba kamenikubali ninenawili sio poaaš
Nikamsalimia Emmy mambo” maana ile salama ya kwanza walijibu wengine yeye akawa kimya nilivyorudia akajibu
“Poa mambo Da Naah” et da naah kidogo nicheke, nikaingia chumbani kwangu kitambo jamani sijaingia tangu nitolewe mbio mbio na baby ile siku ..
Baada ya muda nipo zangu nafuta futa vumbi akaja shoga angu yulee Ile siku ya harusi ya amini nilienda kukaa kwake
“We umejuaje kama nipo hapa”
“Heheheh shoga angu taarifa zishazagaa Bonde lotee,,weee Naah umependezaaa naskia shemu ni mwalabu sijui nilipata umbea yaan nikakutafuta wapii shoga ukajua kutupa jongoo na mtu wake!!”
“Hapana shoga angu nilikuwa mbalii , afu mambo yakawa kibao”
“Una mimba eeeh”
“Heheh we umejuaje huachi umbea jamani khaa!!!”
“Nimekumbuka shoga ako si kakimbiwa na bwana kaibiwa kila kitu cha ndani kaachwa na mimbaa mdomo wote kutoaaa!!!”
“Weee Mungu wangu mika ndo kafanya hivyo??”
“Mwingine nani?? Aliona kapata mume anamaisha magumu kweli analala chini hapo yaan alichukuliwa kila kiti ndani hana mbele wa nyuma ” dah Roho iliniuma sana kusikia aliyofanyiwa emmy na mikaš„š„ masikini huenda ningekuwa mimi leo, Emmy nilikanaa vizuri kweli tangu dada ake anipatie nimuoneshe jiji wanaume wanajua kushawishi sana huenda alimdanganya tu .
Tulipiga story na shoga angu nikampa kadi ya harusi ambayo itakuwa ni sherehe itafanyika Ramada mbezi Beach kule ..
Baada ya yule dada kuondoka nikamuita emmy chumbani kwangu nikaongea nae kama mdogo wangu akanielezea yote mika alimuongopea anafanya kazi Bandari na ananyumba ila huko bandari kuna wizi ulitokea ndo wakasimamishwa kazi alikuwa akimuongopea kila siku lakini kumbe hakuwa na kazi yeyote na ni mwizi tu mtaani kaishia kumuibia kila kitu ndani hata akiba yake yote ndani aliibeba kamuacha hana kitu pia kamuacha na mimba.
Nilimuonea huruma sana nikamwambia emmy nimekuelewa lakini pole huenda mungu alikutumia wewe kuwa mfano sina hata haja ya kukuchukia , nilimpigia simu babydady nikamuambia yale ya emmy.
Japo hamjui lakini alimuonea huruma kweli kweli nikamwambia mi nataka nimuachie chumba changu mana hakina kazi tena pia nimpe hela ya mtaji ajitafute upya , baby akanambia yaan Nasra wangu unamoyo mpaka raha pamoja na yote lakini bado unampatia chochote kitu ..
Abbas alinisifia wee basi mi likichwaškulee navyopenda sifa sasaš
Nikamuita emmy nikamwambia kuwa nitampa chumba changu jumla na pesa ya mtaji, alinishukuru maskin mpaka nikawa namuonea huruma jamani mtoto wa watu ,
.aliniomba msamaha kila sec , niagawa kadi zangu mi nikachukua tu baadhi ya nguo nikamwachia kila kitu yaan hata kijiko sikuchukua nikampa na hela ya mtaji na Kodi ya miezi 6 …
Nikaenda kwa mdogo wangu hapo bado siku 3 tu ndo iwe sherehe ,abbas alinifata mida ya sa moja na piki piki mpaka Hom
Sa kesho yake yaan bado siku mbili hapo iwe sherehe Abbas aliniambia niende kuanza clinic huko huko Temeke hospital , nikaenda mpaka kule juu ambapo wao ndio ofisi zao zilipo si nikakutana na Martha kidogo nicheke alinisalimia mwenyewe tena kwa heshima wee nikamtumia msg baby nipo hapa nje akatoka akanihug na bonge wa kiss , shost anatuangalia tu nguvu zote alizotumia kututenganisha ndo kwanza katuimalisha mungu akiamua kitu kiwe hakuna kitu kinaweza kutenganisha mungu ndie kila kitu kwetu šš
Tulifanya sherehe yetu ilifanya ilihudhuriwa watu wa maana madoctor kama wote , wasudani ndo usiseme walikuwa kibaooo š„°š„° Nyie mimi nikawa wifi na shemeji wa taifa la sudaniš
Nilipewa zawadi mpaka basi , watu wa bondeni walikuwepo .
Baada ya shuhuri tulikuwa tunapumzika pale pale hotelini sasa kuna wale watu mmoja mmoja wanakuja kutupa hongera akaja emmy nae nikamshukuru kwa kuhudhuria Katika sherehe yangu si namuona anamchekea chekea Abbas mmh wee nilimchamba hapo hapo wee nikamwambia emmy Naomba uende sa hivi usiku na hali yako hiyo nmejua kama umekuja hakuna hata haja ya kumshobokea mume wangu ” abbas mwenyewe alicheka Aidani alipoona nimekasirika vile hapendi nikasirike akamtoa haraka njee š”š” Martha nae alikuja et kuaga na kutupa hongera nikamwambia Abbas sitaki ukaribu na huyu dada š” yaan nishakuwa mke sasa mbona atakomaš
Et Abbas akanambia hivi huyo mtoto ndo anakuendesha hivyooo??
“Aah wee nalinda mali yanguu “
“Hata usijalii hii ni fimbo yako, inakuadhibu wewe tuuš š š ”
“Kichwa chako weweee kumbe mtundu hivyooo”
“Haya njoo tufungue usiku wetu, mtoto hana mifupa bado”
Chumbani tulikuwa tupo peke yetuu ,tukala cha usiku …
Alhamdulillah nilijifungua salama mtoto wa kike ,mtoto kama wa Aidani bint yangu ni mrembo yaan mrembo mpaka naogopa jamaniš š
Nashkuru mungu kwa kila kitu š Asanteni kwa kuwa na mimi mwazo mpaka mwisho wa mkasa wangu huu ,
NB wakati wa mungu ni wakati sahihi mnooo Tusikate tamaa mimi niliona uzee Unanikumba wakati sina lolote kumbe fungu langu lilikuwa bado kufika mungu ndio anajua nani ampe kwa wakati gani
NAWAPENDA š
Mwishoo….

