MKE WA DUNIA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU 16
Fadeck alimshika shavu lake na kuugulia maumivu.
“Itoshe Sasa Fedrick. Inamaana wa nje hawakutoshi mpaka utake kumbaka mdogo wangu. Wewe ni mwanaume wa aje lakini?”. Niliongea hayo kwa hasira. Sarah alikuwa kajibanza nyuma ya mgongo wangu anatetemeka Kwa uoga.
“Hivi unanichukuliaje Mamy?, mimi nafanania na wabakaji?”.
“Unataka kusemaje na nimeona. Bila Sarah kupiga makelele inamaana ulikuwa ujambaka. Wewe ni shetani Fedrick. Nakuchukia mno”. Niliongea hayo kwa hasira na kutoka chumbani Kwa Fedrick huku nikiwa nimemshika Sarah mkono.
Korodoni tulikutana na dada wa kazi hatukusemeshana tulimpita mie na Sarah tulielekea chumbani kwao.
“Pole mdogo wangu”. Nilimpa Sarah pole na Bado alikuwa analia.
“Unampa pole ya Nini?, hivi unamjua vizuri kweli mdogo wako?.
“Unataka kusemaje na wewe”.
“Hakuna kitu kama icho ni usanii tu anaoufanya mdogo wako”.
“Yaani unamtetea ni kwa kuwa anakulipa, unashindwa kuwa na utu na Mimi mwanamke mwenzio?” Sarah aliongea hayo huku akiwa analia.
“Wewe ni mshenzi wa tabia. Dada sio kwamba namtetea ila amini Fedrick hawezi kufanya ukatili huo. Nimeishi humu ndani takribani miaka 4 kama kunibaka basi angenibaka Mimi. Mmekuja haya mwaka hajafikisha eti atake kumbaka kwa kitu gani kwanza kipya alicho nacho”.
“Wewe ni mjinga heee!. Unaongea ujinga gani?. Kwaiyo huyu Hana sehemu za Siri mpaka uongee hivyo”.
“Anazo ila naludia tena Fedrick Hana tabia hiyo na kama anayo labda huko nje na sio ndani. Unakumbuka nilishawai kukwambia kuwa ameanza tabia ya kumfulia mpaka nguo za ndani. Hivi dada kusoma hujui na wewe hata picha huoni?. Matukio mangapi ya ovyo mdogo wako anayafanya Kwa Fedrick na unayaona. Na usichokijua. Kila baada ya nyie kuondoka Sarah Huwa anaingia chumbani kwa Fedrick kulala. Anafuataga nini muulize alafu Leo aje aseme baba Amarah anataka kumbaka nikubali?, noooo! Napinga wazi wazi hapo mdogo ako ameucheza mchezo”. Dada wa kazi aliongea hayo. Ni kama vile yaliniingia akilini. Nilimtazama Sarah aliinamisha kichwa chini”.
“Ongea vizuri na mdogo wako”. Hidaya aliyasema hayo na kutuacha mie na Sarah chumbani.
Nilimgeukia Sarah na kumuangalia macho ya mkazo. Sarah hakuwa na ujasiri wa kuniangalia.
“Niangalie Sarah, naamini macho Yako ndiyo yana ukweli kuliko machozi Yako”. Sarah alinitazama machoni tulitazamana Kwa sekunde kadhaa alishindwa kuendelea kuniangalia. Aliinamisha kichwa chake chini.
“Sarah jamani!”. Nilijikuta nimekuwa mdogo gafla baada ya kubaini kuwa Sarah alimsingizia Fedrick.
“Nisamehe dada, nampenda sana Fedrick jamani”.
“Ndo umsingizie mwenzio kuwa ni mbakaji?, mbona umekuwa mkatili kiasi hiki. Hapana kwakweli itoshe Sarah, kesho nakusafurisha kwa mama Yako usije leta matatizo zaidi”.
“Dada usifanye hivyo, nakuapia nimebadilika na Wala simtaki Tena Fedrick. Nitakuwa msichana mzuri na mtulivu. Tafadhali dada usiniludishe mkoani”. Sarah aliyasema hayo huku akiwa analia.
Sikumjibu kitu. Nilitoka chumbani na Moja Kwa moja nilielekea chumbani kwa Fedrick kwa lengo la kumuomba msamaha. Niligonga mlango ila sikujibiwa. Nilinyonga kitasa mlangonulifungua. Niliingia ndani sikumkuta Fedrick. Nilijaribu kuita kuhisi lbda atakuwa bafuni ila sikujibiwa. Ukimya ulitawala chumbani humo. Nilitoka chumbani na kwenda sebleni Moja Kwa moja huko nilimkuta Hidaya na watoto wanakula.
“Baba Amarah yupo wapi?”. Nilimuuliza Hidaya.
“Naona ametoka na gari sijui ameenda wapi. Kuna tatizo?”.
“Hapana. Maliza kula tuongee”.
“Sawa”. Waliendelea kula mie nilienda kukaa sebleni na nilikuwa mbali kimawazo.
Baada ya kumaliza kula waliwapeleka watoto chumbani kulala na kuludi Sebleni kuitikisa wito wangu.
“Samahani kwanza kama nilikutamkia maneno mabaya”. Nilimwambia Hidaya.
“Hapana usijali dada”.
“Namludisha Sarah mkoani kesho”.
“Kwanini?”.
“Siwezi kuendelea kukaa nae, tabia zake zimenishinda”.
“Hata hivyo itakuwa vizuri. Mdogo wako ni ni WA ovyo sana”.
“Naomba kujua maisha ya Fedrick tangu umfahamu?”.
“Nitamzungumzia ninavyomuelewa Mimi, Dada kwanza Fedrick ni mpole sana na huwa si muongeaji sana. Hawezi kujieleza. Nilikuwa naona hata akikosea mama yake akiwa anamsema yeye ataomba tu msamaha basi. Fedrick ni mtu poa sana na ana huruma mno. Ni mcheshi ila si muongeaji sana, ana heshima sana. Ni hayo tu dada”. Hidaya aliyasema hayo kuhusu Fedrick.
“Sawa. Ila nimekosea, najisikia vibaya na Wala sitamani kuendelea kuwepo humu ndani”.
“Unataka kuondoka na wewe?”.
“Yeah”.
“Vipi kuhusu Amarah?”.
“Sielewi nifanyaje”.
“Baki kwaajili yake. Ukiondoka atasumbua sana na bibi yake hayupo. Alafu si ulimuahidi bibi Amarah kubaki najukuu wake. Sasa kwanini unataka kuondoka. Naomba ubaki kwaajili ya mtoto”.
“Acha tuone itakavyokuwa”.
“Sawa. Mie naenda kulala”. Hidaya alielekea chumbani kwake. Huko alimkuta Sarah amekaa kitandani yupo mbali kimawazo”.
“Punguza umbea utasutwa”. Sarah alianza kumsema mwenzio”.
“Jiheshimu uheshimiwa na ukiendelea na huo mdomo wako nitakupoga nakwambia”. Hidaya aliyasema hayo kwa paniki Sarah aliogopa.
Mie nilikaa pale sebleni kumsubilia Fedrick. Majira ya saa tano kasoro usiku simu yangu ilianza kuita. Mpigaji alikuwa ni Bibi Amarah.
“Kuna nini kinaendelea huko?”. Bibi Amarah aliniuliza baada ya salamu.
“Hakuna mama”.
“Unanificha na mwenzio yupo club muda huu. Fedrick kanipigia muda si mrefu. Anaongea kilevi anaonekana amekunywa. Anasema yeye ni mbakaji, ni kweli Fredrick amembaka Sarah?”. Mama aliniuliza swali.
“Hapana mama”.
“Kuwa makini . Mwanangu namjua vizuri hawezi kufanya kitu kama icho”.
“Nimekuelewa mama na mnisamehe mimi”. Nilimaliza kuongea na bibi Amara. Nilishusha pumzi, majira ya saa nane usiku nilisikia honi ya gari nje ya geti, nilijua ni Fedrick. Baada ya gari kuingia ndani ya geti muda mchache mlango uligongwa. Nilienda kufungua.
Fedrick alikuwa amelewa haswaaa. Nilimshika mkono ili nisaidie kutembea ila akilataaa.
“Unataka na wewe nikubake?”. Fedrick aliniuliza ….
SEHEMU 17
Fedrick aliniuliza swali nilibaki nimetoa macho.
“Niache tu mimi sio mbakaji”. Nilimuachia Fedrick na kumtazama tu anavyotembea kwa taabu maana alikuwa anapepeshuka sana. Alianza kupandisha ngazi kwa tabu nilikuwa nyuma yake namfuata. Alijikwaa akataka kuanguka ila niliwai kumdaka. Safari hii alikubali nimkokote mpaka chumbani kwake.
Nilimlaza vizuri kitandani kwake na baada ya hapo nilitaka kutoka ila aliushika mkono wangu.
“Usiniache baki na mimi tafadhali”. Fedrick aliongea hayo huku akiwa amefumba macho. Nilikaa kando yake na yeye aliendelea kuushikilia mkono wangu. Siku hiyo ndipo nilipata nafasi nzuri ya kumuangalia Fedrick. Bhana weee. Fedrick ni HB la kwenda ila nisiseme sana msije niona Malaya 😄.
“Nilijikuta napitiwa na usingizi na Mimi na kudondokea kifuani kwake. Wenyewe hatuna hili Wala lile. Kwa uchovu wa kuchelewa kulala na mwenzangu kwa uchovu wa pombe tulijikuta tunalala muda mrefu sana.
Sauti za watoto ndiyo zilitukurupua kwenye usingizi mzito. Wa kwanza kuamka alikuwa Fedrick alishangaa baada ya kunikuta nimelala kitandani kwake Tena juu ya kifua chake. Nilipogumbua macho na kunikuta nimelala chumbani kwa Fedrick Tena juu ya kifua chake. Niliinuka Fanya na kusimama. Watoto walikuwa wanaruka ruka tu Kwa furaha baada ya kumuona tumelala wote.
Walimkimbilia Fedrick pale kitandani na kumbusu shavuni. Mie nilitoka mule chumbani Kwa speed. Nilienda chumbani kwangu huko niliingia bafuni kuoga haraka ili niwai kazini. Baada ya kumaliza kujiandaa nilitoka chumbani ili niende kazini.
Nilikutana na Fedrick korodoni akiwa na watoto.
“Unaenda kazini?”.
“Ndiyo”.
“Ni sawa ila bado unaamini kuwa mimi ni mbaya?”.
“Hapana na pia nisamehe bule kwa kilichotokea j@ana”.
“Ni sawa. Vipi kuhusu kufanya kazi kwenye kampuni yangu. Upo tayari?”. Nilifikilia kwa muda kidogo na kumjibu.
“Ndiyo”.
“Sawa”.
Niliondoka kuelekea kazini, mpango wa kumuondoa Sarah kumludisha kwao ulikuwa pale pale. Nilifika kazini nilikuwa nimechelewa sana. Nilikuta wafanya kazi wenzangu wananisubilia nje ya duka. Funguo za dukani nilikuwa naondoka nazo mimi.
Nilifungua duka na baada ya hapo nilimpigia simu madame Anna. Nilimwambia aje nimkabidhi funguo na tupige mahesabu sababu naacha kazi.
Aliyashangaa maamuzi yangu, aliniuliza kama Kuna mahali amenikosea nilimwambia hapana.
“Kwanini Sasa unataka kuacha kazi?”.
“Samahani madame. Nimepata mchumba na mipango ya ndoa imeanza kwaiyo natakiwa niwe mtulivu kwa muda”. Sababu yangu haikuwa na mashiko ila madame alinielewa maana hakuwa na jinsi.
Saa kumi jioni Madame Anna pamoja na Jerry walikuja dukani wakiwa wameongozana. Akili za kuambiwa changanya na zako. Nakumbuka Kuna simu Fedrick aliniambia kuwa Jerry ni boss wangu. Hapo ndipo niliamini Sasa.
Madame Anna aliniita pembeni ili tuzungumze.
“Ni kweli umechumbiwa Mamy?”.
“Ndiyo”. Alishusha pumzi na kuinamisha kichwa chake chini. Kimya kilipita Kwa sekunde kadhaaa Madame aliongea.
“Ni sawa nakutakia Kila la heri mwanangu. Niliupenda sana uchapakazi wako, uaminifu wako pia. Mamy sina budi kukuluhusu uende maana sina kubali Cha kukunga’ang’ania”. Madame aliongea kwa unyonge sana.
“Nashukuru pia madame kwa kipindi chote ulicho niamini. Wewe ndiye umeyabadilisha maisha yangu. MUNGU akubariki mno mnoo”.
“Hivi ni kweli unaacha kazi kama alivyoniambia mama?”. Jerry aliniuliza baada ya kutusogelea.
“Ni kweli Jerry”.
“Sababu ni nini hasa”. Swali lake lilikuwa gumu kumjibu, niliweza kumuongopea madame ila nilishindwa kumuongopea Jerry. Nilinyamaza kimya.
“Amechumbiwa na siku za usoni anaolewa”. Madame alimjibu Jerry.
“Ni kweli Mamy?”. Jerry aliniuliza kwa sauti ya unyonge. Niliitikia kwa kichwa ndiyo. Jerry aliniangalia dakika kadhaa bila kusema chochote.
“Kama nimekukosea naomba unisamehe, siamini haya uyaaemayo. Huenda mimi ndiyo sababu ya wewe kutaka kuondoka. Nisamehe Mamy”.
“Hapana Jerry hujanikosea. Huo ndo ukweli”. Jerry alitoka nje. Madame Anna alizungumza.
“Mwanangu alitokea kukupenda ila ameshachelewa. Hatuwezi kulazimisha zaidi ya kukutakia Heri huko uendapo”. Madame aliongea hayo kwa sauti tulivu.
Kumbe bwana Jerry nae alishazama kwangu na mpaka mama yake alikuwa anajua hilo. Sikujua kabda kama madame Anna na Jerry ni mtu na mwanae. Pia nilijiuliza ananipenda kivipi na ikiwa yeye ni mume wa mtu?”. Sikuwa na majibu ya maswali yangu na niliona Haina haja ya kuuliza ikiwa ukweli nishaambiwa.
Tulipiga mahesabu na siku, Kila kitu kilienda sawa. Madame alinipa million Moja kama Asante na hongera kwakuwa naenda kuwa mke wa mtu siku za usoni.
Nilimshukuru na Baada ya hapo nilimkabidhi funguo za duka lake, niliangana na wafanyakazi wenzangu walisikitika ila hawakuwa na namna .Mpaka muda naondoka sikumuona Tena Jerry.
Siku hiyo nililudi nyumbani mapema. Saa kumi jioni nilifika nyumbani. Nilimkuta Hidaya na watoto wamekaa sebleni wanaangalia TV.
” Mmeshindaje?”. Nilimuuliza Hidaya baada ya kukaa kwenye sofa na watoto wangu.
“Hapa hata sio kwema”.
“Kuna nini Tena, au Sarah ameshafanya yake?”.
“Ni bola angefanya yake ila hayupo kabisa. Sarah ametoroka, wakati alipokuwa Anatoka mie sikumuona ila nimeikuta hii karatasi yenye ujumbe chumbani kwetu”. Hidaya alisema hayo na kunipa Ile karatasi…….
SEHEMU 18
Nilichukua Ile karatasi niliifungua ujumbe na kusoma. Ujumbe ulikuwa umeandikwa hivi.
“Dada kwanza Asante kwa malezi Yako mazuri. Wewe sio mbaya umeishi na mimi vizuri kipindi chote. Dada mamy nimeamua kutoroka kwakuwa sipo tayari kuludi kijijini. Naenda kujitafutia maisha yangu. Nampenda sana Fedrick ila naamini hawezi kunikubali Tena kwasababu nimemsingizia alitaka kunibaka. Nakuomba dada yangu usikubali kuolewa na Fedrick kwasababu utakuwa umenikatili mimi mdogo wako. Upo siku tataonana tena. Nimechukua pesa zako laki tano za kuanzia maisha”.
Nilimaliza kusoma ujumbe wa Sarah. Nilishusha pumzi. Nilijikuta mwili unakosa nguvu kabisa. Nilikaa kimya muda mrefu.
“Itakuwa ameenda wapi. Mbona anataka kuniletea matatizo.nitawaeleza Nini nyumbani wanielewe hasa mama yake mzazi”. Nilijiuliza hayo mwenyewe.
“Kwaiyo tunafanyaje?”, Hidaya aliniuliza.
“Sielewi. Sarah Bado mdogo sana na hajalielewa Bado jini la dar. Nahofia usalama wake na sielewi nitampata vipi. Dar ni kubwa mno jamani”.
“Tusubilie baba Amarah aludi”.
“Naanzaje kumwambia habari za Sara tena kwa aliyomsingizia sidhani kama ana hamu nae hata theluthi”.
Nilimpigia simu mama yangu ili kumuuliza kama Sarah yupo nyumbani. Ila aliniambia hayupo.
“Kuna nini kwani?”.mama aliniuliza. Ilikuwa ngumu kumueleza mama kwasababu hakuwa anajua kama ninaishi kwa baba Amarah japo nilimwambia kuhusu kudaiwa pesa baada ya kuharibu simu kipindi Cha nyuma.
“Nakuja nyumbani tuzungumze si upo mama?”.
“Ndiyo ndipo”. Muda huo niliinuka kwenda nyumbani kwa mama. Niliwabeba na watoto maana walikuwa wananililia.
Nilifika nyumbani nilipokelewa vizuri na mama . Baada ya salamu ndipo nilieleza mama uongo na kweli.
Nilimwambia tu nilikuwa naishi Kwa boss wangu kutokana na watoto wetu kutaka wawe na ukaribu sana. Mama alimtazama mjukuu wake na Amarah aliona hilo. Ulikuwa ukiwatazama tu unaelewa kuwa hao watoto wanapendana sana.
“Boss wako Hana mke?”.
“Hana mama na ndo maana nimekwambia Sarah alikuwa anamtawala sana mpaka kumsingizia kumbaka sio mchezo”.
“Duuuh. Sasa tunafanyaje mwanangu, mtoto wa watu hiyo nitamueleza nini mama yake”.
“Nadhani tusikilizie kwanza wiki moja kama Bado atakuwa kimya hatutakuwa na budi kumuambia ukweli tu”.
“Aya sawa”. Tulipokuwa tunaendelea kuongea na mama simu yangu iliita. Ni Fedrick ndiye alikuwa napiga.
“Upo wapi usiku huu na watoto?”. Fedrick aliniuliza.
“Nipo nyumbani, nimekuja kuongea na mama, si Hidaya amekwambia kuwa Sarah ametoroka?”.
“Ndiyo, kwenu ni wapi niwafuate?”. Nilimuelekeza Fedrick. Nilimwambia mama kuwa mama Amarah anakuja kutufuata alisema sio mbaya hata yeye akamfahamu maana si vyema kuishi na mtu asiyefahamika kwenu kutokana na dunia ya Sasa vimbweka huwa haviishi.
Baada ya lisaa limoja Fedrick alifika mtaa wa nyumbani kwetu. Nilimfuata kumpokea. Basi majirani macho kodo kama mnavyojua uswahilini kwa umbea.
Tulifika nyumbani mama alimkaribisha kwa heshima mgeni. Yaani alivyokuwa anamnyenyekea Sasa huyo Fedrick mpaka niliboeka ila si mnajua wamama wa Africa. Baada ya salamu mama alimuwia radhi Fedrick kwa aliyoyafanya Sarah. Maana mambo aliyokuwa anayafanya yalikuwa ni kituvunjia heshima familia nzima.
Fedrick hakuwa na baya mwenyewe na alikubali kushilikiana nasi kumtafuta Sarah. Saa tatu usiku tulimuaga mama. Mama yangu alivyo na kiherehere alitupa eti baraka zote za kuishi kwa upendo,maelewano na masikilizano kama vile ndo tumeona Sasa tunaenda kuishi wote kumbe hata mahusiano hatuna. Ila mama zetu kwa kututakia mema MUNGU awatunze kwakweli.
Tuliludi nyumbani kwakuwa nilikuwa nimechoka sana nilihitaji kupumzika. Niliingia chumbani na watoto kulala. Kesho asubuhi niliamka mapema. Akili yangu ilifikilia nitaanzia wapi kumpata Sarah. Saa mbili asubuhi Fedrick alikuwa tayari ameshajiandaa kwaajili ya kwenda kazini. Alikuja kunigongea chumbani nilitoka alishangaa baada ya kuniona nipo nipo tu hata kujiandaa sijajiandaa.
“Nilijua tutaongozana wote Leo”.
“Hapana siwezi kwenda Leo. Sijisikii vizuri”.
“Nini shida?”
“Akili yangu Bado haijtulia”.
“Sawa. Utakapokuwa tayari utaniambia but nilikuwa nahitaji secretary wa haraka kwakuwa aliyekuwepo nishamuondoa”.
“Lakini mimi sijui chochote kuhusu u secretary”.
“Najua kama hujui ndo maana nilikwambia niachie mie”.
“Basi sawa kesho tunaweza kuongozana”.
“Okay! Siku njema”. Niliona mabadiliko kidogo kwa Fedrick, mwanzo nilimuona Kijana mwenye dharau na kiburi sana, kunisikia na kuniona yeye ni bola kuliko mwengine.
Majira ya mchana mama alinipigia simu na kunipa habari kuhusu Sarah.
“Mama yake amenipigia simu ameniambia amepanga yupo huko mbagala na nadhani ni ile pesa aliyokuibia kwaiyo ondoa shaka familia yake wanajua kuwa Kwa Sasa hayupo mikononi mwako”. Mama aliniambia hayo . Nilishusha pumzi na amani ndani ya moyo wangu ililejea. Sikujali kuhusu pesa alizoniibia nilichotaka kujua usalama wake tu.
Niliendelea kuongea na mama ndipo alinigusia kuhusu Fedrick.
“Anaonekana ni Kijana mzuri sana”.
“Mama bhana, usipagawe na hizo Hela alizokupa Jana”.
“Ukiachana na Hela huyu kijana natamani awe mkwe wangu na naamini inawezekana. Kwanza tuachane na hayo. Basi Jana watu sijui waliwaona wewe na mwenzio. Leo nimesikia maneno huko mtaani eti Mamy amepatwa bwana la maana MUNGU hamtupi mja wake. Ukisema Cha nini mwenzio anasema atakipata lini.
“Huo mtaa kwa umbea upewe tuzo loooh!”.
“Hahahaaa! Ndo umekukuza unakujua mpaka ukucha”. Tulipiga umbea mie na mama yangu. Aliniambia habari za abduli amemzalisha mwanamke mwengine na Sasa anaishi nae kwao.
Ni muda mrefu ulipita sina mawasiliano nae kabisa, hajui mtoto yupoje. Hajui kutoa matumizi Wala chochote kuhusu mtoto. Niliamua kumpotezea na kublock namba yake baada ya kuona Hana msaada wowote kwangu na kilichomuuma alipotaka tuludiane nilimkatalia basi ikawa ndo sababu ya kumsusa mtoto na mimi Wala sikujali.
Kesho Yale niliongozana na Fedrick kazini. Ilikuwa ndo mala ya kwanza kufika kwenye kampuni. Nilikuwa nimevalia suruali nyeusi na shati jeupe mikono mirefu pamoja na viatu virefu vyeusi. Pochi yangu simple, nywele nilibana tu kawaida.
Baada ya kuingia ndani ya kampuni nikiwa sambamba na Fedrick. Wafanyakazi walikuwa wanampa salamu ya heshima. Yaani wakubwa kwa wadogo walimsalimia Fedrick kwa heshima, aisee tutafute pesa.
Niliingia nae mpaka ofisini kwake. Aliniambia nikae kwenye sofa kwanza. Nilitii amri. Nilikaa kwenye Moja ya sofa kubwa lililokuwepo humo ofisini. Nikisubilia hatua inayofuata……
SEHEMU 19
Baada ya nusu saa mlango uligongwa. Fredrick alimluhusu mtu yule aingia. Aliingia mdada mmoja mrembo sana. Walisalimiana na baada ya hapo alimpa kazi ya kunifundisha mambo yanayohusiana na u secretary. Tuliongozana na yule mdada niliuemfahamu kwa jina la safina. Tuliingia kwenye chumba kimoja Cha ofisi kilicho na dilisha kubwa la wazi lenye kutazamia nje.
“Hapa ndiyo itakuwa sehemu Yako ya kazi”.
“Anhaaa! Sawa”. Siku hiyo hiyo nilianza kazi. Nilijitahidi kufanya kazi huku safina akinifundisha mambo mbali mbali. Mambo yalienda vizuri kabisa na maada ya miezi mitatu nilikuwa mzoefu sasa. Upande wa nyumbani watoto tuliwapeleka shule walikuwa wanaenda shule asubuhi kuludi jioni.
Kwenye mshahara Fedrick alikuwa ananilipa vizuri tyu kama vile alivyoniahidi awali. Kipindi icho ndipo nilijua Fedrick ni mwanaume wa aina gani.
Kwanza alikuwa mpole, mcheshi na mtu ambaye yupo makini mno. Chuki baina yetu zilizaa upendo wa urafiki sio wa mapenzi. Asubuhi tulikuwa tunaenda wote kazini na jioni bala nyingi tulikuwa tunaludi wote. Minong’ono ilianza kwa baadhi ya wafanyakazi pale ofisini. Wengine walijua kuwa mimi na Fedrick ni wapenzi. Baadhi ya wanawake walinichukia kwakuwa walikuwa washaliwa kwaiyo walinionea wivu mimi pasipo kujua ukweli mimi na Fedrick tupo vipi.
Siku Moja nilipokuwa kazini naendelea na majukumu yangu ya kazi alikuja mdada mmoja mzuri hakupita mapokezi yaani hakupita ofisini kwangu ili nimpe ruhusu ya kuonana na boss. Alipitiliza Moja Kwa moja ofisini. Nilitoka ofisini kwangu haraka ili kwenda kumtoa yule dada kwenye ofisi ya boss kwasababu hajafuta taratibu.
Nilipoingia ofisini nilichokiona ilibidi niludi tu nyuma nyuma nitoke nje. Fedrick na yule dada walikuwa wanakulana denda. Fedrick baada ya kuniona mimi alitumia nguvu kujinasua mikononi mwa yule dada ila yule dada alikuwa ameng’ang’ania kisawa sawa. Ilibidi atumie nguvu zaidi, alimsukuma yule mdada alianguka chini.
Tayari nilikuwa nishafungua mlango ila kabda ya kutoka Fedrick aliniita.
“Mamy sorry”. Sikumjibu nilitoka ofisini kwake na kuludi ofisini kwangu. Nilishangaa kwanini moyo wangu unauma kiasi icho mpaka kushindwa kuhimili machozi yasinitoke maana tayari nilikuwa nalia. Muda mchache yule dada alitoka akiwa amechukia balaa alisimama nje ya dilisha aliniangalia Kwa hasira. Alinipandisha na kunishusha na baada ya hapo aliondoka.
Baada ya yule dada kuondoka Fedrick alitoka ofisini kwake na kuja ofisini kwangu.
“Nikusaidie nini boss?”. Nilimuuliza Fedrick.
“Nifuate ofisini kwangu”. Aliyasema hayo na kutoka. Nilitii amri ya boss nilimfuata ofisini kwake nilimkuta amejiinamia kwenye meza.
“Boss nipo hapa”. Aliinuka akasimama na kuniomba tukae kwenye sofa.
“Nisamehe Mamy kilichotokea”.
“Mbona hujanikosea. Hayo ni maisha Yako lakini”.
“Najua ni maisha yangu ila si ya Sasa ni ya nyuma. Mamy tangu nifahamiane na wewe nimekuwa mtu mpya hivi unalijua hilo”.
“Unamaanisha nini kusema hivyo”.
“Utanielewa tu ila tambua ukweli kuwa mimi nilikuwa muhuni hapo nyuma na sio Sasa. Huyu mwanamke tulishaachama muda mrefu tu baada ya kukutana na wewe ila nashangaa Leo amekuja ofisini sijui anashida Gani”.
“Anhaa ni sawa. Ni muda wa kazi huu boss”.
“Najua ila tafadhali naomba usilie tena na Wala usinichukulie vibaya sina baya sikuizi”. Nilishangaa kumbe aliniona nilipokuwa nalia. Baada ya mimi kutoka ofisini Fedrick alitoka alinishuhudia nalia ndipo aliludi Tena ofisini kwake na kumtimua yule dada na baada ya hapo alinifuata ofisini kwangu na kuniambia nimfuate ofisini kwake.
“Naweza kwenda?”.
“Yeah”. Nilitoka ofisini Kwa Fedrick.
Jioni muda wa kazi ulipoisha niliondoka pasipo kumuaga Fedrick. Kawaida lazima nimuage kabda sijaondoka na kama Hana kazi basi tutaongozana kuludi wote.
Siku hiyo nilimpia nyumbani kwa mama kumsalimia, kipindi icho mama alikuwa anafanya kazi ya kuuza duka la chakula nililomfungulia mimi.
“Mwanangu huyo?”.
“Mama yangu Mimi”. Nilifika dukani kwake. Alinikaribisha kwa bashasha.
“Unazidi kuwa mrembo”.
“Anhaaaa! Mama taratibu”.
“Unafikilia nakunafkia. Ni kweli unazidi kuwa mrembo si haba baba mjengo anakuhudumia vizuri”.
“Awapi mama. Napambana mwenyewe tu. Alafu mama ujue Mimi na Fedrick tunaheshimiana sana. Hatuna mahusiano kabisa”.
“Sitaki kuamini ila hata kama kweli hamna mahusiano jitahidi awe wako. Usikae kizembe mwanangu bahati haiji mala mbili. Kwani wewe huoni viashiria vyovyote Ishara ya kuwa anakupenda?”. Mama aliniuliza.
“Naona ila bado sina Imani nae. Ana tabia mbaya sana, wanawake kama wote”.
“Mwanangu wanaume wa sikuizi ndo walivyo. Waswahili wanasema chapeke Yako labda kaburi. Kikubwa heshima ndani ipo. Nasema hivyo sina maana kwamba ndo umkubali kila mwanaume kwakuwa hapana ila bola wali nyama vitani kwa maisha ya sasa”. Nilimuelewa mama anamaanisha Nini.
Mama aliongea sana na maneno yake yaliniingia akilini. Niliondoka na kuludi nyumbani, Fedrick alikuwa hajaludi mpaka muda huo.
Niliwasimamia watoto kufanya homework na baada ya hapo tulikula chakula Cha usiku na kuwapeleka watoto chumbani kwao kulala. Kipindi hicho nilikuwa silali nao tena.
Niliingia chumbani kwangu kulala. Kabda ya kulala niliingia bafuni kuoga. Baada ya muda nilitoka bafuni nilianza kujifuta maji mwilini na tauro. Lahaula mlango wa chumba changu ulifunguliwa aliingia Fedrick alinikuta uchi wa mnyama nilikuwa nimekaa kwenye dress table napaka losheni. Nilitoa macho na yeye alipigwa na bumbuwazi sijui akili yake ilienda wapi 😄😄😄. Kuinuka pale kwenye sturi ya dress table ilikuwa noma maana Fedrick angeuona mpaka uchi wangu weee kuweza😄😄😄🤣.
SEHEMU 20
Bwana Fredrick aliendelea kutoa macho kuutalii mwili wangu. Mie muda huo nilikuwa nimejikumbatia kufucha maziwa yangu, sehemu nyengine za mwili zote zilikuwa wazi.
Fedrick aliliokota lile tauro lililokuwepo chini hatua tatu kutoka nilipo. Alinisogelea kwa hatua za karibu mpaka kunifikia nilipokaa. Alinipa lile tauro huku akiwa anatazama kwa macho ya hisia sana, mashine yake hapo ilishasimama. Alizunguka nyuma ya mgongo wangu. Hata sijui ilikuaje nilishtuka nashikwa chuchu zangu. Aliinamisha kichwa chake usawa wa sikio langu na kuninong’oneza kwa sauti nzito iliyojaa hisia.
“Nakupenda sana Mamy”. Nyie shetani alikuwa kazini. Nilipatwa msisimko wa ajabu basi kilichotokea hapo ni vilio tu vya kimahaba. Jamani jamani huyu Fedrick ni moto wa kuotelea mbali. Nililia vilio vyote mpaka vya wanyama 😄😄😄🙌.
Mpaka tunamaliza mchezo mie nipo hoi taabani ukisikia, mtoto ka utaka ndo mimi Sasa. Basi baada ya kumaliza mchezo nilianza kusikia aibu sasa. Hata kumtazama Fedrick sikuweza. Fedrick alinilaza kifuani kwake. Na kuongea maneno kibao ya mahaba. Hakuishia hapo pia aliniomba msamaha kwa makosa yote aliyowai kunifanyia.
Siku hiyo ikawa ni siku mpya kwetu. Tuliingia kwenye mahusiano lasmi. Usiku wetu ulikuwa ni usiku wa huba hubani asikwambie mtu. Hakuna mahusiano yenye raka kama Yale ya Kila mmoja kumuonyesha mwenzake kuwa anamuhitaji sana, anampenda sana.
Kesho yake wote hatukwenda kazini kutokana na uchovu wa sita kwa sita. Watoto walienda shule. Saa tatu asubuhi niliamshwa na Fedrick.
“Amka mamaa umelala Sasa”.
“Nimechoka mno”.
“Najua mpenzi wangu. Ila amka tukaoge tuondoe uchovu kidogo”. Niliamka tuliingia wote bafuni kuoga. Yaani mahaba ya Fedrick ni ya tofauti na wanaume wote niliopita nao huko nyuma.
Huko bafuni aliniogesha huku akiwa ananichombeza tulijikuta tunapeana Tena cha bafuni. Tulitoka huko tuliwa wepesi nakwambia mabusu kama yote 😘.
Baada ya kutoka bafuni Fedrick alielekea chumbani kwake kuvaa na Mimi aliniacha navaa nguo. Tulikutana breakfast. Wee tulishindwa kuficha hisia zetu kabisa siku hiyo hiyo Hidaya alijua kutokana na mapicha picha aliyokuwa anayaona.
Baada ya kumaliza kunywa chai Fedrick aliniambia anataka tutoke. Tulijiandaa hao tukaondoka. Safari yetu iliishia kwenye hotel nzuri ya hadhi. Ilikuwa ishafika saa 7 mchana. Tuliagiza msosi tulikula na kunywa huku tulipiga story za hapa na pale.
Baada ya kumaliza kula Fedrick aliniambia Kuna jambo anataka kuniambia.
“Mamy naomba nikuombe kitu”.
“Karibu”.
“Naomba nikuoe?”.
“Eeeeeh!, unasemaa!”.
“Nataka nikuoe kwakuwa umenitosheleza kwa Kila kitu mama”. Sikuwai kunipa asilimia zote kuwa nitakuja kuwa mke wa Fedrick. Fredrick ni Kijana mzuri hakuna mwanamke asiyetamani kuwa nae.
“Kwanini Mimi Fedrick”. Nilimuuliza Fedrick aliniangalia na kuachia tabasamu.
“Kitu Cha kwanza kilichonivutia kwako ni namna unavyompenda kwangu. Nilikutendea mambo mengi ya ajabu, ulinichukia sana ila hukuwai kumchukia mwanangu hata siku Moja kwa makosa yangu”.
“Kitu Cha kipi una msimamo sana na Wala huteteleshwi na jambo lolote pia ni msikivu, unaheshima na pia ni mtulivu. Ni mpambanaji, itokee hata kesho nimetangulia mbele ya haki najua wanangu wataishi vizuri hata kama sio Leo ila unaweza kuitengeneza kesho Yao ikawa nzuri zaidi.
“Cha mwisho kabisa. Wewe ni mzuri, yaani ni mzuri kweli kweli. Sio wa sura na umbo Bali mpaka tabia. Mamy umenitosha mama. Amini moyo wangu umekudondokea wewe. Wewe ndiye umenibadilisha tangu nianze kuishi na wewe sikutaka uyaone mabaya yangu. Kipindi icho nipo nilibadilika mpaka Leo hii kuachana kabisa na habari za wakawake”.
Fedrick aliongea mengi sana na nilimuelewa, sikuwa na Cha kujibalaguza. Nilikubali kwa moyo mkunyufu kanioe. (Bola wali nyama vitani). Niliona bola kuvumilia mapungufu tajiri na Mali zake kuliko kukutana na masikini jeuri kama Abduli.
Haikuwa Siri tena kuwa Mimi na Fedrick ni wapenzi kazini wafanyakazi walijua. Fedrick alimwambia ma yake na familia yake kwa ujumla. Ni kitu Cha muda mrefu alichokuwa anakisubilia Bibi Amarah hatiyame hayawi hayawi yamekuwa. Mama Fedrick alifurahi mno kwani tangu siku ya kwanza aliponiona matamanio yake niwe mkwe wangu.
“Fedrick alinichumbia lasmi na kunitolea mahari. Mipango yote ilienda sawa. Aliiandaa sherehe kubwa kiasi kwaajili ya kunivusha Pete ya uchumba. Siku hiyo ndipo nilikutana na Jerry baada ya kupotezana nae muda mrefu. Baada ya kumwambia Jerry nimechumbiwa aliacha kunitafuta. Siku ya sherehe ya kuvishwa Pete ya uchumba ndipo alikuja na hakuwa anajua kama ni mimi ndiye mke mtarajiwa wa Fedrick. Alijisikia vibaya lakini hakuwa na namna ujanja ni kupata mawenzake ndo tayari kashanipata.
Tayari nikiwa nishavishwa Pete ya uchumba tulipewa pongezi kwa ndugu jamaa na marafiki. Muda wa kupewa pongezi ndipo Jerry Alipata nafasi ya kunisogelea.
“Umejua kuugusa moyo wangu Leo, haki ya MUNGU Mamy umejua kuupasua moyo wangu Leo”.
“Nisamehe bule ila niliamua kujiepusha na wewe baada ya kujua kuwa ni mume wa mtu”.
“Najua alikwambia Fedrick ili anizunguke, ni kweli nilikuwa mume wa mtu ila ndoa yangu ilikuwa na migogoro kwa kipindi kile na Sasa nishaachana na mke wangu”.
“Usimlahumu Fredrick, mimi na Fedrick tulifahamiana kabda ya kukutana na wewe”.
“Ni sawa, sitaki nikupotezee furaha yako. Nimekubali kuwa wewe ni shemeji yangu. Hata hivyo Fedrick anakupenda sana. Mawatakia Kila raheri’.
“Asante Sana”.
Shughuli iliendelea watu walikunywa, kula na kucheza mziki. Baada ya shughuli kuisha mimi nililudi nyumbani kwetu na watoto maana kipindi icho nililudi kwetu kwa muda nikisubilia ndoa.
Baada ya miezi miwili tangu nichumbiwe hatimaye Ile siku tulivyokuwa tunasubilia Kwa hamu ilifika. Mimi na Fedrick tulifunga ndoa na kula kiapo kanisani mbele ya mashahidi na mashuhuda wengi kuwa tutaishi pamoja siku zote za shida na Raha mpaka pale kifo kitakapotutenganisha.
Baada ndoa tulifuatiwa na sherehe kubwa ya kifahari. Siku ya sherehe nilimuona Sarah mdogo wangu alipemdeza kiasi chake ila alikuwa mjamzito wa tumbo kubwa tu.
Ulifika muda wa zawadi tulitinzwa zawadi kutoka wa watu mbali mbali. Mc alitangaza Kuna mtu special kwa jina la Prisca ni muda wake wa kuleta zawadi. Hakuwa mwengine bali ni mama Amarah original. Alikuja pale mbele na bango kubwa akiwa na wapambe wake. Familia ya Fedrick walikuwa na mshangao hata sisi maharusi pia.
Aliomba kipaza sauti mc alimpa. Alianza kutoa salamu kwa waalikwa ndipo alizungumza.
“Yes, baadhi yenu mnanifahamu hapa mimi ni nani ila wapo baadhi pia hawanijui kabisa. Kwa msionijua mimi ndiye mama Amarah. Sipo hapa kwaajili ya taharuki ila nipo mbele yenu kwaajili ya kutoa shukrani za dhati kwa familia hizi mbili zilizoungana kwaajili ya ndoa za watoto wao.
“Fedrick kama ujuavyo Mimi ni mke wa mtu na mama wa watoto wengine wawili niliozaa na mume wangu. Leo nikuombe msamaha mbele ya hadhira kwa niliyokutendea wewe na mwanangu ila Imani ni kwamba Kila jambo na makusudi yake. Hatukupangiwa kuwa pamoja. Una umepata mke mzuri na mama mzuri kwa wanao”.
“Baada ya kusikia kuwa unaoa, nilipaniki sana, nilifunga safari mpaka Tanzania lengo kuja kuwaharibia mipango yenu ila nilikutana na kitu cha tofauti sana. Fedrick huyu mkeo ni watofauti sana, anaupendo kunishinda mimi aiseee. Nilichunguza na kugundua anampenda sana mwanangu, mabaya yote niliyopanga kumfanyia hayakuwa na nguvu Tena maana nguvu ya upendo wake juu ya mwanangu ilipitiliza”.
“Watu wanajua huyu ni mama mzazi wa Amarah yote ni kwasababu ya upendo wake. NISEME TU ASANTE SANA MAMY WEWE NI MKE WA DUNIA”.
“Zawadi yangu ni hii japo ni kidogo lakini naamini mtakifurahia”. Prisca aliyasema hayo na kuchana karatasi la juu ya lile bango. Alituzawadia milioni mia na magari mawili ya kifahari. Ukumbi mzima ulilindima kwa shangwe na nderemo ariririririiiiiii!. Alitusogelea na kutulumbatia wote kwa furaha. Baada ya hapo aliomba amuone mwanae. Bibi Amarah bila hiyana alimpa mtoto Prisca. Prisca alifurahi baada ya kumuona Binti yake mrembo ila mtoto hakuonyesha kumfurahia mama yake.
Shughuli iliisha, maharusi tulienda fungate. Niliingia lasmi kwenye maisha ya ndoa. Fedrick ni mume mzuri na ni baba mzuri Kwa watoto wake……
MWISHO

