NIMEGUNDUA MUME WANGU AMERUDIANA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI
Mimi ni mama wa mtoto mmoja nilikua naishi na mume wangu vizuri japo wakwe zangu wananichukia..
Kilichonifanya nikuombe ushauri nilimfuatilia mume wangu na kugundua amerudiana na mpenzi wake wa zamani ambaye walikua wanasoma wote
Nikamweleza kama ninajua akadharau na kusema hawezi kuacha kuwasiliana nae nikaona nimwambie kama hutaki kuachana nae mimi naondoka hapa
Kabla ya Kumwambia swala la kuondoka nilimpigia mama yake na kumweleza mama yake hakunipa ushirikiano akaungana na mwanae siku moja niliangalia simu yake nikakuta meseji za yeye na huyo mwanamke kuwa wanaenda kuonana nikanyamaza
Kweli nikaona anajianda nikamuuliza unaenda wapi akanijibu anaenda kwao unarudi saa ngapi wakati sasa hivi ni usiku akanijibu mimi sirudi nikamwambia nimeona meseji zenu unaenda kuonana nae tukagombana sana mpaka kupigana baada ya hapo akachukua nguo zake na viatu akaondoka zake kwao
Mama yake akawa ananiambia nirudishe vitu vya mwanae mimi nibaki na vyangu nikamjibu sawa sasa kila nikimwambia aje achukue vitu vyake anasema atakuja kila siku atakuja sasa hivi yapata wiki mbili hajaja hata kumuona mwanae anatuma hela tu sio kama ya zamani lakini kidogo anatuma
Nishauri nifanyeje kuhusu vitu vyake?

