Sitosahau Nilivyoweka CD ya Wakubwa, Umeme Ukakatika
Kipindi hicho bwana nimetoka likizo Niko kidato Cha tatu, ilikuwa ni mwezi wa 6,
Sasa bwana siku hiyo nimetoka usingizini mchana nyumbani hakuna mtu yeyote, ikabidi niende Kwa washikaji zangu jirani, nikawakuta Wana malizia kucheki muvi zetu zile za wakubwa, Yani warumi, ikabidi niwaambie ebu rudisheni mwanzo tucheki, wakagoma, Waka niambia ngoja wamalizie Ili wanipe CD nikachekie kwetu Ili wao waweke CD ya mziki.
Baada ya muda wakachomoa CD wakanipa, Mimi nikaenda nyumbani Ili niangalie Kwa utulivu, Yani muda ule nimechomeka CD na kuanza kuplay, umeme ukakata, nilisikia nje washikaji wakija huku Wana Cheka, oya, siku hiyo nilihisi Dunia yote nimeibeba Mimi, nikachukua Deki Ili nianze kuifungua nitoe CD lakini nikawaza hapa wakikuta imeharibika lazima wajue ni Mimi tu mana nyumbani nilibaki mwenyewe, nikawaza nipeleka Kwa fundi Ili watoe CD lakini napo nikawaza fundi nitamwambiaje.
Muda huo ni saa kumi jioni, hapo mama yupo kanisani, Mzee yupo kazini na wadogo zangu wapo tuition, washikaji walinicheka nikawa nahangaika tu mpaka nikawaza niende tanesco kuwaambia angalau wawashe kama dakika Moja tu Ili nitoe tu CD lakini wapi, jasho likawa linanitoka tu.
Siku hiyo hata uwanjani sikwenda, washikaji walienda ila Mimi nikabaki nalinda Ili umeme usije kurudi na Mimi sipo halafu wawashe wakutane na vitu vya ajabu, itakuwa musala mkubwa .
Ilibidi nikae hapo, mara ikafika saa 11, umeme haurudi, ikaenda mpaka saa 12, umeme hakuna, mara nikamuona mama huyo anarudi ndo nikazidi kuchanganyikiwa, alivyo zidi kunichanganya ni alivyo niambia nifuate maziwa sehemu, ilibidi nijifanye naumwa hivyo awasubiri wadogo zangu watoke tuition,
Saa Moja Mzee naye akatoka kazini, nikasema hapa Leo naona ni siku yangu ya kufukuzwa nyumbani, naona kabisa Shetani kanipania, mida ya saa mbili usiku ambayo ndo mida ya Mzee kukaa sebuleni kuangalia taarifa ya habari ikafika lakini umeme ukawa bado.
Siku hiyo ilibidi nikachukue madafutari yangu yote nikawaambia Leo nasomea sebuleni, nikawasha mshumaa na nikawaambia sitaki kelele hapa, Kwa vile Mzee alikuwa ana heshimu sana uwezo wangu kielimu basi ikabidi yeye aende chumbani kupumzika, nikasema ahsante MUNGU nashukuru hata Kwa hiki kidogo.
Tulivyo maliza kula mida ya saa tatu mama naye akasema Kuna vitu anaandika vya kanisani mana alikuwa katibu, akawa na yeye yupo hapo sebuleni, kumbuka mama hapo umeme ukirudi lazima awashe Tv afanye mambo yake huku kwaya Zina imba, na kwetu ilikuwa ni marufuku kupiga miziki, ilikuwa ni kwaya tu mwanzo mwisho,
Ilifika mpaka saa 4 usiku umeme haujarudi, mida kama yaa saa 5 kasoro robo hivi mama akamaliza Mambo yake akaenda kulala, Yani muda ule ule katoka kama dakika tano tu umeme huo ukarudi, Yani niliruka chapu mpaka kwenye deki, nikabonyeza na CD ikatoka nikarudisha ya kwaya, nilipumua Kwa Kishindo mpaka nikakaa chini na kutubu kwamba sitorudia kuangalia hizo video Mimi huku natokwa na machozi na jasho juu.


1 Comment
Hey malizia hiyo story ya c,d