Nimefanya Mapenzi na Mama Mkubwa hadi Nimekimbia
Mimi ni kijana wa kiume, umri wangu ni miaka 20, nime maliza kidato Cha 4 mwaka Jana ila Kwa bahati mbaya sikufaulu kuendelea na masomo.
Dada Mimi nimelelewa na bibi yangu, wazazi wangu wote walifariki kwenye ajali ya moto nikiwa na miaka minne.
Mwaka Jana nilivyo maliza kidato Cha 4 mama yangu mkubwa alikuja kunichukua Kwa bibi Ili niende kuuza duka lake, kweli nilienda nikawa nauza duka lake, pale kwake alikuwa na mtoto wakiume mwenye umri kama wangu ila hakutaka niwe nalala naye akanipa chumba Changu.
Sasa Kila usiku akawa anakuja kavaa khanga tu chumbani kwangu anakaa huku ananiuliza uliza maswali, akawa ananichezea chezea na mwisho wa siku akawa ananilazimisha tunafanya mapenzi, ilifikia hatua nikazoea ikawa ni Kila siku usiku, akienda dar kufunga mzigo tuna ondoka wote anachukua chumba tunakaa mpaka wiki ndo tuna rudi.
Ilifikia hatua mpaka nikachoka ikabidi nitoroke nirudi nyumbani Kwa bibi,
Kwa Sasa nina mwezi Niko Kwa bibi, mwanzoni alikuwa ananibembeleza sana nirudi Kwa kuniahidi ataninunulia pikipiki ila nikawa nagoma, Sasa tokea juzi ananitishia nisipo rudi kwake ata mwambia bibi na mamdogo kuwa nilimuibia hela ndo nikatoroka,
Dada Mimi sikuiba hela, hata nguo niliziacha niliondoka na nguo tu ambazo nilikuwa nimevaa, Nilichoka matendo yake tu, miezi 6 niliyokaa pale sikuwahi kupumzika ilikuwa Kila usiku lazima aje.

