NILIVYOTUMIKISHWA KUFANYA MAPEMZI NA MBWA WA BOSS
Episode 26
Tulipofanikiwa tu kuwatoroka wale walinzi usiku ule kule msituni, mimi na Regina tulitokomea ndani ndani kabisa ya msitu kwenye giza totoro kiasi kwamba tulitembea kwa kupapasa huku tukiwa tumeshikana mikono kwa woga, mara tukasikia mchakacho gizani tena ulikuwa ni mchakacho wa kitu kinachotembea kwa kishindo 😳 nikamkumbatia da Regina na kumnong’oneza huku nikihema sana “Da Regi tusimame, tusipokuwa makini tutaliwa na wanyama wakali tafadhali tusiendelee kutembea” Nilimwambia Da Regi huku machozi yakinitoka.😭
“Basi hapa kwa usalama wetu tupande juu ya mti tulale juu ya mti mpaka pakuche kwanza” aliniambia Da Regina, basi tukapapa mti mmoja mrefu kidogo, Da Regi akawa wakwanza kupanda kisha na mimi nikawa namfuata nyuma yake, tulipanda juu kabisa ya mti wenye matawi mengi hapo tukakaa juu ya mti tukinong’onezana. “Mdogo wangu Radhia angalia kuwa makini usije ukapitiwa na usingizi, kumbuka hapa tupo juu ya mti ukijisahau tu kidogo unaangukia chini” alininong’oneza Da Regina “Hata usijali dada wala siwezi kulala kwasababu nina hamu kubwa sana tutoke kwenye huu msitu” Nilimwambia.
“Tutatoka tu mdogo wangu, kama Mungu katoa pale kwenye lile jumba la mateso basi hata kwenye hili pori atatutoa tu, hawezi kutuacha tuangamie maana yeye ndiye aliyewavusha wana Israel katika bahari ya shamu hatoshindwa kabisa kututoa katika msitu huu tumuamini tu yeye” alinitia Moyo Da Reg, kuna muda tulilala usingizi wa mang’amu ng’amu huku tukishtuka shtuka kwasababu tulikuwa juu ya mti, muda huo hata tulikuwa hatujui ni saa ngapi, giza lilikuwa limetanda balaa huku chini ya mti ikisikika michakacho ya wanyama wakipita.
Episode 27
Hatimaye Nuru ikachomoza, mwanga hafifu wa porini ukatoka, kumaanisha kwamba tayari kulikuwa kumekucha “Mdogo wangu Radhia tushuke juu ya mti huu ndio muda wa kuendelea na safari” Alisema Da Rey, tukashuka juu ya mti na kuanza kutembea kwenye vichaka huku tukikata njia, tulihofia kwamba endapo tutatembea na njia basi tunaweza kukamatwa. Tulitembea umbali mrefu sana hata hatukujua ni wapi tunaelekea, mara tukasikia nyuma yetu “Wale paleee😳” tukishtuka na kuanza kukimbia mimi na Da Regina huku walinzi wa ile sehemu tuliyotoroka wakitukimbiza. Tulikimbia umbali mrefu sana hatimaye tukapotezana nao hapo sasa tukaanza kutembea, tulitembea wewe mpaka giza likaingia, ndipo tukafika sehemu kwa mbali kidogo tunaona watu wamekoka moto wanaota, huku wengine wakichoma nyama,, ” Mh Da Regina watakuwa ni kina nani wale usikute ni wale walinzi wameweka kambi ya kututafuta” Nilimwambia Da Rey, “Hapana sio wao kwani husiki wanaongea kikabila” kabla sijamjibu Da Rey mara tulimulikwa na mwanga mkubwa wa tochi mithili ya tochi za wawindaji, nilitetemeka sana kwa woga, ndio wale wale watu waka….
JE NINI KITAENDELEA?
IPI HATIMA YA RADHIA?
JE WATU WALIOKUTANA NAO USIKU HUO MSITUNI WANAWEZA KUWA MSAADA KWAO AU WATAWAONGEZEA MATATIZO?
Episode 28
“Mh Dah Regina tujufiche si unaona kule mbele kuna watu wamekoka moto wanachoma nyama pori, usikute ni wale walinzi wametutafuta wamechoka sasa wameamua kuweka kambi” Nilimwambia Da Regi. “Hapana sio wao kwani husiki wanaongea kikabila” aliniuliza Da Regina lakini kabla sijamjibu ghafla tulimulikwa na mwanga mkubwa wa tochi mithili ya tochi za wawindaji, nilitetemeka sana kwa woga, ndipo wale watu wakaanza kutusemesha kwa kilugha huku wakitufuata, mikoni mwao walibeba mikuki, napanga na mishale.
“Eee Mungu tunusuru na watu hawa ambao hata lugha zao hatuzielewi” niliomba kimoyomoyo huku watu wale wakitukaribia. “Kina dada mmetoka wapi usiku huu huku porini” aliuliza mmoja wao ambaye alionekana yeye anajua kiswahili ingawa ni kile kiswahili cha kilugha. “Acha tu kaka, tumetoka mbali sana na hata hatujui tunapoelekea, tulitekwa na kuletwa huku msitu ili tufanye biashara ya ngono na wanyama kisha waliotuteka wakawa wanatuchukua video na kwenda kuziuza nje ya nchi” Da Regina alimwambia yule kaka naye yule kaka akawa anawatafsiria wenzake kwa kilugha, walitikisa vichwa kwa masikitiko ishara ya kutuonea huruma sana.
Episode 29
“Basi sawa msijali mimi naitwa Clinton, sisi ni wawindaji wa wanyama pori, tutahakikisha mnalala salama na pia kesho tutawatoa hadi barabarani maana kwa usiku huu ni mbali sana” alisema kaka Clinton. Basi tukaongozana nao mpaka sehemu ile waliokoka moto, tukakaa chini wakatuchomea nyama tukala hadi kushiba, baadae wakatugawia makoti yao mazito ili tutandike chini tulale pale karibu na moto kusudi tusihisi baridi, basi tulilala mimi na Da Regina tukiwa tumeshiba sana, hakuna siku tuliyoshiba kama hiyo. “Radhia mdogo wangu tukifanikiwa kutoka kwenye huu msitu, tusiachane kwa muda ulioishi wewe umekuwa kama mdogo wangu, kama unakumbuka
Episode 30
niliwahi kukueleza kuwa mimi ni yatima sina baba wala mama, manyanyaso ya shangazi yangu ndio yalinifanya nikatafute kazi mjini lakini katika harakati za kutafuta kazi nikajikuta naangukia kwenye mikono ya hawa mafirauni, usije ukaniacha Radhia, sina pakwenda na sijui maisha ya huko uraiani yapoje😭” aliniambia dada Radhia huku machozi yakinitoka.
Wakati huo Clinton na wenzake walikuwa wanazunguka zunguka eneo lile kuwinda wanyama. “Usijal Dada Regi nitakuwa na wewe bega kwa bega tumuombe Mungu tu tufanikiwe kutoka” nilimwambia dada Rey.
Basi asubuhi ilifika, jua likachomoza, Clinton na wenzake wakatuambia tuondoke ili watusindikize mpaka barabarani. Tuliongozaza nao huku wakiwa wamebeba, mapanga, mikuki, mishale na wengine walibeba vitoweo. Tukiwa njiani tunatembea mara ghafla tukashtukia😳……
NINI TENA?
TAFADHALI: tumia sekunde chache kuandika “Mungu asante kwa afya yangu na ulinzi”
Kumbuka
watu wengi WANAKUFA
watu wengi wapo MOCHWARI
watu wengi
Watu wengi wanakufa kwa ajali hasa mwishoni mwa Mwaka.
Wengine wana chakula lakini hawawezi kula.
Wengine wanaweza kula lakini hawana chakula.
Mimi na wewe tuko na chakula na tunaweza kula na siku zinasonga, Acha utani tumia japo sekunde kusema AHSANTE MUNGU🙏🙏🙏🙏✋ kisha tukutane sehemu inayofuata…