MLENDA WA PORINI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA…
Kauri hii, aikumpa matumini mgonjwa peke yake, ata wakina Zuleiya na baba yake pia, iliwapa matumaini makubwa, ya mama Zuu kuwa salama, “aya mama sukuma kwanguvu” alisikika Shadya.
Endelea……
Naaaaam!, aikuchukuwa ata dakika, kabla ya kusikia sauti ya kitoto kichanga, kikiangua kilio cha kushangilia, ujio wake wa duniani, na kwa ujuzi aliokuwanao Shadya alimaliza taratibu zote za uzalishaji.
Nusu saa baadae walikuwa njiani, wanaelekea mjini, huku mschana huyu, mrembo ambae akujari ya kuwa anasafari ya kwenda Dar_es_salaam asubuhi ya siku ile, aliekuwa amelowa vibaya sana.
Alitoa baadhi ya nguo zake kwenye begi, kumfunika mtoto, kumzuwia baridi, pia alitoa kanga kwaajili ya mama mzazi, na pia alitoa gauni kwaajili ya Zuleiya, ambae nguo zake zilikuwa zimelowa kama baba yake.
Lakini pia saa kumi na moja na nusu, walipofika mjini, waliwapeleka hospital, na wakapokelewa vizuri, kwa heshima ya msichana yule, ambae ni mtoto tajiri mkubwa, bwana Radhaq, maarufu kwa jina la mwarabu.
Kabla Shadya ajaondoka kuelekea stendi, ambako angepanda bus, kuelekea Dar_es_salaam, ambao alikuwa anamalizia mwaka wa mwisho wa degree ya udaktari.
Alimpatia baba Zuu tsh elfu kumi, ambayo ingewasaidia, kwa gharama ndogo ndogo za matibabu, kabla awajalihusiwa siku chache sijazo, kurudi kijijini, huku mtoto akiwa salama.
“dada natamani siku moja, nikufanyie kitu ambacho, utakuwa unakiitaji sana, iwe kama asante yangu kwako” alisema Zuleiya, ambae kwa hali yake aliona kuwa hapakuwa na kitu anaweza kumpatia Shadya, kama asane kwake.
Pia hapa kuwa na kitu ambacho, Shadya angeomba kwake, kama msaada, “lakini pia, ikitokea kuna kitu, unahisi unaitaji toka kwangu, usisite kunieleza, na kuhaidi, kama ninauwezo nacho nitakupatia” alisema Zuleiya, akiamini kuwa, binadamu tunaishi kwa kutegemeana.
“Usijari mdogo wangu, tuombe uzima” alisema Shadya kabla ya kuondoka zake, uku kila mmoja wa, akuwa na wazo la kuwa, kama kuna siku watakuja kukutana.
Naaaaaam!, sasa kwa msaada wa taa, za nguvu ya umeme, tuna weza kumwona vizuri mschana Zuleiya, ambae kiukweli, licha ya kutokea katika kijiji cha mbali sana, tena ni kijiji kidogo cha mashambani, yani kijiji cha Mbendu.
Lakini kila mwanaume alie mwona, alikubari mwenyewe, kuwa ni mschana mwenye uzuri wa hasiri, utofauti ulikuwa ni kwenye mavazi, ambayo yalikuwa yamechakaa kidogo.
Zuleya ana tafuta sehemu ya kuoga, anaoga na kubadiri nguo, akivaa zile ambazo alipewa na mtoto wa mwarabu, yani Shadya, kisha anatoka na akimpisha baba yake, ambae anaoga na kuvaa nguo zake zile zile, ambazo alijaribu kuzikamua maji kidogo.
Kila mmoja anatafuta sehemu nzuri yenye utulivu, na kuswali swala ya alfajili, baada ya hapo wanatulia kwenye mabenchi, karibu na sehemu ya mapokezi.
Mara kwa mara wawili awa walipeana zamu ya kwenda, kumtazama mama Zuu, ambae alikuwa amelala wodini, na kitoto kihanga cha kiume, ambacho pia muda mwingi kilikuwa kimelala.*******
Siku ya kwanza ilipita vizuri, mama akiendelea kupata baadhi ya sindano za chanjo kwaajili ya mtoto, na pia kumwangalia mama mtoto, kama wanaendelea vyema, ukichukulia ya kuwa mama alikua amechoka sana.
Zuleiya na baba yake, walijitaidi kubana matumizi, kwenye ile fedha waliyo ipata, ilikurybza fedha hiyo kwaajili ya malipo ya mwisho, na pia walitakiwa kutunza fedha, maana awakujuwa lini wataluhusiwa kuondoka.
Sababu baada ya vipimo kadhaa, ilibainika kuwa mtoto, alikuwa na mafua makali sana, yaliyo sababishwa na baridi kali aliyoipata mtoto, wakati anazaliwa, kwenye mvua kali na upepo, hivyo walitakiwa wakae hospital, mpaka mtoto apone.
SEHEMU YA SABA
Kukaa hospital aikuwa shida kwao, kikubwa ni kwamba, walikuwa na matarajio ya kurudi kijijini na mtoto, huku mama Zuu nae akiwa salama, mengine yote yalikuwa yanavumilika kwao.********
Kwakifupi ni kwamba, katika kijiji cha Mbendu, mzee Abdallah alikuwa ni mzee wa kipekee sana, kuanzia kuwa na busara nyingi, ambazo ziliwavutia watu wengine, kuja kuomba ushauri, au usuruisho wanapokuwa na ugomvi, au utata.
Ilifikia wakati wakamchukulia kuwa, ndie kiongozi wa kijiji, au mwakishili wa kijiji pale inapoitajika mwakilishi, pia upande wa mwingine, alikuwa ni mwenye upendo na nidhamu kubwa kwa wenzake.
Ukichilia mambo hayo mzee huyu, ambae kutokana sifa ya ucha mungu na kushika dini, katika kijiji iki, chenye waumini wa dini ya waislam wachache, alipewa uongozi wa msikiti mdogo wa pale kijijini.
Pia alipata sifa kubwa, kutokana na malezi ya binti wake, wa pekee Zuleiya, ambae pia ukiachilia uzuri aliokuwa nao, alikuwa ni nidhamu kwa wakubwa na wadogo.
Pia Zuleiya, akuwa mwepesi kwa wanaume, kama ilivyokuwa kwa waschana wenzake, wa pale kijijini, ambao walianza kushiriki mapenzi, katika umri mdogo sana, pengine mschana angeonekana mjamzito, akiwa na umri wa miaka kumi na tano.
Lakini Zuleiya, mpaka anafika miaka 19, alikuwa bado ajamjuwa mwanaume, kwa uwazi ni kwamba, alikuwa analuhusu mwiko wa mwanaume yoyote, kugusa chungu chake.
Siyo kwamba, hapakuwa na wanaume, waliojaribu kurusha ndoano zao, wapo wengi walifanya hivyo, wakitanguliza zawadi mbali mbali, lakini juhudu zao ziligonga mwamba.**********
Naaaam!, siku ya pili, Zulaya na baba yake wakiwa pale hospital, waliswali swala zote tano, huku dua yao ikiwa ni mama na mtoto watoke salama, huku wanafunga suna.
Siku ya tatu mchana, mida ya saa kumi na mbili za jioni, ikiwa mida ya swala ya magharibi inakaribia, Zuleiya alitoka na kwenda kununua mkate kwaajili ya kufutulu.
Zulaya ambae alikuwa mgeni hapa mjini, alitembea taratibu, kuelekea kwenye duka ambalo toka siku ya kwanza, amekuwa akinunua mkate, kwaajili ya futulu, alitembea taratibu kwenye barabara, ambayo mida hii, ilikuwa na watu wachache sana.
Lakini akiwa anaendelea kutembea, mara akasikia vishindo nyuma yake, Zuleiya akageuka na kutazama nyuma, akamwona kijana mmoja alievaa coverloll, wengi uita over lori, lililochafuka kwa mafuta meusi ya gari.
Kutokana na ugeni na uschana wake, Zuleiya alijikuta anaingiwa na uoga kwa kiasi flani, akiofia kijana huyu wa mjini, kumtendea yasiyopaswa kutendewa, maana alisha sikia hadithi nyingi za wanaume wamjini.
Lakini ilikuwa tofauti kabisa na alivyofikilia, maana yule kijana ambae alikuwa anatembea kwa haraka, alipomfikia, alikuwa wa kwanza kumsalimia, “asalam aleykum” alisalimia yule kijana, kwa sauti yenye utulivu na upole wa hali ya juu.
“Waleykum salam”alijibu Zuleiya, huku ameinamisha kichwa chini, baada ya hapo kijana akaendelea kutembea, akimpita zulaya nae akawa mbele Zuleiya nyuma,.
Pengine ni kutokana na kijana huyu, kuwa tofauti na alivyo zania, Zuleiya, alimtazama kijana huyu kwa macho ya kipekee sana, akimwona ni kijana wakipekee sana, siyo tu kwa huku mjini, pia ata huko kijijini.
Sasa basi, wakati Zuu anamtazama kijana huyu, akamwona anaingiza mkono mfukoni, na kutoa saa, ambayo aikuwa na mikanda, anaitazama kisha anairudisha mfukoni.
Lakini wakati anatoa mkono mfukoni, akadondosha wallet yake, nakijana huyu, pasipo kuwa na habari, akaendelea na safari, “kaka!, kaka!, wewe kaka” aliita Zuleiya, lakini kijana yule akumsikia.
Zuleiya anakimbilia ile wallet na kuiokota, akichelea wasije watu wengine wakaiwai, na kujana yule kupoteza vitu vyake muhimu, na pengine fedha, anapo mtazama tena yule kijana, mbele yake, anamwona anazidi kuyoyoma.
Zuleiya anajaribu kuongeza mwendo, kumkimbilia yule kijana, lakini kiukweli, kijana yule alisha mwacha mbali, na sasa alikuwa anaingia kwenye chochoro inayoenda kutokea madukani.
Zulaya anaongeza mwendo, mpaka kwenye ule uchochoro, ambao hupo tupu, na haina mtu yoyote, ana pita kwenye ile chochoro na kutokea upande wapili, ambako anakutana na watu wengi sana.
SEHEMU YA NANE
Zuleiya anatazama kushoto na kulia, anamwona kijana akiwa anaelekea upande wa kushoto, usawa wa maduka ya vitafunwa, yani keki, mikate na vinywaji, kama vile maziwa safi.********
Naaaaam!, wakati huo huo, kijana alie dondosha wallet ndio kwanza alikuwa anaingia ndani ya moja la duka la vitafunwa, “naomba mkate mkubwa wa mia tano” alisema kijana yule, kwa sauti ya kujiamini, huku anapapasa mfukoni, kuangalia wallet.
Lakini aioni wallet, anapapasa tena na tena, lakini bado ainoni wallet, anatoa kila kitu kilichopo mfukoni, na kukagua tena na tena, lakini hali ni ile ile, “nimeangusha wallet yangu.
Alisema yule kijana, kwa sauti ya mshtuko, maana alijuwa kuwa amepoteza fedha mbayo, siyo tu, ameifanyia kazi kutwa ya leo, ila pia, alipoteza fedha aliyo iifadhi kwa muda mrefu.
Hakika akufikilia leo atakula nini, ila aliwaza kuhusu elfu hamsini na nane, aliyo ipoteza, ela ambayo alikusudia kuifanya ya kuanzia maisha wakati atakapo enda kuishi Dar_es_salaam, ambako alipaga kwenda kujaribu maisha.
Huyu anaitwa Abdulazizi, wavivu kama mimi, kijana huyu umwita Abdull au Abuu, ni mmoja kati ya watu walio zaliwa na kukulia kijijini, lakini yeye aliishi katika kijiji cha ujamaa cha Litapwasi, alikokuwa anaishi na bibi yake.
Ila wakati flani wa likizo, ya mwezi wa sita, alienda kwa mwarabu, yani kule mashambani, kumsalimia mama yake, ambae alikuwa anafanyakazi kama mtumishi wa ndani, na mpishi wa familia ya bwana Radhaq yani bwana mwarabu.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, ambacho alisomea huku mjini, kwenye shule ya sekondari yakutwa ya Ruvuma, akanogewa na msa ya mjini, na kuamua kuishi mjini, akijivundisha ufundi wa magari.
Kazi ya ufundi, aliyoifanya kwenye kalakana moja pale mjini, ilimsaidia kujiingia fdha ndogo ndogo, ambayo ilimsidia kwa kula, na kulipia baadhi ya bili zake, kama vile pango ya nyumba mtaa wa mahenge C.
Pia aliweza kulipia umeme na maji, kuhusu nauri aikuwa jambo muhimu sana, maana wakati huo, safari nyingi zilifanywa kwa miguu, na pia akuwa mwingi wa habari za mapenzi.
Siyo kwamba akuwai kupenda, ukweli ni kwamba, kijana huyu alisha wai kuingia kwenye penzi ambalo, mpaka leo alijamtoka kichwani, japo hakuwa na uwezo wa kumpata tena mschana aiemganda kichwani mwake.
Jambo ambalo kwa sasa, lilikuwa kichwani mwake ni moja tu, ni kutengeneza maisha yake, yatoke katika hali ya chini, na kuwa katika hali ya juu, na sehemu pekee ya kufanya hivyo, ilikuwa ni Dar es salaam.********
Naaaaam!, wakati anajihisi kuchanganyikiwa, mara akasikia, “kumbe na wewe ulikuwa unakuja hapa” ilikuwa sauti ya kike, iliyomfanya Abdulazizi ageuke na kumtazama muongeaji, na ili kujihakikihsia kama anaongea na yeye au la.
Abdulazizi anamwona yule mschana mzuri, ambae alimpita njiani, muda mfupi uliopita, ambae alikuwa ameshika wallet yake anampatia, Abuu anatoa macho kwa mshangao, akimtazama yule dada, ambae ni Zuleiya.
“nilikuita sana, ukusikia, unabahati awakuwa wanapita watu wengine” alisema tena Zuleiya, wakati Abuu anapokea wallet yake toka kwa mschana huyu, ambae akuwa anamfahamu.
“asante sana dada yangu, yani nilikuwa nimeshaanza kuchanganyikiwa” alisema Abdulazizi, ambae anafungua wallet yake, na kuona fedha zake zipo vile vile, kama zilivyokuwa mwanzo.
“asante sana dada yangu” alisema Abdulazizi, huku anachomoa noti tatu za elfu moja moja, na kumpatia Zuu, “hapana, kaka yangu, siyo kwaajili ya malipo” alisema Zuu, pasipo kufikilia kuwa, yeye na baba yake, wanaitaji fedha za kula.
Ilimshangaza adi mwanamke muuza duka, “pokea dada, unastahili kupewa, kwa moyo uliyo uonyesha” alisema mwanamke, ambae kwa umri, aliwazidi wote wawili, yani Abdulazizi na Zuleiya.
“hapana hii ni haki yake, ametafuta kwa jasho lake, mimi nimemwokotea tu” alisema Zuleiya, huku anatoa tsh mia tatu, na kumpatia yule muuzaji, “naomba mikate miwili” alisema Zuu.
“leo vipi kuhusu juice?” aliuliza muuzaji, “leo nina mia tatu tu” alijibu Zuleiya, inamshangaza Abdulazizi na mama muuzaji, “mpe juice mbili na hiyo mikate, nitalipia mimi” alisema Abdulazizi, huku anampatia muuzaji noti moja ya tsh elfu moja.
Muuzaji anaachia tabasamu pana, huku anampatia Zuleiya fedha zake, ambazo ni sarafu za mia mia tatu, Zuleiya anataka kukataa, lakini anaishia kutabasamu.
“asante asante sana, mwenyezi mungu akizidishie ulipo punguza” alisema Zuleiya, ambae kiukweli ni mschana mzuri, kuanzia sura yake, na umbo lake, “Amina dada yangu” alijibu Abdulazizi.
SEHEMU YA TISA
Baada ya kumaliza kuhudumiwa, wawili wale, wanatoka dukani, kila mmoja akiwa na safari yake, lakini katika uelekeo mmoja, Zuleiya ambae alikuwambele, alitamani kumsubiri kijana huyu mstaarab, ili waongozane.
Lakini anashindwa kufanya hivyo, akichelea kuonekana mwanamke mlahisi, anaendelea kutembea, lakini kwa hatua fupi za taratibu, huku akitazama nyuma, kwa jicho la wizi.
Abdulazizi nae baada ya kuona mwanamke huyu, mwenye moyo wa kipekee, anaelekea upande anao elekea yeye, anaongeza mwendo, na kumsogelea.
“kumbe unaelekea huku” anasema Abdulazizi, aikiwa ni namna ya kuanza kumwongelesha mschana huyu, “ndiyo, naelekea hospital” alijibu Zuu, kwa sauti yenye uchangamfu.
“hoooo!, kumbe, pole sana, kwani nani anaumwa?” aliuliza Abdulazizi, huku wanaendelea kutembea, kuelekea upande wa hospital, “mama uangu amekuja kujifungua” alisema Zuu, ambae alimwelezea Abuu, kwa kifupi, hali waliyonayo.
“kwahiyo hiyo mikate ndio futari?” aliuliza Abdull, kwa sauti ya mshtuko na mfadhaiko, “ni kutia kitu mdomoni, siyo lazima ushibe sana” alisema Zuu, ambae akuamini kuwa mwenzie ameguswa sana.
Waliachana nje ya geti la kuingilia hospital, wakiwa wamesha tambulishana kwa majina, na kila mmoja akashika njia yake, Zuu akujuwa Abdulazizi amepanga nini kichwani mwake.
Wakati walipomaliza kufutari, Zuleiya na baba yake, wakiwa wanaongea mawili tatu na mama Zuu, aliekuwa amelala kitandani anamnyonyesha mtoto, aliekuwa anaendelea vizuri.
Ndio wakati ambao Zuleiya, alipoanza kumsimulia baba yake, kuhusu kilicho tokea, wakati alipoenda kununua mikate, kwaajili ya futari, simulizi ambayo iliwasisimua baba na yake.
“kwa huku mjini, kukuta mtu mwenye moyo kama huo, ni mara chache sana” alisema mzee Abdallah, na mke wake akadakia, “ni kati ya vijana wachache, walio pata malezi mazuri” alisema mama Zuleiya.
“tena ni dini yetu” alisema Zuleiya, huku anatabasamu, baba yake akamtazama kwa macho ya mashaka, tofauti na mama yake alie cheka kidogo, “usiniambie kama anataka kukuchumbia” alisema mama Zuu.
“wala atujaongea hivyo, mimi nimewaambia tu” alisema Zuleiya, kwa sauti ya kujitetea, huku aibu ikimzidi na kutazama chini, japo hiyo aikuwa sababu, ya kumwondoa kijana yule kichwani mwake.
“Lakini safari yetu imekuwa na bahati sana, kuanzia njiani tuliposaidiwa na na yule binti mwarabu” alisema mama Zuu, na kila mmoja akaunga mkono, na kumwombea Shadya mafanikio, kwa moyo alio uonyesha kwao.
Ukweli licha ya kwamba akuwai kuwa na mpenzi, lakini kwa mara ya kwanza, Zuleiya alijikuta anamatamani kuwa na mwanaume, na siyo tu mwanaume, ila ni kijana Abdulazizi, yule aliekutana nae jana. *******
Siku ya pili jioni, mida ya saa kumi na mbili, wakati Zuu akiwa amekaa kwenye benchi na baba yake, anajiandaa kwenda kununua, mkate kwaajili ya kufutulu, huku anatamani kukutana tena na Abdulazizi.
Mara akamwona Abdulazizi, huyo huyo, akiwa anakuja upande wao, na kikapu mahalumu cha kubebea vyakura, kikiwa mkononi mwake, nikama alikuwa analeta chakura kwa mgonjwa.
“Baba unamwona yule kijana anaekuja” alisema Zuleiya, akionyesha upande wa kuingilia kule hodini, “huyu alievaa ovaloli?” aliuliza baba Zuu, huku wote wawili, wanamtazama kijana yule, ambae alikuwa ajawaona,.
“ndiyo huyo huyo, ni yule niliekusimulia jana” alisema Zuleiya, “hooo!, kumbe na yeye, anamgonjwa hapa hospital” alisema mzee Abdallah, huku wanamtazama kijana huyu.
Aikuwashangaza sana, kumwona Abdulazizi mida hii hospital, sababu ndio mida ya kutazama wagonjwa, waliamini anamgonjwa, amekuja kumletea chakura, ufanywa hivyo na baadhi ya watu, kubadirisha chakura kwa wagonjwa wao.
Wanamwona kijana huyu, anatembea taratibu, huku anatazama kwa umakini, akiwatazama watu wengi, waliokuwa wanaongea na wao kwa wao, wanaongea na wagonjwa wao.
Wanamtazama mpaka wanapokutanisha macho yao, kijana anatabasamu, na kuanza kutembea kuwa fwata, wakina Zuleiya na baba yake, ambao walikuwa wanamtazama kwa macho ya tabasamu.
Alipowafikia tu, chakwanza wakasalimiana, “salam aleykum” alisamia Abdulazizi, huku anampa mkono mzee Abdallah, “waleykum salam, karibu sana” aliitikia mzee Abdallah, huku nae anaupokea mkono wa Abdulazizi.
SEHEMU YA KUMI
“asante sana” aliitikia huku wanaachia mikononi, kisha Abdulazizi akamtazama Zuleiya, “asalam aleykum” alisalimia Abdulazizi, safari hii, bila kupeana mikono na Zuleiya.
“waleikum salam, habari za toka jana” aliitikia Zuleiya, huku anatazama chini, akikwepa kumtazama Abdulazizi usoni, Abuu yeye anamtazama mzee Abdallah.
“vipi hali ya mama na mtoto, wanaendeleaje?” aliuliza bwana Abdulazizi, swali ambalo, lilimfanya bwana Abdallah, agundue kuwa, Zuleiya na kijana huyu, waliongea mengi sana.
“wanaendelea vizuri, tunaweza kwenda kuwaona” alisema mzee Abdallah, huku anainuka pale alipokuwa amekaa, tayari kuelekea ndani, Abdulazizi anamtazama Zuleiya.
Zuleiya nae alikuwa ameshasimama, “jana uliniambia kuwa, mnafunga suna, nimewaletea futari, naomba muipokee, bila shaka yoyote” alisema Abdulazizi, huku anampatia Zuleiya, kile kikapu cha kubebea vyakura,.
Hapo mzee Abdallah, anasimama na kumtazama Zuleiya, kwa sekunde kadhaa, anamwona Zuleiya, pia ametoa macho kwa mshangao, alionyesha wazi akuamini anacho kiona.
Mzee Abdallah, au baba Zuu, anamtazama Abdulazizi, “asante sana kijana, lakini aukuwa na aja ya kufanya hivyo” alisema bwana Abdulazizi, kwa sauti ya upole yenye msisitizo.
“usijari baba, dada Zuleiya, alinieleza kila kitu, nimeamua kusaidia ilifunga ifanikiwe” alisema Abdulazizi, huku uso wake, ukiwa umechanua kwa tabasamu, “mwenyezi mungu, akuzudishie ulipo punguza” alisema bwana Abdallah.
Na hapo Zuleiya anapokea kile kikapu, ambacho ndani, kilikuwa na vitunza chakula vitatu, na pia kulikuwa na chupa ndogo ya chai, pamoja na vikombe viwili vya chai, na chupa ya maji.
Siyo tu Zuleiya na baba yake, walio shangazwa na moyo wa kijana huyu, ata mama Zuu pia, alishangazwa na kile ambacho alikiona, walimshukuru sana kijana huyu, ambae akionyesha macho ya tamaa kwa Zuleiya, jambo ambalo wao walikuwa wanalihisi.
Ata muda wa swala ya magharibi ulipowadia, wakati wao wanajiandaa kuswali, walimwona pia Abdulazizi anajiandaa kuswali, kwamaana wote wakajuwa yakuwa, kijana huyu, alikuwa mchamungu, na mwenye moyo safi.
Aikuishia jioni ya siku hiyo, hii ilikuwa kwa siku tatu zote, walizo kuwepo hapa hospital, Abdulazizi alipita hospital mapema na uji lishe, wsakati huo ukiitwa uji wa ulezi, ambao ulikuwa na mchanganyiko, wa maindi karanga na ulezi, kwaajili ya mama Zuu.
Pia kijana huyu, jioni alirudi na chakura kwaajili ya futari ya Zuu na baba yake, angekaa nao mpaka muda wa swala ya magharibi, wangeswali pamoja na baba Zuu, kisha angeondoka zake.
Katika siku tatu hizi, siyo Zuleiya peke yake, ni baba na mama Zuu pia, walitegemea siku moja wapo, lazima kijana huyu, angetupa karata yake kwa binti yao Zuu.
Lakini aikuwa hivyo, nimpaka ijumaa mchana, siku moja kabla awajaaluhusiwa, siku ile Abuu, alienda kuwa nunulia nguo wote wawili, yani Zuu na baba yake, kisha wakaenda msikitini.
Saa saba walikuwa wamesha toka msikitini, wanatembea taratibu, kwenye mitaa ya Songea, kuelekea upande wa hospital, “baba naomba kaka Abuu anitembeze kidogo sijawai kuijuwa Songea” lilikuwa ombi la Zuu.
“sasa, usihelewe kurudi ujiandae kwa swala na kufuturu” alisema baba Zuu, akiwa anamkumbusha Zuleiya, kwa kuwa amefunga, asifanye jambo la kijinga, maana ni kama aliona dalili za wawili awa kumezeana mate.
Abuu na Zuleiya walitembea kwa muda wa masaa matano, wakizulula mitaa ya Songea mjini, kuanzia soko kuu, mfaranyaki, stendi kuu, sasa ni stendi ya zamani, kisha majengo.
Sehemu ambayo Abuu akuacha kumpeleka Zuleiya ni kwenye gerije aliyokuwa anafanyia kazi, huku njiani wakiongea mambo mengi sana, walicheka na kufurahi kwa pamoja.
“kwahiyo wewe umesha owa” aliuliza Zuleiya wakati flani, “bado sijaowa, kwani unaona ninafaa kuowa?” alijibu Abuu, huku akiuliza swali, ambalo lilimfanya Zuleiya atabasamu kwa aibu.
“tena unafaa aswaa” alijibu Zuleiya kabla aja uliza swali jingine, “sasa kama ujaowa inamaana unazini?” aliuliza Zuleiya, na kumfanya Abdulazizi acheka kidogo.
INAENDELEA


