Nilimsaidia Pesa Apate Pasipoti, Kafika Ulaya Kasema Hanitaki
Mimi nina mpenzi wangu ambae ndani ya mwaka mmoja hadi sasa tulipitia changamoto nyingi sana alikua anafanya shughuli ndogo ndogo. Lakini kwakua alikua anayo passpot akaniomba nimsapoti pesa ili aweze kupata safari ya kwenda nje kufanya kazi. Nilijitahidi sana hadi tulifanikiwa na Mungu alibariki akaondoka lakini ahadi yetu ilikua nikuoana baada ya wiki moja. Kupita nakaingia katika mtandao wa kijamii
Nilikuta mpenzi wangu amepost picha za mwanamke mbili akiwa ameandika majina ya kimahaba niliumia sana baada ya kumtumia zile picha akujibu chochote kile siku tatu kupita niliamua kumuliza kwani umeyafanya yote haya kwa ubaya gani nilokutendea na mbona ni mapema sana alinijibu ulicho kiona kinajielezea na sitabadilisha mamuzi yangu wewe nitakupenda tu ila Moyo wangu kuishi na wewe ndio siwezi na hata ukipata mtu olewa nae tu ila kwa sasa kama ulipo panga nitalipa kodi chochote nitakusapot na usitegee ipo siku nitabadirisha wazo sahau
Nikamuliza huyu uliemposti ndio unahitaji kuja kuishi nae akanijibu bado sijachagua wa kuishi nae niliamua tu kumpost ila kwako ukweli ndio huo napitia wakati mgumu sana na ninaumia sana siwezi kuelezea ila naumia sana
Nipeni Ushauri Jamani


1 Comment
It is really a great and helpful piece of information. I’m glad that you shared this helpful information with us. Please keep us informed like this. Thanks for sharing.