ALINIAMBIA ANATUMIA NYOTA YANGU, HIVYO INATAKIWA NIRUDI KWAKE
Habari kaka naomba ushauri wenu jamani mwaka 2018 nilikutana na mkaka akasema ananipenda anataka kuniowa hivo ikabidi twende kucheki afya lakini wote tulikutwa tupo salama tukaanza mahusiano. Wakati huo yeye alikuwa na miaka 38 na mimi 24 wakati tunaaza mahusiano alinikuta na mtoto 1 na yeye alisema ana watoto 2 pia alisema mke wake wameachana kwa talaka, alikuwa ananipenda sana na mtoto wangu alitujali pia kwa kila kitu. Tukaanza maisha alikuwa na maisha ya kawaida sana ila Mungu akafanya njia yake akafungua milango ya baraka akawa na hela lakini hivo vyote kapata baada ya kuwa na mimi akajenga nyumba na kununua magari..
Nikapata mimba japo ilinisumbua sana wakati huo mwanaume akaanza kubadilika nikaamua kwenda kwa dada kujiuguza maana nilijua nikiendelea kuugulia pale basi presha itaniuwa nikakonda nikaisha wakati huo mwanaume alisafiri hivo alikaa huko miezi 4 alikuwa hapigi simu wala kunijulia hali yeye alikuwa bize na kujenga nyumba yake huko dodoma siku 1 nikazidiwa hivo nikaenda hospital niliishiwa maji na damu wakanishauri nianze clinic, lakini wakanichukua kipimo cha damu sikupewa majibu wakati tunaondoka nikamwambia dada mbona yule nesi hajanipa majibu akasema ngoja nikamuulze nikiwa nimekaa chini sina lile wala hili dada alirudi akiwa amekosa furaha nikamuuliza nini shida akasema nakuonea huruma mdogo angu.
Sikujua maana yake akanambia nesi kasema alijua unaijua afya yako umekutwa na HIV positive
nililia sana nilihisi dunia yote imenielemea nimeishi kujilinda sana imekuaje basi alikuja na dawa akasema unameza kila siku pia nesi kasema mume wako akirudi njoo nae basi baada ya wiki 2 akarudi nikawa natamani kumwambia ila nikasema atajua huko tukifika nilikuwa nipo tayari kwa lolote nikimfikiria mwanangu alie tumboni natamani hata kujiua nife niliona sisitahili kuwa mama nilikata tamaa basi tulienda kule nesi akampima mume lakini hakuwa na maambukizi ila akadai kuwa ataishi na mimi hivohivo hata yeye ana ndugu zake wana hali kama yangu..
Baada wiki 1 mwanaume akabadilika akawa halali nyumbani mara anakuja na condom ndani ukimuuliza anasema siyo kazi yako kujua wewe si unaumwa unataka nifanyaje mara ukipika chakula hali au ataanza kula yeye mabaki ndo ule wewe nilikuwa na wakati mgumu ambao hauelezeki nilivumilia mpaka nikajifungua ana mtoto lakini yeye alikutwa salama hana maambukizi basi mwanaume akaanza kumchukia mpaka mtoto akawa anaongea mpaka na wanawake mbele yangu akafikia hatua ya kutaka kumchukua mtoto wake akidai kuwa hawezi ruhusu mwanae alelewe na mama mwenye virusi bora ampeleke vituo vya kulelea watoto yatima .
Mateso yaliendelea maisha yakawa magumu akanitelekeza na mtoto akaona haitoshi akamwambia mwenye nyumba kuwa yeye halipi tena kodi nikafukuzwa, nikaja kugundua kumbe alikuwa mume wa mtu pia alinidanganya kuwa ana watoto wawili kumbe ana watoto 5 pamoja na wangu wa 6 ambao 1 mama mwigine 4 mama 1 pia alivonitelekeza mimi alienda kuzaa watoto 2 kila mtoto na mama yake nyumba magari ikawa mali ya mke wake mimi nikaachwa sina chochote hata hela ya kuanzia maisha sina na wakati huo nilikuwa naumwa pamoja na mawazo basi hali yangu ilizidi kuwa mbaya siku 1 nikataka kujiua ndipo nikakumbuka kuwa nina watoto wananitegemea pia naweza kuanza upya nikaamua kumrudia Mungu pia nikamuomba Mungu anisaidie ili niweze kumsamehe huyu mwanaume maana kuna muda nilikuwa natamani hata nisikie amekufa nikamwambia na yeye kuwa mimi sitakulipiza ila Mungu ndo atanilipia.
Hivo akanitelekeza na mtoto nilijaribu kumwambia anisaidie ila alikataa basi nikamwachia Mungu kuna dada 1 akajitokeza akanisaidia mimi na mtoto nikawa naishi kwake hakujali afya yangu mpaka sasa ni mwaka wa 5 tangu tuachane mwanangu sasa hivi ana miaka 6 nashukuru Mungu. Basi mwaka juzi nikaanza kupata taarifa zake kuwa amefilisika yaani magari yote kauza pia baadhi ya nyumba kauza na maisha yake magumu nikasema sitaki kujua chochote kuhusu yeye maani aliniacha kama mnyama hakujali hata damu yake pia kati ya wanawake aliozaa nao aliibuka 1 na kuanza kunitukana kuwa nimeachwa sababu ya ukimwi nikasema sawa yaani alienda kunitangaza mpaka kwa familia yake na marafiki zake, mwaka jana mke wake akafariki niliumia sana maana alimwacha mtoto mdogo ambaye analingana na wangu..
Sasa kilichonileta kwenu ni hiki huyu mwanaue tangu afariki mke wake ananisumbua kuwa yeye anataka turudiane kuna kipindi alinambia kuwa yeye anatumia nyota yangu hivo inatakiwa nirudi kwake pia hata kuolewa sitaolewa labda nirudi kwake amekuwa mtu wa kashfa sana mtoto wala hana upendo nae yaani ana ule wa kinafiki kila anavoniona anadai tukalale sasa nikamuuliza uliniacha kwakuwa nimethirika leo nini kinakuleta eti ni shetani mtoto kutunza mpaka mgombane ila yeye anataka nikawalee hao watoto wake wengine kila anae nisaidia lazima agombane nae yaani mtu wa kuniharibia
Sasa hivi mwili wangu umerudi anaona wivu eti huyo mwanaume ulie nae ana faidi kweli naomba unizalie tena mtoto kashakuwa mkubwa yaani hataki niwe na raha nikamjibu mimi sio kiwanda, simpendi hata kidogo na yeye anajua ila anafosi mpaka sasa hivi sijui kinachomrudisha kwangu na nikimwangalia tabia bado zilezile uongo na kupenda wanawake ukweli sijui anataka nini tena kwangu nashindwa kuelewa sasa hivi anajifanya kuhudumia mtoto wake..mimi bado sijakubali kurudi tena kwake je huyu ni mutu sahihi kwangu au ana lake jambo?

