Namwambia Mume wangu Atamuambukiza UKIMWI, eti Ananitukana
Mimi na mume wangu tuna maambukizi na tupo na watoto wawili ila Mimi natumia dawa mwenzangu hatumii na kuna mwanamke alikuwa anatembea naye wakawa wananitukana. Mwisho nikamuambia yule mwanamke sisi ni wagonjwa ila hakuamini aliona namdanganya. Mpaka amebadilisha dini na akaolewa mke wa pili na nyodo juu, namwangalia tu siipati picha ila Mimi nipo najipanga ili niweze kuondoka Kwa huyu mwanaume maana unaweza kufa kabla ya siku
Kiukweli wanawake wengi tunateseka kwenye ndoa ushauri wangu Kwa wanawake ukiona mumeo hajatulia Kila siku matukio ni Bora uondoke kuliko kuletewa maradhi na Bado akakudharau ni mbaya sana usikae Kwa kivuli Cha watoto huku unanyanyasika matokeo yake ni ugonjwa usiangalie anakupa pesa huku anakunyanyasa nyanyuka uondoke katafute pesa inatafutwa utu hautafutwi

