Nilikeketwa, Naogopa Kumuambia Mchumba Wangu, Ndoa ni Mwezi wa 11
Mimi ni binti , Nina miaka 27 mpaka Sasa, nafanya kazi kwenye taaisisi Moja ya fedha.
Mimi utotoni nilikekeketwa, na hiyo ndo sababu imefanya mpaka Leo niwe bikira Yani sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote, Kila nikiingia kwenye mahusiano na mwanaume likija suala la kufanya mapenzi ndo inakuwa mtihani kwangu, nahofia watanishangaa, japo natamani na Mimi niwe kwenye ndoa au mahusiano mazuri ila naogopa hicho tu.
Sasa Kwa Sasa Niko kwenye mahusiano, huyu kaka licha ya kumpa sharti la kutofanya mapenzi mpaka anioe yeye alikubali, na amesha jitambulisha kwetu na mahari katoa, harusi imepangwa kufanyika mwezi wa 11, Kwa Sasa Nina mawazo nafikiria itakuwaje akinikuta hivi na sikumwambia,
Imefikia hatua mpaka nawaza labda nimwambie sitaki tena kuolewa ila napo tena naogopa mana tayari maandalizi ya Kila kitu Yana endelea.
Naomba unipostie na Mimi, sielewi Cha kufanya Mimi.

