Kila Siku akawa Ananitumia Onyo, Nikae Mbali na Mke Wake
Naombeni ushauri wenu wapendwa
Baada ya kuumizwa sana na wasichana hawa wa rika langu.si unajua hali ngumu ya maisha hii basi naishiwa kupendwa chumbani lakini naachwa sababu ya kujitafuta kipesa
Nikajikuta nimedondokea kwenye penzi la sugarmama…Tulipendana sana na kiukweli namshukuru sana alinisaidia sana na nilimpa furaha.tulikua kwenye mahusiano zaidi ya miaka miwili hivi.
Kabla hajakua na mimi,yeye alikua na mme wake na alizaa nae mtoto mmoja ila kwa kupishana kauli waligombana na kutemgana ndo akawa na mimi.
Mwanzo alikua ana stress nyingi sana,nikamuweka sawa na sikua na nia ya kumtaka ila kwa ukaribu niliokua nao wa kumfariji tukajikuta tumeingia kwenye mahusiano
Mahusiano yalikua mazuri tu.akazama kwenye penzi langu…nikapata chuo nikawa mbali na yeye ila akaamua kuhamia nilipo ili tuwe karibu kwa sababu ya biashara zetu
Sasa baada ya kuendelea vizuri kimaisha yule jamaa yake wa mwanzo akajua kuwa nipo nae
Akapatwa na wivu akawa ananitumia meseji ya kua nikae mbali na mke wake. Nikimwambia mke wake nae anasema niachane nae kwa kuwa waliachana na allipewa na taraka
Sasa kila siku akawa ananitumia onyo nikae mbali na mke wake na huwa mkali zaidi akimuona mke eX wake mwenye furaha sana na mambo yake yananyooka
Sasa,siku moja aliamua kunifata mpaka kwangu kwa kuniomba niachane na mkex wake.kwa vile sikutaka shari wala maugomvi nikaamua nijiweke pembeni kwanza na kumwambia mpenzi wangu amalizane na mtu wake kwa ajili ya usalama wangu…kama ameweza kupajua na kunifata napoishi basi hatoshindwa kunifanyia chochote
Sikuelewa mpenzi wangu alipatwa na kitu gani? Badala yake akaamua kurudiana na yule mme wake sababu mpaka leo sijazijua
Aliniomba msamaha kwa maamuzi aloyafanya,iliniuma ila sikua na budi kumsamehe na kumwacha aanze maisha mapya na mpenzi wake cause sikutaka awe na stress
Sikua na mawasiliano,ikavuka mpaka miezi 8 bila kutafutana,nikapata habari amezaa nae.
Sawa niliachana nae ila hiyo taarifa iliniuma kwa ndani..Nika move on na nikaona labda sina bahati na mahusiano
Baada ya miaka miwili hivi yule akaomba turudiane tena na mimi tangu niachane nae nilikua sina mtu yule wa serious kabisa hadi leo..
Anataka turudiane cause mme wake hawaelewani tena awamu hii anakua anapigwa sana
Jamani naombeni ushauri wenu…kiukweli nikipenda hua napendaga kweli kabisa,na kila siku ananiomba msamaha kua turudiane tusahau ya nyuma yani inafikia hatua hata mtoto wake wa kwanza analia kwa baba yake akisema anataka kurudi kwa uncle na huyu mdada kila siku analia turudiane anajuta kwa alichonifanyia
Na mume wake awamu hii amekuja na vitisho vikali sana…Je niende upande gani na huyu mdada namuonea sana huruma.. Naombeni ushauri wenu jamani… Nipo naangalia kwenye comment zenu.

