KWA UTAMU HUU SIKUACHI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Episode 16
Walipomuona lucia na Boniface ndio baba yake akajikuta anasema “ kumbe huyu kijana ni mpenzi wako mwanangu, kwanini haukututambulisha maana amepambana sana na sisi tukajua ni msamaria mwema tu, kumbe anamahusiano na wewe, maana alikuwa anatuhudumia kwa kila kitu, yaan tupo hospital kana kwamba tupo ulaya, ndio lucia akamuangalia Boniface maana hata yeye mwenyewe hakuwa anajua kama Boniface amefanya byote hayo, na Boniface hakuwa na cha kusema zaidi ya kutabasamu tu..
Basi mama yake akataka kuongea na lucia, na sauti yake ilikuwa ndogo sana, hivyo hata alipomuuliza maswali wengine hawakusikia, ila alimuuliza hio mimba ndio ya huyu kijana, lucia akaitikia kwa kichwa kwa ishara ya kukubali, unampenda, lucia akatikisa kichwa kwa ishara ya kukubali kuwa anampenda, yaan anamuambia mama yake kuwa anampenda Boniface na wakati Boniface mwenyewe hakuwah kumuambia hata kwa bahati mbaya, yaan hata akiambiwa anapendwa huwa anaishia kutabasamu tu bila kujibu lpolote..
“ hata yeye anaonekana anakupenda sana, maana anajali sana kila kibachokuhusu, hakikisha unamtunza na usije ukamkosea hata kidogfo maana wanaume wenye mapenzi ya dhati kwenye zama zenu hizo wanaendelea kupotea, lucia akajibu tu sawa, kisha akamuaga mama pamoja na baba yake kisha akaondoka zake na Boniface…
Walipofika kwneye gari klila mmoja alikuwa kimya sana, ikabidi Boniface au zime ukimya na kusema ‘ unajua kuwa ukiendelea kuwa na mawazo unampa shida kijana wangu tumboni, haya nambie unawaza nini mamaa..
“ Boniface naomba unijibu tu na nakuuliza hivi sio kwa ubaya ila nataka kujua tu, akasema lucia na Boniface akamgeukia kisha akawa kana kwamba anamsikiliza kwa makini sana kisha akasema “ eheee uliza unachotaka kuuliza..
“ kwanini umewasaidia wazaz wangu bila kunipa taarifa?..
Boniface akatabasamu kisha akasema “ unajua kila jambo ambalo linakuhusu linanihusu na mimi pia, nilifuatilia nikajua una stress za kifamilia, na moja ya kitu ambacho sikikubali ni wewe kutokuwa sawa kwa namna yoyote ile ndio maana stress zako kuna namna zilikuwa zinaniumiza sana mamaa, ndio ikabidi nityafyute namna ya kuhakikisha familia yako inakuwa salama wakati wote, maana niliamini ikiwa salama na wewe utakuwa salama pia mamaaa..
Lucia akajikuta chozi linamtoka kwa sababu hakuwa amefikiria kama hayo maneno yanaweza kuja kutoka kwa mwanaume kama Boniface ambae alikuwa anaonekana muhuni na mbabe sana, kumbe hata wahuni wanaweza kuwa romantic wakikutana na wanawake wa ndoto zao..
“ unalia nini mamaa, kama nimekukosea naomba unambie tu kuliko kulia tu kipenzi changu maana unaniumiza na mimi, akasema boniuface na lucia akazidi kulia, ikabidi Boniface apaki gari maana hakumuelewa kabisa my wake na kuna muda akajua labda ni mimba inampelekesha mpaka akawa analia vile, hivyo alipopaki gari akasogea na kuanza kumbembeleza ila kwa namna ambavyo alikuwa anazidi kumbembeleza ndio namna ambavyo lucia alikuwa anazidi kulia, mpaka mwisho Boniface akauliza “ shida ni nini mamaa..
Lucia kwa sauti ya madeko ambayo ilikuwa inatokana na kilio cha chini chni akasema “ kwanini unanipenda hivi Boniface kwanini unanipenda kiasi hichi, unakuwa kama umenipa deni ambalo hata mimi mwenyewe sijui nitakulipa nini, bony embu nambie unataka nikulipe nini kwa kunipenda hivi maana sijui natakiwa kufanya nini ili kuonesha ni namna gani nathamin sana kila ambacho huwa unafanya kwa ajili yangu kila wakati..
Boniface alijikuta anacheka kisha akamfata lucia na kumkumbatia kwa nguvu na kusema “ hakuna kitu ambacho unaweza kunilipa zaidi ya kuwa upande wangu kila ambapo nitakuwa nakuhitaji mamaa, na kuwa ni miongoni mwa watu ambao nikicgoka wewe ndio uwe tulizo langu na tabasamu langu kila nikiwa na huzuni…
Episode 17
Lucia akamuangalia Boniface kisha akasema “ sina cha kukuahidi ila nafurahia sana kuwa karibu yako na kuanzia leo nitapambana sana kuhakikisha kuwa sikukosei wala sikuumizi kwa namna yoyote ile, nakuahidi kuwa mlinzi wa kwanza wa moyo wako na furaha yako, na kuhakikisha hakuna mazingira yoyote yale ya maumivu yako ambayo yanasababishwa na mimi bony, sina uhakika kama nakupenda au laa, ila nina uhakika kuwa nataman kukuona una furaha..
Boniface akatabasamu kisha akamsogelea lucia na kumkiss kwenye paji la uso, kisha akasema “ kwa hatua hio uliofikia ni hatua kubwa sana kwangu na nakuahidi kuwa nitahakikisha unanipenda sana mamaa…
Basi kuanzia hapo maisha yao yakawa ya burudani mno, ila Boniface akawa hataki kumgusa lucia mpaka ajifungue, siku moja Boniface akaamua kumuuliza lucia jambo..
“kwanini ulikuwa unanikwepa sana na hali ya kuwa nilikuwa naonesha kukupenda sana?..
“nilikuwa nakuona muhuni sana, nilikuwa naona namna ambavyo ulikuwa unaongea na wenzako nikaanza kuhisi kana kwamba tuko kwenye dunia mbili tofauti, na mbaya zaidi ni ile siku uliokuja kwenye mahafali ulikuwa unanuka pimbe balaa, na mimi sio mpenzi wa pombe na niliapa kuwa sitakaa nije kuolewa na mwanaume mlevi, na mbaya zaidi ulitaka kuniingilia bila ridhaa yangu kwenye ile siku ya maafali nikatokea kukuchukia sana, na kubwa kuliko ni ule wakati ambao tulikutana kwenye ile hotel ukalala na mimi, nikajua kuwa ni mchezo wako ila baadae nikaja kugundua kuwa nina maadui wengi kazin kwangu kuliko ambavyo nadhan ndio nikaondoa fikra kuwa ni wewe ambae ulihusika na tukio la siku ile…
“ kumbe ule ulikuw ani mchezo kwa bahati nzuri nikatokea mimi, mungu anakupenda sana lucia na nitahakikisha kuwa kila ambae alihusika na tukio lile analipa kikamilifu kila ambalo amelifanya maana hawawez kukurupuka na kufanya mambo kama wanavyojisikia wao bila kujua walikuwa wanahangaika na mwanamke wa nani…
“ kuwa makin lakin maana ni watu wa kubwa sana wale, akasema lucia, kabla hata lucia hajajibu mara wakasikia sauti kutoka mlangoni la mwanamke ambae alikuwa anaongea alikuwa ni brenda dada yake na Boniface ..
“ lucia hatimae leo tumekutana uso kwa uso na wewe, yaan wewe binti umejua kumnyoosha kaka yangu sio mchezo ulikuwa unataka afe nini…
“ umemaanisha nini? Ikabidi lucia aulize maana hakuwa anaelewa dada yake na Boniface alikuwa amemaanisha nini..
Boniface akataka dada yake anyamaze na kweli alinyamaza, ila baadae akamfata lucia pemben na kumuambia kuwa “ Boniface aliugua ugonjwa wa mapenzi mpaka akajaribu kujiua mara kama mbili kwa sababu yako, na alikuwa anataka kuchanganyikiwa enbda[po hatopata penzi lako na hatokuwa na wewe..
“ hapo alipo anatakiwa kunywa dawa ila alikuwa amekataa kunywa dawa kama hatokuwa na wewe, hivyo nakuomba umshawishi aende kwenye matibabu maana afya yake ya akili haipo vizur, akaendelea kusema Brenda na lucia alijisikia vibaya sana, akamfata Boniface kisha akamuomba wakale chakula cha mchana pamoja, Boniface hakuamin, maana lucia hakuwah hata mara moja kufanya kitu kwa ajili ya Boniface …
Basi Boniface akaingia chumban kwake, akaanza kuvaa, yaan kila nguo ambayo alikuwa anaijaribisha akawa anaona kama haimpendezi, maana alikuwa anataka kuonekana handsome sana kwa lucia kuliko kawaida…
Basi mwisho akachagua nguo wakaenda kupata chakula cha mchana na alikuwa anamuangalia sana lucia kana kwamba hakuwa anaamin kama lucia ndio ambae amekubali kuwa nay eye wakati ule, hakuwa anaamin kama mwanamke ambae amemuhangaikia sana hatimae yupo kwenye milki yake tena kirahisi sana..
Basi wakala na Boniface alikuwa ana furaha kupita maelezo, lucia aliliona hilo, mwisho akamuambia kuwa “ unaona je Kama nikikuimbia maana nimekumbuka sana kuimba..
Episode 18
“ohhh imba mamaa, imba maana sijawah kuimbiwa hata mara moja..
Lucia akaanza …
“ nataka nikuambie ahaaaa, jinsi ninavyokupenda mi..
Na kama mapenzi bado nambie nitayaongeza mi..
Nataka nikuambie ahhaaa jinsi ninavyokupenda miii
Na kama mapenzi bado nambie nitayaongeza mi..
Ninataman nyota na mbalamwezi, viwe mali yake yeye..
Nina tamani ila tatizo siwez, huenda ningefanya unielewe..
Wewe ndio ulinifunza mapenzi, nilikuwa sijui nakuambia..
Ukanidekeza kishenzi na nyimbo nzuri nakuambia, so usidanganywe na gari umbo zuri na shepu mimi ukanikimbia..
Ukalitupa thaman penzi ninalo kupenda kisa wamekuvutia..
So usidanganywe na sura, umbo zuri na shape mimi ukanichukia, ukalitiupa thamani p4nzi ninalo kupenda kisa wamekuvutia ,ahhh mwambie asije sikia mapenzi moyo wangu unaumia ee aaa..
Boniface akatabasamu kisha akasema “ asante sana mamaa, nakuahidi kuwa hakuna mwanamke ambae atayavutia macho yangu zaidi yako, maana wewe ndio wa kwanza na wa mwisho kwenye moyo wangu…
Sasa wakati wanaataka kuondoka, wakashangaa maji yanamwagika, kumbe chupa imepasuka, lucia akajikuta bameropoka na kusema “ chupa imepasuka mume wangu nataka kujifungua, aisee Boniface alimbeba lucia juu juu, alipofika akaambiwa atulie, wakaja kumpima njia na wlaipompima njia ndio kama alikuwa amewaambia wanyofoe nati ya uchungu maana ndio uchungu ukaanza kumuuma balaa, akaanza kulia kama mtoto mdogo, alilia sana machozi yenyewe hayatoki alafu wakawa wanakazana kumuambia kuwa asitoe kelele na afanye mazoezi, kweli alifanya mazoezi na baada ya muda akajifungua mtoto wa kiume alikuwa ni copy ya Boniface, yaan hata yeye mwenyewe hakuwa anaamin kama alikuwa amezaa mtoto ambae anaweza ,kufanana na Boniface kwa kiasi kile kwa wakti eote ambao alikuwa na mimba,sio siri Boniface alifurah sana, basi wakaruhusiwa kwenda nyumban na wakamuita mtoto wo ethan…
Basi lucia akala uzazi na Boniface akawa anafuraha sana kwa kupata mtoto, basi wakamlea mtoto mpaka akafikisha miezi sita, siku moja Boniface haluwa vizur maana kuna vidonge vya akili huwa anavitu,miaga, akawa hajanywa, kuna namna kichwa kikawa kinamuuma na akawa anatakiwa kupata hizo dawa mapema..
Sasa lucia alienda kumsalimia, amefika tu akashangaa amevutwa kitandani, kisha Boniface akasema “ nakutaka mamaaa, naomba unisaidie hata kidogo, lucia hakuwa na hiyana akampa mumewe haki yake sasa wakati wanakuja kuamka Boniface akawa anahisi kama alikuwa anaota maana ni kawaida Yake kuota anafanya mapenzi na lucia mara kwa mara, ila alipomkuta blucia pemben yake alishtuka kisha akawa anamuangalia kwa wasiwasi sana maana moja ya kitu ambacho Boniface hawez kuzuia n hisia na uoga wa kumpotyeza lucia//
Mara lucia akaamka, alafu akamsalimia bionifafce kisha aakenda kuandaa chai na kumletea Boniface chumban kwao, Boniface alipomuona tu akaanza kuomba msamaha…..
“ hupaswi kuomba msamaha na wakati wewe ni ,mume wangu na hakuna kitu ambacho ni kosa ila mimi ndio nilikuwa nafanya makosa kwa kutokukupa haki zako za msingi akasema liucia na Boniface akajikuta anatabasamu tu maana alijua kwa kulala na liucia huenda lucia atakasirika badala yake amekuwa mwema sana kwake..
Basi Boniface akaanza kufuatilia ambao walikuwa wanataka kuchafua jina la mke wake, akawatengenezea kesi na wote wakawekwa ndani..
Na baada ya hapo wakaanza maandalizi ya ndoa na mwisho wakafunga ndoa yao ya halali ya kanisani, na lucia akawa officially mrs Boniface…
Na mama yake lucia hajatengamaa kwa asilimia mia, ila anaweza kutembea mwenyewe taratibu taratibu na sauti inatoka na siku zote wanamshukuru sana Boniface kwa kubadilisha maisha yao, na kumasa mtoto wao asije akamkosea mwanaume anaempenda sana kama ambavyo Boniface anampenda na lucia akaahidi wazaz wake kuwa atahakikisha kuwa Boniface anakuwa ni mwanaume na nusu kwake na atafanya kila ambacho kitakuwa kinampa furaha Boniface, na mapenzi kwao yakashamirti sio mchezo…..
MWISHO

