MKE CHANGUDOA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 3
Juma alikasirika kuondoka pekee yake nalishaona wasichana warembo pale baa, lakini akashindwa kufanya chochote. Walifika nyumbani, na kila mtu akaingia kulala. Asubuhi na mapema juma na hasan walitoka na wakenda mbezi beach kuonana na dalali wa nyumba, wakapelekwa kwenda kuona nyumba, juma akaipenda wakafanya utaratibu wa malipo, siku hiyo hiyo juma akaatafuta watu wafanye usafi ili ahamie, akaenda mjini kutafuta vitu vya ndani. Walihangaika siku nzima kufanya manunuzi, mpaka giza linaingia siku iliyofwata wakamalizia, kisha wakaanza kupanga vitu kwenye nyumba. Palipendeza sana nyumba ilikuwa yakisasa na vitu vyote vyakisasa, makochi, tv, meza na vyengine vingi. Baada ya kukamikisha juma akasema “sasa twende nikakamikishe ahadi yangu” waliondoka kuelekea sehemu wanauza magari, juma akanunua gari mbili moja toyota harrie nyengine rav 4 new model, juma akamwambia hasan “wewe chukua hii rav 4 au unataka gari gani?” hassan akamuuliza muuzaji “samahani ni gari gani inaringana thamani na hii rava 4?” akatajiwa aina ya magari akasema “nipatie toyata athletics” wakaandikiwa wakapatiwa card za magari na vitu vyote kisha kila mmoja akawasha gari yake nakuondoka.
Juma alienda kwake, na hasan akaenda kwake. Hasan alipofika nyumbani alimuita mke wake aone gari lao. “mume wangu umepata wapi pesa?”……. “mke wangu sikuwa na pesa ya kununu gari ila juma alinambia akija ataninulia gari kama ahsante”…….. “ahsante kwa lipi? Umemefanyia nini?”……. “siwezi kuhesabu niliyomfanyia, ila kubwa mimi ndipo nilimpatia mchongo wa kwenda south kufanya kazi?”……. “kwanini hukwenda wewe?”……. “mimi nilikuwa nakazi tayari, halafu yeye alikuwa hana kazi hivyo sikuwa na tamaa niliamua kumconect yeye, aende akafanye maana ni kama ndeugu yangu”…… “kwahiyo ndio amekununulia gari”…… “ndio”…… “sawa ikawe kheri in shaa Allah” hasan na mke wake wakaingia ndani, Upande wa juma yeye alikuwa anawaza aende kiwanja gani? “hapa sijui niende wapi lakini inatakiwa nong’oe mtoto mkari sana” alijisemesha mwenyewe, akapata jibu aende the great. Akaingia bafuni akajiandaa akaondoka zake. Alipofika alikaa meza ile ile waliyokaa siku tatu zilizopita, akaletewa kinywa akawa anakunywa mala akawaona wale wasichana tena akawaita, wakaja akawaagiziia pombe, kisha stor zikaanza, mmoja ya wale wasichana akauliza, “juzi ulikuja hapa mlikuwa watatu?” juma akajibu “ndio, yule ni rafiki angu na mke wake” wale wasichana wakaangaliana kisha wakacheka, “kheeeeeh kunguru toka lini akafungwa?”…… “ndio nashangaa” jumaa akawa haelewi akauliza “mbona siwaekewi vipi kwani” mmoja akamjibu juma kwa kusema, “kwahiyo yule msichana ni shemeji yako?”…… “ndio ni shemeji yangu”…… “yule changundoa ndio shemeji yako?”…… “unasemaje?”
************************
“kama huamini wewe mpe pesa kama hakupi utamu”……. “Inamaana mnamjua vizur”……. “hatuwezi msingizia bhana”……. “nuinyi mlimuona lini akijiuza”……. “siku hizi machangudoa wamebadilisha fashion ya kujiuza, unazani utawakuta barabarani kama zamani? Kila kitu kila kitu kinabadilika”…… “mmmmmh sitaki kuamini hilo ila acha iwe hivyo” waliendelea kunywa na story mbili tatu, muda ulivyoenda juma akaona bora aondoke zake, wale wasichana wakamuuliza, “kwa hiyo nunaenda kulala pekee yako? Hutaki campan?” juma akasema, “mimi mgeni hapa hivyo nakaa kwa rafiki yangu na unabidi nirudishe hit gari yake mwenyewe anaenda kazini kesho”… “sasa si unaipeleka halafu tunaenda logde kupumzika mimi na wewe au unasemaje?”……. “tuonane kesho nitakuwa free kwaherini” juma aliondoka.
Wale wasichana walibaki pale wakiendelea kupata vinywaji, “yaani angekubali tu kuondoka na mimi angelia kilio cha mbwa mwizi asubuhi”…… “kwaninavyokujua wewe ungemkomesha”……. “anaonekana kabisa mgeni yule”……. “ningempa vitu adimu akachanganyikiwa kisha akilala tu anapigwa pesa asubuhi akiamka kweupe, halafu nambembeleza”….. “mnalia wote mmeibiwa”…. “khaa yani namuigizia kama vile sijui kitu”……. “nakubalia jeshi langu”……. “mjiji hapa lazima akili iwe kubwa.”
Asubuh na mapema juma alienda nyumbani kwa hasan, alipofika alikuta hasan ndio anataka kutoka kwenda kwenye mizunguuko yake ya kazi ya kutafuta ridhiki, “asalam alyekum kaka” walisalimiana, kisha hasan akasema “sikutegemea kupokea mgeni saa hizi ndio maana natoka”……. “aaaah nimewakumbuka nikaona nije niwaone kabla sijaenda kwenye mishe zangu”……. “ok sawa karibu sana ndugu yangu”……. “ahsante sana, shem ameamka?”….. “yule akisha swali halali tena?”……. “aaaah sawa, anapunguza dhambi sio”…….. “unamaana gani?”……. “achana nalo hilo swala, kwahiyo unaenda wapi?”……. “mimi naenda town maana naweza kupakia niende tunduma kupeleka mafuta”……. “aaaah sawa basi sawa mimi nitabaki nashemeji nikimlinda au unasemaje?”……. “mke wangu hana shida ya kulindwa analindwa na mungu pekee yake”…… “unamuamini sana shem inaonekana si ndio?”….. “ndio kwanini nisimuamini”…. “sasa unaenda na gari au?”…… “hapana naliacha, kwasababu kama nikipakia naondoka zangu”….. “basi ngoja nikupeleke na gari yangu, nikirudi ndio nitamuona shemeji”…… “poaw twende” juma na hasan wakaondoka kuelekea kigamboni.
Walifika na juma akamuacha hasan yeye akaondoka zake, akanijibu wa njiani simu yake ikaita, “oya vipi kaka nikufwate au?”….. “hapana nimepata zari hapa, naenda kupaki than nasepa”…… “oooh poa kwahiyo home huji kuchukua nguo?”…… “nguo zangu zipo kwenye gari mimi standby”….. “oooh poaw basi ukiondoka utanambia mwamba”…… “poaw” juma alitabasamu kisha akajisemea moyoni, ‘ngoja nione utamu wa shem asijilie pekee yake, hapa acha nipite supermarket ninue mazaga kisha nimpelekee shem’ juma alipitia kweli supermarket na kununua vitu kisha alipomaliza alianza safari ya kuondoka kwenda nyumban kwa hasan, alipofika alibisha hodi akakaribishwa na binti wa kazi wa hasana, akaingia ndani na kuketi, baada ya kusalimiana juma akauliza “dada yako yupo wapi?”……. “yupo ndani”…… “muite” binti akaondoka na kwenda kumuita mke wa hasani. Juma alikuwa anawaza anaanzaje kumuingia shemeji yake, akakumbuka maneno ya wale mabinti wa baa kwamba mpe pesa uwone, akatabasamu akijua atampata, na kusibitisha kuwa ni changuduo kweli. Akiwa anafikilia simu yake ikaingia sms, “mwamba mimi naamsha” ile sms ikamfanya juma afurahi, “hili bwege linaondoka safi sana, acha nimsaidie majukumu” mala alifika mke wa hasan, “ooooh shem salam alyekum”….. “walyekum salam shem kwema”….. “kwema”…… “nimekuletea zawadi shemeji”…… “oooh asante sana shemeji mungu akubariki”…… “usijari sana” mke wa hasan akainama kuchuku ile mizigo apeleke ndani, juma akasema “nenda halafu uje nina jambo nataka kukwambia, mke wa hasan alipeleka vitu ndani kisha akachukua simu akampigia mume wake,” amekuja juma hapa”…… “ameniambia atakuja hapo”…… “vipi unaondoka au safari hamna nikuhesabu chakula cha mchana?”…… “sijajua ila usinihesabu naweza kurudi ama nisirudi?”….”sawa mume wangu, shemeji anasema anamazungumzo na mimi”….. “nenda kamsikilize anasemaje?”……. “sawa mume wangu” mke wa hasan akaenda siting room akakaa kisha akamuuliza juma, “shemeji eeh unamazungumzo gani?”….. “mbona unaogopa wakati mkubwa wewe?”…… “ukubwa unahusiana nini na kuogopa”…… “ok basi haina shida, nahitaji hii iwe siri”….. “siri tena?”…… “nahitaji tuwe wote usiku wa leo, maana hasan si anasafiri”…… “unasemaje shemeji?”
“Nataka nikupeleke viwanja vya bata ambavyo hasan hawezi kukupeleka, kila siku mabaibui na madera ngoja nikupeleke sehemu ukaone mambo ya dunia yanavyokwenda twende tukatumie pesa twende ukaenjoy” mke wa hasan alikuwa akimsikiliza tu juma akimwaga sera, “mtoto mzuri kama wewe hutakiwi kuwa hivi? Unatakiwa kuwa na gari yako, na maisha yako”…… “kwahiyo unanichukuliaje mimi?”……”kawaida na lengo ni wewe uwe na furaha”…… “ok subiri” mke wahasan akaamka kisha akaenda chumbani kwake akachukua zawadi alizoletewa na juma akatoka nazo akampa juma mzigo wake kisha akafungua mlango na kusema, “naomba uwondoke, beba mizigo yako ondoka, mimi sio kuku kama utanidanganya kwa punje za mtama naomba uwondoke, usije hapa kama hasan hayupo, pleas ukitaka huu ujinga wako nisimwambie hasan basi kaa mbali na mimi, ukija hapa njoo na hasan au subiri hasan akiwepo ndio uje, laah sivyo nitakuzalilisha” juma akasema “kwani shem tatizo liko wapi, kwani ukitoka na mimi nani atajua, pia hatuendi jufanya chochote kibaya, tunaenda kutembea tu than tunarudi”…… “mimi sio mjinga kama unavyonifikilia, nasema toka nyumbani kwangu” juma akaondoka zake, “mbonw unaacha mizogo yako beba katagute wakumpa”….. “hiyo nilikununulia wewe chukua”……. “nimesema sitaki chukua mizigo yako” mke wa hasan akamtimua juma, juma akaondoka zake na kuelekea kwake.
Jioni juma alichukua tax hadi the great ambako alipanga kuonana na wale wasichana alikaa na kuagiza kinywaji kisha akaanza kunywa na kuanza kuwasubiri, akiwa amekaa mala akaja msichana mmoja kati ya wale aliyokuwa nao siku moja iliyopita, “karibu”….. “ahsante”….. “wenzio wako wapi naona upo pekee yako”…….”wale kila mtu kapata ubavu wake kasoro mimi”…… “kwahiyo sahizi wapo kwenye sarakasi”……. “hahahahaha, acha kunichekesha mimi”….. “basi usijari wewe leo utakuwa na mimi au uanasemaje?”….. “sina neno juu ya hilo, kikubwa pesa tu”…… “kwanini unasema kikubwa pesa”…… “sasa unadhani nitaishije mjini bila pesa?”…… “basi usijari utaishi kiboss kama mimi sawa?”…… “usiwaze kuhus mimi”……. “nataka uwe wangu yaani kila siku tuwe wote utaweza kweli?”……. “sijui”….. “ok sawa maliza kinywaji tuondoke”…… “sawa ila vipi kuhusu yule manzi umejua kama ni changu?”…… “mmmmh sijui ila sijasibitisha hilo”…… “sawa haina shida” walikunywa kisha wakaamua kuondoka na kwenda kupumzika. Walipofika logde, juma aliingia bafuni akaoga, kisha na yule mrembo naye akaingia bafuni alipotoka akaenda kukaa kwenye mapaja ya juma, juma akauliza, “ulisema unaitwa nani?”….. “naitwa niffer”…… “mrembo kama jina lako”…… “ahsante love” wakaanza kutomasana na kisha kupeana penzi.
Hasan alirudi nyumban kwake majira ya saa nne usiku akamkuta mke wake anamsubiri, alipoingia mke wake alianza kulia, hasan akasema “unalia nini mke wangu” mke wa hasan akasema, “kuna yoyote anajua storia yangu?”…… “hapana sijamwambia yoyote?”……. “sipendi kujaribiwa, nitakuja kumtukana mtu waambie rafikinzako mimi sio malaya, waambie kabisa wajue”….. “kuna nini kwani?”…. “mume wangu acha niishie hapo, ila unamarafiki wa ajabu sana sana”…… “bado zikuelewi, yaani sielewi kabisa”…….. “usiwaze mpenzi wangu, usiwaze mume wangu mimi nakupenda, umeniheshimisha kuniweka ndani na kunifanya kuwa nathamani, imani yako uliyoweka kwangu sitaki kuivunja, sitaki kukuangusha acha niendelee kuweka uwaminifu wangu kwako yaani sitovunja uwaminifu wako, nakupenda mume wangu nakupenda sana kipenz changu.”……”nakupenda sana love, mama wa mwanangu, ila sijui nini kimekusibu laazizi”…… “sitaki musisalimiane, sitaki pia mgombane, ila ninachotaka kusema unapokaa na rafiki zako waambie, mimi sio rahisi hivyo, halafu kama wanataka kunijua kiundani waje niwaambie kuhusu mimi. Wengine washamba tu, mimi sio mshamba kama wao”……. “bado unaniacha njia panda”…… “twende ukapumzike mume wangu najua umechoka, ila sitakuja kukusaliti niamini, ipo siku utakuta nimemoiga rafiki yako makofi si unanijua vizur?”…… “khaaa usije nipa kesi nakujua wewe yaani ukimkamata mtu kama juma yule unaua mwenyewe mbovu mbovu yule”….. “sasa mwambie asinipime kina changu kirefu”…… “asikupime?”
“ndio asinipime”……. “kwani anakupima?”……. “hapana ila natoa tahadhari tu?”…….. “ok sawa haina shida, twende ndani” waliingia ndani hasan akaenda kuoga kisha wakapanda kitandani na kulala. Upande wa juma yeye alikuwa na dada poa wake wakiendelea kupeana mapenzi moto moto, “Umezaliwa wapi mbona fundi hivi?” juma alijikuta anamuuliza niffer, niffer akasema “mimi kwetu bara mbona”….. “unajua sana yaani raha mpaka utosini”…… “ahsante sana” waliendelea kusifiana na kupeana raha mpaka asubuhi. Juma akachanganyikiwa na penzi la niffer akamzuia niffer kuondoka, “naomba usiondoke baki hapa, baadaye nataka twende ukapaone kwangu, wewe ni mzuri, unajua mapenzi tulia na mimi kipenzi”…… “utaniweza mimi wewe?”……. “ndio nitaweza”…… “sawa haina shida” wali baki pale logde kwa siku mbili wakipeana uroda. Hassan alishikwa na wasi wasi na kuanza kumtafuta juma akipiga simu ikawa haipatikani, akatuma sms lakini hazikujibiwa alikuwa na wasi wasi sana. Mke wa hasan akamuuliza hasan “mbona unaonekana haupo sawa mume wangu?”….. “ni kweli sipo sawa, namtafuta juma toka jana hapatikani leo ni siku ya tatu hatujaongea sio kawaida sijui amepatwa na nini?” mke wa hassan aliwaza sana alitamani kusema ukweli lakini akaona atawagombanisha marafiki ambao sasa ni kama ndugu, “mume wangu atakuwa yupo sawa, kama kuna tatizo angeshakupa taarifa itakuwa yupo salama”……. “mke wangu unajua mimi na juma hata kipindi yupo south ilikuwa lazima tuwasiliane kila siku, sasa sijui kakumbwa na nini?” mke wa hasan alimbembeleza mume wake, na kujaribu kumsihi na kumliwaza, hassan akauliza “mke wangu ile siku ya mwisho alivyokuja hapa hakuna tatizo lolote lilitokea?” mke wa hasan akastuka hasan akasema “mbona unastuka kuna nini?”…… “swali lako limenistua maana sikutegemea, ila hakujatokea kitu chochote baina yetu”……. “sawa acha mimi nijiandae nitoke niende nikamwangalie kwake” hasan alienda kujianda na kisha kuondoka kwenda kwa juma.
Sehemu Ya 4
Juma yeye ndio alikuwa anatoka lodge amekaa siku tatu na niffer, “niffer kama nilivyokwambia nataka uwe wangu pekee yangu nenda fikilia hilo, naomba kakae chini ulifikilie kwa kirefu sana”….. “mimi ni ndege ila ndege mimi sio kuku wala njiwa mimi ni kunguru, ni ngumu kunifuga sijui ufanye nini, mazoea yameshanijengea tabia tayari hii biashara imekuwa kama tabia yangu, ni ngumu kuacha ni ngumu sana”….. “nenda nyumbani nitakufwata baadaye sawa”…… “ok kwaheri” waliagana na kila mmoja akaenda njia yake, juma alipofika nyumbani alimkuta hasan yupo getini kwake, “kaka vipi umekuja muda mrefu” juma akimuukiza hasan, hasan akajibu, “ndio nipo muda sana hapa, nagonga mlango, napiga simu ila hupatikani”….. “kaka nimekamatika pabaya, vipi lakini”…. “poa kaka, umekamatika kivipi?”…… “ngoja nifungue mlango tuingie ndani?” juma alifungua mlango wakaingia ndani na kuketi siting room, akachuku simu yake akaweka chaji. “leo siku ya tatu sijakanyaga humu ndani”……. “ulikuwa wapi juma?”….. “sikuwa mbali sana ila nilikuwa nipo nimejificha na mtoto mmoja hivi mzuri”….. “yaani mimi naumiza kichwa ndugu yangu yupo wapi kumbe wewe unakula raha tu”….. “ndugu yangu nisamehe lakini nimekutana na msichana, utazani under 18 kumbe anaenda kwenye 30, yaani kitu ‘mang’anyu’ yaani ngoma inanata hivi, nilichanganyikiwa nikatapagawa, nimeshindwa kujizuia nayaka kuoa kabisa”….. “huyo mwanamke unamjua vizur lakin?”…… “mimi simjui nimekutana naye tu baa ila nataka nimuoe”…… “hukuwa na plan za kuoa umepewa nini ndugu yangu?”….. “kaka wewe acha tu yaani sijui nisemeje”….. “kwahiyo unaplan gan?”….. “nataka kuoa hakuna chengine?”…… “hebu nambie huyo msichana umemkuta mazingira gani? Pia umeshamwambia kwamba unataka kumuoa?”…… “ukweli ni kuwa yule ni changudoa, na pia nimemwambia ila amenijibu yeye ni kunguru siwezi mfuga”…… “duuuu pole kaka”…… “pole ya nini”…… “si anakuchomolea huyo demu, halafu wewe ndio ushapenda?”…… “ndio nimependa, ila najishangaa iweje nipende kwa haraka hivi, kwanini nisipate mwanamke anayejiheshimu na kujitunza, ningepata mke kama wako, bro umepata mke yaani nakuambia ukweli?”…… “Ahsante”…. “najishangaa sana kumpata mke wa hivi yaani najikuta naweweseka kabisa, nimekuaje lakini?”….. “juma, mapenzi huwa hayabishi hodi wala hayatoi taarifa, lakini pia ubaya kuhusu hisia za mapenzi hazina macho zenyewe ni kipofu, hivyo kuna wakati hukuingiza sehemu ambayo hukuitegemea, hivyo basi kwakuwa ndio hisia zimekupeleka huko, ombi langu kwako, usiache akili, zitumie akili zangu vizuri, fanya kila kitu kwa umakini laa sivyo utakuja juta”……. “sasa nifanyaje na nimeshampenda?”…… “tutatafuta namna ya kufanya ondoa shaka?”……. “utaenda kuongea naye?”…… “nitajaribu kufanya hivyo?”
Upande wa niffer alikuwa yupo na mashosti zake wakipiga story, “basi bwana bwana yule asitangaze ndoa”….. “eeeh ilikuwaje? Umempa nini mtoto wa watu”……. “labda kampa tope”……. “nyie mnajua kama mimi pamoja na uhuni wote ila tope sitoi”……. “sasa ndio utuambie umemfanya nini?”….. “inaonekana hajawahi kutana na wanawake ambao wanajishughulisha kitandani, mimi niliimiliki show, nilimburudisha haswa, nilikotro kila kitu, kuna muda mpaka alitamani kupiga kelele kwa raha” ‘”hahaha hahaha” walicheka kwa pamoja “yaani nilimpa show”…. “na sindio alitaka show” simu ya niffer ikaita “nyamazeni juma anapiga” akapokea “yes haloo”…… “mambo vipi niffer”….. “niko poaw za wewe?”……. “mimi mzima sijui kwako?”…… “fresh nambie”…… “niffer naomba tuonane baadaye nina mazungumzo na wewe pleas usikatae”…… “unajua ulikaa na mimi siku tatu, bado unataka na leo”…… “ila si nimekulipa vizur au?”…… “kwahiyo na hayo maongezi pia utanilipa”….. “nitakulipa ndio wewe njoo”…… “saa ngapi?”…… “jioni saa kumi”….. “sawa nitakujibu”
Juma alikata simu kisha, hasan akamuuliza juma, “eeeh amekubali au amekataa?”….. “hapana hajakataa ila pia hajakunari”…… “amesemaje sasa”…… “amesema atanijibu baadaye, kwahiyo nitamtafuta baadaye”…….. “ok sawa haina shida ni jambo zuri”…… “sasa tutamwambia nini ili akubali maana yule ameshazoea kujiuza atakubali kweli?”……. “atakubali usijari bwana”…… “watu hawataniseme kweli?”…….. “mbona unawasi wasi sana, inshi maisha yako usifwate watu wanasema nini?”….”sawa bro nipe moyo”……. “sasa acha niende home kwanza maana nilikuwa na wasi wasi sana na wewe, tuonane jioni sawa”……. “sawa haina shida” hassan aliondoka na kurudi nyumbano kwake.
Niffer naye akiwa na rafiki zake waka wanaongea, “shoga limekuganda hilo”……”mwenzangu yaano huyu nwana amenong’ang’ania utazani ruba”,,,,,,, “tatizo mnatoa ufundi wote, jnatakiwa unampa maufundi kidogo tu, sasa wewe unampa vyote vya uvunguni huoni kama ni balaa hilo”……. “daaah sasa sijui anamaongezi gani na mimi?”……. “wewe nenda ukifika utajua anakuitia nini?”……. “sawa nitaenda nikamsikilize” mazungumzo baina ya niffer na wenzie yaliendelea. Upande wa hassan alikuwa yupo na mke wake wamekaa chumbani wanaongea na kijadili, “mke wangu jumaa anataka kuoa?”…… “mbona ghafla hivyo?”….. “hata mimi nimeshangaa sijui kimemkuta nini sijui yamemkuta mangapi?”……. “masikini yaani hata siamini kama ndio yeye”……. “mambo yanabadilika mke wangu, ila ni jambo la kher naye akiwa na mke”……. “yeah ni sabin mume wangu”…… “ok tuachane na hayo, vipi naona niwakati sahihi wa kupata mtoto wa pili au unasemaje mke wangu”…… “sawa mume wangu”…….. “basi itabidi tuanze kumtafuta tuombe mungu sasa aje dume”……. “hahahaha, likija jike?”…… “basi nitashukuru kwani ni mipango ya mungu siwezi kuipinga”……. “ni kweli mume wangu hata mimi natamani aje wa kiume ila mungu ndio mpangaji”…… “sawa nakupenda mke wangu nakupenda sana kipenzi changu”……. “nakupenda pia mume wangu, wewe ndio mficha aibu zangu, wewe ndio unanipa furaha, ni wewe uliyenitoa kwenye ushetani, nakupenda mpaka kufa laazizi”……. “ahsante mke wangu”……. “kuna wakati najiuliza ni kwanini nisingejuana na wewe mapema, nikaishi maisha haya ya furaha?”…….. “kila jambo huwa na wakati wake mke wangu hivyo usiseme sana, mungu pekee ndio hujua, wakati gani ni sahihi”…… “ahsante sana kwa kuniamini, ahsante sana kwa kunipa heshima nashukuru sana sana kipenzi”……. “sawa love ngoja nikaoge kidogo ili nijiandae kutoka kwenda mjini nataka kumpeleka huyu jumaa”……… “sawa mume wangu acha nikakuandalie maji bafuni” mke wa hassan akaenda kumwandalia mume wake maji kisha akatoka na kimwambia mume wake, “tayari nenda kaoge mume wangu” hassan alichukua taulo na kwenda kuoga, alipomaliza alikuta mke wake ameshamwandalia nguo za kuvaa, akavaa na kuondoka.
Hassan na juma walikutana wakawa wanamsubiri niffer, “vipi kwani uliongea naye tena”……”ndio niliongea naye mala mbili akasema atakuja”…… “basi acha tumsubiri subiri”….. “sawa tumsubiri japo nina wasi wasi sana natamani nighairi”…… “kwanini?”….. “unajua yole hana mapenzi ya dhati na mimi, hivyo hata akikubali kuolewa je vipi swala la dini atakubali kweli?”…… “hapo kwenye dini sasa ndio shughuli hapo”…… “kama vipi tuache tu hili swala”….. “hapana usikate tamaa tutafanikiwa wala usijari”…… “yule anakuja sasa utamwambia nini ili akubali?”
“punguza pressure juma” walikaa kimya mpaka niffer alipofika, niffer aliwasalimia kisha akaketi, juma akasema, “karibu sana niffer”….. “ahsante sana”…… “niffer huyu mbele yako anaitwa hassan, yeye ni rafiki ila kwa sasa ni kama ndugu yangu maana tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka kumi sasa”…… “nafurahi kukufahamu hassan”….. “nafurahi pia”….. “hassan huyu ndio mrembo anayefanya nakosa raha, huyu ndio niffer aliyeniteka”….. “niffer umempa nini ndugu yangu maana hakuwa na nia ya kuoa kabisa sasa nashangaa ghafla tu anataka kuoa” niffer akajibu kwa kusema, “wala sijampa cha ajabu, ni yeye tu mwenyewe?”….. “sawa sasa niffer, naomba uwe muwazi, maana ndugu yangu amesema anataka kukuoa sasa sijui wewe unasemaje juu ya swala hili? Kwanza umempenda?” niffer alimwangalia juma kisha akasema, “changudoa huwa hapendi, huwa anafanya mapenzi kama biashara nikwambie tu ukweli miki naishi kwa kuuza mwili wangu, unanilipa nakupa utamu”…… “ila unapaswa kuolewa sasa na kuacha hayo mambo, unapaswa kuwa na nyumba yako”…… “nafahamu hasan lakini mimi sijui kama nitaweza kutulia ndani, mimi sina wikiend, siku zote naenda club na bar, ukinikosa forty forty, utanikuta triple seven, au viwanja vingine unadhani nitaweza kweli?”…… “mimi naamini unaweza ukiamua amua sasa”…… “sijui kama naweza”
“niffer wewe ni mwanamke, naamini ndoto za wanawake ni kuwa na familia kuwa na mtoto hivyo ndio mimi najua”…… “hassan sijuwa kama nitaweza sijuwa kiukweli, natamani lakini siwezi yaani naogopa kuja kufanya vitu vya hovyo sitaki kukutia doa”…… “niffer naomba ukae ufikilie hili kwa makini usikae kuangalia watu, hakikisha unaangalia kesho yako”….. “nitafikilia ila sidhani kama naweza, nani aliwahi kujaribu kuacha hii kazi akaweza? Hamna hayupo?”…… “yupo na kuhakikishia yupo, na ameweza kufanya hivyo, kwanini wewe uwogope”…… “siamini labda aje hapa aniambie yeye amewezaje?”……. “naweza kuongea naye kama atakubali kuja kuonana na wewe basi nitakwambia. Leo nipo na nafasi na hii ndio nafasi yenu pia kuhakikisha mnajitahidi kunishawishi juu ya hili”
Juma akasema “bro kama anaweza kuja mwambie aje, anisaidie kwenye hili”…… “kuongea naye sio shida ila inshu ni kuwa hapendi watu waijue historia yake, anachotaka nikuitengeneza kesho yake hivyo ni kama tutakuwa tunamkumbusha machungu na maumivu ambayo yeye anajaribu kuyasahau” niffer akasema, “anaishi wapi twende?”….. “anaishi nyumbani kwangu”……. “basi twende naamini atakubaki kuongea na sisi”……. “naogopa sana niffer ila kwakuwa lengo letu sio baya basi twendeni” walianza safari mpaka nyumbani kwa hassan. Mwendo wa takriban dakika ishirini mpaka kufika nyumbani kwa hassan. Walifika wakashuka kwenye gari na kuingia ndani. Waliingia ndani na hasan kuwakaribisha, walikaa na kisha hasan alimuita mke wake. Alipofika tu siting room, niffer akasema, “khaaa anifah?”…… “kwani unamjua?”
Hassan na juma wote walishanga kuona jennifer na Anifah wanajuana, anifaha alisalimia kisha aliketi, niffer akasema, “ndio maana moyo wangu ulikuwa unanisukuma kuja huku, habari yako za miaka mingi?” anifah akajibu “nzuri tu habari yako”…… “siamini kweli ni wewe?”…… “kwanini huwamini?”……. “naomba nijue umewezaje kuwa mke wa mtu, tena unavaa hivyo, juma anataka kunioa lakini sijui kama nitaweza kukaa ndani sijui”…… “unaweza kila kitu ni kuweka nia na kufanya maamuzi sahihi, acha nikwambie kitu huwezi ishi maisha ya kuruka ruka kama ndege hali yakuwa wewe ni binadamu. Kumbuka huwishi hapa duniani milele, pia unapaswa kuelewa kuwa unachofanya sio sahihi. Mimi naamini kabisa kunasababu imekufanya uwe hivyo ulivyo uwongo kweli?” niffer alifikilia, akiwa anafikilia anifar akasema,”mimi nilikuwa kama wewe, nilifanya kila aina ya starehe ni stly gani siijui, ni burudani gani siijui, ni party gani sijafanya ila maisha ya uhuni na kuruka ruka nimeona haya maana wala faidi yoyote. Mimi kwakifupi niliingia kwenye kazi hiyo kwa sababu, ya maisha magumu lakini pia ninkutokana na chuki ambayo nilikuwa nayo, wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikimuona mama yangu anapigwa na baba, anatukanwa na kunyanyaswa sana. Baba hakuwahi kwenda shamba wala hajawahi kufanya jambo zuri zidi ya mama.”
“Nakumbukw siku moja mama alinambia, ‘nateseka ila ili wanangu mkuwe unaona maisha yangu hayana furaha kabisa, nimekuwa mtu wa huzuni sana’. Nilikuwa nikawa nayaona hayo, lakini hiyo hali haikuwa kwetu tu, bali hata kwenye baadhi ya nyumba pale kijijini kwetu, niliamini labda inawezekana kuna sababu lakini sikuwahi kuijua. Nilianza kukuwa na kuvunja ugo, nikawa msichana sasa. Katika makuzi nikaanza kuwa na mahusiano nikiwa darasa la sita, lakini kijana niliyekuwa naye akawa na mwanamke mwengine. Nikajiuliza hii inasababishwa na nini? Nikaendelea kukua hivyo hivyo nikapa mahusiano mengine, nikapenda mwaname ambaye nilimpenda naye akaja kunitenda nikasema acha nisome kwanza, nikamaliza form four, nilipomaliza mama akasema itabidi uwolewe mwanangu umekuwa sasa, lakini kabla sijaolewa nilipata mwanaume ambaye alionyesha kunipenda sana.
“nisiwe muwongo hapa nilipendwa na kupenda sana, nakumbuka jioni alikuwa anakuja nichukua tunaenda mazoezini wote, wiki ende tunaenda wote kutembea, alinifanya nijisikie vizur muda wote, alinifanya nimpende sana. Alikuwa ni kijana mpole mcheshi na mzuri pia, nilimpa mwili wangu, akafanya anachotaka, nami zikumzuia, alinilazimisha kuniingilia kinyume na maumbile nilikataa sana lakini mwisho alinambia kama nisipokubali basi anatafuta mtu mwengine kwakuwa nampenda ikanilazimu nikubali, aliniahidi atafanya siku moja tu halafu hatutafanya tena, lakini waswahili husema ukishakula nyama ya mtu hutaacha utaendelea nisawa na mtu aliyeonja buyu la asali. Aliendelea kuniingilia nyuma kila tukikutana, nilijua sio jambo zuri lakini kwakuwa mpenzi wangu anafurahi basi acha nimpe atakacho, nilikubali hayo kutokana na hali ya nyumbani kwetu, nyumbani hakukuwa na amani, pia pesa haikuwepo hivyo yeye ndio alikuwa msaada wangu, alikuwa akinipa pesa na kuniliwaza. Pale nilipokuwa na mawazo basi alijitahidi niweze kufurahi. Lakini naukumbuka msemo wa mama alisema wanaume wameumbwa na tamaa hawaridhiki kamwe ndipo maana mungu aliwaruhusu waoe wake wawili mpaka wanne, japo leo hii naamini kwamba kila mtu na hurka yake, wapo wanaume wametulia na kuridhika. Kijana yule alichonifanyia kikaniingiza kwenye unywaji wa pombe, uvutaji sigara na nikawa sipendi tena?”……. “alikufanyia nini?”
Annifer alikuwa analia, machozi yalitoka alishindwa kabisa kujizuia, hassan alisogea karibu ya mke wake na kuanza kumbembeleza, na kumtia moyo ajikaze. Hassan alimfuta machozi mke wake na kumuomba aendelee, “mke wangu acha kulia, hayo yameshapita, jikaze” annifer akasema, “inauma sana, ndio maana huwa sipendi kuyakumbuka yaliyopita, kwani historia yangu ni mbaya ni yenye kuumiaza, lakini pia ni isiyofaa kwenye jamii”…… “hatuwezi kukijaji kwa jana yako, ila kwa leo yako, kwani hata shetani anaweza kuwa malaika kama atatubu zambi zake. Hata nawe sasa umekuwa mwema kwani umeacha yote hivyo acha kulia mpenz wangu, punguza munkari love” anniffer alivuta pumzi kisha akaanza kwa kusema, “mpenzi wangu yule alinitenda, alinisaliti, lakini ni bora tu angenisaliti kimya kimya, alifanya wazi nikaona, mbaya zaidi alinisaliti na ndugu yangu, alilala na mtoto wa baba yangu mdogo, inamaana alikosa wanawake wengine? Niliumia sana kutuchanganya, kuna wakati usiri unamadhara yake, nikajilaumu maana mdogo wangu alinambia dada kwanini hujanambia kama unatoka n huyu kijana? Na kweli sikumwambia. Hivyo hakuwa anajua na sio kosa lake, lakini yule kijana alifanya makusudi. Toka hapo nikawa naamini kuwa wanaume sio wakuwapenda nikaanza kujiingiza kwenye ukahaba, ulevi na uvutaji sigara, nilifukuzwa kijijini. Sikujari nikaondoka nikaja dar, nikaendelea na maisha yangu ya uzinzi na kujiuza. Nilipata kile ambacho nataka, nilipata pesa lakini pia nilipata penzi, leo nikiwa na huyu kesho nipo na mwengine, hayo ndio maisha yangu”
Jennifer akamuuliza annifer, “sasa ilikuwaje ukaamua kuacha ile kazi na kuolewa? Maan mimi najua ukifanya ile kazi wewe ni kunguru na tunajua kuwa hakuna anaweza kufuga kunguru” annifer akasema, “Jennifer sikuacha kwa siku moja, hapana ila ilichukua muda japo sio mrefu, kwanza kabisa mimi mwenyewe nilichoka lakini pia, siku moja nililala na mume wa mtu, yule mwanaume nililala naye mpaka asubuhi, asubuhi yule mwanaume alipigiwa simu, na mke wake, mke wake alikuwa analia na kulalamika, maneno yake yakanichoma sana, alikuwa akisema, “unaacha familia yako, unaenda kulala na malaya, makahaba, ambao hawajari familia yako, mimi mke wako ninaye kufuria, kupikia na kukufanya upendeze hunijari, ila elewa hao ni wapita njia hapa utarudi tu. Na nikwambie haya unayowafanyia wanao, watakuja kukufanyia wewe uzeeni usilalamike. Na mwambie hiyo mwanamke uliyenaye kuwa, atafute mume wake, ampendezeshe, sio asubiri wenzie wampendezeshe mume wao wamchukue, mwambie atengeneze wakwake wanaume wamejaa tele. Maneno hayo yaliniingia akilini lakini niliumia baada ya kusikia akisema, wanao jana wamelalia uji, hapa ndio nilipatwa na simanzi sana, maana usiku huo tulitumia pesa nyengi sana na yule mwanaume kwahiyo nikashangaa ni vipi anawaacha watoto wake na njaa. Nikajiona mkosefu sana nikajiona sina faida, nipo kwa ajili ya kuwaumiza wanawake wenzang hapo ndio nikaanza kuona ile kazi haina faida ila nikawana najiuliza nitafanya nini nikiach?” annifer alikaa kimya kidogo akijifuta machozi.
“Jennifer unaweza ukiamua, mimi niliamua nikamuomba mungu anipe mtu mwema nitulie, hapo ndio nikakutana na hassan nashukuru hassan akaonyesha nia ya kunioa nami siku kataa nilikubali, japo nilimpa mikakati yangu, naye akakubali na kunitimizia, baada ya kapo nikarudi nyumbani kijijini nikaenda kuomba radhi wazazi, nashukuru wakanisamehe, na hapo ndio tukaanza mikakati ya ndoa.” Jennifer akasema,”duuuuuh pole sana na hongera sana kwa kuthubutu, ila mimi sijui kama nitaweza.”…… “unaweza wewe na mimi kuna tofauti gani? Unanini hasa mpaka ushindwe? Kuna lipi baya ambalo linafanya wewe ushindwe kabadilika?”….
. “juma hata nioa nikisema, na mimi najiona kabisa sifai kuolewa bora nibaki hivi ni livyo, mimi ni zaidi ya shetani.” annifer akamwangalia sana Jennifer kisha aksema, “najua unaweza kuwa unahistori mbaya zaidi lakini haijariahi ila ni ukweli kuwa unaweza, ukiamua yote yanawezekana, ukisha amua basi anza kuswali kama tulivyoelekezwa, hapo ndio utaanza kubadilika” juma akasema, “Jennifer sijui umekumbwa na nini? Ila nikwambie tu ukweli, mimi siwezi kukuacha lakini pia nitakuwa pamoja nawe siku zote, nakupenda sana, naomba usiwe na was wasi kipenzi changu” Jennifer akasema, “wewe hujui tu niliyopitia, hujui roho yangu jinsi ilivyongumu, ungejua wala usinge sema hivyo?”……. “kwani umekutwa na nini?
“sijui nianzie wapi? Na sijui nitumie maneno gani?”……. “anzia popote, ongea chochote tutaelewa”……. “mama yangu alikuwa anaishi na mwanaume asiyempenda ili tu mimi nipate mahitaji, mwanaume huyo alikuwa mshezi, alikuwa akifanya chochote kwa mama yangu. Nilikuwa nikikua nikiona hayo, baba yuoe wa kambo hakuishia hapo, baada ya miaka kumi na tano mimi nikiwa binti wa miaka kumi na saba, siku moja nilizisikia vurugu chumban kwa mama, baba alikuwa akidai mtoto, akisema mama yangu ni gumbu hazai, mama akawa anamjibu kama ni gumba jennifer amamtoa wapi? Hivyo ugomvi ukazidi, baba akaona kama mama anamkesea adabu ni kama vile anamuona yeye ndio tasa. Alimpiga sana na kumuumiza. Kisha baba akaondoka zake. Nilimkuta mama yangu anavuja damu. Nikisikitika sana nilimwambia mama, twende hospital akakataa, nikachukua dawa na kumsafisha sehemu alizoumia. Nikimwambia mama tuondoke pale maana manyanyaso ni makubwa sana. Lakini mama alikataa sikujua ni kwanini alikataa nikimsihi sana lakini wapi? Haikuishia hapo baba aliporudi, alimuingilia mama kwa nguvu mbele yangu nikiona, ulikuwa uzalilishaji, sijui alikuwa ananifundisha nini?” Jennifer alianza kulia na kushindwa kuongea, anifer akamsogelea Jennifer na kumkumbatia, na kumsihi,”nyamaza mpaka mpenzi, pole sana hayo ndio maisha, yana mwisho na mwisho wa kuyasahau ndio huu, huu ndio wakati wa kufungua ukurasa mpya. Nyamaza kipenzi changu, nyama Rafik” annifer alimfuta machozi Jennifer.
Jennifer aliendelea kuongea kwa kusema, “baada ya tukio lile nilikuwa naona aibu kumwangalia mama yangu sikupenda alichofanyiwa, baada ya siku kadha baba alikuja chumbani kwangu akanambia, wewe unakula na kula bure, nimekusomesha mpaka sasa unamaliza form four sasa itabidi ukipie vyote, sikumuelewa alimaanisha nini na alikuwa ana lengo gani? Maisha yaliendelea, japo hayakubadilika, nilifanya mtihan wa kidato cha nne, na tulipohitimu tu, nikawa nashinda nyumban, maana siendi shule. Nilikuwa naenda na mama sokoni kuuza matunda lakini baba alikata akasema sipaswi kwenda sokoni natakiwa nibaki na nyumba niwe nailinda. Kumbe alikuwa na malengo yake. Mama alinambia bakia nyumban, huyu baba yako asije leta matatizo, nikamuuliza kwani huyu ndio baba yangu mzazi? Mama akanambia ukweki hapana sio yeye, nikamuuliza baba yangu yupo wapi? Mama akasema ni story ndefu mwanangu ila ipo siku utajua. Wakati tunaongea hayo kumbe baba anatusikiliza akaingia ndani, na kuanza kumfokea mama, alimpiga makofi na ngumi, kisha akambeba na kumpeleka chumbani, alimchania nguo na kumuingilia kingono kwa nguvu, mama hajawahi kuenjoy ndoa wala tendo lenyewe. Tabu hizikuishia hapo, baba akahamia kwangu, nikiwa nabaki nyumbani, akawa ananiletea zawadi mala nguo, mala hichi na kile, nashanga siku moja akanilietea shanga. Nilistaajabu sana”……. “kheeh alikununulia shanga?”……. “ndio alininunulia, tena sio moja zilikuwa nyingi, akisema wewe ni binti mzuri na mdogo unapaswa uvae hizi shanga, utapendeza sana binti, nilipokea na kusema ahsante, lakini baba alikuwa akiniangalia kwa jicho ambalo hakupaswa kuniangalia vile. Haikuishia hapo mama aliporudi nilimwambia kuwa baba alininunulia shanga, mama akakasilika kwani alijua sio jambo jema. Wakati tuanongea baba kumbe alikuwa nje anatusikiliza, akaingia ndani kwa hasira”
Sehemu Ya 5
Jennifer akanyamaza kidogo kisha akaendelea kusema, “baada ya kufungua mlango kwa nguvu na kuingia ndani, akaniangalia kisha akasema, kwahiyo wewe utanifanya nini? Nimeshamnunulia amua sasa cha kufanya, na naweza kufanya ninachotaka kama hutaki ondokeni hapa kwani mimi nina shida na nyinyi? Mama alinyamaza kimya, hakuongea neno, baba akaniangalia mimi kisha akasema na wewe, unajifanya unamdomo mdomo sana nitakuonyesha uwanaume wangu, kisha akaondoka zake. Nikamuuliza mama yangu, kwana baba yangu yu wapi ni bora niende kwa baba yangu, alichonijibu mama kikinifanya kuzidisha chuki na wanaume nilizidi kuona kuwa hakuna faida ya kuolewa, kutokana na aliyopitia mama yangu?”……”mama yako alikwambia nini?”
“sitaki kulikumbuka jibu la mama kwani mpaka leo naona kama ni mateso makubwa ndani ya moyo wangu, japo siwezi kulisahau, siwezi kulifuta kamwe! Mama yangu alisema, yeye alikuwa ni binti mrembo sana kijijini kwao, na hakuna mtu ambaye aliacha kumsifia, hivyo kutokana na uzuri wake wengi walivutiwa naye na kutaka hata kumuoa, lakini alikuja mjomba wake ambaye yeye anaishi huku dar sijui kama ni mzima mpaka sasa au laah, hivyo mama alichukuliwa na mjomba wake akaja dar, maisha ya dar yalizidi kumbadilisha mama na kuonekana mrembo zaidi, jambo pekee ambalo mama alinisisitizia kipindi chote hicho alikuwa ni mwari hajawahi kukutana na mwanaume yoyote yule, aliendelea kujitunza sana, mjomba ake mama akamtafutia mama kazi ya kibanda cha simu akawa anapigisha simu, enzi hizo simu za mkononi hqzikuenea watu walikuwa wanatumia simu ya mezani. Mama alifanya kazi pale kwa muda, mjomba wake mama akaanza tamaa za kumtaka mama, alianza kumshawishi kila mala alale naye lakini mama alikata. Hali hiyo ikampelekea mama kuogopa kurudi nyimbani mapema maana alikuwa anajua akiwahi kurudi atasumbuliwa na mjomba wake, hivyo alikuwa akichelewa kufunga ama akiwahi kufunga basi harudi nyumbani anatafuta sehemu anakaa kisha ndio anarudi nyumbani. Alichosahau mama ni kuwa alikuwa akimkimbia adui mmoja na kiwakaribisha kundi la maadui, laiti angelijua ni bora angekuwa tu anarudi nyumbani mapema, ila hakuweza kujua, kutokana akili yake ilikuwa ikiwaza kusumbuliwa na mjomba wake tu”
Jennifer akaomba maji, anifar akaamka na kumchukulia maji kwenye friji, kisha akamuwekea kwenye glass na kumpa anywe, jennifer alikunywa funda moja la maji kisha akaweka glass chini na kuendelea kusema, huku akilazimisha tabasamu, “mama yangu alipenda kunywa maji kama hivi hakika naendelea kumkumbuka sana, mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.” waliitikia “amiin” kisha juma akauliza “nini kiliendelea wakati mama yupo kwa mjomba?” jennifer akajibu, “mama aliendelea kurudi usiku, hapo ndio siku moja wahuni wakamlia rada, wakamgoja kwenye kichochoro wakambaka, walikuwa wanne wote walimuingilia, ukumbuke alikuwa ni bikra, hivyo maumivu yake hayaelezeki yalikuwa makubwa sana tena zaidi ya neno lenyewe. Mama aliahindwa kusimama, nguvu zilimuisha hatimaye akapoteza fahamu kabisa, alikuja kustuka yupo hospital, amewekea drip. Nesi alipokuja akamuuliza nani amempeleka pale akaambiwa ni raia wema tu, hivyo mama ilimlazimu aombe simu ampigie mjomba wake.
Mjomba wake alifika alipofika akamuuliza nini kimetokea, mjomba hakuonekana kukasilika, alilipa bill zote pale hospita na baada ya masaa kadh aliruhusiwa kurudi nyumban, lakini alipofika nyumban hali ikawa tofaut, mjomba wake akanza kumtukana mama na kumzihaki kwamba alikula pesa ya mwanaume halafu akaamka ndio maana wamembaka kumbe wala haikuwa hivyo. Mama aliendelea kujiuguza mpka alopokuwa sawa, aliporudi alipokuwa anafanyia kazi, pamewekwa mtu mwengine. Hivyo akawa amekosa kazi, akawa yupo nyumbani tu. Hiyo ilikuwa fursa kwa mjomba wake kuona ndio wakati wa kuzidisha usumbufu kwa mama, lakini mama alikataa, mama aliendelea kukataa huku akisema anaumwa, aliendelea kusema hivyo kwa muda. Mpaka pale mjomba ake alipoamua kumpeleka hospital na kupimwa, majibu yalibadilisha kabisa direction ya maisha ya mama, kwani alikutwa ni mjamzito, hapo ndipo mjomba wake akaamua kumtimua mama na kurudi kijijini, kijijini nako wazazi wake wakamtimu kwa kumuita malaya. Maisha yakaanza kuwa magumu, hakuwa anajua anaenda wapi?”
“baada ya hapo nini kilifwatia?” jumaa aliuliza, jennifer akasema, “akawa mtu wa kutanga tanga, akawa hana sehemu maalum, miezi tisa ikawa kama miaka, lakini hatimaye mungu akamsaidia akajifungua salama, ndipo nikazaliwa mimi. Mtoto ambaye baba yake hajilikani?” Jennifer akaanza kulia, kwa uchungu sana, huku akisema, “wanaume watu wabaya sana yaani mnahalibu maisha ya mabinti wengi sana, mnaua ndoto zao, mnaivunja mioyo yao, na hamna huruma mimi sijawaji penda na sijui kama naweza kupenda tena, moyo wangu unachiki dhidi yenu yaani nawachukia sana, ndio maana nikipata nafasi ya kuwaumiza nafanya hivyo sina huruma kabisa.” annifer akasema,”nyamaza kipenzi usilie, ni kweli kwamba samaki mmoja akioza ni wote ila, kumbuka wanasema ni wote kutokana na ile harufu inayotoka kwenye tenga la samaki, lakini ukimchukua huyo mmoja aliyeoza, ukamtupa wale wengine watabaki wazuri kwa ajili ya matumizi, ni kweli uchafu wa baadhi ya wanaume unachafua hadhi ya wale wanaume wanaojitambua. Jennifer kipenz hiyo chuki naomba ipunguze sawa mama?” Jennifer akamwangalia annifer kisha akasema,”annifer wewe hujui tu, hujui nini kimenikuta unajua kama nimempoteza mama yangu hivi unajua?”…….. “nini kimetokea kwani, hebu tueleze” machozi yaliifuta makeup yote ya Jennifer, yaliufunika uzuri wake na kuijaza huzuni sura yake, annifer alijitahidi kjmbembeleza Jennifer ili aweze kunyamaza, “punguza kulia basi kipenzi, nyamaza”
“mpenzi wangu, naomba nyamaza nipo hapa kwa ajili yako, pleas usijari nitahakikisha unakuwa na furaha, acha kulia” juma aliongea hayo, Jennifer akasema, “nakosa imani na wanaume sina kabisa sina, kama mtu aliyenilia alivunja moyo wangu vipi wewe juma utaweza?” Jennifer akaendelea kwa kusema, “unajua mnaona ni rahisi lakini sio rahisi hivyo?”…… “hebu tuambie ni nini kimetokea kwani” jennifer akafuta machozi kisha akasema, “mama baada ya kunizaa mimi alitafuta kibarua akawa anafanya kazi maisha yakawa yanaenda, ndipo akakutana na baba ambaye ndio mlezi wangu, wakakubaliana na kuanza kuishi wote mama anadai mwanzoni alikuwa ni mtu mwema lakini baadaye akabadilika akawa kama shetani akawa anampiga mama, anamwingilia kinyume na maumbile basi yaani ilikuwa vurugu vurugu. Mama alivyomaliza kunisimulia akasema, hakikisha maisha yako yana kuwa siotegemezi kwa wanaume maana sio wakuwaamini, hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kuongea na mama, ndio siku ambayo niliiyona sura yake na tabasamu lake. “………” kwani nini kilitokea baada ya hapo?”
“siku iliyofwata asubuhi na mapema mama akiamka na kuelekea sokoni, hakuniamsha maana alishaambiwa na baba asiende na mimi sokoni, hivyo mimi nikawa nipo nyumbani, nilikuwa chumban kwangu nimelala, mala nikastuka baada ya kuhisi kuna mtu ameingia chumbani kwangu, nilipofungua macho nilimuona baba akiwa ananiangalia, alipoona nimiamka akasema, usiogope, hapo akanisogelea na kunishika nikasogea pembeni, akanambia usiogope, kisha akanisogelea tena, na kuniambia nataka nikufundishe mchezo mzuri na mtamu, nikamwambia sitaki kufundishwa mchezo wowote, alipoona sitaki akanifwata na kunishika, akanifunua night dress yangu akaichana chupi yangu, akaniminya na na na?” Jennifer alishindwa kumalizia akawa analia, hassan akasema,” alikubaka????”
“ndio alifanya hivyo, ila alipoingiza tu, mama alikuwa amefika, na sijui alijuwa amesahau nini? Moja kwa moja aliingia chumbani kwangu akamkuta baba ndio yupo kwenye halakati hizo, mama alichukua kiti akampiga nacho baba, baba akageuka naye bila huruma akachukua kiti kile kile akampiga nacho mama, mama akaanguka chini, siuweza kuvumilia, pembeni yangu kulikuwa na kipande cha nondo nilimpiga baba cha kichwa, alianguka akafa, nikaita majirani, wakaja tukamuwahisha mama hospital lakini hakufika hata hospital akawa amefariki. Tulizika watu wawili, pale tulipokuwa tunaishi walikuwa hawajui mama kwao ni wapi hivyo alizikwa pale, baba naye alizikwa pale kwako ndip kwao. Nilibaki pekee yangu, sikuwa na mtu wa kunisaidia, sikuwa na ujuzi wala sikuwa najua ni wapi napata pesa. Shida kwangu ziliongezeka maisha yakwa magumu sana kwangu, hakuwahi kutokea jirani wala ndugu wa kunipa msaada na hii yote ni kutokana na marehemu baba alivyokuwa akiishi na majira zake, hakuwa anataka ukaribu wala kujihusha na watu, tena mama akienda hata kwenye shughuli ya jirani akirudi basi anapigwa, majiran walikuwa wanaogopa hata kuniongelesha kwa kumuogopa baba, hivyo hiyo hali ilinijengea wakati mgumu, ukizingatia nilikuwa mdogo sikuwa naweza kujitgemea. Siku moja nilikuwa na njaa sana sikula siku iliyopita na nililala na njaa, na siku hiyo kama ingeisha ingekuwa ni siku ya pili, nikiwa sijui nifanye nini akaja msichana mrembo sana akaniuliza habari yako? Nikamjibu mbaya, akaniuliza tena kwanini? Nikamwambia njaa inaniuma leo siku ya pili sijala. Alinichukua na kunipeleka nikale, baada ya hapo nilimsimulia kuhusu mimi, hapo ndio akanichukua na kuja naye mjini alinambia kuwa nisiwaamini wanaume. Na maneno yake yalikuja kutimia, siku ambayo alikufa mkononi mwangu?” Jennifer machozi yalimzuia kuongea maana yaliziba uzuri wake, huzuni ilitawala iliwagusa mpaka waliokuwa wanamsikiliza.
Ukimya ulitawala, kibaridi cha huzini kilitanda mahala pale, Jennifer hakuwa nasehemu kavu kwenye uso wake, mashamvu yake yalikuwa yamejawa na michilizi ya machozi, macho yake yalikuwa ni kama chemchem isiyokauka, juma alitoa kitambaa chake na kumfuta machozi Jennifer, huku mkono wake ukiwa unampapasa kwenye mgongo. “nini kilimkuta mpaka akafa mkononi kwako?” hassan akahoji, Jennifer akasema, “niliyopitia yawezakuwa ni kitabu cha kuwafunza wengine ujasiri, dada yule akawa dada yangu toka siku aliyonikuta na njaa akanichukua nikaja naye mjini alikuwa amepangisha, chumba na sebure, nilishini naye vizur sana takriban miezi sita, nikapa mpenzi ila hatudumu akaniacha nikabaki nalia hovyo, hapo ndio akaniambia usipende wanaume, watakuumiza kila siku penda pesa zao. Nikamwambia nifanyenini? Akasema kuwa kama mimi, ili upate mwili wangu lazima utoe pesa tena sio ndogo. Hapo ndio akaanza kuniingiza kwenye kazi ya uchangudoa. Niliona ni ngumu ila taratibu nikaanza kuzoea.”
“Nikaona ni kazi nzuri kwani, siumi moyo wala siteseki, sina muda wa kusema nisipojibu meseji baby atanunua, mimi ilikuwa tunakutana leo tunaishia leo leo, mambo ua kugandana hayakuwepo, kijiwe kikaanza kuchanganya nikapata kwangu nikahama, yule dada yangu aliyenisaidia akanambia amefanya kazi hii kwa muda sasa na amefika hatua anatamani kuolewa. Nilimwambia sawa, lakini unasema wanaume ni waongo je utaolewa na nani? Akanambia labda anaweza kubahatisha, siku zikaenda, siku moja akanambia njoo nikuonyeshe shemeji yako, nikaenda kumuona, alikuwa ni mkaka anapesa, mzuri na alionekana mwenye heshima zake, nilimtakia kila la kheri. Walikuwa wenye furaha, lakini kumbe uwongo na hulka la kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja ni wameumwa navyo wanaume, siku moja nikiwa na dada yangu, alikuja mama wa makamo akatusalimia kisha akasema, kati yenu nani sasha? Dada akasema mimi, yule maka akaniuliza na wewe unaitwa nani? Nikajibu naitwa Jennifer, akasema hili liwefundisho kwako Jennifer achana na wanaume za watu usijaribu kuwa na mume wa mtu, tafuta wako, mtengeneze na mtunze, baada ya hapo yule mama alitoa bastora na kumpiganayo sasha ya kichwa, dada yangu aliyenileta mjini naye akaanguka chini, nikamshika akakata roho akiwa kwenye mikono yangu, inauma sana, ni ngumu kuwaamini wanaume siwezi ni bora uniache jumaa?”
Jennifer aliamka na kutaka kuondoka, annifer akamzuia akamwambia,”hapa huondoki, hakuna kwenda sehemu nyengine, kama hutaki kuolewa ni vyema ukabaki hapa, umepitia magumu mengi, umepitia uchafu mwingi basi inatosha, kaa na mimi hapa, utavaa nguo zangu, utakula chakula changu, utalala ndani kwangu, mimi nina ofisi ndogo, tutaenda wote kutafuta ridhiki, achana na hiyo kazi, huna mama huna baba, huna ndugu, wengi ni marafiki tena sio marafiki wema. Siwezi kuruhusu tena urudi huko, nataka uwe mwema nataka kikao hiki kiwe ni moja ya kutubu kwako, machozi na maneno yako yakawe tiba kwenye moyo wako. Wewe ni rafiki yangu historia zetu zimefanana, wewe ni ndugu yangu, wewe ni mdogo wangu, wewe ni damu yangu baki tuanze safari mpya ya maisha.” annifer akaendelea kwa kusema,”tunapaswa kufuta yote ya zamani, tunapaswa kuandika ukurasa mpya, tunatakiwa kurudi kwa mungu, tuanze kufanya ibada, huo moyo mgumu uweze kuondoka, Mungu anaweza kufanya yote amini hilo, mimi haikuwa rahisi ila nimeweza”
Maneno ya annifer yaliingia taratibu kwenye masikio ya Jennifer, yakaanza kupenya kwenye ubongo wake, annifer akaendelea kwa kusema, “Huwezi kuwa mke kama huwezi kuondoa hiyo roho iliyokuvaa, chuki itaendelea kukuumiza miaka yote, na haitakupa faida, hivi jiulize kazi unayoifanya ya kuuza mwili wako huoni kama ni hatari kwa afya yako? Huoni kama wewe huna ndugu, jiulize ukizeheka ni nani atakusaidia na huna mtoto? Mimi nina mtoto wangu huyu wa kike nashukuru ndio rafiki yangu, ndio ndugu yangu naamini kabisa hata kama hatanisaidia sana lakini hata niacha nizalilike. Unapaswa kutafakari, hilo maana umri haurudi nyuma, unazidi kukua unazidi kuupunguza umri wa kuwepo duniani.” annifer aliendelea kwa kusema,”njoo huku twende” annifer alimshika mkono Jennifer na kumpeleka kwenye moja ya chumba ambacho hakikuwa na mtu, “jennifar hiki chumba hakina mtu, nyumba yangu ina vyumba vinne, wewe utalala hapa, hiki ndio chumba chako, hapa ndio utaishi.” annifer alimaliza kwa kusema, “nakupenda kwa ajili ya Allah”
Maneno hayo yalimfanya Jennifer atokwe na machozi na kisha kumkumbatia annifer, kisha akasema “annifer umekuwa rafiki mwema, umeongea maneno ambayo sikutarajia kuyasikia, nashukuru sana, nipo tayari kuishi hapa, lakini mimi sijui chochote kuhusu dini, sijawahi batizwa wala sijapewa kipaimara, sijaenda madrasa wala sijaenda msikitini, sijui chochote.” annifer akasema,”utachagua kama uwe mwislamu kama mimi au mkristo, kama utakuwa muislamu basi nitakuelekeza kila kitu na utajua maana hata mimi nilikuwa kama wewe, sikuwa na dini, sikuwa na elewa uwislamu wa ukristo, nikachagua uwislamu mwanzo nilichagua kwasababu ya mume wangu ni mwislamu lakini baadae nikavutiwa na mafundisho yake nikaamua kubaki kwenye dini hii. Sijui wewe utachagua wapi?”……”Na mimi nataka kuwa wewe, niite annifer yaani mimi annifer na wewe annifer maana annifer na Jennifer yanafanana hivyo sitakuwa mbali na jina hilo.”…… “sawa karibu sana mimi nitakufundisha kila kitu utakaa na mimi hapa?” mke wa hassan akamsilimisha Jennifer kisha akampleka Jennifer bafuni, akaoga akamtolea nguo akabadilisha kisha wakirudi siting room, hapo mke wa hassan akasema, “jennifar ataishi hapa, na kuanzia sasa ataitwa annifer, ili mututofautshe mimi niiteni mama sarah, annifer sasa ni muislam nitajitahidi ajue kila kitu, swala na vingine” juma na hasan walifurahi sana lakini juma akawa na swali kichani je vipi swala la ndoa amelikubali?
“kwasasa naomba mumuache annifer, mpaka pale akili yake itakapotulia, ili afanye maamuzi sahihi” mama sarah alionge maneno hayo na kuongeza kuwa, “annifer amepitia mengi magumu, ni kama mimi lakini binadamu tunatofautiana kwenye swala zima la kuyabeba matatizo, tunatofautiana kwenye kufanya maamuzi, hivyo hatupaswi kumlazimisha sana tukazidisha kumuathiri akili yake hivyo ni vyema tukamuacha akafikili taratibu” mama sarah alipomaliza kusema hayo, juma akasema, “shemeji nakushukuru sana lakini pia niombe radhi kwa niliyokufanyia huko nyuma, sikuwa najua kuwa wewe ni mwema hivi? Sikuwa najua kuwa unajielewa kiasi hiki? Mwanzo nilikuwa najua changudoa hawezi kuwa mke, niliposikia kuwa ulikuwa ni changuduoa nikataka kukujaribu kumbe nilikuwa na kosea, kumbe huwa wengi hufanya bila kupenda, ni kutokana na maisha jinsi yalivyo, huwa wamekutana na mengi. Naombeni sana radhi. Sasa nimejua kuwa hisia zinaweza mpenda yoyote kwani nilipojua kuwa wewe ulikuwa changudoa nikajiuliza bro wangu hassan amefwata nini kwako? Nikawa sijui kuwa mapenzi ni kitu cha siri, lakini pia hisia huweza kwenda pahala popote na bila kizuizi. Naombeni sana radhi sasa nimejua kuwa kila mtu anathamani yake, hivyo tunapaswa kuheshimiana kwani hujui mtu huyo atakuwa msaada wapi?”
Juma aliendela kusema,”Nimeamini sasa ukimuona mtu amempenda mtu mwengine usihoji maana kuna siri ndani ya moyo wake, kuna mengi yamefichika. Nisameheni wote nimejifunza” hassa aksaema, “uliwahi mtongoza mke wangu?”…… “niseme wazi nilijaribu kumshawishi japo sikumwambia nampenda ila nilijaribu kumshawishi, nilifanya hivyo, nisamehe sana kaka” mama sarah akasema, “mume wangu kuna siku niliwahi kukwambia angalia kuhusu marafiki zako sijui unakumbuka?” hassana akajibu “ndio nakumbuka mke wangu”…… “basi nilikuwa namaanisha hivyo nilikuwa sitaki kuwa wazi maana kama ningesema mngegombana na sitaki kuamini kama ungempa nafasi ajielezee, ila leo amejielezea mwenyewe, tena amejielezea kwa kirefu sana na sio kama ipo haja ya kumuwekea kifundo moyoni, inapaswa kumsamehe na marafiki na maisha yaendelee”…… “nimekuelewa mke wangu, maana hata Mtume wa Allah ametufundisha kuhusu kusamehe amesema tusamehe palo tunapoombwa msamaha lakini pia tunapswa kuwasamehe hata wale ambao hawajaomba msamaha. Ili nasi tunapoomba msamaha kwa Allha tusamehewe.”…….. “shemeji mimi nimekusamehe sina kinyongo na wewe.” juma akasema “ahsante shemeji nashukuru sana” hassan naye akasema, “juma tumepitia vingi mimi na wewe, tumekoseana mala nyingi sana kuna makosa ambayo labda saa hizi tusingekuwa wote hapa lakini tuliyamaliza.”
Hassan akaendelea kusema, “mimi niseme tu wewe ni bindamu na binadamu ni wazaifu tumeumbiwa kukosea, hivyo sina budi kukusamehe. Wewe ni ndugu yangu hivyo sina kinyongo na wewe nimekusame ondoa shaka juu ya hilo.” juma akasema, “nawashukuru sana kwa kunisamehe, hakika wewe ni ndugu yangu, nawashukuru sana, niseme ahsante kwa yote umekuwa ndugu mwema kwangu ukiniongoza kwenye mengi ukinisaidia vingi. Naomba Mungu atujaaliye tuwendelee kuwa hivi, atupe afya njema na baraka tele.” wakiwa wanaongea simu ya annifer ikaita, wote wakawa wanamuangalia annifer, annifer hakupokea simu, simu ilipokata akaizima akatoa laini na kuivunja vipande vipande, hassan akauliza,”mbona unavunja laini?”
Walisubili jibu kutoka kwa annifer, lakini hakulitoa. Mama sarah akasema “huwezi kubadilika kama bado unamarafiki wa zamani ambao wanatabia zile zile, hata nami nilibadilisha laini na sikutaka watu wajue naishi wapi, hivyo annifer yupo sawa” baada ya maongezi ya muda mrefu juma na hassan waliaga na kuondoka zao kwenda mjini. Annifer na mama sarah walianza kufundishana mambo kadha ambayo ni muhimu muhimu, “ulijifunza wapi hivi vyote?” annifer alihoji, mama sarah akasema, “vingi amenifundisha mume wangu japo pia kwa sasa nahudhulia darasa la kina mama pale msikitini hivyo naendelea kujifunza vingi”……. “na mimi naweza kwenda kwenye darasa au siruhusiwi”…… “kwanini usiruhusiwe? Unaruhusiwa kwenda nitaenda na wewe kesho jioni maana leo hamna darasa”…… “sawa nitafurahi nikijua kama wewe?”…… “utajua tu annifer”…… “mbona nasikia wale vijana wanao uza laini huko nje?”……. “subiri” mama sarah akamuita binti yake wa kazi, alipokuja akamwambia, “nenda kaangalia kama kuna wale vijana wanauza laini, waite watusubiri hapo nje” Nintendo alitoka nje, baada ya dakika tagu alirudi na kusema, “wanawasubiri hapo nje” mama sarah na annifer walitoka nje wakawakuta wale vijana wakasajiliwa laini mpya, annifer akaiweka kwenye simu, na kuanza kutumia laini nyengine.
Upande wa rafiki zake annifer(Jennifer) waka wanapiga simu ya annifer haipatikani, “huyu Jennifer amepatwa na nini? Simu iliita mala moja sasa hivi haipatikani”…… “au amepata danga atakuwa kazini”…… “hapana sio kawaida yake angesha sema huwa anatoa taarifa”….. “kwani alipoondoka alisema anaenda wapi?”…… “alisema anaenda kwa yule mwanaume ambaye anataka kumuoa”……. “mmmmmh nina wasi wasi sana”……. “ngoja tuone kama asipopatikana mpaka kesho utabidi twende polisi na tuanze kumtafuta maana nijuavyo mimi hana ndugu yule”……. “Ni kweli halafu yule mwenyewe ndio boss wetu hapa, maana sisi wote tunaweza kosa soka ila sio yule”…… “watu wanazaliwa na bahati zao bibi wewe” walicheka kwa sauti na kisha wakasema “weeeeweeeeee” muda ulizidi kusogea hatimaye giza likaingia. Jamani tujiandaeni twendeni kazini. Marafiki wa annifer wakajianda na kwenda kutega mingo. Walienda kufanya biashara ya kuza miili. Upande wa annifer na mama sarah walikuwa wakianda chakula, mala walikuja juma na hassan, wakasalimiana na kisha waliketi na kuanza kula chakula kwa pamoja, “annifer anakichwa chepesi sana anashika halaka ukimwelekeza mashaAllah”…… “mashaAllah, ni jambo jema Mungu azidi kumsimamia inshaAllah” wakaitikia wote InshaAllah. Wakiwa wanakula na kimya kimetawala, sarah akasema, “Mama na wewe utava suruali kama ile ya mamdogo mchana?” waliangaliana kisha mama sarah akasema, “ile suruali sio ya mamdogo, ile suruali ni baba ile, mama yako mdogo ameibiwa nguo zote ndio maana akava kwanza ile, ndio maana umeona sasa hivi amevaa nguo hizo” sarah aksema, “masikini, pole mamdogo basi nikupe na mimi baibui langu uvae, waizi watu wabaya, tuishi wote hapa usiende tena huko hapa hawatakuibia sawa mamdogo” annifer alitamani kulia macho yake yalianza kabisa kujaa machozi na huzuni, annifer akasema, “nitaishi na wewe hapa sawa sarah, siondoki”….. “safi sana, nitakuwa rafiki yako, kama vile mimi na mama, huwa tunasoma hadithi mimi na mama, na wewe utasoma na sisi haditi tukimaliza kula sawa” sarah alikuwa ni binti mdogo sana lakini maneno yake yalimfariji annifer, na kuona kuwa yupo kwenye mikono salama.
Alfajiri mama sarah akamuamsha annifer ili waswali, akamuelekez kwa vitendo baadhi ya vitu kish wakaswali, walipomaliza wakaweka darasa wakaanza kuelekezana vitu mbali mbli vya dini. Kulipambazuka na jua likaanza kuchomoza wakaanza kufanya shughuli za nyumbani kisha annifer akasema, “nahitaji kwenda kule nilipokuwa nataka kwenda kuwaaga, pia nichukue baadhi ya vitu vyangu, lakini pia nataka wasije nitafuta, maana najua watakuwa na wasi wasi wasije enda polisi bure”…… “ok sawa usijari tutamwambia baba sarah twende” walijianda na kiisha hasana, juma, annifer na mama sarah wakaondoka kuelekea kule alikokua anakaa annifer. Safari ya masa mawili wakawa wamefika, walipofika annifer alibisha hodi, na kuingia ndani, “khaaaaa wewe ndio wakuvaa baibui?”
Wote wanne walishanga kumuona annifer vile, “haya Jennifer umekutwa na mangapi shoga angu?” annifer hakuwajibi akaingia chumbani akavuta begi lake akachukua vitu vyake vya muhimu vyote kisha akatoka, “mbona na mabege tena vipi mbona hivyo?” annifer akawaza majibu ya haraka haraka akaona akisema ukweli itakuwa shida maswali yatakuwa mengi, akaona bora adanganye, “acheni niwahi nina msara hivyo sitaki muingie kwenye huu msara, akija mtu yoyote kuniulizia mwambie hamnijui wala hamjui nilipo, sawa?” annifer akatoka mbio mbio akaondoka zake, aliwaacha wenzie na maswali kibao.
“itakuwa amefanyaje?”…… “sasa unamuuliza nani wote tupo humu ndani tutajuaje?”……. “au kaiba?”….. “yule muwoga sana hawezi kufanya hivyo?”……. “mmmmh sasa sijui kafanya nini?” ukimya ukatawala, mmoja akasema, “nahisi inawezekana yule jamaa anayesema anataka kumuoa labda wamekubaliana sasa anatafuta njianya kutukimbia”……. “hiyo sio kweli, hivi unamjua Jennifer wewe?”…….. “kwahiyo unahisi sio hivyo?”…… “ndio itakuwa kitu chengine, Jennifer anawachukia wanaume sana ndio maana nakwambia inawezekana kaiba au kamzingia mwanaume sasa kuna kesi ila kupenda hapana nakata”….. “mmmmh ok sawa acha tumpotezee, ngoja tuangalie kwanza asije kubebe na vitu vyetu”……. “hilo neno halafu tumejisahau kabisa” waliingia chumbani wakakagua sehemu zote, “huyu atarudi umeona nguo zake nyingi anazozipenda kaziacha kabeba chache sana”…… “kabeba tu perfume, mafuta cheni, heleni, na nguo kidogo”…… “basi huyu atarudi anasikilizia upepo tu”…… “tuachane naye tuendelee na mishe zetu” waliendelea na mambo yao bila kuwa wanaujua ukweli kuhusu Jennifer ambaye sasa anaitwa annifer. Upande wa Annifer aliingia kwenye gari na kuwaambia hasan na jumaa, “twendeni sina ambacho nimbacho kina niweka eneo hili tena, naenda kuanza maisha mapya” hasan na juma waliangalia, juma akawasha gari wakaondoka zao. Wakiwa njiani hassan akasema “tupitie mjini tumnunulie annifer nguo maana anaswali hivyo anahitaji nguo za kuswali maana naamini nguo zake za zamani nyingi sio nzuri” walikubaliana na kuelekea mjini kumnunulia nguo annifer.
Walifanya shopping na kisha kurejea nyumbani. “Ahsanteni sana nashukuru kwa upendo na wema mnaoendelea kunionyesha mungu awabariki sana” hassn akasema, “usijari kuwa huru, hapa ni kwako”. Maisha yaliendelea, mama sarah aliendelea kumfundisha annifer mafundisho ya dini na mengine mengi, pia alianza kwenda naye kwenye madarasa ya jioni ya kina mama msikitini, mama sarah hakuishia hapo akaanza kumfundisha kazi mbali mbali, alikuwa akienda naye kwenye saloon yake, alikuwa akienda naye kwenye duka lake la miamala ya kifedha kwa njia ya simu, walianza kuwa marafiki wazuri walishibana kwenye mambo mema, “mama sarah, muda wa swala huu nenda kaweke udhu tuswali acha kuchezea simu” annifer ilikuwa anamkumbusha mama sarah muda wa ibada. Hapa ndio lile neno la kusema, shetani pia anaweza kuwa malaika, ndio linatimia. Kwani kila mmoja ananafasi ya kuwa mtu mwema. Siku moja annifer akiwa anatoka nyumbani anaenda ofisi kwa mama sarah, akiwa njia ilisimama gari nzuri sana na ya gharama, “habari yako mrembo” annifer akageuka kuangalia ni nani anamsalimia, alipomuona alitaka kuondoka lakini akakumbuka, kuwa muungwana hakatai salamu, aliitikia salamu, kisha akataka kuondoka, yule mzeee wa makamo ambaye alikuwa ndani ya gari akasema, “samahani mrembo naomba dakika moja tu niongee na wewe?”…… “nina halaka sana sijui kama utaweza kuongea upesi niwahi”…….. “sawa usijari, mimi sina maongezi marefu sana, kwa kifupi mimi leo sio mala ya kwanza nakuona, ila ni mala ya kwanza kuongea na wewe, kwa kifupi nimevutiwa na wewe, naomba uwe mke wangu, niruhusu nikuoe nimekupenda”……. “hivi umechanganyikiwa au?”……. “hapana nina akili zangu timamu, nakupenda?”
“nimekuelewa, uwe na siku njema” annifer aliondoka akawa amemuacha mzee yule pale akiwa hajui kuwa amekubaliwa au amekataliwa. Annifer alienda kwenye shughuli zake, akafanya kazi mpaka Jioni alipofunga ofisi. Alipofiia nyumbani alimkuta mama sarah, wakasalimia na kisha akaenda bafuni akaoga, alipotoka akamfwata mama sarah, wakaanza kupiga story, “annifer rafiki yangu, nimekaa na wewe huu ni mwezi watatu, nafurahia kuwa na wewe umebadilika na kuwa mtu mwema, nafurahi kukuona ukiwa mtu mpya Mungu akubariki sana kipenzi” mama sarah aliongea hayo, annifer naye akasema, “amiin rafiki, shukrani nyingi zikuendee wewe rafiki yangu, umekuwa na mimi bega kwa bega, nawe Mungu akubariki sana kipenz chagu”….. “amiin”…… “nina kitu nataka kukwambia”…… “niambie tu annifer”….. “Sasa nipo tayari kuishi na mwanaume, nahitaji kuwa na kwangu sasa, nafurahi kuona maisha yenu wewe na shemeji hapa mnavyoishi, ni maisha mazuri yanavutia, naamini ni muda sahihi na mimi kuolewa”…… “waoooow yaani nimefurahi kusikia hivyo, maana jana tu shemeji juma ametoka kunambia jambo hilo hilo?”….. “mbona mimi haniambie au hanitaki tena?”…… “ingekuwa hakupendi angekuwa anakuhudumia kweli? Anakupenda sana ila tulimsihi akuache utulize akili yangu, mpaka pale utakapo amua kwa hiyari yako”….. “sasa nipo tayari”….. “kwahiyo nimwambie?”…… “ndio mwambie, mwambie nipo tayari kuwa mke wake”….. “sawa mpenzi nitamwambia, usiku nitamwambia mume wangu, yeye ataenda kumwambia rafiki yake.”….. “sawa nashukuru” maongezi yaliendelea mpaka muda wa chakula ulipofika wakenda kula, kabala hawajamaliza kula hassan aliingia, akasalimia na kisha kuketi na yeye akajiunga na kuaanza kula. Walipomaliza kula. Hassan akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake.
Muda wa kulala ulipofika, mama sarah alimwambia mume wake kwa utulivu na mahaba makubwa, “mume wangu, nina jambo la kheri nataka kukwambia”….. “jambo gani mke wangu?”….. “ni kuhusi aniffer, annifer amesema yupo tayari kuolewa na juma”….. “MashaAllah, Mungu ni mwema, hatimaye sasa ufahamu wake umerudi sasa ni wakati wa kuishi na mume wake kesho panapo majaariwa nitaongea na juma, kisha nitasimamia maandalizi yote ndoa iweze kufungwa halaka iwezekanavyo.”….. “sawa mume wangu fanya hivyo” baada ya maongezi hayo wapendao walila. Asubuhi na mapema hassan alimpigia simu juma aweze kuja nyumbani.
Juma alipokuja akakutana na hassan wakazungumza, “annifer yupo tayari sasa kuolewa, ametamka kwa hiyari yake, naomba kukuuliza kaka hutamuumiza binti wa watu? Usije mfanya akarudi kwenye maisha yake ya mwanzo, hakika ukifanya hivyo moto wa jahannam yatakuwa makazi yako”…… “bro nakuahidi nitakuwa mume mwema, nitampenda na kumheshimu.”…… “sawa haina shida, inatulazimu tufanye maandalizi ya ndoa”…… “ni kwanini tusifanye kesho kutwa ijumaa?”…… “sawa ngoja tuwaite hawa wanawake” juma alimuita mke wake pamoja na annifer. “annifer nilikuwa naongea na juma hapa na amefurahi sana kuona umekuwa Tayar maana amekusubiri kwa muda mrefu, sasa tumependekeza ndoa iwe kesho kutwa ijumaa hapo msikitini” annifer akasema, “sawa shemeji mimi nipo tayari hata ikiwa sasa”. Wote walikuwa na furaha kusikia hivyo.
Maandalizi yalifanyika, ijumaa ilipofika ndoa ilifungwa, Ndoa ilifungwa saa saba mchana, baada ya ndoa, juma na annifer walielekea airport na kwenda zao hanemoon zanzibar. Walifurahia wiki mbili za mwanzo za ndoa yao. Walipomaliza hanemoon walirudi nyumbani na kuendelea na maisha ya kawaida. Annifer na juma wakiishi kwa amani na wana mtoto mmoja. Annifer hajawahi kuacha kufanya ibada hata siku moja, naye juma kwa sasa naye anaswali swala tano kama mke wake.
****MWISHO***

