KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 26
Licha ya Docra kunisubiri kitandani lakini mi sikwenda; nilimuogopa Israeli. Mara simu yangu iliita nilipigiwa na mke wangu, nilitamani kukata simu ila niliiacha, simu iliita hadi ilikata. Alinitumia meseji aliniambia nipokee haraka kuna kitu anataka kuniuliza. Alinipigia nilipokea, nilijifanya kama nimetoka kulala vile kumbe sikuwa na lolote, aliniuliza kama nimefika Dar nilimwambia ndiyo, ila mke wangu naye ana mambo ya kitoto kweli; eti kwanza alinipiga mabusu ya kwenye simu kisha aliniambia na mimi nimpige busu la kumtakia usiku mwema. Nilishindwa kufanya hivyo mbele ya Docra, nilisimama nikitaka kutoka kitandani ili nikaongelee nje lakini kwa nyuma nilishtuka nimeshikwa shati, Docra hakuniruhusu niondoke, alitaka niongelee pale pale. Licha ya mke wangu kulazimisha busu lakini sikumpa, nilimtakia usiku mwema kisha nilikata simu nilizima kabisa.
“Ni nani huyo?” Docra aliniuliza
“Ni mke wangu” Niliamua kumchana makavu, kwanza alishtuka alikaa kitandani akinitazama kwa macho makali.
“Umesema ni nani?”
“Sikiliza Docra nikuambie, naomba nisikilize kwa makini, tangu nizaliwe sijawahi kumpenda mwanamke kama navyokupenda we we. Tena nakupenda zaidi ya unavyofikiria, natamani ungekuwa mke wangu, na ndio maana nimefunga safari nimekuja huku kwaajili yako, nilianza kukupenda tangu ile siku tumekutana kwenye ndege, Docra nakupenda sana, tena sana. Kubwa zaidi ni muda mrefu niligundua kuwa unanipenda, nilifurahi sana kumpenda mtu ambaye anaonyesha kunipenda, hata hivyo sikutaka kukuambia ukweli wa moyo wangu, nilibaki nateseka na moyo wangu kwa sababu mimi nina mke wa ndoa na mtoto mmoja. Sikutaka kukuambia kwa sababu nilijua utaumia, sipendi nikuumize Docra, niliamua kukaa kimya. Leo hii nimeamua kukuambia ukweli ili ujue ukweli kuhusu mimi, licha ya kwamba nakupenda kuliko ninavyompenda mke wangu lakini nashindwa kumsaliti, licha ya kwamba una bikra lakini naogopa kukutumia, nina sababu kuu 2 ambazo zinafanya niogope; Kwanza naogopa kukuingiza kwenye mapenzi alafu uteseke kwa maumivu ambayo utayapata ukiniona nipo na mke wangu. Pili mimi mwenzio nimekula kiapo cha damu na mke wangu, tulikubaliana yeyote kati yetu akisaliti basi atakufa hapo hapo! Kila nikijaribu kutaka kusaliti nafsi yangu inagoma, moyo wangu unakwama, na ndio maana unaona nimeshindwa kukutumia, nisamehe Docra! huo ndio ukweli wa maisha yangu”
Hadi namaliza kueleza ukweli wangu Docra alikuwa analia kwa kwikwi na sauti, ghafla alisimama kisha alianza kuvaa nguo zake, nilijaribu kumtuliza alinilamba bonge la kofi, alinisisitiza nisimguse wala nisimsemeshe, alinitakia maisha mema kisha aliondoka alisepa zake, hicho ndicho kilichotokea usiku huo, japo niliumia ila sikuwa na namna, nilivuta shuka nililala.
*****
Kulikucha siku iliyofuata, mida ya saa mbili asubuhi nilikuwa nishafika bandarini, magari nayo yaliwasili, tulishusha mzigo kisha tulifanya utaratibu wa kusafirisha. Baada ya kila kitu kukamilika niliongea na Joshua kuwa mzigo wa kutosha nishautuma hivyo bası ajiandae kuuupokea. Alifurahi sana, pia aliniambia kuwa tayari watu waliweka oda ya mchele huo ambao ulisafirishwa hivyo basi nilitakiwa kuandaa mzigo mwingine. Baada ya maelezo hayo niliwaambia madereva wangu watangulie wakaanza kuandaa mzigo mwingine, nilifurahi sana kuona mambo yangu ya biashara yananyooka, pia muda mwingi nilimshukuru Joshua kwa kuifanya biashara yangu iuzike kimataifa.
Baada ya kukamilisha suala hilo hatua iliyofuata ni kurudi nyumbani Mbeya, sikutaka kurudi pasipo kuonana na Docra, kwanza nilimpigia simu lakini haikupatikana, nilijua kumekucha na makucha yake. Nikiwa sina hili wala lile mara niliona watu wengi wakiwa wamejaa kwenye meza ya magazeti, walionekana kushangaa habari flani ya kusikitisha, wengine niliwasikia wakisema kafa wengine hajakufa, nilishindwa kuelewa. Haraka haraka nilikimbia hadi kwenye meza hiyo, nilikutana na habari m baya ya kusisimua ambayo iliandikwa hivi “MREMBO DOCRA MWANACHUO WA CHUO CHA AFYA JANA USIKU ALIWAHISHWA HOSPITALI YA MUHIMBILI AKIWA MAHUTUTI, HALI YAKE HAITABIRIKI; ROBO UZIMA, ROBO TATU KIFO. HALI HIYO IMETOKEA MARA BAADA YA KUNYWA SUMU AKIJARIBU KUJIUA, CHANZO Nl MAPENZI”
SEHEMU YA 27
“Toba walahiii!” Nilijikuta napagawa, nilitazama saa ilikuwa ni mida ya saa 9 mchana. Haraka haraka nilikimbia hadi kwenye garı yangu, niliondoka nilielekea muhimbili. Huko nilikuta watu kama wote, wanachuo walijazana wakitaka kujua hali ya mwenzao. Walibeba maua, chakula, juisi na matunda, kuna baadhi walitoa machozi wakimlilia Docra, kuna dada mmoja muda wote alikuwa akisali kwa machozi; tena alisali kwa sauti akimuombea uzima Docra.
Nikiwa bado nimezubaa mara nilishtuka kumuona Baba na mama yake Docra wakiwa pamoja na daktari. Nilijiuliza baba yake Docra alikuja muda gani? alikuja kwa usafiri gani? alifikajefikaje? majibu niliyapata mara baada ya kuwaona wanajeshi wakiwa wamevalia sare za kimarekani. Nilitulia nikisikiliza mazungumzo kati ya d aktarı na wazazi wa Docra.
“Licha ya kupoteza fahamu lakini pia alipata mshtuko, na kabla hajakunywa sumu alijaribu kujikata mshipa wa damu katika mkono wake; hali hiyo imefanya damu nyingi zivuje, amepungukiwa na damu, hiyo imepelekea viungo vyake vingi kuacha kufanya kazi. Na ndiyo maana umeona tumemuwekea mipira ya upumuaji” Daktari aliongea kwa sauti ambayo ilisikika vema.
“Sawa dokta, na ndio maana tunakusikiliza wewe, sisi tupo tayari kwa chochote”
“Kwanza itabidi aongezwe damu, mtoto wenu ni group “0” kati yenu kuna mwenye group “0”?
“Mh! mi hata sijui, sijawahi kupima damu, labda mama yake”
“Hata mimi sijawahi kupima kujua nipo kundi lipi”
“Basi itabidi mpime kisha aongezewe damu. Kuhusu mfumo wake wa upumuaji nadhani atakaa sawa, pia fahamu zake zitarudi mara baada ya viungo vingine kukaa sawa”
Baada ya maelezo hay o zoezi ambalo lilifuata ni upimaji wa damu.
Baba na mama yake Docra walielekea maabara kisha damu zilitolewa na vipimo vilifanyika. Kitu ambacho kilishangaza watu ni kwa licha ya Docra kuwa na damu kundi “O” lakini wazazi wake walikosa damu ya kundi hilo, hata dokta mwenyewe alishangaa ila alipotezea kwa sababu kitu hicho kinawezekana. Ilibidi wanachuo ambao ndio marafiki wa Docra wajitoe kumchangia damu mwenzao. Kwa jinsi ambavyo alipendwa wanachuo wote walijitolea kumchangia, ila sasa baada ya vipimo tatizo lilikuwa lile lile, hakuna mwanachuo aliyekutwa na group “O”. Wazazi walichanganyikiwa, mbaya zaidi damu ilihitahika kwa haraka, maamuzi yaliyofuata ni kununua damu, ubaya ni kwamba damu ambazo ziliuzwa hazikuwa na uwezo wa kutumika kwa Docra, hatimaye mishe ilifeli.
“Dokta kwahiyo inakuwaje sasa? Au tutangaze kwenye radio kuwa tunanunua damu? Mimi nipo tayari kununua damu kwa gharama yoyote” Baba yake Docra aliongea akiwa analengwa na machozi “Laiti kama india pangekuwa ni karibu natamani angepelekwa huko muda huu, lakini tumechelewa, inabidi tupigane haraka sisi wenyewe. Pia kuhusu wazo lako la kununua damu wala sibishani nalo, ni vema ukafanya hivyo ila tumechelewa sana, damu kwaajiri ya Docra inahitajika muda huu”
Mama yake Docra alikaa chini kisha alianza kulia, baba yake alivurugwa, hadi muda huo mimi hawakuniona, niliogopa kujionyesha m bele ya mshua! Lakini kutokana na hali ya Docra niliona nijipitishe tu, japo sikujua kundi langu la damu ila nilijitokeza mbele yao kisha niliwaambia kuwa nipo tayari kutoa damu kwaajili ya Docra. Baba yake Docra alinitazama kwa macho makali hadi niligwaya, kwanza alizamisha mkono mfukoni alafu alitoa kibarua flani hivi alikisoma kisha alinitazama mimi;
“Wewe ndiye Derick? ” Aliniuliza akiwa amenikazia macho
“Ndiyo” Nilijibu kwa woga
“Kumbe Ni wewe! Nilikuwa nakutafuta sana, alafu wewe nilikupa onyo kuhusu mwanangu lakini hukutaka kusikia. Wewe ndiye sababu ya mwanangu kutaka kujiua, sasa kwa taarifa yako Docra akipoteza maisha nawe uwe umepotea hapa duniani, la sivyo nakunyonga!” Mzee alinifokea waziwazi mbele ya dokta
“Muheshimiwa hapa sio mahala sahihi pa kupeana adhabu, huu ni muda wa kupambania hali ya mtoto wako”
“Dokta huyu kijana anataka kuniharibia binti yangu, alimfuata marekani na sasa amemfuata huku Dar, anacheza na uhai wa mtoto wangu, leo wacha nimuambie kuwa nina mtoto mmoja tu ambaye ni Docra, naongea mbele yenu mkiwa mnanisikia; Mwanangu akifa na huyu kijana namuua, sitanii”
Kwa mbali nilihisi tumbo la kuhara likinisumbua, mtetezi wangu mkubwa alikuwa ni Daktari, yeye ndiye aliniondoa wasiwasi kuwa niwe na amani, isingekuwa yule dokta nadhani ningelambwa risasi pale pale. Dokta aliniuliza kama kweli nipo tayari kumtolea Docra damu nilijibu ndiyo, alinichukua tulielekea maabara, damu yangu ilitolewa kisha vipimo vilifanyika; Baada ya muda dokta alinifuata akitaka kunipa majibu ya vipimo vyangu! Alitaka kuniambia kama group la damu yangu linafanana na Docra au inakuaje? Hapo ndo penyewe sasa.
SEHEMU YA 28
“Dota majibu yanasemaje? Vipi damu zetu zinafanana?”
“Ndiyo, wewe pia una damu group “0” kama Docra”
Weuwee! Unajua kurukaruka? Nilipagawa kwa raha kiasi cha kutaka kujigaragaza chini. Dokta nae alifurahi sana, haraka haraka alinitoa damu nyingine kwaajili ya kumuongezea Docra kisha alielekea ndani ya chumba cha mgonjwa kufanya mapekeche, baada ya dakika kadhaa mwili wa Docra ulipokea drip za damu yangu, kuna muda baba yake Docra alizama chumbani kwa mgonjwa alikuta mwanae akipata damu bomba!
“Dokta hii damu imetoka wapi?” aliuliza akishangaa
“Yule Kijana Derick ndiye kajitolea, damu zao zinaendana”
Baada ya jibu hilo mzee alikaa kimya, alikosa maneno. Matibabu mengine yaliendelea, baada ya hapo hatukusikia tena malalamiko mengine kuhusu mgonjwa kuzidiwa, Dokta alituambia kuwa hali ya Docra imeanza kubadilika, hata ile mirija ya upumuaji iliondolewa kwa sababu mfumo wa upumuaji ulikaa sawa. Taarifa hiyo ilifanya mama yake Docra aache kulia, baba yake alitabasam kwa furaha, mimi japo nilifurahi ila nilikausha nikiogopa kipigo. Kitu pekee ambacho kilibaki ni mgonjwa kuamka kutoka katika usingizi mzito. Utata mwingine ulikuwa muda wa kwenda kumuona mgonjwa, watu wengine wote waliruhusiwa kuingia lakini mimi nilikatazwa, baba yake Docra hakuniruhusu niingie. Giza liliingia, wanachuo walirudi kwao lakini mimi sikurudi. Pale hospital! nilibaki mimi na wazazi wa Docra, kuna muda mzee aliniona nimekaa kinyonge; alinifuata kisha aliniambia niondoke nisije nikampa gundu mwanae, hata hivyo sikuondoka, nilizuga kama naondoka vile ila nililala pale pale hospitali.
Siku ya kwanza ilipita sikupata nafasi ya kumuona mgonjwa, mke wangu aliniuliza kwanini sijarudi nyumbani nilimuambia kuwa bado nashughulikia mzigo. Siku ya pili ilipita Docra hakuamka, pia sikuruhusiwa kumuona mgonjwa. Kitu ambacho kilituogopesha ni mgonjwa kutokula, chakula pekee ambacho alikipata ni drip za maji ambayo alifungwa mkononi. Hiyo ilitokana na Docra kutofungua mdomo pamoja na kutokuwa na uwezo wa kumeza, hata walivyolazimisha kumnywesha uji hakumeza bali aliuweka mdomoni tu. Daktari alituambia kuwa kama mgonjwa hasipoamka kwa siku tatu basi itabidi apelekwe nje za nchi.
Hatim aye ilifika siku ya tatu asubuhi, sio mimi wala wazazi wa Docra ambao walipata usingizi; tulikesha siku mbili mfululizo. Sasa siku hiyo ambayo ni ya tatu ilikuwa ni siku ambayo Dokta alishauri Mgonjwa apelekwe India haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Baba yake Docra hata hakuwa mbishi, yeye kila alichoambiwa alikubali kufanya kwaajili ya kutetea uhai wa mtoto wake. Kumbuka kwamba hadi siku hiyo sikubahatika kumuona Docra wala sikuruhusiwa kuingia chumbani kwake. Haraka haraka walianza utaratibu wa kumpeleka India, kwakuwa baba yake Docra alifika na usafiri wa ndege ya jeshi ilibidi ndege hiyo imchukue mgonjwa impeleke india. Wakiwa katika harakati za kumsafirisha mgonjwa, kuna sauti ya hisia iliniambia mimi ndiye tiba pekee ya Docra, kuna sauti toka juu iliniambia Docra alipona kwa damu yangu hivyo basi anahitaji kuniona mimi tu ili atoke katika giza zito. Niliondoa woga nilipiga hatua nikitaka kuingia chumbani kwa Docra. “We kijana unaenda wapi? we nilikuambiaje? Hivi unanichukuliaje mimi?” Baba yake Docra alinisimamisha, muda huo alikuwa ameongozana na wanajeshi wawili pamoja na mkewe na daktari. “Samahani mzee, nataka nimuone Docra”
“Alafu ukishamuona?”
“Nikimuona atapona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Docra ni mzima, Mungu atabariki atapona kabla ya kwenda india”
“We kijana nitakulamba shaba wewe…Hivi we unauchukuliaje ugonjwa wa Docra? au umetumwa umuangamize?” Hapo sasa mzee aliongea akinifuata kisha alinikaba roba ya shingo, alichomoa bastola kisha alinilengeshea kichwani akitaka kunitwanga. Watu wote hospitali waliacha mambo yao kisha walitazama tukio langu la kutaka kupigwa risasi.
Kitu kingine ambacho kilinishangaza ni kuona namna ambavyo wale wanajeshi wengine wawili walitulia kimya pasipo kunitetea au kumtuliza mwenzao, ilionekana kuwa baba yake Docra ni mtu mkubwa wa kuheshimika, hata mke wake na daktari waliogopa kufanya chochote, kila mtu alikaa kimya akisubiri kuona kifo changu. Hata hivyo Dokta alinitazama kwa uchungu alinionea huruma, pia Dokta alihisi nimebeba upako wa ufufuo na uzima, japo hakuniamini kwa asilimia zote lakini katika hii dunia miujiza ipo, kuna watu wapo mahospitalini hawasikii dawa lakini huwa wanapona mara baada ya kuguswa na vitu vyenye upako toka kwa mwenyezi Mungu.
“Muheshimiwa kwa heshma yako naomba utulize jazba, pia itakuwa vyema kama ukimruhusu kijana aingie ndani akamuone mgonjwa” Dokta alimwambia baba yake Docra
“Aingie wapi? yani hata wewe Dokta upo pamoja na huyu mpuuzi? Huyu ndiye chanzo cha haya mateso yote! Sitamani hata kumuona..na wewe kijana usifikiri kumtolea damu Docra ndo kwamba nimekusamehe, sijakusamehe hata kidogo” “Kadri tunavyochelewa ndivyo hali ya mgonjwa inazidi kuwa m baya, mruhusu akamuone labda uzima wa binti yako upo kwa kijana huyu”
“Sawa ingia, tena tunaingia wote ili kama unataka kumuua umuue m bele yetu. Na ole wako Docra hasipone, wewe ndiye utampeleka india”
SEHEMU YA 29
Kauli hiyo iliniogopesha ila nilijikaza tu, niliwaza vipi kama nikiingia alafu Docra haponi? hizo gharama za kumpeleka india nitazitolea wapi mimi? Mbona balaa!. Baada ya mawazo ya sekunde chache nilipiga hatua kuelekea ndani, baba yake Docra na wengineo nao walizama ndani wakitaka kuona upako wangu. Nilimtazama Docra ambaye alilala kitandani nilijikuta natoa machozi, kila sehemu alipitishiwa mirija ya kila aina, watu wengine wote walinionea huruma jinsi ambavyo nilitoa machozi lakini baba yake Docra alitamani anishike anitafune nyama.
Mwanaume nilikaa pembeni ya mgonjwa, kabla sijamshika nilipiga maombi ya laivu bila chenga, nilitoa sauti kubwa kama muhubiri vile; “Eeeh Mungu wangu wa mbinguni ni wewe pekee ndiye unajua sababu ya huu ugonjwa, ni wewe pekee ndiye unajua kumtibu mgonjwa, naomba leo mtazame binti yako huyu, muondoe katika wingu zito, mtoe katika mateso mazito, kama uliweza kuzuia kifo chake katika ajali ya ndege basi hutoshindwa kitu, kama alitaka kujiua na ulizuia kifo chake basi hutoshindwa kumpa uzima wa milele, ameteseka sana na sasa anahitaji huruma yako. Naomba mkono wangu leo ugeuzwe uwe mkono wako, sina uwezo wa kugawa uzima ila ni kwa uwezo wako, nimshike apone daima afurahie uhai wa dunia yako, amen”.
Kama huna imani maombi yangu ungeweza kuyaona kichekesho, wakati naomba nilikuwa nimefumba macho; sasa ile nafumbua nilikuta watu wote pamoja na dokta wakiwa wamefumba macho, kasoro baba yake Docra tu ambaye alinitazama kwa macho makali.
“Usinitazame mimi, nataka huyo apone. We nipigie makelele alafu nisione lolote, watakuzika mzima mzima” Mzee alinionya mbele ya watazamaji ambao walifumbua macho.
Niliondoa macho usoni kwa baba yake Docra kisha niliyapeleka usoni kwa Docra, watu walisubiri uponyaji tu. Nilinyosha mkono wa ufufuo na uzima nilikamata paji la uso la Docra nikidhani ataamka lakini hakuamka, hata kukohoa tu hakukohoa. Jamani haya mambo ya kujifanya mchungaji sio mazuri, eti mimi nae nilitaka kufufua mtu; we ulisikia wapi? we uliona wapi? tumbo langu la kuhara lilianza tena, niligeuza macho nilimtazama baba yake Docra nilimuona akichomoa bastola, nilijua nimekwisha!. Kwa mara nyingine nilimtazama Docra kisha kwa sauti ya chini nilimuambia “Docra amka kwa uwezo wa Mungu”, ilikuwa ni kazi bure, niliongea nikiwa na imani kubwa ila ndo hivyo mgonjwa hakuamka. Mara nilisikia “Kweche kweche” Baba yake Docra alikoki bastola! Watu wote walimtazama mzee gaidi kisha walinitazama mimi walinionea huruma.
Nilijiandaa kwa lolote, kama kuniua aniue. Hata hivyo sikuvunjika moyo wala sikukata tamaa, kuna kisauti cha upako kiliniambia “Usiogope jipe imani, msogelee mgonjwa kisha mpige busu mdomoni”. Nilijikuta naguna “Mmhh”, eti nimpige busu Docra mbele ya mzee gaidi jamani si kujitafutia kihama huko! Yaani mzee ashuhudie kabisa mdomo wangu ukitua juu ya mdomo wa mwanae? mbona patachimbika. Hata hivyo muda huo nilikuwa naendeshwa na hisia zenye imani ya ufufuo na uzima, niikuwa naheshimu mawazo yangu hivyo basi sikuwa na budi kuubusu mdomo wa Docra. Kwanza nilitazama macho ya watu ambao walinitazama niliwaona wakinichora tu. Taratibu niliusogelea uso wa Docra kisha nilishuka taratibu nikitaka kumpiga busu!
“We fala unataka kufanyaje? Wewe hunisikii au?” Baba yake Docra alinishtua kwa sauti kali hadi niliacha kumalizia busu langu
“Muache kijana afanye kazi yake, mbona unamkwamisha? Kumbuka tupo hapa kwaajiri yake, yeye kasema amebeba uzima wa mwenzie, ngoja tusubiri, kama ni kumuadhibu utamuadhibu baada ya kushindwa kufanya anachokifanya” Dokta aliongea kwa sauti yenye msisitizo.
Baba yake Docra alitulia ila alikuwa ana hasira sana, alafu aliumia sana kuona nimeruhusiwa nimpige busu mwanae, aliona kama nafaidi vile. Kwa mara nyingine nilishusha mdomo wangu ulitua juu ya mdomo wa Docra, nyaya ziligusana, nilipiga busu la kawaida tu lakini sikuona mabadiliko yoyote, sikutaka kuuondoa mdomo wangu, nilitulia nikisubiri kwanza, sekunde na dakika zilikatika; busu lilidumu kwa dakika 3 lakini ilikuwa kazi bure. Kwa sauti ya chini niliongea nikisema “Docra amka basi, mimi ni Derick nipo kwaajili yako”. Baada ya maneno hayo kwa mara nyingine niligusanisha lips zangu na zake, safari hii sikumpiga busu bali nilipitisha ulimi wangu mdomoni kwake, sikutaka kujua hasira za baba yake Docra, mimi nilifanya kile nilichokiamini. Busu la kikubwa lilidumu kwa dakika moja lakini mtu hakuamka, watazamaji waliona ni upumbavu ambao nilikuwa naufanya, hata D aktarı aligeuka akitaka kuondoka, ghafla baba yake Docra alininyoshea bastola akitaka kumaliza kazı kama alivyoniahidi, mama yake Docra alianza kulia kwa sauti ya juu, nami niliona ni bora niondoke juu ya mdomo wa Docra, sasa nikiwa najivuta juu nikitaka kutoka mara nilihisi mkono wa Docra ukipita shingoni kwangu, mtoto alifumbua macho kisha alinivuta kuelekea chini, alinibana zaidi alafu taratibu aliuchezesha ulimi wake ndani ya mdomo wangu!
“Jamani mwanangu ameamkaaaaa” llikuwa ni sauti ya furaha yenye kilio chenye raha kutoka kwa mama yake Docra. Sauti hiyo ilifanya Dokta ageuze njia, alirudi haraka akitaka kuja kuona. Baba yake Docra alishusha bastola chini kisha alitabasam pasipo kutarajia, wale wanajeshi wengine nao walitamani wacheze singeli ili wafurahie ushindi. Maajabu hayakuishia hapo, Docra aliamka kabisa alikaa kitandani akiwa mchovu, mama yake alikimbia hadi nje kisha alirudi akiwa amebeba chakula kwenye sahani, alikaa pembeni ya mwanae akitaka kumlisha lakini Docra alikataa.
“Kula mwanangu una njaa, kula basi” Mama alimsisitiza mwanae ale lakini hakula. Kwanza Docra hakumtazama mtu yeyote zaidi yangu, mama Docra aligundua kuwa mwanae ananipenda hivyo bası alinikabidhi kile chakula nimlishe, nilikipokea kisha nilijaribu kumlisha; huwezi amini Docra alikula bila shida! Hapo sasa hata mzee gaidi alinipigia salute.
SEHEMU YA 30
Wakati namlisha chakula Docra; Dokta alichukua vipimo kisha alianza kumpima mgonjwa maeneo mbalimbali, baada ya vipimo alifurahi sana; aliwatazama wazazi wa Docra kisha aliwaambia kuwa haina haja ya kwenda india wala dubai, mgonjwa yupo kamiligado. Mzee gaidi nusura arukeruke kwa manjonjo ya furaha, hakuamini alichokisikia. Mama yake Docra alishindwa kuendelea kulia, alinitazama mimi hakunipatia majibu, tangu azaliwe hakuwahi kuona upendo kama huo.
Kuanzia hapo kila kitu kilienda fresh, siku iliyofuata alimaliza drips za dawa, maji na damu. Afya yake ilizidi kuimarika, wanachuo walijaa hospitali ili kumtaka hali, alipewa mazawadi kama yote. Licha ya uwepo wangu, licha ya kumuamsha kutoka katika usingizi mzito lakini hakuongea na mimi hata neno moja. Watu wengine wote aliongea nao, hata wazazi wake alichonga nao ila mimi hakutaka kujibu hata pole yangu. Pia kitu kingine ambacho kiliwashangaza watu ni kwamba Docra hakutaka kuniona, alinibadilikia ghafla hata mzee gaudi alishindwa kuelewa imekuaje. M baya zaidi kila akiniona alikuwa analia kisha alijifunika shuka, nikiondoka alitulia, nikiwepo alilia. Ilibidi mzee anichukue pembeni kisha aliniuliza kwanini Docra anabadilika badilika kama kinyonga?. Niliogopa kumsimulia, sikutaka mzee ajue ukweli.
“Sikiliza, mimi najua Docra anakupenda. Kabla hajanywa sumu alituandikia barua alitueleza kila kitu, na ndio maana mimi nakuchukia sana wewe kwa sababu sitaki mwanangu anyanyasike kwenye masuala ya mapenzi. Huyu mtoto nilianza kumchukulia hatua muda mrefu sana, sikutaka kumpeleka hosteli; nilijua akiwa kule atapata nafasi kubwa ya kufanya upumbavu. Vipindi vya chuoni kwao vyote navijua, na akienda chuoni lazima niongee na uongozi wa chuo ili kuhakikisha kama yupo darasani. Kuna muda nilimpa walinzi walimnde muda wote, h ayo yote niliyafanya kwa sababu sikutaka na sitaki aharibikiwe..Wewe ndiye unataka kumuharibu, kwenye barua amendika kuwa anakupenda ila humjali. Kitu pekee ambacho kinanifanya nikuonee huruma ni kuona anakupenda sana, laiti kama ingekuwa wewe ndiye unamsumbua kumtongoza ningekuwa nishaitoa roho yako kitambo sana. Sitaki uwe na binti yangu, nataka umuache asome. Hata hivyo nataka kujua ulimfanyia nini hadi ata ke kujiua?
Ulimchezea alafu unataka kumuacha au? Na kwanini muda huu hataki kukuona?”
“Kwanza mimi sijawahi kumchezea Docra, pia mahusiano yangu na Docra yalianza jana”
“Jana? Ina maana kule marekani mlikuwa marafiki tu?”
“Hadi sasa sisi ni marafiki”
“Sasa mbona unanichanganya?”
“Docra ananipenda, hata mimi nampenda. Mimi nishajaribu sana kumkwepa, nilimuacha asome, pia sikutaka kukukasirisha wewe lakini ilishindikana. Jana nilikuja huku kwaajili ya biashara zangu, Docra alinifuata kisha tulielezana hisia zetu. Licha ya hisia hizo nilimuambia kuwa hatutoweza kuwa wapenzi kwa sababu mimi nina mke na mtoto mmoja”
“Ninii? Wewe kumbe umeoa?”
“Ndiyo. Sikutaka kumchezea Docra ndio maana nilimuambia ukweli. Na hadi hivi ninavyokuambia mimi na Docra hatujawahi kushiriki mchezo wowote, sijamuharibu binti yako kwa namna yoyote, mimi mwenyewe natamani hasinipende ili nyie muwe na amani. Kubwa zaidi nampenda mke wangu na familia yangu, alafu mimi ni mkristu siruhusiwi kuoa wake wawili hivyo basi siwezi kumsaliti mke wangu. Docra baada ya kusikia kuwa nimeoa aliondoka akiwa analia, leo kwenye gazeti ndiyo nikakuta habari kuwa alitaka kujiua, na ndio maana nilikuja hapa kumuokoa kwa sababu nilijua mimi ni sababu. Sasa ebu niambie kosa langu lipo wapi?’
“Huna kosa, nisamehe. İla sasa kama ni hivyo naomba tufanye kitu kimoja, kwakuwa una m ke huna vigezo vya kuwa na binti yangu, asante umemsaidia amepona, najua ataumia ila atakusahau tu. Jambo la muhimu ni kwamba kwa sasa inabidi uwe mbali na Docra, hasikuone kabisa, achaneni moja kwa moja, sitaki muwe karibu hata kidogo, umenielewa?”
“Ndiyo nimekuelewa”
“Yeah! Tena nakupa nafasi ya mwisho nenda kamuage na umtakie maisha mema, sitarajii kama mtakutana tena, na ikitokea unamsumbua hapo sasa utanitakia mabaya. Ni hivyo tu”
Bila kupoteza muda nilimfuata Docra kisha nilimueleza yale ambayo niliambiwa na baba yake. Kwanza nilimuomba msamaha kwa yote, sikusita kumuambia kuwa nampenda sana. Hakunijibu kitu zaidi ya kunisikiliza tu, pia hata hakutoa machozi; tayari alikomaa kwa maumivu ambayo nilimpatia. Nilimueleza kuwa licha ya kumpenda lakini nitajitahidi kukaa mbali na yeye ili nisimpe maumivu zaidi. Baada ya kumueleza hivyo nilimpiga busu la mwishomwisho kisha nilisepa zangu, nilirudi Mbeya.
****
Ulipita mwezi mmoja sikuwasiliana na Docra, sikusikia habari zake, bila shaka hata yeye hakusikia habari zangu. Licha ya kukaushiana lakini haikupita siku bila kumkumbuka, nilijaribu kumsahau lakini nilishindwa. Siku moja nilimtumia meseji ili nimsalimie lakini meseji haikusomwa. Nilijaribu kumpigia lakini hakupatikana, mbaya zaidi hakupatikana wasap, twitter, insta wala facebook, alipotea kila sehemu, nilijua huo ni mpango wa wazazi wake kumtenganisha na mimi.
Hatim aye miezi miwili ilikwisha, sikupata tetesi zozote kuhusu Docra, taratibu nilianza kumsahau. Nguvu zangu nilizielekeza kwenye biashara zangu, mzigo ambao nilimtumia Joshua ulikwisha wote kisha alinitumia fed ha ambazo zilinipagawisha, ilifikia hatua sikutaka kabisa biashara ya ndani, mizigo yote niliipeleka nje. Kazi yangu ilikuwa ni kuagiza mzigo kisha Joshua alimaliza kila kitu, mimi nilitumiwa pesa tu. Niliamua kufungua kiwanda kabisa, nilikuwa nazalisha mchele na unga ambao niliweka kwenye mifuko kisha nilisambaza maeneo mbali mbali.
Miezi sita ilikatika nilimsahau kabisa Docra, bila shaka hata yeye alikuwa amenisahau. Nakumbuka ulikuwa ni mwisho wa mwezi, ni muda ambao Joshua alitakiwa anitumie pesa za mauzo ya mchele na unga ambao nilimpelekea. Sikuwa na wasiwasi nae niliamini atanitumia tu, mwezi huo ulikatika uliingia mwezi mwingine lakini Joshua hakunitumia pesa. Kila nikiwasiliana nae aliniambia mzigo bado haukuisha ulibakia kidogo, pia alinisisitiza nimtumie mzigo mwingine kabla wa mwanzo haujaisha, kwakuwa nilimuamini nilimtumia mzigo wa kutosha. Siku ziliendelea kukatika Joshua hakunitumia pesa, mbaya zaidi alianza kukata simu zangu, ghafla hakupatikana kabisa, nilikosa mawasiliano naye
INAENDELEA