BINTI YANGU ANAOLEWAJE NA MWANAUME AMBAYE NILIKUWA NA MAHUSIANO NAYE
Mimi ni mama wa watoto watatu,tuliachana na mme wangu baada ya kushindwa kuelewana,nikapata mwanaume mwingine tukaanza mahusiano hajaoa ni kijana Bado na alikuwa hajawa na kazi ya kueleweka tukadumu kwa miaka miwili nikamtambulisha kwa baadhi ya ndugu na marafiki,mwaka huu mwanzoni akafuatilia vyeti vyake vya shule na mwezi wa tatu alituma maombi ya kazi baada ya nafasi kutolewa na serikali,majibu yakatoka amepata kazi mkoa wa Mbeya mwezi wa nane akaenda kuanza kazi akitokea Mwanza kwenda Mbeya akaniacha Mwanza
Tukaendelea kuwasiliana vizuri,ghafla akaanza kubadilika akaanza kuwa ananiambia habari za kwangu kuwa anaambiwa na watu nimebadilika navaa suruali navaa skate fupi nikamwambia ulivyoniacha ndiyo hivyo nilivyo mpaka sasa basi ukatokea ugomvi kati yetu.
Sasa kilichoniumiza zaidi ni baada ya kugundua kuwa mmojawapo wa ndugu niliomtambulisha ndo mwiba kwangu pale aliponiambia kuwa mahusiano yetu yamefika mwisho na mwakani anamwoa Binti ambae ni mtoto wa shemeji yangu, huku nilikozaa watoto na ni Binti ambae alikuwa anaelewa Kila kitu kilivyo alielewa mahusiano yetu wazi na hata mama yake huyo Binti alijua mahusiano yetu.
Nimebaki nawaza kwanini wamefanya hivi kwangu yule ni kama Binti yangu anaolewaje na mwanaume ambae nilikuwa na mahusiano nae hii hali imeleta ugomvi mkubwa baina yetu kati yangu na familia ya shemeji yangu

