DOCTOR NIKUNE NA HUKU KUNAWASHA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 12
Nililia mpaka nilihisi kuumwa kichwa ,ilipita zaidi ya dakika 30 nimekaa huko nyuma , simu yangu ndo ikaanza kuita alikuwa anapiga abbas niliitazama basi hasira ndio zikazidi nikaanza upya kulia kidogo nilikuwa nimeanza kupunguza speed , alipiga sikupokea mpaka ikakata,ikaanza tena kuita nilikuwa naitazama tu wala sijapokea akatuma sms (sorry maam simu niliweka mbali kidogo nilikuwa nakazi kipenzi what happen?? Please pokea simu niambie mke wangu) niliisoma ile sms nikaaachana nayo ,simu ikaanza tena kuita, ikaita akapiga zaidi ya mara kumi na sms kibao za kunibembeleza lakini siku pokea ,kidogo nikasikia geti linafunguliwa hata sikuinuka kuona nani anaingia au bi shost anatoka sikujali sec hiyo hiyo simu yangu tena ikaanza kuita abbas amekazana kupiga nikaona huyu asinizoee nikaikata nikaizima wakati naizima nashangaa abbas amesimama kwenye kona ya nyumba ananitazama ,
Kwanza alishusha pumzi akawa ananiangalia kama mtu anaejiuliza , afu akaja nilipo haraka kumbe wakati anaingia alifata mlio wa simu ndo akanikuta huku nyuma
“Dearing shida nini kipenzi changu???” Aliniuliza huku ananishika uso ananifuta machozi basi mimi kumuona ndo machozi yanatiririka tu bila hata sauti kutoa , yaan machozi yanavyotoka jamani kama sifa vile anafuta yanavuja tu ..
“Naomba nipeleke tu kwangu..”
“Nasraa honey, nikupeleke kufanya nini kuna kitu hujakipenda hapa au nimekukosea nambie kosa langu mamaa nambie tafadhali sana , Hasira hazijengi mke wangu haya nambie nimekosea wapi”
“Nyumbani kwangu nilikuwa na amani mi sijaja kula hapa kama kula hata kwangu nilikuwa nakula tena nakula chakula ambacho nakitaka mimi wala sijafata kula kwako”
“Yes!!! Yeah najua hujafata kula , kipi kimekukela au chakula amekuletea kibaya”
“Hata haihusiani na chakula, umenileta humu ndani kama nani yako??”
“Mke wangu mtarajiwa inshaallah mwenyezi mungu ajaalie hilo lipite”
“Sio kweli ,umenileta kama mwanamke wako humu ndani lakini umenitambulisha kwa mpenzi wako mimi ni mfanyakazi wako ndio mana anafanya anachojiskia kwasababu humu ni kwake”
“OMG!!!! Who’s???”
“Hujamuona humo ndani”
“Sijaingia hata ndani nimefika getini napiga simu yako inaitia huku ndo mana nikaja moja kwa moja , embu inuka ” akaniunua akawa amenishika kiuno mkono mmoja mwingine amenishika mkono wangu
Tukafika sebleni ipo pochi tu shoga hayupo akanambia “yupo wapi??” Nikamjibu unaniambia mimi mwangalie chumbani kwake kwani hapa si ndio kwake …
Kweli bwana tukaingia chumbani Martha kajiachia kwenye lile tanda mwenzangu yupo na nguo ya ndani tu chini afu juuu yupo na Tshirt ya baby kajiachia mwenyew. Tumeingia tu nikamsikia abbas Amesema kwahasira “Damn it” akakuna kichwa
“Martha!!!” Alimuita uso wake ulikuwa na hasira yaan ukimtazama tu unajua sio kwema hapaaa
“Ooh umerudi “
“Embu nisikilize Martha, ” alimwambia huku anamtupia taulo ajifunge
“Yes humu ndani ulipazoea nafikiri ulikuwa sahihi kwa sababu nilikuwa alone but now ,siko vile tena sitaki tukosane ni bora tuheshimiane ,, hichi chumba sio changu tena kina mtu na mtu ni huyu , huyu ni mwanamke wangu mpenzi wangu mungu akijaalie ndie atakuwa mke wangu , jana nilikueleza kila kitu nashangaa leo umefanya mambo ya kipuuzi sana ili iweje?? Mimi nawewe tuna mahusiano?? Au unavyofanya hivyo inakuja picha gani?? Mwanamke wangu afikirie nini?? So please Martha wewe ni kama rafiki yangu wa kwanza dada angu ndugu yangu please and please hii tabia isijirudie tena na ka…….”
“Inatosha abbas unaongea sanaaa” Martha alimkatisha kuongea huku anachukua nguo zake kuvaa yaan hata aibu haoni anavaa hapo hapo mbele yetu
“Mh naomba kuongea na wewe” alimvuta mkono abbas lakini abbas alikataa
“Ongea hapa hapa hakuna cha kumficha Nasra ” Nikasema yessssssss🥰🥰hivyo ndio napenda mieeee👌
“Martha alinitazama juu ,chini akasonya afu akatoka alinipiga kikumbo cha nguvu manusra nianguke
“Huyu ana nini mbona kawa wa ajabu gafla???” Abbas akabaki tu anamshangaa mimi mwenyewe nikajiuliza sa kama hana mahusiano na abbas mbona anaigiza vitu vya ajabu hivyo …
Alipo ondoka abbas akanibeba juu juu akanipakata miguu yangu nikaipitisha kiunoni kwake
“Utakuja kuniua nasra ujue?? ” akanambia huku ananibusu mdomoni mi nikacheka mwenyewe nilijiona mjinga khaa sio kwa nilivyopaniki vile
“Hata kama ungekuwa wewe abbas mmh ndo nini vile mtu anatawala kama kwake tena anaingia chumbani kwako anavaa nguo zako”
“Hata sijui huyu mwanamke amekumbwa na nini gafla hivi , hakuwahi kuwa hivii”
“Labda anakupendaa”
“Mmh Hapana aliwahi kuwa na mahusiano na ndugu yangu ye ni DOCTOR muhimbili, na hiyo ndio ilikuwa sababu ya mimi na yeye kuwa Karibu hata walipo achana akabaki kuwa mshkaji wangu”
“Mh” niliguna tu huyu shemeji anataka kuliwa na abbas lakini abbas anakichwa kigumu kweli kweli hata haelewi kidogo tu mimi nimeelewa anataka nini😀😀 ..
Akanambia ” tusiharibu siku yetu et mana kote kumekuwa kizungu zungu kule shost wako akuonee wivu huku aliekuwa shemeji yangu analeta mapicha picha ,embu jiandae tukale afu tuzuruleee mpaka basii ” nikasema hayaa chap nikaenda kuoga akanipa mfuko kulikuwa na nguo nzuri afu zimaonekana za bei ilikuwa suruali ya suti koti lake na kinguo cha ndani afu na kiatu kirefu eeeh🥰🥰nilinogaa nikawa wa kishua hatari ,
Akatoa piki piki yake na hivi nyuma mtoto mashaallah basi nikaubinua bwana weee hakiamungu nilikuwa natamani nimwambie embu twende kule Vingugwe Bondeni kwetu wakanione kwanza nilivyonawiri kwa usiku huu mmoja tu😀 hata kama nikionekana limbukeni Fresh tu mladi moyo wangu nimeulidhisha ….
Tukaenda mpaka mwananyamalia mimi tena naona bado limeandikwa Shishifood aiyaa😋😋🤗 hata sipajuagi napaonaga tu Fb hukoo , nikashuka mpaka natetemeka nisije kutia aibu bure , baada ya kushuka tukaenda kwenye meza kukaa akachukua simu akampigia mtu akamwambia tumeshafika tayari ,,yeah ukija tu nitakuona …okay poa poa…
Alipo kata simu muhudumu akaja pale juu kulikuwa na menu akanipa nichague nakula nini mwenzie hata sielewi ni kama alinisoma flani hivi akamwambia muhudumu tutakuita afu akaondoka yule kaka aliekuja , akachukua menu akanambia ngoja nikuchagulie sawa nikasema asante ,moyoni nasema ulijuaje mi hata sielewi
Akanambia kwa vile sa hivi bado mapema tunywe juice tu baadae tutakula cha usiku then home unaonaje nikasema yote sawa tu ..
Simu yake ikaita akaipokea kama kuna mtu alikuwa anamuelekeza aje upande wetu ,
Akaja huyo mkaka yeye anaonekana ni mkubwa kidogo kwa abbas japo ukiwatizama utasema wako sawa, sema sasa aaaah yule kaka alokuja mungu wangu weeee !!!! Ni MZURIIIIIII !!!!mzuri mpaka anachanganya akili jaman nyie mimi nilikuwa nasema abbas ni mzuri huyu ni kiboko nae ni msudan uuuh🙌🙌
Akanisalimia kwa kunipa mkono Anavyonukia mpaka nikawaza hivi haya sio majini kwelii??😥 ngoja nijichanganyeee …
Chapter 13
Basi anacheka ni vizurii nyie🙌 basi bwana akavuta kiti akawa amekaa kati kati yetu yaan huku mimi kule abbas
“Na huyu ndio mke wetu eeeh!!!” Aliuliza huku anatutazama kwa zamu mimi na abbas nikacheka tu kwa haya mana mtoto wa kike sifa yake kubwa uwe hayaa hiyo ndo Haiba ya kike haya bibi mtoto wa kike ameubwa na hayaa🙊
“Ndiyee!!” Abbas akajibu huku anacheka mpenzi wangu nae akicheka si habaa yaan hawa watu ni wazuri tu mashaallah
“Nasra mi Naitwa Aidan sijui kama uliwahi kunisikia lakini mimi nakujua kabisaa ” nikainama tu chini mana alikuwa ananiangalia usoni
“Kipenzi huyu ni kaka angu kabisa baba etu mmoja mama etu mmoja , kama alivyokwambia anaitwa Aidan,Huyu ndio baba angu na ndio mama angu kwa sasa , leo nimeona nikukutanishe nae chochote kikitokea basi lazima ufike hapaa”
“Ooh Asante sana, nashkuru nimekufahamu”
“Mi pia shemeji yangu na ninakupenda mnoo yaan mpende Dogo asije umwa sonona buree”
Shemeji alikuwa mcheshi kweli hatukupoa hata kidogo mpaka mida ya sa moja ki giza tukaagiza chakula baby akaniagizia masotojo😋 nikawa nakula kwa pozii mbele ya shemu tena nisije kujipa sifa mbaya baada ya kumaliza tukatoka zetu nje ya geti shemu alikuwa na gari tukaagana akanambia atakuja nyumbani ili tujuane vizuri nikasema sawa , nikapanda piki piki tukaenda zetu nyumbani , baada ya kuoga akanambia “nasra tunaweza kuongea au umechoka ??”
“Tuongee tu mi nipo poa mbona “
Akanambia
“Kwanza naomba unisamehe sana kuhusu Martha na tabia alizoonesha kwako tangu mwanzo”
“Haina shida kipenzi hilo mbona nilisha lisahau “
“Mbili naomba nikwambie kuhusu mimi na maisha yangu kiujumla” nikatuliza akili kujua nini anataka kuniambia??
“Mimi naitwa Abbas Sultani muctas, hilo ndio jina langu kamili, mimi sio mtanzania , Tumezaliwa wawili mimi na kaka yangu Aidan yule uliemuona jioni ya leo , baada ya miaka 8 tangu kuzaliwa kwangu familia yetu ilikumbwa na machafuko yale yalioikumba sudan na famililia yetu ilikuwa ni moja ya wahanga wa machafuko yale tulifanikiwa kupona mimi na kaka angu tu wazazi na ndg wote walipoteza maisha hiyo siku , na tukaenda kwenye vituo vya kusaidia wahanga tumekuwa hapo mpaka umri huu wote tulisomea udaktari na baada ya kuona wanafunzi wa Udaktar sudani wanawindwa sana ili kupoteza kabisa msaada ndipo tulitafutiwa sehemu nchi zingine na sie tukajikuta tupo Tz , baada ya kumaliza masomo yetu wengine wamerudi kusaidia lakini kuna wengine wameamua kuajiriwa huku huku ndipo na sie tuliamua kuchagua huku , kaka angu yupo muhimbili na mimi nipo hapo Temeke …huyo ndio mimi nasra ,leo nipo nawewe nahitaji amani zaidi nahitaji tuwe familia …..” nilishusha pumzi nikamkumbatia moyoni anamengi ya uchungu nikamwambia pole sana ,pole sana kipenzi changu nilimwambia huku nampiga piga mgongoni kumtuliza …
“Nakuahidi nitakuwa mke mwema kwako na mama bora kwa watoto wako inshaallah mungu atuweke pamoja “
“Inshaallah nasra nakupenda sana , naamini sijakosea kukuchagua wewe , Macho yangu hayakunidanganya hata moyo wangu unaamini juu ya upendo wako mamaa!!!”
Tukiwa tumaambizana maneno yetu matamu matamu hapo simu nayo ndo ikatushtua baada ya kuita ilikuwa simu ya Abbas na mpigaji alikuwa Martha , abbas akanitazama nikamwambia pokea ,akaipokea akaweka loundly
“Abbas nahitaji kuongea na weww” martha akasema bila hata kusalimia
“Ongea nakusikia”
“Ukiwa mwenyewe “
.”yeah nipo mwenyewe ma mtu anapika huko” moyoni nikasema waoooh🥰
“Umenisikitisha sana abbas sana , unaenda kuokota tu mwanamke wa uswahilini humjui hata tabia yake hivii Abbas unawajua wanawake wa Tz kweli?? Wamejaa tamaa uongo mwingi wao wanafata maslahi tu mhu nakuonea huruma sana sana”
“Sawa Martha nimekuelewa mdogo wangu , nitakuwa makini hata usijali”
” nimekuwa nawewe kwa muda mrefu sana abbas kwahiyo hukuona kitu kwenye macho yangu ,hukua hisia zangu ” maneno ya martha yalifanya moyo wangu udunde fasta fasta ni kweli nilichokuwa nakiwaza sasa anamtamani vipi shemeji yake ..
“Sijakuelewa….”
“I really love you abbas , sio jana wala juzi “
“Niniiii…..????” Abbas alitoa machoo yaan mshangao wake ulikuwa mkubwa mpaka akaziba mdomo
“Nakupenda abbas , kwanini ?? Au mi sio mzuri?? “
“Wewe Martha wewe ,umechanganyikiwa et embu lala huko ” Abbas akakata simu huku anasema mjinga kweli huyu mwanamke aisee sijawahi hata kufikiria
Nikaishia tu kuguna , zikawa zinaingia sms nyingi kweli kutoka kwa Martha et anaomba amuelewe yeye hakuwahi kulala na kaka ake waliachana bila kukutana kimwili khaa huyu mwanamke kweli mjinga , nikajikuta namkumbuka yule kaka jamani alivyovile handsome boy mpaka kawa kama malaika afu wakaachana sijui alimuacha kwa nini nikatamani kumuuliza abbas waliachana kisa nini mmh nikafumba bakuli mana nilimuona abbas kama anahasira nikaona tu huyu hafurahishwi na ujinga wa Martha nikaipokonya ile simu nikamblock afu nikaizima nikaiweka mbali nikarudi kumpa baby wangu kipozeo cha hasira ……
Sijui hata namba angu Martha aliitoa wapi nikawa naona tu msg zake matusi na kashfa et Ooh kwa ajili zangu mimi abbas ananipenda?? Mwanamke mwenyewe sijui hata kutumia lotion za bei ,sina elimu sina kazi nipo nipo tu sielewiki aah nikaona hili la mkosaji nikawa hata simjibu namuacha tu abbas akawa analalamika yaan kama angekua na uwezo angeacha tu kazi au kuhama kitengo Martha anamsumbua sana …
Shemu wangu alikuwa ananipenda mpaka raha mara kwa mara alikuwa anakuja nyumbani ananiletea zawadi kibao mpaka raha siku moja nikamuuliza “kwani Shemeji yangu we na cathy et mliachana kwa sababu ipi” akacheka kwanza akanuliza kwani we umejuaje kama niliwahi date na yule mwanamke??” Mi nae nikacheka tu .
Ilibidi nimwadithie mambo yanayoendlea hapo na maneno yake Martha alishangaa kweli hivi huyu mwanamke anaakili mi abbas hajawahi kuniambia nikamwambia ndo hivyo hata kazini huku abbas hana raha visa anavyomfanyia akanambia ngoja niende huko huko mi nikasema hayaaa ….
Chapter 14
Jioni wakarudi abbas akiwa na shemu ila shemu hakuingia ndani akaniaga juu juu tu akanambia siku ingine atakuja nikasema sawa , nikamuuliza huko kwema , abbas akanambia hata sio kwema mwenzangu hata sijui bro amejuaje visa vya Martha hata sielewi ” abbas akanijibu huku anakaa
Nikawaza moyoni kumbe shemu wangu anafaa 😀😀 hajanichoma nionekane mmbea kaniwekea ulinzi basi nami nikajifanya nashangaa “sa kajuajee???”
“Yaan hata sielewi mi nashangaa tu mtu huyu kawaka hatari,, namuuliza we umeyatoa wapi hataki hata kunambia ila kwa alichokifanya Martha hawezi kurudia tenaa”
“Kafanyaje???”
“Bwanaa kumbe Martha ni mchafu sana wa tabia sanaaa” nikakaa vizur nami kusikiliza
“Et kinajidai unawajua wadada wa Tz wewe, kumbe ni yeye mjinga kweli,na bro kamchana mbele ya kila mtu yaan wale wote tulio tokea sudan kumbe Martha katembea nao aisee yaan hata pale kazini karibu wote amelala yaan leo kila mtu alikuwa nashangaa et huyu Martha kumbe hadi wewe yaan majamaa wanashangaana kaka mwenyewe anasema kamfumania sana tu kuna siku alimkuta ndani ya maabara anazagamuliwa ndo ukawa mwisho wao lakini aliamua kumkalia kimyaa tu”
Duh mi mwenyewe muhuni lakini ye kanizidi ..
Abbas akanambia Tuachane na hayo yunakula nini leo??
Nikaenda zangu kupika ….
Usiku wakati tumelala simu yangu iliita na ilikuwa usiku kweli kweli nikashangaa nani huyu usiku wote huu , kwanza nilisahau😜 Hapo nilikuwa nimepewa simu ingine na baby yaan bonge la tambo Kwahiyo nilikuwa wa kishua kweliii😋…
Nikajikurupua sa hii usiku nani anapiga ilikuwa namba ngeni, abbas akaniuliza ni nani??”
Nikasema hata sijui namba ngeni akanambia sa si upokee kama je mtu muhumu anakutafuta , nikaipokea sasa nikawa nimeweka sauti “Malkia wangu nineshindwa kulala nasra wangu ” mmmh niliguna ni sauti ya kiume sijawahi kuisikia afu kaenda moja kwa moja tena kwa sauti ya kubebisha kwelii
“We nani??” Nikamuuliza kwa hasira
“Oh sorry au jamaa yupo nilifikiri kaingia zamu ya usiku kama ile siku ,nitakucheck basi kesho ila nimemis utamu” simu ikakatwa kabla sijajibu , abbas alikuwa ananitazama na mimi namtazama yaan hapo mwili wote unanitetemeka , ukute hapo kuna siku kama 3 hivi nyuma hakulala nyumbani aliingia kazini Night sasa haya maongezi ni kama yanaendana hivi na tukio la yeye kutokulala nyumbani
Haraka niliipiga tena ile namba ikaita bila kupokelewa nikajaribu tena , abbas akaichukua simu yangu afa akanambia Tulale bwana usiku mkubwa huu ..
Akanivuta kifuani , naapa sikulala usingiz haupiti kila nikifumba macho nakumbuka ile sauti niligundua abbas pia hajalala nikamuita “abbas mpenzi wangu” akaitika “Naam”
Nikamuuliza unaniamini?? Akasema Yeah kuna shida kwani.???
Nikamwambia “abbas naapa kwa mungu mpenzi wangu huyu mtu simjui wala hii namba siijui kabisa ” wala hakunijibu alinilaza kichwa kifuani akawa ananipiga piga mgongoni kama kunituliza , mpka asubuhi inaingia sikuweza kulala kabisa nikamuandalia nguo akaenda kazini, nikawa naitafakari hiyo namba ni ya nani lakini sikupata jibu anaongea kwa kujiamini kweli kama vile mimi ni mwanamke wake tena nililala nae kipindi ambacho abbas yupo kazini nilipiga mara mbili lakini hakupokea nikatulia lakini moyo ulikuwa unanitetemeka sana kila nikikumbuka maneno yale ya usiku
Jioni alipo rudi abbas akaniuliza huyo jamaa alikuwa anataka nini?? Nikauliza jamaa gani??
“Si kuna mtu hapo mi nafika ye anatoka humu getini yupo haraka haraka “
Mmmh nikaguna mana mi hakuna aliekuja ndani nimeshida mwenyewe
Nikamwambia hapana mi mbona sijaonana na mtu tangu kumekucha akasema sawa , wakati tunakula simu yangu iliita namba ile ile iliyopiga usiku , akanambia pokea weka sauti , nikapokea mkono unatetemeka
“I au 2” sikuelewa maana baada tu ya kupokea akaniuliza hilo swali abbas akaninyooshea kidole kimoja akasema sema moja aliongea kwa ishara hakutoa sauti nikasema moja
Akasema” afadhali kipenzi changu maana ule mda natoka tu si nimekutana na jamaa yako getini nimeogopa aisee lakini nimejitahidi kuvunga ili asijue chochote hajakugombeza??”
Daah😥😥 yaan huyu mtu anavyoongea kama vile tunajuana muda mrefu sana nilijikuta natetemeka mwili wote nikamuuliza huku machozi yanatoka “kwani we nani na unataka nini ?? Usizunguke sana tafadhali “
“Aah nasra umeanza maigizo yako ndo mana nimekuliza kama upo peke yako au ?? Sikia nikwambie nasra mi tangu umenionjesha Radha yako ya kiswahili hiyo kiukweli umenichanganya sana kama huyo jamaa anakusumbua njoo nakuoa asubuhi tu sawa mchumba wangu , nitakucheck kesho utanambia kama jamaa ataondoka nitakuja sawa au we uje kwangu ili nifaidi vi…….” abbas alinipokonya ile simu na kuikata alinitazama jicho kaliii mpka niliona machozi yanataka kutoka akainuka bila kusema kitu chakula kikawa kichungu tenaa hakuna alie kula hata nguvu za kumfata chumbani nilikosa kabisa nikabaki nimekaa juu pale ya kiti nawaza mengiii sana😥 huu ni mkosi gani unataka kuamka sa hivii mungu wangu 😥 nilienda kwenye kochi nikajisumata zangu ajabu nililala hapo mpaka asubuhi ndo nashtuka abbas sikukumkuta sijui hata alitoka sa ngapi , nikaenda kufunga geti mana sikutaka yajitokeze kama ya jana kuacha get wazi mtu anaingia hata sijui , nikampigia simu abbas wala hakupokea karibu mara nne😥😥 nikaacha nikaingia zangu chumbani kulala yaan mimi kweli nina mkosi na hu mbona umezidi sasa ?? Ni kwanini inakuwa hivii😭 nilijijuta nalia kwa sauti tu nililia mpaka nikahisi homa na vile sikula tangu asubuhi homa ilinishika, nikaangalia simu labda hata Abbas alinitafuta hamna jamani ,kwahiyo abbas amenichukia kwelii😭😭nikaanza kulia tena upya nampenda sana huyu kaka hakiamungu nampenda mnooo, nikainuka kwa kujivuta ilikuwa tayari jioni nikajikorogea zangu uji hapo nahisi homa kalii nikatafuta panado nikajitetea .
Wakati nipo nakunywa uji geti liligongwa na ulikuwa ni muda wa abbas kurudi nyumbani nikajua ndio yeye nikaweka uso vizur ili asinione mnyonge , lakini Getuni hakuwa yeye alikuwa mkaka tu hivi hat simjui wala sijawahi kumuona
“Hey sister mamboo” alinisalimia kwa kuchangamka kweli huku anacheka ilibidi na mimi nimpokee hivyo hivyo , mkononi alikuwa kashika box
“Samahani naona ulikuwa umelala zako mwenyewe èh”
“Aaah hata usijali Karibu” mi nikamjibu huku acheka tu
“Chukua hii nimepewa na Doctor abbas nikuletee” nikachukua box lile baada ya kuchukua akanipiga kijibao cha shavu huku anasema “mke wa doctor mzuri wewe” nikashangaa anaubusu mkono ule alonigusa nao shavuni afu akasema bye huku anapunga mkono pembeni kulikuwa na piki piki akapanda nikabaki namshangaa huyu kaka vipi?? Baada ya yeye kutoka sasa ndo namuona abbas kwa mbele amesimama ananitazama Subhanallah miguu nilihisi inaishiwa nguvu sikujua kaona lile busu au vipi?? .
Nilibaki pale pale getini mpaka alipo nisogelea akaniuliza “huyo nani” nikamshangaa mana yeye ndie aliemtuma
“Mi simjui!!”
“Humjui ?? Humjui mtu mnapigana ma busu barabarani mnacheka na unaonekana hata unafuraha?? Amekupa nini humo??” Khaa😳 nikazidi kumshangaa huyu vipi, vitu atume yeye afu anipakazie mie!!!!…
Chapter 15
Tunaongea huku tunaingia ndani nimebeba lile box nikamwambia abbas huyu kaka si umemtuma wewe aje hapa leo nimekuwa mimi tena??” Abbas alitabasam tu wala hakunijibu kitu , mi nikaliweka lile box juu ya meza nikamwachia kwa sababu ni lake wakati naondoka akaniuliza “Nasra kuna kitu unanificha?? “
“Sina chochote ninachokuficha Abbas “
“Haya fungua basi tuone wote” moyo mwingine ukanambia itakuwa ni surprise hizoo kaniletea yeye anataka tu kunirusha roho si nikarudi kwa mapana 60 na tabasam limeanza kumea usoni🥰🥰
Subhanallah kilichonikuta baada ya kufungua nilitamani kuzimia mimi mtoto wa watu😥 kulikuwa na pafyumu tena ya bei ,bikini na brazia yake nzuri hatari ,cheni na saa ya mkononi, kulikuwa na kadi juu imeandikwa for you Nasra niliichukua nikakuta jumbe ndefu ikinisifia kwa mapenzi ninayompa anajuta kuchelewa kunijua na hawezi tena kuvumilia mapenzi ya wizi kwani anataka kujiachia ili afaidi mautundu yangu peke yakee ,nifanye mpango kuachana na abbas )
Nilipo mtazama abbas niliona machozi kwenye macho yake ,mkaka wa watu jamani sura yake imetulia hana hata shida na mtu sa kwanini wanamtesa kiasi hichii😭 Ni nani huyu na anataka nini?? Au Emmy kanitafuta ili kuniharibia jamani ?? 😭
Abbas aligeuza kuondoka bila kunisemesha nilimshika mkono nikamwambia “naapa abbas mi mwenyewe sielewi kitu kabisa kipenzi changu ” aliushika mkono wangu akausukuma pembeni akanambia “Inatosha Nasra naomba kupumzikaa”
Daaah😭 kwa hiyo ndo wadada wa Tz maraya ndo kweli ameamini hatuna mapenzi ya kweli tumejaa Tamaa tu!! Kwahiyo ndio ameamini..
Sikuweza hata kusogeza mguu wangu nilihisi kizungu zungu nikaanguka chini..
Nilikuja kushtuka nipo hospital nimewekewa drip , shemu Aidan alikuwa pembeni yangu afu ni asubuhi inamaana nimelala hapo usiku kuchaa .
Shemu alipoona nimeamka akanisogelea nikamuuliza abbas yupo wapi akanambia ametoka hapa sasa hivii, karudi kazini usijali mi nipo nakutazama sawa ,” nikasema sawa, Nikauliza tena nipo hospital gani na shida ni nini??” Akanambia Upo temeke hospital , tatizo huli afu unamsongo wa mawazo sijui unawaza nini shemu ,usituumizie dogo ndo tunaanza kuutafuta ukoo hapo ujue ” Alinambia huku ananitazama Tumboni nikasema nini mbona kama sielewi afu nataka kuelewa”
Shemu akawa anacheka “aah bwana mimi friji langu haligandishi tena siwezi kuvumilia mpaka abbas akuambie , bwana wewe ni mama k” moyo wangu ulifanya puuh ❤ nikasema weee shemu ni kweliii???” Niliuliza kama siamini huku nainuka kukaa
“Yeah wewe ni mama etu mtarajiwa , hutakiwi kuacha kula wala kuwa na msongo wa mawazo shemu kama kuna kitu hakiko sawa naomba uniambie mimi nitakiweka sawa unanielewa eeh”
Nikatikisa kichwa kukubali hapo moyo unadundaaa hata siamini natamani hata kuruka ruka
Shemu aliniona moyo unavyotapa tapa akanikumbatia “Utaegamia bega langu kama abbas hatokuwepo kwa wakati huo jiamini sawa mama etu” oooh nilimkumbatia kwa nguvuuuuu mpaka nikalia nikasema Asante mungu Asante nilijua mimi sina uzazi jamani nimeanza kutamani niwe mama miaka mingi sikuwahi hata kwa bahati mbaya et leo bila hata dawa nimekuwa mjamzito?? Ooh kweli wakati wa mungu ni wakati sahihi haijalishi ni muda gani umepita ..
Nikiwa juu ya bega la shemeji yangu nilisikia mlio kama wa simu yangu inaingia msg , Akanambia shemu simu yako aliileta abbas nikaichukua kufungua ujumbe ni ile ile namba ajabu kuna jumbe zingine zilikuwa zimefunguliwa yaan zilisomwa zinaonesha zilitumwa jana usiku ikabidi nisome hizo za juu ya kwanza ilikuwa ndefu ila alisema anajua kuwa huyu fala kanipiga sana mpaka nimepelekwa hospital anaapa atamrudisha Sudani kwa magoti msg ya pili aliandika kesho Asubuhi nakuja kukuchukua mke wangu nimechoka kujificha ,, na hii iliyoingia sasa hivi ndo ilifanya mwili uishiwe nguvu machoz yalianza kunitoka (mke wangu nasra nafurahi sanaa kunibebea mwanangu kwenye tumbo lako nakupenda na nitakupenda muda wa kuishi mimi nawewe umefika iloveyou)
Shemu akaniuliza vipi mbona kulia tenaa ,,ilibidi nifute machozi nikasema moyoni nitalia mpaka lini simjui mtu huyu ni nani na anataka nini embu ngoja nipambane nae sasa kwa ajili ya mwanangu tuuu💪
“Shemeji, Abbas amekwambia matatizo yetu??” Nilimuuliza swalii akafikiria kidogo akanambia “hapanaaa hajanambia kitu”
“Naomba kuongea nawewe shemu ila sio hapaa tutoke”
“Lakini hali yako bado haipo sawa ujue “
“Tafadhali shemu haiwezi kuwa sawa mpaka nitakapo ongea nawewe”
“Sawa tuondoke “
“Naomba usimwambie chochote abbas”
“Nakuahidi!!”
“Sawaaa” alinitolea zile drip akanisaidia kutembea mwili haukuwa na nguvu vizuri mpaka nje kwenye gari yake , tukatembea na gari mpaka lost beach ipo mikocheni , tukaingia akaniuliza umepapenda nikamwambia ndio pametulia akanambia haya nambie shemu maana nahisi kama roho inataka kuchomoka ,, nikatabasam tu kidogo..
“Aidan” nilimwita kwa jina lake huku nimemkazia macho yaan hapo sitaki tena mzaha
“Naam Nasraa!!” Kidogo nicheke maana sikujipanga kama anaweza kuniitikia hivyoo
“Unaweza kuniamini ?? Walau kidogo tu”
“Macho yako ,yanaonesha upo Serious sanaa kwahiyo nakuamini”
“Asante ,Mimi na abbas kwa sasa hatuna maelewano mazuri na nina uhakika kwa sasa mahusiano yetu yamekalia kuti kavuu muda wowote linakatika na ndio itakuwa mwisho “
“Subhanallah mungu aepushe mbali kabisa shida nini mpenzi “
“Siku za nyuma niliwahi kupokea simu yenye utata ilikuwa usiku sana ……………….” nilimuhadithia Shemeji mwanzo mpaka mwisho wa vile vituko
“Embu kwahiyo wewe humjui kabisa??”
“Simjui simjui wala sijawahi kumuona”
“Sasa eeeh mbona mtihani sana “
“Na leo amenitumia hii msg na jana alituma hizi nina uhakika abbas alizisoma” nikafungua simu upande wa msg nikampa
“Heee huyu mwenda wazimu nini?? Embu kwanzaa ye kajuaje kama wewe ni mjamzito???” Swali la shemu ndio liliniamsha mimi kwenye usingizi wangu kweli kajuaje??
“Kweli kajuaje?? Na kajuaje kama mimi nilikuja hospital jana??”
“Hapo hapooo Nasra !! Inamaana huu ni mchezo nani mwingine anajua kama wewe ni mjamzito ?? Au wewe ulikuwa unajua kabla??”
“Naapa shemu wangu kwa ajili ya Allah mimi ndo leo umeniambia palee “
“Mmh abbas anaweza kweli kukufanyia hivi?? Unahisi”
“Mmmh” niliguna kidogo nikafikiria
“Sasa kwanini afanye hivyoo??” Nikamrudishia swali shemu
“Hawezi hata mimi hainiingii , inamaana anaefanya haya yupo karibu yenu wewe au abbas anajua wewe jana umekuja hospital anajua hata taarifa za ujauzito mana mimi na Abbas ndio tuliambiwa ..embu subiri ” shemu alichukua simu yake na kupiga kwa abbas
“Oya vipi” alikuwa kaweka sauti kubwa
“Poa bro'”
“Mbona huji kumtazama mkeo”
“Nimebanana na kazi ye kama anajiskia vizuri nenda nae home tu ” mmh niliguna tu maana alivyokuwa anaongea🙌
“Hivi kuna mtu yeyote anajua kuwa shemu ni mjamzito “
“Kwani vipi??”
“We jibu”
“Humu ofisini wote wajua maana doctor aliempima ni mshkaji wetu na alikuja kusema huku ” ooh basi sawa mi namchukulia tax anaenda mwenyewe tu kuna sehemu nawahi”
“Poa poa” simu ilipokatwa aidan akasema duuh msela kweli anapitia magumu hata ongea yake haipo sawa, naomba tu usimlaumu ,nikasema poa haina shida ,,,
Akanambia nipe simu yako au andika haya ninayo kwambia afu umtumie nikasema sawa
“Habari kaka najua hunijui wala mimi sikufahamu ,, sijui unata nini kwangu lakini nimeona bora nikutafute ili tuongee kama watu wazima wote , niambie unataka nini kutoka kwamba usizinguke kupita njia ngumu “
INAENDELEA…….

