TAFUTA HELA BROO
PART 11
Tulipoishia
“kwanini nisikupe kwani mimi sina hicho alichokuwa anakupa au?” alisema binti SMS iliyomfurahisha sana Rutu kwa kuwa alikuwa anampenda
“duuuh sikuamini”
“nakuja hapo nije nishuhudie ukimpigia na kumuambia kwamba humtaki tena” ilikuwa mtego mbaya kutoka kwa binti
Endelea nayo
“Unanipa mtihani sana Nsia ujue” alisema mtaalam
“basi hunipendi”
“ooh ok ok ok basi sawa nitamuambia sasa hivi kwanza”
“hapana nataka umwambie tukiwa wote”
“sawa”
Baadaye mida ya jioni jioni mtaalamu aliondoka, na kwenda mpaka kwa binti, ni kwamba alikuwa anampenda sana binti huyu aiseee, mapenzi ya kweli hayaharibiwi na chochote.
Rutu alifika kwa Nsia akamkuta Nsia ameketi sebuleni peke yake, macho kayaelekeza sehemu moja huku akiwa na mawazo ya hali ya juu. Huwezi amini Rutu aliingia mpaka akaketi lakini bado akili ya binti ilikuwa mbali sana
“wewe” alimuita mtaalam ndipo binti akashtuka sana na kumtazama kwa huruma “vipi unawaza nini mpenzi” alisema mtaalam na kumsogelea akaketi pembeni yake
“Rutu naona hata sifai kuwa na wewe maana najisikia vibaya sana”
“usikasirike kwa ulichokiona mchana binti, naomba unisamehe mimi sikujua kama itakuwa hivyo tafadhali”
“sio hv…..”
“nope tulia” alisema mtaalam huku akimshika binti mdomo na kumzuia asiendelee kuongea. Alitoa simu mfukoni na kumpigia Mahadia. “Hiki si ndicho unachokitaka?” aliuliza binti akatikisa kichwa kumaanisha hapana, kuna kingine
Mahadia alipokea simu “halo babyyyy” alianza kwa mbwembwe
“nooo Mahadia, sikiliza nikuambie kitu, kiukweli mimi sikupendi naomba kila mtu afuate mambo yake tafadhali niko na wewe kwa kujilazimisha tu sio kwa sababu ya mapenzi”
“jamani Rutu” alisema binti kwa uchungu “acha utani basi lakini”
“sio utani niko serious, and good bye” alisema mwamba na kukata simu.
“umeridhika sasa haya sogea hapa nikubusu” alisema mwamba na kumvuta binti kweli Nsia akamdondokea kifuani na kuanza kumbusu shavuni kwa hisia
“Rutu naamini unanipenda sana, sitokubali kukupoteza tena” alisema binti mara ghafla akaingia mzee na kuwakuta wameshikana, akashtuka
“tena!!!!!” aliongea kwa mshtuko maana alijua binti yake ameshaachana na kijana masikini kama yule
“shikamoo baba” alisema binti
“marahaba, kwanini wewe Lutu uko hapa?” aliuliza mzee
“samahani niko kwa sababu nampenda binti yako, baba nataka nimuoe Nsia”
“nini? Umuoe binti yangu?…..hahhaaaa…. wewe huna hata kitanda mtoto wangu aje kulala kwenye nyumba ya mama yako au?” alisema mzee kwa dharau
“baba tulia, mimi ninampenda Rutu na niko naye kwa ajili ya malengo, hata usipokubali anioe mimi ninampenda na atanioa tu mda wowote” alisema binti na kusimama kwa hasira.
Kwa hasira mzee alimpiga mtoto wake kibao na kumvuta ndani akamfungia chumbani halafu akatoka na panga, acha Rutu atoke speed ya ajabu, akakimbia mpaka nyumbani na kujilaza kitandani huku akisoma majibu ya message za Mahadia kwenye simu
“sawa Rutu nilijua tu ipo siku utaniambia maneno kama hayo” Rutu hakujibu chochote akiamini kwamba Mahadia sio type yake.
Baadaye alitoka nje na kwenda kutafuta chochote ambacho mama yake alikuwa amepika, alimkuta mama akiwa na hasira sana
“mama umepika?”
“Rutu nikuulize swali moja?” badala mama ajibu alichoulizwa alianza kumfokea mtoto wake
“niambie mama yangu” aliongea kwa huruma “kuna nini tena?”
“umeifanya hii nyumba yangu, guest au?” aliuliza mama kwa hasira
“hapana mama, kwanini” aligundua mshikaji kwamba kuna watu wameshapeleka taarifa kwamba mchana alikuwa na Mahadia ndani hapo
“toka hapa punguani mkubwa wewe, yaani ole wako nisikie tena, nitakutandika usijione umekuwa sana kwangu…. Haya kachukue chakula kabatini kule shenzi” alisema mama kwa hasira kali halafu mtaalam akaingia ndani na kuchukua chakula chake akaendelea kula.
Akiwa anakula iliingia SMS kutoka kwa Mahadia “Mume wangu jamani mbona unanifanya najisikia vibaya hivi sweetie” alisema binti.
Rutu aliitazama ile message bila kuijibu halafu akaanza kujuta “sasa nimemtongoza huyu binti wa nini?” alijiuliza na kutaka kumblock lakini akasita kidogo
Alisita kwa sababu alikumbuka namna alivyoumbuka kule kwa Nsia siku hiyo, hata hivyo muda ulivyopita alilala mpaka asubuhi ilivyofika tena.
Kule nyumbani kwa mzee Swai ndiyo aliamka na kutoka nje ya nyumba, alitaka kwenda chooni lakini alishangaa kusikia sauti ya mtoto wake akiwa anatapika sana pembeni mwa jiko lake ikabidi aende kushuhudia tatizo liko wapi
“Nsia” aliita kwa mshtuko na binti akageuka huku akizidi kupata kichefu chefu
“unaumwa?” aliuliza mzee
“hapana baba kichwa kinauma” alisema binti
“kichwa kinauma ndo utapike, sema unaumwa nini?” alisema mzee kwa hasira na kumsogelea zaidi binti
Nsia hakuweza kujibu chochote aliinuka na kujaribu kujizuia kutapika lakini kila alipojaribu bado kichefu chefu kilimrudia, akarudi chali na kuendelea kutapika tena bila kufahamu tatizo liko wapi.
Utu uzima dawa, mzee Swai alielewa kabisa kwamba binti yake tayari ana kitu kinachomsumbua tumboni na ndicho kilichokuwa kinasababisha ateseke, alimvuta na kumsimamisha kwa hasira
“Nsia una mimba?” alimuuliza kwa hasira binti yake
Nsia hakuweza kujibu chochote alibaki analia tu ndipo mzee akamvuta na kumlamba kibao “Nsia ninakuuliza una mimba?” aliuliza tena kwa mara pila.
Nsia alipiga kelele kwa maumivu makali ndipo mzee akamvutia ndani, “niambie hii mimba ni ya nani, la sivyo ninakuulia huku huku ndani shenzi wewe” mzee aliongea kwa hasira zaidi halafu akamketish kwenye kochi
Tatizo ni kwamba binti hata haelewi kama ni mimba kwa sababu ndiyo alikuwa mgeni kwenye suala zima la mahusiano.
“baba ni ya Bella” alisema binti kwa kuogopa na kuendelea kutetemeka katika mwili wake wote.
“Mungu wangu, Bella tena? Sio Rutu?” aliuliza mzee
“Rutu sijawahi kufanya naye chochote baba naomba …unisamehe” alisema mtoto wa kike ndipo mzee akachanganyikiwa ikabidi aketi chini huku akifura kwa hasira.
Alitoka nje na kwenda dukani akachukua vocha na kumpigia mtoto wake mkubwa aliyefahamika kwa jina la Ndumi
“baba shikamoo” alisema Ndumi
“marahaba hujambo?”
“sijambo baba vipi huko kwema?”
“sio kwema kabisa kijana wangu, ni aibu tele, mdogo wako ana mimba”
“Nsia ana mimba? Ya nani?” aliuliza kwa mshtuko
“ya yule Bella mtoto wa mzee Gauchi” alisema mzee
“Mungu wangu, sasa umeshampeleka kwa Bella huyo au unasubiri nini?”
“nimekupigia wewe mtoto wangu mkubwa ili uniambie nifanyeje”
“mzee mchukue binti mpeleke kwa mwaume huyo aliyempa mimba, kama akikataa ndiyo abaki hapo nyumbani yeye sio mtoto wa kwanza kupata mimba duniani bwana” alisema mtaalam
“sawa kijana nitafanya hivyo”
“sawa…..mambo mengine vipi lakini?”
Mzee alikata simu masuala ya kuulizana maswali mengine alikuwa hataki, alirudi nyumbani na kumkuta Nsia akiwa chumbani kwake bado akamuambia apange nguo zake zote ili ampeleke kwa Bella
Nsia alimtii baba yake akapanga vitu vyote na kuweka mabegi yake sawa halafu akamchukua na kuelekea kwa Bella. Alipofika kwa Bella hivi, Bella alikuwa na mafundi wakipiga bati kwenye nyumba yake, walishtuka kwanza
“baba shikamoo” Bella aliongea kwa wasiwasi………
JE ATAKUBALI MIMBA?
PART 12
“marahaba” alisema mzee na kuweka begi chini
Muda huo pale palijaa watu kibao na kuanza kusikiliza mambo ambayo yalikuwa yanaendelea, mafundi wenyewe walibaki wakishangaa,
Kijana nimekuja kwako hapa kukueleza kwamba binti yangu ana ujauzito na nilivyombana amedai kwamba ujauzito huu ni wa kwako, mimi siwezi kumlea mke wa mtu, hivyo nimekuletea mke wako uoe sasa…… nimemaliza” alisema mzee kwa step na kumuangalia mshkaji atarespond vipi
Bella kidogo alikuwa anajiamini akamgeukia binti na kumuuliza swali moja la msingi “Nsia, una uhakika hiyo mimba ni ya kwangu?”
“ndiyo ni ya kwako Bella” binti alijibu
“ok karibu sana nyumbani, jisikie upo nyumbani sasa” alisema mtaalam kwa hisia halafu akainama na kuchukua begi akalipeleka ndani kwake.
Mzee Swai hakuamini kama ingekuwa kazi rahisi kiasi hicho, alimkabidhi binti begi lingine naye akalipeleka ndani, halafu mzee akaangalia mlangoni mwa nyumba ile naye akaanza kulia kwa maumivu ya binti yake mmoja kugeuzwa mke wa mtu.
Mzee alijitahidi akarudi nyumbani akaenda akaketi kwenye kochi na kuanza kuwaza mambo mbalimbali kuhusiana na maisha alijitia moyo kwamba ni lazima siku moja angeondokewa na binti yake, hivyo aliamua kuingia jikoni peke yake na kujitengenezea chai yake mwenyewe
Baada ya dakika thelathini tu, habari zilimfikia Rutu kwamba Nsia amepelekwa kwa Bella bila hata mahari na hiyo ilikuwa imesababishwa na binti kunasa mimba ya mjeda huyo
“alikuwa na mimba???” aliuliza kwa mshtuko baada ya kuambiwa na paparazi mmoja kwamba binti huyo ameshapelekwa
“ndiyo, pole sana ndugu yangu” alisema paparazi huyo
Kwa hasira Rutu aliinuka kwenye kiti halafu akanyoosha na njia ya kwenda kwa Bella huku akitukana mengi matusi, alifika pale na kukuta mafundi tu wakiwa pale nje
“vipi ndugu zangu” aliuliza mtaalam, Nsia alikuwa ndani na Bella wakiongea ongea aliposikia sauti ya Rutu alishtuka kwanza
“safi kaka kwema” fundi mmoja alijibu salamu
“kwema kaka, vipi Bella nimemkuta?” aliuliza mtaalam na kushika kiuno
Bila wale watu kuelewa tatizo walimuambia kwamba mshikaji yupo ndani
Kwa kuwa alikuwa amepaniki alienda moja kwa moja hadi mlangoni na kugonga mlango kwa hasira “HODIIII” alisema kwa sauti ya ukali ndipo Bella alitoka kifua wazi na kumkuta mshkaji wake akiwa amefura pale
“vipi Rutu” aliuliza Bella
“Bella mshkaji wangu, wewe so mtu kabisa, ulijua kabisa kwamba huyu ni shemeji yako sasa vipi mbona umemchukua kirahisi hivyo”
“kwani wewe unatakaje?” aliuliza Bella kwa dharau
“usinijibu hivyo mseng** wewe” Rutu alisema na kuinama akachukua rungu lililokuwa hapo nje halafu akamsogelea mtaalam na kutaka kumpiga lakini Bella ni mwanajeshi kumbuka,
Aliushika mkono wa Rutu na kuusokota halafu akampiga kibao cha maana usoni, hadi Rutu akaona nyota nyota akadondoka kule
“nooooo usimpige” sauti ya Nsia ilisikika ndani, akainuka na kutoka nje kutazama, “Bella muache Rutu akae bana”
“unampenda si ndio?” alisema mtaalam kwa hasira “haya toka uende naye basi”
“sio hivyo, sasa unampiga mkaka wa watu kisa mimi jamani……” alisema na kumgeukia Rutu aliyekuwa anajiokota chini “wewe Rutu, nenda tu, mimi sikupendi wewe” alisema binti ndipo Rutu alipokata tamaa na kuondoka huku nafsi ikiwa inazidi kumuuma.
Bella na Nsia walishikana viuno na kuingia ndani ya nyumba ile halafu kimya kikatawala.
Mida ilisogea, ikazaba na kusambaa katika maeneo ya Afrika Mashariki giza lilitanda kila kona. Nsia alikuwa kitandani na Bella wakiwa wanakoboana, lakini vile vile Rutu alikuwa kitandani akilia sana.
Mama yake aliingia chumbani kwa mtaalam na kumkuta mwanaye akiwa analia sana
“mwanangu Rutu usilie sana najua unaumia kwa sababu Nsia kaolewa na Bella….. mwanangu ukitaka kupata mwanamke na ufurahi mapenzi, wewe ni mwanaume, jitahidi kutafuta hela sana”
“kweli mama nimeamini hicho kitu” alisema mtaalamu
“sikiliza mwanangu, yule binti aitwaye Mahadia ni msichana mzuri sana, na anakupenda sana, ana nidhamu yule binti sio mchezo, mimi ninafikiri ungempenda yeye achana na Hawa wachaga wanapenda hela mnooo” alisema mama
Rutu aliyasikiliza yale maneno yakamuingia akilini halafu akamuomba mama suala moja “Mama naomba uniache kidogo nifikirie kitu”
“sawa mwanangu chakula kipo jikoni kikiiva nitakuambia” alismeam mama na kutoka nje halafu akaendela kwenda kupika chakula chake kwa weledi.
Hata hivyo baada ya dakika kadhaa, Rutu alichukua simu yake na kumkumbuka Mahadia kwa mara nyingine “Hello” alituma SMS
“nani?” Mahadia alituma kwa kuonyesha kwamba ameshafuta namba yake
“mmh umeshafuta namba yangu?”
“sijui kama nimefuta naomba tu unieleze kwamba, wewe ni nani”
“haya bwana nikutakie tu usiku mwema” alisema mtaalam
Kumbe Mahadia alikuwa ana act tu ili kujionyesha kwamba ana thamani kubwa kama mwanamke lazima uringe kidogo usionekana bei chee kwani mtu akioneshwa anapendwa huwa na kiburi kupitiliza
Alikuwa hata hajaifuta namba ya Rutu, so jamaa alivyomalizia tu SMS ya mwisho hivyo binti aliogopa kidogo na kuamua kumchokoza
“nimeangalia M pesa kumbe ni wewe Rutu” aliandika
“hahaha, cha kushangaza M pesa yenyewe sijasajili kwa jina langu,” alisema mtaalam baada ya kugundua binti bado anamzimia
“mmmmh haya bana, umenikera sana jana, hivi wewe una nini lakini Rutu” alisema binti
“samahani dear, kuna story nilisikia kutoka kwa mama ndiyo maana nilikuambia vile” mtaalam alijaribu kudanganya ili aonekane kwamba hana makosa
“heeeee, story gani tena”
“mama alijua kwamba umekuja kwangu juzi, hivyo alikuja akasema kwamba mim nimeharibika akaniambia nihame nyumbani kwani yeye ameshanichagulia mwanamke wa kuoa hivyo niachane na wewe, lakini leo nimemuelewesha kwamba mimi nina mapenzi na wewe hata hivyo amenielewa na kuniruhusu nikuoe”
“mmmh jamani kweli?” aliuliza binti
“kweli mpenzi naomba unipe nafasi hiyo usikasirike”
“usijali Rutu nakupenda sana kipenzi changu sitokuacha kwa sababu ya mambo madogo kama hayo”
“sawa baby, mimi ngoja nilale zangu nikiamka tu nitakucheki”
“haya byeee”
Rutu alitoka nje na kwenda moja kwa moja hadi jikoni kuangalia msosi, alikuta mama akipakuwa wali akafurahi sana maana njaa ilikuwa kali japo alikuwa hana hamu ya kula kulingana na stress alizokuwa nazo.
Alichukua sahani yake na kurudi ndani akala, alipokuwa anazidi kutafuna kuna SMS iliingia kwenye simu yake aliisoma ilikuwa ni ya Nsia
“ninaomba unisamehe Rutu siwezi nikawa na wewe kwa sababu nimepata mimba, halafu pia nilikusaliti katika hali yako ya umasikini, hata ungenioa kwa upendo bado nisingekuwa mke sahihi kwako, acha niendelee na Bella maana naye anaonekana ananipenda sana” aliisoma akapata hasira na kuijibu
“sasa unanitumia message za nini Malaya wewe” alituma
Muda huo huo iliingia SMS nyingine kutoka kwa Bella “TAFUTA PESA BROO” alituma Bella na vi-imoji vya kucheka kwa dharau
“shukrani kaka, nitazisaka sana tu” alituma mshkaji na kuzima simu yake akalala.
*
Ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri, Nsia alizinduka kutoka usingizini, alikuwa amechoka hasa kwani usiku alitumika vilivyo, alipapasa mikono yake na kujaribu kumgusa Bella lakini alikuta kitandani hakuna mtu.
Alishtuka kidogo akatazama pale Bella alipokuwa amejilaza. Aliona mashuka tu yakiwa yamekaa pale, akashtuka na kuwaza itakuwaje kama mtaalam amemtoroka?…………..
PART 13
Binti alipatwa na hofu, akawaza labda mtaalam alikuwa ameshamtoroka muda mrefu, akashuka kitandani na kwenda kuwasha taa.
“Bella” aliita kwa sauti ya uoga kidogo na kujaribu kufungua mlango ili achungulie nje, alishangaa mlango nao umefungwa kwa nje hawezi kutoka “BELLAA” aliita huku akitikisa mlango ule kwa nguvu lakini haukufunguka, ikabidi arudi kitandani, aliangalia simu yake ilipokuwa ile ndogo ilikuwepo, halafu ile smartphone aliyokuwa amepewa na mtaalam haikuwepo bali ilitolewa laini zikawekwa kwenye stuli
Binti alianza kulia akijua tayari ameshatapeliwa penzi lake “Bella jama” alisema kwa uoga na kutetemeka, alichuku laini akaweka kwenye ile simu ndogo na kuwasha.
Alijaribu kumpigia Bella kwani alikuwa anapatikana basi? aliogopa sana binti wa watu. Akiwa anaendelea kushangaa iliingia SMS kwenye laini yake ambayo ilitumwa muda wa saa tisa na mtaalam Bella.
“SAMAHANI NSIA KIUKWELI MIMI SIKUKUPENDA, NILIKUTAMANI NA SIJAWAHI KUWA NA NDOTO YA KUKUOA MAANA MIMI TAYARI NINA MKE NILIYEMUACHA KAMBINI NA TUNA WATOTO WAWILI TAYARI. NAOMBA UNISAMEHE MIMI NIMEAMUA KUONDOKA NAOMBA USITOE MIMBA YANGU NITAKUTUMIA HELA ZA MALEZI”
“toka, mshenzi wewe” binti alisema kwa hasira na kuifuta ile SMS halafu akaanza kulia kwa sauti ya chini na kwikwi, hakuamini kile alichokuwa amekiona kwenye SMS ‘kumbe ndiyo mapenzi yalivyo hivi?” alianza kuilaumu nafsi yake kwa kumtamani mwanaume mwenye pesa zaidi.
Binti alichanganyikiwa zaidi na kujikuta anashindwa kuelewa afanye nini, alichukua simu yake na kumpigia baba yake.
Mzee akiwa usingizini alishtuka na kuitazama akakuta ni Nsia anapiga simu ‘mh anapiga simu ya nini usiku huu?’ alifikiria na kupokea “hallo Nsia”
Sauti ya kilio ilisikika kutoka kwa binti yake “babaaa” binti aliongea kwa huruma sana
“vipi mwanangu mbona unalia” mzee alishtuka na kushuka kitandani kwa wasiwasi mkubwa
“baba, Bella ametoroka amenifungia ndani na kuniandikia SMS ya kwamba niondoke maana yeye ana mke wake mjini huko alikotoka” alisema binti
“unasemaje Nsia?????”
“ndiyo hivyo baba naomba uje unifungue”
Kwa kuchanganyikiwa mzee alishuka kitandani na kwenda mpaka pale kwa Bella, akakutak una kofuli zito ambalo mtaalam aliweka ili binti asiweze kutoka akamzuia kutoroka
Mzee alipiga mlango Fatuma ukaenda kutua ndani, “mwanangu” alisema kwa upendo wa hali ya juu kabisa halafu akamshika binti mabegani
“baba” binti alisema kwa huruma na kuinuka akiwa anatetemeka bado
“imekuwa hivyo ulivyoniambia kweli?” aliuliza mzee
“ndiyo baba, naomba unisamehe nirudi nyumbani”
“twende nyumbani chukua kila kilicho cha kwako tuondoke, sawa?” alisema mzee kwa hisia kali, alikuwa anampenda mtoto wake maana alikuwa ni binti wa kipekee wengine wote walikuwa midume mitupu
Walichukua mabegi na kuondoka wakaelekea nyumbani na kuendelea kuishi maisha yao ya kila siku
*
Hata hivyo Rutu yeye alishtuliwa saa kumi na mbili kamili na simu iliyokuwa ikiita, aliinuka na kuifuata simu kwenye chaji halafu akaipokea na kuanza kuongea
“Mahadia” aliongea mtaalam
“baby umeamkaje?” aliuliza mtoto wa kike
“safi niambie”
“samahani najua nimekukatia usingizi wako baby lakini kuna kaka yangu alikuwa anafanya kazi katika movie library moja huko Songwe sasa amepata kazi akahama mkoa alitaka amuachie mtu akae pale nikaona bora nikushtue wewe ulivyosema unataka kazi”
“kwani babe pale kuna kazi gani?”
“kazi ni kuwawekea watu movie kwenye simu, flash au CD na kukodisha pia, hivyo nafikiri ni vizuri kama ungeenda akufundishe kutumia hivyo vitu kabla hajaondoka” alisema binti
“kulala sasa ndo tatizo si unajua ni mbali”
“kila ktu anakuachia, hadi chumba alichopanga kwa hiyo cha muhimu ni kutafuta kodi ya kulipia chumba na frame ndio maisha yaendelee”
“ok babe niende lini?”
“leo leo wahi sa hivi ukapate fursa”
“poa”
Mtaalam alikuwa ameamka na zali, leo akatoka mapema kabisa na kwenda jikoni leo kwa mikono yake mwenyewe akaanza kupika chai wakati bado mama yake alikuwa amelala.
Ndani ya dakika 45 alipanda gari moja kwa moja akaondoka na kuelekea songwe kwa ajili ya kwenda kujipatia riziki hiyo hakutaka dharau ya kuambiwa atafute hela na mwanaume mwingine kama ilivyomtokea kwa Bella
Bado mtaalam alikuwa hana habari kwamba Bella amemtoroka mtoto wa kike.
Mida ya saa mbili kasoro, Rutu alikuwa Songwe, alipofika alimkuta Mahadia akiwa anamsubiri stand maana alitaka kumuonyesha kwamba anamjali sana. Alimpeleka mpaka katika ofisi hiyo ndogo ya kaka yake na kuwaacha wakiongea yeye akaondoka.
Ni kweli mambo yalikaa poa sana, hivyo mtaalam aliondoka na kurudi zake nyumbani lakini alimuachapo binti huko huko songwe kwa kaka yake.
Baada ya Rutu kufika nyumbani mama alimpokea kwa upashukuna
“bora umekuja Rutu, umesikia kwamba Nsia ametorokwa na Bella hajulikani alipoelekea?” mama alisema
“weeeee masihara” alisema kwa mshangao
“kweli vile, binti amesharudishwa kwao kule nyumbani” alisema mama
Kwa sababu Rutu alikuwa anampenda binti sana, aliona sio vyema asithibitishe hilo, alienda mpaka kwa mzee Swai, ndipo akashangaa kukuta hamna mtu nyumbani
Alipokuwa anataka kuondoka arudi nyumbani alimuona mzee akija kwa speed ya hatari “Rutu” mzee aliongea huku akihema sana
“baba shikamooo…..vipi mbona unahema sana?” aliuliza
“samahani kijana, umemuona Nsia?” aliuliza
“hapana mzee kwanini?” aliuliza mtaalam
“ametoroka na kila kitu chake sijui ameenda wapi” alisema kwa uoga mzee yule
“ametoroka????” aliuliza zaidi
“ndiyo mwanangu yaani ni matatizo tu uwwwiii” mzee alikuwa amechanganyikiwa…… ilibidi waingie ndani kuangalia kama labda yupo, lakini walikuta hayupo na nguo zake zote ameshachukua kule ndani.
“Mungu wangu” Rutu aliogopa lakini akapata wazo “labda amemfuata Bella” alisema mtaalam na kutoka nje akarudi nyumbani……….
JE BINTI KAENDA WAPI?
PART 14
Ni mwezi ulikuwa umepita tangu Rutu aanze kazi katika movie library iliyokuwa ikifahamika kwa jina la KINGS & QUEENS STUDIO ambapo studio hiyo alirithishwa na kaka yake Mahadia.
Hata hivyo Nsia haikujulikana alipokuwa ameenda, na hata pale walipojaribu kuipigia namba yake ilkuwa haipatikani, vivyo hivyo, Bella naye alikuwa hapatikani na wala hakurudi nyuma
Kwa haraka haraka baba alijitia moyo kwa kusema kwamba binti yake alitoroka kumfuata Bella au labda ni mpango waliokuwa nao wa kutoroka na kwenda wote mjini, hivyo hii ilimpunguzia kupata presha zaidi.
Siku moja jioni, Rutu alikuwa ndo anatoka zake kazini, ndipo Mahadia akampigia simu
“mume wangu kipenzi” aliongea binti
“niambie mahabuba wangu, ninayekupenda sana”
“nimekumiss baba watoto, leo hata sijui najisikiaje tangu asubuhi” alisema mtoto wa kike
“kwanini wasema hivyo mpenzi”
“ni kwa sababu kila ninapopiga hatua hivi, nikisikia chupi ikinigusa gusa kule kunako, yaani natamani nije unisugue mpenzi”
“wooow” alisema mtaalam
“njoo basi maana mimi mwenyewe natamani nikusugue sana mpenzi”
“mmmmh, tatizo hapa home hawataruhusu nitoke usiku huu labda nitoroke baby” alisema binti
“wewe toroka halafu nitakurudisha saa kumi na moja hawatashtuka”
“mmmh, emb ngoja nicheki”
“poa”
Walimaliza maongezi hayo jamaa naye akafika geto maana siku hizi alikuwa haishi tena nyumbani kwa wazazi, alikuwa amepanga na vihela vya kula kidogo alikuwa akivipata pata.
Mida ya saa tano usiku alisikia mlango ukigongwa
“nani?” aliuliza
“fungua bwana” ilisikika sauti ya Mahadia akiwa amekuja kumtembelea mshkaji kama alivyokuwa ameahidi toka mwanzo.
Mtaalam alifungua mlango halafu wakakumbatiana na kuanza kubusiana mdomoni “ule kwanza basi mpenzi” alisema mtaalam
“mmmh unilishe” binti alisema na kufunga mlango. Aliketi pembeni mwa jamaa hapo kitandani kisha wakaanza kulishana wali kwa kijiko, kulishana vijiko viwili tu nye…. Zishawapanda wakaanza kunyonyana ndimi na kuanza kuvuana nguo mpaka mwisho kabisa dudu ikaingizwa ile mtaalam ameanza kuchochea tu hivi, mlango ukagongwa kwa nguvu na kwa fujo huku sauti zikisikika kwa nje za hasira kali
“fungua mlango wewe, tusije kukuuwa hapa” ilikuwa sauti nzito sana ya vitisho
“ni nani huyo?” mtaalam aliuliza binti akawa tayari ameshatetemeka
Kumbe alikuwa ni kaka yake Mahadia alikuwa ameshashtuka kwamba mdogo wake ametoroka nyumbani kuja kuliwa na jamaa.
“kaka yangu” binti alisema kwa sauti iliyojaa wasiwasi.
Kwa mshtuko hadi mashine ya Rutu ililala akaamua kushuka kitandani na kuanza kuvaa nguo zake, binti naye hivyo hivyo, huku mlango unazidi kupigwa kwa nguvu
“fungua mlango…..au tuingie nao nini……wewe bwege” walisema watu waliokuwa nje
Ilibidi mtaalam akafungue mlango kwa ajili ya kusikiliza kinachofuata, kumbe usiku ule binti alipotoroka nyumbani walimsomea ramani, naye alipokuja kwa Rutu tu, nyumbani walienda kutafuta masheikh na kuja nao kwa ajili ya kufunga ndoa ya mkeka kwa nguvu pale
“broo mimi sio muislam”
“acha ubwege wewe tulia hapo” alisema kaka wa binti, kitendo kilichofanya jamaa awe mpole.
Ndoa ya mkeka ilifungwa pale na jamaa akaachiwa mke wake halafu wao wakasepa, nyuma wakisubiri mahari yaletwe na jamaa siku zote
“hahahahhaa” Rutu alicheka
“unacheka nini Rutu” binti Mahadia alishangaa sana
“eti mimi sa hivi ni mume wa mtu”
“heee sasa ndo ucheke?” aliuliza binti
“nimefurahi sana, wamenirahisishia mipango bwana, daaaah, haya niambie mke wangu, au wewe hujafurahi kuwa na mimi” alisema mtaalam
“jamani Rutu acha ukorofi wako bana, hadi hamu imekata”
“njoo ulale huku usiogope haya ndiyo maisha hatujui tumekuja duniani ili nini, tusubiri kifo tu” alisema mtaalam na kumvuta binti wakakulana kisha wakalala.
Ilipita zaidi ya miezi mitatu, wakiwa kwenye ndoa yao Mahadia sasa alikuwa na mimba ya zaidi ya miezi miwili.
Siku moja usiku Rutu alikuwa anakatiza katika mtaa mmoja uitwao mtaa wa Mahoji huko huko Songwe ambapo katika mtaa huo alikuwa anaenda kuchukua movie katika studio moja hivi.
Alipofika mtaa huo alimpigia mwenyeji wake simu na kumuuliza yuko wapi ili ampatie hizo movies kwenye flash
“ulizia bar kwa mangi ndipo nilipo now” alisema yule mwenyeji wake
“poa mwamba”
Rutu alikata simu na kuanza kuulizia maeneo hayo ya bar ya kwa mangi yako wapi, ndipo walipomuelekeza naye akaenda moja kwa moja
Alipofika katika bar ile aliangalia angalia kwenye kaunta, mara akaona jamaa ameketi kwenye kiti kirefu huku akiwa ameshikilia kiuno cha msichana mrembo sana.
Ilibidi naye asogee na kuvuta kiti kingine akaketi na kusalimia. Alipomtazama yule mrembo hivi alishtuka maana hakuamini ni Nsia yuko pale bar tena amevaa hovyo kama mwanamke kahaba
“Nsia!!!!!” aliita kwa mshtuko Nsia naye akageuka
“Rutu!!!!!” alisema binti……………
PART 15
“mh mnafahamiana?” aliuliza yule jamaa aliyekuwa amemshikilia kiuno,
Ilibidi binti ajitoe kwa jamaa na kutaka kukimbia, lakini kwa bahati nzuri Rutu alimdaka “unakimbia unaenda wapi?”
“niachieeee…….niachiee bana” binti alisema huku akijitoa mkononi mwa jamaa, lakini kamwe jamaa hakumruhusu ajitoe mikononi mwake, binti alianza kulia
“Nsia vipi unalia tena?” aliuliza mtaalam na kushuka kwenye kile kiti halafu akamvuta kwa nguvu mpaka nje ya ile bar akasimama naye
“niachie mkono sasa”
“nikikuachia utakimbia” mtaalam alikataa katakata “niambie kwanza Nsia, kumbe unakaa huku tumekutafuta muda wote ule baba yako amesumbuka wewe unafanya ujinga huku?” alisema mtaalam ndipo Nsia akaanza kulia
“niachee Rutu nifuate maisha yangu”
“maisha gani? Kuna maisha hapa? Nieleze ukweli wewe unafanya nini huku?” aliuliza mshikaji
“usitake kujua hata baba yangu hapaswi kujua nilipo tafadhali” alisema binti
“Nsia, inabidi urudi nyumbani baba yako alipata ajali yuko pale nyumbani amekatwa mguu, hana hata wa kumpikia wewe uko huku unakula maisha tu?” alisema mtaalam
“alipata ajali???” aliuliza mtaalam
“ndiyo ina maana hujui?”
“jamani baba yangu” binti alianza kulegea kidogo kidogo
“twende nyumbani tafadhali nataka ukalale pale halafu kesho tuende wote mpaka nyumbani kule?”
“Rutu naogopa sana kwenda nyumbani, hii ni kwa sababu bado nafsi yangu ina hofu”
“Nsia una hofu gani? Ee embu nieleze kilchofanya ukakimbia ni kitu gani?”
“Rutu, unajua hapa nilipo sijiamini kama mimi ni Nsia yule wa zamani?” alisema
“hayo utanielezea nyumbani, wait a minute” alisema mtaalam na kuondoka akaenda kule ndani akachukua kile kilichomleta na kuondoka nacho mpaka pale binti alipokuwa anamsubiri
“tusepe” alisema mwamba na kumvuta binti mkono wakati hajui hata anampeleka wapi
Walifika hadi maeneo ambayo mwamba alikuwa akiishi, ndipo akakumbuka kwamba ana mke “Nsia, nina mke” alisema mtaalam
“sawa haina shida usijali Rutu oa tu mimi mwenyewe hata usingekuwa na mke nisingekubali unioe” alisema binti huku Rutu akimgongea mke wake
“kwanini unasema hivyo”
“basi tu, niliingia mkenge”
baada ya Mahadia kufungua mlango mtaalam na binti waliingia ndani wakamsalimia na kutambulishana ilivyokuwa Mahadia akaelewa. Aliwatengea ugali wakaanza kula huku wakipiga story
“nieleze kwanini ulitoroka nyumbani Nsia”
“Rutu usinikumbushe tafadhali” alisema binti akaacha kula na kuanza kulia
“nini tatizo naomba unieleze tafadhali Nsia, sisi ni kama ndugu tumekuwa pamoja usiogope kabisa”
“Rutu, nilipelekwa kwa Bella baada ya kuishika mimba yake”
“ndiyo ninakumbuka”
“usiku huo huo Bella alinitoroka na kuondoka huku akiniachia SMS kwamba yeye ana familia huko mjini na alinitamani sio kunipenda, niliumia sana ikabidi nirudi nyumbani kwa ajili ya kuendelea kuilea mimba yangu…. Halafu akazima simu akawa hapatikani tena
Baada ya kufika nyumbani asubuhi ile baba aliondoka akaenda kazini na kuniacha peke yangu nyumbani, nilijaribu kumpigia kwa mara ya pili Bella simu yake ikapatikana kwa wakati huo. Aliipokea ile simu na kukata halafu akanitumia SMS
“acha kunisumbua sumbua Nsia nenda kliniki ukapime mimba pamoja na ukimwi, tafadhali angalia mwanangu asipate ukimwi huo niliokuachia” hiyo ni SMS ambayo Bella alinitumia nikachanganyikiwa baada ya kuisoma.
Niliingia ndani nikachukua nguo alizowahi kuninunulia nikazichoma moto huku machozi yakinitoka ndipo nikaamua kukimbia nyumbani nije nidange ili nipate hela ya kula” alisema Nsia maneno yaliyohuzunisha
“sasa mbona mimba hauna au umeshazaa?”
“hapana Rutu niliamua kuitoa nikiamini yule mtoto sio wa haki kwangu, hata hivyo nimetembea na wanaume wengi sana nikilipiza kisasi cha ugonjwa”
“ulishawahi kupima ukathibitisha kwamba una ukimwi”
“hapana sitaki presha mimi rafiki yangu” alisema binti na kunawa mikono manake ameshashiba
*****
Asubuhi na mapema Rutu alimuacha mke wake ofisini halafu yeye akachukua time yake kumpeleka binti hospitalini aende kupima afya, binti alitetemeka sana kwa kuogopa.
Upande mwingine lilitoka jibu kwamba binti alikuwa bado ni mzima sana, walipanda gari na kwenda kwa baba yake huko Komboi, alipofika komboi watu wote walikuwa wakishangaa kwani binti alikonda sana na hii ilikuwa kwa sababu alikuwa anafanya kazi asiyoipenda kazi ya kujiuza kwenye mabaa huko songwe
Binti alishangaa sana alipofika kwao kwani alikutana na uso wa kaka yake anayemfuatia akiwa anafeka majani uwanjani
“kaka” alimuita kwa hisia na kwenda kumkumbatia
“Nsia umetoka wapi?” aliuliza Lwani, kumbe ndugu zake wote walikuwa ndani wakatoka na kumtazama mdogo wao kwa kwa furaha
“baba yuko wapi?” binti aliuliza kwani alikuwa ameshaambiwa kwamba baba yake alikuwa amekatwa mguu kwa sababu ya kupata ajali mbaya iliyosaga mifupa.
Ndugu zake walianza kulia wote binti akaogopa sana “yewo….mnalia nini” alisema binti
“zunguka nyuma ya nyumba” alisema mtaalam Ndumi
Baada ya binti kuzunguka nyuma ya nyumba yao hakuamini alikutana na kaburi jipya kabisa likiwa limepangwa pembeni mwa kaburi la mama yake
“baba!!!!!” binti alikimbilia kaburi lile na kupiga magori huku akiusoma msalaba ulioandikwa Utukufu S Swai, hakuamini macho yake
“nini kimemuuwa baba jamaniiii?” aliuliza
“baada yaw ewe kutoroka mzee alipata presha sana, hata hivyo alikuja kupata ajali nyingine iliyopelekea kukatwa mguu na hatimaye kufariki baada ya wiki mbili tu”
“jamani babaaaaa” binti alilia kwa uchungu mpaka basi
Alihisi kosa ni la kwake kusababisha baba yake afariki dunia
Rutu alipanda pikipiki na kuamua kurejea katika mji wake alipokuwa akiishi na mke wake mpya aitwaye Mahadia
HERI WALE WANAOLIA SASA MAANA WATACHEKA
OLE WAO WANAOCHEKA MAANA WATALIA NA KUSAGA MENO