TAFUTA HELA BROO
PART 01
Baada ya maisha kumpiga vibaya mno kijana Rutu huko jijini Dar es Salaam aliamua kupanda gari na kurudi katika mji wao mdogo huko Mbeya.
Akiwa ndani ya gari alikutana na rafiki yake mmoja aliyekuwa anafahamika kwa jina la Bella ambaye ni muda mrefu hawakuonana
“Daaaah mwanangu kweli milima haikutani lakini binadamu tunakutana” Alisema kijana Rutu baada ya kumkuta Bella akiwa amekaa tena kwenye siti zinazofuatana kabisa
“hahaha ni hatari mwanangu vipi kumbe na wewe ulikuwa jijini hapa dar”
“yaaah man yani nimechoka vibaya mno mzee, bora nlivyopata nauli nisepe zangu mwanangu”
“kwanini boss unasema hivyo” alisema mtaalam
“naongea hivyo maana maisha niliyoyapitia kamwe sikuwa na ndoto ya kuyapitia kabisa boss vipi wewe unapiga mishe gani dar”
“mwanangu mimi ni mwanajeshi, nimepata likizo ya miezi mitatu hapa nataka nikakae pale nyumbani hata mwezi mmoja nifanye mchakato hata wa kujenga kibanda cha kulala tumetia aibu man”
“ahahhaa ni kweli kama mkwanja upo ukafanye mambo” Rutu alisema huku akiitoa simu yake mfukoni kulikuwa na sms kutoka kwa mpenzi wake
“Baby kweli unakuja” alituma mpenzi wake mmoja aliyefahamika kwa jina la Nsia
“yaani huyu msichana ananielewa kichizi mwanangu” alisema mtaalam kwa hisia huku akitikisa kichwa kwa furaha
“Ni nani huyo?” Bella aliuliza
“Ni Nsia yule binti wa mzee Swai”
“Mh kale kadogo kashafaa kula?” aliuliza
“kitambo sana, ni miezi sita nimeondoka kule sasa kanalalamika sana kwamba niko mbali kamenimiss eti kademu haka”
“hahaha ulishapiga?”
“hhahahaa kwanini niwe muongo sijapiga ananiambiaga mpaka tuonane mzee” alisema mtaalamu
“aiseee embu nionyeshe picha yake nimkumbuke vizuri”
Rutu alichukua simu yake iliyochoka choka sana akatoa password na kufungua picha ya binti ambayo alikuwa nayo moja tu, tena alikuwa ameipiga kwenye picha iliyooshwa hivyo haikuonekana vizuri
Safari iliendelea mpaka ikafika mida ya saa mbili usiku
“baby umefika wapi jamani mimi silali mpaka nikuone” aliandika mtoto wa kike
“usijali baby nimekaribia mida yaa saa nne najua nitakuwa mitaa ya nyumbani kabisa love”
“sawa dear, zawadi yangu umeniletea?” alisema binti
“ndiyo nimekuletea honey but ni ndogo usije ukalalamika sana sina hela mpenzi”
“haina shida hata usipoleta bado ntakupenda Rutu nimekumiss sana”
“jamani nakupenda sana mpenzi” aliandika mtaalam
“sawa baby nakusubiri nikubusu”
“sawa mpenzi”
Basi safari iliishia katika mtaa wa Komboi ambapo mtaalamu aliposhuka Mbeya mjini alipanda gari nyingine na kuelekea maeneo ya kwao kijijini kabisa
Hakuwa peke yake, walikuwa pamoja yeye na Bella maana walikuwa wazawa wa mtaa mmoja,
“Mwanangu Rutu tutasomana kesho mzee ngoja niwahi” alisema Bella na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwako
Hata hivyo wakati Bella akiwa anapita maeneo ya kwa kina Nsia alimuona mtu akiwa amechuchumaa kwenye giza
“oyaa” alimuita kwa uoga maana hakujua kwamba ni nani kumbe alikuwa ni nsia
Nsia naye kwa kuona mabegi yamebebwa na mtu huyo akajua ni Rutu ikabidi amtanie
“sasa ndo unaenda wapi huko na wewe mtoto wa daslam” aliongea kwa hisia na kuinuka pale alipokuwa amechuchumaa, alijua ni Rutu na alishangaa anaelekea wapi wakati sio mitaa ya kwao
“Hhhaaa, nani wewe?” alisema mtaalam
“mmmmh mi Nsia bwana” alisema binti na kuanza kumsogelea jamaa
“ahahaa binti wa mzee swai” alisema mtaalam Kiswahili chake kikiwa kidar es salaam kabisa kitendo kilichofanya binti apagawe kwa sauti aliyokuwa anaongea
Alimsogelea Bella, “pole na safari” aliongea akiwa anamtazama kwa makini ndipo akagundua sio Rutu “samahani nimekufananisha, kuna mtu ninamsubiri hapa”
“ahaa usijali, ila naona umekuwa sana Nsia”
“kawaida jamani” alisema na kurudi nyuma akamuandikia sms Rutu “mbona haufiki jamani Rutu au ndo hutaki kuniona kabisa” binti alisema alikuwa anatamani sana amuone mshikaji wake
“Nsia usiku mwema” alisema Bella akachukua mabegi yake na kuendelea kutembea.
Binti alibaki pale akimsubiri Rutu, baada ya dakika kumi na tano Rutu alitokea akiwa amevaa hovyo kabisa, binti hakuamini kama jamaa angevaa hivyo wakati ametokea jijini Dar
“Mambo Nsia” alisema na kumsogelea akiwa anataka kumkumbatia
“safi jamani pole sana Rutu”
“Asante” Rutu alimkumbatia binti kwa nguvu “Nimekumiss mpenzi”
“Nimekumiss pia dear, vipi maisha ya Dar yanasemaje lakini”
“Ukisikia Marioo akikuambia kwamba Dar Kugumu basi baby uamini anachokisema maana Dar ni hatari mpenzi huwez amini ndani ya miezi sita nimefanikiwa kununua T Shirt moja tu”
“jamani pole sana mpenzi, nilikuambia ubaki tutafute kazi huku huku ukakataa”
“daaah kweli, lakini nimejifunza kitu mpenzi”
Rutu alianza kumshika shika binti kwa hisia, halafu akamuachia, aliingiza mkono mfukoni akatoa Mkufu na kumvalisha binti halafu pia akatoa Lol Pop na kumpa msichana huyo
“hiyo ndiyo zawadi ya pekee niliyoweza kukuletea Nsia”
“asante mpenzi inatosha” alisema
“Ok naomba niondoke niende nyumbani tafadhali nimechoka sana nafikiri tutaonana kesho”
“mi sitaki” binti alisema na kumkumbatia
“baba yako akikukuta hapa itakuwa ni kesi mpenzi”
“kwanini iwe ni kesi”
“kwa sababu niko na wewe”
“iya kwani hajui? Anajua vizuri na nimemwambia unakuja so nataka unioe sasa mimi nimechoka kukaa kwetu”
“kweli mpenzi?”
“ndio mume wangu
Rutu alimvuta na kumkumbatia binti akiongea maneno ya mahaba na kumsifia sana binti “wewe ni mzuri kushinda mabinti wote hapa mtaani, mtoto mweupe halafu una figure daaah bora haukuzaliwa huko kwenu uchagani mimi ningekujulia wapi kipenzi”
“jamani napenda wewe unaponisifia sana Rutu, nilikuwa nimemiss kuwa karibu na wewe, nilikuwa nasikia baridi sasa hivi nahisi joto ulivyonikumbatia kipenzi”
“Haya baby ngoja basi mimi niende nyumbani nikalale halafu asubuhi tutaonana tafadhali”
“sawa mpenzi ninaomba asubuhi uje kwetu”
“poa mpenzi” Rutu alimuachia na kuondoka bila hata kumbusu binti
*
Asubuhi na mapema binti aliamka na kuanza kufanya usafi huku chai ya baba yake ikiwa inachemka jikoni maana alikuwa hana mama, mama alikuwa ameshafariki kitambo
Baada ya chai kuiva vizuri binti alienda sebleni ambapo baba yake alikuwa ameketi akisikiliza magazeti kwenye redio
“baba leo haununui kitafunwa jamani?” aliuliza na kummiminia chai kwenye kikombe
“chukua hela hapo kwenye meza kuna elfu moja nenda kalete skonzi” alisema mzee
“sawa baba”
Binti alienda kwenye meza akachukua hela na kuelekea dukani kwa ajili ya kwenda kununua vitafunwa hata hivyo akiwa njiani kuelekea dukani alimkuta Bella akiwa amesimama anaongea na simu mkono wa kushoto, halafu wa kulia ulikuwa umeshikilia tablet moja kali ya Apple
Bella alibaki akimshangaa binti alikuwa ameshakuwa mkubwa kabisa wakati akiondoka mbeya alimuacha akiwa mdogo kabisa,
Binti alipomuona alibaki akimshangaa kwani jamaa alikuwa ameng’aa hasa kulingana na hali ya uchumi aliyokuwa nayo, na nguo alizokwa amevaa zilikuwa za bei hasa, binti akapita na kwenda dukani kununua vitu alivyoagizwa
Bella mwenyewe alipomuona binti alishangaa kwani binti alikuwa amependeza hasa na alikuwa tayari ni mwali kabisa wa kufungisha ndoa
Baada ya kukata simu Bella aliamua kumfuata nyuma mpaka pale dukani ambapo alikuta mtoto wa kike akinunua scones na simu yake ndogo alikuwa ameshikilia mkononi
Muuza duka alipomaliza kumhudumia alimpa mfuko na Nsia akaanza kuondoka
“wait wait wait” alisema Bella binti akaanza kumshangaa “Oya mangi, embu muongezee tena scones kumi mpe na vocha ya buku mbili” alisema Bella binti akatabasamu na kugeukia dukani alikuwa anataka apewe vitu vyake alivyoagiziwa na mwamba
“jamani asante” alisema binti
“samahani Nsia wewe ndiye niliyekukuta pale kwenu ukiwa umechuchumaa jana?” aliuliza mtaalam
“ndiyo ni mimi, kumbe wewe ndiyo umekuja jana kaka” alisema mtoto wa kike
“ndiyo, samahani lakini, naomba tuchat leo”
“mmmmh, haya nitajie no yako” alisema binti na kuishika simu yake tayari kwa kuandika namba ya mwamba
“07643958436”
“ok powa” binti alipokea vile vitu alivyonunuliwa na kuondoka……………
JE PENZI LA RUTU LITADUMU?
PART 02
Baada ya binti kufika nyumbani, aliweka vitafunwa mezani na vocha, halafu akaenda jikoni kwenda kuchukua kikombe kwa ajili yake
Mzee wake alipofunua mfuko na kutazama ndani alishangaa anakutana na scones nyingi sana ikabidi asite kidogo mpaka pale mtoto wake aliporudi
“mwanangu mbona skonzi ni nyingi hivi kwani ulichukua shilingi ngapi?”
“baba hamna hizo hapo kaninunulia Rutu” alidanganya
“mh Rutu kaja kumbe?”
“ndiyo baba”
“haya umuambie basi aje anisalimie maana ni muda mrefu sana sijamuona kijana yule” alisema mzee
“atakuja leo baba” alisema
“sawa”
Basi walianza kunywa chai na vitafunwa kadhaa, lakini hawakuweza kumaliza, baada ya binti kumaliza kunywa chai alitoa vyombo mezani halafu akarudi sebuleni akaketi kwenye kochi na kuiweka ile vocha
Mtu wa kwanza kabisa kumcheki alikuwa ni Rutu hii ni kwa sababu alikuwa anampenda sana, alimuandikia message nzuri ya mapenzi na kumtakia asubuhi njema
Hata hivyo haikuchukua muda mzee Swai aliinuka na kuondoka akaenda zake kazini maana kazi yake alikuwa akivuna mpunga kwenye mashamba ya watu na kulipwa kwa siku shilingi 5000
Mzee huyu alikuwa na mke wake mnyakyusa ambaye alikufa miaka sita iliyopita wakati Nsia akiwa na miaka kumi na mbili tu, Nsia ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wane wa familia, hii alikuwa ni mtoto wa kike pekee na kaka zake walikuwa wakiishi huko Uchagani kwa babu yao mzaa baba
Ikiwa ni mida ya saa saba mchana Nsia alikuwa akichati kwenye simu yake, hakuwa na papara ya kumuandikia sms Bella kwani alihisi wataanza mada zingine ambazo ni za mapenzi wakati yeye ana Rutu wake ambaye anampenda sana
“hodiii” sauti ya Rutu ilisikika nje ya nyumba
“karibuu” binti alisema huku akijiweka vizuri usikute amekaa vibaya jamaa aone mambozi
“shikamoo baba”
“baba hayupo, karibu ndani”
“asante sana” alisema mtaalamu na kufika katika mlango wa sebule akavua ndala zake na kuingia ndani
Binti alipomtazama Rutu alionekana kama vile amekonda sanaa, sura ilipauka, hata nywele hakunyoa, alikuwa na uvimbe uvimbie katika uso wake uliosababishwa na kuumwa kwa mbu mara nyingi huko jijini Dar es Salaam
“vipi Rutu mbona umekonda sana” aliuliza binti huku akimshangaa
“mmh nimekonda sana kwani?” Rutu aliketi kwenye kochi
“sana mpenzi kuna nini tatizo lakini dear”
“baby maisha yalinipiga sana huko Dar naomba tuyasahau yote, niambie baba yuko wapi nilitaka kumuona”
“baba hayupo ameenda kazini sijui atarudi jioni kama kawaida yake?” alisema binti
“oooh sawa nilitaka nimsalimie, ila Nsia umependeza sana mpenzi nimefurahi sana kukuona vipi kuna mtu anahudumia hapo nini”
“hahahaa, jamani hamna mtu yeyote zaidi ya baba yangu”
“mh haya bana, nlikumiss sana mpenzi, I’m sorry niliondoka bila kukuaga, nilijua utalia sana”
“usijali Rutu, mimi ninakupenda katika hali yoyote ile”
Haikupita dakika nyingi, alisikika baba akija kutoka kazini kwani siku hiyo aliwahi isivyo kawaida yake
Leo hakuja peke yake alikuja akiwa amefuatana na Bella walikuwa wakiongea kwa nguvu sana, mzee aliingia mpaka ndani akamuona Rutu akiwa ameketi pale.
Kwa nidhamu Rutu aliinuka na kumsalimia mzee kwa mkono
“baba shikamoo” alisema Rutu
“aaa marahaba bwana za siku nyingi”
“nzuri tu baba”
“karibu sana” alisema mzee na kuketi. Bella bado alikuwa nje “Bella karibu ndani” alisema mzee kwa nguvu
Nsia aliposikia Bella anakuja pale ndani moyo ulimuenda mbio hadi akainuka na kwenda chumbani kwake kukaa kwanza
Bella aliingia na kuketi pale pale alipokuwa ameketi Nsia, na kumsalimia Rutu halafu wakaendelea kupiga story kama dakika kumi na tano hivi
“Nsia kawaletee wageni soda” mzee alimuita binti yake
“sawa baba”
Binti alitoka chumbani akiwa hajiamini sana kupita pale sebleni, lakini baba yake alimpa shilingi 2000 na kumuagiza dukani akalete angalau soda za wageni
Baada ya binti kuondoka Bella alianza kukorofisha “mzee umeshakuza sasa”
“haha. Muda mrefu sana ni mahari tu nasubiri”
“ndiyo lazima usubiri mahari kweli, vipi lakini mbona kaka zake hawaji huku tena, kina Ndumi, Elibariki na Lwani” aliuliza Bella
“watakuja mwezi wa kumi na mbili hapo”
“sawa kabisa”
Muda wote Rutu alikuwa kimya akisikiliza porojo porojo za watu hao wawili mpaka binti aliporudi na kuwafunulia soda, zilikuwa soda mbili, moja ya Rutu na nyingine ya Bella,
“haaah mbona hamjachukua za kwenu?” aliuliza Bella
“haina haja mwanangu” mzee alisema huku akiipokea chenji kutoka kwa binti yake
Bella alielewa moja kwa moja uchumi ndio unaowakaba familia hiyo akaamua kufungua wallet yake na kutoa elfu ishirini
“Nsia nenda dukani, chukua soda yako wewe na ya baba, halafu hela itakayobaki chukua, Sabuni mche, Sukari, Mafuta na mchele kidogo” alisema mtaalamu na kumkabidhi
“mmh asante mwanangu, kweli mgeni njoo, mwenyeji apone, si unaona sana Mungu akubariki kabisa mwanangu” alisema mzee
Hali hii ilimuathiri kisaikolojia Rutu aliumia sana kwani alitamani yeye ndiyo awe anatoa hizo mikwanja kwa mzee ambaye alitarajia awe mkwe wake.
“Hivi Bella” Rutu alianza kuongea baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu
“niambie mzee Rutu” alisema mtaalam
“jeshi linaonekana lina mkwanja sana au?”
“hahahaa, kawaida, unaweza ukadhani nina maisha mazuri lakini maisha bado ni cheche” alitamka
“daah, sawa mzee tukitoka hapa kuna ishu ninataka tuongee”
Baada ya binti kurudi kama kawaida yake alienda kujificha chumbani na kuishika simu yake. Aliisikia nafsi ikimshauri kwamba amtumie sms Bella lakini hakujua kwamba ni shetani tu anamsumbua
Kabla ya kumtumia mshkaji sms, ilipenya kwenye simu yake, akaifungua ilikuwa ni ya Rutu “mbona umeenda kujificha chumbani mpenzi” alituma Rutu
“hahaha, naona aibu” binti alijibu ile sms
“aibu ya nini sasa” aliuliza
“kukaa na wanaume watupu hapo unafikiri mchezo?”
“hahaaa haya bwana”
Baada ya Rutu kutuma hiyo sms binti alikunywa soda yake halafu akamtext Bella
“ASANTE”
Bella alipoitoa simu mfukoni alikuta ni namba mpya hata hakuwa na mbwembwe akauliza ni nani
“Mi Nsia”
“oohoo kumbe namba yako sasa asante ya nini na wewe”
“kwa vocha na vitu ulivyotununulia”
“aaah kawaida bana wala usijali”
“haya powa”………………
PART 03
Siku moja baadaye, ilikuwa ni asubuhi na mapema ambapo Rutu alikuwa ameketi nyumbani kwa Bella wakiwa wanapiga story tofauti tofauti. Bella alikuwa akisubiri lorry lilete mchanga aliokuwa ameagiza kwa ajili ya kufanya ujenzi pale nyumbani kwao
Hata hivyo urafiki wao ulikuwa umeshakuwa kwa kiasi kikubwa sana, hii ni kwa sababu walikutana wakati muafaka kabisa na kwenye kazi yenyewe
“mwanangu Bella inabidi unisevu kidogo man na mimi niwe na maisha mazuri si unaelewa tena”
“wewe unatakaje Rutu”
“daah nikopeshe mtaji hata wa laki mbili nianze hata biashara ya kuuza genge mwanangu kukaa kaa kizembe style kiukweli sitaweza mwanangu”
“sikiliza broo, mimi kukupa mtaji siwezi, ila ngoja nikuambie kitu kimoja, kwa sababu hapa nataka nianze msingi kuanzia kesho basi mimi nitahakikisha fundi anakupa kazi kama msaidizi wake mpaka kazi itakapoisha ninaamini utakuwa na zaidi ya laki tano maana nitakuwa nakulipa mimi mwenyewe……. Zege unaliweza?”
“ndiyo ninaliweza vizuri kwanini nishindwe?” aliuliza mtaalam
“haya sawa basi umepona”
Muda huo huo liliingia lori mbili, moja ikiwa na matofali na pamoja na cement halafu nyingine ikiwa na mchanga mwekundu kwa ajili ya kuunga joint.
Hata hivyo gari zile zilishusha vitu na kuondoka kwa ajili ya kwenda kuleta zaga nyingine. Rutu aliingiza cement ndani na kisha kuamua kuondoka akaenda hadi nyumbani kwao kwani alikuwa anahitaji kwenda kufua nguo zake.
Kitendo cha kuondoka hivi lorry zililirudi round ya pili na kuanza kupakuwa vitu nyumbani kwa Bella kumbe binti Nsia naye anakatiza mitaa ile ile akiwa ameshilia muwa anaendelea kula, alimuona Bella akiwa ameshika simu yake kubwa na kuongea na madereva wa malori hayo yaliyokuwa yameleta mchanga na matofali
Binti alisogea karibu kwa ajili ya kumtaka hali Bella
“mambo” alimsalimia
“safi, embu subiri nimalizane na madereva halafu tuongee” alisema Bella
“powa” binti aliongea huku akiwa anazidi kula muwa wake taratibu pembeni mwa barabara na kuchat kwenye simu yake ndogo ya goroka
Baada ya Bella kumalizana na madereva hao alimrudia binti “huogopi kula miwa na baridi hii”
“aahaha wala…..mi naona kawaida tu” alisema huku akiitazama simu ya mtaalam tablet ya maana iliyokuwa mkononi mwake “mmh simu yako kubwa”
“ahaa hii” mtaalam alijibu akiwa anaiangalia angalia simu yake
“ndio , ni sh ngap” aliuliza binti
“milioni mbili”
“duuuuh simu unanunua ghali hivyo”
“kawaida tu” alisema mtaalam “vipi wewe mbona sikuoni mtandano ni nini” aliuliza
“aku hata sina smartphone kaka”
“unasoma?” aliuliza Bella
“hapana shule nilimaliza mwaka juzi, nipo home tu maana sikufaulu” alisema na kucheka kwa kuona aibu ya kufeli tayari
“haya bwana, nikajua mwanafunzi ndiyo huwa haruhusiwi kuwa na simu kubwa”
“hamna wala, nasubiri baba yangu aninunulie”
Wakati wanaogea hayo yote kulikuwa na mtu alikuwa akiwaona kwa mbali, na alikuwa ni mtu ambaye anafahamu fika kwamba binti yupo katika mahusiano na mtaalam Rutu hivyo akaamua kumfuata hadi nyumbani
“Oy Rutu vipi mzee?” aliuliza huyo jamaa aliyefahamika kwa jina la Michael
“good man, niambie” mtaalam alijibu akiwa anafua nguo zake tarattiiiibu kwenye beseni
“daah naona unafua kwanini usimwambie mtoto aje akufulie?”
“mtoto bwana sitaki nimchoshe sana sa hivi, nikumuoa lazima atanifulia sana ndo maana namvungia sasa hivi”
“hahahaa, lakini mbona kama namuona anaongea na Bella pale kwa Bella?”
“acha man”
“kweli mzee” alijibu Michael
Rutu alichukua simu yake akampigia binti ili kujua kama ni kweli binti yupo na Bella alimtumia message na kumuuliza yuko wapi
“nipo nyumbani” Nsia alijibu na kutulia kidogo halafu mwamba akapatwa na hasira akainuka na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Nsia nyumbani
“hodiii” aliita mtaalam kwa mzee Swai
“karibuuu” sauti ya binti ilisikika kutoka ndani ya nyumba yao mshkaji
“wee Nsia”
Nsia alitoka nje akamkuta jamaa amefura, ameketi barazani kwenye sakafu “vipi mpenzi”
“ulikuwa wapi Nsia lakini mbona wanifanya nipagawe mimi?”
“jamani mbona nilikuwa hapa nyumbani tu Rutu”
“wewe haukuwa kule kwa Bella?”
“mmh kwa Bella????…. mbona mimi sijatoka leo Rutu” binti alisema kwa kudanganya, yaani karoho ka usaliti kalikuwa kanamuandama tayari
“ndiyo wewe nmeambiwa kwamba ulikuwa kwa Bella kule mnaongea, embu nieleze mlikuwa mnaongea nini”
“jamani jamani jamani, watu wa komboi wananitaka nini mimi? Saa ngapi nilikuwa kwa Bella? Haki ya Mungu sijaenda kwa Bella leo hata sijamuoana mpenzi”
“so ulikuwa hapa nyumbani?”
“ndiyo Rutu, usisikilize maneno ya kuambiwa mpenzi”
“daaah, haya bwana basi sawa ngoja mi nikaendelee kufua”
“haya baby mimi ndo napika nikimaliza nitakutext uje ule”
“sawa”
Mida ya usiku kwenye mida ya saa nne usiku, Rutu alikuwa amejilalia kitandani, leo alipigiwa simu na mshkaji wake ambaye alikwa ni mshkaji sana kipindi yuko Dar
Mshkaji huyo alikuwa akimuuliza kama jamaa alifika salama, na alipojua kwamba jamaa alifika salama basi akafurahi na kumpa hongera kwa kuukimbia mji maana hali ni tete
Hata hivyo haikuishia hapo, Rutu alipoongea na huyo jamaa aliamua kumuomba vocha naye akamtumia buku kutoka M pesa
Jamaa alipojiunga tu na MB za wiki alianza kuingia mtandaoni kwa ajili ya kuperuzi, vivyo hivyo jamaa aliamua kuingia mtandao wa WhatsApp ambapo alipenda sana kutazama status za watu
Katika kuangalia status alishangaa kuona kama vile Nsia kapost status.
“Ebo!!!” alishtuka kidogo na kurudi nyuma ili aangalie kama ni kweli au ameona vibaya.
Aliporudi nyuma tu hivi akaona namba ile ile anayoijua na kwa jina lile lile la Nsia alilolisevu, aliona limepost status WhatsApp halafu amepost selfie ya picha yake kwa nguo zile zile alizokuwa amevaa mchana “amepata wapi smartphone huyu demu” mtaalam alijiuliza huku akisikia mwili wote ukiwa wa baridi
“daaah” alisema kwa sauti ndogo halafu akamtumia message ya kawaida binti hakujibu
Mtaalam akajua labda binti alikuwa amelala, lakini alipojaribu kumtext WhatsApp alishangaa message inaleta tick mbili halafu alimuona pia binti yupo online mida ile……………
PART 04
Hali hii ilimfanya Rutu aanze kujisikia vibaya na kuamini kwamba binti ameshaanza mambo mengi
“nakuona online lakini text zangu hutaki kujibu, sawa” alisema mtaalam ndipo binti aliposhtuka kwamba kumbe jamaa anamuona akiwa online
“jamani samahani, nina MB tu sms sina” alituma binti WhatsApp
“oh sawa Nsia, ila mbona najisikia vibaya nilivyokuja wewe umebadilika sidhani hata kama bikira unayo tena”
“ipo Rutu, hakuna mwenye uwezo wa kuitoa isipokuwa wewe tu mume wangu”
“kweli Nsia?”
“ndiyo mpenzi usiwe na wasiwasi na mimi, ni mwaka na miezi mitano tangu tuwe wote kwenye mahusiano, nije nikuache leo kweli Rutu? Hapana nitakupenda katika hali zote”
“asante mpenzi, vipi simu umepata wapi?” aliuliza
“baba kaniletea”
“wooow hongera sana kipenzi, bora sa hivi nitakuwa nakuona live mtandaoni”
“ndiyo dear”
“poa mi nalala mke wangu”
“haya”
Hata hivyo Rutu aliridhika na maneno ya binti lakini wakati yeye analala, Bella alimpigia Nsia simu na kuanza kutupa ndoano
“Nsia mambo vipi mbona online umepotea tena”
“jamani ni usingizi umenishika ninataka nilale”
“ok sawa hiyo, simu niliyokupa ni nzuri au nikakununulie mpya kabisa” alisema mtaalam
“ni nzuri nashukuru sana ka Bella, unanitendea mambo ambayo ni makubwa kwa mda mfupi tu una roho nzuri sana kaka B”
“hahaa, usijali ni haki yako unajua wewe nimegundua ni mtoto mzuri sana, yani kama sio kukosa hela tu basi ungewashinda wanawake wote hapa mtaani, yaani kwanza mtoto mweupe kama wewe ninataka siku moja nikupelekea shopping nikakununulie nguo upendeze halafu na hizo nywele usuke rasta yako ya maana wakukome hapa mtaani, halafu nataka nikuoe”
“mmmmmmh jamani”
“mbona waguna Nsia au hujapenda nilichokuambia”
“nimependa sana lakini kunioa haiwezekani kwa sababu tayari nina mchumba”
“mmmh mchumba yupi unaye?” Bella aliuliza lakini kiukweli ni kwamba alijua kabisa binti anatoka na Rutu
“sitaki kukutajia lakini wewe uelewe tu nina mpenzi na ninampenda sana siwezi kumsaliti hata chembe”
“daaah, sawa Nsia, mimi nikutakie basi usiku mwema” alisema mtaalam na kukata simu ka hasira
Kutokana na ile hali ya kukata simu kwa hasira binti aliogopa akihisi labda jamaa atamnyang’anya simu au pia atamchukia na alipenda angalau wawe marafiki tu
“Ka Bella usikasirike naomba tu tuendelee kuwa kama kaka na dada jamani usinune sawa ee” alituma sms binti
Bella alipoisoma ile sms alitabasamu na kutafakari ‘hahaa hajui tu kwamba lazima aingie mkenge huyu manzi?’
Bella hakuijibu ile message alilala zake.
Asubuhi na mapema mtoto wa kike hakuweza kulala vizuri alimuandikia sms Bella “Morning” huku akimsahau mpenzi wake wa siku zote
Zaidi ya dakika kumi na tano zilipita bila Bella kujibu ile sms binti akajua jamaa amekasirika sana ikabidi binti apande hewani
“halloo” Bella aliongea kwa sauti ya uchovu maana alikuwa ndo ametoka usingizini
“mmmh mwanajeshi unalala hivyo kweli wewe una uwezo wa kuilinda nchi dhidi ya vita?”
“hapana, ni kwamba niko likizo acha nile maisha kidogo bwana ah”
“haya bwana vipi lakini mimi nikajua upo macho lakini haujibu sms zangu eti kisa umekasirika”
“hapana, sijaona text kabisa lakini jana uliniudhi
Hivyo pia upande wa Rutu naye aliamka mapema sana, kutokana na jana yake kujiunga aliamua kumpigia Bella ili amuulize kama kazi inaanza siku ile au la, lakini alimkuta Bella yuko bize anaongea na simu nyingine.
Alipokuta yupo bize aliamua kumpigia roho yake, Nsia kumtakia hali, lakini naye pia alimkuta bize.
Kwa haraka haraka hakuhisi chochote kwani bado alikuwa hana wasiwasi juu ya hao watu wawili akiamini Nsia anampenda sana na hawezi kumsaliti, lakini kumbe Bella ameshamtamani binti na alikuwa anatumia nguvu ya pesa kumpata bila mtaalam kugundua kirahisi
“Waiii, leo kila mtu yupo bize, wamenikamia na dakika zangu” aliinuka na kwenda kuweka simu kwenye chaji halafu akatoka nje
“mama” alimuita mama yake
“mwanangu”
“shikamoo mama umeamkaje”
“marahaba kabisa, vipi hali yako”
“hali yangu mbaya mama”
“ubaya wake nini”
“njaa”
“mh kanunue basi vitafunwa tunywe chai jamani mwanangu, hiyo Dar mbona kama imekupiga sana”
“ungejua sina hata mia usingeongea mama, hata hivyo nataka niende mpaka kwa Bella nahisi pale kuna kazi leo
“sawa”
Baada ya kunywa chai Rutu aliinuka na kwenda ndani, akaichukua simu yake kisha akatoka, alipotoka akielekea barabarani aliitazama akakuta kuwa alipigiwa mara tatu na Nsia, ikabidi naye ampigie sasa ili apate kumsalimia
“Nsia mambo jamani”
‘safi tu vipi”
“poa ndo umeamka?”
“hapana kwanini unaiuliza hivyo?”
“nilimpigia Bella mda mda kidogo nikamkuta bize, na wewe nikakupigia muda huo huo nikakuta uko bize”
“mimi sijui labda alikuwa anaongea na mtu mwingine huko sio mimi halafu hata sina namba yake” binti alianza kujishtukia mwenyewe wakati hata jamaa hajamuambia kwamba alikuwa anaongea naye
“aaaah, jamani kwani nimesema ulikuwa unaongea naye?”
“mimi nikajua unanihisi vibaya, haya niambie basi haraka haraka maana mimi ninataka nipike halafu naenda mjini kuna kitu nafuata”
“sina cha kukuambia zaidi ya kusema kwamba ninakupenda mpenzi wangu”
“hata mimi pia nakupenda sana Rutu”
“ok baby, basi wewe pika ukienda town utaniambia basi” alisema mtaalamu
“sawa”
Rutu alikata simu na kwenda moja kwa moja hadi kwa Bella, alikuta vijana kama watano hivi wamekuja kikazi,
“wewe Rutu mbona nakupigia upo bize mzee, kazi ndo inaanza sasa hivi” Bella alisema
“samahani nilikuwa naongea na mtu”
“ok powa, nimeshamueleza fundi, wewe utakuwa kama msimamizi hapa, maana mida mida ninatoka na nitarudi kama saa kumi hivi” alisema Bella
“poa kamanda nakukubali sana mzee”
“poaaa”
*****
Kazi ilianza, leo mambo yalikuwa ni bomba kidogo upande wa Rutu, alikuwa ashike mkwanja kwani hali yake ilikuwa ni tete.
Ilikuwa ni shughuli ya kuchimba msingi tu ambapo mpaka mida ya saa tano asubuhi, Bella aliaga na kumuachia Rutu jukumu la kuangalia ile kazi kama msimamizi, huku yeye akifanya vikazi vidogo vidogo pale nyumbani kwa Bella
Bella alitoka hadi barabarani akadandia Pikipiki na kuondoka mpaka mjini, halafu akamuandikia sms Nsia,
“Nimeshafika hapa mjini, wewe ukifika njoo moja kwa moja hadi, SS Hotel”
“pouwah” alijibu Nsia…………………
PART 05
Bella alitoka hadi barabarani akadandia Pikipiki na kuondoka mpaka mjini, halafu akamuandikia sms Nsia,
“Nimeshafika hapa mjini, wewe ukifika njoo moja kwa moja hadi, SS Hotel”
“pouwah” alijibu Nsia
Ee bwana kumbe alikuwa anatoka na Nsia waende mjini
Nsia alikuwa amevaa nguo yake nzuri ambayo alikuwa akiiamini kila siku, leo alikuwa anaenda kutembea na mtu ambaye bado sio mpenzi wake maana alikuwa hajamkubalia, lakini hii yote ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ameshatekwa kwa kutumia pesa
Binti alimuandikia Rutu message “mpenzi wangu ndo naondoka, nitakucheki basi nikirudi” alituma lakini Rutu hakujibu kwa sababu alikuwa bize na kazi
Hata hivyo binti alienda hadi kituo cha bodaboda na kupanda pikipiki halafu akaondoka mpaka mjini kwenda kukutana na mtaalam Bella
Alipofika mwisho wa safari alifungua pochi yake na kutoa simu mpya aliyokuwa amepwa na Bella, halafu akaitoa password kwa kuandika neno bella na kutazama sms ilikuwepo ya Bella “Mbona haufiki”
Naye alijibu “nimeshafika niko hapa nje ya SS Hotel”
“ok ingia ndani”
“no bana njoo nichukue” alijibu binti
Bella alitoka nje akamkuta mtoto wa kike yuko pale nje ameng’aa hasa, alikuwa ametupia nguo yake ambayo aliipenda, lakini Bella aliona ni kawaida kwani yeye nguo kama hizo kuziona kwake ilikuwa ni jambo la kawaida kipindi yuko jijini Dar es salaam.
“pole na safari, embu twende ukale” alisema na kumshika mkono wakaanza kuingia ndani na kuketi kwenye meza ya kifahari halafu mtaalam yeye tayari alikuwa ameshaanza kunywa wine
“unakunywaga pombe?” binti alimuuliza baada ya kuona wine ikiwa mezani nyekundu kwenye glass
“hahaha, mara moja moja si unaelewa” alisema binti “agiza chochote unywe, chakula nimeshaagiza wataleta muda sio mrefu”
“mi nataka soda tu”
“ok muhudumu, embu leta soda huko mbona unaona wateja hafu unatulia tu”
“samahani kaka, soda gani” aliuliza
“mwambie aniletee fanta orange”
“Fanta orange bwana”
Wakati wanaendelea kusubiri binti aletewe soda binti alikuwa anaona sana aibu hakuwahi kukaa karibu na mwanaume sehemu kama hiyo
“Nataka ule haraka ukasuke halafu ukachukue nguo nakununulia then urudi nyumbani ok?” alisema mwamba
“mmmh hapana kaka naomba nisisuke baba ataniuliza sana nimepata wapi hela bwana” alisema binti kwa uoga halafu muhudumu akaleta vinywaji
“Oooops, come on wewe ni mtu mzima now usijali utamwambia umepata ofa kwa msusi wako sawa?”
“daaah unanipa mtihani kaka” binti alisema
Bella alimsogezea mkono akamshika kwenye shavu huku akimuangalia kwa ukaribu sana, “usiogope mtoto mzuri kama wewe unapaswa upendeze hadi watu washangae sawa?”
“haya” binti alisema kwa upole huku akiutoa mkono wa Bella uliomshika shavuni
Kijana mmoja alileta nyama pale walipokuwa na kuziweka mezani kisha akaondoka zake, wakaanza kula nyama binti alikuwa anaona aibu sana kula mbele ya Bella, yaani alikula ile basi tu, kati ya vinyango hamsini yeye alikula vitano tu kwa sababu ya uoga wake
“sasa kwanini unanifanyia hivi vyote kaka yangu”
“sikuwa na mpango wa kuoa kabisa mpaka miaka mitano ijayo, lakini kweli Nsia nilipokuona tu hivi nafsi inaniambia nikuoe kabisa ninatamani niwe na wewe maisha yangu yote
“jamani, si nilishakuambia sitaweza kuolewa na wewe ?”
“kwanini sasa au kwa kuwa mimi nina sura mbaya sana Nsia”
“no una sura nzuri lakini mwenzako ameshawahi Bella mbona unanipa mtihani”
“sio mtihani Nsia ninakupenda kweli, naomba please tule haraka halafu tuondoke hapa”
Bella alionekana asiekuwa na haraka ya majibu hali iliyopelekea kukaa na binti vizuri kwa muda huo halafu baada ya kula na kulipa wakatoka na kwenda mpaka duka lang nguo lililokuwa likifahamika kwa jina la Three Legend Classic Pendeza ambalo ni duka la nguo lililokuwa na Hair Dressing Salon
“utanunua kwanza nguo au utasuka?” aliuliza Bella
“nasuka kwanza” alisema
Basi waliingia ndani ya salon ile na binti alishambuliwa na wasusi watatu kwa pamoja ili tu muda usiende sana, Bella yeye aliondoka akaenda mpaka katika guest house moja iliyokuwa ikiitwa Kibiriti Guest House ambapo aliingia akiwa na mwanamke mwingine nje na Nsia
Baada ya saa moja Bella alirudi na alikuta binti ameshapendezeshwa kwa upande wa nywele akawaka akawa bomba mno, alilipa shilingi 60000 binti akiona hivi halafu akamchukua na kumuingiza katika duka la nguo akaanza kumchagulia nguo za kumpendeza binti
Wakati wanachagua simu ya binti iliita akaitoa kwenye pochi na kutazama alikuwa anapiga Rutu akaitazama kisha akamtazama bela macho yakagongana
Bella alijifanya haelewi chochote aliendelea kuchagua nguo za kumpendeza binti lakini pia Nsia hakuthubutu kupokea simu ya Rutu akijua labda atapoteza moto kwa kile alichokuwa anafanyiwa na Bella
“mbona hujapokea simu”
“hamna kuna mtu ananisumbua tu sitaki kupokea simu yake” alisema huku nafsi ikimsuta akiamini anachokitenda sio sawa
Baada ya kuchagua nguo binti alipelekwa katika chumba kimoja cha kuvalia ili apime kama zinamkaa, halafu akishapima moja anarudi na kujionyesha kwa mtaalam, mtaalam akipenda basi ujue kwamba imenunuliwa hiyo
Aliweza kuchukua nguo zake kama sita hivi na viatu vya kutosha halafu mtaaalam akalipa sh laki sita binti akitazama hivi. Walitoka nje huku wakiwa wameshikilia mfuko wenye nguo
“sikiliza binti sasa hapa inabidi wewe upande pikipiki yako na mimi nije baada ya nusu saa ili watu kule wasishtuke, shika hii hapa” mtaalam alisema huku akimkabidhi hela ya nauli
“sawa asante”
“sawa tutawasiliana kwenye simu, likitokea tatizo lolote nyumbani naomba uniambie”
“sawa”
Binti alifunika kichwa chake kwa mtandio ili watu wasione nywele zile, alitoka pale akaenda hadi nyumbani wala hakumkuta baba… alifungua mlango na kuzama chumbani kwake huku akihema kwa nguvu
Ni kweli bado hisia zake zilikuwa kwa Rutu bado hivyo alichukua hatua ya kumwandikia sms “Mpenzi ndo nimerudi now uko powa”
“niko powa sana mpenzi nilijua uko bize ndo maana nilipiga mara moja tu na kuacha”
“sawa mpenzi, uko wapi?”
“nipo kazini hapa kwa Bella nikitoka tu nitakupitia”
“sawa mpenzi”
Baada ya kuongea na simu hiyo Bella naye alifika nyumbani. “Oi oi oi” alisalimia kwa mbwembwe kumbe ni mnafiki tu
“umesharudi?”
“hamna sijarudi” alitania
“hahahahahaa” wote walicheka,
Ile ghafla simu yake ikaita akaitoa mfukoni kumbe aliyekuwa anampigia alikuwa ni Nsia na namba aliisevu hivyo hivyo Nsia, duu alivyoishika tu kwa kuwa alikuwa karibu na Rutu, Rutu aliona jina hilo……