DEREVA WA BABA
SEHEMU YA SITA
Morgan akamfata mynda huko huko, nae akaenda kuelezea shida yake amempenda sana na Morgan kweli alikuwa amempenda huyo dada sana tuu 🤌
Mynda akamwambia mie mbona nishaongea na mwenzio tayar na tumeelewana ,🙄🙄🙄 Morgan alilitoa jicho kama kabanwa na mlango yaan. Huyu Robby naenda kumtoa meno, akataka kuondoka kwa hasira 🤨🤨
Mynda akamshika mkono ,akamwambia yaan wewe ni mtu wa hasira sana aisee😊😊 ,mwenzio kasema ananipa laki tano we mpandie tu hakuna kinachoshindikana bwanaaa😇
Ikabidi Morgan awe mpole baada ya kusikia mambo ya kupandiana dau sasa😆😆 , sio kama hana hela , Hawa vijana wote wanahela za kuchezea nyingi mnoo na hawana kazi yeyote bado wanatumia za wazazi wao , Wanadai muda wao wa kutafuta hela haujafika😅😅
Morgan akamwambia Mynda mie nakupenda sio nakutaka kwa usiku mmoja Noo!!! Nataka uwe wangu yaan ikiwezekana basi tuwe familia ,,, Mynda alichekaaa🤣🤣 akamwambia we babaa weee mbona wa zamani sana wewe 😆🙌🏾
Sikuhizi hakuna kuoana baba kupendana ilikuwa zamani we kama unataka familia nilipe nikuzalie utamtunza huko mtoto unapo taka wewe😒”
Mmh🙄🙄🙄 akaona leo amevamia mtumbwi wa vibwengo akasema okay unataka shingap one night?? Mynda akamwambia nilipe juu ya mwizio fanya hata laki saba hivii ukinipa ml 1 nakaa na wewe wiki zima🤗🤗🤗
Mmh Morgan akasema okay nipe namba yako nitakucheki , Mynda akamwambia hakuna cha namba we toa Advance bwana 😇 , Morgan hakuwa na ajizi alitoa laki 3 akampa
Ndio mynda akatoa namba ya simu yake😅😅,
Morgan alirudi ndani akiwa na hasira na Robby moyoni akasema sina shida tena na huyo dem lakini nakukomesha hautampata nitamlipa ya wiki yote baada ya hapo utajua wewe sasa afu tuone nani mjanjaaa 🤨🙌🏾…. mesha alimuona jinsi Morgan anavyomtazama sana Robby akaelewa hapa kuna shida ikabidi awaite chembe kwenda kuongea nao 🤔🤔
Lakini kila mtu akasema yeye hana shida na mwenzie na hakuna alieweka wazi kuwa kuna shida imetokea au alienda kuongea na mynda kila mtu ikabaki siri yake🙌🏾 , wakati kina mesha wametoka huku nyuma kinywaji alichokuwa anatumia Irene kilikuwa kimeisha , Ikabidi Lawrence amfatie , na tayar muda ulikuwa umeenda sana yaan usiku 🤥
Baada tu ya Lawrence kurudi na vinywaji irene akasema yeye imetosha anataka waende kulala , Lawrence akasema si unaenda kwenu ?? Irene akakubali akaona hapo hapo Lawrence akimpeleka kwao ndio akamuone na mama yake hakujali hata usiku 🙌🏾
Alichukua simu yake akampigia Yaksun, Yaksun alikuwa amelala tayar nyumbani kwake chumba chake kimoja cha uwani sio mbali sana kutoka kwenye nyumba ya wazazi wake ni mtaa wa pili kutoka hapo ,
Mlio wa simu iliyokuwa imechomekwa chaji ndio ulimshtua Yaksun ☹
Akajiuliza usiku huu nani anampigia simu,akajiinua kivivu akashangaa namba ya irene hakuwa amehifadhi lakini jioni ilivyompigia alinakiri namba za mwisho ndio mana haikuwa shida kuikumbuka …
“Usiku huu bint msumbufu huyu aiseee” aliongea huku anairudisha hakutaka kuipokea,Akarudi kitandani kabla hata hajavuta shuka ikaita tena akainuka kwa hasira akaenda kuipokea
“We vipii mbona hupokei simuuu???” Ilikuwa sauti ya Ireene tena akiongea kwa ukali wa kulalamika kwanini simu yake imeita haikupokelewa?? Yaksun akajikuta hata zile hasira zake za kupigiwa simu usiku zinaisha akabaki kimyaa
Irene akaanza kuita haloo haloo halooo muda wote palikuwa kimya baada ya sec za irene kuhangaika akidhani hakuna mtu hewani ndio Yaksun akaita Ndio nakusikia …
Yaksun aliongea sauti nzito ya kiume 😇Irene akatoa kwanza simu akatazama namba ni ya Yaksun au Amekosea mbona sauti nzito sana 😅😅🙌🏾
“Naa..naa..naongea na Yaksun??” Irene akauliz huku hana uhakika kama ndie au vipi Yaksun akajibu ndio Mbona usiku😋?? Irene kwa nyodoo akamwambia nataka uniijie hapa ulipo nileta ,,
khaa Yaksun akamwambia sa hii sa 7 hii si uchukue Tax jamani mie nimeshapeleka Gari kupack na nimelala tayar we chukua tax 🤥…
Irene akaona mbona huyu kaka anadharau sanaa yaan anamwambia aje kumchukua yeye analeta nyodo 🤨, akaanza kufoka kwa amri kama kawaida yake🙌🏾 , Yaksun hakumjibu akaitaka tu ile simu kitendo cha kukata simu irene alipandwa na hasira akaanza kupiga simu kwa hasira bila kupokelewa ☹☹
Mesha akamuona kama amepanick akamuuliza akamuelezea , mesha akachukua simu yake akampigia Yaksun , akamuomba sana kistaarabu amfate , Yaksun ikabidi ainuke tu lakini ndo kwa hasira na yeye🤨🤨, alikuwa anavaa huku anajilalamikia mwenyewe huyu Mwanamke hivi analinga niniii☹☹ …
Lawrence na Irene walikuwa wamesimama nje ya Geti ,wanamsubiri Yaksun kina mesha nao walikuwa pembeni wao walikuwa na gari yao🤔🤔, Morgan na Robby kila mtu alikuwa anaipiga namba ya mynda muda wote lakini hakuna aliepokelewa simu yake ☹🙌🏾
Na hata walipo mtafutia macho bado hakuonekana 😒😒,simu zilikuwa nyingi wote wanapiga bila kujuana kuwa wanapiga 😅😅😅
Msg iliingia kwa Robby baada tu ya simu kukata (bwana wee embu usinisumbue simu nyingiii kama nimechukua Roho yako bwana hicho kijilaki ndo usumbue wakati wenzio wanalipa kwa dollar embu mwambie na hiyo mjinga mwenzio muache kunisumbua,mnanipigia sanaa pesa yenu nawatumia wote ) 🙄🙄🙄 Robby akasema au sijaelewa akarudi kuisoma sms mara ya pili na tatu , tunamsumbua wangap?? ,ndio akapata akili ya kumuangalia Morgan akamuona kweli yupo bize nae anahangaika na simu kama anampigia mtu alicheka sanaaa🤣🤣🤣🤣 akamfata akamwambia vipi akupokelei mzee ulimpa shingap advance 😅😅🙌🏾
SEHEMU YA SABA
Morgani akamgeukia na bonge wa ngumii🤣🤣🤣yeye mawazo yake Robby itakuwa kaongeza dau kwahiyo yeye kachinjiwa baharini😅😅🙌🏾 ,
sasa anamletea dharau na dharau morgani hajapenda 🤨🤥
Robby kwake hakutegemea kwahiyo ilikuwa gafla sana hata kukwepa alishindwa ngumi tayar ilikuwa imemfikia usawa wa jicho lake la kushoto 🥺🤥🤥,
Aah nae akasema hii imezidi alirudi na ngumi jiwe kwa Morgan 🤥, Morgan aliiona ile anakwepa kumbe alikuwa amekanyaga sehem mbaya akaenda mzima zima chini🤣🤣
Robby akamfata kwa juu ngumi mbili za hasira tayar kundi lote mpaka Lawrence akafika kuwaamua tena Lawrence alifoka mpaka kiswahili wakati hakijui🤣🤣 hakuwa anataka kujiingiza kwenye ugomvi wao ila aliona kerooo🤌🤨.. akawaambia wanaume mnagombana kisa malaya 🙄😳??
Ndio Robby akawaonesha ile msg aliyo tumiwa na Mynda ikabidi Morgani aanze kuomba samahani sasa mana hakujua😔😔🤥 ,
hayo yanaendelea na lile zogo la marafiki Yaksun alikuwa kafika muda amepack mana alipiga honi za kuwaita mpaka akachoka hakuna hata alieonesha dalili za kusogea alipo 😡😡😡 yaan kazi alihisi inataka kuota kipele hii irene kawa kama yeye ndio anayetoa mshahara wake🙄🙌🏾 …
Karibu lisaa zima liliisha la kuwasuruhisha Morgani na Robby kwanza wote washkaj wamesoma chuo wote yaan wanajuana kitambo sana kila kona wapo 🤌, mpaka wamemaliz kuelewana hapo maana wote wametapeliwa Yaksun akajikuta mpaka amesinzia ndani ya gari😒😒🥺 , ndio wanakuja kumgongea kioo awatolee lock kwenye milango 🤥
Akatoa kimya baada ya kuingia ,Lawrence alimsalimia kwa kingeleza maana yeye hajui kabisa kiswahili☹☹ ,Yaksun hakuitikia akawasha gari bila hata kuwauliza tunaenda wapi😒😒, irene akacheka nae akaongea kwa lugha hiyo hiyo akamwambia Lawrence hajui hata kingeleza huyo baby 😅🤣🤣
Wakageuza kichekesho,Yaksun hakuonesha hata dalili za kuwaza ujinga wao yeye alikuwa zake kimyaa muda wote ni kujilamba lamba tuu midomo kama wazungu 😅 hata hilo halikumshuhurisha pia Yaksun 😒🙌🏾 …
Akawafikisha nje ya geti la nyumba kubwa ya kina Irene🤔🤔, akasimama nje ya geti hakupiga honi kuomba kuingia ndani 🙄 akawageukia nyuma akamwambia tayar tumefika jamani mie sintaigiza gari ndani vyema mkashukia hapa🙌🏾 …
Irene akamwambia washuke kuingia ndani Lawrence akamwambia mie sintaingia ndani ila nitakuje kesho asubuhi 🤔🤥
Irene alikasirika mana alijua huyu ndio kaja hivyo kwao sasa anamletea habar za kuwa anakwenda kulala hotel kisha kesho asubuhi ndio atakuja hapo kwao😔😔🙌🏾 , Irene akamwambia basi tunakwenda kulala wote huko huko mie nimekumiss sana bwaa😔😔
Irene alikuwa anaongea kwa Kujibebishaa mpaka basi ila alikuwa anatumia lugha ya English ambayo Yaksun hakuwa anawaelewa 🤔🤥
Lawrence akaanza kumshika shika Irene maeneo ya Bibi huko🤗🤗 na vile alikuwa amekunywa pombe ndo kabisaaa mambo yakawa simple tu miguu chwaaa mmoja kasikazini mwingine kusini😆😆,
Lawrence akamwambia irene amwambie Yaksun ashuke kwenye gari akawasubiri nje anafanya chap🙄🙄 irene akamwambia hapana tusifanye hapa twende tu hotel nitalala huko mama hawezi kugomba🤭🤭🙌🏾
Lawrence akakataa hilo🙄🙄 akamwambia anaheshimu sana taratibu za nyumbani hawezi kuwakosea adabu wazee😐😐 mana kabla ya kuja alipitia taratibu za wazazi wa kiafrika kwahiyo anajua heshima zotee 🤔🤌
Irene ikabidi akubali mana yalikuwa yamemfika shingoni🥺🥺 akamwambia Lawrence kesho asubuhi aje lazima akamwambia hata usijali kipenzi mie kesho hata kabla hujaamka nitakuwa hapo mlangoni 😒🙌🏾
Irene akamuita Yaksun , Yeey muda wote alikuwa kimyaa kama hayupo hapo😒😒 , Yaksun akaitika bila hata kugeuka☹ , irene akamwmabia naomba unisubiri hapo nje dakika moja tu🤨🤨 ,,
🙄🙄 Yaksun akawageukia kwanza akasema kama nitashuka hapa nitaondoka moja kwa moja😳 hii ni nje ya kazi🙌🏾 embu kuwa na heshima kidogo madam kama unashindwa hata kujilinda mwenyewe nani atakuja kukulinda🙄🙄 wewe sio wa kufanya kila sehem wewe sio malaya ok muwe na kazi njema😳😳🤨🙌🏾…
Yaksun akafungua mlango ili kutoka☹, maneno yake yalikuwa kama dharau au kejeli kwa Irene🤨 , Yaksun aliongea makavu wala hakupindisha maneno😳😳🤨 , Wakati Yaksun anashuka irene akamzuia asitoke🤥 , Lawrence akamuuliza vipi🙄??
Mana yeye hakuelewa Lugha , Irene akamwambia wewe nenda mie nitaenda ndani kesho asubuhi uje 😒😒
Lawrence hata hakuuliza mara mbili alishuka kwenye gari, Akaita Tax kurudi hotel aliko kuwa kafikia🤨, irene akabaki kajiinamia humo humo ndani ya gari aibuuu😔😔😔
Hakutegemea kama Yaksun anaweza kuelewa alichotaka kukifanya ndani ya gari🤭🙌🏾 ,Hata hamu ya kushuka hakuwa nayo alitamani kuongea neno lakini hakuweza kusema🤥🤥☹
Alikuwa kajiinamia zaidi ya dakika 10🤔😔, Yaksun akamuita bibie vipi mbona hushuki🤔🤔?? Irene akabaki kupikicha vidolee😟😟 , akajitengeneza vizuri 😟😟 Akamutia Yaksun!!! Yaksun akaitika Naam huku anamtazama😐
Irene alikuwa anapikicha tu vidole kawa mdogoo sio yule wa matambo😅😅😅 ,Akamwambia Yaksun sio hivyo ulivyo fikiria hatukua tunataka kufanya mapenzi sema tu wewe hukuelewa vizuri 😔😔😔
Irene alikuwa anaamini kwakuwa walikuwa wanaongea lungha ngeni lazima Yaksun hakuna alicho ambulia ila tu alicheza na nyakati au aliotea 🤣🤣
Yaksun akasema ooh sawa madam haina shida ,naomba uniruhusu mimi niende kupumzika😒🙌🏾….
Irene akamwambia naomba basi nikuombe kimoja cha mwisho tafadhali 😔😔, Yaksun Akasema mhuu kipii hikoo 🤨,,
Naomba unipeleke alipo Lawrence nakuomba Yaksun nakuombaaa😟😟🙏 ohooooo Yaksun alijikuta anachoka kabla hata hajatoa jibu🙄🙄 irene alimuomba kweli na hiyo ilikuwa mara ya kwanza irene kuomba kitu mana yeye anatumia amri tu😆😆
Yaksun akasema poa ni wapii🤨?? Irene akamuelekeza😒😒
SEHEMU YA NANE
Kwa kuwa irene alikuwa ameambiwa hotel aliyokuwa amefikia Lawrence haikuwa shida kufika😒
Akili yake ilikataa kabisa yeye kulala nyumbani🤥 halafu Lawrence akalale peke yake🤔 wakati amekuja kwa ajili yake🥰 , hiyo heshima anayoizungumzia yeye hata haijui kwanza 🙄🙄
Yaksun alimpeleka mpaka nje ya hotel akashuka 😒😒baada ya kuhakikisha ameingia ndani ya geti naye akawasha gari kurudi nyumbani kwake😐😐 kwa jinsi alivyochoka hata hakuhitaji tena kupeleka gari parking akawaza kwenda nalo nyumbani moja kwa moja 🤨🤨…
Irene baada ya kuingia ndani kabla ya kufika mapokezi alimpigia simu Bro mesha akamuuliza Lawrence yupo chumba kipi 🤥, baada ya kupewa maelekezo na mesha ndio akaingia na ilikuwa baada ya kupiga sana simu ya Lawrence haikuwa inapokelewa ndio kampigia mesha 🙄😒
Baada ya kufika mapokezi akatoa utambulisho wake na mtu ambae anamtafuta😒😒 , ikapigwa simu ya mezani chumbani kwa Lawrence mara mbili haikupokewa
Ikabidi wamruhusu kwenda kwa jinsi alivyojitetea sana 😃😃😃😅,
Alipo fika akausukuma mlango kwanza kujaribu kama upo wazi au vipi🤗, ikawa bahati kwake mlango sijui alisahau kufunga au aliamini sana usalama wa hiyo hotel 🙂
Irene akaufungua moja kwa moja hakuwa na shaka Lahaula alicho kionaa😳😳😳 kwanza Alibaki kasimama pale pale mlangoni nguvu za kuingia ndani akakosa😲😲😲😲
Akamuita Lawrence 😩😩😩 aliita kwa hasira hiyo sauti yake ndio ilimshtua Lawrence Aliekuwa amelala kitandani akitazama juu na juu yake alikuwa mwanamke tena anajipimia size yake 😩😩😩😩😩 Sauti ya Irene ndio ikawashtua Lawrence akakurupuka akamsukuma pembeni yule dada 😩 lahaula bado irene akapigwa na mshanago mwingine baada ya kumuona huyo dada ni yule mynda aloo😩😩😩 yaan yule dada aliekuwa anagombaniwa na Morgan pamoja na Robby et ndo kalala na Lawrence 🤨🤨 , Huyu huyu Lawrence ambae hata hakuwa anafatilia ule ugomvi tangu mwanzo na ndio huyo huyo mwisho aliingilia tena kwa ukali akawashangaa kwanini wanagombea malayaa😒😒😒 ..
Irene akamuuliza Lawrence kwahiyo ni wewe ndie ulie lipa kwa dollar😳😳??
Lawrence akavuta shuka mana muda wote alikuwa amebaki kapigwa na butwaa☹. Mynda alikuwa anavaa nguo yake taratibu kama vile hakuna fumanizi maeneo hayo
Lawrence Kainuka kumfata irene alipo kuwa kasimama 😥😥,
mynda akamvuta akamwambia embu nipe kwanza pesa yangu afu nyie mkaendelee kubembelezana huko mie sina muda wa kupoteza bwana kuwatazama😏😏😏
Heee🙄 Irene akabaki kuwatazama sasa hajui aondoke apigane au afanye nini🥲🥲
Miguu yake ilikua inatetemeka anahisi kama homa lakini sio Homa hasiraa mpaka anatamani kumpiga huyo mynda lakini anajizuia🤨🤨 ,akabaki kuhema haraka haraka😒😒
Lawrence akamwambia mynda embu nenda nitakutafuta tafadhali niacheee😳!!,Sasa Lawrence anaongea English wakati mynda uzuri wa buree kichwani ni zero zero zimekumbatiana😂😂😂
Mynda akamwambia bwana wee usinichanganyee embu nipe pesa yangu we vipiii nipe pesa yangu!!😡
Mynda sasa alikuwa kashapanic anaongea kwa sauti ya juu kama kuna ugomvi 😬😬
Irene akabamiza mlango akatoka mbio, Lawrence nae ilibidi afate mbioo nyuma na shuka lake ndani akiwa pwee mtupuuu🧐🧐 ni tamaa tu za kutaka kujaribu kwa Mynda lakini sio et hampendi Irene🥴🥴 anampenda sana tu sema ndo vilee alijawa na tamaa kuonja vingine radha zake 😎😎
Lawrence alifata nyuma majuto sasa ndio yalikuwa yanafata kichwani yanazomea kwa kasiii nae anajiona kweli jitu zima hovyo 🤕🤕, Mynda yeye alikuwa ashavaa ila pesa yake hajapewa baada ya kumuona Lawrence amemfata nyuma irene nae akatoka mbio 😲😲,we mwehuu embu nipe hela yangu bwanaa nipe hela yanguu unataka kunilala kwa mkopo we mzungu vipiii???,
Mynde alikuwa anakimbia huku maneno yanamtoka wakageuka kuwa vituko kwa baadhi ya wageni walio kuwa wanaingia hapo hotel pamoja na wahudumu 🤥…
Irene alikuwa anakimbia huku analia akatoa hadi nje ya Geti Lawrence wakati anataka kupita nje ya Geti mlinzi alimzuia akamwambia huwezi kutoka ukiwa na mali ya Hotel kakaa😔😔. Lawrence alijitetea mno hawezi kuiba atarudisha tu hata hivyo vitu vyake vyote vipo humo humo hotel kwahiyo amuamin 😶😶
Mlinzi alikataa kata kata akamwambia haiwezekani😒😒 ,Na mynda nae akawa amefika akamshika shuka lake Lawrence vizuri akamwambia hayaa we baba nipe hela yangu huwezi kunilala mkopo mimi na unipe ya usumbufu kunikimbiza kimbiza mie kama mwendawazimu kama ulikuwa unampenda sanaa huyo mwanamke si ungekuwa nae yeye badala ya mimi embu usinichanganyee naomba hela yangu …😏😏😏
Lawrence akawa mpole akamwambia ipo huko ndani😒😒, Mynda hata hakujibu alimvuta kwa nguvu kumrudisha ndani ,mlinzi kimya akarudi kuketi eneo lake 😒 ..
Irene hakuwa hata anaamini macho yake kile yalichoona alibaki tu kusema yaan Lawrence😔😔. Lawrence wewee aaah sio kweli mungu wangu yaan Lawrence unanunua malaya na wewe daah😪😪 ..
Hapo anaongea machozi yanamtoka kichwa kinamuuma akachukua simu yake akampigia Yaksun huku analia😭😭 , Hakuwaza hata kumtafuta mesha ndio msiri wake 😔😪🙌🏾..
Simu ya Yaksun iliita mpaka ikakata bila kupokelewa akaipiga tena ikaitaa pia haikupokelewa😒😒, Sio kwamba Yaksun hakuwa ameiona simu alikuwa bado yupo njian anaelekea kwake kupumzika simu ilikuwa inaita anaitazama tu 🤨🤨
Ilipo ita mara ya tatu aliishika huku anajisemea Huyu mwanamke ni msumbufu embu ngoja nimuoneshe kwanza Ili asiniendeshee😲🙌🏾 ..
Yaksun akaipokea ile simu hakusubiri hata irene aongee akasema yeye mfululizo tena kwa ukari haijawahi kutokea 🤨🤨😳
SEHEMU YA TISA
Yaksun akapokea simu huku tayar alishachoka kumvumilia Irene yaan alichoka haswaa
Akamwambia sikia wewe nimeajiriwa na baba yako na sio wewe sawa 🤨🤨🤨we dem wewe afu kama hiyo kazi kesho nitaacha 🙌🏾tafuta dereva anaeweza kuvumilia kero zako au mwambie bwana wako akue…..” Yaksun alikuwa anaongea kwa hasira na alimaanisha kweli hiyo kazi ataacha😬 , Kabla hajamaliza maneno yake alisikia kama irene anavuta mafua ya kilio 😪😪
Mmh kwanza akaguna akatoa simu sikioni akatazama aliempigia ni iren kweli au 🤔🤔
Akakuta ndie yeye🤔🙄, akarudishia simu kwenye sikio akaita haloo haloo😟😟!! Lakini palikuwa kimyaa akaita tena haloo ☹☹,Akajibiwa na ile ile sauti ya kuvuta mafua ya kilio 🧐🧐
Akajikuta anauliza kwa wasi wasi we irene unaliaa😳😳?? Weweee , ikawa kimyaa mara simu ikakatwa 😫😫
“Mungu wangu huyu bint ana ninii😢??” Yaksun akajiuliza huku anainuka haraka haraka alishasahau kama alitakiwa kulala muda huo na alikuwa kachoka 😕😕🙌🏾
Alitoka haraka mpaka ndani ya Gari haraka haraka akasahau chini hakuwa amevaa chochote 😲zaidi ya Ki pensi kifupi cha kulalia kilichombana haswaa juu alikuwa kifua wazii 😟😟
Sio kama alitoka maksudi hapana 😟😟 hali ya Irene ilimchanganya 😧😧yaan kwanini irene ampigie simu huku analia kuna ninii 😢😢, aliwasha gari huku akiipiga simu ya Irene ikawa inaita tuu bila kupokelewa 😩😩, Ikamfanya azidi kuchanganyikiwa 😫😫
“Shiit. Sasa nilimpeleka kufanya nini huko kama amepata tatizo nitawaambia nini wazazi wake mungu wangu ooh naomba iwe salama please irene pleas be Safe mamy😔😔😔”
Yaksun akakanyaga mafuta kwa kasii😠😠 , Usiku huu bara bara ilikuwa nyeupeee haikuwa na mpishe mpishe ya watu wala magari🤌 ikampa nafasi kukanyaga mafuta kikweli kweli🙌🏾🙌🏾 , gari ikawa inateleza tu kwenye lami 🤔
Dakika 20 tu Akawa anafikia eneo alilo muacha irene kwenye hiyo hotel 🤨🤨 , simu haikuwa bado inapokelewa …🤥🤥
Muda huo na Lawrence nae ndio alikuwa anatoka nje wakiwa wameongozana na Mynda🙄 baada ya kwenda na kumpatia pesa yake😒😒
Mynda akasogea hadi karibu na irene🙄 akaaanza kucheka kwa jinsi irene alivyokuwa kajikunyata hakuwa na pa kwenda usiku huo😪😪 ndomana aliganda hapo nje kwa muda mrefu hakukuwa na tax wala piki piki 🙌🏾🙄
Mynda akamwambia yaan we bint wa kizamani kwelii🙌😅😅😅 hivii Mpaka leo bado kuna ma bint wanalilia dudu ya yuyuu🤣🤣🤣 we umenikuta kwani mie naikata et naikataa au uliambiwa ibaki kwenye pachu pachu yangu🤔🤔 , nalitumia naliacha we unatumia muda wote. Dada angalia pesaaa mapenzi achia kuku kwa vifaranga vyakee👌👌 pole weee 🙌🏾…. “
Irene alipatikana kweli akabaki kimya😥 ,Lawrence alikuwa anaawatazam tu hata haelewi nini afanye 😟😟,,Baada ya mynda kutema nyongo yake akasogea pembeni akachukua simu yake akaitafuta namba ya Morgan 🤔🤔🤔 “bora hata nikamalizie usiku wangu kwa huyu anaonekana shababi hichi kizungu uwiii cha baridiii🤣🤣sasa sijui huyu dada analilia niniii?? Yaan hicho kidudu cha kumfanya achanganyikiwe show enyewe zero uwiiii🤣🤣🤣 Embu we kaka pokea simu nije kukesha kwako” Simu ya morgani ilikata bila kupokelewa🤌 …
Muda huo huo na Yaksun ndio alikuwa anapack gari kwa break kalii baada ya kumuona Lawrence anamvuta Irene kumrudisha ndani🤔🤔 ,Lawrence alikuw kwenye zoezi la kumshawishi irene aingie ndani wakayamalize😪😪 …
Yaksun hakuuliza na hakuna aliemuona wakati anakuja kwa kasii☹☹,Mynda ndie alivutiwa na tukio hilo maana yeye peke ndio aliona tangu Gari inafunga break za nguvu Yaksun kushika akiwa nusu uchi na kwenda kwa kasi upande walipo Lawrence na Irene 🙄🙄
Hakuuliza nini kinaendelea alimshuka Irene kwa nguvu akamvuta nyuma🤔 ,Irene akashutuka amevutwa na naniii,Lahaulaaa🙄🙄🙄alipo geuka akabaki mdomo wazi yaan jinsi Yaksun alivyo na ki pensi kifupiiiii kimeficha tu nanihii akee basi😩😩😩 macho ya irene yakatua kwenye nani hii 😲😲😲 hee ndo Yaksun akashusha macho kutazama alipo tazama irene si ndio anakuta kituko alicho nacho🙄🙄
Baridi nalo likamvaa yaan ile hali sasa ya kuwa nipo uchi ndio akaanza kuipata hapo😅😅😅 ,aibu sasa mbele za watu akajilaumu moyoni lakini usoni akajikaza kama hakuna baya alilo fanya☹ ,akamwambia irene tuondokee😳😳!”
SEHEMU YA KUMI
Iren akabaki anamshangaa akamuita we Yaksun upo sawa 😔😔?? , hakujibu kitu akamvuta waondoke 🤥🤥
Lawrence akamuuliza irene kwani huyu ni Dereva au bwana wako🤨?? , Lawrence aliuliza kwa ukalii nae alimbadilikia😠😠 , kabla irene hajajibu akamfata Yaksun akamsukuma ili amuachie irene wake😒
Lawrence akamwambia we mwanaume mpumbavu unakazi ya kuingilia mahusiano ya watu unafikiri unamuweza irene😳😳??”
Lawrence aliongea kwa kingeleza ,Yaksun akamsogelea hatua tatu mbele yake 🤨
Akamjibu kwa lugha yake ile ile alotumia akijua Yaksun ni Debe tupu🙌🏾
Yaksun akasema basi angalia na utazame vizuri kama huyu mwanamke namuweza au simuweziii😳😳 , Yaksun akamvuta irene karibu yake 🙌🏾
Irene yeye alibaki amebutwa kusikia Yaksun anaongea English tena imenyooka sio kabisa ya Chuo cha udeleva hapanaa🙄🙌🙌 irene alijikuta anagombana na mawazo yake😅😅
Tukio ambalo hakuna aliekutegemea hata huyo Irene mwenyewe alishangaa amevutwa na Yaksun moja kwa moja Yaksun akaitulisha midomo yake juu ya Lips za Irene ,,,Hee🙄🙄🙄Irene ilikuwa gafla sanaa ,Yaksun akaanza kunyonya ndimi 🤗🤗ni sec tu hata irene akili haikuweza kufanya kazi kisha akamuachia akamgeukia Lawrence akamuona anatetemeka kwa hasira ,Yaksun akamwambia Umeona umeona namuweza kwahiyo kaa mbali nae,
Lawrence alikuwa na hasiraaa yaan Mpenzi wake ananyonywa mate mbele yakeeee😳😳🤨 ,alisogea huku mkono kaandaa kurusha ngumii ,Kabla hata hajarusha Ngumi Yaksun akamsukuma kule akapepesuka manusura aanguke mzungu wa watu🤣🤣🤣
Irene akamuuliza we Yaksun umefanya niniii😔😔???” Moyo wa iren ulikuwa unakwenda mbio kwa busu la Yaksun🙌🏾 na ilichukua sec kadhaa tu akaachiwa lakini aliona kama Yaksun alitumia saa zima kuchezea ndimi yake🤭🤭, nguvu hata za kumtetea Lawrence alikosa mate ya Yaksun yalikutana mengi mdomoni kwake yakafanya akawa mzito hata kufikiria kwa wakati huo 🤥🤥
Alikuwa anameza tu mate mfululizo ubaridi ukamuingia akajikuta hawezi kabisa kumkatalia Yaksun wakati anampeleka kwenye gari😥😥 ,Lawrence akabaki anaita anamuita irene itaa ,Yaksun akaondoa gari kwa kasi sana 🙌🏾,wakati wanaondoka Irene aligeuza macho kutazama alipo Lawrence kwa mbali sana akamuona mynda anasogea alipo Lawrence😥😥🧐
Akageuza macho akamtazama Yaksun😒😒 ,,Yale mawazo yoooote ya kumuhusu Lawrence na upuuzi wake iren yalipotea😧😧 ,akili yake ilikuwa inakumbuka vile Yaksun alimvuta akamwambia Lawrence ngoja nikuoneshe kwamba namuweza akampa busu😘🥰🥰 Mwili wa irene akajikuta vipele vya kusisimka vimetokaaa mwili wotee 😅😅😅🤗
Akajikumbatia ili kupunguza ule msisimko😊😊 ,Yaksun akamuuliza unahisi baridi madam😒 , irene akamtazama jicho kaliii yaan anamuita madam tena kwa heshima halafu kitu alichomfanyia pale anajisahaulisha auu😩😩😩 Yaksun akapotezea tu 🙌🏾
Yaksun alipeleka gari mpaka nyumbani kwake, baada ya kusimamisha gari ndio akamgeukia Irene akamwambia samahani naomba nivae then nikupeleke nyumbani kwenu siwezi kwenda hivii🤔🤔🤔
Irene akamtazama kwa makini sanaa🤔🤔 jinsi Yaksun alivyokua anaongea sio kabisa na yule aliemfanyia kituko dakika chache nyuma🤔🤔🤔
Wakati Yaksun anataka kushuka irene akamshika mkono “ah yak…..”Yaksun alipo mtazama iren akajishtukia akaachia haraka haraka mkono wa Yaksun na maneno yakaishia hapo🤭🤭 ,hawana mazoea hayo 🙈
Yaksun akafunga mlango wa gari akarudi kuket kwenye siti yake akamwambia “samahani kwa kile kilichotokea pale madam sikupanga ila kwakua ulinipigia simu hali yako sikuona kama ni nzuri na pia samahani kwa yale maneno niliyokutamkia mwanzo🙌🏾 ,huenda ulinipigia simu ukiamini naweza kutoa msaada kisha nikakuangusha so sorry 🙏 ,Wacha nikavae nikupeleke nyumbani 😒😒”
Maneno ya Yaksun kidogo yalifanya irene atabasam na jinsi alivyoongea kwa upendo 🥰🥰,Irene akamuuliza “kwahiyo ulikuwa haupo nyumbani kwani hadi yaan nama.. mmh et nguo🤔🤔..” irene alikuwa anashindwa aweke vipi swali lake likae sawa mana akili yake ilikuwa imevamiwa na ka kitu wanaita wivu 🤗🤗🤗 hapo akili yake ilikuwa inamwambia huenda alikuwa na mwanamke wa mtu huyu kakurupushwa 😅😅😅
Yaksun akajitazama alivyo akasema “sorry simu yako ilinichanganya sana hata yaan daah nimejua kama sijavaa baada ya kukuona upo salama😒😒 ”
Irene akashangaa yaan yeye ndo kamchanganya hadi atoke hivyoo akamwambia “serious Yaksun its mee🤨🤥??”
Yaksun akatabasam🤗🤗 akamwambia “Ngoja basi nikavae mamaa uwahi nyumbani 😬” mmh irene akamuuliza “kwahiyo unaniacha hapa😔😔??”
“Hakuna tatizo usalama asilimia zote so relax okay🤗”
Mmh Irene akili yake ikamwambia huyu ana demu wake huko ndani hataki kumuingiza yaan usiku na giza et abaki ndani ya gari😅😅😅akamuita haraka huku anashuka mbio mbio 😂😂😂
Akamwambia” Yaksun mie naogopa twende wote tu huko ndani🤭🤭” akaongea kwa sauti ya kudeka ashasahau tukio alilo pigwa na bwana ake kabisa😅😅😅kaanza na kujibebisha kwa bebe za watu🤣🤣
Yaksun akasema ooh sawa haina shida😆 , Akamtanguliza mpaka Geto😒😒,chumba kilikuwa kimoja tu tena mitaa ya Kiswahili 😷,Chumba cha mwanaume kimepangiliwa hatari sio kama vyumba vya masela 😅😅,Kuna Bonge wa Bedsofa inawaka taa pembeni sofa moja la watu wawil ,Frij ndogo ya milango miwili Meza na jiko la ges plate mbili M_tv mkubwaa showcase ya kijanja ,Chini kuna Zulia ukikanyaga kama unataka kuzama vile 😅😅😅
Kuta zilikuwa na picha nyingi nyingi za Yaksun zingine za familia , Mwanga ulikuwa hafifu lakini unaona vizuri sana chumba kilivyo kizurii🥰🥰🤗🤗
Irene ilikuwa kazi yake kukagua tu chumba vyenye kinanukia sasa khaa yaan kamshinda hadi yeye wa kike🤗🤗🤗
Yaksun akachukua nguo zake akamwambia “nisubiri nichange nguo basi 🤔🤔”
Inaendelea……