NILIKULA NAULI YAKE MARA TATU KUMBE NI MJEDA
Episode 16
Sikutaka kubweteka kama bwana ndio kaanza kunielewa namna hii ni muda wa mie pia kuonesha manjonjo yangu ✋
Kwenye friji lake kulikuwa na nyama, kwenye kapu dogo lililokuwa jikoni lilijaa maungo mbalimbali.
Sijui ni sifa au ni nini nilijikuta nikiweka maungo mengi utadhani ni sifa hivi 😁 sikuwa hata nikisoma maelekezo nilichotaka Mimi ni nyama kunukia.
Navyo penda ubwabwa mie, niliukalia ipasavyo mpaka nilipo hakikisha umeiva.
“Chakula kimeiva karibu 🤗” Nilimtumia ujumbe
“Ahsante, kaoge pia na wewe baada ya kumaliza chakula nitaishambulia K yako 😋” Khalid alinitumia ujumbe ulionishtua moyo
Huenda huu ni wakati wangu wa kufurahia maisha, niliingia bafuni ni kaoga.
Sijui ni ukorofi au nini lakini sikuona sababu ya kuvaa nguo zangu. Nilitafuta tafuta kwenye kabati mpaka nikapata nguo zake za kunitosha nikajitupia 😀
Khalid alikuja muda sahihi, mie huyu nikiwa nimejiamini kupita kiasi nilipakua ubwabwa kisha nikajaza minofu kwenye bakuli 😓
“Nikajua umepika samaki 🙄 hapana nikajua ni maharage, kwani umeweka nini na nini humu ” Khalid aliuliza huku akigeuza geuza minofu kwa kutumia kijiko
“Nimechanganya viungo vyote vilivyo kuwa kwenye kikapu 😁” Nilijisemesha
“Kuna viungo kwa ajili ya dagaa, nyama,samaki na mboga za majani kwani hujui kusoma au ni vurugu tu umeamua kufanya cheusi mangara 🤕”
🙄 mie huyu nilikaa kimya baada ya kuona njmeharibu badala ya kujenga
“Nilikuwa natania hata mie mara ya kwanza niliweka hivyo viungo kwenye chai nikijua ni viungo vya chai 😀” Mara huyo alianza kucheka nikasahau hata kama nimeharibu
Khalid alikula ubwabwa na mboga yangu yenye ladha ya samaki, maharage, nyama na mboga mboga
Mie huyu sikuwa hata nikiisikia hiyo ladha nilijikuta tu nikibugia kama nafukuzwa hivi ✋
“Hujawahi kula vyakula vyenye ladha kama hii et eeh 🙄”
“Siku zote huwa nakuwa na uchu na chakula nilichopika mwenyewe 😁” Nilijichekesha baada ya kuona naumbuka
😆😆😆 Khalid ni kucheka tu
“Naweza kujua kwanini umeniita hapa 🙄” Niliuliza
“Nilikupa kazi unitafutie demu mwenye sifa kama za Bianca lakini ukashindwa. Utakuwa demu wangu kwa muda pindi atakapo patikana nakutema ✋”
😁😁😁 Mie huyu ni kujichekesha tu lakini ndani ya moyo niulimja kuona nipo hapa kwa muda, yaani ni kama alikuwa ananiambia nimshikie nafasi Mwanamke mwingine
Baada ya kupata chakula, Khalid aliingia kuoga.
Nilitarajia tunalala lakini haikuwa hivyo, tulitoka out jamani nyie 👌
Mida kama hii kila mtu anakuwaga na wake. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu nilimshikilia Khalid mkono, nilitaka kila mtu aone nimemshikilia. Tuliingia kwenye hotel nzuri hivi yenye hadhi ya five star 🌟
“Punguza kunishika mbwa wewe utanikosesha mademu ✋”
Nilibetua zangu midomo kwa maneno anayo zungumza 😏
“Vipi kwani wewe huyo unanipenda Mimi hata ubetue midomo 🙄 hiyo si ni dalili ya wivu “
“Sielewi hata….✋” Nilijibu
Simu ya Khalid iliita, ilionekana kuwa simu ya siri. Alinielekeza anatoka nje kidogo
Sikuwa na shaka, lakini baada ya kuondoka tu niliijiwa na wazo la kujipoteza kidogo. Nilipitia mlango wa nyuma…..ile napambana kujificha simu yangu ilikwapuliwa 😩
Ni heri uniibie nguo lakini si simu, niliianza kumkimbiza Kibaka aliyenipora mwenyewe mdogo tu au kisa na maana ni chalii wa chuga
Nyie watu sijui hata alipotelea wapi, nilijikuta nimeingia sehemu za Wahuni 😩 kulikuwa kunanuka bhangi hatari.
Nilitaka kuondoka lakini kila nilipogeuka nilikutana na Wahuni wakipuliza zao vitu roho inapenda 😳
Nilijikuta nikiwa mtu kati, wenyewe walinitazama kwa kunikadiria
“Shika uvute yote hii mpaka utakapo maliza ✋” Binti mmoja aliyekuwa haoni hata vizuri aliniambia huku akinikabidhi kipande cha sigara.
Mie huyu na uhuni wangu sijawahi kutumia hivi vitu 😭
“Oyaaa unavuta au na kuchinja hilo shingo lako 😏” Nilitishiwa huku panga likikwaruzwa kwaruzwa ukutani
Sikuwa tayari kufyekwa, nilishika zangu kipisi cha sigara ni kataka kukitia mdomoni lakini ghafla nililishuhudia buti la Kijeda likikanyaga ardhi.
Niliachia tabasamu pana baada ya kumuona Khalid 😊
Nilikitupa kipande cha sigara kule
“Mbwa wewe unatupa sigara…🥶” Nilifokewa
Ile natazama vizuri hakuwa hata Khalid ni wenge langu tu 😩
Mie huyu niliangua kilio niliangua kilio cha majuto 😭
Episode 17
😀🤣😆 Hawa Mateja walianza kunicheka kwa kitendo cha Mimi kuangua kilio
“Cheza kamatia chinj bwege wewe ili tukusamehe ✋” Mhuni mwingine aliongea
Mie huyu kusikia nicheze kamatia chini nilianza kucheza kama nafukuzwa 😩
“Hapana, hiyo wamekupa rahisi hebu cheza komasava 😏” Mhuni mwingine aliniambia
Mie huyu tena nilianza kucheza vizuri zaidi hata ya wenye wimbo
“Oyoooooh 😲” Wahuni walinishangilia
“Hebu tuchezee mziki gani ule kweli 🙄?” Mhuni mmoja aliuliza akionekana kupoteza Kumbukumbu
“Unataka kusema wimbo gani ule 🙄 hebu ngoja nikaulize!”
“Chapu basi usichelewe ✋” Mhuni mwingine aliongea
“Kwahiyo mmeniruhusu ni kaulize 🙄” Niliuliza nikiwa na shauku ya kusikia
“Wee fala ni kiziwi vipi 🥴 nimeruhusu nenda ukaulize au mpaka hawa mbwa wengine wakaulize ✋ huoni kama mie ndio na akili kuliko wao 😏 fanya haraka kwenda”
Kusikia hivi niliondoka kama upepo, sikujua naenda uelekeo gani lakini niliondoka kwa kukimbia 😀
Sikujua hata naelekea wapi mbwa hawa wamejua kunitesa, bahati nzuri au mbaya niliiona ile hoteli ya five star 🌟
Si nikajitia kuingia, lakini kila nilipokuwa naangalia mazingira yalikuwa tofauti na hata nilipoitafuta kona niliyoingia na Khalid ilikuwa imekaliwa na watu 😩
“Kwani hizi hotel za five star 🌟 zipo ngapi ni kama nimechanganya mambo hizi 😁” Nilijiongelesha huku ni kijichekesha
“Zipo tano, sasa sijui unasemea ipi ✋”
“Zipo tano 🙄”
“Ndiyo”
“Kutoka hapa mpaka kambi ya Wanajeshi ni shilingi ngapi ✋”
“🤭🤭🤭🤭🤭” Dada wa mapokezi alicheka, sikuelewa ni nini kimemchekesha
“Mbona umefurahi namna hiyo shoga yangu 😁” Ilibidi nijichekeshe pia
“Ni shilingi 2000 tu ukichukua bajaji mida ya mchana, lakini kwa kuwa ni saizi ni usiku utalipia elfu tano, lakini wewe huyo unaenda huko kufanyaje au ndio unataka kwenda kudanga 😀”
“Siyo kudanga hata ✋”
“Kuna rafiki yangu anatafuta pisi hebu tulia hapo ni kuunganishe naye achana na habari za kujipeleka Kambini kwao 👌”
“Yupi huyo tena ✋”
“Tulia hapo aje, mwenyewe ukimuona lazima usisimkwe kama hautamuelewa si unakataa my dear 😏”
“Sawa….” Nilijikuta tu nikiwa tayari kumsikiliza
Alinipa ishara ni kakaa kwenye kiti, baada ya kama dakika mbili hivi nilishangaa kumuona Khalid, eti ndio rafiki wa huyu Dada wa mapokezi kaja niunganishwe naye 😩
“Weee kichaa ulienda wapi 😏 nimeitrack simu yako nikamfuma nayo dogo mmoja hivi, ilikuaje ikamfikia” Khalid alinifokea
“Sikumbuki hata 😤”
“Na bado unaendeleza utapeli wako eti uko umekaa hapa uunganishwe na mie hebu simama tuondoke ☹” Aliongea
Mie huyu nilikuwa mpole nisije kutiwa kibao cha kichwa 😣 kwa heshima na upole niilipokea simu yangu kwa mikono miwili.
Nilimkonyeza Dada wa mapokezi wakati naondoka. Nilimuona haamini kabisa kama mie na fahamiana na Khalid
Kutoka hapa hadi porini siyo mbali, tutatembea kwa miguu ✋
Mie huyu sikuwa na neno nilikubali tukaanza kutembea kwa miguu. Heeeeh! tulikuwa hatufiki jamani 😩
Nilishindwa kutembea jamani nilisimama 😏
“Oyaaa bado kidogo tufike naomba utembee ✋”
“Nimechoka naomba kubebwa 😩”
“Kubebwa 🙄? sawa”
Khalid alinirudia akanibeba mgongoni 😊
Sikuamini kama kanibeba eti, kilicho ni changanya zaidi ni pale alipoanza kunisihi nisije kwenda mbali na yeye bila taarifa ✋
“Kwahiyo unanipenda 🙄”
“Ni kwa muda tu atakapo patikana mwingine sitakuwa na muda na wewe ✋”
Nilijikuta ni kiachia tabasamu kutokana na maneno yake, hakuna upendo wa muda nilielewa fika huyu mbwa ananipenda ni vile tu hawezi kuzungumza moja kwa moja 👌
Episode 18
Siku zilizidi kwenda nilikaa wiki mbili na si moja tena kwa Khalid kama alivyokuwa amesema ✋
Kwa kipindi chote hicho tulikaa kaa kama Mume na mke
Safari yangu ya kurudi Mwanza iliwezekana kupitia yeye 😊
Nyie watu acha tu, nilikuwa natumiwa matumizi kila mwisho wa wiki.
Hakuacha kujishaua kama pindi atakapo patikana Mwanamke mwingine atakaa mbali na Mimi ✋
Mie si mtu wa kulala hovyo ila baada ya kurejea kutoka Arusha nilikuwa ni mtu wa kulala hovyo 🤔
Sikutaka kufikiria mara mbili nilienda zangu pharmacy kupima mimba.
Majibu niliyopatiwa yalishtua moyo wangu 😩
Nilihisi kama na danganywa hivi nilichukua kipimo nikaenda kujipima mwenyewe 😩
😭😭😭 niliangua kilio, mie huyu ujauzito tena jamani.
Nilishika simu nikampigia Khalid lakini hakuwa akipatikana. Nilipiga siku ya kwanza, siku ya pili, wiki nzima, mwezi hadi miezi miwili lakini Mwanaume huyu hakupatikana 😣
Mie huyu bila aibu nilijipeleka nyumbani kwa Mama Monica kwenda kulalamika
“Sina taarifa yoyote kuhusu mapenzi yenu, nastaajabu hata kusikia una ujauzito wa Khalid 🤔”
“Si ndio na kufahamisha Mimi hapa 😩”
“Atakuwa kaenda vitani, akirudi salama sawa asiporudi salama sawa pia 😏”
“Mbona umemkatia tamaa Kijana wako mara hii 🙄”
“Jeuri sana ✋”
“Basi hata uchungulie kwenye kibuyu chako tujue ni kitu kinaendelea 😓”
“Mie huyu nichungulie kwenye kibuyu kujua habari zake? 😀”
“Ndiyo, ni mwanao wa pekee 😓”
“Siwezi kuangalia bure leta pesa hapa ni kufanyie kazi ✋”
Eeeh sielewi kwanini Mama Monica kawa mchungu hivi hasa kwa Kijana wake. Mie si ndio nimewekwa mimba bhana nilijishika mfukoni nikatoa shilingi elfu hamsini
“Hii elfu hamsini tuna angalia tu maeneo ya Tanzania ✋kama atakuwa huko uzunguni utaongeza nyingine 🥴”
Mie huyo sikuwa na namna zaidi ya kukubali.
Mama Monica alienda ndani akarudi na kibuyu chake.
Chenyewe kilikuwa kimechoka asikuambie mtu.
Alikishika akaanza kuangalia huku akiongea maneno yake anayo yaelewa yeye
“Oyaaa, huyu jamaa yako hayupo Tanzania ✋”
“Eeeh 😳”
“Hakuna cha eeeh dondosha laki moja hapa tuendelee kumtafuta kwenye Nchi za wenzetu ✋”
“Mama Monica hela yote hiyo 😓”
“Kipindi una mtapeli Khalid mbona hukusema hela nyingi 🤗 acha nirudishe zangu kibuyu ndani na kazi nyingi za kufanya ✋” Mama Khalid aliongea akataka kusimama
“Eeh subiri nikupe pesa 😩” Niliongea kisha ni kamhesabia
Mama Monica alizishika akazihakiki
“Kujishaua tu, sasa mbona hadi umezidisha badala ya laki moja umeweka laki na nusu 😀 na ndio imeenda hivyo mizimu si watu wa kurudisha, ukijitia kudai wanakuomba dola kabisa”
Mie kimya nilimuacha akafanya yake 😤
“Khalid yupo Nchi moja inaitwa Ethiopia, kuwa na amani yupo kikazi…. mazingira yamembana hawezi kushika simu. Mizimu wamenituma ni kuambie bwana ako atarudi ✋” Mama Monica aliongea
“Kwahiyo yupo Ethiopia 😳”
Kabla Mama Monica hajani hakikishia nilishangaa baada ya kumuona Khalid mwenyewe akiwa ndani ya magwanda yake 😁
Episode 19
Mama Monica alipambana kufunika kibuyu chake lakini alichelewa tayari kilikuwa kimeonekana machoni kwa Khalid
“Mara ngapi nimekuzuia kuhusu utapeli wako? hii kazi wewe huiwezi usiniambie ulikuwa unamtapeli mpenzi wangu 🥴”
“Kumtapeli kivipi?…usitishwe na hiki kibuyu mie nimetunza zangu mboga za maboga na yeye ndio alikuwa hapa kuniomba anataka kuanzisha bustani kwake 😏” Mama Monica aliongea huku akidondosha mbegu za maboga
Mmmmh nyie sikufikiria kama hata huyu anaweza kuwa na utapeli 😀
“Kwanini kule kwako hujafunga mlango?…..nimekaa muda mrefu nimekusubiria mpaka nimechoka. Umekuwa mnene kiasi hebu njoo ndani unipe maji ya kunywa 😉” Khalid aliongea
“Na mkiyakosa hayo maji msije, nyumba yangu ila nyie ndio mnajifanya wenyeji hapa. Haya Jema mwenyewe ingia ndani utafute hayo maji ukiyapata kanywe soda kwa Mangi nitalipia 😏” Mama Monica aliongea
Mie huyu hata sikutaka kumsikiliza, mkono wangu ulikuwa umeshikiliwa na Khalid.
“Wala sina hata haja na maji ya kunywa nilitaka tu uingie ndani, sina uhakika kama umewahi kuingia ndani kwetu”
“Sijawahi, ulikuwa wapi muda wote huo wa miezi miwili nimekutafuta sana kwenye simu bila mafanikio 😓”
“Kazi yangu ni ya ajabu sana, kuna muda napotea tu kama ghafla, kwa kipindi chote hicho nilikuwa na kukumbuka sana sema sikuwa na uwezo wa kupata mawasiliano ✋”
“Wewe huyo ulikuwa unani kumbuka Mimi?….kwani hujapata bado mtu wa kukaba nafasi yangu 🥺”
“Nakupenda wewe, kwa sasa sina wazo hilo tena”
“Nina ujauzito wako, na hii ndio sababu imenifanya nije hapa kwenu kumuuliza Mama yako kuhusu wewe”
“Ungekuja Arusha pale Kambini kuuliza kuhusu Mimi…..siku nyingine ukinikosa kwenye simu kwa muda mrefu usisite kuja Kambini nimekuruhusu lakini pia unaweza kuniamini ukaendelea kunisubiri mpaka nitakapo kuwa narudi ✋”
“Nimefurahi kuona unajieleza kwangu namna hii”
“Unajua kwanini Mimi na Mama yangu tunapishana kauli muda wote 🥴”
Nilitikisa kichwa kuashiria sijui
“Nimeshamkataza kujitia tapeli kwa kuishi kama Mtaalamu lakini kawa kichwa ngumu hasikii kabisa, hili jambo linanipaga hasira na ndio maana huwa simzingatii kuhusu mambo yake ✋”
“Inaonekana alivyokuwa binti mdogo kama Mimi hapa alikuwa ni bonge la tapeli 🥴 ni ngumu sana kumtoa kwenye huu mstari muache tu aendelee kuishi hivyo ataacha mwenyewe”
“Siku zote Waswahili hujuana kwa Vilemba pamoja na kuongea hivi nilijua ni lazima tu utamtetea Mbwa wewe 😀”
Kabla sijatia neno nilisikia nikiitwa nje kwa sauti kubwa
Mie huyo nilienda kwa haraka nikiwa na Khalid.
Nilishangaa baada ya kumuona rafiki wa zamani Tausi akiwa na kaumuka uso inaonekana aligika
Hakuwa pekee yake. Alikuwa na Mwanaume mmoja hivi aliyeonekana kuwa mbabe sana yaani hata uwepo wa Khalid pamoja na mavazi yake haukumtisha 😳
“Jema nimepigwa kwa sababu yako wewe….huyu Mwanaume amekutafuta sana leo baada ya kukukosa watu ndio kumuelekeza kwangu 😭 bila hata kunielekeza shida ni nini alianza kunipiga eti mie huyu nimekufundisha utapeli 😓 mie huyu ndio nilikushauri umdhulumu mimba yake” Tausi aliongea huku akilia
Niliishia tu kumtazama sikuwa ni kielewa maelezo yake 😳
“Nyie mbwa hebu nyoosheni vizuri maneno yenu na si kuzunguka huku na kule ✋” Mama Monica aliuliza, bila shaka hata yeye hakuelewa nini kina zungumziwa
“Jema ni kubwa la mbwa kanitapeli sana nauli zangu, kila nilipokuwa natuma nauli aje ziliishia tumboni kwake ✋ nilijikuta ni kikata tamaa kabisa juu yake 😓 nilipomtishia kumuua alikuja. Mimi hapa maisha yangu si mazuri hivyo baada ya kunasa mimba aliniaga kuwa anaenda kwao kupumzika ✋ sikuwa na baya nilimruhusu. Mbwa huyu kitendo cha kuondoka tu kwangu aliniblock 😭” Mwanaume huyu aliongea huku machozi yakimporomoka
“Una mfahamu huyu 🙄” Khalid aliniuliza
“Wala hata simfahamu na mbaya zaidi sielewi nini anaongea ✋”
“Huelewi eeeh ☹” Mwanaume huyu aliongea akitaka kunipiga
“Uwanja wangu siyo sehemu ya kufanyia vita ✋…fanyeni kuondoka hapa mkazungumzie huko” Mama Monica aliongea
“Msiklize Mama, nendeni huko mkaelewesheni tena itapendeza kama mtafanyia mazungumzo yenu Polisi na si hapa mbele yangu ☹” Khalid aliongea kwa sauti tata akaingia ndani
“Ni ngumu mlevi kuacha pombe 🥴” Mama Monica aliongea na mie kwa fumbo kisha akaingia ndani, hakuishia hapo alifunga mlango kwa ndani
Nilimgeukia Tausi kwa mara nyingine anipe maelezo kwa sababu sikuwa nikimuelewa cha ajabu alinicheka kimtindo 😁
😳😳😳 nilimkodolea macho zaidi baada ya kujua yeye na huyu Mwanaume wako hapa kuniharibia na si kingine
“Haya tuondokeni 😭” Niliwaambia kwa sababu hakukuwa na umuhimu wa kukaa hapa tena
Walinisikiliza jamani, mie nilielekea kwangu na wao wakashika njia yao. Yaani baada ya kuniharibia hawakuwa na shida na Mimi tena 😓.
Mbwa hawa hata samahani tu hawakuomba
Mie huyu ni kulia tu 😭 njia zima
Episode 20
Walimwengu wabaya jamani 😓 sikuelewa kwanini Tausi kaamua kunifanyia hivi. Lakini pamoja na yote haya sikukosa hamu ya kula.
Siku ya leo nilitaka kujikaangia mwenyewe chips na si kununua ✋
Nilienda dukani kwa Mangi nikiwa mnyonge kupita kiasi
“Hiyo sura sasa 😀” Mangi alivunjika mbavu
“Ungejua nilivyo vurugwa wala hata usingenicheka mbwa wewe 🤕”
“Haya nisimulie kilichokupata ✋”
“Nipe kwanza mayai manne na viazi vya buku nisije kusahau”
Mangi alinipatia vitu vyangu ndipo nilivuta kiti ni kakaa. Sikuwa na kifua nilimsimulia kila kitu
😆😆😆 Mangi wa watu alicheka na hata sikuelewa ni kitu gani kina mfanya avunjike mbavu
“Kitu gani hapo nimekufurahisha ☹”
“Nimejikuta tu nacheka, ni kuambie kitu wewe vunga kama hamna kitu kibaya kilichotokea…..kama huyo Khalid kafia ile hatua ya kupenda kupita kiasi ni lazima atakutafuta mwenyewe….ila wewe ni mbwa pamoja na yote ila hamu ya kula ipo pale pale 😀”
🤣🤣🤣 Nilijikuta ni kicheka pia pengine ni kwa sababu Mimi ni mjamzito na ndio maana sikaukiwi hamu ya kula
“Tena wala usijitumishe vimeseji wala kupiga simu. Tulia zako aje mwenyewe kukubembeleza kama asipokuja mazima kausha hivyo hivyo hakuna kuinamisha kichwa ✋” Mangi alinijaza upepo
Mie huyo tena nilijikuta ni kivimba pia 😏
Nilienda zangu nyumbani ni kajikaangia chips langu a.k.a zege.
Baada ya kumaliza kula nilipanda kitandani ni kapumzika kidogo.
Ghafla tu hasira iliniijia, hivi huyu Tausi kanionaje 🤕 nilivaa kijora changu cha rangi ya machungwa kisha ni kashika barabara
Kufika ghetoni kwake nilikutana na bonge la mziki. Yaani alivyokuwa kalifungulia utahisi yeye ndio analipa kodi kubwa kuliko Wapangaji wote ✋
Vile napenda mziki sasa nilijikuta ni kicheza kwanza na hata ni kajisahau kama nipo hapa kumfundisha adabu 😆
“Oyoooooh 😲” Tausi ni kunishangilia tu akiwa dirishani
“Niletee maji ya kunywa unataka kuniua na huo mziki wako 😩” Niliongea nikiwa nimechoka kiuno acha tu
“Siyo maji tu shika na haka kajuisi umuangamize huyo kiu kwenye koo lako 😆” Tausi aliongea, mwenyewe alikuwa amevaa zake pensi na kitop
“Haya ni nini kile ulifanya wewe na yule bwana wako utadhani Baba njelekela kwa ukubwa wa mashati yake 😏”
“Kufanya vipi tena, leo si ni siku ya wajinga kwani wewe na timu yako mlikuwa hamjui 🙄”
Mie kukodoa macho tu 😳…. lakini hata kama ni siku ya wajinga sasa ndio huyu Mbwa afanye utani kama ule
“Kuhusu kuvimba uso shoga angu nilienda eti kufumania jana wacha nipigwe Mimi badala ya kupiga ✋ yaani tangu urafiki wetu uyumbe hata nguvu zangu zimeyumba”
“Wee naye wa moto, sasa ndio upite mle mle 😤 huu ni ujauzito aisee kama ndio nitakasirikiwa mazima jiandae kumlea mwanangu. Yaani Mimi hapo na wewe tutalea huyu mtoto na kuambia 😏” Niliongea
“Kulea mtoto kivipi? kama watakutelekeza wala usiumize kichwa ukisha jifungua huyo Mtoto tutaenda kumtelekeza nyumbani kwa Mama Monica au Kambini kwa Khalid ✋ nipo tayari nitafute nauli kwa udi na uvumba ya kunitoa hapa na kunirudisha” Tausi aliongea
Wote tulijikuta tukicheka 🤣 ushoga wetu ndio ulirudi hivyo. Tulianza kupika na kupakua, mie huyo hata sikuwa na habari kuhusu kumtafuta Khalid wala kwenda kwa Mama Monica.
Ushauri wa Mangi niliuzingatia sana, na hata hivyo nilikuwa na bata kama lote kwani kila usiku tulienda club na shoga yangu. Tulikuwa tumerudi tumechoka ✋ tukiamka asubuhi ni kulala, tukiamka mchana ndio kupika na kulala baada ya hapo ni kulala 😀
Asubuhi moja nikiwa mwenyewe nafanya zangu usafi, nilishtukia mlango ukifunguliwa kwa nguvu na buti paaaah 😩
Nilihisi pengine ni vibaka, nilishtuka baada ya kukutana na Khalid, alikuwa amefura kupita kiasi vile ni mweusi sasa alifanana na mkaa 🥶
“Shi …shiii…shikamoo” Nilimsalimia 😵
“Shikamoo na wewe cheusi mangara usiyekuwa na mshipa wa aibu 😏”
“Kosa langu ni lipi hapo eti Mwanaume wewe 😏 halafu kuhusu weusi mbona hata wewe ni mweusu kuzidi Mimi Babu weye” Niliongea bila kufikiria
Khalid alinitazama kwa macho ya mshangao 😳
Mie huyu ndio kumpanda kichwani sasa bila ngazi, nilianza kumchamba na kitu kilichonifanya ni angue kicheko ni kidoti chake 🤣 yaani tangu nimfahamu sikuwa kuona kama ana kidoti mfano wa jokate
🤣🤣🤣🤣🤣 nilizidisha kucheka bila kufikiria yajao.
Nyie watu 😩 nilishtukia tu Khalid anapiga ngumi kwenye meza yangu ya mbao ikavunjika 😳
Episode 21
“Weeee Mwanamke unanicheka Mimi 🥶”
“Siyo kukucheka tu sikutaki 🥶 umevunja meza inayo ni kumbusha enzi zangu nilivyotolewa bikira, baada ya hasira zako kuisha fanya kusepa mie huyu msela sibabaishwi na uwepo wako mwenyewe najiweza 🥴 kama niliweza kula na kunywa kwa kukutapeli wewe sishindwi kutapeli wengine, na kwa wakati nitahangaika na wenye Nchi siyo Mjeda tena 😏” Nilivimba
Heeeeh! 🤣🤣🤣🤣 nilishangaa tu Khalid akivunjika mbavu sikuelewa ni kitu gani kinamchekesha namna hiyo
“Kitu gani kinakufurahisha hivyo…😩” Niliuliza baada ya kuona anacheka hadi nakosa amani
“Oyaah wewe sikuwahi kugundua kama una komwe kubwa namna hii. Yaani ingetokea ungezaliwa wa kiume ungekuwa na upaa ukiwa na miaka minne ✋ “
🤣🤣🤣 nilijikuta ni kicheka tu, nilisahau kuhusu kupasuliwa meza yangu. Niliingia jikoni ni kapika.
Baada ya kumaliza kupika chakula tulijiachia kitandani kukazia uumbaji ✋
“Nadhani wiki ijayo narudi kazini, kabla ya kwenda kazini nataka niende kwenu. Si vizuri tumbo kuendelea kuwa kubwa bila kwenu kuwa na taarifa, hata kama si wafuatiliaji wazuri kuhusu Mtoto wao tutawasaidia kuwa wafuatiliaji ✋”
“Unataka kwenda kwetu 😳”
“Ndiyo mbona kama una hofu 🙄”
“Unaweza kwenda tu bila hata mie, nitamuambia Tausi akusindikize 😊”
“Muda huo wewe unakuwa wapi? 🥴”
“Nyumbani siwezi kwenda kwa sasa kuna kosa nilifanya….hivyo wewe kama unataka kwenda nitakuunganisha na Tausi ✋”
Nyie nilipewa kibao cha kichwa ni kaanza kuona nyota nyota 😩
“Huyo Tausi ananisindikiza kupeleka maiti yako au ni nini unataka kusema 🥶 nitakukanyaga teke mbwa wewe”
“Sawa tutaenda, kuitana Mbwa siyo poa 😏…..”
“Nikikuacha hapa unaweza kutoroka mbwa wewe, tutalala hotelini asubuhi sana tutaondoka ✋”
Mie huyu sikuwa na usemi tena, ndoa naitaka ila nikifikiria kosa nililoliacha nyumbani miaka 5 iliyopita nilisikia kulia 😓
Unajua ilikuaje?… kipindi hicho ndio naanza kukua basi mwenzenu niliiba baiskeli ya Baba aliyopatiwa na Mjomba wake 😩 haikuwa baiskeli tu ya kawaida iliendeshwa na Mababu wa ukoo enzi na enzi. Mie huyo nimepata penzi jipya hicho kipindi si ndio nilijichanganya ni kamhonga Mwanaume ili nipendwe zaidi. Hata nilipendwa sasa 😭 Mwanaume huyo alikuwa ni tapeli alihama Kijiji. Mie huyu sikuwa na jeuri ya kuendelea kukaa nyumbani ndio chanzo cha kutoroka. Sasa huyu Mjeda naye anataka twende nyumbani si ndio kunichanganya 😓
Kulivyo pambazuka tuliondoka jamani, njiani tulimkuta Mama Monica, Mangi pamoja na Tausi wametusubiria
Mie ndio kuchanganyikiwa 😳 leo si ndio nitaenda kuabika huko vile Baba yangu hanaga msamaha 😩
Tausi ni mmbeya ☹ Mangi ndio usiseme si ndio watayaandika sana magazeti pindi tutakapo rudi 🥴
Nilikaza moyo liwalo na liwe bhana, kwetu siyo mbali sana kiivyo. Tulifika baada ya masaa mawili kupita.
😵😵 Baba yangu alikuwa anafuta futa viatu vyake baada ya kuniona tu alitaka niruke kichura chura
“Subiri atuzalie mtoto wetu ndio muanze kupeana adhabu za makosa yenu ya nyuma 😏” Mama Monica alinikingia kifua
🤣🤣 Muda wote nilikaa nyuma ya Mgongo wa Khalid.
Baba akisimama, mie huyo nilisimama pia ✋
Mahari ilitolewa, wengine wote walikuwa tayari kulala lakini mie huyu sikuwa tayari
“😁….lala tu yameisha mwanangu nimesha samehe ✋” Baba yangu huyu alitaka kuniingiza kwenye mtego
“Kunalalika basi hapa 😏 mie nitatangulia Mjini ✋”
“Mwanangu naomba ni kuchape hata fimbo mbili tu hasira iishe 😓” Baba aliongea
Kila mtu alinishauri nichapike fimbo mbili 🙄. Nyie kitendo cha Baba yangu kuushika mkono alichapa fimbo 10 😭
Yote kwa yote yaliisha, tulilala hapa kulipo pambazuka tuliondoka
Maisha yaliendelea ulikuwa ni mwendo wa kujidekeza tu ✋…nilimpanda kichwani Mama Monica hadi akasalimu amri vile Khalid hakuepo na alikuwa na dhiki na Mjukuu alikoma nyie 🤣
Nilijifungua mtoto wa kiume mwenyewe ana nguvu asikuambie mtu. Kila Khalid alipopata likizo alikuwa anakuja, kwenye ulazima nilimfuata ✋
Jema mie kutoka kwenye kumtapeli Khalid nauli yake hadi ndoa. Huu ni zaidi ya utajiri 🤭 ahsanteni kwa kunisoma jamani.
💥MWISHO💥