USIROGWE UKAONDOKA NYUMBANI NA KWENDA USIPOPAJUA KWA KIGEZO CHA KUTAFUTA MAISHA
SEHEMU YA NNE
Ilipoishia,
Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani,,,,,, mzee usiombe yakukute
Endelea,
Tukamaliza UE, chuo kikafungwa watu wakasepa zao makwao, wengine kwenye mikoa waliyoomba field, mzee mzima nipo bado sina muelekeo, Mfukoni sina hata coin, Daah ntafanyaje sasa, ila uzuri ni kuwa niliomba field makampuni mbali mbali ya hapo hapo Dar, Mungu saidia nikapata kampuni mmoja maeneo ya Temeke, Fine ila sasa nauli ya kwenda huko napataje, ntaishi wapi nitakula nini, ukisikia mtihani ndo huo sasa.
Nakumbuka siku hiyo nipo maeneo ya chuoni kule uwanjani nimekaa chini ya mti nna mzigo wa mawazo, mara nikapata wazo, pale Pugu madogo wa advance si bado wapo, kwanini nisiwe naenda kuwapigia pindi usiku? Sitakosa hela ya kuishi, nikaona ni wazo zuri, ila mziki unakuja nauli sasa natoa wapi, nikapata wazo hivi Frank alishamaliza hela yangu kweli? Hela zake ndogo ndogo mpaka niiikashindwa kujua kama kanimaliza au laa, banaee nikanyanyua simu nikamuendea hewani, nikamchana live kuwa hela yote nimempa jamaa wa pc (uzuri na yeye alikuwa anajua nimeiibiwa PC ya watu), basi nikamwambia anitumie hela maana sina hata ya kula, kweli mara nikasikia triiiiii, tigo imedhibitisha umepokea elf kumi kutoka kwa Frank, nikasema poa.
Ilikuwa kwenye saa nne hivi asubuhi nikapanda room (ufunguo nilikuwa nao), nikachkua begi nikaweka nguo zangu kadhaa nikasepa huyoo mpaka Ubungo, nikadandia gari ya Goms, niikafika Goms kama saa saba hivi, nikazuga pale mpaka kama saa kumi hivi nikadandia gari mpaka shule.
Nikapita nikaanza kuwatangazia madogo wa advance kuwa jioni kutakuwa na pindi la hesabu na physics, topic elfu 3 , kwa vile baadhi ya madogo walikuwa wananijua bado hivyo sikupata shida, wakajioganize nikawaambia nitarudi saa moja tuanze.
Basi saa moja nikarudi, nikakuta darasa lina madogo kama kumi hivi wa physics, nikaanza wakata pindi pale, ila nikaanza na intro maana nilikuwa sijajiandaa, basi nikamaliza wakaingia wa hesabu, kidogo walikuwa wengi, basi nikakata pindi hadi kama saa nne hivi, nikajivuta mapinduzi 3 nikatia mbonji pale mpaka asubuhi, kulipo kucha nikagonga uji na mandazi ya mama Mahinda pale nikasepa nikadandia gari huyoo mpaka Temeke nikaenda kuripoti field.
Basi ndo ikawa ratiba yangu hiyo, usiku nagonga pindi asubuhi nasepa kazini, uzuri kule field msosi wa mchana unagonga huko huko, mambo kidogo yakawa byeee, Mungu saidia nikamaliza field vizuri, matokeo yakatoka sina sap nikasema alhamdulilahi rabila lamini.
Basi chuo kikafunguliwa kuanza mwaka wa pili, ila ikaibuka kipembembe nyingine, kwamba mpaka ulipe ada uende na risiti ndo uruhusiwe kusain boom (maana mimi niilikuwa napata bumu 80%, kwaiyo kuna pasenti natakiwa nilipie ada), Daah sasa itakuwaje na sisi tunategemea tupate boom ndo litusaidie kulipia ada, huu nao ukawa mtiti mwingine.
Basi tukaenda pale block O ndo zinapatkana zile karatasi za risiti, ukishaipata unaenda na risiti basi wanakugongea muhuri ile karatasi halafu unaenda kwenye office ya loan unawaonesha ndo wanakuruhusu kusain boom, Sasa nilikuwa na mshikaji wangu kidosho, tukachukua zile karatasi, tukachukua na karatasi yenye muhuri basi tukaenda mpaka Riverside kwa wachonga mihuri, tukamuonesha ule muhuri akasema buku kumi kuutengeneza , tukabagain nae mpaka akakubalii buku tano, chap akatutengenezea, tukajaza zile karatasi tukaziigonga muhuri tukasepa haaoo hadi chuo, tukaunga mstari pale ofisi ya mikopo ila kiroho kinadunda, nikaacha kidosho atangulie kwanza, mara kidosho akazama, akakaa weee mara akatoka akaninyooshea dole, yaani safi, ikafika zamu yangu nikazama ndichi, basi nikawaonesha pale namimi nikasaini nikasema imetoka hiyo ikirudi pancha
Nikapanda paka room, kufika nikakuta kuna mabegi tu kwamba kuna watu wameshafika lakini hawapo pale, basi wazo likaniijia ukijumliisha na machungu ya kuibiwa pc, nikafungua begi moja la mgongoni nikakuta Dell mpya, nikaichukua nikafunga begi ile nataka kutoka nikaskia jamaa wanakuja, Daah hii balaa sasa, nikabaki na pc mkononi huku natetemeka, nahisi haja kubwa na ndogo zinakuja kwa mpigo, jamaa wamesha karibia mlango
SEHEMU YA TANO
(Kabla ya kuendelea niweke sawa kitu hapa, ni kuwa kabla hatujafunga chuo tulienda kuongea na waden, tulikuwa kama wa nne hivi wanaroom, tukaongea na wadeni ili tukirudi mwaka wa pili tuendelee kukaa room yetu pale pale, basi wadeni akasema atatupa vitanda viwili yaan double kwaiyo kila kitanda anataka laki mbili, basi tukakubaliana pale jamaa watoe alafu boom likija toka tunarudishiana, kwaiyo room yetu mwaka uliofuata ilibaki ileile ila wakachanganywa badae madogo wa first year)
Endelea,
Nikiwa bado nimesimama nawaza cha kufanya wazo likanijia, nikapita mlango wa kibarazani (baadhi ya room kwenye yale mahall zina vibaraza), nikatokea kibarazani, wazo jingine likanijia, nikashika zile kingo za kibaraza nikabembea nikarukia kibaraza cha room nyingine, Yaani hata sijui ule ujasiri nlitoa wapi maana inatisha sana, fikiri floor ya 11, ukiangalia chini unaona watu wadogo, mzeee wacha!!!!
Basi nikafungua mlango wa baraza wa ile room, Mungu saidia nikakuta hakuna mtu kwenye ile room, nikapanda juu ya meza nikaiweka ile pc juu ya kabati, nikashuka kucheki mlango upo wazi, nikatoka nje nikaona mlango wa room yetu maana ni majirani nikapiga hesabu, nikaona ngoja niingie room, nikafungua mlango nikaingia, nikakuta kumbe ni mshikaji mmoja kaja na demu wake kumuonesha room, basi nikawasalimia pale, nikamtaniatania shemu pale, Jamaa akaniuliza ndo umeingia nikamwambia ndio, huku najifanya napanga panga vitu vyangu basi nikawaaga pale nikamwacha jamaa na demu wake, kilichoendelea mimi sijui.
Basi nikashuka paka Kariakoo (kuna sehemu pale chini kunauzwa vitu panaitwa kariakoo) nikanunua juice na keki nikatafuta sehemu kwenye kivuli nikakaa nikala huku nawaza kwanza jamaa akigundua pc yake haipo itakuwaje, pili jinsi ya kwenda kuichukua kwenue ile room maana sina mazoea sana ya kuingia ile room.
Basi niikamaliza pale nikatoka nikashuka Coet kwenda kucheki cheki ratiba ya vipindi na matangazo, nikapata wazo niende kutembea Mabibo basi nikapiga zangu shatle pori (kutembea kwa miguu) kuelekea Mabibo yote ni kupoteza muda ili baadae nirudi room.
Basi nikazuga zuga Mabibo kule, jioni nikageuza zangu campas, kufika room nakuta jamaa wananisubiri kama kuku aliepigwa na jua sasa kashikwa na kiu balaa, Basi ile naingia tu nakumbana na swali toka kwa jamaa mmoja, Oya Akili sina umechukua PC yangu kwenye begi? Basi kwanza nikarilax halafu nikajibu kwa utani “imeshaenda hiyoo” , Jamaa akanisihi niache utani niwe serious, basi nikamwambia sijachkua kwa kweli, maana nilikuja mchana nikamkuta flani na demu wake basi nikasepa sahivi ndio narudi.
Basi nikamwona jamaa machozi yanamlenga, anatafuta PC hadi chini ya mto kana kwamba kaiweka huko, Basi bana gumzo likawa ndo hilo pc imeibiwa pc imeibiwa, tukakaa sana pale room tukijadili jinsi ya kuipata, jamaa akaahidi kama hataiona mpaka kesho asubuhi basi ataenda kwa mganga Bagamoyo, kweli tukampa support tena mimi ndo nakazia nikijifanya nna machungu ya kuibiwa PC na mimi, basi tukatawanyika pale kwenda cafteriia kutafuta menyu.
Kwenye saa tatu hivi nikaenda kwenye ile room niliyoweka PC, nikagonga nikaingia nikakuta kuna mshikaji kalala, nikajifanya namuulizia mshkaji flani hivi, jamaa akasema hajarudi kula bado, basi nikasema ngoja nimsubiri huku najifanya nasikiliza bongo fleva za zamanii zilizokuwa zinapiga kwenye PC pale mezani, jamaa akaendelea kulala tena kageukia ukutani sijui alikuwa kapiga mtungi, basi nikazuga pale nikapata chance nikapanda juu nikaivuta ile pc alafu nikarud nikakaa, nikatoa begi mgongoni nikaiweka halafu nikatulia
Basi nikamuaga jamaa nikamwambia ntarudi badae, basi nikatoka nikaenda kushukia ngazi za mwisho kabisa wa jengo ili kupunguza chance ya kukutana na wanaroom.
Basi nikashuka chini nikakamata shortcut ya kwenda Msewe, maana jamaangu kidosho alikuwa ameamua kupanga mtaanii, basi nikafika kwa kidosho pale nikakuta kapika ugali tukala, nikamwambia kesho kuna sehemu naenda sasa naacha begi langu pale nitalipitia nikienda, akasema poa.
Nikarudi zangu chuo, tukalala kukakucha asubuhi PC haijapatikana, Kweli jamaa akajiandaa huyoo Bagamoyo kwa bibi, mi nikajua ni biti tu ili kutia woga kumbe mshikaji kaenda kweli, Mida ya mchana akarudi akasema bibi kasema amesha mwona aliyechukua, ni wa humuhumu ndani kwahiyo kasema kesho wote tuende kwake, tukasema poa
Kesho kweli wote tukajiandaa haoo mpaka kwa bibi, tukafika tukakuta bibi ana mtu mwingine anamuhudumia hivyo tukaambiwa tusubirii nje kwenye jamvi, tukakaa pale wee, ila mimi moyoni Amani sina kabisa, sema najilazimisha tu nionekane nipo sawa, yaani ningepimwa presure pale nadhani ingekuwa juu karibu na kufa, mwisho tukaitwa tukaingiia, kwa vile chumba ni kidogo halafu tupo kama nane hivi basi tukajipanga chini kwa msitari,
Bibi kavaa kaniki yake, kajifunga na mavitambaa mekundu, kuna katoto ka kike ndo kinatafsiri yale Bibi anayosema maana sisi hatuelewii, Basi bibi akaanza na bonge la biti, halafu kila akiongea ananiangalia mimi machoni, basi macho yakigongana mi naangalia chini, basi daah yaan najiskia huku chini nimetota kabisa kwa hofu na woga, Bibi akaanza kuchoma ubani, mara akapandisha mashetani, akaanza kusema sasa, kwamba wazee wameshamwona aliechukua mali ya watu, lakini wazee wameona huruma wameamua kumpa huyo mtu nafasi, airudishe hiyo mali kwa mwenyewe, wazee wao wanajua kufunga tu, kufungua hawajuii kwaiyo asiije akalaumu mtu, wazee wametoa siku tatu hiyo Mali ipatikane (yeye anaita mali sijui hawezi kusema laptop).
Basi bibi akamaliza kutoa maneno yake pale huku yakiitafsiriiwa na kale katoto, basi akachukua kibuyu chake ambacho muda wote kilikuwa kinafuka moshi, akaanza kumpitishia kila mtu, anamzungushia kichwani huku anasema maneno yake, alipofika kwangu akanata kwanza, akatia pozi, watu wote kimya, mwili nikahisi kuparalize, nikasema enheee ukisikia kimbembe ndo leo, Basi nikajikaza mtoto wa kiume, bibi bado kapozi kwangu, watu wote wananikodolea mimi kuona ni nini kitatokea
SEHEMU YA SITA
Nikiwa na mimi nimeduwaa sijui nini kitatokea, mara nikaona bibi akanivuka akaendelea kwa mwingine nikashusha pumzi kwanza maana haikuwa poa, Bibi akamaliza zoezi lake akarudi akakaa kwenye kiti chake, akaanza kuongea kwa Kiswahili sasa, kwamba kama tulivyosikia wazee walivyosema kuwa wao wameshamjua aliyechukua mali, kwahiyo ni bora airudishe tu, na tena akasisitiza kuwa yeye anajua kufunga tu kufungua hawezi kwahiyo anatoa siku tatu mali iwe imerudi kwa mwenyewe.
Akamwambia jamaa kwamba aende ila ikipita siku tatu hajaona mali yake basi arudi, bibi atampa dawa na maelekezo ya kufanya.
Basi tukaaga pale tukaondoka kurudi chuo, kwenye gari nna mawazo tu, Sauti moja inaniambia nikairudishe PC ya watu, nyingine inaniambia acha woga wewe kwani uliivyoibiwa ya kwako ulirudishiwa, Basi bana nikaziacha hizo sauti zishindane zenyewe atakaeshinda ataniambia, mi nikapitiwa na usingizi kwenye daladala nikapiga mbonji
Nakuja kushtuliwa mawasiliano, daah basi tukashuka tukapiga shortcut pale tukatokea chuo, nikafika room siku hiyo nikapiga mbonji balaa.
Basi bana kesho yake nikatia maguu paka kwa kidosho nikachkue begi langu ambalo ndo lina ile pc, nia na madhumuni nije niirudishe PC ya watu sitaki matatizo mie, Nikafika kwa kidosho nikachukua begi langu nikaanza safari kurudi chuo, ila ikabidi nizungukie Ubungo mataa maana ile short cut ya Msewe kuna mto umejaa baada ya mvua kunyesha, Haya ile nimefika mataa sauti ya kunikataza nisirudishe sijui ikaibukia wapi, ikaja na nguvu balaa ikaniambia acha ubwege wewe, kuwa na akili basi hata kidogo, yaani wewe huna Pc, alafu ushatoa laki sita kumlipa mtu PC, halafu leo unarudisha hii, Bwege kweli wewe, Daah basi pale pale nikabadili mawazo, nikadandia daladala huyoo mpaka DIT, kuna mwanangu pale tulipiga nae Pugu, nia nikifika nimwachie mwamba mzigo ule anisaidie kuusukuma (kuuza),
Basi kweli nikafika nikamkuta mwamba, tukaenda room kwake, mimi nikajifanya kama nimeenda kumtembelea tu, basi tukafika room , nikatoa PC yangu (kumbuka ndo naitoa kwa mara ya kwanza, kwahiyo sijui hata password yake) nikawaza itakuwaje sasa kwenye password, jamaa si atashtukia si yangu nikianza kuhangaika na password, nikapiga moyo konde, nikaiwasha mara lahauala Pc haina password, nikajiona kama Sterling vile nacheza movie.
Basi nikajifanya naitumia pale huku napanga jinsi ya ku muingia jamaa, Basi sijui ni nini kilitokea ila ghafla nikaona jamaa kaanza kuishobokea pc yangu, anaisifia kinyama, mara ooh portable, mara ooh ukiwa nayo mademu watakushobokea, mara akasema kama vipi anipe ile yake aniongezee na hela kidogo, nikamuuliza sh ngapi akasema laki mbilii, nikasema ndogo ( ila kimoyo moyo nasema leta hela hiyo wewe), Basi jamaa akaniomba sana, basi kishingo upande nikajifanya
nimekubali, basi jamaa Akanipa ya kwake HP nzuri tu, akanihesabia na kibunda nikasema fresh, tukafuta futa vitu pale na yeye akahamisha hamisha vitu vyake pale basi nikasepa zangu
Basi bana, zikapita siku tatu zikakata PC haijarudi, jamaa akarudi kwa bibi, akapewa dawa moja kama majivu hivi akaambiwa hiyo kila mtu ajiipake kwenye paji la uso kama njia ya msalaba vile, nyingine ni majani ayaweke juu ya mlango, yule aliyechukua labda atafute mlango wake awe anapita ila asilogwe akapita chini ya ile dawa
Basi akaja akaleta mrejesho na dawa pale tukapaka, na nyingine akaweka juu ya mlango basi tukakaa kusubiri matokeo, ila mimi nikawa nimeshajitoa muhanga liwalo na liwe siogopi mtu wala kitu, nikajipa moyo uchawi hauendi kwa mentally, Basi siku ya kwanza ikapita hola, ya pili mara wiki mara mwezi ndo ikawa imeisha hivyo hakuna chochote kilichotokea, maisha yakaendelea na jamaa akajipanga tu kutafuta pc nyingine maana hamna jinsi.
Basi shule ikaendelea shule ngumu kishenzi, mi najifanyaga mzee wa msuli tembo lakini pale nilinyoosha mikono, Ndo nikapata jibu kwanini Frank alikuwa anapataga yale matokeo (ila pale Coet nyoko sana, sjui wanakomoa wale)
Basi tukapiga test, tukamaliza UE tukafunga shule semista imeisha hiyoo, Nikabeba begi langu huyoo kijijini maana nlivyokuwa nimewamis, Basi nafika kijijini naona kumebadilika balaa, madogo niliacha wadogo saivi wakubwa, Nikakuta dogo kajenga room pale home kavuta mke eti nae kaoa, nikacheka sana, Haya maisha bana.
Basi nikakaa pale home asubuhi wanaondoka wote wananiacha home peke yangu, Sasa kuna katoto ka diwani pale tulisoma nacho msingi sema nlikaacha kama madarasa matatu hivi kalikuwa kadogo, sasa nimekuta mtoto kapevuka huyo , yaani pisi kali kwelikweli, Basi kidume kwa mara ya kwanza toka nizaliwe na mimi nikashuka nondo, mtoto akanielewa basi akawa anakuja homu, Siku ya kwanza kaja home niko peke yangu mzee nikala mzigo kwa mara ya kwanza, sitaisahau hii siku maana ili nitesa sana (nitakuja kuelezea huko mbeleni)
Basi ikawa ndo mchezo wetu, yaani kwa zile wiki mbili nlizokaa homu niliibutua sana ile mbususu
SEHEMU YA SABA
Basi nikakaa pale nyumbani takribani wiki mbili, hatimae muda wa kurudi chuo ukafika, nikapaki kila kilicho changu nikadandia chuma huyoo kurudi Dar, ila moyoni sijaridhika kabisa kumuacha mtoto Happy maana alikuwa ameshaniteka akili, nikiwa kwenye gari namuwaza yeye hasa tulipokuwa tunafanya yetu, kwa vile nlichukua namba zake basi tukawa tunachati karibu safari nzima.
Tuliahidiana mengi, tukaahidiana kuoana, pia akasema atafanya mpango aje Dar maana anti yake anakaa Dar.
Basi nikafika chuo, shule ikaanza kama kawa inaanza kama haitaki vile ila ngoja ichanganye ndo utaimba haleluya, Basi muda mwingi nikawa natumia kuchat na Happy, sometimes hata nikiwa darasani, usiku ndo usiseme tulikuwa tunaongea mpaka masikio yanauma.
Nikawa kila nikikaa nawaza tu ile siku ya kwanza tulivyofanya, yaani niliona dunia imebadilika nikaingia ulimwengu mwingine kabisa, daah jamani raha sana.
Sasa nikawa hata nikiwa nasoma mawazo hayo yananijia najikuta nimeacha kusoma naanza kuwaza hayo maujinga, Nikawa sasa kila nikimwona msichana mwili unabadilika, nahisi joto, mawazo yananijia najikuta namvua nguo kimawazo na kuanza kufanya nae kimawazo halafu napata raha eti.
Basi nikawa na tabia naenda kukaa kwenye kimbweta ambacho kwa mbele kuna wadada waliovaa sketi fupi, halafu naanza kula chabo kiaina, najifanya nasoma kumbe nakula chabo, natengeneza mawazo ya kimapenzi tu kichwani.
Hii hali ikanisumbua sana, nikajikuta natafuta video za ngono naanza kutazama basi zinanisisimua kichizi, mwisho nikapata solution, nikaanza kujichua, Yaani hizi tabia sikuwa nazo ila siku nilipokutana na Happy ndo imeharibu kila kitu, Yaani muda mwingine natoroka darasani naenda chooni kujichua, ikawa balaa mzee.
Nikawa na video zangu za ngono kwenye Pc, basi natoroka naenda chooni, nafunga mlango nawasha pc, nachomeka ear fone, naangalia video za ngono halafu naanza kujichua.
Daah, basi ndo ikawa tabia yangu, kujichua kwa kwenda mbele, kwa siku naweza jichua mara tatu mara nne, Sometimes nakaa nawaza, Happy umeniletea nini hiki, mbona ntajiharibu sasa, Nikiwaza nitafute demu ndo siwezi maana naanzaje, Happy mwenyewe nlimuotea sababu ni wa bushi, hawa wa chips mayai nawezaje.
Sasa siku nikakaa nikawaza sana, hivi mimi Akili sina nnavyojichua hivi, si baadae nitakuwa hanisi, nitakuwa siwez tena kazi, sasa hata nikija kuwa na maisha mazuri halafu kazi hamna ndo itakuwa nini sasa.
Nikasema lazima niache hii tabia, ila ntaachaje sasa, Basi bana katika stori stori na majamaa wakagusia ishu za madada poa, wakataja maeneo sjui Kimboka, sijui wapi, Nikasema sasa hapa ni bora nijichanganye huko kuliko kuendelea na hii tabia yangu.
Nakumbuka siku hiyo nikajikoki naenda Kimboka, ila nikawaza nikionekana huko si itakuwa story ya town, nikasema poa, Ikafika usiku kama saa tatu hivi, nikashuka Ubungo nikanunua kofia, nikatinga kofia yangu nikadandia daladala huyoo hadi Buguruni, Nikakuta kumechangamka balaa kama sio usiku vile.
Basi nikatembea Hadi hapo sehemu, Ebwanaeeee asikwambie mtu, wadada kama wote, ni mapaja tu yana metameta, basi nikasimama zangu pembeni nikawa naangalia, yaani ni kujichagulia type unayotaka, wanene,wembamba, weusi, weupe, watoto, wamama yaan ni wewe tu na roho yako, paka albino wapo mzee.
Basi nikatulia naona machizi wanajiokotea tu wanazama huko ndani ndani, nikajisemea kumbe ni kweli sodoma ipo, Basi nikaona dada mmoja kamkwida jamaa anataka hela yake, jamaa akampiga bonge la bao alafu akamwambia usinizoee, jamaa akasepa, basi huruma ikaniingia, nikamfata yule dada nikamuuliza ni nini kwani, akasema jamaa wameenda nae short time halafu kamdhulumu hela yake, nikamuuliza sh ngapi akasema buku tatu, basi nikatoa buku tano nikampa, alifurahi sana, akaniona nna roho nzuri balaa.
Basi akanipeleka kule ndani ya baa akanitafutia kiti nikakaa nikaagiza soda, akasema nikae pale nisiondoke anakuja, Basi akawa anaenda anakaa halafu anakuja, tunapiga stori kidogo halafu anaondoka tena, ikawa ndo hivyo, akaniambia nimsubiri akimaliza tuondoke wote tukalale, nikasema sawa, kimoyo moyo nasema Hivi akili sina ndo mimi nimekuwa hivi kweli??
Haya bana, ilipofika kama saa saba hivi usiku akaja akanichukua twende zetu, Basi tukatoka akaita bodaboda akatupeleka huko ndani ndani kumbe ndo kwake, Tukaingia ndani ana kiitanda kameza cha tv na vitu vidogo vidogo, Basi akawasha tv pale tukawa tunaangalia huku tunapiga stori stori.
Akaniambia yeye anaitwa Jane, akanipa historia yake pale, Basi tuliongea mengi.
Sasa ikafika muda wa kulala, bana mtoto akaanza mambo, haya mambo nlikuwa nayaona kwenye zile video zangu tu sasa leo nakutana nayo live live mbona balaa, Mtoto alinilegeza balaa, kiufupi anajua Mambo, Basi mtoto akataka nitumbukize, sijui akili zilinijia wapi nikakumbuka kondom, akasema pale ndani hakuna kondom, nikasema bila kondom mi sifanyi, akanilazimisha balaa, yaani ikawa mkuku mkuku pale ndani, ye anataka hivyo hivyo mi nataka kondom, basi kukuru kakara kama nusu saa nzima, mwisho akachoka, nikaona kainuka kafungua mlango akaondoka.
Nikabaki nawaza hivi mimi nafanya nini, nimekuja kuwaje paka nakuja kulala kwa makahaba, Mara mlango ukafunguliwa akaingia, mkononi kashikilia pakti za kondom, Nikasema hapo sawa, Basi nikala mzigo pale vizuuuuri, mtoto kajaa ufundi balaa, Basi tukalala mpaka asubuhi, Asubuhi wanakuja rafiki zake pale, ni wale nilikuwa nawaona pale wanajiuza, akawa anawatambulisha kuwa mi ni shemeji yao, basi sawa, nikakaa mpaka mchana tukala ugali fresh, Nikaondoka zangu kurudi chuo.
Itaendelea