Nilimpima Ukimwi Bila Yeye Kujua, Nikagundua Ameathirika
Mimi huwa Nina kawaida, kabla ya kulala na mwanamke yeyote lazima nimpime magonjwa yote ya zinaa ikiwemo virusi vya UKIMWI.
Nilikuwa nimempata binti mmoja hivi anafanya kazi sheli, Sasa tulikuwa tume kubaliana juma mosi tushinde wote kwangu Kwa sababu ni siku ambayo nashinda nyumbani, Sasa nikawa nime mwambia Mimi silali na mwanamke kabla sijampima, yeye akasema haina shida anajiamini na Yuko sawa tu.
Sasa Leo asubuhi nilimwambia achukue usafiri aende maabara Moja hivi ambayo huwa naitumia sana kuwapimia, pale Kuna jamaa ambaye ni rafiki yangu na ndo dokta hapo, akisha wapima huwa ananipa majibu Mimi.
Sasa bwana, jioni hii dokta kanipigia simu kanipa majibu kuwa binti anao UKIMWI ila magonjwa mengine Hana, ila dokta akanishauri nisimwambie binti kuhusu hicho kitu.
Binti yeye mpaka muda huu ananitumia sms kuwa anatamani jumamosi ifike haraka , Yani ana hamu sana na Mimi kuashiria kwamba Hana hofu na majibu ambayo nimeambiwa,
Dada naomba unipostie hivi ni sawa kutomuambia huyu binti? Mana bado ni mdogo ana miaka 22 tu.


1 Comment
Wonderful post but I was wanting to know if you could write a litte more on this subject? I’d be very grateful if you could elaborate a little bit further. Bless you!