Mwanaume Ninayetegemea Anioe, Nilimpiga Bibi Yake
Kaka naomba unisaidie kwa ushauri kwa sasa naishi na mwanaume tume tambulishana kwao na kwetu. Nina watoto wa tatu huyu wa kwanza nimezaa na mwanaume mwingine alinikuta na mtoto sasa kwenye harakati za kutoa mahari akasema tukaishi wote tukaweke mipango ya ndoa sawa kwakua alinikuta na mtoto nikasema maneno yakiwa mengi ataahirisha kila kitu tukaondoka tukienda kupanga mipango ya ndoa maana anasema hajajipanga kifedha basi nikakubali
Kufika maisha yanaendelea na kila nikimuuliza kuhusu ndoa haeleweki wazazi wangu wanakosa la kufanya maana amesha nizalisha watoto wawili halafu bado wadogo hata nikiondoka nao sitaweza kufanya nao kazi kila nikimuuliza kuhusu ndoa haeleweki huyo mtoto alie nikuta nae amempeleka shule ya praivet nilifurahi lakini niliona kama ndo chambo Cha kuninyasa mama matumizi hanipi nikimkumbusha akijitahidi ananipa elfu hamsini
Akamleta mama yake kipindi nataka kujifungua nikajifungua mamake ni mtu mongeaji sana Mimi ni mpole siwezi ongea maneno mengi kila akiongea Kuna maneno namwitikia tu anaanza kukutukana na kukuchamba nikajifungua nilinyojifungua mamake akawa anahitaji kitovu Cha mtoto na nywele za utosi nikamnyima alinitukana sana mbele za watu nikampigia huyo mwanaume hakuongea lolote huyo mama alirudi kwake akiwa ana hasira
Akamleta mjukuu wake niishi nae ikiwa huyu mwanaume naishi nae mbalimbali yeye yupo mkoa mwingine Mimi mkoa mwingine amenambia niishi huku ndo makazi yake yeye yupo huko kikazi anakuja siku Moja Moja sasa huyu mjukuu wa kike ambae ni mjomba wake tukakaa siku zikaenda akapata kazi ya uwalimu wakujitolea kiujumla anamtegemea kila kitu huyo mjomba wake mpaka nauli ya kwenda kazini ana mtoto wa mwaka mmoja Mimi pia ni mjamzito wa mtoto huyu wa tatu nikawa namtafuta mtu wa kunisaidia nikawmbiwa usimtafute mtu wa kukusaidia huyu nitakae mpata wa kukaa na huyu mwanangu anatosha sikumjibu nikajisemea kwani ananipangiaje
Nikampigia huyo mwanaume akasema ndiyo huyo Mmoja anatosha nikamwambia anatosha vipi na Mimi ni mjamzito najisikia vibaya na huyu mtoto mwingine ndo nimemwachisha na wakati huyo atakaekuwa na mtoto wa mjomba wako inatakiwa awe karibu nae akawa hana mwelekeo
Basi nikamleta huyo wa kunisaidia siku zikaenda mjomba mtu akaanza drama akawa anampigia mjomba wake tunakula vitu vizuri yeye hatumpi anasema namnyanyasa maneno mengi sana akiwa anaangalia kwenye simu akiongea na mjomba wake ikawa nyumba Haina amani ananitukana kwenye simu nikavumilia bibi yake akaja kwa hasira kutoka kwake na kutaka kunimwagia maji ya moto
Ulikua ugonvi mkubwa sana huyo mama nilimpiga kulikuwa na kimbao chini sijui hata nilinyanyua vipi Ile kipande Cha mbao nika mpiga nacho kichwani akamwita mtoto wake wakamwambia nimempiga ugomvi ndo ukaiva ikawa tunapigana na huyo mwanaume wakawa wao ndo watazamaji hicho kitu mpaka Leo kinaniumiza naujiuliza hapa nasubiri ndoa gani naomba ushauri

