Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

NILIDHANI MGENI, KUMBE MKE MWENZA

(PIGO LA MKE MWENZA)

PART: 13

ILIPOISHIA

Niliamka kisha nikaficha shati lake pamoja na suruali huku nikisubiria kama wamemkamata au kumuona ama la na nini atafanya baada ya kurudi nyumbani.

SONGA NAYO…

Mtima wangu ulianza kuweweseka huku nikiomba sana shoga angu Kapipa asigundue chochote.

Maombi yangu yote, hayakupata majibu pasipo kupata uhakik kutoks kwa baba Furaha ambaye alimkimbiza Majura.

Baada ya nusu lisaa hivi, niliwaza nini nifanye kwa wakati huo maana mwanadamu tunaishi mara moja.

Niliinamisha kichwa changu chini mithili ya kobe anayetunga sheria kisha nikaamua kufanya maamuzi magumu sana.

Nilijifungia chumbani kisha nikaanza kuufinya msosi wangu japo ladha ilipotea kabisa mithili ya mgonjwa wa Malaria.

Baada ya kumaliza kula, gafla vishido vilisikika kwa nje huku vikiambatana na makelele.

Bila kupepesa macho, nilijua ni baba Furaha ndipo nilipofunga mlango wangu vizuri huku nikisikilizia nini kitatokea.

“‘Ndo amefikia hatua ya kunivua nguo!, hee! , ni bora nife kuliko kukaa ndani maana nitamchinja mda huu” alisikika akifoka kweli kama simba aungurumavyo.

Sauti hizo zilinifanya niogope  sana japokuwa nilikuwa na nakala kutoka kwa mwenyekiti.

“Kwani inakuuma nini mme wangu?, umeshaachana naye sasaa wanini?, muache atafunzwa na ulimwengu” Joy alisikika  akimjibu baba Furaha.

“Nimuache nini!, hee!.. unaona ni fair hii..!, nakuuliza hii ni fair?”

“Jamani sasa mbona unanikasirikia mimi?, samahani kama nimekukosea lakini ogopa sana kufanya maamuzi ukiwa na hasira..” Joy alimjibu.

“‘Naomba panga langu hilo!..leo ataniambia, yaani analeta mwanaume mpaka nyumbani kwangu!, walahi naapa kama noma na iwe noma” alisikika akisema.

Maneno hayo yalizidi kuniweka kwenye wakati mgumu sana huku nikitamani mwili wangu uwe kama popo niweze kutoweka gafla.

“‘Nakuomba sana mme wangu …nakuomba please…msamehe na usifanye makosa hayo kwani damu ya mtu haimwagwi hivihivi kama maji..”

Joy aliomjibu.

“‘Hivi angekuwa wewe ungefanyeje!, jaribu kuvaa viatu vyangu afu uone kama vinakutosha!, hii ni dharau na nikiburi. Nitaongea nini mbele za watu kwa aibu hii..!” Baba Furaha alifoka.

“Ni kweli siwezi kuvaa kiatu chako kikanitosha. Hii ni njia nzuri ya kuachana naye kabisa huku upendo wote ukiuhamishia kwangu. Usimtukane wala kumpiga ila yeye ataondoka mwenyewe tena ndani ya mda mfupi” nilimsikia Joy akiongea.

“Amenivua nguo zote afu kibaya zaidi yule jamaa amekimbia na kutuacha bila kumuona hata sura yake!, sasa nataka walau amtaje..”

“‘Nikuulize kitu mme wagu?”

“‘Sawa uliza japo nimepagawa hapa.”

“‘Hivi unanipenda kweli?”

“Sasa unaniuliza swali gani hili!, ebu uliza swali la maana”

“‘Ndo ninamaana yangu wala usinidharau. Nijibu …”

“‘Ndiyo nakupenda..”

“Asante sana mme wangu nami nakupenda. Unapenda kuwa na mie mda wote?”

” Ndiyo napenda”

“‘Asante. Sasa nakuomba utulie tukalale ili mda wote tuwe wote . Nakupenda sana ndo maana sipendi uingie matatizoni. Umenielewa my..”

“‘Nimekuelewa ila sidhani kama jeraha la moyo wangu linaweza pona bila kumfanyia kitu kibaya..”

“‘Yameisha bwana..achana naye huyo mshamba hajui hata kuoga”

Baada ya kusikia kauli hiyo, nilipandwa na hasira kali sana nakutamani nimfate hapohapo nimfumue kabisa.

” Yaani ndo wakuniita mshamba eti sijui kuoga ! Labda sio mimi. Nilidhani kina akili kumbe kiazi” nilijisemea mwenyewe huku moyo wangu ukinung’unika.

********

Kwa mbali ukimya ulitawala kama dakika 2 hivi ndipo niliosikia mlango wa chumbani unafunguliwa vile.

Nilishusha pumzi yangu chini na kunyoosha mikono yangu juu mara baada ya ujumbe wangu kumfikia baba Furaha lakini pia kushindwa kumtambua Majura.

Japokuwa hakumtambua, bado nilibaki na mashaka kwa  Majura nini ataenda mwambia mkwewe akiwa amevaa kaptula pamoja na kaushi tu.

Sasa nilianza kuona hali ya hatari kuishi nyumbanj hapo ndipo nilipoanza kuwaza njia mbadala nami ya kujikomboa.

Baada ya kuona amani imetawala, nilichungulia taratibu hapo sebuleni kupitia uwazi mdogo uliokuwa katikati ya mlango kisha nikaona mambo shwari.

Taratibu nilifungua mlango huku nikiwa natabasamu mara baada ya kumkomesha baba Furaha .

Baada ya kufika sebuleni, nilishangaa kumuona baba Furaha akiwa amekaa huku ameshika tama.

Moja kwa moja, mboni za macho yetu ziligongana huku kila mtu akibaki ameduwaaa…..

PART: 14

ILIPOISHIA

Moja kwa moja mboni za macho yetu ziligongana huku kils mtu akibaki ameduwaa..

SONGA NAYO…

Hakika nilitamani ardhi ipasuke nami nizame kuzimu lakini haikuwezekana .

Nikiwa nimepigwa na butwaa, niligeuza shingo langu pembeni kisha nikatoka nje huku baba Furaha akibaki ameniangalia bila kuongea chochote.

Ukimya wake uliniacha na maswali mengi sana ambayo sikuyapatia majibu yake.

Baada ya kujistiri, nilirejea ndani ndipo nilipomkuta baba Furaha akiwa hivyohivyo.

Sikumsemesha chochote kile na badala yake nilienda kujipumzisha kitandani.

Ni usiku uliokuwa mrefu sana kwani nilikuwa naogopa sana kama anaweza kunifanyia kitu kibaya .

Mungu si athumani, kulipambazuka bila shida yoyote ile ndipo nilipoamka na kuendelea na shughuli zangu za kawaida .

Ilipofika mida ya saa nne asubuhi, niliona nielekee kwa Majura ili nidake habari nini kiliendelea mara baada ya kurudi nyumbani akiwa na kaptula pamoja na kaushi.

“Hodi.” nilibisha hodi kwa tahadhari.

“Karibu shoga yangu” Kapipa alinikaribisha huku akionesha ana jambo moyoni mwake.

(Bila hiyana, niliingia ndani . )

“‘Habari za siku moja mbili..” nikiwa nimejikaza kisabuni, nilimwambia Kapipa.

“‘Ni nzuri kiasi ila kuna majanga shoga yangu..”

“Hee! ..majanga tena! Kuna nini?”

“‘We acha tu yaani sijui nikwambieje” Kapipa aliongea huku akiwa ameshika tama.

“Ebu nambie shoga angu…”

“Hapa nipo nauguza mwenzio…” aliniambia

“Nani tena shoga yangu..? ” nilimuuliza.

“‘Shemeji yako jana kavamiwa mida ya usiku na kikundi cha vijana. Wamemjeruhi na jiwe kisogoni lakini nashukuru anaendelea vizuri” Kapipa kwa masikitiko makubwa, aliniambia.

“Duuh!..’jamani pole sana. Afu mtaa huu hivi vitendo vimeongezeka sana.Ni suala la serikali kuimarisha ulinzi” Nilimjibu huku roho ikinisuta

“Ndo hivo vipi huko mmefikia wapi na kichaa wako? Maana nimesikia makelele yakitokea huko mida ya usiku..” Kapipa aliniambia.

“Mhh nipo lakini hali inavyokwenda ..sijui nifanye nini maana hatuongeleshani wala nini. Nimebahatika kupata nakala kutoka kwa mwenyekiti kuhusu ulinzi lakini bado naishi kwa hofu kabisa…””nilimwambia kwa sauti ya huruma.

“Shoga yangu ngoja nikutone neno moja, siku zote utamu wa asali  hauwezi kulinganishwa na utamu wa muwa mchanga ulioteshwa kwenye tingatinga”.aliniambia huku akitabasamu.

“Mhh unamaanisha nini?” Nilimuuliza.

“Wewe wathamani sana hivo thamani yako haiwezi linganishwa na kitu chochote kile. Ninachokuomba, rudi nyumbani utulie afu waachie waishi watakavyo lakini ndani ya wiki moja atakuja kukufata nyumbani tena kwa faini juu” aliniambia.

“Mhh ni kweli lakini atakuja kweli kunifata au ndo nitawapa njia laini?” Nilimuuliza kwa mashaka

“Kukufata lazima. Yaani ndani ya wiki moja tu!, utanipa mrejesho. Ni bora uondoke ili atulize kichwa nawe utuize kichwa..”

“‘Sawa lakini kuna chakula changu na mizigo yangu nitamuachia nani?”

“Hilo suala dogo, tegeshea ameondoka utoe mizigo yako yote afu ilete nyumbani hapa.”

“‘Sawa shoga yangu ngoja nitafanya hivo japo inaniuma kujenga nyumba yangu tena kwa jasho afu anakuja kukaa malaya..!!”

“‘Shoga najua unaumia lakini  njia niliyokwambia ndo hii..” aliniambia

“‘Sawa shoga yangu, vipi naweza kumuona mgonjwa ili niondoke?”

“‘Amepumzika itakuwa siku nyingine…”

“‘Sawa sasa ngoja nirudi nyumbani nifanye mchakato wa kuhamisha vitu vyangu..”

( Nilimuaga)

Nilianza kurejea nyumbani na nilipofika nyumbani, nilimkuta Joy peke yake.

Nilimuangalia kwa jicho kali sana huku nikitamani kummeza mzimamzima lakini niliamua kujizuia ili kuepusha majanga.

Bila kuchelewa, nilianza kuhamisha mizigo yangu taratibu mpaka nikafanikiwa kuzihamisha zote.

Nilibahatika kukutana na vijana wawili ambao niliwapatia debe moja la karanga na kunisaidia kuzibeba mpaka kwa Majura.

Wakati napitapita mtaani, nilisikia kwa mbali habari za kufumaniwa kwangu kutoka kwa watoto wadogo sana waliokuwa na miaka kama mitano hivi.

Asee niliogopa sana huku nikiona kama siri inaenda kufichuka.

Licha ya hali dhuruba hiyo, nilisonga mbele mpaka kwa Majura.

Nilitunzà mizigo yangu kisha nikamuaga shoga yangu.

Baada ya kufika nyumbani, nilijiandaa harakaharaka kisha nikambeba Furaha  mgongoni kuelekea nyumbani.

Nyumbani kulikuwa na mwendo kidogo hivo ilinilazimu kupanda bodaboda.

Mnamo mida ya saa 11 hivi, nilifika nyumbani na kupokelewa na mama ambaye alikuwa ameketi kwa nje huku akisuka mkeka…..

PART: 15

ILIPOISHIA

Mnamo mida ya saa 11 hivi, nilifika nyumbani na kupokelewa na mama ambaye alikuwa ameketi kwa nje huku akisuka mkeka…..

SONGA NAYO

Wahenga wasema mtoto hakui kwa mama ndivyo nilivyopokelewa na mama.

Baada ya mda, mzee wangu aliwasiri nyumbani kisha nikamsalimia lakini sikuweza kuwambia chochote kwa wakati huo.

Ilipofika mida ya saa 2 za usiku, nilijongea moja kwa moja mpaka jikoni kisha nikaanza kupiga story na mama aliyekuwa anamalizia kumenya ndizi.

Nilifikia hatua nikataka kuongea lakini niliogopa wapi nianzie ndipo nilipoamua kukaa kimya na kuongelea tumboni.

Nikiwa nimeketi kwenye kigoda, mama alinitazama kisha akaniuliza

“Mbona unaonekana mwenye mawazo?”

“Kwani umenionaje mama!” Nilishangaa kidogo.

“‘Unaonekana hii siyo kawaida yako mwanangu” aliongea huku akinitazama.

“Mama hapa nilipo nina matatizo..” nilikatisha..

“‘Matatizo gani tena!” Aliweka kisu chini kisha akanitazama kwa mshangao.

“Mme wangu ameoa mke mwingine. Yaani ninaishi bila amani kutokana na vituko ninavyofanyiwa” niliongea huku machozi yakinilengalenga.

“‘Hee! tabia kaianza lini tena! , mbona alikuwa mtulivu na mwenye heshima!, siyo bure atakuwa kachezewa” mama alitikisa kichwa.

“‘Hakuna chakuchezewa mama ila ameanza kubadilika mda” nilimjibu.

“Mhh …sasa amekufukuza au umtoka mwenyewe..” aliguna

“‘Nimetoka mwenyewe ili aje nyumbani kunifuata” nilimjibu huku nikihesabu vidole vyangu vya mikononi.

“‘Hapo umefanya cha maana, wewe tulia hapa nyumbani, atakuja mwenyewe”

Baada ya kuniambia hivo, aliniacha jikoni kisha akasikika akiongea na mzee kwa sauti ya chini.

Nilijitahidi kutega masikio lakini sikupata picha nzima japo niliwasikia wakiliongelea jambo langu.

Badaye chakula kilikuwa tayari kisha tukapata cha mtume.

***

Maisha yalindelea nyumbani hapo huku nikisaidiana na mama katika shughuli nzima ya kilimo.

Wiki ya kwanza, ilikatika bila kuona dalili yoyote ya baba Furaha akija nyumbani.

Hali hiyo, ilizidi kunichanganya na kunipa maswali mazito kichwani mwangu.

“‘Ina maana amegairi kuja nyumbani au anaogopa?” Nilijiuliza kimoyomoyo.

Kwakuwa nilikuwa nyumbani, sikuwa na hofu yoyote ile kwani nilikuwa nakula na kulala vizuri..

Kilichokuja kuniuma, ni habari ambazo zilianza kuzagaa mtaani kuwa nimeshindwa ndoa na nipo najiuza kwa waume za watu.

Kuna kidada kimoja ambacho kilikuwa na sura kama limao!, asee nilitamani kukibutua lakini nilikaa kimya licha ya mdomo wake mchafu wa kunichafua.

**

Mwezi wa kwanza ulikata bila kuonekana, wapili, watatu, wanne , ndipo nilipoona dalili za kujifukuza mwenyewe kwenye nyumba yangu.

Siku ya jumamosi jioni, nilienda kumtembelea mama mdogo kisha nikamsimulia kisa kizima.

Mama mdogo alishika tama kisha akasema,

“Mwanangu!..,nakuita tena Mwanangu..!,siku hizi ukitoka kwenye mji wako usitegemee mme akufate!, sio aibu kama itawezekana rudi nyumbani kwako maana kuendea kukaa nyumbani kunachelewesha maendeleo yako”

“Sasa nitaedaje mwenyewe bila kunifuata?, huoni kama atazidi kunidharau?” Nilimuuliza.

“Hapana, hawezi kukudharau kwani kama ni kujifunza atakuwa amejifunza”

” Sawa asante ngoja nisubiri mdamda kidogo huenda atakuja”

“Kama angekuwa wa kuja, asingemaliza hata wiki 1”

Maneno hayo niliyaweka kichwani mwangu huku nikiyatafakari kwa kina.

Tuliagana nami nikarudi nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani, sikumwambia mama juu ya kile nilichoambiwa kwani ningeonekana mchonganishi kwa mama mdogo .

Mwezi wa 5 ulikatika na hatimaye nusu mwaka ulikatika bila baba Furaha kuja nyumbani.

Siku moja mida ya saa 11 jioni, nilimwambia mama juu ya hatima yangu yakutaka kurudi nyumbani kwangu.

Mama alipokea taarifa hiyo kwa matumaini lakini alipomwambia mzee wangu, alikataa katakata.

“‘Unaenda huko kufanya nini!, sijafa bado niko hai hivyo sijafikia hatua ya kudharauliwa namna hii. Kama ametenda kosa afu hataki kuja nyumbani, si anaweza hata kukua?, . Tulia nyumbani ” mzee aliongea kwa sauti ya ukali kidogo.

“‘Mme wangu sasa ataendelea kukaa nyumbani mpaka lini?. Hii ni aibu kwetu ..” mama alimjibu mzee

“Hee! Kwani hapa si kwao, aibu ipi!, hakuna aibu mtoto kuishi nyumbani”

“‘Jinsi wanavyotuzungumzia huko nje afu kaacha mali zake..”

“‘Nasema kwamba, abaki atulie na kama hatokuja hapa, asiende kabisa. Nimemaliza”

Baada ya kuongea hivo, wote tulikaa kimya huku tukiwa hatuna chakuongea.

Maisha yangu yalianza kuwa ya wasiwasi huku nikipanga nini cha kufanya.

Mama aliniletea dawa ambayo ilikuwa imesagwa na kuwa kama ugoro kisha akanimbia,

“Hii dawa utaiweka kwenye chai ya mme wako mara baada ya kuitenga kwenye kikombe” aliniambia.

“‘Inafanya kazi gani?” Nilimuuliza.

Kabla hajanijibu, alinikatisha kwa kufungua dawa nyingine kisha akaniambia’,

“Hii hapa utaiweka kwenye chai ya mke mwenza ila hakikisha mtoto wako asithubutu kuonja wala wewe..” alinielekeza .

“Sasa nitaiwekaje wakati hatupati hata kidogo?, afu pia niambie zinafanya kazi gani?”

“‘Suala la kutopatana ni rahisi kulitatua, ukifika wasalimie wote tena kwa heshima. Ndani ya mda mfupi utaona matokeo. Kuhusu kazi za hizi dawa, ningekwambia ila masharti yanakataza.”

“‘Mhh sawa mama ila lakuomuomba radhi mke mwenza ni gumu sana kwangu.”

“‘Nimeshakwambia, jifanye mjinga ufanikiwe ulichokipanga..” mama aliniambia.

Mambo yote yalikaa sawa bini sawia huku nikisubiri mda upi mzee hatokuwepo nitoroke kurundi kwangu.

Ilikuwa mida ya saa 4 asubuhi siku ya jumatano mara baada ya mzee wangu kuelekea shamba, ndipo nilipofungasha kila kilichochangu huku nikishirikiana na mama ili nirudi kwangu.

Kila kitu kilikaa sawa kabisa..

“Zingatia maelekezo kama nilivyokwambia, ukikosea shauri yako. Hasa hiyo ya mke mwenza kuwa makini”

“‘Sawa mama nitafanya hivo..” niliitikia na wakati huohuo, bodaboda alionekana nami nikamsimamisha na safari ya kurejea kwangu mara baada ya miezi 7 ikaanza…

“‘Safari njema…”

“‘Ayaa bye…” nilimpungia mkono huku boda ikitembea taratibu….

JE NINI KILICHOENDELEA?

PART: 16

ILIPOISHIA

Nilimuaga mama na kuanza kuelekea nyumbani kwangu mara baada ya miezi 7

SONGA NAYO…

Dereva bodaboda, aliongeza mwendo kidogo mpaka nikaanza kuogopa mara baada ya miti kuonekana ikirudi nyuma kwa kasi sana.

Nilipaza sauti kwa dereva huyo ndipo alipopunguza speed.

Mnamo mida ya saa 6 za mchana, niliwasiri nyumbani nakumkuta baba Furaha akiwa amekumbati katoto kachanga ambako kalikuwa na miezi kama minne hivi au mitatu.

Nilishutuka kisha nikamsogelea na kumsalimia,

“Shikamoo mme wangu” alikaa kimya huku akizidi kunishangaa kisha akasema,

“‘Ni wewe au nimekufananisha”?

“‘Ni mimi kwani  nimebadilika?” Kwa tabasamu nilimjibu huku Furaha akiwa anashangaa katoto hako.

“‘Umenene sana..” aliongea huku akinitazama.

“‘Mhh..mbona nipo kawaida..!” Niliguna kwa tabasamu.

“‘Karibu tupo..” alinikaribisha.

“‘Asante..”

Niliingia ndani huku nikiwa natetemeka kwenye moyo wangu.

Mara baada ya kuketi kwa dakika kama 3, Joy alitokea jikoni  kisha akanipita kama vile hanioni.

Nilipata mtihani mzito wa kumsemesha kwani mda wote alionesha kunidharau.

“‘Baba Zawadi naomba mtoto nimnyonyeshe” Joy aliongea.

Baada ya kauli hiyo, nilijua moja kwa moja kuwa kapata mtoto jina lake Zawadi.

Nilipiga hesabu za mda aliokaa na baba Furaha kisha nikagundua kuwa alikuja na ujauzito tena mkubwa.

Nilichungulia kwa jicho la chongo lakini kusema ukweli mtoto alikuwa mzuri sana tena sana.

Nilishanga kuona wanapata mtoto mzuri kiasi hicho japo sikuongea hadharani.

Nilinyanyuka taratibu kisha nikaelekea chumbani kwangu ndipo niliposhangaa kuona wanalala kitandani mwangu.

Kwakuwa nilikuwa sijafanikisha lengo langu, nilitoka na kuingia chumba cha wageni na kukuta kagoro ka nchi 2 na nusu kama wanavyolalia wanafunzi wa hostel.

Niliweka mizigo yangu kisha nikafanya usafi kwani palikuwa pamejaa vumbi kila sehemu.

Baada ya kumaliza usafi, nilirudi sebuleni nakuanza kuongea na baba Furaha huku nikihisi njaa kweli.

Mara kadhaa mama Zawadi alijipitisha akiwa amenuna huku akiewa anaonesha hali ya hasira.

Kwenye mida ya sas 7 na nusu mchana, chakula kilikuwa kipo tayari lakini cha maajabu sikupata msosi.

Baba Furaha aliniita kisha tukala kwenye sinia moja huku mama Zawadi akiwa anaangalia kwa jicho kali.

Baada ya kumaliza kula, nilijitoa ufahamu na kumfata mama Zawadi kisha nikamsalimia.

“‘Habari za siku nyingi”

“‘Ni nzuri tupo karibu” alinijibu japo uso haukuonesha furaha.

” Ohh..! Hongera kwa kupata mtoto, anaitwa nani?” Nilimuuliza

“‘Anaitwa Zawadi..”

“‘Jina zuri…” niliongea kisha nikamuomba walau nimshike kidogo.

Alianza vizingizio kuwa atanikojolea lakini nilimhakikishia kuwa siyo shida.

Kwa mara ya kwanza, nilimshika mtoto huyo aliyekuwa anatabasamu.

Badae nilimkabidhi mtoto wake nami nikamuaga baba Furaha kuwa nafika kwa jirani

Baba furaha alionesha kukataa huku akitaka tukapumzike chumbani tena mda wa mchana.

Nilitamani kukubali lakini nilimwambia badaye naye akanielewa.

Kwenye mida ya saa 10 jioni hivi, nilianza safari ya kuelekea kwa shoga yangu Kapipa ili nikachukue mizigo yangu.

Baada ya kufika, nilimkuta Kapiapa akiwa ameketi kwa nje.

Aliponiona, aliingia ndani na kutoka kwa speed kali huku akiwa ameshika rungu lenye kilo kama 5 hivi.

Asee bila kuuliza wala kupoteza mda, niligeuka na kutimua mbio kali sana  huku kwato zangu zikigusa kwenye kisogo changu.

Nikiwa nakimbia kwa kuhema, nilijikuta najikwa chini na kudondoka ndipo nilipochubuka kwenye goti langu la kushoto pamoja na kiwiko cha kulia.

Niligeuka huku nikiwa nakiona kifo mbele yangu.

Kapipa alirusha rungu hilo na kutua pembeni kabisa mwa kichwa changu.

Asee sijui nilipata wapi nguvu kwani nilijikuta nimeshaamka huku mbio zikiendelea.

Ndani ya dakika 5 , niliweza kumuacha kwa umbali mkubwa sana kiasi cha kumfanya akate tamaa.

Nilipunguza mwendo na kuanza kutembea kuelekea nyumbani huku nikiwa kama ningeenda na Furaha , ningekamatwa kiurahisi kabisa.

” Sasa kwanini amenifanyia hivi?, ! Ina maana siri imefuchuka au kuna kosa lingine? Nilijiuliza huku nikiwaza..

Sikupata jibu la moja kwa moja huku nikiwa nahema.

Nilikunja kona na kuelekea kwa jirani yangu nilipokuwa nimetunza debe 3 za mahindi maharage na karanga.

Bahati nzuri nilimkuta nyumbani kisha tukasalimiana na kunipatia mizigo hiyo.

Uzito wa mizigo hiyo, nililazimika kutoa 2000 kwa vijana wawili ambao walinisidia kubeba.

***

Baada ya kufikisha mzigo huo nyumbani, niliuweka sehemu ya wazi na kumwambia mama Zawadi asipate shida yoyote ya chakula kwani kipo chakutosha..

Alishukuru sana huku akiwa haamini kabisa kwa upendo wangu kwani walikuwa hawana chakula kabisa kwa ndani.

***

Usiku baada ya kumaliza kupata chakula cha pamoja.

Nilienda kulala kwenye kagodoro kangu ka nchi 2 na nusu huku roho yangu ikiwa inaniuma sana.

Nikiwa nimeanza kupata usingizi kwa mbali, gafla nilisikia mtu anagonga mlango wa chumbani kwa sauti ya chini.

Nilishutuka kisha nikaamka na kufungua mlango.

Ile nafungua mlango, baba Furaha alingia ndani huku akisema,

” Usiogope ni mimi”

” Mhh.. :” niliguna.

” Mbona waguna? Aliniuliza huku akiwa amenikumbatia na kunishika kifuani mwangu.

“Hapana hakuna shida” nilimjibu huku nikihisi kama ananitekenya kwenye maembe yangu.

Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka huku nikihisi kama joto linaongezeka kwa kasi sana.

Taratibu alinishika na kunilaza kwenye kigodoro hicho kisha akataka kunitoa kanga niliyokuwa nimejifunga.

” Unataka kuamfanya nini my?” Nilimuuliza huku nikiwa nashusha miguu kama mbuzu aliyejinjwa na kukaribia kukara roho.

” Mhh..! , sogea basi..” aliguna kisha akanivuta..

Wakati  ananivuta, gafla mlango ulisukumwa kisha sauti ikasikika,

” Baba zawadi nakuomba mara moja nikwambie jambo”  mama Zawadi aliongea.

Baba Furaha aligeuza shingo lake na kuonekana ameduwaa .

” Subiri kidogo nakuja kama dakika 10″ alimjibu.

” Hee ! Kwani unafanya nini humo? ” dakika 10 nikusubirie wewe, heloo makubwa …” aliongea kwa sauti ya juu.

Baba Furaha aliniachia taratibu kisha akaninong’oneza sikioni,

” Usifunge nakuja dakika 1…”

Sikumjibu chochote kile wala kuonehmsha ishara yoyoye lakini moyoni nilichukia sana tena sana..

PART: 17

ILIPOISHIA

Nikiwa nimelala huku baba Furaha akiwa amenikumbatia, gafla mama Zawadi ( Joy) alisikika akimuita mlangoni…

SONGA NAYO…

Baba Furaha baada ya kusikia sauti ya Joy, alianza kuniachia taratibu huku akidai nisifunge mlango .

Sikumsemesha chochote huku hasira ikiwa imenipanda mpaka kooni.

Sikuona raha wala sababu ya kuwa na mme kama anapata ujasiri wa kuniacha katika hali mbaya sana.

Baada ya kuondoka, mwili wangu haukupoa haraka yaani niliteseka huku nikiapa kumfanyia kitu kibaya mama Zawadi na ikiwezekana baba Furaha.

Kama alivyoniambia, sikufunga mlango mpaka mida ya saa 7 usiku bila kuona dalili yoyote .

Kwa hasira niliifunga mlango huku nikisibiria mtu agonge lakini wapi.

Nilijikaza hivohivo mpaka hapo mwili wangu uliporudi kwenye hali yangu ya kawaida.

Mnamo mida ya saa 12 za alfajiri, nilifungua dawa niliyopewa na mama na kuiandaa vizuri ili ifanye kazi.

Ilipotimia mida ya saa kamili, niliaza kuchemsha chai na walipoamka, walikuta chai tayari.

“‘Karibu chai mdogo wangu” nilimwambia Mama Zawadi aliyekuwa ameweka mwaki mdomoni huku amejifunga kanga shingoni na kuishia magotini

Aliitikia kwa kuinua kichwa . Moyo wangu ulifurahi japo furaha yenyewe ilikuwa ya mashaka kwani mama hakuniambia dawa inafanya kazi gani.

Bila kuchelewa, nilimimina dawa hiyo kisha nikaikoroga mithili ya kahawa iliyosagwa.

Baada ya kumaliza, chai hiyo niliiweka pembeni kisha nikamimina dawa nyingine kwenye kikombe kikubwa ambacho alikuwa anakipendelea sana baba Furaha.

Kwa masharti niliyokuwa nimepewa, sikuruhusiwa kuonja hata ladha yake hivo hicho kiliniweka kwenye mashaka.

Baada ya mambo yote kuwa tayari, niliweka karanga kwenye kisosi kisha nikamuita baba Furaha aliyekuwa kwa nje huku akionekana kachoka

“‘Baba Furaha karibu chai iko tayari..” nilimwambia huku nikitabasamu.

“‘Asante sana ndo maana nilikuwa nakumis kila siku. Mama Zawadi unaona, saa moja chai tayari …”

“‘Kwahiyo unamwambia ili iweje!, basi mpelekee mashitaka yote kwake tuone utapata nini” Mama Zawadi aliongea huku akiwa amekunja uso.

“‘Jamani msigombane, sisi sote ni kitu kimoja. Tuishi kwa amani” niliongea kwa tabasamu.

“‘Sasa anaongea ili iweje!.” Mama zawadi alisonya.

“‘Yaishe basi …” baba Furaha aliongea kisha akaanza kupata chai.

Baada ya kumeza fundo mbili, nilitetemeka huku nikimuongalia usoni kwa kuhofia ladha ya chai.

Nikiwa katika taharuki hiyo, baba Furaha alishindwa kuzuia hisia zake mpaka akajikuta anangea.

“Aisee tangu nianze kunywa chai, ya leo ni tamu tena tamu yaani ladha yake inanukia vizuri. Mke wangu hongera kwa kupika kiasi hiki.” Aliongea huku mama Zawadi akiwa amemuangalia huku mkono mmoja umeshika kikombe cha chai.

” Asante sana kwa kushukuru lakini mbona huwa napika hivi kila siku?” Nilimuangalia kwa macho ya mwisho wa mwezi.

Kitendo hicho kilimfanya Mama Zawadi anyanyuke na kuacha chai bila hata kuionja huku akionekana mwenye kukasirika sana.

“‘Dada unaenda wapi?, karibu chai bwana  .Achana na huyu maana anapenda sana utani. Mzoee ndo huwa yupo hivi…” nilimvuta kanga Mama Zawadi.

“‘Utani gani huu!, anafanya makusudi. Mda wote yupo na mimi sijui anataka nini. Endelea hivohivo” aliongea kwa hasira.

“‘Kwani nimekukosea nini?” Alimuuliza.

Mama Zawadi hakumjibu chochote na badala yake aliishilia chumbani.

Nilichukua chai hiyo na kuimimina kwenye thermosi ili isipoe huku nikihakikisha masharti yanafuatwa.

Baba Furaha baada ya kumaliza chai yake, aliomba nimuongezee chai na ikiwezekana nimpe hata niliyomtunzia mama Zawadi.

“Niongee maana chai ni tamu sana” aliongea huku akiwa amenua kikombe chuu kuelekea mdomoni.

“‘Mhh..jamani imebaki ya mama Zawadi mme wangu..” nilimjibu.

“‘Si amesusa!.weka tu atajua mwenyewe”

“Hapana mme wangu sio vizuri. Anahisi njaa kama wewe tena ananyonyosha..”

Baada ya kumwambia neno hilo, alikaa kimya kisha akatoka kwa nje.

Nilibaki na mtihani mzito sana wakuhakikisha mama Zawadi anakunywa chai hiyo iliyokuwa imewekewa dawa tayari.

Bila kupepesa macho , nilimfuata mpaka mlangoni kisha nikamuita.

“Dada karibu unywe chai. Ameshaondoka huyo msumbufu…'”

“Asante sana sina hata hamu maana kashanivuruga mda huu..” alinijibu.

“‘Hapana bwana, njoo upate chai ni tamu sana”

“‘Hivi haijapoa kweli..?”

“‘Hapana nimeiweka kwenye thermosi”

“‘Ayaa naja..”

Baada ya kunijibu hivo, nilifurahi sans kuona lengo langu linataka kukamilika.

Ndani ya mda mfupi sana, alifungua mlango kisha akaketi kwenye stooli ili apate chai.

Alimimina chai kwenye kikombe lakini kabla hajanywa, niliingia chumbani ili kusikilizia atasemaje kuhusu ladha maana zilikuwa dawa mbili tofauti.

Nikiwa chumbani, nilisikia sauti kama ya Furaha akiongea na mama Zawadi hapo sebuleni.

Nilishutuka na kufungua mlango gafla na kumkuta Furaha ameshikilia kikombe kidogo cha chai huku akikohoa kweli.

“‘Hee ! Amekuwaje huyu..” niliongea.

“‘Kanywa fundo kama 3 za chai ndo naona anakohoa hivi, sijabahatika kuonja chai hii au uliweka pilipili? Ebu onja tuone…”

Baada ya kuniambia hivo, nilibaki nimeganda kama barafu huku nikiwa sielewi kwani masharti aliniagiza siruhusiwi hata kuonja….

JE ILIKUWAJE?

PART 18

ILIPOISHIA…

Nilimuona mwanangu Furaha akiwa anakohoa kweli huku mama Zawadi akiwa naye anashangaa kumuona hivo.

SONGA NAYO….

Ndani ya dakika 5, hali ya Furaha ilibadilika gafla hasa pale alipoanza kutapika mfululizo.

Macho yalinitoka huku nikiwa sijui nini nikifanye kwa mda huo,

” Kwani umempa nini?” Nilimuuliza mama Zawadi huku machozi hakinilengenga machoni mwangu

” Sijampa chochote tofauti na chai hii. Ebu jaribu nawe kunywa maana sijaonja” aliniambia huku akinitazama .

Baada ya kuniambia hivo, sikutaka kuongeza neno lolote wala kujibizana naye.

Niligeuza shingo langu na kwa hasira nikaimwaga chai hiyo mbele yake huku nikiwa nimekasirika..

” Sasa mbona umeimwaga?” Aliniuliza.

” Niache kwanza, naomba nisaidie nimuite bodaboda nimkimbize hospitali”

” Sawa ila mhh…” aliguna.

Baada ya mda wa dakika kama 10 hivi, nilifika nyumbani hapo nikiwa na boda ndipo nilipombeba Furaha aambaye alikuwa amelegea kwelikweli.

Nilipanda kisha safari ikaanza lakini baada ya dakika kama 5 hivi, Furaha alinitapikia sana kiasi cha kumfanya dereva asimame ili nimpanguse.

Alisimama kama nilivyomuomba  ndipo nilipomfungua.

Cha maajabu huku nikiwa siamini kabisa, niliona kinywa chake kiko wazi huku akiwa ametoa macho bila kufumba.

” Hee! mwanangu …mwanangu..!” Niliita huku nikimgusa kwenye kifua ili kuona mapigo ya moyo lakini yalikuwa yametulia tuli.

Dereva aliegesha pikipiki kisha akamuangalia mtoto Furaha ndipo aliposema,

” Pole sana. Mtoto kashatangulia mbele ya haki sasa kifuatacho unatakiwa ujikaze kiume na ubebe mwili wa mtoto mpaka nyumbani ili kuepusha gharama”

Aisee sikuamini kabisa, niliangua kilio kikali sana lakini dereva yule alinizuia.

Kwa uoga mkubwa sana, nilimbeba mwanangu kisha tukarejea nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani, nilimkuta  mama Zawadia pamoja na baba Furaha wakiwa wanena jambo.

Bila kuchelewa, niliangua kilio kikali sana ambacho kiliwashutua.

” Hee! Kuna nini!” Baba Furaha aliongea kwa mshangao.

” Furaha…Furaha hatunaye tena..yuuh…hooo…” nilipiga kelele .

Baba Furaha alinyanyuka haraka na kuuchukua mwili wa Furaha ndani.

Kilichofuatia hapo sikuweza kukijua kwani nilikuja kupata ufahamu na kukuta tayari mwanagu kipenzi ameshalazwa kwenye nyumba yake ya milele.

Niliumia sana na kujiuliza hiyo dawa alonipa mama ilikuwa na nini?, sikutaka tena kuka nayo ndipo nilipoibeba kwa siri kisha nikaitumbukiza chooni.

Baada ya mwezi mmoja tangu mwanangu apoyeze maisha, baba Furaha naye alianza kuwa kama mtu asieye na akili nzuri.

Alianza kutokwa na udelele mdomoni kama mtoto mdogo huku mda mwingine akiwa anacheka mwenyewe kama kichaa.

Asee hali iloniwia ngumu sana kwani sikuwa na sehemu ya kukimbilia mara baada ya kukumbuka jinsi nilivyotoroka nyumbani mara baada ya kukatazwa na mzee.

Habari za chinichini, zilianza kusambaa mtaani kuwa mi mchawi nimemtoa kafara mtoto wangu huku nikitaka kummaliza mme wangu na mke mwenza..

Asee, nilianza kuwa kwenye wakati mgumu sana huku nikiwa sijui nini hatima ya yote hayo.

Katika hali isiyo ya kawaida, Mama Zawadi alitoroka nyumbani hapo mara baada ya baba Furaha kuanza kuugua ugonjwa wa ngozi ulimfanya ngozi kuwa na vipele .

Aliacha mtoto mchanga sana mwenye miezi 8.

Asee mme wangu hakuwa na akili tena na sina cha kumpa huyo mtoto.

Baada ya kuwaza nini nifanye, niliamua nimlee mtoto huyo kwa kumnunulia maziwa ya ng’ombe kutoka kwa jirani.

Siku s nyigi, hali ya baba Furaha ilizidi kuzorota sana lakini akili yake ilirudi sawa ndipo aliposhangaa kumuona mke wake kakimbia na kuacha mtoto.

Aliinamisha kichwa chake chini kisha akamwaga chozi mbele yangu na kuniambia maneno haya,

” Mke wangu, najua nilikukosea sana tena sana, nakuomba umtunze mwanangu maana ni damu yangu mimi mda si mefu natangulia mbele ya haki. Sikuwahi kujua kama unauvumilivu mkubwa kiasi hiki kwangu licha ya mataizo haya niliyonayo..”

Maneno hayo yalinichoma moja kwa moja mpaka moyoni mpaka nikajikuta namwaga chozi kama mtoto mdogo.

Kwa hasira kali nilizokuwa nazo mara baada ya kumpoteza mwanangu , sikuwa na matumaini tena na mama.

Mda ulisonga na baba Furaha akawa hivyohivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ndipo nilipochukua nafasi hiyo kumuomba msahama shoga yangu Kapipa huku nikidhani huenda ndo anatenda mambo nyumbani kwangu.

Aliaanza kwa kukataa kuongea na mimi lakini badaye alikubali mara baada ya kumpigia magoti mbele ya Majura.

Haikuwa rahisi lakini niliongea ili kuweka mambo sawa japo Majura alipata wakati mgumu sana.

Ndani ya mwezi mmoja, tulianza kuongea kama mwanzo ndipo aliponiambia nimpeleke kwenye maombi.

Mnamo siku ya jumamosi mida ya saa 2 za asubuhi, tulikodisha bodaboda kisha akatupeleka kanisani.

Bila aibu, nilimfuta mchungaji kisha nikamueleza kila kitu ndipo aliponimwagia maji ya upako na badaye nikatubu.

Baada ya hapo, alianza kumuombea baba Furaha na ndani ya dakika 1 tu, alidondoka chini na kuanza kutupatupa miguu.

” Toka…toka…kwa jina la mtotowa bwana nasema tokaaa!..tokaaaa!!..tokaaaa!!”

Kwa mshangao mkubwa, baba Furaha alizinduka gafla na kuonesha tabasamu.

Nilijikuta natabasamu kisha nikamshukuru mchungaji.

Tulirudi nyumbani japo hakuwa vizuri kutokana na hali ya kuugua kwa mda mrefu.

Baada ya mwezi mmoja, alirudi kwenye hali yake ya kawaida huku akiwa ananiheshimu sana .

Kwa kuwa hali ilikuwa vizuri, nilirudi nyumbani kumuomba msamha mzee wangu kisha nikamsamehe mama lakini nikaapa asinipe dawa nyingine kwani suluhisho la matatizo ni Mwenyezi Mungu.

Maisha yaliendelea na tulifanikiwa kupata mtoto mwangine wa kiume anayeitwa Gabriel.

Miaka mitano mbele, habari zilianza kuzagaa kuwa mama Zawadi aliolewa na Tajiri kwelikweli ndipo nilipofuatilia na kukuta ni kweli.

Mme wangu alijua lakini alisema,

” Mke wangu wewe ndo mtu pekee kwangu ambaye nitakuheshimu na kukuoinda kwa gharama zote”

Kauli hiyo iliniacha na tabasamu mwanana kisha wote tukakumbatiana.

Giza lilizizima na nuru ikaangaza..

…….MWISHO……..

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!