SAMAIRAH
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 3
Oya bajaji njoo ,yule jamaa aliita ile bajaji ambayo ilikuwa imewabeba akina Aryan baada ya kutoka hospitalini kwa mara nyingine ikawarudisha hospitalini wote watatu wakiwa hoi.
Walipelekwa kwenye ile hospitali ambayo walitoka kumtibu Gwae,walipokelewa upesi kisha wakaanza kufanyiwa matibabu
Aryan alikuwa anafahamu zake ila damu nyingi ndio zilikuwa zinamtoka
Gwae alipelekwa tena kwenye chumba cha kufunga p.o.p huku Abbas na Aryan walisafishwa yale majeraha ambayo walipigwa na chupa.
Saa tisa usiku ndio Abbas alizinduka na kumkuta Aryan yuko pembeni yake ,Aryan alisikia maumivu makali alivyopeleka mkono kichwani alikutana na pandeji ndipo akakumbuka jana alipigwa na yule kijana ambae ndio anatembea na mama yake.
Abbas aliuliza mama yangu yuko wapi? Lile swali lilimfanya Aryan ainamishe kichwa kisha akasema mama yako amewakana mbele ya yule kijana ambae ulimwona yuko nae na amesema hawajui wala hawatambui.
Yale majibu yalimfanya Abbas alie kama mtoto ,ndipo Aryan alichukua jukumu la kumnyamazisha hadi aliponyamaza.
Asubuhi palipo kucha Aryan alimwendea daktari na kumweleza kuwa awaruhusu wakamalizie mtihani halafu watakuja kulipa pesa ambazo zimetumika katika matibabu, yule dakatari alikuwa muelewa aliwaruhusu ndipo waliondoka wote watatu ,huku Gwae amefugwa mhogo ama gamba gumu mikono yote miwili.
Aryan alikuwa na hasira alienda hadi nyumbani alimwacha Gwae kwa mama yake kisha wao wakaingia darasani wakiwa na bandeji,
Ile Aryan anaingia darasani
Jesca alikuwa wakwanza kumwona alimkimbilia na kwenda kumkumbatia,ile anayapeleka macho yake kwenye paji la uso ndipo alikutana na bandeji kubwa aliyageuza macho yake na kumwangalia na Abbas alishangaa kumwona ana bandeji usoni,
Mara Nanaa akaja pamoja na mwenzake Lusi walimsalimia kisha wakamwambia pole Aryan umefanyeje? Kabla hajawajihu Joyce akaingia darasani taratibu akiwa anachechemea maana tokea alivyochomwa bisi bisi mguu wake bado hujapona.
Joyce alikuwa kashika zawadi ya Aryan alivyomwona Aryan na bandeji Joy alijikuta akibaki mdomo wazi ,mara kundi la akina Kudra likaingia darasani kwa fujo walishangaa kuwaona Aryan na Abbas wamesimama huku wanafunzi wenzao wakiwashangaa.
Mara mkuu wa shule akaingia huku kashika fimbo ,mkuu aliongea kwa ukali nani kavunja kioo cha nyumba yangu usiku na kuniibia pesa.
Kudra na Mussa waliwanyoshea mikono Abbas na Aryan ,mkuu hawa ndio wezi angalia usoni wanabandeji bila shaka hao ndio wezi maana inaonekana wamepasuliwa na vioo walikuwa wakiiba
Mara polisi wakaingia wakiwa wameshikilia pingu ,mkuu wa shule aliwanyoshea mkono akina Aryan na kusema wezi wenyewe ndio wale
Tulipoishia jana baada ya mkuu wa shule kuingia darasani akiwa kaongozana na polisi , aliuliza mwizi aliyevunja dirisha na kuiba pesa zake,akina Kudra waliwanyoshea mikono Abbas na Aryan kuwa hao ndio walioiba maana hata kwenye vichwa vyao walikuwa na bandeji tena zinaonekana bado mpya,
Polisi waliwafuata Aryan na Abbas kisha wakawaambia mpo chini ya ulinzi,Aryan hakupenda kabisa kubisha alinyoosha mikono yake na kufungwa pingu huku Abbas nae akitii amri ya polisi
,Aryan aliwaangalia wabaya wake wanao yasakama maisha yake alijua kuwa hii ni njama imefanywa na akina Kudra ili wafukuzwe ,kazi na ndio ilikuwa siku ya mwisho wamalizie mitihani,
Akina Jesca walimshika Aryan huku wakilia na kusema Aryan hajaiba jamani Aryan hajaiba,Joyce nae alianza kulia taratibu maana mtu ampendaye ndo hivyo anasemekana ni mwizi hivyo hatomwona tena.
Mara walimu walibidi wakaongee na polisi ili wawaachie akina Aryan wamalizie mitihani ,halafu wakishamaliza watawachukua na kuwapeleka kituoni, mkuu wa shule aliwaka na kusema hapana kunifundisha kazi pelekeni kituoni.
Walipakiwa kwenye difenda kabla gari haijawasha kuna gari ya wawekezaji walio wekeza kwenye hio shule ,waliomba wanafunzi waachiwe kisha uchunguzi ufanyike kwanza halafu waachiwe wakamalizie mtihani,
Aryan na Abbas waliruhusiwa kisha wakaingia darasani ,ile wanaingia darasani ndipo na Samairah aliingia darasani ,lakini Samairah kabla hajaingia darasani alimfuata muwekezaji mmoja na kumpatia flashi kisha akasema baada ya kumaliza mtihani ataichukua.
Basi polisi hawakuweza kuondoka walikaa mlangoni kabisa na chumba ambacho akina Aryan wanafanya mtihani,Aryan alifanya mtihani wake kama kawaida.
Tukirudi nje wawekezaji walitoa laptop kisha wakaweka ile flash waliopewa na Samairah, kila mmoja alibaki kukodoa macho hatimae waliita na walimu waje kushuhudia wakati huo mkuu wa shule yupo kwenye ofisi yake.
Kwenye laptop kulikuwa na video iliyorekodiwa majira ya saa kumi na moja alifajiri ,kulikuwa na kijana Mussa pamoja na Kudra wakiwa katika nyumba ya mkuu wa shule.
Mkuu wa shule ndio aliwaambia akina Mussa ,sasa tutafanyaje ili tumfukuze Aryan shule,Kudra alitoa wazo mkuu sisi tunakupa pesa kisha tunabomoa haya madirisha yako ya vioo na kuyapasua halafu ,tutasingizia Aryan kaiba pesa sababu yeye kwao ni masikini na kibaya zaidi hana nyumba,nyumba yao ishaunguaga moto kitambo,’
Mkuu wa shule alitabasamu na kusema hakika ninyi mnaakili alipewa kiasi cha pesa kisha Mussa na Kudra wakabomoa vile vioo vya madirisha ,
Wakati wanafanya hayo bibie Samairah aliwanasa na kuchukua mkanda kupitia kamera ,na kuhifadhi kwenye flashi , wawekezaji walipata ukweli kuhusu mkuu wa shule ,walichokifanya walichukua polisi na kwenda kumkamata mkuu wa shule na kumpeleka kituo cha polisi aeleze kwanini anashiriki katika masuala ya rushwa tena na wanafunzi wake.
Aryan alimaliza mtihani akatoka nje cha ajabu hakukuta polisi wala mkuu wa shule, alivyouliza polisi wako wapi ,wanafunzi wakidato cha kwanza walimweleza kuwa kesi imegeuka kwa mkuu wa shule na ashakamatwa ,Aryan alishidwa kuelewa , ,
Samairah alimaliza mtihani na kumfuata Aryan ,kisha alimsalimia na kumweleza kila kitu walichokifanya akina Mussa ,Aryan aliuliza sasa akina Mussa wanataka kunifanya nini mimi, kuniua ama kuniachisha shule, Samairah alitabasamu na kusema safari bado ndefu ,
Aryan umefanyaje hapo kwenye paji la uso ,Samairah aliuliza ,Aryan nae hakupenda kumficha kilichotokea alimweleza kila kitu kilicho wakuta jana.
“Pole” ndio neno alilolisema Samairah kisha akaondoka ,tukirudi kwa Aryan aliwaza sasa “tushamaliza mtihani na kesho ndo siku ya kupewa matokeo na kufunga shule” , Aryan alifurahi ili aweze kukaa mbali na akina Mussa.
Hatimae masaa yalienda jua likazama na siku nyingine iliwadia siku hio wanafunzi walipendeza na wengine walifurahi maana ndio ilikuwa siku ya kufunga shule
Kengele iligongwa na wanafunzi walikusanyika mahali wanakofanyiaga shughuli za kishule kama ilivyokawaida kulikuwa na wageni wawekezaji wa hiyo shule ,mwalimu wa zamu aliwaambia wanafunzi wakae kimya na wasikilize kwa makini maneno yatakayosemwa na waalimu pamoja na wageni waliopo mbele yao.
Kudra alimnong’oneza Mussa na kumwambia mhula huu tunaosha sababu nishaongea na mkuu kila kitu ,mimi nitashika nafasi ya kwanza wewe wapili halafu na Jesca watatu. Basi walikaa kwa makini ili waweze kushinda hizo zawadi .
Mwalimu wa taaluma alisimama na kuanza kusoma matokeo ya kidato cha kwanza kama ilivyo kawaida ,walisoma wanafunzi watatu bora na kumi bora,waliobahatika kupata nafasi ya kwanza hadi ya tatu walizawadiwa begi na makaunta book na kupigiwa makofi na shule nzima,ila kwa msimu huu wawekezaji waliboresha vizuri mshindi wa kwanza anapata shilingi laki mbili wapili laki moja na watatu elfu hamsini.
Wanafunzi walifurahi sana ,hatimae mtaaluma alisoma matokeo ya kidato cha pili na alivyomaliza alihamia matokeo ya kidato cha tatu,kwanza mwalimu wa taaluma alisema katika shule hii darasa la maajabu ni kidato cha tatu,kwanza wanafunzi wana akili sana pili wana ushindani mkubwa
Mtaaluma alitaja nafasi ya kwanza mhulaa huu imeshikwa na watu wawili wamegongana ,Aryan ,pamoja na bibie Samairah,wanafunzi walishangilia kwa fujo hasa hasa wanafunzi wakike wanavyompenda Aryan ,basi walianza kutaja Aryan ,Aryan,nakuwafanya hadi wawekezaji kutabasamu,
Aryan na Samairah wakiwa na ufaulu sawa sawa ,walibeba zawadi zao.
Mtaaluma aliendelea nafasi ya pili wamefungana watatu ,,mwalimu wa taaluma alivyosema hivyo Mussa na Kudra walijiuliza hio nafasi ni yetu ,watatu mimi wewe na Jesca, halafu Kudra akauliza hivi mkuu wa shule kala pesa zetu alafu hajafanya sawa wala hapa simwoni ,”mtaaluma alianza kutaja majina ,wakwanza ni “j” yaani alitaja “J” Jesca kasimama ,ndipo akamalizia Joyce basi Jesca alikaa kwa hasira na kuwaangalia akina Mussa
Walikuwa Joyce,Abbas,na Nanaa
Basi makofi yalipigwa nderemo na vifijo vikatawala, ndipo Mussa akaanza kukunja sura, nafasi ya tatu alikuwa Jesca pamoja na Lusi
Hakika kidato cha tatu kiliweka historia
Nafasi ya nne alikuwa Amina ,kuanzia nane na kumi ndio zilikuwa namba zao akina Mussa na Kudra.
Kudra wala hakusubiri waalimu wamalizie aliondoka akiwa na hasira na kwenda kukaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule, hili li mkuu wa shule naenda kumtoboa hicho kitambi anipe pesa zangu ni maneno aliyoongea Kudra.
Baada ya waalimu kumaliza maongezi hatimae walipewa tarehe ya kufungua shule ,ndipo mwalimu Farida alisema naomba wanafunzi wakiume wa kidato cha tatu ,
Waje hapa ,walienda kama walivyoambiwa.
Mwalimu aliwaambia wapande kwenye gorofa ya nne ya jengo la hapo shuleni ,halafu kwa juu yake kulikuwa na sehemu ya kuhifadhi maji walikuwa wameweka matanki ya maji
Jamani wanafunzi nane naomba mpande mkateremshe lile tank la lita 2000 mtalisukuma tu halafu litaashuka taratibu mkiwa huko juu muwe makini msisukumane mtadondoka ,kati ya walio chaguliwa Mussa na Aryan walikuwemo ,
Mussa akiwa na hasira hajapata nafasi ya kwanza halafu Aryan kaongoza, ‘Mussa aliwaza leo Aryan ndio siku yake ya mwisho tukipanda juu naenda kumsukuma adondoke chini ,leo ndio leo ,ni mawazo aliyoyawaza Mussa
Walipanda kwenye gorofa la pale shuleni hadi gorofa ya nne halafu kwa juu yake.walifanikiwa kuteremsha lile tank,
Lakini walivyomaliza wanafunzi walianza kuteremka ngazi na kushuka,
Mussa alimvuta Aryan shati na kumwambia wewe boya naona unajifanya kisa unashika namba moja ,Aryan ukweli sikufichi na unaona hapa tulipo nakusukumiza chini udondoke
Leo ndio siku yako ya kufa Mussa aliongea huku akitoa kisu chake kidogo mfukoni mwake.
Alimshika shati ,Aryan,na kumwambia nimekutafuta sana leo ndio nimekupata mahali pake unaona hichi kisu nakuchoma nacho tumboni.
Aryan alimwangalia Mussa ambae yupo siriazi ,kiukwelii kabisa ,Aryan aliona akizubaa anaweza kufa alitoa sauti kwa nguvu jamani msaada naku……
Aryan hakuweza kumalizia tayari Mussa alikizamisha kisu tumboni,Aryan alifumba macho akiwa ameshikilia mpini wa kile kisu kilichopo tumboni,Aryan alijikuta anakuwa kimya
Halafu Mussa akatabasamu na kusema wewe boya nimekuwinda sana alimsukumiza chini,
Tambua wapo gorofa ya nne kwa juu yeke sehemu ambayo ilikuwa na matanki ya maji sasa amesukumizwa chini,
Na chini pana umbali, kibaya zaidi sehemu anayosukumizwa chini kulikwa na mawe makubwa mfano wa yale ya kujengea msingi.
Aryan ndio anashuka kisu kikiwa tumboni na chini ni mbali na mahali anakokwenda kkudondokea pana mawe
Mussa alimchungulia na kuona Aryan anavyoteremka alitabasamu na kusema kuanzia sasa hakuna tena Aryan ,dakika sifuri tutaita marehemu
Tulipo ishia jana,baada
ya Aryan kufanyiwa unyama na Mussa alichomwa kisu tumboni,na kurushwa chini toka kwenye gorofa ya nne ,hatimae Aryan akiwa na hali mbya alifumba macho na kubaki kimya , alihisi kama roho inanyofoka tumboni kisu kimekitwa mahali pabaya.
Maeneo hayo jirani na hilo gorofa bibie Jesca walikuwa wapo na Samairah walikuwa wanapeana sweta,Jesca alikuwa kavaa sweta ya Samairah, Samairah alimwambia Jesca hebu nipe sweta yangu niwahi nyumbani kabla hajalivua lile sweta ndipo walisikia kicheko cha Mussa akicheka kwa dharau baada ya kumrusha Aryan.
Jesca aligairi kuvua sweta na kusema nani huyo anataka kunichungulia aone chuchu zangu (jesca anavopenda kujishaua) sasa ndipo walipogeuza macho ,juu walimwona Aryan akishuka toka gorofa ya juuu,Jesca alikuwa wakwanza kuogopa baada tu yakuona alisema mama yangu uwiii yule si Aryan ,alifumba macho na kulala chini huku kaziba masikio” mawazo yake yote aliyahamisha na kusema Aryan ndo unakufa bado sijaonja penzi lako”, wakati anaendelea kuwaza pale Samaira alikimbia upesi na kuwahi mahali ambako Aryan atadondokea.
Huwezi amini Samairah alisimama na kukinga mikono yake ,pale pale Aryan alitua mikononi mwa Samairah kutokana na uzito alionao Aryan ,hata ingekuwa warushiwa kitu cha kilo tano toka gorofani ukikidaka lazima mkono ushuke chini
Lakini kwa Samairah lilikuwa jambo la kushangaza alimdaka Aryan wala mikono yake haikutetereka ,
Samaira akiwa kamdaka Aryan aliita” Aryan uko salama “,ndipo alipoyapeleka macho yake tumboni mwa Aryan aliona kisu kikiwa kimekitwa tumboni.
Samairah alimtizama Mussa juu gorofani wala hakumwona , Mussa alijua tayari ashagundulika alianza kushuka ngazi upesi
Hio sehemu ilikuwa mbaya kuna mawe makubwa ,Samairah alianza kupiga hatua akiwa kambeba Aryan, Jesca nae alifumbua macho yakiwa yametawaliwa na machozi na kujua tayari Aryan kama si kupasuka kichwa basi mwili wake ungevunjika nyang’a nyang’a, Jesca hakuamini macho yake baada ya kumwona Samairah akimlaza Aryan akiwa anahema kwa tabu,
Mwalimu Farida hakuwa mbali na eneo hilo nae aliweza kushuhudia lile tukio aliwahi mahali aliko Aryan, na kuuliza “Aryan nini kimekusibu” kabla hajajibiwa nae aliona kisu tumboni mwa Aryan,
Ile hali ilikuwa yatia huruma Aryan alishidwa kuongea na kusema jamani kuna watu wenye roho mbaya alipo ulizwa nani kamfanyia kitendo hicho Aryan hakusema hata kidogo aliishia kulia.
Jesca nae alikuwa akilia na kuwaza kimoyo moyo,itakuwa si vyema Aryan anapoteza maisha na sijaonja lips zake ,nipate walau busu la handsome maana nampenda hadi sijielewi Jesca aliupeleka mdomo wake na kugandisha na mdomo wa Aryan kisha akampiga busu zito,
Aryan anafumbua macho alishangaa kumwona Jesca akimbusu ,,Aryan aliyafumba macho yake tena, ,mwalimu Farida alimpigia dereva wake alikuja na gari upesi hawakupenda kupoteza muda maana walijua wakizubaa Aryan anapoteza maisha.
Gari lilikuja na Aryan alipakiwa ndipo mwalimu Farida,Jesca pamoja na Samairah walipanda na kuanza safari ya kuelekea massana hospital. Hatimae Aryan alipokelewa upesi na kupelekwa chumba cha watu mahututi, madaktari bingwa walishika zana zao na kuanza kuushughulikia mwili wa Aryan
‘Tukirudi kwa mtaalamu wa roho mbaya naweza sema Mussa baada ya kushuka kwenye lile gorofa alikimbia alipo toka nje ya jengo la shule alimkuta Kudra akiwa kasimama mahali Aryan anapitaga wakati anarudi nyumbani ,Kudra nae alikuwa kajifunga kitambaa usoni ,huku mkononi kashika kisu kama kile ambacho Mussa alimkita nacho Aryan tumboni.
Mussa alikuwa anakimbia kujiokoa maana akigundulia lazima angefukuzwa shule kwa kitendo alicho kifanya ,
Mussa alikuwa anacheka na kujisemea lini mtu akichomwa kisu cha tumbo akapona ha ha ha Aryan fanya kuwasalimia kuzimu kuanzia sasa tuko huru .
Mara Mussa alisikia anaitwa alivyogeuka Kudra alishusha kitambaa alichofunga usoni na kuongea ” oya mwanangu yule boya yuko wapi” ,Mussa alicheka na kuonekana mwenye furaha baada ya kumwona rafiki yake Kudra alisema huyo kuanzia sasa hivi hesabu marehemu kisha akamwelezea tukio zima jinsi alivyomfanyia ,Kudra alifurahi kisha wakasema sasa tuko huru ,tufanye jambo moja tukavue haya manguo ya shule halafu baadae tukawatafute akina Joyce,Nanaa na Lusi wanako ishii ili tukiwapata nawao tuwafanyie kitu kibaya ikiwezekana tuwachukue tuwapeleke bahari beach ili tukaogelee ,hapo ndipo tutapata bahati yakuwazamisha kwenye maji hadi kufa kwao.
Ni mawazo aliyoyatoa Kudra kisha wakaondoka na kuelekea majumbani kwao,
Tukirudi hospitali ya massana baada ya Aryan kufikishwa hapo,madaktari walishidwa kumtibu na kusema hili tatizo wao hawataweza labda apelekwe muhimbili na kwamba akicheleweshwa muda wowote anaweza akapoteza maisha ,mwalimu Farida wala hakupenda kuchelewesha walichukua ambulesi ya pale hospitali kisha safari ya kuelekea mhimbili ilianza hawakuchukua muda sana hatimae waliweza kufika na kupokelewa ,Aryan alianza kufanyiwa matibabu kwa umakini wa hali ya juu.
Wakati huo Samairah kabaki na mwalimu Faridi huku Jesca aliondoka na kurudi kwao,njia nzima aliwaza Aryan hawezi kupona ila hata akifa sawa nishaonja busu lake tamu ila ndio hivyo atapoteza maisha ,Jesca aliwaza na kuingia kitandani kwake kulala.
Siku zilizidi kuyoyoma huku Abbas akiendelea kumhudumia mdogo wake Gwae,,maana mikono yake miwili yote imevunjika ilikuwa ni kazi kubwa kumvulia nguo kumwogesha na kumlisha hio kazi aliifanya Abbas, huku mama yao akiendelea na tabia yake yakutoka nyumbani na kushinda baa asirudi nyumbani hadi siku tatu,
Ilikuwa siku ya juma pili ndipo Abbas alikaa na mama yake sebuleni ,alimuuliza mama lini utaacha pombe na tuishi maisha mazuri kama kipindi cha nyuma.
Lile swali alilouliza Abbas lilimkera mama yake kisha akainuka na kufunga kitenge vizuri kiunoni,we Abbas siku hizi wajifanya umekuwa ee na umefikia hadi umri wa kuniuliza maswali hayo ,we mtoto nimekuzaa mwenyewe sitaki unifuatilie, nitalala na mwanaume yeyote nitakae mpenda na hamna mtu yeyote wa kunikataza ,na ukiendelea kunifatilia mwanangu oohoo sikufichi nitakuua hata kama nimekuzaa ,tena nitakuua kifo kibaya tofauti na cha baba yako nilimuua kwa sumu,.mama aliongea na kuingia chumbani kwae ,yale maneno ya mama yake yalimuuma sana,nakujikuta akilia ,
Abbas akimwangalia mdogo wake ambae bado mdogo ndio wanaishi katika maisha ya shida namna ile alizidi kuumia ,kilichomchanganya zaidi rafiki yake Aryan ambae alikuwa mstari wa mbele nae hali yake si nzuri bado yuko hospitali,
Mama yake Aryan alikuwa anaenda kumtembelea mwane hospitali kila siku huku Samairah nae alijitahidi kuhudhuria walimpelekea chakula ,na mahitaji mbali mbali, kutokana na upasuaji aliofanyiwa alibahatika kuokolewa maisha yake na alitumia mwezi mzima hadi akapona ndipo wakaruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani,
Mwalimu Farida alitumia gari yake kumrudisha Aryan nyumbani pamoja na mama yake ,
Siku hiyo wakati Aryan wanarejea nyumbani toka hospitalini ,” bibi aliwaza akiwa amebaki peke yake nyumbani,, mwanangu Ramso umenifanya hadi leo maisha yangu ya kutanga tanga namna hii umenitapeli nyumba yangu ukauza na kwenda kula raha .
Bibi alionekana siku hiyo amemkumbuka sana mwanae basi na alivyochoka kukaa nyumbani bibi alibidi atoke nyumbani na kutembea tembea kunyoosha miguu ,bibi alitoka zake na kutembea hadi barabara kuu ,bagamoyo road bibi alifika barabarani na kuona magari mengi yakipita ,bibi alijikuta anakumbuka maisha ya nyuma na kujisemea zamani nilikuwa naendesha gari langu binafsi leo hii nasimama barabarani naangalia magari ya watu ,mimi sina hata nyumba ya kukaa ndo natanga tanga hivi.
Bibi alijikuta anawaza wakati huo alikuwa anataka kuvuka bara bara upande wa pili,
Kelele za watu zilisikika zikisema “uwiii bibi anagogwa na gari sasa huyu bibi na uzee wake atavukaje barabara peke yake.?” Haikupita dakika moja baada ya bibi kufika kati kati ya barabara kuna gari ndogo aina ya V8 ili mgonga bibi na kumrushia mtaroni kisha gari hio ili hama bara bara na kujibamiza kwenye henga za bara barani.
Derava alijibamiza kwenye kioo cha mbele na kuning’inia huku uso wake hutamaniki na damu huku bibi amevunjwa kiuno na miguu yote,
Gari ambayo ilikuwa nyuma ya ile iliyomgonga bibi ,kumbe ndio gari ambayo Aryan alikuwemo.
Dereva alishika breki ,Aryan alifungua mlango na kushuka alivyomwangalia dereva wa ile gari ya mwanzo iliyopata ajali alimgundua kuwa ndio yule kijana siku ile alikuwa na mama yake Abbas na walikuwa wanaitana baby.
Mara bibi mtaroni alijaribu kutupa macho na kubaini nani kamgonga japo alikuwa kaumia mno damu zikimvuja kwa wingi alijikakamua na kutazama kwenye gari alimwona mwanae Ramso akiwa katokeza kichwa kwenye kioo ,bibi aliita “Ramsooo mwananguuu nini hiki umefanya” pale Aryan aligeuka na kutizama mtaroni akamwona bibi akiwa nyang’any’a hoi bini tahabani
Tulipo ishia jana baada ya ile ajali kutokea ,na aliyemgonga bibi ni mtoto wake kabisa wakumzaa ,na ndiye huyo huyo kijana alimpiga Abbas chupa ya kichwa huku akisema mama yake na Abbas ni mpenzi wake,
Bibi kwa kilio cha kwikwi alimwangalia mwanae ambae hajitambui kaning’inia kwenye dirisha aliita Ramso Ramso ,bibi alijaribu kuinuka na kujikuta akibaki pale pale ,bibi alikuwa kavunjwa miguu yote miwili kibaya zaidi kiuno nacho kilikuwa kimevunjika.
Aryan alipiga hatua za kwenda kumpa bibi msaada ile anapiga hatua kuelekea mtaroni Aryan alijikuta akisimama na kufumba macho ile gari iliyomgonga bibi ilikuwa imelala upande mmoja sasa tairi zilirudi nyuma na gari kwenda kitako na kwenda kutua mahali bibi alipo ,
Mpenzi msomaji na msikilizaji siwezi elezea kamwe mwonekano wa bibi jinsi ulivyokuwa ,bibi alikufa kifo kibaya,lile gari lilimkandamiza na kufanya bibi kichwa kipasuliwe na kifua kuwa kama chapati ,
Aryan alijikuta akilia kama mtoto , akiita bibi bibi
Mjukuu wako nimepona amka unione ,Aryan wakati akilia alikumbuka maneno ambayo bibie Samairah alishawahi kumwambia siku za nyuma
“Mogy usinione nipo kimya nakuonea huruma ipo siku utapoteza mtu ambae upo karibu nae sana” ,leo hii yametimia.
je Samairah aliyajuaje? Haya yote hayo yalikuwa mawazo ambayo yapo kichwani kwa Aryan.
Gari iliyopata ajali ilivutwa, watu walijaa na kusikitika jinsi vifo vya watu hao wawili vilivyotokea,tena mama na mwanae ,bibi alifanikiwa kutolewa na yule mwanae wote walikuwa wamepoteza maisha ,ni msiba uliomliza sana Aryan pamoja na mama yake maana ndiye alikuwa amejenga ukaribu nao mkubwa,Aryan alilia sana akiwa pamoja na bibie Samairah, msiba ulifanyika maeneo ya kunduchi hatimae waliwazika.Aryan alirudi nyumbani pamoja na Samairah akaenda kwao.
Tukija maeneo ya kawe beach tunawaona akina Mussa pamoja na Kudra wakiwa wanacheza mpira kwenye fukwe za bahari ,wakiwa sambamba na wadada watatu ambao muda wote walitembea pamoja si wengine ni Joyce,Nanaa na Lusi ,
Mussa alianza kuongea jamani sisi ni marafiki ambao tumejuana kwa muda mfupi,nimewaita tuje tufurahi wote hapa beach tucheze mpira tukichoka tunaingia baharini tuogelee
Nanaa alifurahi na kusema jamani mimi napenda kuogelea leo ndio mmenipatia ila na Aryan angekuwepo hapa beach pangenoga mno maana huyo mwanaume nampenda hadi sijielewi,ni maneno aliyoyaongea bibie Nanaa na kumfanya Joyce aachie mpira na kuanza kuwaza.
We Nanaa tena usithubutu kukaa karibu na Aryan maana nampenda hadi sijielewi ,yale yalikuwa mawazona aliyeyawaza ni bibie Joyce.
Kudra aliufuata mpira na kuuchukua huku nae akiwa na wazo lake rohoni ,nyie wazeni ujinga kwanza leo ndio mwisho wenu wa kuishi maana huyo Aryan hamtamuona tena ngoja muda wa kuingia kuogelea ufike ,wapuuzi nyie ,
Musaa alimsogelea Kudra na kumuuliza hivi Aryan yupo? Maana toka nilivyomchomaga kisu sijawahi kumwona yeye wala kale kademu Samairah , nahisi atakuwa amefariki maana kisu cha tumboni si cha kawaida.
Kudra alicheka na kusema aah kama ivyo poa wala usijali na hivi vijiwanawake vinajifanya vinampenda huyo boya leo tunawazamisha kwenye maji
Wakati akina Kudra wapo zao baharini wanaogelea ,
Tukija maeneo ya tegeta ,tunamwona mama yake Abbas akiwa anaingia nyumbani na kijana mdogo huku wameshikana viuno ,mara anamkiss ,
Walizama ndani ya nyumba ile wanafika sebuleni walijiachia kwenye sofa ,yule kijana alianza kumtomasa mama yake na Abbas huku akimpapasa mgongoni ,mara Abbas akaingia akiwa ameongozana na mdogo wake Gwae ,alichokiona Abbas alijikuta akidondosha machozi ,yaani mama yake mzazi alikuwa na kijana mdogo ambae huyo kijana anasoma darasa moja na wanajuana.
Abbas aliita Issa kwanini unanifanyia hivi? Isaa alicheka kwa dharau na kusema alafu wewe dogo jiangalie hebu ondokeni mie nifaidi vitu vya kikubwa, ki ukweli ilimuuma sana Abbas ,itawezekana vipi mama yake atembee na kijana mdogo tena anaumri sawa na wake,kibaya zaidi huyo Issa ndio kundi moja na akina Mussa wabaya wao wa maendeleo.
Abbas alijikuta analia na kutoka hapo nyumbani , aliondoka moja kwa moja hadi maeneo ya mbezi na kumkuta rafiki yake Aryan,alimwelezea kila kitu ambavyo mama yake anavifanya kwa sasa ,hata Aryan pia aliumia na kuwaza kwa kina.
Abbas sikia wewe ni muislamu yawezekana mama yako ana matatizo makubwa ama kuna jini mbaya ka mwingia ndio maana mama yako anafanya vitendo vibaya sasa sikia usijali wewe ni rafiki yangu nakuahidi tutasaidiana hatimae mama yako atakuwa sawa.
Inabidi tukamtafute ostadhi Othumani ili aje amsomee mama yako dua kama kuna mapepo ama majini yaweze kutoka ,Abbas alicheka na kusema sasa wewe umetoa wazo zuri tutaanzaje kumshawishi mama hadi akubali kukaa kitako na kusikiliza dua ya ostadh Othumani ,Aryan alimwangalia rafiki yake na kumwonea huruma ,kisha akamwambia usijali tutapata wazo lingine ila kwa sasa twende tukamwone huyo ostadh ,
Walitoka na kwenda kumtafuta ostadh ili waweze kumsaidia mama yake aondokane na huyo pepo mubaya,
Tukirudi maeneo ya baharini tunawaona akina Kudra na Mussa wakiwa wanacheza michezo mbali mbali kwenye fukwe za kawe ,wakiwa na lengo lao la kuwauwa akina Joyce Nanaa na Lusi wawazamishe kwenye maji hadi wapoteze maisha.
Hatimae Nanaa aliingia ndani ya bahari huku wakiogelea na aakina Mussa mara Joyce nae akajikuta ananogewa aliingia kwenye bahari na yeye kuendelea kuogelea ,Lusi nae hakupenda kupitwa aliingia kwenye maji huku wakiwa wanacheza michezo mbali mbali kama kukimbizana ,akina Joyce hawakuwa na mashaka hata kidogo na akina Mussa kama wanamawazo mabaya ya kuwaua.
Wao walicheza na kuonesha ukaribu kama marafiki wanao soma darasa moja, alianza Mussa akamshika mkono Joyce na kuanza kumvuta kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari, huku Kudra kawashika mikono Lusi na Nanaa ,na yeye alianza kuwavuta kuelekea kwenye kina kirefu, Mussa na Kudra walikonyezana kwa kubinyiana jicho.
Wakati huo kajua ndo kanaendea kuzama ufukwe ulikuwa kimya mno hapakuwa na watu ,Mussa alimgeukia Joyce na kumshika shingo kisha akamvuta na kumzamisha kwenye maji wakati huo Kudra nae kawazamisha akina Lusi na Nanaa.
Kudra alijisemea kimoyo moyo nyie wasalimieni kuzimu mnajifanya mnahamia shuleni kumbe nia yenu mapenzi yamewachanganya mnamtaka Aryan ,halafu mnakuja na kushika nafasi za juu kwenye masomo wapuuzi nyie.
Masikini wadada wawatu walianza kunywa maji taratibu huku wakijaribu kujiokoa lakini hawakufanikiwa , matumbo yalizidi kutanuka jinsi walivyokuwa wakinywa maji.
Hatimae waliishiwa nguvu za kujikomboa mikononi mwa wauwaji wale ,walianza kuona mwili ukikosa nguvu.
Gafla yalitokea mawimbi makubwa baharini yaliwazamisha hadi akina Mussa na Kudra nawao walifunikwa na mawimbi wakajikuta wanawaachia akina Joyce bahari ilianza kuwavuta na wao kuwapeleka kwenye kina kirefu zaidi kibaya zaidi Mussa pamoja na Kudra walikuwa si wazoefu wa kuogelea wakajikuta na wao wakianza kuyanywa maji ya bahari taratibu jinsi yalivyo na chumvi nyingi sasa mmh.
Bahari ilizidi kuwavuta na kuwapeleka zaidi kwenye kina kirefu wakati huo Joyce ,Nanaa na Lusi ndio walikuwa wamezama kabisa hata hawaonekani sijui ndo washakufa ama laaa.
Lakini pembeni mwa bahari kulikuwa na binti mrembo kasimama huku akishuhudia jinsi akina K.udra wakitapatapa
Tulipo ishia jana baaada ya mawimbi makubwa kutokea baharini na kuwazamisha akina Kudra kisha bahari ikaanza kuwavuta taratibu kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari wakati huo akina Joyce na wenzake ndio kabisa walikuwa hawaonekani.
Kudra alianza kutapa tapa na kujikuta akizidi kuzama ,ndipo likatokea wimbi kubwa na kuwasomba akina Mussa pamoja na akina Joyce walirushiwa pembezoni kabisa mwa bahari ambapo palikuwa na maji kidogo .
Mussa na Kudra wakiwa na matumbo makubwa baada ya kunywa maji mengi walipozamishwa na mawimbi ,walikuwa hawajitambui lakini mahali walikotupwa na maji kulikuwa na mrembo kasimama huku nywele zake ndefu hadi mgongoni akiwa amezitindua ,alikuwa kavalia gauni jekundu na refu ,alikuwa ni bibie Samairah aliwaza mambo mengi moyoni mwake ” hivi ninyi akina Mussa ni nini hasa mnataka ,kwanini mnataka kuwaua wenzenu tena pasina hatia ,Samairah alitikisa kichwa kisha akamfuata Joyce ambae alionekana kupoteza fahamu kabisa alimgusa maeneo ya puani na kugundua kuwa bado anapumua ,aliinama na kumpuliza mdomoni huku kaziba pua za Joyce ,pale pale Joyce alikohoa na kuanza kutapika maji ,huku akipiga piga kifua chake ,hatimae Samairah alimfanyia Nanaa na Lusi kisha waliweza kuzinduka.
Joyce na wenzake walishangaa kumwona Samairah maeneo haya ,Joyce aliuliza huku akifuatiwa na kikohozi ” Samairah umekuja peke yako ama upo na Aryan” lile swali lilimfanya Samairah atabasamu kisha akawashika mikono wote watatu na kuwaambia naombeni mnifuate maana sasa hivi naona mshapata ahueni.
Samairah aliwatupia jicho Mussa na Kudra kisha akatikisa kichwa na kuwaambia akina Joyce twendeni tuondoke na hawa wapuuzi waacheni hivi hivi ,
Akina Joyce walianza kumfuata Samairah,ndipo Nanaa aliuliza ,Samairah kwani nawe ulikuwa hapa baharini? Maana kwa kumbukumbu zangu mara ya mwisho niliona Kudra amenikaba shingo kwa nguvu na kunizamisha kwenye maji, ndipo nilianza kunywa maji na hatimae sikujua nini kiliendele,
Samairah aliwaangalia na kuwaambia ,kuanzia leo iwe mwanzo na mwisho wa kutembea na akina Kudra si watu wema hata kidogo maana hawa akina Kudra walinifuatilia mimi na kunishawishi kuja beach nao niliwagomea,
Nilivyogoma Mussa alimnong’oneza Kudra na kumwambia huyu Samairah tumwache kwanza tuanze na akina Joy tukahakikishe wanafia baharini ,
Maneno ya Samairah yaliwafanya akina Joyce wapate picha kamili jinsi walivyozamishwa kwenye maji ,akina Joy walimkumbatia Samairah na kumshukuru kisha wakamuahidi kuanzia leo sisi tutakuwa marafiki zako ila mwanzoni tulikuwa tunakuchukia kwa sababu upo karibu na Aryan
Samairah aliwaambia sawa ila kuweni makini,walifika maeneo ya kawe na hatimae kila mmoja alichukua usafiri na kwenda makwao .
Mida ya saa mbili usiku ndipo akina Mussa walipiga chafya na kuzinduka ,kila mmoja alivyoangalia tumbo lake ,walishangaa kuwa na matumbo yamejaa maji ,
Kudra alikuwa wakwanza kurudisha kumbukumbu alimwambia ,oya Mussa mpaka sasa tuko fresh Aryan tushamuua na akina Joyce naimani washafia ndani ya maji ,Mussa alidakia na kusema kesho zamu ya kumtafuta Samaira nae tutapanga mbinu ya kumnasa
Walijipongeza na kuondoka baharini baada ya kuzunguka ,lakini Kudra alikumbuka kitu,
Oya Mussa hivi wakati tumewazamisha akina Joyce baada ya wimbi kubwa kutokea ,tulizamishwa na maji chini lakini tulivyoibuka niliona kama mwanamke kasimama pembezoni mwa bahari na akiwa kanyoosha mkono mahali tulipo
,Mussa alicheka na kumwambia wewe acha zako labda ulikuwa ndotoni twenzetu tukachukue bajaji tuondoke
Waliondoka zao .
Tukirudi maeneo ya tegeta tunawona Aryan na Abbas wakigonga geti kwenye nyumba flani hatimae walifunguliwa ,walimsalimia yule mkaka aliyewafungulia geti kisha Aryan akauliza braza ivi tumemkuta ostadh Othumani ? Yule kijana aliitikia yupo tena kakalia kibarazani anasoma Qur’an ,Aryan alisema ooh afadhali waliingia na kumsalimu ostadh
“Assalaam alaykum ,”(ikiwa na maana amani iwe juu yako) Aryan alisalimu kisha Othumani aliitikia ,”waalaykum salaam Warahmatullah Wabarakatuh”(amani , rehma na baraka ziwe nanyi pia) karibuni mashekhe. walikaribishwa kwenye jamvi kisha akina Abbas walikaa na kukunja miguu “hiyo style ya kukunja miguu huitwa tahiyatu,”
Othumani aliwaangalia akina Aryan kwa makini na kugundua huenda wanamatatizo labda wamegombana maana Abbas alikuwa kakunja sura mno ,yote akifikiria mambo anayofanya mama yake.
“Ehe karibuni shekhe “Othumani aliwaambia ndipo Aryan akakohoa kidogo kuweka sauti yake vizuri na kuanza kuongea, ostadh tumekuja kukuona wewe tunashida tena si shida imekuwa tatizo na kumsababishia rafiki yangu kuwa na mawazo ,ehee shida ipi hio Othumani aliuliza huku akizinyoosha ndevu zake.
” ostadh mama yake na Abbas nadhani hata habari zake hapa mtaani umezipata siku hizi anafanya vitu vya ajabu anatembea na waume za watu ,na watoto wadogo kiukweli ostadh inatia aibu haswaa, tulikuwa tunaomba ukatusaidie walau kumsomea dua ,maana kadri siku zinavyozidi kusonga ndipo anazidi kubadilika tunakuomba sana.
Ostadh wala hakuwa na maneno mengi aliuliza kwani sasa hivi yuko wapi”? Abbas aliinua kichwa na kumjibu kuwa yupo nyumbani , ostadh aliinuka na kuvaa kubaz zake kisha wakaanza safari ya kuelekea kwa akina Abbas
,wakiwa njiani kuna gari aina ya kirikuu lilipita huku likitangaza kuwa kuna kongamano kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya tegeta nyuki atakuwepo mchungaji Petro atawaombea wakazi wote wa tegeta pamoja na viunga vyake ,wenye mapepo ,majini ,wagumba mikosi na nuski zote wataombewa na kupokea neno la mungu.
Ni maneno waliyoyasiki kwenye gari likitangaza na kutaja siku ya juma pili,Abbas aliwaza ostadh akishidwa kumponyesha mama na dua zake itabidi nitumie mbinu nimpeleke mama kwa huyo mchungaji Petro huenda angeweza kuyatoa hayo majini.
Haikua mbali walifika nyumbani walimkuta mama yake na Abbas yuko na mwanaume mwingine tofauti na Issa ,tena walikuwa wamekaa sebuleni wakipapasana ,Abbas kitendo cha kuingia ndani na kuwakuta mama yake akiwa katika pozi la kimapenzi aliumia sana na kutoka nje ya nyumba ,maana kulikuwa na mwarobaini mkubwa Abbas alienda zake kukaa nje ili kutoa aibu, ile anafika kwenye mwarobaini alisikia sauti ya mdogo wake Gwae akilia.
Abbas aliinua kichwa juu alihisi kuchanganyikiwa baada ya kumkuta mdogo wake kafugwa miguu juu kichwa chini kaning’inizwa kama mtu anae uza mkungu wa ndizi,Gwae alilia lakini hakupata msaada wakati huo mama yake ndio akibadilisha wanaume ,
Hakika kile kitendo kilikuwa kinauma mno ,Abbas ilibidi achukue ngazi na kumfungulia kamba mdogo wake kisha akamuuliza , Gwae nani kakufunga juu ya mti ” mama kasema nifugwe na yule mbaba aliyekuja nae ndio kanifunga.
Abbas alimwangalia mdogo wake ambae mikono yote imevunjika halafu bado anateswa aah Abbas alizidi kuwaza mama katoa wapi hiyo roho ya kinyama,
Ostadh alikaribishwa ndani na Aryan kisha akamwambia ostadh aanze na kisomo , kitendo cha mama yake na Abbas kumwona ostadh alitabasamu na kumwambia subiri ni malize na huyu kisha zamu yako itafuata ,Othumani alimsogelea mama yake na Abbas na kumwambia ,mama nimekuja hapa kwa lengo moja la kukutoa katika mateso ya jini mbaya jini mahaba tuweze kukusomea dua hilo pepo litoke na urudi katika hali yako.
Maneno ya ostadh ndio kama yalimvuruga mama Abbas aliinama chini ya kochi na kutoa chupa ya bia alinyanyua ili ampige ostadh lakini Aryan aliwahi akaudaka mkono wa mama yake na Abbas yule mwanaume ambae alikuwa yupo na mama Abbas
Alinyanyua shati lake upande wa ubavu wa kulia kisha akatoa bastola na kumnyoshea ostadh,we ndo unajifanya unasomea watu dua ili kuwatoa majini ee ,sasa sikia huyu ni mpenzi wangu ,nakupa dakika mbili uwe ushapotea la sivyo nitasambaratisha kichwa.
Ostadh hakuwa na neno hata moja aliinuka kisha akatoka nje taratibu na kuvaa kubaz zake huyo kuelekea kwake ,sasa walibaki Abbas ,Aryan na Gwae ,pamoja na mama yao.
Yule mwanaume ambae alikuwa kajazia kwa mazoezi aliwaambia akina Abbas watoke nje kisha wao wafanye mambo yao wakimaliza watawaita waiingie ndani.
Abbas na mdogo wake walitoka na kukaa nje ,lakini chumbani kwa mama Abbas alianza kuzungumza na yule mwanaume,
JOSHUA ,sikia huyu mwanangu siku hizi kajiona kakua sitaki kumuua kwa kumpa sumu kwakuwa hizi kazi wewe unaiweza naomba uwanyonge pamoja na Gwae wafe tu maana naona kama wananikera kera tu hapa nyumbani nataka nibaki peke yangu nikitaka kufanya jambo lolote na fanya ,
Kwanza najuta kwanini nilizaa hizi taka taka , ,Joshua kwa sauti yake nzito alisema sawa hio kazi mbona dakika siruri tu ngoja niwafuate hata nje niwatwage risasi halafu nikimbie.
Wakati mama Abbas anapanga na Joshua Aryan alikuwa kasimama karibu na dirisha alisikia kila kitu ambacho mama yao anataka kuwaua ,Aryan kwa mwendo wa haraka aliwaendea akina Abbas na kuwaambia
“Abbas nakuomba hapa hatuna muda wa kukaa mama yako si mama tena nimemsikia kwa masikio yangu akimwambia yule mwanaume aje awaue naomba tukimbie ,Abbas nae alishaanza kuwa na hofu na mama yake alivyoambiwa hivyo alikimbia pamoja na Gwae .
Gwae kwakuwa amevunjika mikono yake miwili na alikuwa bado hajapona vizuri alikimbia kidogo alibanwa na vichomi na kushidwa kukimbia kabisa na kujikuta anasimama na kuinama huku akiugulia maumivu wakati huo Aryan ashakimbia na kuondoka zake ,
Abbas alivyoona mdogo wake kashidwa kukimbia alimrudia ili amshike mkono amsaidie kukimbia .
Ile anageuka tu alishangaa anadakwa mkono na Joshua ,”Joshua alikuwa kashika upanga huku akihema juu juu ” , Joshua aliongea kwa ubabe ” we dogo unaweza kushindana na mimi ? Sasa unaona hili panga nakufyeka”,wakati huo Gwae kadondoka chini kwenye kauchochoro flani cha pale mtaani kwao ilimbidi kutembea na magoti ili ajibane vizur kwenye gogo la mti ili Joshua asiweze kumuona na anusuru maisha yake “wakati huo
Ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku palikuwa na giza giza huku taa za nyumba za majirani zilikuwa zimeangaza ,
Gwae akianza kujiburuza ili ajifiche kwenye sehemu ambayo hataweza kuonwa ,wakati anasogeza goti la mguu wa kushoto huku akigeuka kumwangalia Joshua kumbe maeneo hayo kulikuwa na nyoka,Gwae akajikuta anamgusa mkia wa nyoka tena alimkandamiza na goti ,kawaida ukimgusa nyoka kwenye mkia huwa anakuwa mwepesi kurusha kichwa ili kubaini mbaya wake ama kuuma chochote kile
Sasa , masikini Gwae aliudondokea ule mkono ambao ulikuwa umevunjika na bado hujapona kisha akalala chali.
Yule nyoka alirusha kichwa na kutua shingoni mwa Gwae ,huku Gwae anajitahidi kutokutoa sauti ili Joshua asimkamate …..
__________________
Baada ya Abbas kukamatwa na Joshua na Fwae kudondoka chini ,kisha nyoka alitua kichwa chake shingoni mwa Gwae.., na Gwae alijikuta akinyanyua mikono yake iliyofugwa mhogo ama gamba gumu (p.o.p) yule nyoka aliliuma hilo ganga kisha akaruka na kuondoka zake ,.Gwae alijikuta kama kagandishwa na theluji,
Wakati huo Abbas kashikiliwa shati na Joshua “we mtoto inaonekana unamfuatilia mama yako sana na ndio kanipa pesa nikuue ,ila najua hii ni dunia” ,Joshua aligeuka nyuma na kumwona mama yake na Abbas akija kushuhudia jinsi mwanae anavyouliwa ,kumbe Joshua hakupenda kitendo cha mama yake na Abbas kutaka kuwaua wanae.
“Joshua alimnong’oneza Abbas ,sitakuua ila nikinyanyua upanga kisha nitakupiga na ubapa halafu udondoke chini kisha mimi nitakubeba na kwenda kukutupa ,Abbas baada ya kuambiwa vile alianza kutetemeka maana Joshua mwenyewe anatisha kwanza uso wake unangeu za kila aina huku mikono yake ikiwa imekomaa mno.
Mama yake na abbas aliita Joshua fanya kama nilivyokuambia hatuna muda wa kupoteza ,Joshua alinyanyua upanga kisha aliugeuza ubapa kisha alimpiga Abbas maeneo ya begani kisha akamshika maeneo ya shingo na kubonyeza mshipa wa fahamu,pale pale Abbas alidondoka chini na kupoteza fahamu
Joshua alitoa kichupa kidogo ambacho kilikuwa na damu ,ila haikuwa damu ya binadamu bali ilikuwa damu ya mnyama
Alimpaka Abbas maeneo ya shingoni na kumwagia damu kwenye shati kisha ,akawekea na upanga wake damu.
Kisha alianza kumfuata mama yake na Abbas alimwonesha upanga,mama Abbas alivyoona damu akajua kazi tayari imeisha ,alifurahi na kusema mwanangu nenda salama huko uendako afadhali mimi nimepata uhuru sasa
Haya Joshua shika kiroba hichi kamfungie humu kisha ukamtupe huko hata baharin samaki wale ama ile mindege ya baharini ,kisha mama Abbas akarudi na kuondoka zake,
Joshua alianza kuwaza ” ukweli dunia imeisha japo mimi naishi mjini kwa kazi hizi za kutumwa kuua watu ,kukaba na kuwafanyia watu vitendo vya kinyama ila leo siwezi wafanyia hawa watoto yawezekana huyu mama kuna mtu kamloga ama amekubwa na jini mahaba ,sasa kwanini anataka kuwaua watoto wake ,daah.
Joshua alijiwazia na kuingiza upanga wake ndani ya suruali kisha alimchukua Abbas na kumfunga kwenye roba ,mama Abbas aliagiza gari ikaja na Abbas akapakiwa kwenye buti kisha safari ya kuelekea kutupwa baharini kuanza.
Wakati huo Aryan alirudi na kumkuta Gwae kalala chini alimshika mkono na kumwambia tukimbie ,lakini Aryan alivyopiga jicho aliona Abbas akipakiwa nae bila kuchelewa alikodi piki piki na kuanza kulifuatilia hilo gari ,Aryan alitaka ajue ni wapi rafiki yake anaenda kutupwa ,wakati huo Aryan alikuwa akidondosha machozi na kujua kuwa rafiki yake tayari ashauliwa.
Na Gwae baada ya kuachwa na tayari ilikuwa ni usiku aliogopa kwenda nyumbani maana alijua huenda akauliwa alibaki amekaa nje huku baridi kali likimpiga ,
Gwae aliwaza aende kwa rafiki yake Rashidi lakini alivyokumbuka jinsi mama Ashura alivyo mvunjaga mkono basi aliamua akae nje tu usiku kucha ,
Kibaya zaidi mikono yake yote imevunjika na bado haijaanza kuimarika ,
Tukija maeneo ya mbezi ya afrikana lile gari lililompakia Abbas lilikata kona na kuingia kwenye barabara ya vumbi kisha walifika mahali kulikuwa na miti mikubwa halafu katikati ya hiyo miti palikuwa na nyumba ,haikuwa hata na geti ,Abbas alishushwa na kutolewa lile roba alilofugwa nalo ,kisha dereva aliwasha gari na kuondoka wakati huo Aryan nae alikuwa maeneo hayo alitaka apate uthibitisho ili hata akienda polisi aweze kuwapa maelezo kamili,
,
Joshua alimshitua Abbad maeneo ya shingoni na ndipo pale alizinduka na kujikuta yupo katika mazingira mapya kabisa ,Abbad akiwa haelewi aliuliza “wewe ni nani na hapa niko wapi ” Joshua alimwangalia Abbas kisha akafungua mlango na kuingia ndani
Kisha akamwita Abbas nae aingie ndani ,
Abbas alikubali na kuingia ndani kisha alipewa kiti kidogo na kukaa.
Joshua alitoa upanga wake na kuutupia chumbani mwake kisha akavua shati na kuwasha mshumaa ,Abbas alijikuta akitoa macho makubwa baada ya kuona kovu kubwa mgongoni mwa Joshua ,na Abbas kuwaza huyu atakuwa jambazi nini
Wakati Abbas yupo ndani Aryan nae alikuwa kwa nje ya hiyo nyumba alivyochungulia kwenye upenyo mdogo wa dirisha alishangaa kuona Abbas yupo salama ,Aryan alijikuta akishusha pumzi na kusema inamana pale yule mtu alivyoinua panga alimkata au alifanyaje ,Aryan aliwaza kwa haraka na kusema yawezekana huyu mtu alimchukua Abbas si mtu mbaya wacha nigonge mlango nipate kujua
Wakati huo Abbas kakaa huku wameangaliana na Joshua kwa nje walisikia mlango ukigongwa ,Joshua aliinuka na kuufungua mlango,na kumkuta Aryan kasimama nje ,kabla Joshua hajaongea chochote Aryan aliwahi kujitambulisha na kusema
Mimi ni ndugu yake na Abbas huku akilia ,Joshua hakuwa na kipingamizi alimwambia aingie kisha awasimulie kwa nini ameamua kufanya hivyo.
Aryan nae alikaa chini kisha Joshua alianza kueleza ,” mimi kwa jina nafahamika kama buda ,hili jina nililipewa na watu hasa kwa kazi zangu za kuua watu ,nimepewa kazi na mama yake Abbas kanipa laki tano hiii hapa ,Joshua alizimwaga pesa chini kisha akaendelea kuongea ,katika maisha yetu ama familia yetu ,baba yetu ni tajiri mkubwa sana tu hapa mjini anaitwa Kizza ,
Akina Abbas na Aryan walivyosikia Joshua kasema yeye ni mtoto wa Kizza walishituka maana na wao wana mwanafunzi mwenzao wanaosoma nae anaitwa Kudra Kizza ,ambae muda wote huwa anajitapa kuwa ni mtoto wa kitajiri.
Joshua aliendelea kusimulia, mimi wa wapili kuzaliwa ,wakwanza ni kaka yangu alikuwa mkandarasi ila kwa sasa kawa kilema tena kilema cha kudumu hata baba yangu hamtaki kumwona machoni mwake ,”Joshua baada ya kutaja kaka yake mkandarasi ” Aryan alikumbuka yule mkandarasi aliyedondokewa na gorofa,na kujua huenda ndio kaka yake na Joshua ,
Joshua aliendelea kueleza mdogo wetu wa mwisho anaitwa Kudra ila kanasoma sasa ivi,baada ya Joshua kutaja ivo Aryan alijua fika hapa muda wowote anaweza kuuliwa maana anajua fika Kudra huwa anamchukia ,
Joshua aliendelea, katika familia yetu tushapewaga laana kubwa sana watoto wote wa Kizza watakuwa na roho mbaya kupita maelezo ,ndio maana mimi nilijikuta naingia kwenye kazi ya kuua binadamu ,natumwa na watu kamuue fulani ,nami naenda naua.
Ila kwa huyu kijana sijui shetani gani kanipitia roho yangu imekataa kata kata kukuua hivyo tambua mama yako si mtu mwema chukua hizi pesa alizonipa nikuue ,kapange chumba uanzishe maisha yako , na uhakikishe mdogo wako unamtumza mama yako si mtu mwema kuanzia hivi sasa.
Joshua alimpa Abbas pesa zote alizopewa na mama yake ili amuue ,lakini akina Aryan walivyokuwa ndani kwa Joshua walikuwa wakisikia kaharufu kama cha mzoga ama kitu kilichojifia na kuanza kutoa harufu,
Joshua aliwaangalia na kuwaambia hii nyumba yangu nakaaga mwenyewe hapa na nimeiwekea zindiko hamna mtu yeyote anaeweza kuiona lakini nimeshangaa wewe kijana umeionaje?
Joshua alimuuliza Aryan “Aryan alifikiria na kusema mbona inaonekanika tu ,Joshua aliguna na kusema we dogo usinidanganye hii nyumba hamna mtu yeyote anae weza kuiona labda jini na wachawi Lakini binadamu wakawaida hawezi kuona ila dogo sitaki kukuhoji sana ipo siku tutakutana naomba muondoke”.
Abbas alitangulia kusimama kisha akatoka lakini Aryan alivyosimama alitupa macho kwenye chumba kimoja ambacho mlango wake ulikuwa wazi alishangaa kuona mwili wa mtu ukiwa umevimba tumbo halafu kinywa kipo wazi
Aryan alijua fika kuwa Joshua akiua watu anakuja kuwaweka katika hii nyumba maana kasema hamna mtu anaeweza kuiona,Aryan nae alitoka walitembea haraka haraka na kutoka eneo ambalo Joshua anakaa.
Abbas hebu simama vua hilo shati vaa sweta langu ,Aryan alimwambia Abbas nae alifanya hivyo maana shati lake lilikuwa limepakwa damu kisha walianza safari ya kurudi tegeta kwa ajili ya kumtafuta Gwae tayari ilikuwa ishatimia saa saba usiku
Waliweza kufika maeneo ya tegeta walipitia mahali ambako palikuwa nyumba ya akina Aryan walikuwa wakinyata kwa umakini.
Maana Aryan wakati anamfuatilia Abbas alimwambia Gwae asiende kulala kwenye nyumba ya mtu yeyote akiona wanachelewa aende akalale kwenye hilo gofu la akina Aryan
Sehemu Ya 4
Aryan walivyofika pale walishangaa kusikia sauti za vifijo huku sauti ya mama Ashura ikisikika kwa sana walisogea taratibu na kuchungulia Aryan na Abbas wakajikuta wanafumba midomo yao kwa mshangao.
Walikuta wachawi wakicheza kwenye uwanja wa kwa mama Ashura,huku mama Ashura akiwemo na yeye, walikuwa wamejifunga rubega kaniki na vitambaa vyekundu kichwani lakini kwa chini kulikuwa na mtoto kalala na walikuwa wakiimba na kumzunguka huyo mtoto.
Aryan aliangalia vizuru waliweza kuona ni kitoto kichanga kilimwagiwa unga unga kisha mama Ashura alisema nyofoa hicho kitovu unipe nile
Mama mmoja alikashika katoto na kuvuta kitovu puuu, halafu mama mwingine alimpa mama Ashura na kusema kata haka katoto shingo
………………,…………………
Tulipo ishia jana ,, Walikuta wachawi wakicheza kwenye uwanja wa kwa mama ashura,huku mama Ashura akiwemo na yeye, walikuwa wamejifunga rubega kaniki na vitambaa vyekundu kichwani lakini kwa chini kulikuwa na mtoto kalala na walikuwa wakiimba na kuzunguka huyo mtoto.
Aryan aliangalia vizuri waliweza kuona ni kitoto kichanga kilimwagiwa unga unga kisha mama ashura alisema nyofoa hicho kitovu unipe nile
Mama mmoja alikashika katoto na kuvuta kitovu puuu, halafu mama mwingine alimpa mama Ashura na kusema kata haka katoto shingo ,
Mama mmoja alishika kale katoto kisha akakanyonga shingo ,na kumpatia mama Ashura,yote hayo walikuwa wakiyafanya huku Aryan na Abbas wakishuhudia
Baada ya kunyonga kale katoto ,wale wachawi walimwaga maunga unga yao kisha walipotea ,
“Aryan hivi ndio nimeona wachawi ama naota ,?” Abbas alimuuliza Aryan,na kumfanya Aryan amzibe mdomo na kumwomba atulie maana alijua kuwa yale mazingira si salama walizama kwenye nyumba ya akina Aryan ambayo ilichomwaga moto na akina Kudra , walimkuta Gwae kalala kajikunyata masikini, hakika alikuwa anatia huruma alikuwa kalala usingizi mzito mara anarusha rusha miguu mara mikono ,yote hayo alifanya baada ya mbu wengi kumshambulia.
“Gwae mdogo wangu amka tuondoke”,Abbas alimwamsha lakini kitendo cha kumshika mkono alitaka kupiga yowe ila Abbas aliwahi na kumziba mdomo ,
Walimuamsha kisha wakatoka ili waanze safari ya kuelekea mbezi kwa akina Aryan.
Lakini walipiga hatua tatu walisikia kilio nyumba ya tatu ,Aryan aliwaomba akina Abbas wasimame ili waweze kujua nini kimetokea mbona watu wengi ,vilio vilizidi kuongezeka na kufanya watu wa majumba ya jirani waamke na kwenda kuangalia kuna nini mbona watu wanapiga mayowe usiku tena usiku wa manane.
Akina Aryan walisogea eneo hilo ,walivyoangalia vizuri walibaini kuwa kuna msiba umetokea ,mama bonge alifika na kuuliza nini shida? Ndipo mama mwingine alijibu “mama bonge si una habari kuwa mchana waleo Zuhura alijifungua mtoto? Mama bonge alijibu ndio nilisikia hizo habari mama Ashura ameniambia.
Yule mama alimwambia mama bonge kuwa Zuhura mtoto wake amefariki dunia muda si mrefu ,tena Zuhura wawatu alijifungua mtoto mzuri na mwenye afya ,unaambiwa mtaa mzima hamna mtu aliyemuona mtoto huyo kasoro mama Ashura, mchana alikuja wakati Zuhura anapelekwa hospitali kujifungua na alivyojifungua mama Ashura alimpokea mtoto na kucheka kicheko ambacho kiliwafanya manesi washangae.
Pale pale Aryan aligundua kumbe wale wachawi walivyowaona pale wanamnyonga mtoto kumbe ni mtoto wa Zuhura ,Aryan alijikuta akitikisa kichwa na kulaani sana wachawi kwa mambo yao ya kuua watoto wa watu.
Akina Aryan walifanikiwa kuondoka eneo lile na kwenda hadi mbezi mahali wanapokaa kwa sasa waligonga geti na kufunguliwa waliingia ndani ,kisha walilala.
Tukija maeneo ya sinza tunamwona bibie Jesca kaamuka asubuhi na kuingia bafuni kuswaki lakini siku hiyo mawazo yake yalikuwa yametawaliwa na Aryan ,alimuwaza sana Aryan maana anampenda kuliko maelezo ila Aryan hadi sasa hajawahi kuonesha wazi kama nae anampenda ,,Jesca alianza kuwaza mambo ambayo alishawahi kumfanyia mama yake na Aryan alivyokuwa akifanya kazi za ndani kwao ,hasa kumpiga vibao ,kumfulia nguo za ndani,
Jesca alijikuta akipiga piga kichwa chake ngumi na kujikuta analia ,alinawa uso na kuswaki alitoka safari yake moja kwa moja hadi kwa akina Samairah ,bahati nzuri alimkuta Samairah yupo nje ,
“Ooh vipi hali shoga angu” Jesca alisalimu huku akimkumbatia Samairah ,safi za kunisusa , Samairah alichombeza.
Mmmh nani akususe si unajua sasa hivi tumefunga shule hivyo kuonana inakuwa nadra ,ila Samairah mimi na shida ya kitu kimoja ,ehe shida gani Jesca? Samairah aliuliza
“Jesca alikaa kimya kwa muda kisha akaanza kueleza ,”ujue Samaira mimi sikujuaga yule mama ambae anakaa nyumbani ni mama yake na Aryan na tayari nishamfanyiaga vitendo vya ajabu mama wa watu ,alikuwa akishinda ndani akilia yote sababu yangu, muda mwinginge nilikuwa nikikuta kapakua chakula anataka kula mimi nachukua maji machafu namwagia chakula chake ,mama wawatu alishindaa njaa huku nilimdekisha nyumba mara tano kwa siku,,
Huyo mama nilishawahi kumpiga mara kibao kumuunguza moto,je nitafanyaje ili anisamehe na mimi nampenda Aryan kupita maelezo na sitaki nimkose Aryan, nisaidie please”, Jesca alihitimisha na kumfanya Samairah awaze
Mimi mwenyewe Aryan nampenda ila nahofia kumwambia kuwa mimi nina asili ya kijini halafu wewe unataka nikupe ushauri mmmmh mbona mtihani ,siku zote Samairah ni mtu anaependa binadamu waishi kwa amani alimuahidi kuwa atampelekea kesho kwa Aryan ili akaombe msamaha kwa mama yake.
Jesca alifurahi kusikia hivyo kisha waliingia ndani kwa akina Samairah na kwenda kuendelea na story zingine;
Tukija maeneo ya tegeta tunawaona tena Abbas na Aryan wanaingia kwa ostadh Othumani ili wakamwombe msamaha kwa kilichotokea jana ili kama kuna njia nyingine ya kumsomea dua mama yake na Abbas apate kupona maana walihisi atakuwa katupiwa jini ,tena jini mbaya, walifika na kumkuta Othumani akifyeka majani kwenye nyumba yake walimsalimia kisha wakamwomba wakae pembeni wazungumze kidogo,
Othumani aliitika wito kisha wakatoka nje ya nyumba na kuanza kuzungumza.
Ostadh nadhani jana ulijionea jinsi huyo mama sasa hivi alivyo tunaomba msaada wako kwa mara nyingine tupate kumnusuru ,aliongea Abbas na kumfanya Othumani awaze kwa kina kisha aliwaambia hilo usijali leo nitahakikisha namaliza kila kitu ,ila kwa sasa twendeni msikitini tukatafute vijana wenye nguvu ili wakamkatate mama yenu kisha wamfunge kamba ndipo tutasoma dua kwa pamoja naimani kwa uwezo wake Allah (Mwenyezi Mungu) atapona Othumani aliongea
Hawakuwa mbali na eneo la msikiti walitembea kidogo hatimae walifika walikuta watu wapo msikitini maana walikuwa wanashiriki katika kujenga msikiti ,ostadh aliomba vijana watano nao waliitikia wito na hatimae walienda hadi kwa mama yake na Abbas.
Kwanza walifika na kukuta akichoma nguo za wanae Abbas na Gwae huku akiongea maneno ambayo yaliwafanya Abbas na Aryan wabaki midomo wazi ,”mama alianza kuongea ,wanangu nimewazaa mwenyewe japo baba yenu nilimuua ,lakini nilimuua kwa maana alikuwa akininyima uhuru sikuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo ,nanyi nimeshiriki kuwauwa ila najua hata tukija kukutana huko mliko tangulia mtaniuliza maswali mengi ambayo sitakuwa na majibu yake .
Wakati anarusha begi lenye nguo za Gwae kwenye moto aligeuka na kumkuta mwanae akiwa na ostadh Othumani ,mama alishituka na kunyoosha mkono na kusema wewe Abbas umefufuka ama umefanyaje ,mama aliinuka kwa mshangao na kuanza kukimbia lakini vijana waliwahi na kumkamata walimfunga kamba kwenye mikono na miguu kisha walichukua mkeka wakatandika na kukaa “tahiyatu” kwa ajili ya kumsomea kisomo ama dua kama kuna jini mbaya aweze kutoka,
Ostadhi aliita pamoja na mashehe watatu akiwemo na yeye walimkalisha kati kati kisha wakamzunguka na kuanza kusoma dua , Othumani alianza kusoma dua ya kutoa majini na kujikinga na majini wabaya inaitwa “AYAT KURUSIY ” waliwasha ubani mzuri uitwae ubani maka ,huu ubani waweza utumia hata nyumbani huwa unakinga na kufukuza majini wabaya ,huu ubani maalum si kana kwamba upo sawa na ubani zingine lahasha! mpenzi msomaji na msikilizaji huu ubani ukiuwasha huwa watoa majini wabaya upesi na nia njema ama kutibu husaidia endapo utatia nia na dua ambayo wataka kufanya basi dua yako lazima ifanikiwe
Basi ostadh aliwasha ule ubani
Alianza kusoma
” Allahu lailaha illa huwaalihayuu liqayumu,
Lataaqudhusinatu walaa nauumu,
Lahumafii samawati wamaafil-ardhwi,
Maandhaladhii yashifaghuu ghindahu illa miidhin,
Yaghlamu maabaina aidihimu wamaa khalfahum,
Walaayuhituna bishayiini min ghilmihi illa bimashaa a Wasigha kurusiyu samawati wal-ardhwi,
Walaa yauduhu ihdhuhuma wahuwa lighaliyu lighadhiimu.
Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila yeye, Na ndiye mwenye uhai wa maisha,
Msimamizi wa kila jambo,
Kusinzia hakumshiki wala kulala,
Ni vyake vya peke yake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini,”
“Na nani huyo awezae kuombea mbele ya Mwenyezi Mungu bila ya idhini yake?”
Ayajuwa yaliyo mbele yao viumbe na yaliyo nyuma yao,
Wala hao viumbe hawalijuwi lolote katika yaliyo kwenye Ilimu (elimu)yake,
Ila kwa alipendalo Mwenyezi Mungu,
Enzi yake imeenea mbinguni na ardhini,
Wala kuvilinda hivyo hakumshindi ni yeye peke yake ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu.”
**** aalisoma dua hiyo ndefu huku wamemshikilia mama Abbas wamewasha na udi ,gafla mama Abbas alianza kubadilika miguu yake na kuwa kama si ya binadamu ,miguu ilibadilika na kuwa mabaka mabaka kama nyoka aina ya chatu.
Dua hiyo wakati wanasoma nyumbani kwa mama Ashura alianza kuhisi maumivu makali kwenye kichwa chake mara tumbo linamuuma mno ,mama Ashura alianza kuhaha huku akizidi kukabiliwa na kichwa alihisi kinataka kupasuka.
Huku Othumani anazidi kuisoma dua ,kule mama Ashura anazidi kupata maumivu makali ,wakati mama yake na Abbas miguu ilianza kubadilika na kuwa kama chatu ina mabaka mabaka meusi na ya njano iliyopauka,
Mama Ashura alijikuta akitoka kwake mbio na kuanza kukimbia huku akishika kichwa chake na kusema kinauma jamani kichwa kinataka kupasuka
Mama Ashura alizidi kupiga makelele huku akikimbia peku peku alichana dera lake alilolivaa na kulifanya kama mpasuko flani na kuanza kukimbia ovyo huku akisema kichwa chamuuma
Watu walijua mama Ashura kawehuka ama kawa kichaa maana alikua akikibamiza kichwa chake kwenye mashina ya miti ama ukuta alizidi kukimbia watu nao walianza kumkimbiza safari yake ilienda moja kwa moja hadi kwake na mama Abbas alifika pale na kudondoka huku akipigiza kichwa chake chini paaa paaa na kusema sirudiii tena sirudiii tena.
Mama Ashura alianza kugara gara ,huku mama Abbas nae akigara gara na kusema tumbo na kichwa chamuuma ndipo ostadh alizidi kupiga kisomo cha dua
Mama Ashura alipaza na kusema mimi niacheni niacheni mimi, nimemtupia jini mahaba sasa kwanini mnataka kuniua?
Mama Ashura alizidi kuhaha
Huku mama yake na Abbas povu zito likizidi kutoka mdomoni na huku akishikilia tumbo lake na kusema utumbo unataka kunyofoka.
Tulipo ishia jana baada mama Ashura kuzidi kupiga kelele na kujibamiza kichwa chake chini na kusema yeye ndiye alimtupia mama Abbas jini mahaba huku mama Abbas povu zito lilizidi kutoka mdomoni na kushikilia tumbo na kusema anahisi utumbo unataka kunyofoka ,…..
“Mashekhe walizidi kupiga kisomo kizito na kuzidi kuwafukuza hao majini wabaya aliorushiwa ,mama Abbas miguu yake ilichukua muda hadi ikarudi katika hali yake yote hayo yalikuwa yakiendelea Abbas na Aryan walishuhudia kwa macho yao na kuzidi kushanga “
Kisomo kiliendelea ndipo mama Ashura akaanza kuporomosha maneno ,” mama Abbas nilitokea kukuchukia pasina sababu ,yote sababu nilimpenda mume wako na mume wako akanikataa mimi ,nilitumia kila njia lakini mume wako alikuwa ni mtu wa dini haswaa ,masaa yote alikuwa wakusoma masihafu ,nilivyoona nimegonga mwamba kumpata ndipo niliamua kukutumia jini ambaye alikuendesha hadi ukamuua mume wako kwa kumkorogea sumu , si wewe uliyehusika bali ni jini niliyemtuma kwako ndio alikuendesha hadi ukafanya hivyo “aliongea huku akilia na kujutia alichomfanyia mama Abbas
“Msiniuee jamani msiniuee
Ostadh alizidi kusoma dua ya kuvunja na kutoa kabisa majini wabaya kwa mama Abbas pamoja na kwa mama Ashura baada ya lisaa limoja wote wawili walikuwa kimyaaa ,hamna hata anaeongea ilibaki tu wakihema kwa kasi.
Ostadh alitoa chupa yenye mafuta ghadhwimu na kuwawekea kwenye nyuso zao huku akisoma na dua kisha alimwambia
Shehe Abbas tumemaliza kazi na sasa mama yako yuko salama
Ila kesho nitarudi kwa ajili ya kumsomea dua nyingine kwa ajili ya kinga zaidi na hata huyu rafiki yake mama Ashura najua mwashangaa kumwona hapa ,huyu kavutwa na dua ambazo tunafanya na ndiye alikuwa mshirikina alizidi kumtupia majini mama yako ili awasambaratishe ninyi ,yote anafanya hivyo kwasababu ya uzinzi alimtamani baba yako ,kibaya zaidi alikutana na baba yako kajikinga ndio kahamia kwa mama yako.
Ila kuanzia sasa mama Ashura tumewatoa majini wake wa kishirikina kuanzia sasa ni mtu mwema kabisa na hatakuwa na uwezo wa kumdhuru mtu.
Abbas alivyogeuka kumwangalia Aryan hakumwona wakati dua inasomwa hata Aryan nae alijisikia kizungu zungu ila alijikaza na kuondoka eneo hilo na kwenda kukaa mbali ndipo alisikia nafuu tambua hata Aryan kuna nguvu flani za bangili zilimwingiaga machoni hivyo mbeleni tutapata kujua zaidi.
Ostadh alimpa Abbas maji ya dua na kumwambia haya utaweza kummiminia mama yako kichwani pamoja na mama Ashura ,ostadhi na mashekhe wengine waliondoka na kumwacha Abbas pale aliendelea kumngojea mama yake hadi aamuke ,kweli ilipita nusu saa mama yake na Abbas aliamka na kukuta kafunguliwa kamba.
Alimwangalia mwanae huku akionekana kama vile kapungua uzito zaidi ya kilo tano,Abbas alimsogelea mama yake na kumuuliza mama uko salama? Mama akiwa haelewi kitu chochote alimwangalia mwanae na kumuuliza Abbas “kwani kitu gani kimetokea mbona sielewi ?”
Abbas alimwinua mama yake na kwenda nae hadi sebuleni ,mezani kulikuwa na chupa za bia nyingi huku glasi moja ilikuwa imejazwa bia ,mama alifika sebuleni na kuuliza mwanangu hizi chupa za bia za nani ? “nani anakunywa pombe ? Kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakipiga ?” Mama Abbas aliendelea kumuuliza mwanae maswali yaliyomfanya Abbas ashangae,Abbas hizi bia za nani ,mama aliendelea kumuuliza mwanae huku akionekana kushangaa sana zile chupa za bia pale mezani.
Ukweli zile bia zilikuwa ni zake lakini alivyosomewa dua na wale majini wabaya wameondoka hivyo pombe ameichukia kupita maelezo , Abbas alianza kuwaza “Ina maana mama yangu kapona? Hadi anauliza hizi bia za nani au atakuwa kapona” ,Abbas alimwambia hizi bia si zilikuwa zako unakunywa pamoja na hizi sigara?
Mama aliwaza kisha akatikisa kichwa na kusema mwanangu muogope Mungu wewe ujue utakuja kuchomwa moto ee lini mimi nimekunywa bia? Mimi sijawahi kunywa bia wala kuvuta sigara hivyo naingia chumbani nisizikute hizo bia hapo
Mama aliongea na kuingia chumbani ,hadi Abbas alishangaa kweli mama yake kapona ,alifurahi mno ,kisha alizikusanya zile bia na kutoka nazo nje moja kwa moja kulikuwa na kigrosary pale nje alimpa mhudumu na kumwambia hizi bia kama utauza sawa kama utakunywa sawa mama kasema hazitaki ,Abbas alimwambia yule mhudumu.
Yule mhudumu alimwangalia Abbas na kumwambia ole wako uniletee kesi hapa za mama yako kama umemwibia pombe zake mi sipo nachukua na naziuza maana nashida na pesa mie ,wakati huo Abbas ashaanza kuondoka ,alimwambia muhudumu we uza pesa ukipata ni za kwako ,
Wakati Abbas anafika nyumbani anamkuta Aryan nae karudi Aryan aliuliza vip mama kafanikiwa kupona ? Kabla Abbas hajamjibu aliinuka na kumkumbatia Aryan na kumwambia hadi sasa mama kanambia hata hajawahi kunywa bia wala bia hataki kuziona.
Ile wanaingia ndani walimkuta mama sebuleni katoa nguo za kiume kila aina ,kisha akamuuliza Abbas
Mwanangu umekuja narafiki yako Aryan,oooh
Aryan habari yako ? Mzima? Na mama yako hajambo?
Aryan kwanza alichelewa kujibu maana haamini kama kweli ile salamu imetoka kwa mama yake na Abbas ambae alikuwa anamchukia aliitikia kisha Mama akauliza Abbas hizi nguo za mume wangu marehemu ama za nani ? “Aryan aliangalia zile nguo na kuzibaini ni za wale wanaume ambao alikuwa anawaingiza nyumbani leo hii hakumbuki ni za nani.
Huko nje mama Ashura nae kazinduka na kujinyoosha aliuliza jamani hapa nipo wapi? ,ndipo mama Abbas alitoka nje na kumwangalia ,alimwona akipangusa mafuta ambayo yalikuwa utosini mwake ,
Mama Abbas aliita wewe si mama Ashura ama
nimekufananisha ,mama Ashura alijiangalia kisha nae akauliza ndio mimi ni mama Ashura ,
Alikumbuka kitu kisha akapiga magoti na kuanza kulia ,mama Abbas nisamehe ni ibilis alinipitia nikakurushia majini nisamehe shetani jamani shetani hiiihihihiii
Mama Abbas alimfuata na kumkumbatia kisha akamwambia yaliyopita yamepita kikubwa tumrudie muumba wetu ,na ijumaa nitakupitia mapema tupate kwenda kuswali ,.mama Ashura nae aliapa kwa mambo anayoyafanya kuanzia leo naachana nayo, ukweli mama Abbas alibadilika na kusahau vibwanga vyake vyote vya baa ,ndipo waliagana baada ya kuongea maongezi marefu.
Mama Ashura aliondoka na kwenda nyumbani alifika kwenye chumba chake ambacho anawekaga tunguli zake alikuta zikiwa zinafuka tu moshi alizitia kwenye kiroba na kwenda nyuma ya nyumba alizifukia na kwenda kwenye begi lake alitoa kitabu kimoja cha Qur’an na kuanza kukifungua ,ndipo alipokumbuka alikuwaga ni ostadhati mzuri aliongoza chuo cha kiislamu cha pale msikiti wa kati na alikuwa akiwafundisha madrasa wabint wadogo,yote aliyarudia akasema kuanzia leo nakuwa mama Ashura wazamani asante Mungu sitaki tena uchawi wala ushirikina nakurudia kukuabudu ewe muumba wangu.
Alifungua kabati lake alichukua mtandio na kujitanda usoni kufunika nywele zake ,hakika mama Ashura alipendezea ushungi ;
Tukirudi katika upande wa pili mama Abbas alimuuliza mwanae Gwae wangu yuko wapi, Abbas wala hakuwa na haja kumficha alimweleza yupo kwa akina Aryan mbezi mahali walikohamiaga nyumba mpya.
Pale ndipo mama Abbas alianza kukumbuka matukio aliyoyafanya nyuma kutembea na wanaume zaidi ya watano kwa siku kukesha baa ,kuwatesa watoto ,aliondoka kimya kimya na kuingia chumbani mwake ,
Akina Abbas na Aryan nao waliondoka kuelekea mbezi kumchukua Gwae nakumlete nyumbani lakini ile wanafika tegeta nyuki walimwona Samairah akishuka kwenye daladala akiwa na Gwae ,ilibidi wasimame kwanza.
Samairah aliwaona na kuwaita Aryan mambo nimewamiss mjue ,alitembea haraka haraka akiwa kamshika Gwae mkono hatimae alifika mahali waliko akina Aryan
Alimwangalia Aryan na kumuuliza vip mmemaliza dua?
Aryan aliguna ilibidi aulize swali kwa Samairah dua? Dua gani hio Samairah ,
“Samairah akacheka na kusema naelewa mbona, Samairah alikuwa na uwezo wa ajabu vitu wanavyofanya akina Abbas na Aryan vyote alikuwa anavitambua “okay tuachane nayo lakini mama yake Abbas si karudi katika hali yake?
Maswali ya Samairah yalifanya Aryan aanze kurudi nyuma taratibu ,huku moyoni akiwaza Samairah kajuaje kama tumeenda kwenye dua ,na nani kamwambia kama walienda kwa mama yake na Abbas ,pale Aryan alipata wasi wasi maana hawakumwambia mtu yeyote zaidi yao sasa ugumu unakuja Samairah kajuaje haya yote.
Samairah alimwangalia Aryan na kumwona ana wasi wasi mkubwa nae alitabasamu na kusema najua bana ila ondoa shaka
Twendeni nyumbani kwa mama Abbas leo nikamwone ,
Mara Hwae alidakia na kuita aunt ulivyokuwa nyumbani ujue niliona miguu yako kama ina kwato kama zile za kwenye movie tunazozionaga za farasi ama pundamili…..
Kabla Gwae hajaendelea kuongea jambo jingine Samairah aliwahi na kumfunika mdomo ,kisha akawaza kwa undani ina maana huyu mtoto aliniona ?
Kisha akamwangalia Aryan na kuendelea kuwaza kimoyo moyo, we Aryan nakupenda ila uwe unaniambia kama unaenda kufanya dua maana ipo siku utaja sababisha nigundulike kwa watu.
Aryan alizidi kumwangalia Samairah na kuishiwa nguvu lakini Samairah alinyosha mkono wake ili amshike Aryan bega lakini kunakitu ambacho Aryan alikiona, alikodoa macho kwa mshangao huku akihisi mwili wake kukosa nguvu
Alijikuta taratibu anafumba macho na kutaka kukimbia…
Tulipoishia jana baada Samairah kupeleka mkono ili amshike bega Aryan ili waondoke ,kuna kitu ambacho Aryan alikiona na kujikuta akifumba macho na kukosa kipi afanye kwa wakati ule ,
Aryan kwa mara nyingine aliitoa mikono yake taratibu na kuanza kuangalia huku akijiuliza ,ni kweli ni yeye? Sauti ya mtu ambae akimkokota baba mmoja kakaa katika baiskeli za walemavu ,
Jamani msaada ,msaaada jamani yule mkokotaji ndio alikua akiongea ndipo Aryan alivyotupa jicho alikutana na yule mkandarasi ambae alitaka kumtoa kafara ,wakati akifanya kazi ya ujenzi moja ya gorofa lilikopo mbezi ,
Leo hii Aryan anamshuhudia yule mkandarasi kwanza alikuwa amekonda huku nguo zake kuonekana chafu na zimefubaa mno ,,mkandarasi à likuwa hana mikono wala miguu yote ilikuwa imekatwa ,ndipo Aryan alirudisha kumbu kumbu zake na kukumbuka jinsi lile gorofa lilivyo mdondokeaga huyu mkandarasi na yeye alikumbuka jinsi alivyomrushia kwenye nyaya za umeme ili apigwe shoti afe ili mkandarasi aweze kupata tenda nyingi katika kazi zake za ukandarasi,
Leo hii kawa omba omba yote hayo yalikuwa mawazo ambayo akiyawaza Aryan
“We Aryan unashangaa nini?” Samairah aliuliza ,”unashangaa kilema huyu?” Mogy alitikisa kichwa kuashiria ndio anamshangaa ,Samairah alicheka na kusema huyu baba namjua vizuri alikuwa mkandarasi halafu niwaambie kitu ,Aryan na Abbas
Aliwashika mikono na kuwa nong’oneza huyu ni kaka yake na Kudra ,usimwone kachakaa hivi baba yake tajiri ,Samairah aliongea na kumfanya Aryan na Kudra wakumbuke hata Joshua aliwaambia kuwa ana kaka yao ni mkandarasi lakini kwa sasa ni kilema ,leo hii wakaambiwa mkandarasi ndio kaka yake na Kudra.
Gwae alimwambia Samairah ,aunt mpe huyu baba msaada si unaona hana mikono eee ,Samairah alitabasamu na kumwambia Gwae asante nawe usije lipiza ubaya kwa wabaya wako waliokutendea ubaya ,Samairah aliingiza mkono kwenye pochi alitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumuwekea kwenye kikombe huyo makandarasi.
Ile Samairah anampa mkandarasi hela ndipo mkandarasi nae aliinua kichwa chake na kumwona Aryan ,alitaka kuruka kwenye kibaiskeli ila hakuwa na uwezo maana hakuwa na mikono ,Aryan alimwambia yule anae mkokota mkandarasi wasogee pembeni aweze kujua nini hatima yake ,mkandarasi japo alikuwa anamwogopa Aryan akijua huenda anaweza kumpiga ama kumjeruhi hasa akivuta kumbu kumbu jinsi alivyotaka kumpigisha shoti ya umeme hadi afe ,mkandarasi alijikuta akichanganyikiwa kisawa
Sawa ,kwakuwa hana mikono na miguu hakuwa na namna tu.
Aryan alimvuta mkandarasi hadi pembeni kisha akachuchumaa na kumwangalia mkandarasi machoni,mkandarasi alikosa cha kufanya na kujikuta machozi yakimbubujika ,kibaya zaidi hana mikono huenda angeyapangusa yale machozi yanayo mtoka wakati akilia na kujutia alichokuwa anakifanya nyuma angali mzima,
“Siku zote Aryan ni mtu wa kutangaza amani na anapenda kuishi na watu vyema, alimwonea huruma kisha alitoa kitambaa chake kipya alikuwa kisha akamfuta mkandarasi machozi huku akiongea maneno mazito
“Najua unahofu na mimi labda wahofia nitakupiga ama kukuua hapana mimi siko hivyo hata kidogo ,ila nakupa pole kwa wakati huu mgumu unaoupitia ,hebu kumbuka ulikuwa na kitambi kipindi wajenga magorofa yako leo hii umekuwa kimbau mbau ,umekondeana wakati wewe bado kijana ila waonekana mzee ,
Wakati huo maneno Aryan anaongea ,mkandarasi alizidi kuangua kilio kisawa sawa na kufanya watu wakusanyike ili kujua huyo kilema anatatizo gani ,pale pale nyuma ya stendi ya tegeta nyuki.
Aryan aliendelea ,natamani ningekuwa na uwezo nikuwekee viungo vyako utembee ujionee mengi ,hii dunia ni duara kila siku tunaambia ,uliwaua wavuja jasho kwenye gorofa yote sababu ya kutaka utajiri na kupata tenda nyingi za ujenzi ,sitaki kujua toka umeanza ujenzi wako umeua wafanya kazi wangapi ,hilo unalijua mwenyewe na roho yako , ila tambua roho ya mwanadamu huwa inakisasi ,ukiua mtu na ukagusa damu yake lazima nawe yatakukuta kama yalivyowakuta wao,
Ndipo pale mkandarasi alianza kuongea ,”nimejifunza leo na kesho natamani miguu yangu na mikono ingekuwepo nitembee niuambie ulimwengu kuwa roho ya binadamu mwenzie ni mbaya mtu asije kuthubutu kumuua mwanadamu ili apate mali nimejifunza” mkandarasi aliongea huku akitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa.
Alimwangalia kijana Aryan kisha akamwambia ,usiniambie sana nimejifunza ,kila nilalapo roho za wafuu ,watu niliowatoa kafara zinanitesa usiku kwenye njozi ,mateso ninayopata siwezi simulia ni mabaya mno ,
Wafu wananinyonga usiku,muda mwingine hadi nakufa kabisa lakini wananirudishia pumzi yangu na kunifanya niendelee kuishi ,
Najiwa na viumbe waajabu mimi ,nachomwa kisu naona kabisa mchana kweupe naugulia machungu masaa matatu lakini machungu yanaisha na kujikuta nipo kama awalii lakini siwezi jilaumu katika familia yetu tumepewa laana mbaya hadi kufa kwetu hivyo wacha niendelee na safari yangu atakae nisaidia anisaidie kama hamna nae aniache.
Sukuma baiskeli twende ,”mkandarasi alimwambia kijana ambae anamsaidia kusukuma hiyo baiskeli waondoke zao ,Aryan alitingisha kichwa kisha akataka kuondoka lakini aliangalia.
Lakini katika ile baiskeli kuna chuma kilikuwa kimekaa karibu na mdomo ili akiwekewa hata chakula ale lakini Aryan aliona kuna unga na hakuweza kuutambua ule unga ni wa nini.
Mkandarasi alimwangalia Aryan kisha akamwambia sogea ni kuambie Aryan alisogeza macho karibu na lile chuma ambalo lina unga ,mkandarasi aliwaza haraka haraka.
Wewe mpumbavu ndio ulinusurika kufa na kunifanya mimi niwe kilema nimezunguka hii dar nzima nikikutafuta nawe nikusababishie ulemavu wa kudumu kama mimi ,
Mimi sasa hivi si mtu wakuishi najua nitakufa kwa madhabi yangu niliyofanya na nitaendelea kufanya hadi kufa kwangu
Aliwaza na wewe kuanzia leo utakuwa kilema kama mimi.
Wakati Aryan hajui chochote anachowaza mkandarasi alimwambia asogeze uso aweze kumwomba msamaha ,Aryan nae alifanya vile alivyoambiwa na mkandarasi
Ki ukweli mkandarasi japo ni kilema hana miguu yote wala mikono lakini bado alikuwa gaidi mno ,
Alichokifanya alimpulizia Aryan ule unga ambao ulikuwa wa bluu na kuonesha kama kuna vimadini vidogo vidogo vikimeremeta , ule unga uliingia machoni mwa Aryan ,kisha mkandarasi alitabasamu na kujiwazia kuanzia leo utakuwa kipofu ,
Kisha yule kijana ambae alikuwa anasukuma kile kibaiskeli alimsukumizia Aryan kile kikombe ambacho watu walikuwa wakitoa msaada wa pesa
Halafu mkandarasi alisema mwiziii jamani mwizi ananiibia mimi japo nikilema ,watu walikuja upesi wakati huo Aryan anahisi macho yake yanawasha kwa uchungu mno alianza kuyapikicha kwa nguvu huku machozi yakimtoka ,watu walianza kumpiga Aryan na nondo,mbao,kuni hakika Aryan huruma yake ilimponza leo hii kageuziwa kibao kuwa ni mwizi,
Alizidi kupewa kipigo haswaa
Aryan alianza kutaka kujitetea wakati huo mkandarasi ndio anasukumwa na kuzidi kutoweka,
Machoni kawekewa sumu ambayo inaenda kuua kiini cha jicho na inafanya kazi dakika moja ,wakati Aryan akiendelea kupigwa kwa nguvu watu wanamrushia mawe na kusema mwizi ,Aryan macho yake yalikuwa hayaoni hata kidogo,
Alijaribu kuita akina Samairah na Abbas lakini walikuwa tayari washatangulia nyumbani kwa mama Abbas,Aryan akiwa hoi mwili mzima umetapakaa damu
Mara kuna gari ilikuja na kupaki pembeni walishuka watu upesi na kusema mwacheni mwacheni msimuue sisi tunaenda kumshughulikia,
Kwa kuwa Aryan alikuwa haoni alijua labda polisi wamekuja kutoa msaada lakini alivyosikia mu-bebeni huyu bwege pakieni kwenye gari tumpeleke masikani kwa kazi ya kumzika akiwa hai.
Ile sauti Aryan aliielewa ni ya Kudra ,mara Mussa alimtandika teke la kwenye taya ,Aryan akajikuta taya la juu na yachini zinapishana
Mussa alisema leo tumekunasa wewe nyumbu ,wakati huo Aryan kapigwa kipigo cha mwizi na vile vile mkandarasi kampa upofu ,sasa yupo mikononi mwa wabaya wake na wanasema wanaenda kumzika mzima mzima.
Hana msaada tena akina mudy na Samairah washatangulia nyumbani
Tulipoishia jana baada yaAryan,kupigwa teke na Mussa kisha wakajipongeza ama kufurahia kumpata Aryan “,we boya afadhali leo tumekunasa kwanza “,waliwaambia raia wasimpige wao wataenda kumshughulikia ,gari ilisogezwa vizuri Aryan alipakiwa kwenye buti ya gari tena kama mzoga vile ,Aryan akiwa anavuja damu, akawa anaita Samaira ,Abbas,mama njooni mniokoe nipo katika mikono ya watu wabaya ,Aryan ndani ya buti ya gari aliendelea kulia na kuichukia huruma yake maana ndio iliyomponza ,alimwonea huruma sana mkandarasi kukosa mikono na miguu ,lakini kumbe mkandarasi bado anakisasi nae leo hii amemtia upofu ,
Ule unga ulikuwa ni sumu mbaya sana uliingia machoni mwa Aryan dakika chache tu alikuwa haoni , akiwa ndani ya buti ya gari aliomba dua za kila aina ,huku akisikia jinsi tairi za gari zikizunguka kwa kasi aligundua yawezekana gari ipo mwendo sana ,alitulia maana hata nguvu za kujitetea wala hakuwa nazo tena ,kipigo alichopigwa kilikuwa cha aina yake,
Huku ndani ya gari Mussa na Kudra pamoja na Issa nae alikuwepo walizidi kujipongeza kumnasa Aryan na wakisema leo ndio mwisho wake ,,walimpeleka hadi maeneo ya bweni ,na kumshusha kwenye nyumba moja ambayo ilionekanika ni ya kifahari
Walimrusha chini kama gunia , hawakujali kama anaweza kuumia au laa ,wao walimrusha chini , walimsogeza hadi kwenye kivuli kwa kumburuza kama gogo ,Aryan alijikuta ngozi yake ikichubuka ,
Kudra alimsogelea machoni na kumwangalia hakika alizidi kucheka kwa nguvu ,baada ya kuona macho ya Aryan yanaanza kumeguka meguka mboni ,vijinyama nyama vinatoka ,
“Khaaa Mussa njoo mcheki huyu zobozo macho yake yanavyoharibika vibaya kumbe kawekewa ile sumu ambayo nilikuambia siku tukimpata tumwekee maana ile inatengeneza upofu kwa haraka.
Kudra aliongea na Mussa kuuliza sasa ni nani ka mwekea hio sumu? ,
Ki ukweli wakati mkandarasi anamuwekea sumu Aryan na kuondoka walipishana na akina Kudra wala hawakuonana ,hivyo hawakujua kama kaka yake na Kudra ndio kafanya lile tukio
Kudra aliagiza tena ile sumu apewe na Issa alimletea upesi na kuweka tena machoni mwa macho ya Aryan,macho ndipo yalizidi kuharibika kumeguka vijinyama ,huku Aryan akilia kwa uchungu ,
Katika nyumba ile ambayo yupo Aryan alikuwepo mama yake na Aryan ambae nae alikuwa katekwa na Jesca na aliingizwa ndani
” we mama nimekuambia unisamehe yale makosa yote niliyokufanyia kwetu na umwambie mwanao Aryan anipende mimi kama mimi ninavyompenda ,unanisikia?” Masikini mama wawatu alifugwa kamba huku akipigwa na kuambiwa atoe msamaha na amwambie mwanae ampende Jesca ,mama alizidi kuchezea kichapo ,lakini kauli yake ilikuwa ni ile ile ” Jesca upendo si wa kulazimisha ila wewe ni mbaya toka rohoni siwezi kukusamehe pia mwanangu hawezi kukupenda mwanaharamu kama wewe ,” nipigeni mniue ila mwanangu naomba mwacheni asome kiasi anachotaka yeye mama alisema “
Ndipo Kudra aliingia na kumfungulia mama yake na Aryan kisha akamwambia Jesca yule bwege tumemkamata yupo pale nje sijui aliiba maana tulikuta anapigwa na watu ndipo tukamchukua ,Jesca alivyosikia Aryan yupo nje aliachia kisu ambacho alikuwa anamtishia mama yake na Aryan kumchoma tumboni ,alifanikiwa kutoka nje na kumwona Aryan ,mwili wake ukiwa umetapakaa damu
Jesca aliwangalia alivyomchunguza macho ndipo alibaini kuwa Aryan haoni tena ,Jesca aliumia maana alikuwa anampenda mno lakini alivyoona macho yanavyozidi kuharibika alisema Aryan basi tena kwa uzuri wangu siwezi kumpenda kipofu inabidi uzikwe tu ukiwa mzima nisiendelee kukuona tu kwenye hii dunia ,
Mama yake na Aryan alitolewa nje nakufanikiwa kumwona mwanae akiwa katapakaa damu mwili mzima alivyochungulia macho ya mwanae ndipo alizidisha kilio na kuita Aryan ,Aryan mwanangu ,hapo ndipo Aryan aliisikia sauti ya mama yake alinyoosha mkono ili amshike mama yake mkono wake kwa mara ya mwisho ,mama alinyoosha mikono yake na kumshika mwanae akiwa analia kwa uchungu akiwaangalia akina Mussa na Kudra walikuwa hawana hata shida walikuwa wanacheka.
Jesca nae aliumia sana alisimama na kumwambia Mussa na Kudra mmefanya nini sasa kumharibu Aryan macho ,ni bora tungemtesa mama yake yeye akabaki tu ,ila isiwe kesi naomba mmfukie akiwa hai nisiweze kumwona katika maisha yangu ,
Kudra aliita vijana wake wakiwa wanaongozwa na Issa kwanza walimshika mama yake na Aryan walimvuta na kumshika mikono,Aryan alibebwa juu juu na kuzungushwa nyuma ya nyumba palikuwa na shimo ambalo tayari lishaandaliwa Aryan alirushiwa na kwenda kujibamiza kama gogo puu, tambua haoni na mwili wake umepigwa mno.
Kudra aliwaagiza kundi lake wamfukie Aryan akiwa hai walianza kurusha udongo bila shaka huku mama yake na Aryan akishuhudia mwanae akizikwa akiwa hai ,hakika ilikuwa inauma mno alilia mama wawatu hadi sauti ikakauka ,,kwa nje walisikia geti likigogwa na Mussa alikimbia na kwenda kufungua wakati huo Aryan udongo unaendelea kurushwa ile Mussa anafungua geti alishikwa shati na binti wa kike kisha akazama nae ndani huku kijana mwingine akaingia na kufunga hilo geti ,
Mussa jinsi alivyoshikwa alijaribu kujinasua lakini yule binti alikuwa kamshikilia kwa nguvu sana ,Mussa aliita Samairah na wewe pia umejileta ,
Kumbe walikuwa akina Abbas na Samairah hatimae wameingia ndani kutoa msaada kwa Aryan ,Kudra alivyomuona Samairah nae alikuwa anampendaga aliwaamuru vijana wake waache kumfukia Aryan waje wamkamate Samairah ili ambake mchana kweupe pee ,vijana waliacha na kumshika Samairah ki ukweli siku hio Samaira alikuwa watofauti alikuwa akishika mtu mkono ama shati hawezi kumtoa mkono wake.
Samairah akiwa amemkaba Mussa hatimae mama yake na Aryan aliweza kuona ile bangili ambayo yeye alishawai kumpa Samairah kipindi anaondoka kwa akina Jesca ,leo hii mama anaiona ile bangili ikiwa ipo mkononi kwa Samairah ,wakati huo Abbas amekimbia na kwenda kumwinua mama yake na Aryan chini.
Mama vip upo salama? Abbas aliuliza huku akimwinua wakati huo Samairah bado kamshikilia shati Mussa . ,Mussa kila akijaribu kujinasua kwa Samairah alishidwa na kujikuta shati lake likichanika tu, Kudra alichukua kisu na kuanza kumfata Samairah kwa lengo la kumchoma ama kumjeruhi lakini ile anapiga hatua Samaira alimwangalia Kudra maeneo ya tumboni ,pale pale Kudra hata hakusogea hatua nyingi alihisi tumbo linauma tena maumivu yasiyo eleweka japo yeye huwa anajiona mbabe ila kwa maumivu ya tumbo aliyoyapata akajikuta ananywea chini na kushikilia tumbo lake huku akiita watu waje wamsaidie ,jamaan tumbooo ,oooh tumbo ,ni malalamiko aliyoyatoa Kudra na kujikuta akigara gara chini ,kama mtoto
Samairah alimwachia Mussa ,Mussa nae alijikuta anakuwa mpole yaani kama vile mtu punguani asie na akili timamu ,Mussa akawa wakuitika itika ovyo huku akimwogopa sana Samairah.
Samairah alianza kupiga hatua kuelekea kwenye lile shimo ambalo Aryan alianza kufukiwa ,wakati akipiga hatua na mkononi kavaa ile bangili ,ile miale ya lile bangili ilianza kuonekanika machoni mwa Aryan , macho yalikuwa yameharibika na kuurojeka hapakuwa na mboni tena zaidi ya utepe utepe mweusi ,ule unga ulikuwa ni sumu mbaya yaani ukiguswa na maji halafu ukaweka kwenye ngozi,basi ngozi yako itaanza kukatika katika ovyo.
Ndipo macho ya Aryan yalivyoorojeka na kumfanya Aryan kupitia maumivu makali mno na kukata tamaa kabisa ya maisha nakujiona safari yake ya kifo imekaribia ,lakini kadri Samairah anavyosogea kwenye lile shimo ndipo macho ya Aryan yanaanza kurudi kama mwanzo.
Aryan alianza kuona rangi za bluu na kijana kwenye mboni zake,zile rangi ndio zipo kwenye ile bangili aliyoivaa Samairah,,,,,
Mpenzi msikilizaji naomba nikurudishe nyuma kwenye vipande vilivyopita ,tunakumbuka siku mama yake Samaira alivyoishikaga ile bangili ilipogusana na pete ambayo alikuwa ameivaa ndipo kuna mwanga ulitoka wa blue ukiambatana na wa kijani uliingiaga mwachoni mwa Aryan na kumfanya akapoteza fahamu.
Leo hii Aryan anaanza kuona ile miale ,ndipo Samairah alivyofika kwenye lile shimo alimwona Aryan akiwa kajaa udongo , Aryan alifumbua macho yake na kujikuta anaona vizuri sana ,Samairah alinyoosha mkono ishara ya kumsaidia ,ili amtoe kwenye shimo ,Aryan nae aliinua mkono wake taratibu alianza kuvutwa kwenye shimo na bibie Samairah ,
Ki ukweli hapo Aryan hakuamini kabisa macho yake kama yanaona tena ,Aryan alizidi kumwangalia Samairah usoni ambapo Samairah muda wote alikuwa akitabasamu tu ,pale ndipo Aryan aligundua Samairah ni mrembo sana
Samairah alimwangalia Aryan ambae mwili wake ulikuwa na damu ,”Samairah alianza kuwaza ,naweza kuyafuta hayo majeraha na Aryan akabaki kama alivyo awali ila nahofia Aryan ataniogopa na atanitenga nami sitaki kitu hicho kitokee hivyo hakuyafuta majereha ya Aryan.
Aryan alitoka kwenye shimo na kujikuta akimkumbatia Samairah kwa nguvu ishara ya shukrani kwa msaada wake ,ndipo Aryan alivyogeuza macho alimwona mama yake akija mbio huku akisema mwanangu uko salama?
Aryan alivyoangalia alimwona pia Abbas nae alikuwa anakuja ,Aryan alimwachia Samairah kisha akamkumbatia mama yake ,
Mama alimwangalia mwanae machoni na kumuuliza “eti kwa sasa unaona? Ndio naona mama, Aryan alijibu ,mama alishangaa maana alivyoona macho ya Aryan yalivyoharibika alishangaa mno leo hii anaona vizuri tu.
.
Mara Jesca nae alikuja na kumkumbatia Aryan ,huku akionekana mapepe mno ,”Aryan wangu mzima haaa nilijua ushakuwa kipofu ,alimkumbatia kumwambia Aryan nakupenda hata mama yako ameridhia niwe nawe na si huyu Samairah kwanza wanawake weupe wabaya kitu maji ya kunde nakuambia utaona utamu wake ,achana na weupe wa Samairah mimi nakupenda Aryan ,
Hakika maneno ya Jesca yalimfanya mama yake na Aryan agune na kuwaza moyoni mwake utalazimishaje mtu akupende ,mama alitikisa kichwa na kusemea nakuchukia sana Jesca ila mungu anisamehe kwa kukuchukia ulitoa amri mwanangu azikwe angali mzima kwakuwa alikuwa kipofu ili usimwone tena sasa imekuweje?
Aryan nae alianza kuwaza,Jesca ulitoa wazo nifukiwe kwenye kaburi nikiwa mzima maana nishakuwa kipofu nimetoka na naona sasa wasema wanipenda Aryan aliguna kidogo mmmh.
Pale bibie Jesca anaupeleka mdomo wake ili wagusanishe lipsi zao na Aryan,mtoto kaweka lipstick kwenye lipsi zake na alivyo nalipsi nyembamba za kuvutia alihitaji apate denda kwa Aryan.
Lakini Samairah hakutaka kushuhudia kile kitendo alifumba macho ,pale pale Aryan alimsukuma Jesca na kumwambia we Jesca achana na mimi.
Ndipo Aryan alipo angalia vizuri alimwona Kudra kainuka chini ,alikuwa akiinuka kwa tabu na mkononi alikuwa kashika bastola
Alijikaza na kuwanyooshea akina Aryan ,Samairah mama Aryan pamoja na Abbas,,
Kudra akiwa hoi tumbo lilizidi kumkata kwa maumivu nae alijikakamua kwa ubishi aliwanyooshea bastola hasa hasa Aryan aliweka kidole kwenye sehemu ya kubinya ili risasi itoke amtandike Aryan hakutaka tena kumwona akiwa hai,
Aryan aliwahi na kumkinga mama yake ili kama kufa afe yeye mama abaki.
Lakini mama Aryan nae alisema mwanangu acha mimi aniue wewe ubaki wakawa wanagombania nani apigwe risasi mwingine abaki ,
Kudra aling’ata meno kwa uchungu ama maumivu ya tumbo anayoyapata na kuifyatua risasi,,
Wakati huo mama Aryan kamkumbatia mwane asife ,ili risasi impige yeye na tayari risasi ishaachiwa na Kudra kafyatua ile risasi ,na kusema safari njema kuzimu halali yako.
Lakini tayari mama Aryan alikuwa kumkinga mwanae ili asipigwe risasi sasa akawa amemgeuzia mgongo Kudra na tayari akafyatua risasi.
Aryan akajikuta anafumba macho na kusema mama hapaaanaaaaaaa!!!!!!!!
Tulipo ishia jana ,wakati mama na mwanae wanagombania nani amkinge mwenzie ,Aryan hataki mama yake aingie katika matatizo ama kupoteza maisha huku ,mama hataki mtoto wake afe anaona bora yeye apigwe risasi na si Aryan
Wakati wanagombana Kudra alifanikiwa kujikakamua japo tumbo lilikuwa linamuuma alifanikiwa kufyatua risasi ,wakati risasi inakuja kwa kasi Aryan aliiona ,na mama yake ndio alikuwa amemkinga mwanae asipatwe na ile risasi.
Lakini ile risasi Aryan aliiona, cha ajabu hawakujua mahali imepotelea na ilikuwa inaenda kumpiga mama yake maeneo ya mgongoni, kitu kilichomfanya hata Mussa na Kudra wabaki wameduwa.
Halafu Samairah alitabasamu na kumkonyeza Jesca ,ki ukweli ile risasi Samairah aliipoteza kwa kupitia uwezo wake ,aliiangalia ile risasi na macho yake yanauwezo wa kuvuta kitu chochote cha kumdhuru mtu anakifuta kabisa ,ina maana ile risasi iliishia kwenye macho yake lakini yeye hakudhurika ila tu vitone vidogo vya machozi ndio vilitoka tu,
Samaira alimwangalia tena Kudra maeneo ya tumboni tena ,ndipo Kudra alilegea mwili wote na asijue nini chanzo ,akina Mussa waliwahi kwa Kudra na kwenda kumuamusha baada ya kuona kalegea,
Wakati huo akina Aryan Jesca na Samairah bila kuwasahau akina Abbas na mama yake na Aryan ndio walikuwa wanaondoka taratibu kwenda nyumbani japo liliwafanya kundi la Kudra wasiweze kuelewa chochote ,wakati wanaelekea nyumbani basi Jesca alikuwa kimbele mbele mara amshike mkono Aryan mara amshike mama yake na Aryan ki ukweli alikwa anawakera sana akina Aryan ila ndio hivyo Aryan hupenda amani ndio maana alishidwa kumwambia ukweli.
Jesca alianza kuongea ” mama Aryan kiukweli nilikutesa ila nisamehe yote hayo niliyafanya sikujua kwamba wewe ndio mzaa handsome Aryan ujue mama nakupenda ee ,Jesca alimkumbatia mama yake na Aryan ,yote hayo anayafanya ili kumshawishi mama yake na Aryan amsamehe makosa yote aliyoyafanya nyuma.
Mama Aryan alimshika mkono Samairah kisha akamwambia Samairah mie nakupenda ila ingependeza kama mwanangu akimaliza shule akuo…. kabla hajamaliza Aryan alidakia na kumwambia mama kuoa tena subiri bana ,nikifika muda wa kuoa nitachagua nimpendae
Basi Jesca kusikia hivyo alidakia na kusema si utanioa mimi ee,hapo Aryan aliona kama wanamkera wakati huo washafika maeneo ya kibo complex ,Aryan aliomba ashuke walau akapate maji ya kunywa maana alikuwa anasikia kiu mno,alishuka na kuvuka barabara upande wa pili alinunua maji lakini watu walimwangalia sana maana nguo zake zilionekana zimechafuka na udongo mbaya halafu mwili wake ukiwa na majeraha ,basi kila mtu alisema lake kila alipo mwangalia Aryan.
Wapo walisema huyu labda walikuwa wanapigana na wengine walisema labda kapigwa na vibaka ,basi Aryan alinunua maji akanywa, pia alirudi na kupanda kwenye gari maana Samairah alikodi gari .
Aryan alianza kumuuliza maswali Jesca
“Jesca kwanini ulimteka mama yangu na kwenda kumtesa huko ” Jesca alifikiria na kukosa jibu alimwangalia mama yake na Aryan na kukumbuka alivyompeleka kule kumtesa alimpiga tena makofi na kumlazimisha amsamehe.
Jesca alizidi kuchanganyikiwa na akakumbuka ule ushauri aliupewa na akina Mussa akamteke mama yake na Aryan amtese hadi aseme ametoa msamaha ,pale ndio Jesca akagundua kuwa Mussa huwa anamtaka kimapenzi ila yeye hampendi ,hivyo Musa alitumia njia ya kuzidi kumfanya Jesca achukiwe na mama yake na Aryan ili ampende yeye .
Pale pale alianza kulia na kuomba msamaha na kuwaeleza kuwa hayo mawazo alipewa na Mussa ,Abbas aliwaza na
Wakati huo Abbas alishuka maeneo ya kibaoni na kwenda zake huku akina Samairah ,Aryan,Jesca na mama yake na Aryan waliendelea na safari. Jesca aliendelea kulia na kusema nisamehe huku moyoni anajisemea ,mwenyewe moyoni “utapewaje mawaza na mtu “,
Jesca aliongea kwa hasira”Kama Aryan unampenda Samairah na hunipendi mimi nitahakikisha huyu Samairah nampoteza ili unipende mimi bora nigaramie pesa ili unipende mimi sina kingine alimwambia dereva simamisha gari aliteremka kwenye gari akiwa na hasira na kuchukua boda boda kuelekea kwao.
Mama Aryan alimuuliza mwanae ,hivi utakubali mtu akulazimishe umpende?, Aryan hakujibu ndo kwanza aliangalia majeraha yake aliyopigwa kisa mkandarasi kamsingizia kuwa yeye ni mwizi alijiangalia na kufanya kuwakumbuka akina Kudra jinsi wanavyo yaandama sana maisha yake ,Aryan akajikuta anakosa raha ,vile kumbukumbu za ukaribu wake na bibi ambae tayari ameshatangulia mbele ya haki ,kiukweli Aryan bado alitamani aendeleee kuwa karibu nae.
Aryan aliendelea kukumbuka maneno ambayo bibi alikuwa akimwambiaga kuwa “binadamu akiamua kuyaandama maisha yako hata ufanye wema kiasi gani bado ataendelea kukutesa” yote hayo Aryan alikuwa akiyakumbuka na kujisemea bibi tulijuana juu juu kwa huruma yangu nikaamua kubeba jukumu la kuhakikisha unaishi maisha yenye ahueni lakini alipangalo mungu kamwe mwanadamu hawezi tia kipingamizi.
Hatimae walifika mbezi walishuka na kuingia nyumbani na kumwacha Samairah akielekea kwake , ,Aryanalifika nyumbani na kuoga vizuri kisha akavaa nguo zingine safi ili akatafute dawa za kupunguza maumivu Aryan aliwaza aende moja kwa moja hadi maeneo ya mwenge ili akatafute dawa kisha akamnunulie na mama viatu ,
Tukirudi maeneo ya bweni ,baada ya akina Mussa na Kudra kuachwa na akina Aryan ,Kudra alishangaa tumbo lake limepona tena baada ya dakika tano ,pia kumbu kumbu za Mussa zilirudi maana nae alivyoshikwa shati alijikuta anakuwa kama zezeta flani ,waliungana tena na kuchukua gari lakini walivyowafuatilia akina Samairah na Aryan hawakufanikiwa kuwaona tena .
Hivyo iliwalazimu kila mmoja aende kwao ,
Tukija maeneo ya mwenge tuna mwona Samairah akiwa kapanda bajaji lakini kwa nyuma alikuwa anafuatiliwa na Jesca tena akiwa nyuma yake wakati huo Samairah hana hata habari kama kuna mtu anamfuatilia ,
Walifika mwenge pale kwenye mataa wanapaita makutano ya bara bara wakati huo Aryan nae yupo maeneo yale ya pale pale mwenge, kuna kilema alikuwa anakokotwa barabarani ili avushwe upande wa pili ,lakini gafla yule ambae alikuwa akimsukuma kilema kwenye kibaiskeli kuna mdudu aliingia machoni na kufanya asione ,alikumbatia macho yake ili kumtoa yule mdudu kwenye jicho,
Lakini walikuwa katika eneo hatari mno ,kuna lori kubwa lilifeli breck kwenye mataa na kujikuta likikimbia spidi ya juu kuelekea aliko yule kilema ambae alikuwa kavalia sweta kubwa na alifunika kichwa chake na kofia hivyo Aryan hakufanikiwa kumjua ni nani.
Lile lory lilikuwa linaenda kumgonga yule kilema ,kila raia aliyekuwepo maeneo hayo alifumba macho wengine masikio ili wasiweze kushuhudia jinsi kilema yule anagongwa na lile lory ,sauti za mshangao zilirindima maeneo ya mwenge kila mmoja alisema jamaniii yule mwenye lori anakwenda kumgonga yule kilema masikini !!!
Lakini Aryan alikuwa karibu na eneo hilo ,alichokifanya aliruka na kuishika ile baiskeli ya kilema na kuivuta kwa nyuma pale pale lori likapita mahali alipokuwa kilema lakini tayari alikuwa kaokolewa na Aryan.
Ile kofia ya sweta ambayo yule kilema alikuwa amejifunika sura yake isionekane ilitoka na Aryan kuibaini ile ilikuwa sura ya mkandarasi ,daaaa mkandarasi aliinua kichwa na kumwangalia Aryan kisha akacheka he he he he umeniokoa ,kumbe bado waona ina maana ule unga hujaozesha hayo macho ? Aliuliza
Mkandarasi alicheka na kufanya kila mtu ashangae lakini Aryan akiwa kashikilia ile baiskeli ya kilema ambae alikuwa kakaa mkandarasi alikuwa bado hajaiachia Aryan alishangaa kwa mara nyingine anakutana na mkandarasi na alishagundua mkandarasi si mtu mwema kwake
Aliachia ile baiskeli lakini nyuma yake kulikuwa na yule mtu anae mkokota mkandarasi alitoa kisu kikali cheupe chenye icha kali bila kuchelewa alikikita maeneo ya mgongoni kwa Aryan puuuu!
Aryan alijikuta akicheua damu na kukosa cha kufanya tayari kachomwa kisu na mtu ambae anamkokota mkandarasi inaonekana yule mtu alisetiwa ,ama dili walipanga popote watakapo mwona Aryan wamuue.
Aryandamu zikaanza kumtoka wakati huo Samairah nae anashuka kwenye bajaji ili akamwangalie nani kachokwa na kisu
Maana alisikia sauti ya Aryan akisema jamani kisuuuuuu ,huku mkandarasi akacheka na yule anae mkokota alishika baiskeli na kuendele kumsukuma na kuondoka zao eneo la tukio.
Masikini Samairah nae wakati anaenda kumwangalia Aryan ,nyuma kulikuwa na mbaya wake anamfuatilia bibie Jesca alishika usukani wa gari na kusema ,
“Ngoja nikuuwe wewe unajifanya na weupe wako leo nakuondoa alimwelekezea gari na kwenda kumgonga Samairah ilisikika sauti ya kishindooo paaaaaaaaaaah
Wakati huo Jesca anacheka na kusema nimekumaliza akachochea gia ili aondoke lakini alivyogeuka nyuma alijikuta anaachia usukani na kusema mungu wanguuu uwiii
Nini hiki nimefanya? Jesca alijutia huku akionekana kuchanganyikiwa
………………………..
Tulipo ishia baada ya Aryan kumwokoa mkandarasi kunusurika na kifo cha kugongwa na gari lakini mkandarasi bado hakuwa na shukrani hata kidogo yule kijana anaefanya kazi ya kumsukuma kibaiskeli ,mkandarasi walikuwa wamepanga mbinu na mkandarasi nia yao wamuue tu Aryan aondoke katika huu ulimwengu kwa kuwa anajua yeye ni kilema hawezi kufugwa jela ,alitoa kisu na kukikita mgongoni mwa Aryan kisha mkandarasi akaendelea kucheka ha ha ha ha pia na yule naliyemchoma Aryan kisu alikiachia pale pale kisha akaendelea kumsukuma mkandarasi na kuanza kuondoka katika eneo hilo huku Aryan akiwa ameganda pale baada ya kisu kuzamishwa katika mwili wake.
Bibie Samairah nae wakati anaenda kuangalia nani kachomwa kisu ,kumbe nae mbaya wake alikuwa anania mbaya alimwelekezea gari Samaira ,
“Jesca akiwa anatabasamu anakwenda kumgonga Samaira
Ki ukweli gari ilimpitia Samairah juu lakini cha ajabu alichokishuhudia Jesca alijikuta anachanganyikiwa peke yake na kutetemeka mwili mzima.
Alikuta kamgonga mama yake mzazi alijikuta anaachia usukani huku akiita mamaa kwanini mama umefanya hivyooo? Alifunga breki za gari hadi tairi nusu ziwake moto ,
Kila mtu alishangaa ile ajali ,ndugu msikilizaji kama unaroho nyepesi waweza ukapitisha macho juu juu.
“Mama yake na Jesca aliharibiwa mno aligongwa utumbo uliruka mbali na miguu kubakia kwenye tairi, mikono nae ilikuwa ipo na kichwa ,lakini mama alibakia kifua na mdomo alitoa kauli moja tu kisha akayafumba macho,alisema “KWAHERI JESCA” taratibu aliyafumba macho yake ,Jesca akajikuta analia kwa uchungu mno na kujutia kwa nini wivu wa mapenzi unamfanya anampoteza mama yake mzazi ,
Jesca aliinua kichwa ili kumwangalia Samairah yu mahali gani maana yeye ndiye chanzo cha kifo cha mama yake ,
Alimwona Samairah kasimama pembeni huku amemshika Aryan mkono huku akiendelea kutema damu baada ya kuchomwa kisu ,
Jesca kwa hasira alimrukia Samairah ili kumpiga sijui kaokotaje jiwe alitaka kumpiga usoni ,lakini Samairah alikwepa na kumwambia Jesca kweli wewe ni rafiki yangu ngoja nimuwahishe Aryan hospitali nitakuja kukusindikiza tukamzike mama yako
Watu walishangaa ile ajali ilifanya watu wasahau kama Aryan kachomwa na kisu ,watu walikuwa wakishangaa damu zilizotapakaa kwenye lami.
Viungo vya mama yake na Jesca ,kiukweli watu walishidwa kujizuia walijazana pale na kushangaa viungo vimezagaa kwenye bara bara ,polisi waliweza kufika kwenye eneo la tukio ,kumbuka baba yake na Kesca ni mkuu wa polisi kitengo cha usalama wa barabarani aliweza kufika pale na kukuta damu zimezagaa alivyomtazama mwanae ndio alikuwa kakumbatia kichwa na kifua cha mama yake akilia ,
Baba wala hakushangaa alicheka kisha akasema Jesca nani kakupa funguo ya gari?
Jesca hakujua nini amjibu baba yake zaidi ya kuendelea kupiga kilio ,baba yake aliita kitengo maalumu kwa ajili ya kuubeba mwili wa mke wake ili kwenda kuhifadhia kwa ajili ya maandalizi ya mazishi ,baba alimsogelea mwanae na kumwambia ,kweli nimeamini maneno ya mganga ,aliniambia nitatajirika sana ila nitampoteza mke wangu nimpendae shauri ya wivu wa mapenzi na alinambia mwanangu nawe utakufa kwa laana za watu kwa uovu uutendeao watu ,
Baba aliuliza “kwanini umesababisha ajali na kumgonga mama yako?,hapo ndipo Jesca akajikuta akitoa macho na kushidwa nini chakujibu ,alianza kukumbuka matendo aliyoyafanya nyuma na kila mtu alishamwambia utakufa kwa laana ,alishawahi kumwagia mwanafunzi mwenzake chai ya moto ,usoni ,ashawahi kumuunguza mama yake na Aryan ,maji ya moto kwenye mkono wake pasina sababu ,pia na kumteka mama yake na Aryan na kwenda kumtesa ,
Jesca aliendelea kukumbuka ,hata mama yake Aryan alishamwambia hawezi kumpenda hata kidogo maana amejaa uovu hivyo hawezi kuridhia awe mpenzi ama mke wa mtoto wake.
Sehemu Ya 5
Jesca akazidi kukumbuka na sasa baba yake amemtamkia kuwa sharti la mganga aliyempa utajiri alikwisha kumwambia mama yake atakufa kwa ajili ya wivu wa mapenzi ,ndipo Jesca alijikuta akigonga kichwa chake kwa nguvu
Kwanini mimi nimekuwa na wivu ,ona nimempoteza mama yangu ,kwanini Samairah ,kwanini Samairah,Jesca alianza kupiga makelele huku baba yake , akimwangalia tu ,
Jesca alikuwa kavalia suruali ,aliingiza mkono mfukoni aliweza kutoa
Kikaratasi kidogo ambacho kilikuwa na unga ,tena unga ule hatari sumu ,ambayo Aryan alipuliziwa kwenye macho na mkandarasi ili awe kipofu ,maana huo unga ukigusana na maji ya aina yeyote na kugusa mwili wa binadamu basi mwili lazima ukatike katike vinyama ,
Jesca alijiona hana bahati pia kwenye ulimwengu hastahili kuishi upesi alikifungua kile kikaratasi alitoa ule unga akatia mdomoni ,kwa pembeni kulikuwa na chupa la maji lilikuwa na maji kidogo aliokota na kufungua upesi aliyanywa yale maji.
Dakika hazikupita hata mbili ki ukweli ile ilikuwa sumu kali mno ,alianza kukatika katika ulimi ,baba yake akimwongelesha mwanae ,aliita Jesca umekula nini mwanangu ,mwanangu nini umekula ,
Jesca tayari alishaanza kulegea alimwangalia baba yake kisha akamjibu ,baba nilisoma kwa dharau na kujiona mimi ndio mimi ,nikijua baba yangu unautajiri wa jasho lako kumbe utajiri wa kupitia waganga ,nimepata laana nyingi kwa watu niliringia utajiri wa kichawi baba mimi sifai kuisha kwa…
Jesca hata hakumalizia tayari alianza kutema vipande vya ulimi ,ulimi wa Jesca uliorojeka na kukatika katika ndani ya dakika mbili meno yalianza kutoka moja moja ,ile sumu ilikuwa haifai hata kidogo kila ikigusa kiungo kilikatika
Jesca alijikuta anadondoka chini utumbo wote ulisagika sagika baada ya kuimeza ile sumu ,baba yake alizidi kuchanganyikiwa ,aliita gari ili amuwahishe hospitali ya pale mwenge aliwahishwa na kupelekwa chumba cha watu mahututi ,kutokana na ile hospitali kuwa na uhaba wa vyumba ililazimika apelekwe chumba ambako Aryan yupo anatibiwa baada ya kuchoamwa na kisu.
Na Aryan alikuwa anatibiwa mahali alikochomwa na kisu,wakati Aryan ameshapoteza kumbu kumbu ,huku madaktari wakijitahidi kumpatia huduma .
Upande wa Jesca alivyoingizwa kwenye kile chumba aliko Aryan ,pale Aryan alijikuta akifungua macho alianza kupata ahueni alivyogeuza macho aliweza kushuhudia mwili wa Jesca ukifunikwa na madaktari kusema tayari ashakufa ila inaonekana amemeza sumu kali mno ,madaktari ilibidi wampasue tumbo Jesca waweze kujua nini hasa ama hio ni aina gani ya sumu ,kitendo cha kugusa tumbo la Jesca tayari lilikuwa lishaanza kuoza na kukatika katika ,ili bidi wamfunike na kupelekwa kwenye sehemu ya kuifadhia miili yaani mwochwari.
Baada ya Aryan kupata ahueni ,ndipo Samairah aliruhusiwa kuja kumwona ,Samairah alikuja akiwa katabasamu ila alikuta Aryan akiwa katika dimbwi la mawazo mazito akiwaza ,
Samairah aliuliza Aryan unaendeleaje? Aryan alimwangalia Samairah na kumwambia nashukuru mungu niko salama lakini Jesca kapatwa na nini mbona nimeshuhudia kama amekufa?
Samairah alimwangalia sana Aryan na kuguna ” mmmmmmh we hujui ki ukweli Jesca kafariki na kajiua mwenyewe kwa kujua maovu yake aliyowatendea watu ,Samaira alimwambia Aryan.
Aryan aliuliza tena ,maovu gani hadi ajiue ?
“Samairah alitabasamu na kusema Aryan huwezi elewa kwa sasa ila … Samairah hakumalizia na kuwaza itakuweje endapo Aryan atajua mimi si binadamu kamili?
Mara Samaira alitabasamu na kusema ,Aryan wacha leo nikuweke uwazi ,kiukweli ile ajali ambayo uliiona pale baada ya wewe kuchomwa na kisu ,ile ajali ndo ingetakiwa nife mimi ,ila mimi sikufanikiwa kufa wala kudhurika
Aryan alidakia sasa ni nani aliyekufa pale maana mie niliona viungo vimetengana mara miguu imenasa kwenye matairi ya gari utumbo ulidumbukia mtaroni ,
Sasa ni nani alokufa ?
Aryan aliuliza ili aweze kuelewa ,Samairah alikaa kidogo kimya kisha akamwangalia Aryan huku akahofia kusema ,lakini aliona akiendelea kumficha Aryan kwake itakuwa tabu kidogo maana Aryan anaandamwa na watu pasina sababu.
Samairah aliangalia kucha zake kisha akashika nackless aloivaa shingoni aliangalia chini na kumwambia Aryam
“Mtu alokufa sio mtu hilo lilikuwa boksi tu tena lenye taka taka ,hivyo mama yake na Jesca yupo hai tena yuko nyumbani
Ila Jesca ndio kafa sababu kajiua mwenyewe kwa kujutia aliyoyafanya.
Aryan ilibidi ainuke kitandani na kusema ile ajali ndo ilikuwa box?
Na si mtu kugongwa na gari?
Hebu niweke wazi Samairah nielewe….
Samairah aliangalia kucha zake kisha akashika neckless aloivaa shingoni aliangalia chini na kumwambia
Mtu alokufa sio mtu hilo lilikuwa boksi tu tena lenye taka taka ,hivyo mama yake na Jesca yupo hai tena yuko nyumbani
Ila Jesca ndio kafa sababu kajiua mwenyewe kwa kujutia aliyoyafanya .
Aryan ilibidi ainuke kitandani na kusema ile ajali ndo ilikuwa box Aryan alizidi kukodoa macho alijaribu kusimama ila mgongoni mwake palikuwa na jeraha alilochomwa kisu,
Samaira alisema ndio hilo lilikuwa box kwani wewe uliona nini?,Samairah alimuuliza swali Aryan,Aryan alisema “mbona niliona mwili wa mwanamke umesagwa sagwa na gari” ,kabla Samairah hajaeleza mama yake na Jesca aliingia hospitalini akiwa analia ,jamani mwanangu kwanini umeamua kujiua ,mimi mama yako bado niko hai ,
Kwanza hospitali nzima kila mtu aliacha kufanya shughuli zake na kumshangaa mama Jesca ,ki ukweli sura ya marehemu aliyeletwa kuwa amegongwa na gari ,ndio ile ile mama Jesca anaonekana mzima hali iliyowafanya watu kupata hofu na kujua labda maiti kafufuka.
Hata baba Jesca alimuogopa mkewe na kusema sielewi hata kidogo ,mama aliendelea kulia kwa kwikwi mno huku akitaja jina la mwanae, daktari ilibidi aondoke na madaktari wengine kwenda sehemu ya kuhifadhia miili ya marehemu ,walienda sehemu ambako walihifadhi mwili wa mama Jesca walifungua kila mmoja alibaki mdomo wazi na kuzidi kubaki njia pamda .
Ki ukweli walikuta mabox ,ilibidi watoke na kusema kweli huyu ndio mama halisi wa mtoto aliyekufa na ile ajali iliyotokea si ajali ya kawaida kama mlivyozoea ile ni miujiza ama mambo ya kishirikina lilikuwa box ambalo limegongwa na gari ,daktari alitoa ufafanuzi huku watu wakizidi kushangaa tukio hilo.
Wakati baba yake na Jesca anamwogopa mkewe alitoka nje na kutaka kukimbia japo alikuwa kavalia mavazi ya polisi usalama wa barabarani ,lakini wakati anatoka kwenye geti la hospitali alishangaa kuona njemba moja akiwa amefunika uso ,yule njemba hakupenda kupoteza muda alitoa kile kitambaa ambacho amefunika macho , ki ukweli hali aliyoiona kamanda wa polisi alianza kutetemeka ni mtu ambae anamjua vizuri
Si mwingine alikuwa Joshua ,ambapo kwenye vipande vilivyopita alipewaga kazi ya kuwaua akina Abbas na mdogo wake Gwae ,lakini hakuwaua na alishaeleza kazi yake huwa anapewa tenda za kuua watu.
Sasa leo kakutana na baba yake Jesca, ki ukweli baba Jesca alianza kukumbuka miaka ya nyuma iliyopita alikuwa anatembea na mke wa Joshua kisha alimpa mimba mke wa Joshua na kumtishia endapo atasema atamuua ,mke wake Joshua hakusema hadi alivyobanwa na Joshua alieleza kuwa ameahidiwa kununuliwa gari na kamanda Jacob ambae ni baba yake na Jesca ,
Ndipo Joshua alimuuaga mke wake baada ya kugundua anatembea na kamanda Jacob na kuahidi kuwa atamtafuta Jacob nae atampa malipo ya kutembea na mke wake ,sasa wamekutana .
Joshua alitabasamu na kusema kamanda, mimi muda wangu wa kuishi umekisha hivyo siwezi kukuacha tunakufa wote ,
Joshua aliongea kisha alifunua koti lake alitoa nondo iliyochogwa ncha kali kisha aliirusha na kuikita kwenye kitambi cha Jacob,pale pale Jacob alitoa jicho kubwa na kubaki ameganda kabla hajatulia Joshua alitoa panga na kumfyeka Jacob huku watu wakishuhudia.
lakini Joshua alipo maliza alitoa kachupa kadogo kalikuwa na ule unga ambao Jesca aliula na kufa papo hapo ,na Joshua aliuchukua ule unga akatia mdomoni akasukumizia na maji.
Joshua alikaa chini na kusema polisi nikamateni ,mara difenda ya polisi ikiwa imejaa polisi walifika pale hospitalini na kukuta Joshua kalala huku kafumba mdomo ,ki ukweli polisi walikuwa hawajui chochote walifika na kumwambia upo chini ya ulinzi bila yakujua kama amekula sumu ,
Huku wameshikilia bunduki zao ,mmoja alimsogelea Joshua alimgeuza Joshua akiwa hoi alitikisa kichwa kisha aliachama mdomo wake na kutema ulimi ukiwa na rangi nyeusi pale pale akafumba macho tayari alikuwa ameshafariki ,huku Jacob nae kauliwa pale pale hospitani. Ni matukio yaliyoacha historia na kuongelewa kwenye vyombo vya habari na mitaani.
Mama Jesca alitoka hospitali akiwa analia ,aliita mume wangu ile anataka kutoka alipishana na madakatari wakiwa wamebeba mwili wa mume wake ,pale pale mama alipoteza fahamu ,ki ukweli lile tukio liliweka historia kubwa mno .
Aryan aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata nafuu ,akiwa kaongozana na Samairah aliendelea kuuliza ,hivi ulishawai kuona ajali inatokea mtu amegongwa halafu unakuja kusikia mtu kagonga box? Aryan aliuliza huku akimwangalia Samairah ,
Samairah alianza kuwaza ni heri niondoke hapa duniani maana hata Aryan akigundua mimi si binadamu kamili ataniacha ,Samairah alikosa kabisa furaha na kukosa la kufanya ilibidi amchukue Aryan hadi nyumbani anakoishi alimkabidhi mama yake na kuwaaga Aryan na mama yake kuwa yeye anaenda mbali na hadhani kama atarudi tena waweze kuonana katika hii dunia.
Mama Aryan aliumia sana maana ametokea kumpenda sana Samairah alimpenda na wote hawajui kama yeye ni nusu mtu nusu jini ,Aryan nae alianza kuwaza matukio ya zamani wakiwa shuleni ,walikuwa pamoja alimletea chapati alimsaidia pesa za matumizi leo hii Samairah anasema anaondoka kwa nini ? Na anaenda wapi Aryan alizidi kujiuliza maswali pasina kupata majibu
Samairah alivyomaliza kuwaaga aliondoka lakini nyuma Aryan alimfuata na kutaka kujua kwanini Samairah anataka kuondoka ,
Aryan aliita “Samairah kwanini wataka kuondoka na waenda wapi?” Samairah alimwangalia Aryan na kumwambia naenda mahali aliko mama yangu na baba yangu ,Aryan alikaa kimya na kumuuliza wewe si uliniambia unaishi mikocheni sasa mama yako yuko wapi, Samairah alimwangalia Aryan kisha akaendelea kutembea ,maana anahofia kumweleza ukweli ,
Samairah aliuliza Aryan kwa mfano ukapedwa na jini na akataka muoane utakubali ? ,Aryan alicheka na kusema hata kwa dawa siwezi kukubali kupedwa na jini mimi, ki ukweli lile jibu lilimfanya Samairah adondoshe machozi maana mtu mwenyewe anayempenda hataki kusikia habari za majini halafu yeye ni jini.
Samairah alimwambia nenda kwa akina Abbas kamuulize gwae akuelezee kitu flani kuhusu mimi nakupa hiyo kazi ,Samairah aliongea kisha akapanda piki piki na kumwambia Aryan kwaheri hatuwezi tena kuonana , Samairah akiwa kwenye piki piki alikuwa analia na kujutia moyo wake kwanini ulimpenda Aryan wakati Aryan hataki hata kuoana na jini.
Samairah aliondoka hadi baharini ,alivyofika alikaa akajiinamia kisha alipangusa machozi yake na kusema naondoka mie sitakuona tena Aryanalikaa kimya kwa muda kisha alimuita mama yake kisha akaongea lugha isiyoeleweka alipotea na kwenda aliko mama yake ,aliumia sana maana Aryan kamwambia hawezi kuoa jini ,na swali lile Samairah aliuliza kwa mtego .
Tukirudi upande wa pili
Mama Jesca alizinduka kisha taratibu za mazishi ya mtoto wake pamoja na mume wake yalianza kuandaliwa akina Mussa walipata hizo taarifa za kupotelewa na Jesca na wao walienda kwenye msiba ,walifanikiwa kuwazika Jacob pamoja na mwanae Jesca, kiukweli ulikuwa msiba mkubwa sana kwa mama yake Jesca
Baada ya kumaliza mazishi walikaa siku kama kumi nyumba ya mama Jesca iliungua moto ,magari na kila kitu vyote viliteketea ki ukweli watu walijitahidi kuokoa vitu lakini vitu vilikuwa havibebeki hata kidogo vilikuwa vizito mno,yote sababu ya utajiri ulikuwa wakichawi ,mali zakamanda Jacob ziliisha na mama Jesca kuishi kama masikini ,alianza kutanga tanga mitaani nae alivyoona maisha magumu aliamua kujinyonga ,hivyo familia yote ilifariki.
Siku zilikatika hadi shule zilifunguliwa ,Aryan akiwa darasani alimkumbuka sana Samairah ,alianza kukumbuka jinsi alivyomuokoa alivyotekwa na akina Mussa ,
Jinsi alivyomdaka alivyotupwa toka gorofani na akina Mussa ,Aryan alizidi kusema hapana lazima nimtafute Samairah nimemkumbuka halafu nimeanza kuwa nae na hisia za kumpenda ,
Hatimae yalifika majira ya saa nane waliruhusiwa na kurudi nyumbani , siku hiyo Aryan alikumbuka alivyoambiwa na Samairah siku wakati anaondoka ,Samaira alimwambia ukitaka kujua yeye ni nani akamuulize Gwae ,maana Gwae ndio anamjua Samairah ni nani
” oyaa Abbas ndugu yangu leo sijielewi najikuta nimemkumbuka Samairah na sijui nitampata wapi maana aliaga anaondoka na mimi nilikosea sikumuuliza anaenda wapi ,hebu twende kwenu nikamuulize Gwae jambo flani ,
Waliondoka hadi kwa akina Abbas walifika na kumkuta mama Abbas akiwa na mama Ashura wamekaa kibarazani wakiwa wamejitanda vizuri mitandio yao wamefunga ushungi
Huku wakichambua njegere ,waliendelea na kupiga story zao.
Aryan alifika na kuwasalimia kwanza mama Ashura alivyomuona Aryan alitabasamu na kusema Aryan baba Assalam alaykum pole na masomo ,ki ukweli mama Ashura alikuwa kabadilika kawa mkarimu anaswali swala tano pamoja na mama Abbas huku wakiwa na chuo cha kufundisha mafunzo ya kiislamu.
Aryan aliitikia na kusema yes hadi raha watu ambao walikuwa wanaongoza kwa tabia mbaya mtaani leo hii wamekuwa watu wa dini ki ukweli inatia furaha sana.
Mara Gwae alirudi kutoka shule ,cha kwanza alienda hadi kwa mama Ashura alimsalimia ndipo mama Ashura akamsaidia kumtua begi la shule mama Ashura aliinuka na kwenda kumtengea chakula Gwae ,ki ukweli upendo ulizidi maana hata Gwae ashaponaga mikono yake iliyovunjika.
Baada ya Gwae kumaliza kula,Aryan alimwita Gwae kisha wakatoka nje lengo lake alitaka kujua Samairah ni nani , kwanza alimuuliza Gwae hivi tokea umemuona Samairah ulishawahi kuona kitu gani ambacho kipo tofauti na watu wengine ,
Gwae alishituka na kuinuka alianza kukimbia na kusema Samairah sio binadamu huyoo ile Gwae anakimbia ili asimweleze Aryan maana alishapewa onyo kali na Samaira asieleze chochote kuhusu Samairah aliambiwa asiseme chochote
Lakini Gwae alijikuta anamparamia kilema mmoja ambae alikuwa amekokotwa na kibaiskeli huku kaongozana na vijana saba.
Aryan kuangaalia mbele alijikuta amezungukwa na vijana saba waliojazia huku kwa mbele yake kuna kilema asiyekuwa na miguu wala mikono si mwingine alikuwa ni mkandarasi.
Mkandarasi alicheka kwa nguvu na kusema wewe kijana unanini mbona hufi nakufanyia kila kitu kibaya lakini hadi sasa hujadhurika sasa leo nimekuja ,mzima mzima ,sina mikono wala miguu ila leo lazima nikuue mwenyewe ha ha ha mkandarasi alicheka kwa dharau………
Mkandarasi alicheka kwa nguvu na kusema wewe kijana una nini ? mbona hufi ?,nakufanyia kila kitu kibaya lakini hadi sasa hujadhurika sasa leo nimekuja ,mzima mzima ,sina mikono wala miguu ila leo lazima nikuue mwenyewe ha ha ha mkandarasi alicheka kwa dharau kubwa mno ,Aryan akiwa bado kahamaki wale vijana sita waliokuja nao walimshika Aryan upesi kisha wakamsukumiza matambara mdomoni ili asiweze kupiga kelele ,walimfunga kitambaa machoni kisha wakampakia kwenye gari ,mkandarasi alikuwa akichekelea wakati huo Abbas alikuwa yupo ndani anavua nguo za shule ,
Lakini mkandarasi aliamuru hata Gwae akamatwe na yeye sababu alishuhudia Aryan, wakimkamata wanahofia taarifa kuja kusambaa kutekwa kwa Aryan ,masikini Gwae bado mtoto mdogo lakini akaingia kwenye matatizo kama yale,
Abbas anatoka nje akiwaita Aryan na Gwae hakuona kitu ,alivyoangalia chini aliona kuwa kuna gari imekuja maeneo yale, Abbas hakuwa na mashaka sana alijua labda Aryan ameondoka na Gwae ,maana huwa anapenda kutembea nae.
Safari ya mkandarasi kilema iliishia maeneo ya salasala kuna jumba moja kubwa geti lilifunguliwa kisha akaingia ndani,Aryan akiwa kafugwa macho pamoja na Gwae walishushwa na kuingizwa ndani ,Gwae alikuwa akilia tu ,machozi ndio yalikuwa yakibubujika lakini sauti haikutoka yote sababu ya kufugwa matambara mdomoni,
Aryan alishushwa na mkandarasi kwakuwa ni kilema huwa anabebwa juu juu ama kutembea na baiskeli yake ,Aryan alishushwa chumba kimoja pamoja na Gwae na kile chumba kilikuwa na giza totoro. walitolewa matambara mdomoni kisha wakaambiwa nawapa dakika kumi kwa ajili ya sala ya mwisho .msali maana leo lazima mfee ,”mkandarasi aliongea” na kupelekwa kwenye meza ya chakula .alilishwa kama mtoto yote sababu hana mikono wala miguu.
Aryan alijua fika leo hawezi nusurika kamwe alimshika Gwae mkono na kumuuliza ,Gwae leo ndo tumeambiwa tunauliwa naomba unieleze chochote kuhusu Samairah japo ashaondoka ila ningependa kujua ,yeye ni nani ,
Gwae alimshika Aryan mkono kisha akasema ,kaka Aryan ,mi najua Samairah si kiumbe mbaya ,alitusaidia sana pale mama yetu alivyokuwa akinywa pombe na kutaka kutufukuza ,Samairah alikuwa yupo upande wetu ,vile vile mimi nampenda sana aunt Samairah kwanza anapenda kucheka cheka muda wote . Gwae aliongea huku akionesha sura ya huzuni ,aliendelea kueleza.
“Kunasiku mliniacha nyumbani kwenu mbezi Samairah alikuja na kunikuta nimekaa ndani ,Samairah alisema anahisi joto ,na siku hiyo hapakuwa na umeme ,alitoka zake nje na kuzunguka nyuma ya nyumba,.
Mimi nilijua labda kaondoka nilianza kuzunguka nyumba ya kwenu taratibu nikishangaa maua ,ki ukweli nilishituka baada ya kumwona aunt Samairah kajiachia, kwanza
Miguu yake ni kwato kama za farasi alikuwa na manyoya mepesi na meupe mazuri ,ila alikuwa na kichwa cha binadamu ila kichwani alikuwa na masikio makubwa ,
Nilivyomuona tu alishituka na kurudi kwa umbo lake la kawaida ,na kuinuka upesi, kuja kushituka kanishika mkono ,
Ki ukeli nilimuogopa sana ila aliniambia nisiseme chochote kuhusu umbile lile nililo liona ,ndipo nilipataga ujasiri na kumuuliza wewe ni nani ,aunt Samairah aliniambia kuwa yeye ni jini ila jini asiyedhuru watu ovyo.Basi tokea siku ile sikumuogopa tena ,
Gwae alimalizia kuelezea na kumfanya Aryan akumbuke kabla Samairah hajaondoka alimuuliza swali mfano ikitokea ukipendwa na jini utaweza kumuoa ,Aryan alitabasamu na kusema khaa kumbe lile swali alikuwa anajiongelea yeye , moyoni Aryan aliwaza Samairah nakupenda hata kama wewe ni kiumbe tofauti na mwanadamu.
Ile Aryan kusema kimoyo moyo kuwa anampenda Samairah ,chini ya bahari ndipo makazi ya Samairah yalipo pamoja na familia yake ,ujumbe aliupata ,kipindi chote Samairah toka aondoke kwenye ulimwengu hakuwa na furaha lakini siku hiyo alijikuta akitabasamu baada tu ya Aryan kusema na nafsi yake anampemda Samairah.
Yaani Samairah alikuwa akisikia kila kitu Aryan anachozungumza na aliamini huenda ipo siku Aryan atasema anampenda hatimae ndoto zake zimetimia.
Samairah alitabasamu na kusema kama kweli Aryan ameridhia kunipenda ,basi sina budi ya kuishi mwenyewe acha nianze safari ya kurudi duniani tena kwa ajili ya Aryan,
Samairah alimuaga mama yake kuwa anatoka kidogo mama yake alimruhusu kisha alijiandaa kuondoka kuja duniani kwa ajili ya Aryan.
Maana kwenye moyo wake alisikia Aryan alivyojisemea kimoyo moyo kuwa anampenda yeye.
Turudi mahali Aryan na Gwae walipo taa ziliwashwa kisha mkandarasi akiwa kaongozana na vijana watatu aliingia chumbani akiwa amekokotwa kwenye baiskeli ,hatimae aliingia hadi ndani.
Mkandarasi alimwangalia Aryan na kumwambia wewe kijana mimi nishakuambia hadi kufa kwangu lazima nikuue,,najua nitakufa nikiwa na chuki mbali mbali nimeua watu wengi sana najua nitaenda kuchomwa moto siku yangu ya mwisho .
Mkandarasi aliomba Aryan akamatwe kisha asogezewe shingo ya Aryan karibu na mdomo wake ,wale vijana walifanya kama alivyowaambiwa ,mkandarasi alicheka na kusema nakung’ata kwenye koo halafu damu yako niinywee ili ujue kuwa nina hasira na wewe,umenisababishia nipate ukilema sasa sitaki kukuona kwenye hii dunia, mkandarasi aliupeleka mdomo wake ili amng’ate Aryan koo ili afe yote sababu hana mikono na hataweza kumshika ,wala kumpiga
Lakini kabla hajamng’ata kuna mdada alikuja na kumwita baba samahani nakuomba mara moja , mkandarasi aligeuka na kuuliza kunanini mwanangu? Aryan aliachiwa na kusimamishwa ,ukweli Aryan alibaki ameduwaa baada ya kumwona Joyce akiwa kavalia suruali iliyo mbana ,Aryan alishangaa imekuwaje asome na Joy kumbe baba yake ndio mkandarasi.
Aryan alishidwa kujizuia aliita Joy,pale Joy kugeuka alimwona Aryan maana hata Joy anampenda balaa alikimbia na kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na kuambiwa atoke kwenye kile chumba. Ki ukweli Joy alilia baada ya kuona kuna panga kwenye kile chumba mahali aliko Aryan na anamjua baba yake akiletaga mtu nyumbani ujue kuna jambo,
Joyce aliondoka na kwenda kuchukua simu aliwapigia akina Mussa na kuwaomba waende nyumbani kwao wakamsaidie,
Joy aliwapigia cm wabaya wake Aryan ,akina Kudra na Mussa ,ukweli Kudra anajua kuwa Joy ni mtoto wa kaka yake ila huwa anamchukia sana Joyce maana yeye ndio wa mwisho katika familia ya mzee Kiza na yeye ndie atakae achiwa mali nyingi ndio maana anakuwaga na kiburi kibaya sana.
Mkandarasi aliwaamuru vijana wake wamlaze Aryan chini walitekeleza, Aryan alilazwa na kukandamizwa miguu na mikono ,kisha nondo mbili zilizochongoka zililetwa kisha wakaambiwa waziingize machoni mwa Aryan ,
Basi kijana mmoja aliinama ili azipigilie machoni mwa Aryan,ndugu msikilizaji yaani nondo inagongelewa kwenye jicho na inaurefu wa sentimita 40 Aryan akiwa kapoteza tumaini aliyafumba macho yake kisha akasubiri kitakachotokea kitokee ,
Jamaa aliiweka nondo kwenye jicho la kushoto kisha akachukua nyundo agongelee ,lakini kila akipeleka nondo kwenye macho ya Aryan anajihisi kizungu zungu kikali na kushidwa kugongelea kila akijitahidi ndipo kizungu zungu kinazidi kuongezeka , yule jamaa ilibidi amwambie mkandarasi sielewi kila nikitaka kugonga hii nondo nasikia kizungu zungu mno kidogo nidondoke.
Kwa nje ya hiyo nyumba tunamwona mwanadada akiwa amejitanda ushungi mweupe pee alitembea huku akiangalia huku na kule ,mara kuna gari iliingia nyumbani kwa mkandarasi Jaoy alitoka upesi na kuwafungulia walikuwa ni akina Mussa Joy aliwaelekeza mahali aliko Aryan ili wakamuokoe.
Lakini Joy alivyowaambia kuwa anaenda kuwaokoa akina Aryan na Gwae pale pale Kudra alicheka na kusema kumbe tumemnasa huyo choko kirahisi walienda upesi na kuingia chumba aliko Aryan akiteswa.
Kwanza walikuta amechanjwa na wembe mwili mzima ,huku akipigwa virungu kwenye magoti ila kila wakitaka kumdhuru macho walikuwa wanashidwa mkandarasi alimwagiza kijana wake mmoja akalete ile dawa ya unga ili wamwekee Aryan kwenye macho ,
Mkandarasi aliendelea kuongea” we kijana nimetokea kukuchukia umenisababishia ukilema hadi nami nikupatie ukilema ile sumu ililetwa na wakaambiwa wamuwekee machoni lakin Mussa alikataa na kusema haihitaji hivyo inabidi tumchinje ,Mussa alitoa wazo Aryan achinjwe maana na wao waliingilia kati.
Mussa alitoa kisu na kutaka kumchinja walishangaa Aryan akainuka zile kamba walizomfunga zilifunguka.
Kwa nje walisikia sauti zikiwaita Kudraa ,Kudraa njoo na Mussa upesi Kudra alitoka kuwahi mahali anakoitwa ki ukweli ile sauti Kudra aliifahamu na alikimbia huku akisema mama umepatwa na nini?
Wakati Kudra anakimbia kutoka nje akidhania anaitwa na mama yake. Huku Mussa nae alimfuata akiwa kashika kisu baada ya kugairi kumchinja Aryan.
Pale pale Aryan alipata nafasi ya kutoka na ili akimbie ,wakati Kudra akiwa nje aliona kama mama yake anamwita huku akikimbilia kwenye korongo flani na kinachomshangaza alikuwa anakimbia kwa kasi sana toka azaliwe hakuwahi kumwona mama yake akikimbia namna hiyo hilo jambo lilimtia wasiwasi “inawezekana vipi mama yangu akimbie namna hii?”
Mussa na kudra walianza kukimbia ili kubaini mama yake amefanyaje mbona anakimbia.
Kwa mama Kudra akiwa anakimbia huku anageuka nyuma bahati mbaya kwa mbele kulikuwa na korongo refu mno ,gafla mama Kudra alijikwaa na kudumbukia kwenye lile korongo lilikuwa refu mno ,uwiiiiiiiiiiii mama alipiga yowe huku akibiringita na kwenda kujibamiza kwenge gogo la mti chini pwaaa ,mama alipasuka kichwa kikajigawa mara mbili
Wakati huo akina Mussa na Kudra nao wamefika eneo hilo wakati wanachungulia kwenye lile korongo refu ,bahati mbaya Kudra nae aliteleza wakati anataka kujiokoa nae asidumbukie alimshika Mussa akamvuta na Mussa nae akayumba akadaka kimti kidogo wakati huo Kudra kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashikilia kimti kidogo mno.
Walianza kupiga kelele jamani msaada msaada
Kudra aliangalia chini anamwona mama yake kalala chini huku kichwa kimepasuka kati kati na ubongo umemwagika akiangalia juu kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashika kimti kidogo.
Mara Aryan baada ya kuwakimbia wale vijana wanaotaka kumuua ili kujiokoa asiuliwe na mkandarasi alitokea kwenye lile korongo na kuwakuta Mussa na Kudra wamening’inia, endapo Mussa ataachia kale kamti .wakidondoka chini lazima wafe
Maana chini palikuwa na umbali mrefu ,sasa Aryan kasimama anawaangalia wakilia na kuomba msaada ,
“Aryan tusaidie ndugu yangu” Mussa alianza kujitetea na kumwita ndugu yake wakati huo alishika kisu na kutaka kumchinja mara gafla kale kamti alokuwa amekashikilia kalianza kung’ooka mizizi mara kakakatika ……
Tulipo ishia jana baada ya akina Mussa kuning’inia kwenye poromoko ama korongo refu walianza kupiga kelele jamani msaada msaada !!!!! .
Kudra aliangalia chini anamwona mama yake kalala chini huku kichwa kimepasuka kati kati na ubongo umemwagika akiangalia juu kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashika kimti kidogo.
Mara Aryab baada ya kukimbia ili kujiokoa asiuliwe na mkandarasi alitokea kwenye lile korongo na kuwakuta Mussa na Kudra wamening’inia, endapo Mussa ataachia kale ka mti wakidondoka chini lazima wafe maana kuna magogo kwa chini .
Na chini palikuwa na umbali mrefu ,sasa Aryan kasimama anawaangalia wakilia na kuomba msaada ,
“Aryan tusaidie ndugu yangu” Mussa alianza kujitetea na kumwita ndugu yake. wakati huo alitaka kumkata na kisu na kutaka kumchinja.
Wakiwa wanahangaika kujiokoa mara gafla kale ka mti alokuwa amekashikilia kalianza kung’ooka mizizi mara kakakatika
Aryan aliwaza kwa haraka na kujisemea mimi sio mtoa hukumu japo wanayaandama maisha yangu ,bila sababu wacha niwasaidie Mungu ndiye anaetoa baraka na hukumu ,Aryan aliwahi na kuudaka mkono wa Mussa na kuanza kuuvuta huku Kudra kashikilia mguu wa Mussa , Aryan alijikaza kwa nguvu zake zote na kuanza kuwavuta taratibu taratibu hatimae alifanikiwa kuwatoa nje wote wawili .wakiwa hawaamini kama wametoka salama ,Mussa na Kudra wakiwa wanahema juuu juu ,baada ya kunusurika kufa.
Lakini Aryan aliinuka ili aondoke maeneo yale maana anajua fika licha ya kuwasaidia pia wataweza kumdhuru ,mara kikundi cha mkandarasi kilikuja wakiwa wamembeba Gwae juu juuu ,Aryan aliwaza hawa watu hawana nia njema huenda wanakuja kumrushia Gwae kwenye hili korongo ,na kweli waliweza kufika maeneo yale Aryan alitaka kukimbia ila Mussa alimshika shati na kumwambia oya we boya sisi hatujakuomba utusaidie kwenye hili korongo .kwanza sisi tungejiokoa wenyewe halafu mie nimejifunza makareti hatari hapa ningejibinua na sarakasi wala nisingekufa sasa Mussa aliongea huku kamshika Aryan mkono.
Unaliona hili korongo tuna kudumbukiza sasa zamu yako kudumbukia kiherehere chako tu cha kutusaidia sisi hatunaga huruma ,wakati huo mkandarasi nae kafika akiwa amekokotwa kwenye baiskeli yake ,alimwona Aryan na kumwambia we kijana huwezi nikimbia kamwe hapa lazima ufe leo bado kauli yake ilibaki pale pale lazima Aryan afe.
Wakati huo Kudra alikimbia na kwenda chini ya lile korongo pale ambako alihisi mama yake kaangukia na kupasuka kichwa lakini cha ajabu alifika wala hakuona damu wala aina yeyote ya mtu ,Kudra aliita mama ,mama!!!!!!! Lakini hapakuwepo na mtu wa aina yeyote aliangalia chini ya lile korongo akaona nyayo tu za pundamilia zimepita eneo hilo la korongo.
Kudra ilibidi atoke kwenye lile korongo hadi nje kabisa alijaribu kumpigia mama yake simu,mama alipokea simu na kusema yupo salama tena yupo kwenye kikao ,cha kushangaza mama yake alikuwa yupo kwenye kikao tena mzima wa afya Kudra alizidi kuchanganyikiwa ,mbona nilimwona mama yangu kabisa kadondokea kwenye hili korongo sasa mbona simwoni ,Kudra hakuelewa ni mchezo gani anauchezewa alihisi yupo ndotoni lakini hakuwa amelala.
Alitoka hadi kwa akina Mussa alifika mahali pale mara kwa mbali aliwaona Joyce akiwa na Samairah wanatembea huku wakielekea mahali aliko Aryan pamoja na kundi la akina mkandarasi.
Aryan aliweza kumwona Samairah aliwaza huenda atamsaidia lakini aliwaza atawezaje kumsaidia angali yeye ni mwanamke? Aryan alikuwa bado hana tumaini la kupona ama kujiondoa mikononi mwa wabaya wake.
Aryan aliwaomba wa mwachie Gwae aondoke ili kama wataweza wamuue yeye ila Gwae abaki ,
Mara Gwae alimwona Samairah aliita antiii umerudi??? Antiii antiii ,Gwae alifurahi kumwona Samairah kwa mara nyingine.
Pale ndipo Mussa alipomuona Samairah akaanza kufanya masifa alimshika Aryan ili amsukumize korongoni kwa bahati mbaya kamba ya kiatu chake ilikuwa imetoka sasa aliikanyaga na mguu mwingine ile anafanya rafu amrushie Aryan kwenye korongo
Mussa alijikuta kayumba na kuporomoka kwenye korongo huku akipiga kelele za kuomba msaada jamani nakuuuu faaaa
Hapakuwa tena na msaada alienda mzima mzima korongoni.
Huku akina Kudra wakiwa wanashangaa baada ya Mussa kuteleza kwenye korongo ,wakiwa bado hawaja kaa sawa gafla kalizuka ka upepo chenye vumbi jingi kaliwazunguka mahali waliko akina Kudra ,mkandarasi na kikundi chake
Kibaiskeli alichokuwa nacho mkandarasi kalianza kuserereka taratibu na kufika kwenye korongo unaambiwa mkandarasi alitangulia na kuanza kubiringita kwenye lile korongo ,hakuwa na mikono wala miguu hivyo alikwenda kujibamiza kwenye aridhi unaambiwa shingo yote iliingia tumboni .
Huku utumbo wake ulipasuka pale pale mkandarasi alipoteza maisha huku pembeni Mussa nae kavunjika vunjika kila kiungo nae alipoteza maisha,,kale kaupepo kalichozuka gafla kaliisha wakati huo Gwae ashafika kwa Samairah na kumkumbatia,Aryan akimwangalia Samairah na kukosa nini afanye
Joy alimkimbilia Aryan na kumkumbatia huku kikundi cha mkandarasi wakishuka bondeni kwenye like korongo kwenda kuutoa mwili wa mkandarasi na Mussa.
Kudra alinusurika pale pale alimpigia magoti Aryan na kumwomba msamaha kwa yale yote mabaya aliyoyafanya na kumshukuru kumuokoa kwenye like korongo ,wakati Kudra akiomba msamaha huku rohoni akiwaza wewe mpuuzi kaka yangu Yusuph amefariki ambae ndio mkandarasi na Mussa rafiki yangu amefariki yote sababu yako sasa endapo utakubali kunikumbatia ili tusameheane itakuwa imekula kwako na ndio utakuwa mwisho wa uhai wako,,ni wazo alilowaza Kudra moyoni mwake.
Basi aliendelea kuomba msamaha huku akilia machozi ya kinafiki ,siku zote Aryan huwa ni mtu anaependa amani ,alimsogelea Kudra alimshika mkono na kumwambia yaishe nishakusame….
Kabla hajamalizia ni kosa kubwa mno alilo fanya ,kumpa Kudra mkono ,Kudra alimvutia kwenye korongo,Aryan aliserereka mzima mzima lakini kabla hajadumbukia alishangaa mkono wake umedakwa
Kucheki nani kaudaka mkono wake alikuwa ni mrembo Samaira akiwa amemkodolea macho ,Samairah alianza kuwaza ,wewe ndiye umenifanya nimerudi kwenye huu ulimwengu sasa hawa watu wanaokufanya ukose amani leo ndio mwisho wao.
Samairah alianza kumvuta Aryan taratibu huku akisaidiana na Joyce ,pale ndipo Kudra aliwaza kwa mara nyingine ya kumuua Aryab pale pale korongoni,nyie mnajifanya mnamsaidia ee sasa nawasukumiza wote Kudra aliwaza huku akionekana mwenye hasira na kulipiza kisasi.
Ile anapiga hatua akawasukumize alishangaa tumbo linamkamata huku anajisikia kizungu zungu kikali ,alijaribu kusimama alijikuta anayumba huyoooo aliporomokea kwenye korongo wakati huo Aryan ashatolewa na Samairah waliondoka eneo hilo upesi na kuanza kukimbia wakiwa wanne ,Arysn,Gwae Joyce na Samairah ,baada ya kufika mbali ,Aryan ilibidi amuulize Joyce ,
Vipi Joyce mbona umeungana na sisi? Wakati baba yako nae kafia kwenye korongo, Joyce alitabasamu na kuwaambia
Ni story ndefu mno ila kwa ufupi yule si baba yangu kabisaa
Baba yangu walishakufaga kwenye ujenzi wa gorofa moja maeneo ya mbezi kimara wakati huo Yusuph alikuwa mkandarasi ,wa hilo gorofa ,mama yangu alikuwa akiuza chakula kwenye lile gorofa alikuwa akiwapikia wajenzi na vibarua lakini cha ajabu Yusuph ambae ni mkandarasi alisababisha kifo cha
,mama yangu alikuwa akipika chakula chini na yeye akiwa juu alichukua tofali toka juu na kwenda kumpiga mama yangu kichwani mama yangu alifia hapo ,huku baba yangu alipigwa shoti ya umeme siku hiyo hio kwenye hilo gorofa ,
Mimi sikuwa na ndugu ndipo huyu mkandarasi alijitolea kunilea.
Aryan bana naomba tuishie hapo maana nikiendelea kuwapa story nitajikuta naanza kulia ,basi waliacha na kuondoka wote hadi maeneo ya mbezi mahali anakoishi Aryan ,njia nzima Aryan alikuwa akiwaza ina maana Samairah ni jini? Au wamemsingizia maana wanaona mzuri na kaumbika ,Aryan aliwaza na kujikuta akitabasamu ,na kusema yes Samairah ni kisura kiukweli hamna mfano ,japo nilisema sitopenda tena wanawake ila Samairah hata nikiambiwa ni vempare nitakuwa nae.
Wakati Aryan anayawaza hayo alikuwa ameshikilia mkono wa Samairah huku wakitembea taratibu ,alijikuta hisia za mapenzi zinaanza kumtembelea Aryan alishidwa kujizuia alimwangalia Samaira na kumwambia
Samairah wew ni nani?
Lile swali lilimfanya Samairah akose tena furaha na kuhofia akimwambia tu yeye ni jini Aryan hatakubali kuwa nae ,sasa Aryan kasimama kwenye njia katikati na kumuuliza Samairah wewe ni nani?
Samairah alimwangalia Aryan kwa huruma na kujisemea moyoni “yaani Aryan ungejua ninavyokupenda wala usingenitesa hivi nimekuja kwa ajili yako ila kama bado unaniuliza maswali hayo heri nirudi zangu tu nikae mbali na wewe”
Wakati Samairah anawaza Aryan alimshika mkono Samairah na kumvutia kwake ,hapo hapo Samairah yeye alikuwa anasikia raha mno akiangalia macho ya Aryan na kusema wewe mwanaume kwanini ulipendelewa uzuri namna hiii
Pale Samairah alianza kulegeza macho na kusahau kama kaulizwa swali na Aryan.
Gafla Aryan alivutwa mkono na Joyce ,”Joyce aliwaangalia Aryan na Samairah na kushangaa hivi ninyi mnapendana eee ,Mungu wangu ,ila kama Samairah unampenda Aryan mimi sina kinyongo na wewe kuanzia leo nitakuwa rafiki yako japo nampenda sana Aryan ila nitakuachia.
Wakiwa wamesimama njiani kandokando ya barabara ,kuna mtu akiwa kavalia mavazi meusi tiii alishuka kwenye gari akiwa ameongozana na vijana wawili wakiwa wamevalia suti nyeusi
Yule mzee alitoa miwani yake na kuuliza ndio hawa ? Mbona wanaonekana wadogo ,aliongea huku akitoa bastola mfukoni.
Kijana mmoja alidakia na kusema Mr Kizaa ndio hawa waliowaua watoto wako kwenye korongo.
Aryan kugeuka tu mlio wa risasi ulisikika tii tiii tii tiii zilipigwa risasi nne ,akina Aryan,Samairah ,Joyce na Gwae wote wakawa wameshalala chini ,Mr Kizza alisema hapo vipi kawakagueni kama bado wako hai na hata mkikuta wanahema wapigeni tena risasi zingine wafe pale pale haiwezekani waue watoto wangu Kudra na Yusufu nami nimewaua wabaya wenu mkakutane kuzimu pamoja .
Yule mzee Kiza baada ya kuwapiga risasi akina Aryan,aliondoka na kuingia kwenye gari kisha akaiangalia bastola yake na kusema ,wasalimieni kuzimu…
___________________________
Aryan kugeuka tu mlio wa risasi ulisikika tii tiii tii tiii zilipigwa risasi nne ,akina Aryan ,Samairah ,Joyce na Gwae wote wakawa wameshalala chini ,Mr Kizza alisema hapo vipi ,hebu kakagueni kama bado wako hai waongezeeni risasi na kuhakikisha wamekufa kisawa sawa ,aliongea kisha akakaa kwenye gari yake.
Yule mzee alikuwa anajiona vibaya mno aliangalia saa yake mkononi kisha akasema harakisheni nikazike wanangu ,wale vijana wake walienda kukagua kama Mr Kizza kafanya kazi yake ,
Kijana mmoja alimwangalia Kizza na kusema boss ndio maana umepewaga jina Kiiza au kisa wavaaga mavazi meusi kama giza nini ,wale vijana waliwakagua akina Aryan kama kweli waoivyopigwa risasi na Kizza wahakikishe kama wamekufa. Huku Kiza anawaza mambo yake ,Samaira aliinuka na kuwaangalia wale vijana ndani ya sekunde moja wale vijana walianza kucheia damu huku kila mmoja kashika kifua chake ,ndipo Mr Kizza alishuka kwenye gari na kwenda kuwatazama vijana wake aone wamekubwa na nini ki ukweli walikuwa wamepigwa risasi kifuani ,jambo lililomfanya Kiiza kuhamaki ,aligusa masikio yake na kusema mbona sijasikia mlio wa risasi hawa vijana wamefanyajwe? Kizza aligeuka kuwatazama akina Samairah ni kosa moja alilofanya,Samairah aliiangalia ile bastola yake kwa sekunde kisha akacheka ha ha ha.
Kiza aliangalia bastola yake huku kuonekana kuchanganyikiwa na kujisemea ina maana sijamlenga huyu bint? Kisha akamnyoshea bastola Samaira ,wakati huo Aryan ,Gwae na Joy wamedondoka chini wakiwa hawajitambui ,
Samairah alicheka na kutabasamu kila mara , Mr Kizza kafyatua risasi nyingine pale Samairah aliiangalia ile risasi upesi kisha akamtizama Mr Kiiza kwenye paji la uso.
Yaani Samaira alikuwa na uwezo wa ajabu akikuangalia mahali kama wataka kumfanyia ubaya basi ubaya unakurudia wewe mwenyewe.
Basi alivyo mtizama Mr Kizza kwa umakini ,kitendo cha Kiza kufyatua risasi ile risasi ilimgeukia mwenyewe na kutua kwenye paji la uso pale pale Kiza alidondoka kama gunia la mkaa chini huku damu nyingi zikiwa zinamtoka kwenye paji la uso.
Taratibu Mr Kiza alijinyoosha na kukata roho na kuwaacha akina Samairah wako salama kabisa wala hawakuguswa na risasi ya aina yeyote zile risasi ambazo Kiza aliwapiga ,hazikuwapiga akina Aryan bali Samairah kwa uwezo wake alizigandisha hewani ndipo wale vijana wa Kiza walivyoenda kuwakagua ,zile risasi aliziachia na kuwapiga vifuani hatimae kusababisha kucheua damu na kupelekea kufa pale pale.
Samairah aliwainua akina Aryan na Joy wakiwa hawaelewi kilichotokea walikuwa na kumbu kumbu kuna mtu alikuja na gari alishuka na kuwanyooshea bastola lakini kilichoendelea hawakikumbuki. Basi Samairah aliwaambia twendeni nyumbani walienda hadi kwa akina Aryan ,walipofika waliingia bafuni kila mmoja akaoga kisha Samairah alisema ana maongezi na akina Aryan pamoja na Joy.
Wakati huo mapolisi walifika eneo la tukio na kumchukua Mr Kizza akiwa tayari ashapoteza maisha na vijana wake walienda kuwapima hospitalini ili kubaiini muuaji lakini cha ajabu kila wakijaribu vipimo ,majibu yalitoka giza totoro hapakuwa na picha wala mtu alowaua kesi ikawa imeishia hapo .
Tukirudi kwa akina Aryan walivyomaliza kula kisha mama yake na Aryan alifurahi kumwona Samairah kurudi ,Samairah aliomba awaeleze nia yake ya kurudi tena na kuwa karibu na Aryan ,kwanza kabisa alimwambia Joyce ,kuanzia leo utaishi hapa kwa akina Aryan sisi tutakutunza utaishi utakavyo ki ukweli Joyce alifurahi maana hana wazazi zamani alikuwa akiishi kwa mkandarasi nae ashakufa.
Ndipo Samairah alilitoa lile bangili aliliweka mezani ,kisha akamwita Gwae na kuuliza umeliona hili bangili? Gwae alitabasamu na kufanya upengo wa magego mawili ya juu uonekana na kusema ndio aunt nimeiona,Samairah alishusha pumzi na kumuuliza Aryan hii bangili uliiokota wapi ,
Aryan alivuta kumbukumbu na kusema kuwa aliiokota baharini kipindi walipoenda baharini na baba yake kwa ajili ya kupata utajiri , Samairah alitabasamu na kueleza kuwa hii bangili inamilikiwa na majini ,ila nawaomba msiniogope ukweli mimi ni jini ila nusu mtu nusu jini ,tokea nilipozaliwa nilipewaga hii bangili kwa ajili kuwa malikia wa viumbe aina ya majini wekundu lakini ilikuja kutokea vita kubwa sana ya majini ndipo nilinyang’anywaga hii bangili ,siku ambayo watu walishuhudia mwezi ukimezwa na jua na ndio huwa siku ya watu kupata utajiri ukienda kwenye kingo za bahari unaweza okota madini ama vito vya dhahabu ,na vya thaman sana.
Lakini siku hio bahari ilikuwa tofauti iliweza kuwameza watu wote alinusurika Aryan ambae aliachwa na baba yake mbali na bahari ,ndipo kuna ndege wa blue anae tokea katika falme za majini weupe alipopita usawa alikokaa Aryan aliidondosha hii bangili na Aryan alifanikiwaga kuiokota hivyo hii bangili ndio utajiri wenyewe ndio maana siku mama yangu alipoiona hii bangili aliwanunulia hii nyumba na kusema kuwa mnatakiwa muishi pazuri kila kitu mnachotaka mtakipata ,pia mama Aryan pole kwa kupotelewa na mume wako ambae ni baba yake na Aryan .
Hii bangili huwa haipotei ndio maana siku ya kwanza mama aliponiona kwa marehemu Jesca ulinivalisha yote sababu hii bangili ni yangu,na mateso yote anayoyapitia Aryan ya yametokana na waganga walikuwa wanawaelekeza watu katika familia yenu mtu akitaka utajiri,walipewa sharti yeyote akifanikiwa kumuua Aryan lazima ataipata hii bangili na akisha imiliki anaeweza kuwa tajiri wa dunia.
Samairah aliwakumbatia wote kisha akaaga anarudi aliko toka maana anahofia kujitambulisha kuwa yeye ni jini ,lakini cha ajabu kila mmoja alimkumbatia na kumwambia hapana kurudi huko tunaomba uishi huku uishi na sisi.
Gwae alimwangalia na kumuuliza aunt nasikia majini wanaweza kupotea kama upepo ni kweli? Samairah alimwangalia Gwae na kumshika mashavu na kumwambia ndio tuna uwezo wa kupotea ,Gwae alimwambia huwezi aunt kama kweli wewe ni jini hebu potea nione maana mie nilikuona kama vile farasi na zile kwato zako
Samairah aliwaangalia wote na kuwauliza mnaniruhusu nipotee?
Mama Aryan alimwangalia mwanae kisha akamwangalia na Joy kisha wote walimwambia potea tuone.
Samairah alifumba macho sekunde akatoweka kila mmoja alishtuka baada ya dakika moja walisikia akitoka ndani ya chumba akiwa ameshikilia jagi la juice basi ilikuwa furaha kubwa ,walimzoea na wakawa wanaishi nae akitaka kupotea anapotea na akirudi anarudi wala hamna mtu anaeogopa.
Gwae akawa anapenda kukaa na Samairah alikuwa akiondoka tegeta na kwenda mbezi kwa ajili ya kumwona Samairah ,ndipo Samairah aliamua kununua nyumba mbili zikiwa zimefuatana tena za kisasa ndipo alimuhamisha na mama yake Abbas, walianza kuishi wote mbezi walikuwa marafiki toka zamani na mama Aryan. Maisha yalizidi kusonga mbele huku penzi la Aryan na Samairah likizidi kukua .
Samairah hakuishia hivyo alimfungulia duka kubwa mama Ashura la nguo yote sababu alijuwa rafiki na mama Abbas ,maisha yaliendelea shuleni Aryan ,na Joy ndio waliendelea kusoma ila ,Samairah hakurudi tena shule maana yeye alikuwa akisoma kwa ajili ya kumlinda Aryan .
Baada ya akina Jesca kufariki na Mussa pamoja na Kudra darasa lilibaki na vinara wa tatu nafasi ya kwanza alikuwa an a chukka Aryan yapili Abbas na tatu alikuwa Joyce, alifuatiwa na Nanaa pamoja na Lusi ,masomo yaliendelea walifanikiwa kufaulu kidato cha nne hatimae cha tano na cha sita,
Aryan aliamua kusomea kazi ya uandishi wa habari kutokana na kipaji chake, huku Samairah akiendelea kusimamia biashara mbali mbali jijini dar es salamu , hatimae mahusiano yao na Aryan yalizidi kunoga miezi kadhaa ilikatika hatimae miaka sasa Samairah alishika ujauzito wa Aryan.
Aryan aliweka juhudi zake za kuwa mwandishi wa habari hodari na hatimae aliajiriwa katika kituo cha Mwai tv na alikuwa repota aliyeaminika ,yote kutokana na kujituma kwake na bidii katika kazi zake.
Maisha yaliendelea familia ilikuwa ya furaha kila siku ,siri ili baki kuwa siri ,hamna mtu mwingine aliyejua kama Samairah ni jini tofauti na akina Arya ,mama ake ,Joyce na Gwae ,waliifunga siri ambayo ilidumu.
Hatimae Samairah alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume hakika ilikuwa furaha hasa kwa Aryan na Samairah bila kumsahau mama Aryan,pamoja na Joyce , Joyce aliishi maisha anayoyataka alibadilisha gari kila alitakalo ,hatimae alikuja kubadili dini na kuitwa Sabrinah ,
Kutokana na mfanano wa Aryan na Abbas, alivyomkosa Aryan alijikuta akidondokea mikononi mwa Abbas ,ila hakujutia kamwe penzi lake kumpa Abbas ,walipendana hatimae walifunga ndoa ,watu walisherekea sana.
Mtoto wa Samairah na Aryan walimpa jina Mukhusin ,hakika Samairah aliweza kumlea mwanae vizuri na kumtunza vyema .
MWISHO

