KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 37
Sala yangu ilitumia dakika 15, hatimaye zilibaki dakika 15 Docra aondoke, nilitoka nje nilizama kwenye gari yangu kisha niliondoka kwa kası ya ajabu. Si unajua tena mambo ya dar foleni, bası nikiwa nakaribia hotelini njiani nilikutana na bonge la foleni ya magari, nilisubiri nikidhani foleni itapungua lakini wapi, nilitazama saa zilibaki dakika 7 Docra aondoke. Weuwee! Unajua kuvurugwa? Nilipagawa hadi nilijionea huruma. Nilisogeza gari kwenye parking ya benki flani kisha nilishuka, nilianza kukimbia kuelekea hotelini, nilichapa mwendo hadi mjengoni, hatimaye zilibaki dakika 2, sikutaka hata kuwasikiliza wahudumu, nilipita mapokezi kwa spidi kali kila mtu akinishangaa, moja kwa moja nilizama kwenye chumba husika, nilimkuta Docra akibeba mkoba wake akitaka kuondoka.
“Usiondokee…usiondokee” Nilimvamia hadi kitandani na mabusu yalianzia hapo hapo. Nilishtushwa na mlango ambao uligongwa, nilienda kucheki nilikutana na muhudumu ambaye aliniuliza kwanini nimeingia bila hodi? Docra alikuja mlangoni alimwambia kuwa mimi nipo na yeye, muhudumu aliondoka.
Nilifunga mlango kisha kwa mara nyingine nilimvamia Docra, kilichofuata hapo nashindwa hata kusimulia, ila ngoja niwaelezee kidogo; sikuwa na haja ya kumtoa mtu viwalo, nilichokijua ni kuupitisha mdomo wangu juu ya kifua chake na kat i kat i ya mapaja ya ke, sikutaka kusikiliza kelele ambazo alinipigia; nilijua kuwa hizo sio kelele bali ni burudani isiyoumiza. Mambo ambayo nilimfanyia hata m ke wangu hajawahi kuyapata, ilikuwa ni kama naweka heshima bar. Maandalizi tu yalitumia saa nzima, nilihakikisha kila sehemu ya mwili wake inakuwa laini laini, kuna muda alinikumbatia kwa nguvu kisha alinipa ishara niingie vitani; Nilitaka kupigana kirahisi lakini nilikutana na upinzani, kumbe jeshi hilo lilikuwa linaingia vitani kwa mara ya kwanza, hivyo basi sikutakiwa kuwa na papara, nilitumia akili nyingi kuhakikisha naliteka jeshi hilo! Vita haikuwa ndogo hata kidogo, kila nikipiga bastola nililambwa teke, kila nikipiga bastola nililambwa ngumi, kuna muda nilijifanya kama sitaki vita vile; ghafla nilipiga bunduki ilipenya hadi kwa waasi, nao hawakuniacha salama, walinikandamiza meno ya bega.
Mapambano yaliendelea, kuna muda nilishinda lakini nilianza upya. Waasi walinilalamikia kuwa niwaonee huruma lakini sikujibu kitu, wao ndio walitaka vita, nilipiga mishale, nililenga shabaa, ilifikia hatua waasi walinogewa na vita, walijibu mashambulizi ambayo yaliwaingiza katika furaha yenye ushindi wenye raha! Hadi tunakuja kumaliza vita Docra alikuwa hoi bin taaban, hakutaka kunitazama usoni, alivuta shuka alijifunika kisha alianza kulia kilio ambacho hadi leo sikujua kina maana gani.
****
Mahusiano yangu na Docra yalianza rasmi, siku ya kwanza ilipita tulilala pamoja, hata hivyo usiku sikulala usingizi niliogopa kufa. Kwakuwa sikupata usingizi asubuhi niliwahi kuamka, nilijaribu kumuasha Docra aliniambia kuwa hawezi kuamka pia alishindwa kutembea. Nilienda kuchukua gari yangu pale benki, niliikuta ikiwa salama kabisa, nilizama ndani kisha nilirudi hoteli nilimkuta Docra bado kalala lakini alikuwa macho. Nilimuuliza vipi kuhusu mzigo ambao nilimletea, alikubali kufanya biashara ya mchele na unga ila alitaka tuifanye wote wawili, yaani iwe ni biashara ya mapenzi yetu. Alinivuta kitandani kisha alinituliza kwa busu maridani, kwakuwa usiku sikulala nilipitiwa na usingizi. Nilikuja kushtuka mchana saa 8, Docra alikaa pembeni akiwa anatabasam tu, mezani kulikuwa na chai ya asubuhi pamoja na chakula cha mchana, nilimuuliza yeye kama amekula aliniambia alikuwa ananisubiri niamke ili tule wote. Kwanza tulioga kisha tulikula pamoja, nilitaka nikaonane na dereva wa kenta ya mizigo lakini Docra alinikataza, aliniambia kuwa siku hiyo ni siku ya kufurahia penzi letu, marufuku mtu kutoka nje.
Kwa mara nyingine tulipanda kitandani, kwa mara ya pili tulipigana vita nyingine, taratibu alianza kuzoea mapambano, ilikuwa ni mwendo wa bandika bandua. Siku nzima tuliimaliza chumbani, kazi yetu ilikuwa ni kula, kuoga na kupigana. Siku iliyofuata Docra alikuwa mzima wa afya, hapo sasa tulielekea kwa madalali ambao walitutafutia chumba cha biashara ambacho kilifanana na aina ya biashara yetu. Nilimpigia dereva nilimuelekeza aniletee mzigo katika chumba hicho, alifanya kama nilivyomuambia, mzigo ulishushwa uliwekwa ndani ya mjengo. Nilikaa Dar kwa wiki moja, tulihakikisha biashara inakaa sawa kisha nilimuaga kuwa narudi nyumbani. Kwakuwa alijua kuwa nina mke aliniruhusu niende ili nisihisiwe vibaya na mke wangu, tuliagana kimapenzi, tuliachana kimapenzi, yeye alibaki Dar akiendelea kusimamia duka letu.
Nilifika nyumbani mke wangu hakujua chochote kilichoendelea, na uzuri ni kwamba sikufa wala sikufufuka; maisha yaliendelea. Wiki moja ilikatika nikiwa Mbeya, muda wote Docra alikuwa akinipigia simu akinijulia hali, kuna muda aliongea na mwanangu na mke wangu pasipo shida yoyote. Biashara zangu zote zilikwenda powa, nilikuwa nawasiliana na baba yake Docra ambaye alinipa “updates” zote kuhusu duka langu la marekani.
Sasa siku moja hivi nikiwa dukani kwangu nilipigiwa simu na Docra ambaye alitaka kuniambia kitu flani, kwanza aliniambia nisishtuke na nisiwe na wasiwasi, nilimuuliza ni kitu gani hicho? Aliniambia kuwa ana ujauzito wangu.
SEHEMU YA 38
Nilishtuka japo sikushangaa sana kwa sababu siku tupo vitani sikutumia kinga wala tiba, kitu pekee ambacho niliogopa ni ishu hiyo kumfikia mke wangu; sikujua ataipokea vipi. Docra yeye alifurahi sana, aliniambia kuwa Mungu ametuletea baraka na anajisikia vizuri kubeba mimba yangu.
“Derick au umechukia mimi kushika ujauzito?”
“Hapana, ila sijui itakuwaje siku mke wangu akijua. Pia bado sielewi hatma ya mimi na wewe”
“Una maana gani kusema huelewi? Kwamba unataka kuniacha au?”
“Kama nilikula kiapo na nimemsaliti mke wangu kamwe siwezi kukuacha. Wewe unajua kuwa nakupenda sana, na kwa jinsi ambavyo nakupenda nipo tayari nikuchagua wewe kuliko mke wangu; hilo liko wazi siwezi kulikataa”
“Kweli Derick?” Aliniuliza akiwa anafurahi
“Yeah! Hata hivyo siwezi kumuacha yeye kwaajili yako na siwezi kukuacha wewe kwaajili yake.”
“Kwanini umesema hujui hatma yetu?”
“Kwa sababu mimi ni mkristu, nina mke na familia. Nimekupa ujauzito wewe ambaye tunapendana, sasa hili penzi letu hatma yake nini? Kwamba nitakuwa nakuzalisha tu au tutaachana kisha utaolewa na mtu mwingine?”
“Mh jamani, kwani we unaweza kuruhusu tuachane?”
“Nimekuuliza tu kwa sababu hadi sasa sielewi cha kufanya”
“Derick mimi nataka unioe. Kama wakristu huwa huwaoi mke zaidi ya mmoja basi naomba wewe uwe wa kwanza kuoa wake wawili, mimi nipo tayari kuwa bi mdogo, na nakuahidi nitakuwa mwema kwako. Vipi umekubali?”
“Mh! sidhani kama naweza kukataa ombi lako lolote, ila sasa vipi kuhusu wazazi wako? Wataruhusu kweli?”
“Labda shida itakuwa kwa mke wako, mimi kila kitu nimeweka sawa. Mama yangu anajua kuwa nakupenda, baba yangu anajua kuwa nakupenda, kubwa zaidi wote wanajua kuwa mimi na wewe ni wapenzi. Hata kuhusu hii mimba yangu wanafahamu, pia nimewaambia kuhusu mpango wangu wa kuolewa na wewe; wamekubali.”
Tuliongea mambo mengi, kubwa zaidi alinisisitiza kuwa anataka ndoa. Kwakuwa nilimpenda nilimkubalia kila kitu japo kuna ugumu niliuona mbele yangu. Baada ya kukata simu nilitulia nikiwaza jinsi itakavyokuwa; “Dah! Hata kama nampenda Docra ila siwezi kumuambia mke wangu hii ishu, itabaki kuwa siri yangu” Niliwaza, mara nilihisi maumivu ya kichwa, nilihisi labda ni kichwa cha stress tu lakini kadri dakika zilivyozidi kwenda mbele maumivu yalizidi, nilirudi nyumbani ili nikapumzike. Mke wangu alinikanda maji kichwani, kutokana na uchovu niliamua kulala. Asubuhi niliamka nikiwa mzima, ila sasa nikiwa naenda kazini ghafla nilikanyaga chupa ambayo ilizama chini ya sendo zangu hadi kwenye mguu wangu, maumivu ambayo niliyapata nilijikuta nakaa chini nikiugulia uchungu wa chupa. Jamaa yangu mmoja ndiye alinisaidia kuchomoa kile chupa kisha alinipa lift ya boda alinirudisha nyumbani, mke wangu alinipa tiba ya asili; alinimwagia mafuta ya taa ili kuzuia sumu na damu. Jeraha hilo lilinisumbua kwa wiki nzima; leo linapona alafu kesho linajaa majimaji yenye usaha, siku nyingine lilivuja damu, nilipona mara baada ya kupewa matibabu ya hospitali.
Zilipita siku mbili mara baada ya kupona jeraha la chupa, siku hiyo nikiwa narudi kutoka kazini nilijikwaa kwenye jiwe kisha nilidondokea mkono wangu, haukuvunjika wala haukupinda ila ulivimba; ulikuwa mkubwa kama mguu vile. Mke wangu baada ya kuniona alinishangaa, aliniuliza nina shida gani? mbona kila siku majanga tu?. Kiukweli hata mimi sikujua kwanini majanga yamezidi, nilijua labda ni vihoma vya kawaida tu. Siku zilikatika nikishinda ndani, michongo yangu ilianza kukwama, hata kuhusu biashara ya nje ni Docra ndiye alinisaidia kutuma mizigo na kila kitu.
Mkono ulinisumbua kwa muda mrefu hadi nilishindwa kuelewa, m baya zaidi hata kitandani nilishindwa kumtimizia mke wangu, alinipigisha mazoezi ya kutosha lakini sikuwa na hamu ya kuingia vitani, alinishangaa sana. Kabla sijapona mkono mara miguu nayo ilianza kuvimba, kichwa kiliuma, mke wangu alinipeleka hospitali lakini baada ya vipimo madaktari walisema sina tatizo lolote. Nikiwa hospitali Docra alinitembelea kuja kuniona, huwezi amini baada ya kumuona Docra nilihisi kupona, sikuhisi maumivu yoyote, hata tulivyorudi nyumbani nilishangaa mkono wangu ambao ulivimba ulirudi kwenye hali yake, miguu nayo iliaoha kuvimba, maumivu ya kichwa yalipona.
Siku hiyo Docra hakutaka kulala nyumbani kwangu, aliaga kuwa anaondoka ila hakuondoka, alichukua gesti kisha alinitumia meseji kuwa amenimiss. Pia kitu kingine ambacho kilinishangaza ni kwamba baada ya Docra kuondoka nyumbani kwangu; homa yangu ilianza, mikono na miguu vilianza kuvimba tena. Nilimuaga mke wangu kuwa naenda kucheki biashara lakini alikataa aliniambia nipumzike nisije nikapata matatizo mengine. Hata hivyo Docra alizidi kunisumbua niende gesti, na ukicheki hata mimi mwenyewe nilimiss penzi la bebi wangu mpya, nilimtoroka mke wangu nilienda kwa Docra. Ajabu ni kwamba nilivyofika gesti viungo vyangu vyote vilipona, hata vitani nilipambana vizuri sana, nilipambana hadi nilishinda kwa kishindo.
“Docra” Nilimuita mara baada ya kumaliza vita.
“Nambie mume wangu”
“Hivi hujaniendea kwa mganga kweli?”
“Una maana gani kuniuliza hivyo?” Aliniuliza akinishangaa
“Tangu nianzishe mahusiano na wewe kila siku nimekuwa naumwa, mara leo kichwa, kesho mkono, kesho kutwa mguu. Mbaya zaidi nikiwa nawe tunafanya vizuri tu lakini nikiwa na mke wangu sifanyi kitu, kwanini?”
SEHEMU YA 39
Wakati namuuliza swali hilo sikuwa na maana ya kumuwazia ubaya, sikumaanisha kwamba yeye ni mshirikina wa moja kwa moja, ila nilitaka kujua tu kama kuna shida yoyote. Hata hivyo hakukasilika wala hakununa, alitabasam tu kisha alicheka kidogo alafu alinitazama usoni, alibaki ananitazama tu pasipo kunijibu kitu chochote.
“บทacheka badala ya kunijibu?”
“Hivi unaona nafanana na uchawi mimi? Kwa jinsi navyompenda mkeo na mwanao nitaanzaje kumroga? Ili iweje? Ili umuache alafu uwe na mimi? Hapana. Mimi sina shida yoyote, wewe ndo una matatizo”
“Matatizo gani?”
“Sijui mwenyewe. Alafu kwani anayepata shida ni mkeo ลน wewe? Kama ningekuwa namroga mkeo, sasa kwanini shida uzipate wewe?” “Kwahiyo ku m be unaniroga mimi ili niachwe na m ke wangu upate nafasi ya kunichukua?”
“Yaani nikutese wewe nikupendae kweli? hivi umeingiliwa na imani gani be b i?”
“Sio imani, hiki kinachoendelea katika mwili wangu ni ushirikina wa wazi. We kama umeniendea kwa mganga naomba acha mambo h ayo, mi nishakuambia kuwa nakupenda na sitomuacha m ke wangu, nipo tayari nikuoe ila sitoitelekeza familia yangu. H ayo masuala ya kurogana mi siyataki hata kidogo, utafanya nisikupende wakati nakupenda” Niliongea kwa sauti kali ya msisitizo
“Jamani bebi mi sijaenda kwa mganga wa kienyeji wala wa kizungu. Nishakuambia kuwa naipenda familia yako, hata ukiamua mimi na mkeo tuishi nyumba moja mi nipo tayari na nitakuwa mstaarabu kwake”
Docra aliongea akijaribu kunipooza kwa kunishika sehemu mbalimbali; nilihisi ananifanyia danganya toto tu, kwa hasira nilisimama nilitoka kitandani, nilivaa nguo zangu nikitaka kuondoka, alinizuia akiniambia hana kosa lolote lakini sikumsikiliza, niliondoka nilirudi nyumbani. Docra alinitumia meseji kuwa ameumia sana na ameamua kurudi Dar. Sikujali wala nini, siku ya kwanza ilipita sikuumwa, siku ya pili ilikatika sikuumwa, wiki moja ilipotea nilipiga kazi zangu bila shida, pia hata mke wangu alivyoniomba mchezo niliucheza bila shida yoyote, hapo sasa niliamini kuwa ni kweli Docra alihusika kutaka kuniharibia familia yangu. Pia nilihisi ameacha kuniroga kwa sababu nilimfokea. Japo nilimpenda sana lakini nilijikuta namchukia kwa kitendo chake hicho.
Siku zilizidi kusonga pasipo kuwasiliana na Docra, tulinuniana, alikasirika kwa sababu nilimwambia mchawi, pia nami nilichukia kwakuwa sikupenda upuuzi wake. Sasa nikiwa naamini matatizo yameisha siku hiyo nikiwa kazini mke wangu alinipigia aliniambia kuwa ameniandalia chakula kizuri, alinitaka nirudi nyumbani nikale kisha nitaendelea na kazi. Kwakuwa namjali sana wala sikukataa, nilizama kwenye gari yangu kisha nilimfuata nyumbani. Sasa nikiwa barabarani sijui nilijisahau nini, ile nacheki mbele nilishtuka kuona mbuzi kasimama, nilinyonga usukani nikimkwepa; nikiwa nadhani nimeepuka ajali hiyo mara nilishangaa mbele ya gari yangu kuna mtu kasimama! Na ukicheki nilikuwa kasi sana, nilipiga kona ya haraka nikitaka kumwepa mtu huyo; Mungu mkubwa nilifanikiwa ila sasa gari yangu ilinyosha moja kwa moja hadi kwenye nyumba ya mama moja hivi ambaye tulizoea kumuita chaumbea wa mtaa, akianzaga kuongea hamalizi, akianzaga kuchamba hamalizagi, nilishuka haraka haraka nikitaka kwenda kuona kama nimebomoa nyumba ya watu, nilikuta sehemu ya ukuta ikiwa imemeguka! Kabla sijakaa sawa chaumbea alitoka nje akiwa amevimba kwa hasıra kali, moyoni nilijisemehe “Nimeingia cha kike, cha! Cha kike ewaaa!”
“Hiyo nyumba utanijengea mpya, siwezi ishi kwenye nyumba yenye majeraha” Hilo ndilo lilikuwa neno la kwanza kutoka kwenye mdomo wa mama chaumbea.
“Mama angu nisamehe, ni bahati m baya tu imetokea”
“Hiyo bahati mbaya ipo kwenye nyumba yangu tu? nyumba zingine huzioni? Hivi nyie wenye magari mnatuonaje sisi makapuku? Pesa kidogo tu unagonga nyumba yangu kwa bahati mbaya, je ungekuwa mtoto wa biligeti si ungetamani unioe mke wa pili…Nasema nafumba kwa sekunde 1, nikifumbua nisikute jeraha kwenye nyumba yangu…Hii nyumba nilivyoipata unajua? Unajua nimedanga mara ngapi? Unajua nimeharibu ndoa za wanaume wangapi? Eti leo kiulaini tu unanibomolea alafu unasema ni bahati mbaya, jamani majiraniiiiiiiiiiii….utailipa hii nyumba leo”
SEHEMU YA 40
llikuwa ni mshike mshike, watu walimiminika kama wote, yule mama alikuwa akiongea akiwa ananisasambua, mara animwagie ladhi, mara ajitingishe, m baya zaidi walikuja wambea wanzie ambao walishadadia mambo wakisema “Mkomeshe huyoooo, anajikutaga njomba nchumari sana huyooo”. Mke wangu naye alikuja lakini alikaa kimya kwa sababu yeye sio muongeaji sana, aliniuliza kuna nini? Nilimueleza ilivyokuwa, alijaribu kumuomba msamaha yule mama lakini hakukubali. Ilibidi mwenyekiti wa mtaa aje asuluhishe ugomvi, katika suluhu niliambiwa nitoe laki tatu za kutengeneza ukuta. Ukuta wenyewe hata haukubomoka sana ila bası tu nilikutana na mama mwenye domo lake ambaye alinikomalia kisawasawa, mke wangu ndiye alilipa zile pesa kisha tuliondoka.
“Mume wangu mi nahisi kuna tatizo” Mke wangu aliniambia mara baada ya kufika nyumbani
“We unadhani tatizo ni nini?”
“Nahisi kama kuna mtu anakuchezea vile, hapa tusipoenda kwa mganga utajikuta unapoteza kila kitu, kila siku itakuwa mihangaiko tu”
“N i kweli m ke wangu, hata mimi nilihisi kama wewe, tena nahisi kuna mtu mmoja hivi ndiye anatuchezea huu mchezo”
“Nani huyo?”
“Sina uhakika ila nahisi ni Docra”
“Kumbe fikra zetu ni sawa, hata mimi nilianza kumuhisi yule binti, haiwezekani akiwa hapa nyumbani unapona lakini akiondoka unaumwa….Hivi rafiki yako Ostadhi Kasulu si yupo? Ebu twende” Tuliondoka tulielekea kwa jamaa yangu mmoja hivi ambaye ni Ostadhi. Huwa anasuluhisha matatizo mengi ya watu hasa haya ya uchawi, kwakuwa ni jamaa yangu niliamini atanipa majibu ya uhakika kama Docra ndiye ananitesa au kama kuna mtu mwingine. Moyoni niliwaza endapo nikikuta Docra ndiye ananichezea ningemuacha siku hiyo hiyo hata kama ana ujauzito wangu. Japo roho iliniuma kumuacha ila kama ni mchawi niliona hatonifaa.
Tulifika kwa Ostadhi Kasulu, kwanza tulicheka kwa furaha tukikumbushana mambo mengi kisha nilimueleza matatizo yangu. Tuliingia kilingeni kwake ambako vilijaa vitabu vya dini. Aliniuliza umri wangu na jina kamili kisha aliwasha ubani alafu alianza kuongea na jini lake, baada ya muda yule jini alitaka kuongea na mimi; aliniambia nimuulize swali lolote ambalo linanisumbua, nilimuuliza kwanini napata ajali na homa za mara kwa mara? Pia kama kuna mtu ananisumbua ni nani? na kwanini ananisumbua?. Jibu pekee ambalo nilipewa ni kwamba hakuna mtu aliyekuwa akinisumbua, niliambiwa kuwa matatizo hayo yote nimeyataka mwenyewe kwa kuvunja kiapo, na hili nisipate matatizo zaidi ilibidi niweke wazi kwa mtu husika pia nitubu. Nilishtuka kusikia habari za kiapo, hata mke wangu alishtuka ila alitulia kimya kwa sababu hakujua ni kiapo gani. Sikuuliza swali lingine nikiogopa kutindinganya mambo, Ostadhi alimaliza kuniagua. Japo hakutaka pesa ila nilimpa kiasi flani kisha mimi na mke wangu tuliondoka, yaani ile tumefika nyumbani tu vuruÄŸu zilianza.
“Kumbe ndio maana kila siku majanga, tulimuhisi vibaya binti wa watu kumbe tatizo ni wewe mwenyewe. Haya niambie ni kiapo gani hicho ambacho umevunja? Au umenisaliti?…Niambie kama umenisaliti” Mke wangu alifoka kwa nguvu lakini nilitulia, niliwaza nimuambie ukweli au nikaushe? Niliogopa kusema ukweli kwa sababu akili ya mke wangu naijua, hakawiagi kuzimia.
“Mke wangu sijakusaliti” Nilijibu kwa sauti ya upole
“Sasa kwanini ostadhi aseme umevunja kiapo, ni kiapo gani?” “Nikiwa marekani nililazwa hospitali kwa wiki moja, madaktari wengi walinitibu lakini sikupona. Alikuja dokta flani hivi ambaye aliniambia kuwa ana uwezo wa kunitibu hadi nipone. Tulikula kiapo kwamba akinitibu nikipona nitamlipa pesa million 10. Yule dokta alinipambania hadi nilipona, lakini mke wangu wewe unajua kwamba million 10 ni pesa nyingi; baada ya kupona nilikimbia hospitali, sikumlipa yule daktari. Siku moja alinitumia meseji aliniambia kuwa nitamkumbuka kwa kuvunja kiapo, nahisi yeye ndiye chanzo oha haya yote” Mwanaume nilitunga uongo pale pale
“Una uhakika na hayo maneno yako?”
“Ndiyo, nilivunja kiapo cha kumlipa yule mtu”
“Dah! Mi nilijua ni kiapo chetu cha usaliti, yaani laiti kama ungeniambia umenisaliti muda huu ungeenda kunizika…”
“Ah ah ah! Mke wangu nawe kwa hasira tu hujambo” Nilijichekesha kama mazuri kumbe hata sio jambo zuri
“Ndo nakuambia hivyo, mimi nimekutana na vishawishi vingi sana; nimetongozwa na kila aina ya mwanaume, marafiki zako na wengine husiowajua. Wenye pesa na wasio na pesa lakini sikuthubutu kuwakubalia, hata zawadi zao nilikataa kwa sababu sikutaka na sitaki na sitotaka kukusaliti milele…Hivyo basi sitaki unisaliti baba Monica, nakwambia siku nikisikia umenisaliti humu ndani zitatapakaa damu kila sehemu” “Siwezi mke wangu…mi siwezi kukusaliti”
“Sawa. Sasa na wewe kwanini hukumlipa huyo dokta? Kwanini una roho ngumu kiasi hicho mume wangu? Mtu anakutibu homa isiyotibika alafu humlipi kweli jamani? na ndio maana laana inakuandama, majanga yanakusumbua, Mungu hapendi mambo hayo. Mtu unafanya biashara za mamilion, unapata zaidi ya million 100 unashindwaje kumlipa mtu million 10? Ebu mlipe muda huu, namba yake si unayo?. Tena nakuongezea million 5 umlipe huyo daktari leo hii, sawa baba Monica?”
“Sawa mke wangu”
Mke wangu aliamini uongo wangu, aliniongezea pesa million 5 ili nimlipe dokta wa uongo ambaye nilidaganya kuwa ananidai kumbe hanidai. Baada ya kupokea pesa hizo nilijidai kwenda benki kisha nilifanya malipo ya uongo uongo nilirudi na risiti ya benki ambayo ilionyesha kuwa nimefanya muhamala wa million 10; mke wangu aliamini kuwa ni kweli nimelipa deni, kumbe mwenzie zile pesa nilijitumia kwenye akaunti yangu nyingine ya benki. Nilifanya yote hayo ili kutunza siri yangu ya usaliti.
Baada ya kutuliza msala huo nilirudi kazini, kazi ziliendelea na sikupata matatizo yoyote. Ilikatika wiki moja sikujikwaa, sikuanguka wala sikugonga nyumba za watu kwa garı. Sikuumwa kichwa, tumbo wala miguu; hali hiyo ilifanya mke wangu aamini uongo wangu, mke wangu aliamini kuwa matatizo yangu yalitokana na kiapo nilichokula na daktari ambaye sikumlipa. Alifurahi sana kuona naendelea vizuri, pia alijilaumu kumuhisi vibaya Docra.
****
Tangu nigombane na Docra kwa kumuhisi kuwa ni mchawi hakunisumbua tena kwenye simu, sio kwamba hakunipenda; hapana, alinipenda sana ila alikaa kimya akituliza maumivu yake ya kuitwa mchawi. Hata mimi niliumia sana kugombana na Docra, maumivu yangu yalizidi kila baada ya kukumbuka kuwa nilimtuhumu kaniroga kumbe nilijiroga mwenyewe. Kiukweli nampenda sana Docra, sitaki kumpoteza. Na kwakuwa mimi ndiye nilimkosea niliamua kumpigia simu, simu iliita weee lakini haikupokelewa, kuna muda namba ya Docra haikupatikana; nilijua kanizimia simu makusudi. Hata hivyo sikuvunjika moyo, nilisubiri hadi namba ilipatikana; nilimpigia tena lakini alikata simu yangu. Niliamua kumtumia meseji;
“Docra pliiz bebi pokea simu yangu, mwenzio huku sina amani kabisa, nakosa raha kwaajili yako mpenzi; pokea basi kuna kitu nataka tuongee” Nilimtumia ujumbe huo ambao licha ya kusomwa lakini dakika zilipita sikujibiwa. Nilimeza mate ya uchungu na mateso, nilimuomba Mungu ujumbe wangu ujibiwe, ni kweli Mungu alijibu maombi yangu; meseji ya Docra iliingia kwenye simu yangu, nilifungua ili nisome.
“Nani bebi wako? Nani mpenzi wako? Ina maana umeanza kupenda wachawi? Kijana mzuri fanya yaliyo mema, usisumbuke na mimi usije ukajiingiza kwenye ushirikina; Nikutakie maisha mema” Huo ndio ulikuwa ujumbe niliotumiwa na Docra, jamani nisiwe mnafki; mimi mwenzenu nilivurugwa, nilipagawa, nilipata tabu sana, kwa ufupi ni kwamba nilikiona cha mtemakuni.
INAENDELEA