USIKU WA KAFARA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 3
Neema alichelewa kwani kabla ya kurudi ndani ya gari alifikiwa na mzee juma ambae alimshika na kumvutia kifuani kwake
“Mtulie msije mkafa kabla ya wakati …kijana mmoja amfunge aliekuwa chini na mwingine amtoe huyo kinyago alie bakia kwenye gari”
mzee juma aliongea akiwa kamkumbata neema kwa nyuma ya mgogo na muda huo misuli ya maumbile yake ikimsimama kuwa sambamba nyuma ya mak*lio ya neema.
Dolla alikuwa kama ana karibia kupoteza fahamu kwa kuto kuamini anacho kiona na muda huo kijana alieshika panga na kamba alijipenyeza ndani ya gari kumchukua
“niacheee” dolla alipiga ukelele mdogo
“wewe nitakucharanga kama kuni utulie” yule kijana alimfokea dolla kisha dolla hofu ikamtawala akakamatwa na kufungwa kamba mikononi mwake na kushushwa chini…
Tayari mzee juma alishakutwa na hamu ya kumuingilia neema lakini alihofia kwenda kinyume na amri ya yule kiumbe mkongwe walio muita jina la malikia na mzee juma alijua wazi yote yale wanayo yafanya pale yalionwa wazi na malikia….
” Haya fungeni na huyu nyau kisha muwaonganishe tuondoke….wewe mpumbavu acha kelele zako za kulia kama mtoto nitamuua yoyote kati yenu ambae ataongea au kuujiliza” mzee juma aliongea na kumsukumiza neema huku akimkemea baraka aliye kuwa ana ugulia maumivu ya kuchomwa kwenye paja..
Wote walifungwa mikono yao kwa ustadi mkubwa kisha mzee juma akakata mti mrefu kisha waka msimamisha baraka na dolla kisha wakaufunga mti ule kwenye shingo ya baraka kisha ukafuata kwa dolla na kumaliziwa kwa neema , mti ule ulifungwa shingoni mwao hivyo wote walikuwa wamefungwa kwenye mti mmoja .
Kisha wakainuliwa kwa pamoja mti mmoja mrefu ukiwa umepita pembeni mwa shingo zao zilizo fungwa kwa kamba ipasavyo.
mze juma aka msogelea baraka kisha akauchomoa kwa nguvu ule mshale kutoka kwenye paja la baraka ,hapo baraka alishindwa kuvumilia alipiga kelele za uchingu.
“kwani jamani tume wakosea nini” neema aliuliza lakini hapohapo kofi zito la mzee juma lilitua shavuni pake nae akalia kwa uchungu.
“Nime waonya sitaki hata kidogo kusikia mkiongea nita wa chinja….. haya ongoza safari ianze” sauti ya kikatili ili wa fokea …wakaanza kutembea kwa mstali ulio nyooshwa na ule mti ulio lalia mabega yao huku baraka akiwa mbele akitembea kwa kuchechemea na maumivu makali yakiukumba mguu wake…
Maskini baraka!
Ikawa vijana wawili wanawaongoza mbele huku nyuma wakifuatiwa na mzee mkatili …naam mzee juma.
****************
Gady hakuwa na ujanja wowote wakati akiwa pale chini akamuona kijana mwingine wa kundi lile la mbweha akifika eneo lile kwa nia ya kumsaidia muhaini mwenzake.
“Nilidhani anaendelea kukimbia…. kumbe ulisha mdhibiti….” aliongea yule haini bweha
“ah hana ujanja huo” yule aliempiga gongo gady alijibu na haraka waliifunga mikono ya gady kwa mbele kiustadi kisha wa wakamuinua
“yule mwingine yupo na shija anapelekwa kwa njia ya mkato na wewe mpeleke huyu kwa njia hiyo mimi naenda kumuangalia mzee juma kwenye gari lao”haini yule aliongea akimaanisha tayari john kaushaanza kuongonzwa kuelekea kwa goroza kwa njia ya mkato
“sawa naona tutakutana makao makuu” mwenzake alijibu na wakaachana….
Gady akiwa chini ya uangalizi wa haini mmoja aliekuwa na shoka kali ,gady akasurutishwa kutembea kuelekea kwenye pango la goroza.
safari ikaanzq
Ndio mbweha hawa binadamu ambao ni vibaraka wa goroza walifanikiwa kuwanasa vijana watano akasalia sarah aliekimbizwa na dalu…..
*************
Sarah alikimbia kwa mwendo ambao kwa hakika kama angekuwa kwenye mashindano ya riadha basi hatu hussein bolt bingwa wa mbio asinge weza kumfikia sarah..
Sasa sarah alikimbia bila kupiga yowe wala kuita msaada aliacha kupiga yowe baada ya kujua anapoteza pumzi na kelele zile zinamfahamisha adui yake sehemu alipo.
Kuna wakati sarah aligeuka nyuma na hakumuona yule alie mkimbiza..na alipo zidi kutokomea sarah akakiona kichaka kikubwa haraka sarah akaingia mule huku akihema akiwa kalala kifudi fudi akihisi pumzi zikimuishia ….
palikuwa kimya sana…
Kimya kile kilimaanisha mtu alie mkibiza hakuwa kabisa eneo lile , sasa sarah akawa anawaza afanye nini ndani ya msitu ule…
Lakini kabla hajafikiria mengi macho yake yakamshuhudia dalu mbali kidogo na kichaka kile akiwa na panga akiangaza huku na kule huku akiwa kajikunja kutokea kiunoni..
Kumbe dalo alikuwa ana msaka sarah kwa kumvizia na mawindo yaliyo tawaliwa na ukimya wa hali ya juu..
Macho yalimtoka sarah na muda huo alisikikia sauti ya kuburuzika kwa kitu pembeni yake alipo angalia alikiona kitu cheusi kirefu kikiburuzika taratibu…
Alikua ni nyoka..!!!!! hakuwa nyoka au kijinyoka bali lilikuwa ni joka!
Lahaula!!!! mbele yake kuna dalu na pembeni yake kuna joka refu….like share ije mapema…
“Nakufa ..” neno hili lilipita kichwani mwake….ilikuwa ni bora akamatwe na dalu kuliko kufa kifo cha kugongwa na nyoka…
Sarah alijibiringisha kwa kasi na kutokea upande wa pili wa kichaka huku joka lile likimkosakosa kumgonga nalo likitanabahi na kurusha mate…na muda huo sarah alishatoka nje ya kichaka na kutimua mbio .
Hii ikawa salama kwa sarah kuliepuka joka lile lakini kwa kulikwepa joka lile sarah akawa kajianika wazi na kumfanye adui yake amuone….naam dalu alimuona saraha akikimbia…
“Mjinga unasumbua leo utazaa namimi hukuhuku” dalu alifoka huku akiwa ana mkimbiza sarah tayari dalu alishapata matumaini ya kumkamata…
Sarah alihamaki huku akiendelea kutimua mbio akibadili uelekeo na akiurudi upande wa barabara.
*****************;**
Gadyson alitembea nyuma akifuatiwa na yule haini alie shika shoka kali, wakati anatembea gadyson kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka chini kama mzigo yule haini akamfokea huku akimuinua gady alipo anguka pale chini aliinuka na kipande kidogo cha mti chenye unene wa vidole viwili akawa kakifumbata kwa mikono yake miwili iliyo fungwa .
“Tembea kiume nyang’au wewe” yule haini alimfokea gady huku akimsukuma atembee.
Gady alitembea kama hatua kumi kisha akaanguka tena na muda huu alijingusha makusudi! na alivyoanguka alijipindua chali…
“wewe mshenzi unanitania” yule haini aliongea kwa hasira huku akimuinamia gady ili aikamate shingo ya gady…
Wakati yule haini anainama gady nae alisukuma juu mikono miwili ilio shika kipande cha mti huku huku shabaha yake ikiwa imelenga uso wa haini..
Yule haini alikuaa kafanya kosa kumuinamia gady aliye lala chali.!
Wakati anainama alikutana na kipande cha mti ambacho kilizama kwenye jicho lake ! akashindwa kulizuia yowe huku akiachia chini shoka lake na mikono yake yote ikienda kwenye jicho lilitobolewa na kipande cha mti ,haini yule akapepesuka na kutanga tanga akikabiliana na maumivu makali kutoka kwenye jicho ambalo muda ule halikuwa jicho tena ila chongo lilio vuja damu.
Shambulizi la gadyson lilikuwa limefanikiwa !
Gady akabilingita mpaka kwenye ile shoka akaishika na kusimama nayo haraka akiwa kaishika kwa style ya kushambulia..akimtazama adui yake aliehangaika kutafuta njia ya kukimbia huko yowe la mtu yule likizidi kuamsha viumbe vilivyo kuwa mstuni mule..
Gady akapiga hatua kumsogelea adui yake na kuinua shoka gady akamshumbulia kwa kumpiga shoka na kumnyamazisha kabisa, mwili wa kibaraka wa goroza ukaanguka chini huku koromeo lake liki mwaga damu!
shoka lilikuwa lime chimba shingo yake na kuli kata koromeo.
Pakawa hakuna yowe wale kelele zaina yoyote kilicho sikika pale ni mtiririko wa damu na sauti hafifu ya mkoromo kutoka kwenye koromeo la bweha haini kibaraka wa goroza…
Gady alikuwa ameua! akawa kasimama na shoka liliotiririka damu likiwa kwenye viganja vya mikono ilio fungwa.
Haraka haraka akazikata zile kamba alizofungwa kwa kutumia shoka lile kisha akaondoka akikikimbia akiwa na shoka akiuacha ule mwili ukitokwa na damu.
Hakujua nini kimetokea kwe nzake na sasa alikuwa anakimbia kutafuta msaada na njia ya kuokoa maisha .
Alikuwa hajawahi kumjeruhi mtu kwa siraha tangu azaliwe lakini leo amejikuta amemshambulia adui yake na kumuondoa uhai wake kitu hiki kikamfanya akimbie akiwa kachanganyikiwa, wakati akikimbia alijikuta akivuka barabara huku akikimbia bila kujua alijikuta kaitambuka barabara na kuingia upande wa pili wa wa msitu ule huku akizidi kutimua mbio.
Hatimae akahisi kuishiwa pumzi ikamlazimu aanze kutembea huku akitweta…
Wakati akitembea ghafla akahisi vulumai likija kutokea nyuma yake ,alipo geuka aliwaona watu wawili wakija upande wake huku waki kimbia mbio kana kwamba walikuwa kwenye mashindano wakiwa umbali wa hatua zisizo zidi miamoja na kumi wakija upande wake…
Gadyson kuona hivyo alipiga hatua moja kubwa mpaka nyuma ya mti mkubwa akajificha pale kisha akachomoza kichwa chake kidogo akichungulia kule walipo tokea wale watu, akaona bado wana kuja upande wake.
ikamlazimu gady kubaki pale nyuma ya mti huku akiwatazama watu wale ambao walizidi kuja upande wake ,na mara wakakalibia.
“sarah…” gady alijikuta akilitaja lile kwa sauti ya chini baada ya kumuona mmoja kati ya wale wawili aliofukuzana wakija upande wake.
Kumbe watu wale walikuwa ni sarah na dalu…
dalu alikuwa anaendelea kumkimbia sarah huku akikaribia kabisa kumkamata.!
Gadyson akamuona sarah akipita mbele ya ule mti aliojificha yeye na muda huo huo macho yake yakamuona dalu aliekuwa na panga akimkimbiza sarah wakiwa karibu kabisa.
Hapo gadyson akatambua sarah anafukuzwa na mtu mbaya, dalu alipopita tu ndipo gadyson nae akaingilia mbio zile huku yeye gady akiwa nyuma ya dalu..
Haikupita dakika gadyson alimkalibia kabisa dalu kisha gady akainua shoka lake na pigo zito la shoka lilitua kichwani kwa dalu !
Dalu akajikuta akianguka chini huku akishindwa hata kupiga kelele wala kuomba maji .
Sarah alisikia mtu akianguka lakini sarah hakutaka kusimama
“Sarah simama nishammaliza huyu mimi ni gadyson” gady alipaza sauti
sauti ilimfikia na kumshitua sarah ikamlazimu ageuka ndipo akamuona dalu akiwa chini huku gadyson akiwaamesimama imara.
“Gadyson ” sarah aliita kuhakiki alichokisikia
“ndio nimimi” gady aliitaka huku akimalizia kumuua dalu
“nini kimewatokea..” gadyson aliuliza huku akimsogelea sarah
sarah hakujibu ila alimsogerea gady ubavuni kwake na kuanza kulia
“tupo kwenye hatari bora nisinge kuja huku” sarah alilia na kumsimulia jinsi walivyo vamiwa kwenye gari na yeye alivyo kimbia.
“sijui hawa watu wa ains gani …hata sisi tulikamatwa ila mimi nilijitetea wamemchukua john…sarah tuondoke kwanza eneo hili sio eneo zuri” gady aliongea kisha akainama na kuchukua shoka yake shoka ambayo tayari ilisha dhurumu uhai wa vibaraka wa wili wa goroza..
Gady akamshika mkono sarah na kuondoka nae kutafuta sehemu nzuri!
Sasa mwezi ulizidi kung’aa mstuni mule na kufanya mtu kuonekana kirahisi ,gady na sarah wakatembea kwa muda wanusu saa mpaka walipofikia sehemu ambayo haikuwa na miti mingi na wakasogea chini ya mbuyu mkubwa wakakaa wakiwa wamechoka..
“Hapa sijui wenzetu kimewakuta nini …sijui tuelekee upande upi ili tutokee kijiji jirani yaani sielewi kabisa” gady aliongea akiwa kachanganyikiwa.
“Kwani hatuwezi kurudi kwenye gari letu tulichukue na kuondoka maana kwa muda tuliokaa litakuwa lisha poa” sarah alitoa ushauri
“wewe hauoni kama tutakuwa tunachezea roho zetu..kama tutakuta hawa watu tusio wajua wapo kwenye gari” gady aliongea kisha akajikuta anajikosoa mwenyewe
“ila kuwakuta sio rahisi maana nilimsikia mwenzao akisema wana tupeleka makao makuu yao ..ila mbaya zaidi nakumbuka funguo yenyewe ya gari baraka aliitia kwenye mfuko wake wa suruale” gady aliongea na hapo moyo wa sarah ukaingiwa na hali ya kukata tamaa…
Kimya kikapita…
“Ila gady nakumbuka mchana uliniambia umetokea kunipenda” sarah alivunja ukimya na gady akapata hali ngumu kidogo kwenye kujibu swali lile
“nd..ndio”
“Naomba ukafanikiwa kutoka humu salama fika nyumbani uwaeleze yote juu ya safari hii na kifo kitakvyo nikuta” sarah aliongea kwa majonzi akiwa hana tumaini akijihisi mkosefu kwa wazazi wake kwa kutowashirikisha safari ile , alijua mpaka muda ule wazazi wake wanahangaika kumtafuta kwa kumpigia simu.
“ah usiseme hivyo lazima tutoke humu salama” gady alisema huku akimkubatia kwa nguvu sarah wote machozi yakiwatoka
“nikuambie kitu gadyson”
“niambie sarah”
“MBEZI “B” NYUMBA NAMBALI 1002 HAPO NDIPO KWA WAZAZI WANGU NIKIFA FIKA UKAWAAMBIE YOTE YALIO TUSIBU KWENYE HII SAFARI NILIO WAFICHA” sarah aliongea kwa hudhuni..
“Ah usiseme hivyo sarah…” gadyson alishindwa kumalizia kauli akihisi donge zito likimkaba kooni wakabaki wamekumbatiana pale.
Tayari walikuwa wamesha maliza dakika thelathini wakiwa chini ya mti ule wakitawaliwa na majonzi….
Kwa mbali hatua kama miatatu gady alimuona mtu kwa mbali akitembea huku mtu yule akiwa kambeba mtu mwingine mabegani kwake ,moyo wa gady ukashtuka akamuonesha mtu yule sarah
“atakuwa nani yule au atakuwa baraka na john ?” sarah aliuliza
“ah itakuwa..sasa wewe baki hapa mimi niwanyatie nijue ni kina nani…usijali utakuwa salama” gady alimbembeleza sarah
“kuwa makini mpenzi..” hah! sarah alijikuta akimuita mpenzi gady …gady hakuamini .
wakabaki wametizamana kwa upendo kisha midomo yao ikakutana kila mtu akashindwa kuzuia hisia zake kwa mwenzake..
“sarah subiri nakuja” ikamlazimu gady kujitoa katika busu zito kwani hawakuwa mazingira salama.
Gady alimuacha sarah pale nayeye akiwa kashika shoka alianza kumnyatia yule mtu alie beba binadamu begani ,
gady alikuwa akihama mti hadi mti na hatimae alianza kumalibia yule mtu!
Ghafla akamuona yule mtu akisimama na kumtupa mtu alie mbeba begani kisha kuondoka !
ile nadharia ya kuwa huenda mtu yule alikuwa mwenzao ikamtoka na kuhisi yule ni adui …gady son akasubiri yule mtu alipo ondoka nakutoeka kabisa .nae gady akanyata mpaka pale …. gady hakuamini macho yake baada ya kufika eneo lile!
Kumbe kulikuwa na shimo na ndani ya shimo gady aliziona maiti mbili ikiwemo moja ilio tupwa na yule mtu.
Gady alipoangalia kwa makini alitambua miili ile ilikuwa ni miili ya baraka na john!
Gady alikumbwa na hali ya kuto kuamini ilimtawala akaliachia shoka lake chini kisha akaingia ndani ya shimo lile fupi hata bila ya kufikiri.
Machozi yalimtoka huku akishudia miili ya rafiki zake wakiwa wamekwisha kuawa kwa kuchinjwa sasa gady alijua wazi wapo kisiwa cha umauti.
Mara akaiona funguo ya gari ikiwa kwenye luksi ya suruale ya baraka na hapo wazo la kujikomboa likamrudia haraka akaichukua funguo ile kisha akatoka mule shimoni .
Ile anatoka tu shimoni akakutana na ugeni mpya machoni pake!
Mbele yake kulikuwa na mtu alikuwa na amemulekezea mshale uliovutwa ipasavyo kwenye upinde wa kibaraka wa goronza….
“hakuna atakae pona kati yenu usiku huu” yule mtu aliongea akiwa anazidi kuvuta ule mshale kumlenga gadyson.
Balaaaa
Sasa gady akajuua amekutana nakifo na huenda ulikuwa ndio mwisho wake.
“tume wakosea nini ” gady aliuliza
“subiri utajua ukifika kuzimu” yule mtu mwenye upinde akamfokea
muda huo macho ya gady yaka muona sarah kwa mbali akija kwa kuvizia , gady alihamanika akatamani amwambie sarah akimbie!
Yule kibaraka wa goroza akaona hamaniko la gady kibaraka yule akajua lazima nyuma yake kutakuwa na kitu ikamlazimu kibaraka yule ageuke kujua nyuma yake kuna nini.
Kosa kubwa!!!!
Sehemu Ya 4
Kibaraka yule alifanya kosa kugeuka, kwani alivyogeuka tu gady ali mrukia na kumzoa wote waks jibwaga chini upinde na mshale vikaanguka pembeni huku wao wakibiringita huku kila mmoja akimshambulia mwenzake kwa ngumi nzito ,…! likawa balaa gady akipigania uhai wake.
Hatimae kibaraka alifanikiwa kujizuia kubiringita na akawa kamuweka chini gady huku akiwa kamkalia na kumtupia ngumi za uso.
Lakini ghafla alipigwa na kitu kizito kichwani kutokea nyuma yake..
Sarah alikuwa kafika na kulichukua shoka na kumpiga yule kibaraka!
Muda huo huo gady akamsukuma pembeni haraka gady akainuka na kilulichukua shoka kutoka kwa sarah kwani aliona sarah hajui kulitumia …
Muda huo kibaraka alikuwa anatafuta njia ya kukimbia lakini muda huo huo gady alimsogelea karibu na makali ya shoka yakaanza kuuchimba chimba mwili wa huyu kibaraka.
Alimkata kila mahali na kufanya mtu usitamani kuiangalia maiti yake na sarah alifumba macho kwani kitu alichokuwa anakifanya gady ni cha kikatili, kisha gady akauburuza mwili ule na kuutupa shimoni mule …
“tuondoke sarah funguo ya gari ninayo ….wenzetu wameuawa ” gady aliongea akamkamata mkono sarah wakaanza kuondoka , hakuthubutu kuacha shoka yake kwani alijua muda wowote wanakutana na adui…
Mpenzi msomaji baraka na john walikuwa wameuwawa kwani walipo fikikishwa kwenye pango lile kizee kilichoitwa malikia kiliamulu wachinjwe huku damu zao ziki tiririkia kwenye chombo cha sadaka.
Mpenzi msomaji sipendi nikusimulie yaliyo mtokea dolla na neema , ila nisipo kusimulia utajua vipi yaliyo wakuta?
Neema na dolla waliwambwa kwa kufungwa kwenye jiwe kubwa ndani ya pango wakafungwa vitambaa vilivyo waziba midomo na pua wakawa wana hema kwa tabu , kisha mishipa yao ya damu ikakatwa damu zao zikaanza kutililika mpaka kwenye jiwe ambalo juu yakeulilazwa ule mwili wa gunzani usio kuwa na uhai .
Damu ya neema na dolla ilipoanza kufika kwenye jiwe alio lazwa gunzani , taratibu uhai ulianza kuulidia ule mwili wenye futi nane naamu mwili wa gunzani.
Uhai ulikuwa unatoka kwa neema na dolla na kuingia gunzani..Nedma na dolla walikuwa wanskufa kifo cha taratibu chenye maumivu makali.
Yule malikia kikongwe alikuwa amepiga magoti mbele ya sanamu la goroza huku mawazo yake na hisia zake zikiwa hazipo dunia hiii.
****************************
Sarah na gady walitembea kwa mwendo wa haraka mwendo ulio wa gharimu kutumia dakika arobaini wakiambaa barabara na hatimae kwa mbali waliiona gari yao hapo mioyo yao ikapta furaha na tumaini..
Wakiwa wanaendelea kukalibia gari yao ghafla mbele yao kukatokea msichana aliekimbia huku nguo zake zikiwa zime chanika chanika
msichana yule aliangukia miguuni kwa sarah
“nisaidieni anataka kuni ua” msichana yule alipiga kelele na muda huo macho yao sita yakamuona mtu mrefu asie pungua futi saba akiwa mbele yao..
Alikuwa ni gola na yule msichana alikuwa ni diana .
Kumbe gola alipo ambiwa amrudishe diana kijijini yeye hakufanya hivyo ila alipo ondoka pale pangoni alikaa mstuni na kusubiri diana arudiwe na fahamu ndipo amuingilie kwa lazima na kumfaidi kigoli yule..na sasa diana alikuwa karudiwa na fahamu na kujikuta mikononi mwa gola alie anza kumchania nguo yake ya ndani ili ambake, diana alipo pata upenyo akachoropoka na kuanza kukimbia hatimae alikutana na kina sarah huku gola akiwa mbele yao.
Gola akiwa na bisu kubwa mkononi mwake akampita gady kama vile hakumuona huku akimfuata kigoli wake diana , gady kuona hivyo akajua sarah na yule msichana mwingine watakubwa na hatari muda wowote…
Gady akapiga hatua za haraka na kumshambulia gola kwa kumpiga shoka la mgongo lakini makali ya shoka yale yakishindwa kuuchana mwili wa wa gola.
Shoka ili dunda na gola alimgeukia gady..
Gady hakuamini kwamba makali ya shoka lile yalio ua maadui wake watatu yameshindwa kwenye mwili huu.
Tatizo gady hakujua kuwa alio waua walikuwa ni bina damu vibaraka wa goroza na huyu alikuwa ni gola mlinzi wa falme ya goroza na hakuwa binadamu…
Gady aliinua tena shoka ili ajaribu shambulio la pili na hapo gola akashika lile shoka kwenye makali , macho yakamtoka gady akajikuta akiachia shoka na muda huo mkono wa gola ukakamata shigo ya gady na na kumuinua kwa mkono mmoja huku akimning’niza hewani kwa kabali ya mkono mmoja.
“Sarah kachukue bunduki ya baraka” baraka aliongea kwa tabu na muda huo sarah akatoka mbio huku diana akimfuata nyuma mpaka kwenye gari lao ambalo lilikuwa hatua kazaa kutoka pala ..
Gola akiwa kamning’niza gady alie rusha rusha miguu na mikono, gola akainua mkono wake mwingine ulioshika kisu kirefu kisha kwa nguvu akakizamisha tumboni kwa gady na kumuachia akianguka kama mzigo huku yowe zito likimtoka gady..
Sarah alifungua mlango wa mizigo na kuichukua bunduki kisha akarudi mbio na kukuta gady katupwa chini akipiga yowe .
Sarah alikumbuka jinsi walivyo elekezwa na baraka jinsi ya kuitumia bunduki!
Sarah akaemulekezea bunduki gola kisha akavuta chuma cha stanby na kufyatua risasi mbili zilizo kita kifuani kwa gola..
Lakani gola hakuyumba wala kuanguka alikuwa kama hajapigwa na chochote ,risasi hazikumdhuru …gola akaanza kupiga hatua kumfuata sarah kwa hasira…
Sarah alihamanika na kugeuka akimbie lakini alijikwaa na kuanguka , na gola akamsimamia mbele yake huku akimtolea tabasamu la kuchukiza.
Gady alijiinua tena huku akipata maumivu makali akijikaza na kusimama akaingiza mkono mfukoni kwake akatoa funguo ya gari kisha akapiga hatua kumsogelea gola alie mpa mgongo.
Gady alipo mkalibia gady akatenda kitendo ambacho kilitisha kukitizama mara mbili.
Kwanza aliirusha ile funguo ya gari pale alipo anguka sarah kisha akachomoa kile kisu kwenye tumbo lake na kukikita kwenye ubavu wa gola…
“We die together…” gady aliongea kwa sauti hafifu
ilikuwa ajabu mara ya kwanza shoka lilidunda kwenye mwili wa gola hata risasi haziku mdhuru gola lakini sasa hivi kisu kilizama ipasavyo kwenye mbavu za gola…. hii ilimaanisha kisu hiki cha ajabu sana.
“Sarah chukua funguo hiyo kimbia kijiji hakipo mbali” gady alipaza sauti yake hafifu huku muda huo akichomoa lile bisu ubavuni mwa gola na kulizamisha mgongoni kwa gola ambaye hakupiga kelele aina yoyote.
Sarah alishindwa kuamini kinachotokea gady alikuwa katapakaa damu akimshindilia visu gola…
“Nimekwambia kimbia” gady alipaza sauti ya mwisho
na hapo sarah akajua kinachotokea ., nacho ni kwamba gady alikuwa anajitoa muhanga.
Gola alimgeukia gady na kumpiga ngumi nzito kifuani, gady akapepesuka nakuanguka chini akikiacha kile kisu kikiwa kimezama kwenye mgongo wa gola.
Sarah aliinuka na kuchukua ile funguo na kuanza kukimbia kuelekea kwenye gari ambapo diana alikuwa nje akihamaki huku macho yake yakishuhudia mapambano mazito baina ya gady na gola.
“Ingia tuondoke” sarah alimpigia kelele diana huku yeye akiiingia upande wa dereva na kuiweka bunduki upande wa pili, macho ya sarah yalisha shuhudia gady akitupwa chini kwa mara ya pili , hivyo ilikuwa wazi gady asinge pona mbele ya kiumbe yule…
Gola aligeuka na kumuona sarah na diana wakiingia ndani ya gari . gola akachukia akachomoa kile kisu na kukirusha akiwa kamlenga diana.
kisu kile kili mkosa kidogo diana sentimita chache badala yake kile kisu kili pasua kioo na kuangukia ndani huku diana akipiga yowe la woga.
Gola akapiga hatua awahi kabla hawaja washa gari lakini ghafla miguu yake miwili ikakamatwa.
Alikuwa ni gady alio ikamata miguu ile miwili akizuia gola asimfuate sarah wake alie mpenda.
Ghadhabu zikazidi kumpanda gola akawa na kazi ya kuitoa miiguu yake kwenye mikono ya gady.
*****************–****************
Mzee mkongwe akiwa bado kapiga goti mbele ya sanamu la goroza ghafla akasikia chafya nzito kutoka kwa gunzani , ni ule mwili ulio lala juu ya jiwe kwa muda mrefu.
Mzee yule akafumbua macho huku akiwa na furaha..
“Ahsante goroza. gunzani anarudi” aliongea kwa furaha , alipo angalia kwenye lile jiwe waliofungwa neema na dolla akagundua mmoja wao alikuwa amesha kufa na mmoja bado.
Neema alikuwa amesha iaga dunia.
Wazo lingine likamuijia yule mzee juu ya sadaka mbili zilizo bakia.
Tayari walikuwa wameshaua vijana wanne sasa walibakia wawili ambao mbweha dalu na mwenzake walitakiwa wawafikishe lakini mpaka mda ule hawakufika, hii ikamlazimu mzee huyu kikongwe awatafute kwahisia na kuwaangaza vijana wake…hapo ndipo alipo shuhudia miili mitatu ya vijana wake ikiwa imeuwawa.
Mzee huyu alishtuka kwani haijawahi kutokea tangu waanze kafara hizi za kila mwisho wa mwaka hajawahi kuawa hata kijana mmoja lakini leo vijana watatu wame uwawa.
Mzee huyu alipo jaribu kutafuta kwenye hisia zake mtu aliuwa vijana wake ,ndipo taswila yake ilipo muonesha balaa lililoendelea kati ya gady na gola huku akimuona gady wakati ule akimchoma gola kisu cha ubavu.
Mzee yule aliacha kila kitu na kutoka nje ya pango ma kuwakuta wanachama wake wakiendelea kuabudu.
“acheni kila kitu tuka wasaidie wenzetu wanapambana na mwanadamu mbaya” alipaza sauti huku akinyoosha njia.
Wanachama wakamfuata nae akawa mbele kuongoza msafara wa kwenda kumsaidia gola.
***************************
Sarah aliwasha gari na kuanza kuliondoa eneo lile huku macho yake yakimshuhudia gady akiwa kamzuia gola kwa kukamata miguu yake.
muda huo diana alikuwa siti za nyuma yake huku akishangaa michoro ya kisu cha gola kilicho pasua kioo na kuangukia kwenye siti! diana alihisi kuwa alishawahi kusimuliwa na mama yake juu kiumbe kilicho miliki kisu aina hii.!
Akiwa kachanyikiwa alizidi kuongeza mwendo huku akipata tabu kuuzoea uskani huu wa gari hii manual.
Gola aliinama na kumpiga ngumi zito gady iliotua kichwani ,Gady akahisi kizunguzungu ila bado aliishika miguu ya gola
Gola akaishika shingo ya gady na kuikaba ipasavyo .
Hali ikawa mbaya kwa gady akajikuta akiacha miguu ile na muda huo huo gola akainua mguu wake na kukikanyaga kifua cha gady kwa nguvu ..
gola akaondoka ambio akilikimbiza gari lakina sarah.
Sarah alizidisha mwendo wa gari huku roho ikimuuma kumuacha gady, mara ghafla alishuhudia mtu akitokea porini akikimbia sambamba na gari lake kihoro kikamkumba sarah baada ya kumuona mtu yule akiruka kutokea pembeni ya barabara kuja upande wao na mtu huyo alitua kwenye dirisha upande aliokuwa yeye.
Alikuwa ni gola ambaye aling’ninia kwenye gari mkono mmojaukiwa umeshika vyuma za kuwekea mizigo juu ya gari…na mkono meingine akaupenyeza dirishani na kuikamata shingo ya sarah…
Haraka sara alikanyaga breki za ghafla ili amtupe kiumbe huyu lakini hakuwa hivyo gari ilisimama na kiumbe yule hakutupwa alikuwa dirishani na mkono wake ukizidi kumkaba sarah…
Wakati sarah anafunga brek diana alifungua mlango huku akiwa na kile kisu akiwa anakumbuka siku moja usiku mama yake alimsimulia kuna viumbe wanaishi duniani ,hawapigiki na wana kisu kimoja ambacho ni cha falme yao na kila anae kimiliki kisu hicho ni mlinzi wa ufalme ule wa kiza. na mongoni kwake kuna kitu kinacho mlinda na kufanya wao waishi…
diana alihisi ndio kile kisu kwani siku ile mama yake alimtajia michoro ambayo ipo kwenye kile kisu …naamu michoro hiyo aliiona kwenye kile kisu ambacho kilimilikiwa na gola.
Hivyo diana alizunguka gari na kumkuta gola akimkaba sarah.
Diana alimdandia gola mgongoni na muda huo akakizamisha kile kisu chini ya shingo ya gola .
Kwa mara ya kwanza gola akatoa kwa na yowe kali huku akimuachia sarah.
Diana kuona hivyo akachoma tena huku safari hii akiwa anachana kwa kushusha kisu chini!
Hapo msitu mzima ukatawaliwa na kilio cha gola huku kitufe kidogo kikitoka kwenye mwili wa gola palipo chanwa na kisu kikianguka chini.
Gola alizungusha mkono wake na kumkamta diana lakini gola alikuwa amechelewa tayari kinga yake ilishaanguka chini
Sarah kuona hivyo haraka akachukua bunduki na kamulekezea kichwani gola na muda huo akafyatua risasi ilio kibanjua nusu ya kichwa cha gola huku mwili wa gola ukitupwa chini….
Gola alikuwa kasambalatishwa .
Sehemu Ya 5
Diana alikuwa mgongoni kwa gola hivyo wakati gola anaanguka chini walinguka pamoja huku ule mwili mzito wa hayati gola ukimlalia diana.
Kisu kikaanguka karibu na kile kitufe ambayo ni kinga ya viumbe hawa .
Sarah hakuamini alishuka kwenye gari huku akiukodolea macho mwili wa gola huku akimuona diana akijitoa chini ya mwili ule ….
Kabla hajaenda kumsaidia ghafla akaliona kundi la washirikina wakija mbio wakiongozwa na yule kizee mkongwe malikia wa viumbe vile…
“Tunakufa …dada chukua hicho kisu ukichome hicho kitufe ukipasue” Diana alipaza sauti kumwambia sarah .
Sarah haraka bila kujiuliza akachukua kile kisu kisha kwa nguvu zote akakichoma kile kitufe kika pasuka na kumwaga damu nyeusi ..na muda ule ardhi ilitikisika huku wale washirikina wakianguka chini na yule kikongwe akikumbwa na udhaifu akaanguka chini..
Sarah hakuamini anachokiona akahisi yupo ndotoni!
“mama….” diana alijikuta akitamka huku akipiga hatua kwenda kwenye lile kundi la washirikina waliokuwa hawa jiwezi…
Diana hakuamini! kumbe hadi mama yake alikuwa ni mmoja wa wanachama wale
“mama umefikaje huku na mbona upo kwenye sale zao” diana aliongea huku akilia sana akimtazama mama yake aliekuwa chinitaabani…
Sarah akawa yupo kwenye mshangao ….
*********;*************************
Kule pangoni hatimae dolla nae aliaga dunia na hapo uhai wake ukaangukia kwa gunzani
Gunzani aliinuka kwenye jiwe mwili wake ukiwa umerudiwa na uhai pamoja na nguvu…
Aliporudiwa tu na uhai hisia zake zilimuonesha wenzake wapo kwenye matatizo…
Gunzani akatoka nje kwenda kuwasaidia wenzake…
Sarah akiwa pale akimuangalia diana akimlilia mama yake ghafla akamuona mtu akiibuka kutoka mstuni akiwa ni mrefu kuliko hata gola …..alikuwa ni gunzani
“Wewe ondoka hapo” sarah alipaza sauti huku akijaribu kumfyatulia risasi gunzani lakini bunduki ilikuwa imeisha…
Diana alishtuka na kuanza kukimbia lakini alichelewa ghafla alinyakuliwa hewani…
Lah. huyu gunzani alimnyakua diana kama kifaranga kinavyo nyakuliwa na mwewe…..
Sarah alikimbia kwenye gari ambalo likuwa na halijazima akatupia kisu na bunduki ndani ya gari kisha akiliondoa gari kwa mwendo wa ajabu akikikimbia kifo….
******-*
Gari ilikuwa kwenye mwendo usio wa kawaida huku sarah akizidi kuchochea speed ,gari ikawa katikati ya barabara ikijaribu kuuacha msitu wa kifo…
Ghafla kwenye kona sarah aliona gari nyingine ikija upande wake nayo ikiwa speed akajaribu kukanyaga blek kwa nguvu huku akikata kona….
Sauti ya msuguano wa gurudumu (tire) na rami ikatawala eneo lile ,gari aliondesha sarah ikaburuzika na kuacha bara bara na kwenda kuu gonga mti kwa kishindo….
Ilikuwa ni kishindo kikubwa kilichopelekea sarah kupiga kichwa chake kwenye kioo na kupoteza fahamu ,huku gari lake likifuka moshi mzito mweusi..
Ile gari nyingine iliyo koswa koswa kugongwa na sarah gari ya sarah ilikuwa ni gari ya polisi ,polisi ambao walipewa taarifa na kampuni la kusafirisha watalii kuwa kuna gari imekwama mstuni…
<<<<<<<<
Kila gari la kampuni hili la kusafirisha watalii hua zina fungwa GPS ambayo huwa tambulisha hatua kwa hatua kila zinapo enda gari zao…Gps hiyo huwa julisha viongozi wa kampuni popote gari ile sehemu ilipo.
Hivyo watu wa mitambo waliweza kuiona gari ya dereva wao baraka kupitia mitambo yao ikiwa imesimama katikati ya msitu kwa muda mrefu na haikuwa na dalili ya kuwashwa..
Hii ili maanisha gari hii inamatatizo kwani walipo piga simu ya baraka iliita bila kupokelewa..
Haraka uongozi wa kampuni wakafikisha taarifa kituo cha polisi kilichokuwepo bagamoyo na kuwasihi waifuatilie gari ile iliyo kwama katikati ya msitu ikiwa na watalii watano kutoka ndani ya nchi…
Haraka gari yenye polisi kumi wakiwa na siraha za moto ikaondoka ikiwa mwendo wa mkali ikielekea sehemu walipo elekezwa…
Gari yao ilikivuka kijiji cha mvila huku wakiwa kwenye mwendo mkali, ghafla kwenye kona kali walikutana gari jingine nalo ikiwa kwenye mwendo mkali zaidi ys wao…dereva wa gari ya polisi alihamanika huku akishuhudia gari iliyo endeshwa na msichana ikipoteza muelekeo na kutoka barabarani na kwenda kugonga mti……>>>>>>>>>>>>>
Kumbe sarah alikuwa ameendesha gari kwa umabali mrefu sana na bila kupata ajali basi angeingia kijiji cha mvila.
“Ah wazee hii ndo hii gari tulioambiwa tuifuatilie” afande mmoja alipaza sauti huku akiimulika ile gari kwa kurunzi yenye mwaga mkali…
“kweli mpakieni kwanza huyo demu kaaumia vibaya tumuwahishe hosptal” mkubwa wao aliongea ,wakasaidizana kumtoa sarah kwenye gari akiwa hajitambui kabisa ,wakampakia kwenye gari yao wakageuza kurudi bagamoyo…
Sarah alifikishwa hosptalini akapokelewa na kupelekwa wodini kupata huduma … na taarifa hii ikafikishwa kwa meneja ya kampuni ya utalii ilio muajili hayati baraka..
Sasa ikawa polisi wana jadiili kwani walijua huko mstuni kutakuwa na matatizo kwani kwa mwendo aliopatanao ajali sarah ulionesha kuna kitu alikikimbia huko alipo waacha wenzake.
Polisi wakaamua kuongeza nguvu ikabidi waondoke na gari mbili huku wakiwa polisi ishirini na mbili…
Safari ikaanza kuelekea eneo la tukio…
1 january (1/1/2017)
Saa kumi alfajiri…..
Kundi la askali lilifika eneo la tukio ndani ya msitu ulionuka damu wakiwa na siraha zao wakitembea mwendo wa tahadhari ndipo walipo anza kukutana na maiti kila eneo
kwanza waliona zile maiti za washirikina na wa livyo zidi kutafuta wakafanikiwa kuuona mwili wa kijana shupavu akiwa kalala kwenye dimwi la damu nae alikuwa ni gadyson…
Katika maiti zote zilizo onekana maiti ya gola haikuonekana wala yule malikia kikongwe ..
“jamani kuna mmoja mzima” polisi mmoja alipaza sauti akiwa kachutama mbele ya msichana diana alielala chini..!!!
Polisi wote wakamsogelea wakiwa na hamu ya kujua nini kilimtokea msichans yule ….
“Nini kime wakuta binti” kiongozi wa polisi hawa aliumuuliza diana baada ya kuona angalau anaweza kuongea japo kwa sauti dhaifu…
“Ni maharamia wamefanya haya …walitukamata kijijini usiku “diana aliongea huku akiwa omba wampeleke hosptali kwani hali yake sio nzuri…maelezo yake yakiwa hayajitoshelezi
“Askali saba mchukueni mpelekeni kwenye gari mumuwaishe bagamoyo kwenye hosptal tulio mpeleka mwenzake..
Haraka diana akachukuliwa na kupelekwa ndani ya gari , safari ya askali saba wakimuwaisha diana hosptal ikaanza.!!!
Diana alipona vipi wakati jana usiku alikamatwa ns gunzani?????……
Rejeaa …jana usiku..
Gunzani alimkamta diana kwa hasira akiwa kafura muda huo diana alipiga kelele za kuomba msaada..
“Gunzani wamemuuwa gola hawa binadamu wabaya waue wao na rafiki zao ” yule kikongwe aliongea kwa sauti ya kukoroma huku akilia ….muda huo huo gunzani akanyonga shingo ya diana na kuivunja ..pale pale diana akapoteza uhai wake kwa kudhurumiwa…
Kisha gunzani akaufukia chini ya ardhi mwili wa diana …kisha akambeba yule mzee pamoja na maiti ya gola…akawahimisha eneo lile kuwapeleka sehemu nyingine….
“Wewe peke yako ndo umebakiwa na nguvu sisi ni wadhaifu nenda kawauwe wote wanaoshirikiana na yule msichana alie pasua kinga ya uhai wetu” ni maneno ya yule bibi kizee yaliyo penye kwenye sikio la gunzani mwenye ghadhabu….
Gunzani kwa hali ya kuto tarajia alijigeuza na kuchukua umbo la dianâ pamoja na sura ya ya diana!!!..
“Naenda kumuua yeye na rafiki na jamaa zake “Gunzani aliongea akiwa kwenye umbile la diana………
>>>>>>>>>>>>>>
La haula!!!!! yule diana walimchukua wale askali alikuwa ni kiumbe gunzani ndani ya mwili na surah ya diana na walikuwa wanampeleka kwenye hosptal alio lazwa sarah..
MWISHO

