Niliwadanganya Wazazi Nina Mtoto, Ili Nimuoe Single Mother
Mie ni Mwanaume Wa miaka 32 Nikiwa na miaka 24 Nilipata Mchumba ambae ni mwanamke mwenye Mtoto mmoja na babaake Alishakufa kwa ajali alikuwa bodaboda sasa mimi ili niwe na huyu mwanamke niliamua kwanza kuwadanganya familia yangu kwamba na mimi nina mtoto hapo nipo chuo sasa familia ilibariki suala la kuwa na mahusiano na ilikuwa rahisi kwa sababu wote tulikuwa na watoto
Sasa changamoto inakuja mama yangu anaumwa saana anatamani kumuona mjukuu nakumbuka kaka yangu alifariki mwaka 2021 nilitafuta mtu akawa kama Bibi wa binti yangu na niligharamia akaja msibani kutoka uko mbali kwahiyo wazazi wanamjua bibi yake na sio mtoto sasa shughuli inakuja wazazi wanataka wamuone binti yangu lakini changamoto ni hayupo na sijui cha kufanya naenda kuumbuka maana mama anamhitaji Sana ndio nawaza niwaambie ukweli au nitoe sababu na kama sababu nitoe ipi na kuna kipindi niliwahi pewa gunia mbili za mpunga nikaambiwa moja niache kwaajili ya matumizi na lingine nikawape wakwe mie nikapeleka kituo cha watoto yatima sasa wanahitaji kumuona mtoto.
Msaada tafadhari……


3 Comments
Hey very cool site!! Man .. Beautiful .. Amazing .. I will bookmark your blog and take the feeds also…I’m happy to find so many useful information here in the post, we need develop more strategies in this regard, thanks for sharing. . . . . .
Great wordpress blog here.. It’s hard to find quality writing like yours these days. I really appreciate people like you! take care
Keep working ,impressive job!