MKE WA DUNIA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU 11
Namna aliyokuwa anaendesha Kwa mwendo kasi iliniogopesha. Alionekana kufulu kwa hasira.
“Fedrick unafanya nini Sasa?”. Niliongea kwa paniki.
“Kumbe wewe ni mwanamke mpumbavu eeeh!. Mamy wewe ni kahaba?” Aliyasema hayo huku akilisimamisha gari. Kando ya barabara.
“Unasemaa!”. Nilihamaki Kwa hasira baada ya Fedrick kuongea hayo.
“Niambie wewe ni kahaba?”. Fedrick aliniuliza tena. Nilijikuta naunyanyua mkono wangu na kumpiga kibao cha nguvu shavuni mwake, hakutegemea kama nitaweza kumuadhibu maana alitulia kama amepigwa na shoti.
Muda huo machozi yalikuwa yananitililika mashavuni.
“I’m sorry Mamy”. Fedrick aliniomba msamaha. Nilitoka kufungua mlango wa gari ili nishuke. Alinizuia na kulock milango ya gari.
“Niache niende zangu tafadhali”. Mala simu yangu ilianza kulia, aliyekuwa anapiga ni Jerry. Nilipokea haraka na kuiweka masikioni lengo ni kumwambia Jerry nilipo ili anifuate.
Kabda sijaongea Fedrick alinipokonya simu alikata na kuzima kabisa.
“Kila napokutana na wewe umekuwa ukinipatia maumivu Makali sana moyoni mwangu. Kwaiyo umekuja kwenye maisha yangu ili kuniumiza?. Nakuchukia sana Fedrick, I hate you.”. Niliongea hayo huku nikiwa nalia Kwa uchungu.
“Ni sawa unanichukia najua hilo. Mamy hata kama ni wewe ungejusikiaje kama ungejua kuwa mimi natembea na rafiki Yako?”.
“Mimi na wewe tuna uhusiano Gani Fredrick?”.
“Inamaana hujui mimi na wewe tupo vipi?”.
“Ninachojua sikujui hunijui, tafadhali Niache niende zangu na ukae mbali na maisha yangu?”.
“Kwaiyo mimi mbaya ila Jerry ni mzuri sio?”. Fedrick aliniuliza Kwa paniki.
“Hajawai kuwa mbaya kwangu tangu nimfahamu. Ni mpole, Hana kauli mbaya kama wewe pia ana huruma. Hawezi fanya jambo kwa kunikomoa Bali anafanya kwa kunivusha. Jerry ni rafiki mzuri mno sijuti kumfahamu”. Niliongea hayo makusudi tu japo ni kweli tangu nifahamiane na Jerry hajawai kunitendea baya. Niliongea hayo kwa lengo la kumuumiza Fedrick na kweli yalimchoma moyoni. Aliinamisha kichwa chini.
“Toa lock niondoke zangu”.
“Ni sawa ila acha nitakupeleka. Ni usiku saivi huwezi kwenda peke yako”.
“Usijali kuhusu Mimi”. Nilifungua mlango ila Bado Fedrick alikuwa ameweka lock.
“Fedrick tafadhali to lock niende zangu”. Fedrick hakuongea chochote aliwasha gari na kuliondoa eneo hilo.
Alinipeleka mpaka home kwangu. Ilikuwa majira ya saa sita usiku. Baada ya kunifikisha alitoa lock ya milango haraka nilifungua mlango na kushuka kwenye gari.
“Unaweza kwenda ila naomba ukae mbali na maisha yangu”. Niliongea hayo nikiwa nje ya gari na Fedrick alikuwa ananitazama kupitia dirisha la gari alilosusha kioo.
“Naweza kukaa mbali na maisha yako ikiwa wewe ni mama wa mwanangu. Mamy jiandae hivi Karibuni nitakuamisha hapa”.
*Never siwezi kukaa karibu na wewe, Mimi ni Malaya nawezaje kuwa mama wa mwanao?, mimi ni masikini na Wala sina hadhi ya kuwa na wewe tajiri”. Fedrick alinitazama hakuwa na lakuongea zaidi.
Nilipiga hatua kusogelea mlango wa chumba changu. Niligonga mala Moja tu Sarah aliitikia nilijua Bado alikuwa macho anaangalia Tv maana Sarah ni mpenzi sana wa Tv. Alifungua mlango niliingia ndani na kumuamuru afunge mlango.
Baada ya kufunga mlango niliona amebadilika gafla ni kama vile alikuwa amenuna.
“Mmekula?”. Nilimuuliza.
“Ndiyo ila sijapenda”.
“Shida nini?”.
“Kwanini ulinidanganya. Si nilimuuliza unatoka na Fedrick ukakataa na huyo aliyekuludisha ni nani?”. Sarah aliniuliza huku akionekana kuchukia.
“Alafu Sarah ujue wewe Bado mdogo sana, achana na habari za huyo Fedrick sio muoaji yule”. Niliongea kwa hasira maana nilishavulugwa na yeye anataka kunipanda kichwani Kwaajili ya mtu huyo huyo aliyenivuluga.
Full story utaipata kwa muandishi na mtunzi wa simulizi hii Nuru Halisi. Namba yangu ya whatsp wailiana na chama HURU
“Lakini mie nampenda nipo tayari kumpa hata bikra yangu”. Nilimtazama Sarah kwa hasira Kwa sekunde kadhaa nilijikuta nacheka. Nilicheka sana mpaka Koo liliniuma. Nilifuata maji kwenye friji nilimimina nikanywa baada ya hapo zikuzungumza chochote nilienda chumbani nikapanda kitandani kuanza kutafuta usingizi. Usingizi nao uligoma kuja, nilikumbuka kuhusu Jerry.
“Hapana ni bola nisiiwashe hata hivyo sitaki ukaribu nae Tena. Hata yeye pia amenikosea Kwanini anitambulishe kwa marafiki zake kuwa mimi ni demu wake na wakati Wala sina mahusiano nae. Pia Jerry ni rafiki wa Fedrick sitaki kuwa na ukaribu nae tena nitaoneoana mwanamke wa ovyo.
Palikucha asubuhi nilijiandaa Kwaajili ya kwenda kwenda kazini. Nilipokuwa tayari na kuhakikisha Kila kitu kipo sawa nyumbani nilielekea kazini. Nilifika kazini nilishangaa baada ya kunikuta gari la Jerry.
“Khaa si Jerry huyu?”. Nilijiuliza mwenyewe nikiwa nimesimama Kwa mbali nakitazama gari. Nilianza kusogea taratibu. Nilifika dukani nilijifanya kama vile sijaliona lile gari. Nilifungua duka Jerry alikuwa ananitazama tu kupitia kioo Cha mbele. Nilipokuwa dukani napanga panga nguo Jerry aliingia muda huo mimi tu ndiye niliyekuwa nimefika.
Nilijifanya kama sijamuona vile na yote ni kwasababu sikuwa na majibu ya kumpa pale atakaponiuliza nilienda wapi Jana baada ya kuniambia anaenda chooni na hata aliponipigia nilipokea na kukata na baada ya kukata simu sikupatikana Tena mpaka muda huo. Basi niliendelea kujifanya kama vile sijamuona na kuwa busy na kupanga nguo.
“Mamy I sorry. Najua nilikukwanza jana kukutambulisha kwa watu kuwa ww ni mpenzi wangu. Nisamehe bule rafiki yangu”. Jerry aliongea hayo kwa sauti tulivu. Karoho kalitulia baada ya kuyasikia mengine nisiyoyadhania.
“Usijali nimesamehe”.
“Ni kweli?”.
*Yeah!”.
“Kama umenisamehe kweli basi acha unachokifanya kwanza alafu niangalie”. Niliacha kupanga nguo na kumgeukia Jerry. Jerry alikuwa ananiangalia kwa tabasamu Bomba.
“Una amani?”. Nilimuuliza
“Yeah kwa sasa Nina Amani japo ulinipa wasiwasi zaidi baada ya kukata simu na kutokupatikana kabisa. Nilijua umepatwa na matatizo. Huwezi amani nimefika hapa sukani saa 12 asubuhi”.
“Usijali nipo salama”
“Okay sawa. Basi nikuache uendelee na majukumu Yako ya kazi japo nilikwambia Leo usifike kazini”.
“Usijali nipo fiti”. Jerry aliniaga aliondoka.
Nilifanya kazi zangu kama kawaida. Majira ya saa mbili kasoro nilifika nyumbani kwangu palikuwa kimya sana na hata taa za ndani hazikuwashwa. Nilipofungua mlango na kuwasha taa nipata mshtuko wa wazi wazi. Seble ilikuwa nyeupeeee hakuna hata kijiko, Sarah Aquram hawapo pia. Gafla nilianza kutokwa na majasho usoni……
SEHEMU 12
hofu ilinitawala moyoni mwangu nilijua labda Sarah ameamua kutoroka kwakuwa Jana alikwazika baada ya kuniona nimeludi na Fredrick.
Niliingia chumbani napo palikuwa kweupe hakuna kitu. Nilitoa simu yangu kwenye pochi na kumpigia Sarah ila simu iliita mpaka ikakata pasipo kupokelewa. Nilitoka nje kumuuliza jirani yangu. Nilikuwa nimepagawa haswaa asikwambie mtu.
“Kuna gari ilikuja walisaidiana na mdogo wako kuamisha vyombo na baada ya hapo waliondoka. Mie nilijua unahama”.
“Hapana nahisi kuchanganyikiwa. Niliyasema hayo huku nikiwa nimeshika kichwa changu. Taratibu nilikaa chini. Mala simu yangu ilianza kuita nilitazama nani mpigaji niliona ni namba ni Fedrick. Iliita mpaka ilikata pasipo kupokea. Alipiga Tena lakini sikupokea. Baada ya kuona sipokei alitumia ujumbe usemao’.
“Kwanini hupokei simu?, watoto wapo huku kwangu”. Ujumbe ulisomeka hivyo, nilishtuka kiasi. Nilimpigia simu Fedrick alipokea.
“Umesema Sarah na Aquram wapo huko kwako?”.
“Yes”.
“Hivi una akili kweli wewe?, kwanini umewachukua na kuchukua vitu vyangu bila makubaliano?”.
“Wewe njoo ndipo tuelewane. Au umesahau kuwa nakudai?”. Milichukizwa na tabia za Fedrick na kuzidi kumchukia. Yaani kunidai hiyo milioni Moja ndio anitawale kupitiliza.
Niliinuka pale chini kwa hasira nilibeba pochi yangu na baada ya hapo niliondoka kuelekea nyumbani kwa Fedrick.
Nilifika nilifunguliwa geti na mlinzi. Ilikuwa ni majira ya saa tatu usiku. Niliingia ndani na kukutana na familia nzima. Yaani Fedrick, mama yake, Amarah, Aquram, Sara, na dada wa kazi. Walikuwa wamekaa wanaangalia TV ma watoto walikuwa wanacheza game.
Watoto baada ya kuniona wote walinikimbilia na kunikumbatia.
“Nilikumiss mama, usiniache tena”. Amarah aliyasema hayo. Huwezi amini hasira zote ziliniisha.
“Karibu mwanangu”. Bibi Amara alinikaribisha.
“Asante”. Nilienda kukaa kwenye sofa na watoto waliendelea kucheza game wenyewe kwa furaha. Ukimya ulitawala kwa dadika kadhaa, niliamua kuvunja ukimya ule maana sikuelewa nini sababu ya kuamishwa familia yangu.
“Samahani naomba kufahamu kwanini mmeamisha familia yangu. Fedrick si nilikiahidi kukulipa hata hivyo vitu nyangu ulivyochukua ni zaidi ya pesa unayonidai. Sijapenda njia uliyoitumia maana hayakuwa makubaliano yetu”.
“Naomba nizungumze na wewe. Tafadhali nifuate chumbani kwangu”. Bibi Amarah aliyasema hayo na kunyanyuka kuelekea ndani kwake.
Niliinuka pia na kumfuata nyuma. Tulipandisha mpaka juu gorofani kwenye moja ya chumba. Tuliingia humo. Chumba kilikuwa kizuri sana. Tulikaa kwenye sofa lililokuwepo chumbani humo na bibi Amara alianza kuzungumza.
“Jana usiku saa sana usiku Fedrick aliludi kutoka kwenye sherehe ya rafiki yake. Alikuja kunigongea chumbani kwangu muda huo nilikuwa nimelala ila nililazimika kufungua mlango maana alikuwa anagonga Kwa fujo sana. Alilalamika sana Jana kuhusu wewe.
“Eti ni kweli Mamy wewe na Jerry ni wapenzi?”. Bibi Amarah aliniuliza. Kabda ya kumjibu nilijiuliza anafahamiana nae kumbe?”.
“Hapana mama, Jerry ni rafiki yangu na pia ni mteja watu mkubwa dukani napofanya kazi. Sina mahusiano nae”.
“Onhooo! Sawa. Basi nikuombe kitu mlbinti yangu”.
“Sawa”.
“Kuanzia Sasa naomba uishi hapa, si uliniahidi utakuwa tayari kumlea Amarah kama mwanao na tulikubaliana kuishi hapa hata kama hamna mahusiano na baba yake”.
“Lakini mama sidhani kama inawezekana. Siwezi kuishi na Fadeck kutokana na anavyonichukulia”.
“Nitaongea nae. Sina muda mrefu wa kuendelea kuwepo hapa. Nataka nimuache Amarah kwenye mikono Yako coz nimeona ww ndiye mama mzuri kwake na yeye pia ametokea kukupenda sana. Utakuwa huru kwenye mambo Yako kikubwa tu uwe makini na watoto. Imani yangu kupitia wewe unaweza ukambadilisha baba Amarah pia na kuwa vile inavyostahili”.
“Mh sawa ila kama nitashindwa nitaondoka”. Tulikubaliana hivyo na mama na baada ya hapo tulitoka sebleni.
“Mama Amarah naomba uishi vizuri na mwenzio umenielewa?”.
“Sawa”. Fedrick alijibu na baada ya hapo alitutakia usiku mwema na kwenda chumbani kwake.
Nililetewa chakula nilikula baada ya hapo niliwachukua watoto nikaenda nao kulala chumbani Kwa Amarah.
Sarah alienda kulala na dada wa kazi na mama alienda kulala chumbani kwake.
Palikucha asubuhi nilijiandaa kwenda kazini. Nilipokuwa tayari nilitoka chumbani ili niende kazini nilikutana na mama Sebleni. Tulisamiliana na baada ya hapo nilimuaga ili niondoke.
“Msubilie Fedrick muongozane”.
“Nitachelewa mama acha tu niende kwenyewe”.
“Hapana muda si mrefu anashuka maana ndo muda wake huu wa kwenda kazini”.
“Mama,” kabda sijamaliza kuongea nilimuona Fedrick anshuka kutoka juu gorofani nilinyamaza kimya. Alifika pale sebleni alisalimiana na mama yake mie kama vile hkuniona. Baada ya kusalimiana na mama yake alianza kupiga hatua kutoka nje.
“Fedrick utampeleka mwenzio kwanza kazini kwake”.
“Muda hauruhusu, nitachelewa kazini”.
“Nimesema na aliludi tena”. Mama aliongea kwa ukali. Nilijisikia vibaya kuona analazimisha mambo na mwanae hataki.
“Sawa”. Fedrick aliitikia kiroho mbaya, tulitoka nje na kuongoza mpaka parking ya magari. Tuliingia kwenye gari Moja wapo. Humo kwenye gari Kila mtu alikuwa bubu, Kwa dharau za Fedrick alivaa na Headphone masikioni kabisa.
Tulifika barabara kuu alisimamishwa gari kando ya barabara.
“Shuka hapa utachukua Taxes sina muda wa kupoteza Nina mambo mengi ya kufanya. Shika nauli hiyo”. Yaani nna alivyokuwa anaongea Sasa ni madharau tupu jamani.
“Nina pesa hata hivyo, Asante”. Niliyasema hayo na kushuka kwenye gari lake. Na baada ya Mimi kushuka tu liwasha gari na kuliondoa eneo hilo. Nilibaki kulitazama tu mpaka likatoweka machoni mwangu.
“Nitaweza kweli kuishi nae huyu bwana na dharau hizi?”. Nilijiuliza mwenyewe moyoni.
Kwakuwa alinisogeza mpaka karibu na kazini nilipanda boda boda Kwa Bei ya elfu tatu tu.
Majira ya saa Moja usiku nililudi kazini, na kukutana na habari nyengine. Bibi Amarah aliniaga kuwa kesho anaondoka kwaiyo anaomba nisije nikaondoka nikamuacha Amarah peke yake na kama Kuna matatizo yatajitokeza basi niwe huru kumwambia kwakuwa anamjua mwanae vizuri.
Sikuwa na namna zaidi ya kukubali. Ilipita wiki moja tangu Mama aondoke nyumbani. Jumamoss Moja nilipokuwa dukani simu yangu iliita mpigaji alikuwa Jerry, mala nyingi Huwa namvungia. Hata alipiga simu sipokei, siku hiyo niliamua kupokea simu kwani roho inanisuta kwasababu hajawai kuwa mtu mbaya kwangu.
Baada ya kupokea simu tulisamiliana na ndipo aliniambia kesho atanifuata kwangu anamazungumzo na Mimi”….. Nilibaki njia kuu nimwambie ukweli au niendelee kufanya Siri….
SEHEMU 13
Sikujua nimwambie Nini Jerry.
“Mbona upo kimya?” Aliniuliza baada ya kuona kimekaa kimya.
“Anhaaa! Sawa”. Nilimjibu hivyo.
“Mbona kama vile haupo sawa?. Niambie nini shida Mamy?”.
“Hakuna nipo sawa tu mbona”.
“Sawa”. Saa tano asubuhi nitakufuata.
“Sawa”. Niliitikia lakini sikuwa nimeliafiki kabisa.
Nililudi nyumbani simu hiyo mapema saa kumi jioni tulifunga duka. Boss alitupa time ya kupumzika. Nililudi nyumbani nilipokelewa na watoto kwa furaha. Yaani Amarah na Aquram walikuwa wanapendana balaa.
Nilikaa na watoto sebleni tunacheza michezo mbali mbali, dada wa kazi alikuja na kuomba kuzungumza na Mimi. Yule Binti alikuwa ananiheshimu sana na kwa umri yeye alikuwa mkubwa.
“Nimeamua nikwambie mapema ili baadae yakitokea ya kutokea usije kunilahumu na kusema kwanini sikumwambia. Dada mdogo wako Huwa anaingia chumbani kwa Kaka Fedrick muda mnaokuwa kazini. Sijui Huwa anafuata Nini, Leo hii ameingia na kutoka na nguo chafu za kaka. Amefua mpaka boxes”. Hidaya Binti wa kazi aliyasema hayo nilibaki mdomo wazi.
“Usiku hana tabia ya kutoka mnapolala?”.
“Sijawai kumuona akitoka labda kama ananiviziaga nipitiwe na usingizi na si unajua nachoka sana. Nililala ni kama mfu”.
“Sawa, kaendelee na kazi zako my dear”. Baada ya hidaya kuniambia hayo niliona ni hatari Sasa hii. Nilimuita Sarah ili nizungumze nae.
“Tabia za ajabu nyumbani kwa watu sitaki”.
“Nimefanyaje dada?”.
“Nani amekupa Mamlaka ya kuingia chumbani Kwa Fedrick”.
“Nilifuata tu nguo dada”.
“Ndo mpaka boxes unamfulia?, hivi Sarah una akili kweli wewe?, unachokitafuta na utakipa na usipobadilika nitakuludisha Kwa mama mkoani. Kuwa na heshima. Fedrick ni mkubwa sana kwako yafaa kumuheshimu sana kama kaka yako”.
“Lakini dada mimi nampenda na unajua hilo. Huoni kuwa hii itakuwa nafasi nzuri ya yeye pia kunipenda mimi?. Sio kwamba najipendezeka ila nataka anipende ndo maana namfulia mpaka boxes. Nataka awe msafi”. Yaani akili za Sarah zinachosha anavyoongea Sasa mpaka anakuita hasira unatamani Umtie makozi akili ikae sawa.
“Kwaiyo ndo unajipa majukumu yasiyokuhusu ili upendwe?, nani alikwambia mwanaume Huwa anapenda mwanamke mwenye shobo?. Sasa nakwambia Tena ole wako nisikie umeingia chumbani kwa Fedrick ujue safari ya mkoani inakuhusu”. Sarah aliondoka kwa hasira.
Usiku tulikusanyika kwenye meza ya chakula. Mambo aliyokuwa anafanya Sarah ni aibu tupi. Kwanza Kila mmoja Huwa anajipakulia mwenyewe chakula ila Sasa ajabu Sarah siku hiyo alimpakulia chakula Fedrick. Wote tulishangaa hata Fedrick mwenyewe. Mtu nimetoka kumsema jioni usiku anaendelea🙌.
Alimpakulia chakula na kulundikia kwenye sahani kama vile anakula mwanaume wa kisukuma kumbe anakula mwanaume wa dar ten wa kishua anayeshinda amekunja nne ofisini.
“Inatosha”. Ilibidi Fedrick mwenyewe amzuia maana alikuwa anayajaza tu 🤣. Fedrick alipunguza kile chakula niliona Sarah alivyonisikia aibu.
Nilikuwa busy kuwalisha watoto kwanza Sarah alikuwa anakula kwa mapozi khaaa 😄😄😄 nyie kupenda ni shida sana. Fedrick mwenyewe hakuwa na habari nae kabisa. Fedrick alimaliza na kuniambia nikimaliza kula nimfuate chumbani kwake ana mazungumzo na mimi.
Sarah mdogo wangu alijikuta anaropoka na kumuuliza Fedrick.
“Mazungumzo gani?”. Wote tulishangaa. Fedrick alimuangalia na kuishi kutabasamu tu na baada ya hapo alipandisha juu gorofani.
“Jifunze kuwa na stara, ujue wewe ni mwanamke Sarah?”. Hidaya alimwambia hayo Sara.
“Na wewe nyamaza fata yaliyokuleta achana na Mimi”. Sarah alimjibu Hdaya Kwa paniki”.
“Achana nae”. Nilimwambia Hidaya hayo ili kuepusha zogo. Baada ya kumaliza nilielekea chumbani kwa Fedrick. Nilifika mlangoni nilipiga hodi aliniluhusu miingie.
Niliingia nilimkuta yupo busy anachezea laptop yake,
“Tunaweza kuzungumza?’. Nilimuuliza baada ya kuona kama vile Hana habara na mimi na yeye ndiye aliyeniita.
“Wait kidogo Kuna kazi ya muhimu namalizia”.
“Basi naweza kwenda na ukimaliza utaniita”.
“Huwezi kusubilia?, kaa hapo kwenye sofa au ukikaa karibu na mimi nakutia kichefu chefu?”. Fedrick aliniuliza hayo.
Sikutaka mambo yawe mengi, nilikubali kukaa kwenye sofa humo chumbani kwake kumsubilia amalize anachokifany kwenye laptop.
Nilikaa kama dakika kumi na tano nilisikia mlangonunagongwa. Fedrick aliniambia nikafungue. Nikiinuka pale kwenye kochi na kusogelea mlango.
Nilifungua nilishangaa baada ya kumuona Sarah, mawazo yangu nilijua watoto ndio wanaogonga mlango. Sarah aliniangalia juu mpaka chini na mie nilikuwa namtazama tu.
“Ni nani na ana shida Gani?”. Fedrick aliniuliza.
“Ni Mimi Sarah”. Sarah alijibu baada ya hapo alinishika mikono wangu na kunivuta kwanguvu. Tulifika mpaka chumbani kwao ndipo aliniachia mkono.
“Una matatizo Gani wewe?”
“Nimeshindwa kuvumilia, niambie muda wote mlikuwa mnafanya Nini?”. Sarah aliniuliza kwa paniki. Nilichukia nilijikuta naunyanyua mkono wangu kwa mala ya kwanza na kumuadhibu Kwa kumpiga kibao cha shavu. Sarah alianza kulia na kuugulia maumivu.
“Tafadhali uwe na heshima, mimi ni dada yako na najitambua. Sitaki nikutamkie maneno mabaya kwaiyo usivuke mipaka”. Niliyasema hayo na baada ya hapo nilitoka mule chumbani na kuludi chumbani kwa Fedrick……..
SEHEMU 14
Nililudi chumbani kwa Fedrick nilimkuta amekaa kitandani.
“Mdogo wako ana shida gani?” Fedrick aliniuliza.
“Usijali. Nishamalizana nae”.
“Okay, Nina jambo Moja nataka nikuambie”
“Nakusikiliza”.
“Kwanza una elimu Gani?”. Fredrick aliniuliza swali gumu. Kwa miaka ya hivi Sasa mtu asiyefika elimu ya form 4 anaonekana ni kilaza haswaa.
“Mbona upo kimya?”.
“Wee elimu yangu ya Nini?”. Niliona anazingua tu na yeye. Elimu kitu gani bhana na watu tuna ishi 😄😄.
“Okay! Nataka nikuajili kwenye kampuni yangu. Hivi kuanzia Sasa unatakiwa kuacha kazi unayoifanya”.
“Mh!, hapana siwezi kuacha kazi kwasababu kazi hiyo ndiyo inayonifaa. Sina elimu ya kuajiliwa kwenye kampuni Mimi”. Nilimjibu Fedrick. Aliniangalia na kitabasamu. Nilichogundua Kwa Fedrick ni mtu anayependa kutabasamu sana.
“Basi chagua maliwi. Uache kazi ukae nyumbani au nikuajili kwenye kampuni yangu, uwe mfanya kazi wangu na mshahara wako utakuwa mzuri tofauti na unaolipwa Sasa”.
“Fedrick ujue sikuelewi mambo Yako”.
“Utanielewa tu”.
“Kazi siwezi kuacha. Sipo tayari kuajiliwa na wewe nevar”. Nilimjibu Kwa ujeuri Fedrick maana dawa ya moto ni moto tu 😄.
“Kwaiyo haupo tayari kuajiliwa na mimi ila kuajiriwa na Jerry ndo upo tayari sio?”. Fedrick aliongea Kwa paniki sikuelewi anamaana gani kusema hivyo.
“Kwanini unapenda kunitawala, najuta kukufahamu Fedrick”.
“Sikia mie sinaga muda wa kuzogoa na mademu. Chagua Moja kati ya kuacha kazi au kukuajiri mwenyewe na kukulipa mwenyewe?”.
“Hakuna chagua kati ya hayo. Tafadhali usinipangie Cha kufanya kwanza nimekwambia sina elimu ya kuajiliwa huko”.
“Unaeidhika na hako ka laki nne unakolipwa na Jerry?”. (Huyu anaongea Nini?).
“Sijakuelewa?, unamaanisha kwamba?”.
“Hiyo laki nne unayolipwa unaona ni kubwa?, Mimi nitakulipa mala mbili yake endapo utakubali kuacha kazi kule”. Fredrick aliongea hayo.
“Kwani unamjua boss wangu?”. Nilimuuliza swali la kitoto.
“Wee chizi eeeeh!. Kwani nimekwambia nini?”.
“Heeee! Kwaiyo boss wangu mimi ni Jerry?”.
“Unajuaga nani?”. Sikia nikwambie. Utakuwa secretary wangu na kuhusu elimu niachie Mimi. Jumatatu tutaongozana wote kazini sawa!”.
“Mh!”. Niliguna tu. Jerry aliniambia naweza kwenda anataka kupumzika.
Nilitoka chumbani kwake nilishangaa kumkuta Sarah mlangoni amejibana. Nilimpita Wala sikumsemesha kitu. Nilienda chumbani kwangu na watoto wangu. Muda huo watoto walikuwa wameshalala.
“Inawezekana vipi Jerry awe boss wangu kule na mie najua boss wangu madamu Aneth. Lakini inawezekana nakumbuka siku Ile alitoa ruhusu yeye kutoka nae kwenye party na nilipomuuliza madam aliniambia anataarifa hizo. Ila mbona ananunuaga Hadi nguo jamani”. Nilijiuliza mengi pasipo majibu.
“Kwakuwa kesho tumepanga kuonana nitamuuliza”. Niliyasema hayo na kuvuta shuka langu.
Palikucha asubuhi Sarah alikuwa ameninunia na mie Wala sikumjili. Niliona utoto unamsumbua. Nilimsaidia Hidaya kuandaa vitafunia. Muda wa chai wote tulikusanyika mezani. Kama kawaida Sarah shobo zake Alitaka kummiminia Fedrick chai ila Fedrick alimzuia.
“Acha nitamimina mwenyewe. Alafu tukiwa kwenye meza ya chakula naomba uwe mtulivu ipo siku utatuunguza Sasa”. Fredrick aliyasema hayo. Niliona Sarah amepooza gafla, alikaa kwenye kiti Kwa aibu.
Tulipokuwa tunakunywa chai Fedrick aliniambia.
“Mamy baada ya chai nataka tutoke na watoto”.
“Hapana mimi sitoenda Nina safari”.
“Mama bhana twende wote. Baba mama asipoenda na mimi siendi”.Amarah aliongea hayo.
“Huyu nae bhana. Mie nasafari zangu nae anataka kunialibia”. Niliyasema hayo moyoni.
“Mama twende wote”. Aquram mwanangu aliniambia.
“Kama ana safari basi nitaenda Mimi”. Sarah aliyasema hayo. Niliona Fedrick kamkata jicho la mwana nikome.
“Tunataka kwenda na mama”. Amarah aliendelea kukazia.
“Eti mama si tunaenda wote?”. Amarah aliniuliza Kwa sauti ya kujitilisha huruma.
“Ni sawa tutaenda”. Nilimjibu. Walifurahi na kuanza kuruka ruka Kwa furaha. Sarah alinuna balaa.
Tulimaliza kunywa chai nilienda kuwaandaa watoto ilikuwa ni majira ya saa nne asubuhi. Wote tulikuwa tayari kwa safari. Tulienda kupanda gari hao tulaishia.
Tulienda kinyerezi parking, ni hotel nzuri yenye na inavutia sana, si wakubwa Wala watoto. Tuliwapeleka watoto kwenye michezo tukamuachia mdada maalumu anayewasimamiwa watoto kwenye michezo na sisi tulitafuta sehemu tulikaa.
Tuliagizia vinywaji tuliletewa. Ukimya ulishika nafasi. Fedrick alikuwa busy na simu. Simu yangu ilikuwa mezani. Ilianza kuita mpigaji alikuwa ni Jerry.
Nilijitazama na kumtazama Fedrick naye alinikata jicho hilo woiiiih🙌. Niliacha iliita mpaka ilikata. Jerry alipiga Tena. Fredrick aliniambia nipokee.
Nilipokea na kuweka masikioni,
“Muda ndo huu mama, nikufuate wapi?”. Jerry aliniuliza ila kabda ya kumjibu nilimtazama Fedrick naye alikuwa ananitazama kwa umakini akifuatilia mazungumzo yetu.
“Nisamehe Jerry nimepata dharura hatutoweza kuonana Leo”. Nilimwambia hayo Jerry ila nafsi ilinisuta.
“Onhooo! Usijali Mamy. Kesho nitakuja kazini kwako.
“Sawa. Nikutakie siku njema”.
“Na kwako pia, kuwa makini”.
“Asante Sana”. Nilikata simu na kushusha pumzi mdogo mdogo. Fedrick aliendelea kuchezea simu yake baada ya Mimi kumaliza kuongea na simu. Nilijitoa ufahamu na kuamua kuvunja ukimya.
“Fedrick!”.
“Naam!”. Aliitikia na kunitazama.
“Samahani naomba kujua kama kile ulichoasema Jana usiku kama unamaanisha”.
“Kuhusu kazi?”.
“Ndiyo”.
“Namaanisha na ndo maana nimekwambia kesho tutaongozana wote”.
“Kwa kesho haitowezekana. Natakiwa nifike ofisini kuweka mambo sawa ndipo niache kazi”.
“Najua una appointment kesho na Jerry, Uongo?. Mama Aquram achana na Jerry yule ni mume wa mtu kaa nae mbali utakuja kujiingiza matatizoni endapo utaendelea kuwa karibu nae na usije nilahumu kwa kusema Kwanini sikumwambia kabda. Naludia tena kukwambia. Jerry ni mume wa mtu”. Fedrick aliyasema hayo na kuniacha kwenye viulizo….
SEHEMU 15
Baada ya Fedrick kuniambia kuwa Jerry ni mume wa mtu nilikuwa na viulizo vingi sana. Anaonekana anamfahamu Jerry vizuri na kama alivyoniambia kuwa ni marafiki.
“Umesema ni mume wa mtu?”.
“Kipi hujaelewa”. Alinijibu kwa dharau kama ananipandisha na kunishusha.
“Sawa, nimekuelewa”. Nilikubali ila moyoni nilikuwa na maswali mengi”.
Hatukuwa na maongezi Tena Kila mtu alikuwa busy na mambo yake. Sikuona maana wa huo mtoko, majira ya mchana tulikula chakula na baada ya hapo watoto walitaka kuogelea. Fedrick alikataa kwenda kuogolea nao ilibidi mimi niwapeleke.
Nilienda kubadilisha nguo na kuvaa nguo maalumu kwaajili ya kuogelea, niliwavalisha na watoto. Tulielekea kwenye swimming pool tulipita alipokuwa Fredrick. Fedrick alinishangaa baada ya kuniona nimevaa kipensi Cha jinsi kiufupi na top. Namna alivyoniangalia nilijisikia aibu.
Nilitembea kwa mwendo wa haraka haraka kukwepa macho ya Fedrick. Tulifika kwenye swimming pool tulidumbukia ndani ya maji. Niliweka umakini kuwaangalia watoto wasije mudhulika.
Waliogelea mpaka walipotosheka waliniambia. Tulitoka kwenye maji tukapita pale pale alipokaa Fedrick maana ndiyo njia. Basi nilivyokuwa nimeloa vile vichuchu vyangu vilichomoza kwanza unaweza dhani sijawai kumnyonyesha. Maungo yalinichora sana. Fredrick alikuwa ananiangalia jicho hilo🙌🙌 sijui ndo kumezea mate. Basi nilivyo na kaumbo kazuri namba nane na mungo yalivyo wazi ilikuwa lazima apagawe kama ni kidume kweli😄😄😄.
Baada ya kubadilisha nguo tuliludi na kukaa pamoja mezani. Vililetwa vinywaji na nyama choma tulianza kula taratibu. Mala alikuja mdada mzuri na kumkumbatia Fedrick nyumba ya mgongo.
“Woiiiih! Baby”. Tulibaki tunashangaa tu mie na watoto wangu. Fedrick aligeuka kumuangalia yule mdada. Nilimuona tu amebadilika gafla. Alikunja sura
“Naona upo na baby Amarah”.
“Yeah nipo na familia yangu”.
“Ni nani huyu Binti?”. Yule mwanamke alimuuliza Fedrick Mimi ni nani.
“Unataka kumjua”.
“Yeah!”, alijibu huku akiniangalia Kwa munipandisha na kunishusha.
“Unaweza ukafata yaliyokuleta hapa”.
“Jamani”.
“Kwani ilikuja na Mimi?”.
“Nooo! Baby ila naamini hatujakutana kwa bahati mbaya”.
“Fanya kama vile hunijui. Nipo na watoto sitaki niwajengee picha mbaya”. Fedrick aliyasema hayo na baada ya hapo alituambia tuondoke haitaji kuendelea kuwepo hapo. Aliinuka na kuongoza njia na sisi tulimfuata nyuma. Timuacha yule dada amesimama anavyonza tu.
Tulipanda kwenye gari na kuliondoa eneo hilo. Kwenye gari ni ukimya tu ndiyo uliotawala. Tulipita kwenye Moja ya Super market. Fadeck aliwanunulia watoto vitu vya kula kula na Mimi alininunulia chocolate. Sijui kwanini alininunulia ila nilipokea hata hivyo napenda sana chocolate.
Tulifika nyumbani saa 12 jioni. Fedrick alipitiliza chumbani kwake Moja Kwa moja ni kama vile hakuwa sawa.
Majira ya saa mbili Usiku chakula Cha usiku kilikuwa tayari. Sarah alienda kumgongea ili akale.
“Endeleeni kula sipo sawa na sihitaji usumbufu pia”.
“Shida nini my?”. Sarah aljiloga kumuita Fedrick my.
“Umeniita?”. Fedrick alimuuliza Sarah, Sarah aliinamisha kichwa chini na kuanza kujiminya vidole vyake. Fedrick alikuwa anamuangalia tu. Alikuwa amevaa chupi, kanga na shati tu. Basi alianza kuivuta vuta kanga yake mala Ile kanga ilianguka na kubaki na kichupi na shati aliyovaa ni fupi pia iliishia kiunoni.
Sarah aliendelea kufanya madoio ili ampagawishe Fedrick. Mala ajisugue miguu yake mala ang’ate midomo yake. Fedrick alikuwa anamuangalia tu ila watoto wa sikuizi ni hatari tupu.
“Fedrick alikuwa anamuangalia kwa kumpandisha na kumshusha. Sarah akaona kamnasa mwanaume akaongeza manjonjo mtoto wa kike. Mala ajing’ate vidole.
“Unamatatizo Gani wewe?”. Fedrick alimuuliza Sarah.
“Fedrick ukweli mwenzio nakupenda sana. Nipo tayari kuwa mke wako na nitakupa ,zawadi ya usichana wangu. Mimi ni mwanamke niliyejutunza mpaka Leo simjui mwanaume. Nakupenda jamani na nipo tayari unitoe bikra yangu”. Fedrick alimuangalia Sarah muda mrefu na kutabasamu.
“Ni sawa kama usimavyo wewe ni Bikra sikataki ila unachembe chembe za kikahaba. Ujue wewe ni mdogo sana ulifaa uwe shule saivi. Sasa huna hata haiba ya kike kwa mambo unayofanya. Watu wa aina Yako wanakuwaga Malaya. Anakushinda hat dada Yako ana stara na utulivu”.
“Hapana sio hivyo jamani. Tatizo nimeshindwa kuendelea kuvumilia na ni kwasababu nakupenda sana”.
Fedrick aliinuka pale kitandani alianza kupiga hatua kumsogelea Sarah. Alimsogelea mpaka kwa ukaribu kabisa. Upande wangu nilipoona kimya tangu Sarah aseme ameenda kumuita Fedrick ni muda mrefu ma hajatoka niliingiwa na hofu. Niliinuka kwenye meza ya chakula na kuelekea chumbani Kwa Fedrick.
Mlango ulikuwa umeludishiwa kidogo tu na Kuna uwazi ulikuwepo wa kuona ndani. Nilipigwa na bumbuwazi baada ya kuwaona Fedrick na Sarah wamesimamiana Kwa ukaribu sana na Sarah alikuwa wazi sehemu ya chini. Sarah alikuwa wa kwanga kuniona maana aliutazamia mlango. Baada ya Sarah kuniona alifungua vifungo vya shati rake haraka haraka. Fedrick alimshika na kumzuia ndipo Sarah alianza kupiga makelele.
“Nisaidieni, kaka Fedrick ananibaka jamani nisaidieni” alipiga makelele huku akiwa analia. Niliusukuma ule mlango na kuingia. Niliiokota Ile kanga ya Sarah na kumfunika. Nilimgeukia Fedrick na kumuangalia kwa hasira sana. Fedrick alitingisha kichwa ishara hawezi kufanya kitu kama icho.
Nilinyanyua mkono wangu na kumpiga kibao cha shavu. Tena kibao kilikuwa cha nguvu haswaaaa!………
INAENDELEA…….

