MKE WA DUNIA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU 06
Wote tulipigwa na butwaa baada ya kutambuana. Haraka nilikwapua mkono wangu.
“Ni wewe?”. Baba Amara aliniuliza.
“Unamfahamu?”.bibi Amara nae alimuuliza mwanae.
“Mama samahani. Naweza kuludisha hizi pesa na kuondoka”. Niliyasema hayo, nilifungua pochi nilitoa zile pesa na kumnyooshea mkono bibi Amara kumkabidhi zile pesa alizonipa kwaajili ya kulipa deni.
“Mbona sielewi. Na Kwanini uludishe hizi pesa?, Fredrick unamfahamu Mamy?”. Hapo ndipo niligundua kuwa yule Kijana anaitwa Fredrick maana siku Ile tulipogongana gafla na kusababisha simu yake ivunjike sikutambua anaitwa nani.
Fredrick hakujibu swali la mama yake kama ananifahamu.
“Mamy, unamjua baba Amara?”.
“Ndiyo namfahamu ila sikufahamu kama ni baba Amara”.
“Umemjuaje?”. Bibi Amara aliniuliza.
“Ndiye huyu anayenidai”. Muda wote huo Fredrick alikuwa kimya tu.
“Kwamba ni huyu ndiye anayekudai milioni Moja na aliyekudhalilisha?”.
“Ndiyo, mama chukua hizi pesa. Usijali nitapata pesa nyengine na nitamlipa. Naweza kuondoka Sasa”. Niliyasema hayo nilimfuata mwanangu ambaye alikuwa pembeni ya Fredrick nilimshika mkono na kumnyanyua”.
“Ebu subili kwanza, Amara nendeni mkacheze kule kwenye bembea”. Bibi Amara aliyasema hayo. Amara alimshika mkono Aquram na kutoka nae nje.
“Usiniambia kuwa una mdomo mchafu kiasi icho?”. Bibi Amara alimuuliza Fredrick. Fedrick alinyamaza kimya hakuwa na lakuongea mbele ya mama yake.
“Hivi unajua maisha anayoishi huyu Binti mpaka kumpa deni. Alafu MUNGU alivyo wa ajabu mwanao ndiyo amedata Kwa mwanae mwanao amempata rafiki wa kweli na anampenda sana huyu bibi si umeona mpaka anamuita mama?”.
“Mama samahani. Kilichotokea siku Ile ni hasira tu. Kuna mtu alinivuluga”.
“Kwaiyo ukiwa na hasira ndiyo unawasumanga masikini na kujiona wewe ni MUNGU mtu. Unataka Kila mtu akuogope. MUNGU huyu ona Sasa kilichotokea pesa Yako mwenyewe ndiyo ulikuwa unalipwa. Mamy nisamehe mimi kwaajili ya baba Amara.
“I’m sorry”. Fedrick aliyasema hayo.
“Usijali nitakulipa tu kama tulivyokubaliana”.
“Hapana usifanye hivyo tena. Nisamehe kwa maneno Makali niliyokutamkia, ni hasira tu”. Nilinyamaza kimya Wala sikumjibu.
Aliinuka pale sebleni na kutoka nje kwa aibu. Bibi Amara aliniambia hizo pesa nibaki nazo tu ila nilikataa. Nilimkabidhi zile pesa. Alizipokea shingo upande. Amani yote niliyokuwa nayo ilitoweka baada ya kumuona fedrick.
Majira ya saa nane mchana baada ya chakula niliaga kuondoka ila bibi Amara alinigomea aliniambia mpaka jioni ndipo niondoke. Sikuwa na jinsi na watoto nao hawakutaka kuelewa kutenganishwa.
Tulikuwa tumekaa nje ya nyumba kwenye bustani ya maua mazuri bibi Amara alianza kunisimulia maisha ya mwanae ya nyuma.
“Ni Kijana mzuri sana ila hajapat bahati ya penzi la kweli na naweza kusema hajawai kupendwa maana wote anaowapenda wanaishia kumuuliza”.
“Umeniambia mama Amara yupo nje ya nchi muda mrefu?”.
“Yeah. Anaitwa Prisca, mahusiano kati yao yalikuwa ya muda mrefu tangu wakiwa wadogo. Walikuwa marafiki na baadae kuwa na mahusiano. Alibeba mimba kipindi icho alikuwa amemaliza A level na tayari wazazi wake walikuwa wameshamtafutia chuo nje ya nchi. Wazazi wake walipobaini kuwa mtoto wao mjamzito utata ndipo ulianzia hapo. Walichukizwa mno na kupelekea familia zetu kuwa maadui. Hatukuwa na ukaribu wa sana ila tulikuwa tunafahamiana”.
“Basi kesi ilikuwa kubwa sana, wazazi wa Priaca walitaka kumshtaki Fredrick. Kipindi icho marehemu mume wangu alikuwepo ilibidi atumie nguvu ya pesa. Aliwaomba kesho isipelekwe mahakamani, Prisca akijfungua atamsomesha yeye nje ya nchi na Anatoa fine ya milioni tano kwa kitendo alichofanya Fedrick. Wazazi wa Prisca walikubali. Mume wangu aliwapa milioni Tano na familia kubeba jukumu la kulea mimba ya Prisca mpaka pale alipojifungua.
Kipindi Prisca anajifungia Fedrick alikuwa ameshaanza chuo na alisoma chuo nje ya nchi. Basi baada ya Prisca kujifungua tu wazazi wake walianza kuchachamaa mtoto wao apelekwe chuo kama tulivyoahidi hapo mtoto hata arobahini hajafikisha. Tuliomba wasubilie mtoto aache ziwa ila waligoma kata kata, walidai mbona Fedrick anasoma na yeye ndiye sababu ya kumkwamisha mwenzie”.
“Tulitupa miezi mitatu tu na kutuambia Process za chuo zianze. Hatukuwa na namna zaidi ya kukubali tu maana hatukutaka migogoro kabisa na mume wangu alikuwa na ugonjwa wa presha na ndio uliomuuwa”. Mama aliyasema hayo kwa hudhuni huku machozi ya kimlenga machoni.
“Tulimaliza kufanya utaratibu wote, tulimlipia na Ada ya mwaka mmoja na huduma zote za muhimu tulizitimiza. Baada ya miezi mitatu ikiwa imebaki siku Moja tu Prisca asafiri nje ya nchi chuo jioni siku hiyo jioni alikuja na wazazi wake nyumbani. Tuliwapokea vizuri na baada ya mapokezi ndipo alituambia lengo la wao kuwepo hapo ni kumleta Amara maana kesho yake mama yake anaondoka kwaiyo Amara tutamlea sisi maana ndiye damu yetu”.
“Lilikuwa jambo la Gafla hatukutegemea kabisa.
“Kwaiyo mnavyosema ni damu yetu na kumleta hapa ni kwamba hamumtaki huyu mtoto kabisa na mmetususia?”. Mume wangu aliwauliza.
“Unadhani upumbavu alioufanya mwanao ni haki?. Huyu ni damu yenu sisi hatuhusu. Kwanetu anaenda chuo. Hakuna mtu wa kumlea”. Baba Prisca aliyasema hayo. Tulifika mbali mpaka kuandikishana kuwa Amara hawahusu kabisa na siku zote atakuwa upande wetu. Na baada ya hapo waliondoka, Prisca alienda nje ya nchi kusoma”.
“Tuliendelea kugharimu masomo ada na Kila kitu chake na Bado waliendelea kuwa na mahusiano na Fedrick. Baada ya miaka miwili mume wangu alifariki dunia Kwa maradhi ya utu uzima. Baada ya kifo Cha mume wangu aikuchukia muda mrefu Prisca alianza mabadaliko katika kuchunguza tuligundua kuwa amepata mwanaume wa kizungu na wapo mbioni kufunga ndoa. Ilikuwa ngumu Fedrick kukubaliana na ukweli kwamba Prisca sio wake Tena. Mwanangu alimpenda sana yule binti ila ndo hivyo aliishia kumtenda vibaya.
“Nisiwe muongo mwanangu. Fedrick amekuwa muhuni sana baada ya kusalitiwa na Prisca. Anabadilisha wanawake kama nguo, hali hii inaniumiza sana. Natamani aoe awe na familia huenda atatulia ila hataki kabisa kisikia habari za kuoa. Mamy naomba unisaidie kwa hili. Nataka uwe mke wa baba Amara, nataka uwe mama Amara…….
SEHEMU 07
Bibi Amara aliongea hayo kwa masikitiko sana na kuniomba nikubali kuolewa na mwanae.
“Mama kwanini umetaka niwe Mimi na sio wengine?”.
“Kwasababu, kwanza unaonekana ni mtulivu na mwenye upendo sana, heshima na mvumilivu pia. Mwanangu anatakiwa aoe mwanamke mvumilivu haswaa na atakayeweza kumbadilisha”.
“Mmmh!. Naona itakuwa ngumu”.
“Ni kweli na yote ni kwasababu alishakukosea mwanzo. Mamy najua moyo wako umejawa chuki. Unachukia Fedrick kwa kile alichokufanyia. Nisamehe Mimi”.
“Amna mama sio kwamba namchukia ila naogopa kuishi na mwanaume, nawaogopa pia wanaume”.
“Nakupa muda ulifikilie hilo na nakuahidi endapo ukikubali maisha Yako yatabadilika kwa siasi kikubwa sana”. Bibi Amaya aliyasema hayo na niliielewa anamaanisha Nini.
Ilikuwa ngumu kukubali. Fikilia hata wewe, mtu anakusimanga na kukudhalilisha mbele za watu ndo aje awe mumeo kweli?, si ndo atakusimanga na kukuzalilisha sana tu.
Majira ya jioni niliaga ili niondoke na mwanangu.
“Usijali baba Amara alisema atakupeleka”. Mama aliniambia.
“Amna naweza tu kwenda mwenyewe mama Wala usijali”.
“Unamuogopa au kuhofia Nini?. Hawezi kukufanyia jambo lolote lile nishaongea nae”.
“Sio hivyo”. Kabda sijamaliza kuongea mama aliongea yeye.
“Najua usafiri wa dar. Usimsumbue mtoto. Muda umeenda saivi acha akupeleke sawa”.
“Sawa”. Nilikubali shingo upande.
Fedrick alikuja na tayari alikuwa amevalia nguo nzuri. Hapo ndipo niliweza kumuangalia kwa utulivu.
Ni Kijana mzuri mwenye mvuto wa kiume. Navyosema ana mvuto wa kiume namaanisha ana mwili kama Simba. Yaani juu mnene kiasi chini mwembamba(model). Ni handsome balaa na ana macho ya duara mazuri sana kama faru wa jua Kali๐๐.
Story hii mwandishi na mtunzi ni mimi chama HURU . Hii story Haina season ogopa matapeli wanaokata vipande vya story na kuviunga baada ya hapo wanauzia kwa season. Namba zangu za whatsp ——————–.
“Tunaweza kwenda?”. Aliniuliza ndipo nilibaini ana sauti nzuri ya kiume.
“Ndiyo”.
“Haya twendeni wanangu”. Fedrick aliyasema, aliwashika mkono watoto na kutoka nao nje. Miminilifuatia nyuma na mama. Niliagana na mama na kuingia kwenye gari Moja wapo la kifahari.
Safari ilianza huku ukimya baina yangu na Fedrick ukitawali. Walikuwa wanasikika tu watoto nyum ya gari wakiongea kwa furaha wenyewe.
“Umeolewa?”. Fedrick alivunja ukimya na kuniuliza.
“Hapana”. Nilimjibu Kwa ufupi tu.
“Unaishi na nani nyumbani?”
“Na mdogo wangu na huyu mwanangu, hata hivyo maswali Huwa sipendi naomba tuishie hapa na kuhusu Hela Yako nitakulipa tu kama tulivyokubaliana”.
“Sihitaji Tena, hata hivyo huna uwezo wa kunilipa”.
“Kwa sababu ni masikini?”. Nilimuuliza kwa hasira sana.
“Sina maana hiyo ila kipato chako hakikidhi mahitaji”.
“Nitalipa ili niwe huru na niondoke kwenye fedheha. Ni kweli Mimi ni masikini kama ulivyosema ila haimaanishi sina haki wala thamani”.
“Unajieleza sana na maelezo Yako hayana tija. Mamy unaonekane wewe ni mjeuri sana”.
“Yeah ni mjeuri kwa watu kama nyie mnaojiona ni bola kuliko wengine”. Fedrick aliniangalia Kwa tabasumu na kuendelea kuweka umakini na barabara.
Alitufikisha Kona nilishuka kwenye gari na kufungua mlango wa nyuma ili nimtoe mwanangu na kuagana na Amara. Watoto walianza kulia kama kawaida yao. Nilitamani kumpiga Aquram na kumuondoa kuondoka nae ki nguvu ila nilimuhurumia Amara. Muda huo Fedrick alikuwa amesimama kwa kuegemea gari.
“Mama chimamy usiniache”. Amara aliongea hayo huku akiwa analia, Aquram nae alikuwa analia. Niliwatazama Kwa zamu na kushusha pumzi. Nilimgeukia Fedrick nilimkuta sambamba ananitazama.
“Kwaiyo tunafanyaje?”. Nilimuuliza Fedrick.
“Hata mimi sielewi pia. Ikiwezekana twende wote mpaka kwako na baada ya watoto kulala ndipo niondoke na Amara”. Fedrick alishauri hivyo nami sikuwa na budi kukubali.
Tulifika mpaka kwangu ilikuwa majira ya saa mbili usiku. Nilimkuta Sarah ameludi, tulisalimiana na kumuuliza nyumbani wanaendeleaje.
“Wote hawajambo wote wanakusalimia, naona tumepata ugeni?”.
“Acha tu. Kamuuliza anatumia kinywaji gani”. Nilimwambia Sarah muda huo tuliwaacha Fedrick na watoto ndani.
“Si mgeni wako lakini dada, ni vyema ukaenda wewe na anaonekana bishoo mpaka namuogopa”.
“Hana lolote mpumbavu tu Wala usimuogope. Nenda kamuulize kwanza”. Sarah aliingia ndani huko alimuuliza Fedrick anatumia kinywaji gani.
“Hapana sihitaji chochote. Unaonekana ni mkarimu sana kuliko mama Aquram”. Sarah alitabasamu baada ya kumwagiwa sifa. Alitoka nje na kuniambia kuwa mgeni wangu amekaa kunywa chochote.
“Achana nae, anajikuta yeye ndo tajiri wa kwanza dunia nzima”.
“Khaaa! Dada mbona unaonekana una hasira nae sana, alafu kwanza ni nani huyu?”.
“Ngoja aondoke ntakupa kinaga ubaga”.
Tuliingia ndani nilimkuta Fedrick yupo busy na simu na watoto wapo busy kucheza game. Amara alikuja na game lake la mkononi basi hawakuwa na dalili yoyote ya kulala na hata Fedrick alitulia hakuwa na dalili ya kuondoka kabisa……
SEHEMU 08
Sarah ndiye alikuwa kama mwenyewe wa Fredrick walikuwa wanapiga story za hapa na pale kama vile wanajuana. Mie nilikuwa busy nazuga na simu yangu kuperuza mitandaoni.
Saa nne na madakika kadhaa ndipo watoto walianza kusinzia. Nilianza kuwabembeleza mpaka walilala. Baada ya watoto kulala nilimwambia Fedrick anaweza kumbeba Amara wakaondoka.
“Mbona kama unatufukuza?”.
“Hapana”.
“Okay”.
Alimbeba mwanae hao wakaondoka. Ndipo Sarah aliniuliza. Baada ya kumwambia kuwa baba Amara ndiye Kijana aliyekuwa ananidai alishangaa.
“Mbona balaa”.
“Tena sio dogo na mbaya zaidi sikujua kama ni baba Amara na hata bibi Amara hakujua kama ni mwanae ndiye ananidai. Amesikitika sana yule mama hakutegemea kama mwanae anaweza kuwa na kauli mbaya kiasi kile”.
“Kwaiyo mmemalizana vipi?”.
“Ndiyo, ila nataka nimlipe pesa Yale kama tulivyokubaliana.
“Khaaa! Bado anataka kulipwa tu?”.
“Mimi ndo nimetaka kumlipa”.
“Una Hela za kuchezea wewe?”.
“Sipendi dharau, nisipomlipa ataendelea kuniona masikini. Lazima nimlipe”.
“Mh aya”. Tulilala ma palikucha salama asubuhi, nilijiandaa kwenda kazini. Nilifika kazini na kuendelea na majukumu yangu.
Alikuja mteja Kijana mzuri wa kiume. Alipokelewa vizuri na wahudumu yaani wauzaji nguo baada, alianza kuangalia bidhaa. Namna alichokuwa anatembea alikuwa ameweka mikono yake yote kwenye mifuko ya suruali yake macho yake yaliangaza huku na kule.
Katika kutembea huku akiwa anapepesa macho aliniona mie kwa mbali nimekaa maana mie ndiye nilikuwa napokea pesa za mauzo. Baada ya kuniona alinitazama muda mrefu na kutabasamu. Alinisogelea karibu na kunisalimia.
“Habari za majukumu?”.
“Salama karibu sana”.
“Nimekaribia. Naweza kupata nguo nzuri itakayonikaa Bomba na iwe original?”.
“Ndiyo, nguo za hapa ni original kabisa, karibu kujichagulia uipendayo”. Nilimwambia yule Kijana.
“Labda nikuombe kitu kama hutojali”.
“Bila shaka”.
“Naomba unichagulie wewe maana wanawake mpo vizuri kwenye kuchagua vitu”. Nilitabasamu na hata yeye aliniangalia kwa tabasamu.
“Sawa”. Nilichukua jukumu la kumchagulia. Aliniambia anataka Tisheti mbili na jinsi mbili. Nilimchagulia. Alionekana kuzipenda. Alifanya malipo zaidi ya pesa aliyotakiwa kulipa.
“Pesa imezidi sana, ilitakiwa ulipie laki na ishirini tu, umenipa laki na nusu”.
“Usijali, hiyo nyengine utakunywa soda, nimevutiwa na ukaribu wako na pia unaonekana ni muaminifu. Nikutakie siku njema”.
“Asantee sana. Karibu Tena”.
“Nitakaribia”. Kijana yule aliondoka. Siku hiyo ilikuwa na bahati.
Majira ya jioni Bibi Amara alinipigia simu na kuniambia anahitaji muda mzuri wa kuzungumza na Mimi.
“Ni sawa mama, karibu nyumbani kwangu weekend”.
“Nahitaji tukutane sehemu tofauti na nyumbani”.
“Hakuna shida”. Nilikubali ombi lake na baada ya hapo alikata simu. Nilijua tu nini anachokitaka, sikuwa tayari kabisa kuingia kwenye ndoa kwa wakati huo. Niliapia kusimamia msimamo wangu na kuyapambania maisha ya badae ya mwanangu.
Juma mosi jioni kabda ya kufunga ofisi alikuja Tena yule Kijana niliyemchagulia nguo na kunipa Hela ya soda. Kwa mala nyengine Tena aliniambia nimchagulie nguo. Tulianza kuzunguka wote kumchangulia nguo ila mala hii nilikuwa nampimia mwilini mwake. Yaani nachukua Tisheti nampimia kama itampendeza. Nilifanya hivyo huku tukiwa tunapiga story mbili tatu ndipo aliniuliza jina langu”.
“Naomba nikufahamu jina lako kama hutojali sana”.
“Naitwa Mamy”.
“Una jina zuri sana. Naitwa Jerry”.
“Nimefurahi kukufahamu”. Nilimchagulia nguo na baada ya hapo alifanya malipo. Alizidisha tena pesa elfu hamsini na kuniambia iliyozidi nitafanya ya soda.
“Naweza kupata mawasiliano Yako?”. Aliniuliza.
“Yeah”. Alinipa simu yake nikamuandikia namba yangu na baada ya hapo alinibeep na kuniomba nisave namba yake. Nilifanya hivyo. Aliniaga na kuondoka.
Jumalipi ndiyo ilikuwa weekend yenyewe ambayo nilitakiwa nikutane na bibi Amara kwaajili ya mazungumzo.
Tulikutana kwenye Moja ya hotel ya kifahari tukiwa wawili tu, mimi na yeye. Baada ya Salam maongezi yalianza huku tukiwa tunashushia na vinywaji.
“Mwanangu uniwie radhi ila si kwa ubaya. Mamy naomba uwe mkwe wangu. Naomba ukubali kuwa mama wa Amara. Mtoto anasumbua anakutaka wewe na mwanao, mjukuu wangu ametokea kukupenda sana. Tafadhali usiangalie makosa ya baba yake. Mtoto anahitaji upendo wako, ametokea kukupenda na mbaya zaidi hamjui mama yake kabisa. Kuna muda anasumbua anataka kuongea na mama yake ila ndo hivyo Hana ukaribu na mama yake kabisa”.
“Naomba ukubali kumlea Amara na kumfanya kama mwanao, naamini wewe ni mwanamke mzuri utakuwa mama Bora kwake”.
“Ni sawa ila mimi kuolewa na Fedrick hapana, naolewaje na mwanaume nisiyempenda?, si sawa na kujikatili mwenyewe?. Hata Fedrick pia hanipendi na hajawai kunipenda”. Nilimwambia bibi Amarah.
“Najua ila ushawai kuona chuki unaozaw upendo au kusikia?. Watu wanaochukiana ndio wanapendana. Tafadhali Mamy kubali mwanangu akuoe ili uwe mama wa mjukuu na wajukuu wangu”. Mama aliyasema hayo na kunipigia magoti kabisa. Hakuona aibu kunipigia magoti mbele ya watu. Nilijisikia vibaya mno. Nilipotaka kumuinua alikataa na kuniambia endapo nitakubali kuwa sehemu ya maisha ya familia yake basi atainuka. Nilibaki njia kuu nisielewe nini nichague.
“Endapo utaona nafaa na Mimi kusikilizwa basi naomba uinuke mama yangu tuzungumze kwanza”. Niliongea hayo kwa sauti ya unyenyekevu. Bibi Amarah aliinuka na kuketi kwenye kiti na mimi pia nilikaa.
“Niambie umekubali?”. Aliniuliza, niliinamisha kichwa chini na kufikilia kwa muda mrefu.
“Hapana ila nipo tayari kuishi nae nyumba Moja kwaajili ya kumlea Amarah, kuolewa na Fedrick haiwezekani. Mama ndoa ni makubaliano na malidhiano kati ya wapenzi wawili na sio kama tunavyotaka kufanya. Endapo nitamlidhia na yeye kuniridhia tutafunga ndoa ila Kwa Sasa tujipe muda……
SEHEMU 09
Niliongea hayo kwa sauti tulivu na ya kumsihii msikilizaji anielewe. Bibi Amarah alikuwa makini kunisikiliza na baada ya kumaliza kuongea ukimya wa sekunde kadhaa ulipita. Bibi Amara alivunja ukimya na kuzungumza.
“Ni kweli upo sahihi na nimekubaliana na maamuzi Yako”.
“Nashukuru kwa kunielewa”.
“Kwaiyo upo tayari muda wowote kuishi nyumbani kwa Fedrick?”. Nilifikilia kwa sekunde chache na kumjibu.
“Ndiyo nipo tayari ila kama mwenyewe atakubali”.
“Sawa na kuhusu Fedrick usijali, Hana shida. Nataka niondoke ndo maana nimetaka uwe mama wa mjukuu wangu, ili nitakapoondoka nijue kabisa mjukuu wangu yupo mikono salama’.
“Hakuna shida mama”. Baada ya mazungumzo tulikubaliana mimi na familia yangu kuamia Kwa Fedrick. Tuliondoka pale hotelini mimi nililudi nyumbani.
Nilipofika tu nyumbani simu yangu iliita mpigaji alikuwa Jerry kama nilivyoisave namba yake. Nilipokea na kuweka simu sikioni.
“Hello mamy!”. Nilisikia sauti ya Jerry kutoka kwenye simu.
“Hello, habari?”.
“Salama mzima Mamy?”.
“Nipo salama sijui wewe”.
“Jambo la heri, nami pia nipo salama mamaa!”.
“Niambie rafiki yangu”.
“Nilikuwa nakusalimia, nimekumiss mno”. Niliguna na kujionea maajabu. Ila kwakuwa najua janja janja za wanaume ni kuishi nao kwa akili sana.
“Asante Sana. Basi nikutakie usiku mwema maana nimechoka sana Leo nahitaji kupumzika ili kesho niwai kazini”.
“Okay my dear. Goodnight”.
“Na kwako pia”. Nilikata simu na kuitupia pembeni. Baada ya muda Sarah alikuwa amemaliza shughuli zake tulikuwa tumekaa sebleni ndipo nilimwambia kuhusu kuamia Kwa Fedrick. Sarah alifurahi sana.
“Mbona umepagawa?”.
“Nikuulize labda”.
“Uliza?”.
“Unampenda kwani Fedrick?”.
*Khaaaa! Wee Sarah wewee!, naanzaje kumpenda mjinga yule. Yaani ni kwaajili ya heshima tu ya mama yake ndo maana nimekubali ila bila hivyo nisingekubali”.
“Basi vizuri dada. Mie mwenzio tangu nimuone alipokuja home nimechizika mwenzio wallah moyo wangu umezama kwake”. Sarah aliyasema hayo akiwa anaanisha kile asemachi. Nilibaki mdomo wazi tu.
“Haswaaa!”.
“Huo ndo ukweli dada, na bola tunaenda kuishi nae huenda nitakuwa mke wake na mama wa watoto wake”.
“Ujue una hatari wewe?”.
“Hatari gani dada?, kwani kumpenda mtu ni dhambi?”.
“Hapana sipo tayari uwe na Fedrick. Sipo tayari kabisaa!. Fedrick sio mtulivu kabisa atakuchezea na kukuacha”.
“Wee umejuaje?, au ushalala nae?”.
“Sarah wewe Bado mdogo japo hatujaachana miaka mingi ila Mimi nimekutangulia na nayajua mengi sana kuhusu wanaume. Mpaka Sasa Nina miaka 21 ila nimepitia heka heka za Kila aina, unadhani mwenzio niliwai kuwaza au kupanga kuzaa nje ya ndoa, au kuzaa na mvuta Bangi?, tulia mdogo wangu utapata mwanaume mzuri na mwenye Nia ya kukuoa kabisa”.
“Lakini dada mbona Fedrick ni mzuri na ana pesa tu. Kwani hafai kuwa mume wangu?”. Maswali ya Sarah yalikuwa yanaboa aiseee ila sikutaka kumjibu Kwa hasira na sikutaka anitafsili tofauti.
“Sawa. Kama unaona ni mzuri na anafaa kuwa mume Kila laheri nakuombea, ila tunapoenda kuishi kule naomba uwe mtulivu na kama ulivyosema unampenda ni sawa ila tafadhali sana usijirahisishe mdogo wangu kwa mwanaume. Hii itatuaribia sifa wote mimi na wewe na hata familia pia”.
“Nimekuelewa dada usijali”. Nilimaliza kuzungumza na Sarah nilikuwa hoi maana mtoto alionyesha uchachari sio pw.
Kesho yake ilikuwa jumatatu. Nilijiandaa na kwenda kazini. Majira ya jioni saa 12 mfanya kazi mwenzangu alikuja eneo langu la kazi na kuniambia kuwa Kuna mtu ananiita nje yupo kwenye gari.
“Unamfahamu?”.
“Yeah sura yake si ngeni wewe nenda utamjua tu”. Nilitoka nje na kweli niliona gari jeusi limepaki pembeni na duka. Nililisogelea na kulifikia karibu. Baada ya kulifikia lile gari vioo vilivyofungwa vilishushwa ndipo nilimtambua mtu yule ni Jerry.
“Onhooo! Kumbe ni wewe boss?”. Niliongea hayo.
“Ndiyo ila haifai kuniita hivyo na ikiwa unajua jina langu jamani. Sasa Nina u boss Gani mimi”.
“Kuitwa boss sio zambi hata hivyo unastahili pia”. Niliyasema hayo.
“Tuachane na hayo mamy. Ingia basi kwenye gari nmazumzo na ww kidogo”. Niliingia kwenye gari bila hofu.
“Mnafunga saa ngapi hapa?”.
“Muda si mrefu”.
“Okay!”. Alitoa wallet na kutoa elfu kumi kadhaa kwenye wallet.
“Shika hii”.
“Ya nini Jerry?”.
“Wee zipokee kwanza”. Nikizipokea zile pesa na kuendelea kumtazama Kwa macho ya kiulizo.
“Badae nataka kutoka na wewe kwenye party ya rafiki yangu. Naombabupendeze na kama pesa itakuwa ndogo niambia nikuongeze”. Nilibaki nimetoa macho tu maana imekuwa gafla sana alafu Sasa pesa aliyonipa ni nyingi sana. Kwa kuniangalia kwa macho tu haikuwa chini ya laki tatu.
“Mbona ni gafla lakini Jerry na kwanini umenichagua Mimi?”.
“Kwasababu nimeona ww unafaa, tafadhali usinikatalie na pia usiniamgushe Mamy”.
“Ni saa ngapi party yenyewe?”.
“Saa nne usiku inaanza”.
“Muda ni mbaya sana, siwezi kwenda nitachelewa sana kuludi na pia kesho kazini”.
“Usijali kuhusu kazi na kesho utaingia mapumziko maana najua utakuwa umechoka sana”.
“Mbona unaongea kirahisi hivyo Jerry?, mie nimuajiliea.
“Najua, na Mimi ni muajiri pia. Usijali mamy na pia niamini sawa?”. Nilimtazama Jerry machoni ila sikuwa na ujasiri wa kuendelea kumtazama zaidi baada ya kukutanishana macho kwa macho. Nilijikuta nakubali tu mwenyewe……
SEHEMU 10
Baada ya kukubali Jerry aliniambia tushuke kwenye gari tuingie dukani. Tulishuka na kuingia dukani. Alianza kunichagilia nguo, viatu na baada ya hapo aliniambia nipige mahesabu ya dukani then duka lifungwe coz ashaongea na boss wangu.
Sikutaka kumuelewa kilahisi. Nilimpigia simu boss na kumuuliza kama Kuna ruhusa nimepatiwa kutoka kwake.
“Yes ila kuwa makini sawa?”.
“Sawa”. Baada ya kumaliza kuongea na muajiri wangu. Nilipiga maheshamu na baada ya hapo tulifunga duka. Tayari ilikuwa saa 12 na nusu. Jerry alinipeleka mpaka mtaa naoishi, nilishuka kwenye gari. Aliniahidi saa tatu usiku atanifuata na nihakikiahe nimependeza haswaaa.
Nililudi nyumbani, nilimwambia Sarah namtoko wa gafla. Alihoji na hofu yake alijua labda mtoko wangu unahusiana na Fedrick barafu wa moyo wake ๐๐.
“Unajua kabisa mimi na Fedrick ni panya na paka Sasa presha ya Nini mdogo wangu?”
“Sasa ni nani unatoka nae usiku huu mpaka amekufanyia shopping?”.
“Ni rafiki yangu. Hutakiwi kuwa na presha bhana”.
*Sawa”. Alikubali ila hakuwa na amani na hilo nililijua na mumpuuza kwakuwa utoto ulikuwa unamsumbua.
Nilipomaliza kuoga nilivaa zile nguo zilinipendeza sana. Nilibeba pochi yangu nikaelekea saloon. Huko nililembwa mtoto wa kike. Nilipendeza balaa. Baada ya kuhakikisha nimependeza maana milisisitizwa mala mbili mbili hakikisha umependeza sana nami sikutaka kuwa mzembe maana pesa nimepewa.
Saa tatu na dadika kadhaa simu yangu iliita na muda huo ndio nilikuwa nimemaliza kupambwa. Mpigaji alikuwa Jerry, nilipokea na kuweka simu sikioni.
“Sawa nipe dakika tano nakuja”. Nilimwambia Jerry na baada ya hapo nilijitazama Tena kwenye kioo. Nyie nilipendeza sio pw, nilitoka saloon na kwenda alipo Jerry.
Kwa mbali nilimuona Jerry kasimama nje ya gari. Aliponiona jicho likamtoa mtoto wa kiume. Baada ya Jerry kuniangalia kwa macho flan hivi nilipoteza umakini wa kutembea si nikajikwaa bhana. Nilipepesuka na viatu nilivyovaa ni virefu ilikuwa kidogo nianguke ila nilijikuta mikononi Kwa Jerry. Namna alivyonidaka nyie ilikuwa ni kama muvi za kihindi ๐๐.
Tulitazamana machoni huku Jerry akiwa na tabasamu hafifu usoni mwake. Jicho lake Sasa nyie alikuwa ananitazama kwa macho flani hivi mpaka nilijionea aibu na kuinamisha macho yangu chini.
Jerry aliniinua na kuniuliza.
“Upo sawa Mamy?”
“Ndiyo, Asante”. Niliyasema hayo huku nimeinamisha kichwa chini.
“Aiseee wewe mwanamke ni mzuri sijapata kuona, kumbe aijakosea kukuchagua kabisa. Umependeza sana. Nilivyokuona kwa mbali nilikupotea kabisa.
“Uongo huo Jerry”.
“Kweli Mamy, ebu panda kwenye gari tuwai kwanza”.
Tulipanda kwenye gari na safari kuelekea kwenye party ilianza. Humo kwenye gari Jerry hakuchoka kuniangalia na kunisifia.
Gari lilisimama kwenye Moja ya hotel nzuri ya kifahari. Jerry alifungua mlango na mimi nilitaka kufungua ila Jerry alinizuia na kuniambia atanifungulia yeye. Ilibidi nitulia. Jerry alikuja kunifungulia mlango na baada ya kushuka garini aliongea machache kabda ya kuingia ndani ya hotel ambapo Kuna party.
“Mamy Cha kwanza kabisa naomba uwe jasiri, humo ndani Kuna watu wengi sana, pili naomba tuongozane kwa kushikana mikono”.
“Ni sawa hakuna shida”. Jerry alinishika mkono, tulitembea kuelekea lango kuu la hapo hotelini.
“Tuliingia ndani na Moja kwa moja tuliongoza mpaka ulipo ukumbi. Tuliingia ndani ya ukumbi ni kweli watu walikuwa wengi sana na mpaka muda huo sikujua ni party ya Nini.
“Unaogopa?”. Jerry aliniuliza.
“Hapana”. Alitabasamu na kuniachia mkono. Aliupitisha mkono wake kiunoni kwangu hali iliyonishtia mshtuko wa wazi wazi. Kabda sijautoa mkono wake nilimtazama nilikuta naye ananiangalia. Alinipa ishara ya kwamba niwe mtulivu.
Tuliongozana mpaka kwenye Moja ya meza waliyokaa watu wengi wanawake Kwa moja wanaume walinizunguka meza Ile. Jerry alinisogezea kiti. Taratibu nilikaa na kumsalimia wa pembeni yangu nilishtuka Kwa kushika mpigo ya moyo wangu almanusura presha ipande๐๐.
“Khaaaa wewe, umefata nini huku?”. Fedrick aliniuliza huku akiubana mkono wangu Kwa vificho watu wasitushtukie.
“Onhoo bwana Fedrick, habari?”. Jerry alimsalimia Fedrick haraka aliniachia mkono wangu. Nilihisi maumivu maana alinishika Kwa nguvu.
“Salama kabisa, naona ndo unafika broo”.
“Yeah ndo tumefika saivi na shemeji yako hapo”. Fedrick aliniangalia mie sikutaka hata kumuangalia hapo mapigo ya moyo yalikuwa juu sio pouwa na hata sijui nilikuwa naogopa Nini maana mimi na Fedrick hatujawai kuwa na ukaribu wa kimahusiano hata urafiki.
“Mamy huyu ni rafiki yangu anaitwa Fedrick”.
“Sawa”. Nilijikaza na kujibu hivyo.
“Fedrick ni shemeji yako huyu”.
“Sura yake si ngeni sana au huenda nimemfananisha?, eti Mamy nimekufananisha?”.
“Ebu acha kumzingua Shemeji ako”. Jerry alijibu akiamini Fedrick alikuwa anatania tu pasipo kujua tunafahamiana. Shughuli ilianza, ilikuwa sherehe ya kuvishwa Pete ya uchumba. Rafiki yake Jerry alikuwa anamchumbia mwanamke.
Shughuli ilienda vizuri ila upande wangu sikuwa na uhuru kabisa maana Fedrick alikuwa amenitawala Kila niendapo mimi na Jerry naye yupo pembeni yenu. Basi Kuna muda Jerry alienda msalani hapo ndipo Fedrick alinishika mkono kwa nguvu na kunivuta mpaka nje ya Hotel. Aliniingiza kwenye gari kwa bavu na kuliondoa hapo hotelini Kwa speed ……
Yule wapembeni yangu hakuwa mwengine Bali ni Fredrick. Muda huo na Jerry nae alikuwa ameshakaa pembeni yangu upande wa kulia alafu Fedrick alikuwa upande wa kushoto
INAENDELEA

