๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐ ๐ฃ๐จ๐ก๐๐
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 61
TULIPOISHIA..
Wakanijibu hakuna malipo yoyote zaidi ukiombewa na ukipona Unatakiwa ununue Bible na Tenzi kisha inabidi uende kanisa lolote la Kikristo au Kipentecost kama wao vinginevyo unaweza kuludiwa na tatizo lako maana ukikaa tu bila kwenda kanisani shetani anakurudia tena.
Basi ilipofika saa kumi na mbili na nusu nilishangaa kuona watu wachache sana ndio wanaondoka lakini wangine walikuwa wakijiandaa kulala hapo hapo…!! Aisee ikabidi na Mimi nimtume July akachukue godoro ili nilale hapo hapo kudadeki…!!
ENDELEA NAYO
โWatu wangine bwana Kama mpumbavu, yaani mgonjwa wakumpeleka hospital yeye kamleta hapa kuombewa..sasa ananukaa mpaka wangine tunashindws kulala..!!โ
Ilikuwa ni sauti za minongono ya watu wangine waliokuwa na wagonjwa wao pale uwanjani, sasa walinzi pamoja na watoa huduma wangine wakawa wameipata ile halufu ya mpenzi Wangu โญโ Gฮ ivyo wakasogea ili wajue tatizo ni nini, basi alisogea bwana mmoja akiwa kavalia suti huku shingoni kaweka skaffu ambayo ndio inafanya atambulike Kama mtoa huduma pale uwanjani au shemasi;
โHabari yako nduguโ
Alifika na kunisalimia huku akinipakono, nilimuitikia vizuri kabisa tena kwa busara zote kisha akaniuliza tena huku macho yake yakimtazama โญโ Gฮ Wangu;
โAisee uyu mgonjwa wako anatatizo gani ndugu yangu..??โ
Muda uo tayari watu walishasogea huku wakiteta kuwa uyo ni wakupelekwa hospital tu maana ameshaoza tayari ata akiombewa haponi, nilikata tamaa kutokana na yale maneno yao basi nikamjibu uyu shemasi lile swali lake;
“Kwakweli uyu ata Mimi sielewi tatizo lake kiukweli, ila alikuwa akiingiliwa kimapenzi ndotoni alafu akija kuamka anajikuta kweli kafanya mapenzi…!โฅ๏ธ Na kibaya zaidi anakuwa kaumia vibaya sana sehemu zake za siri..๐ฉ…Amekaa pale Muhimbili zaidi ya mwezi na wiki zake lakini madaktari haoni ugonjwa wowote alafu anazidi kunuka tu huku akioza nakutokwa na wadudu sehemu za uke na haja..hali ilipoendelea ivyo ndipo uongozi wa hospital ukanifukuza ukidai mke wangu ana nguvu za giza kwaiyo ni ngumu kuweza kutibiwa na dawa za kawaida za mzungu…basi nikiwa nimekata tamaa ndipo nikasikia nakuona kwenye TV๐บ, hiki kinacho endelea hapa ndipo nikaona nije kujaribu..๐!!”
โPole Sana ndugu yangu na pia ongera kwa roho ya uvumilivu na Upendo wa ajabu ulionao kwa uyu mwanamke, Mimi naweza kusema mahali ulipofika sasa ni mahali sahihi kabisa tena hutakiwi kusema umekuja kujaribu hapana, sema nimekuja kupona maana hakuna linalo shindikana kwa mungu, Ebu fikiri kama yeye aliweza kumuumba uyo binti atashindwa nini kumfanyia matengenezo madogo tu kama ayo..kitu pekee kinacho hitajika ni imani na moyo wenye imani kuwa MUNGU ANAWEZA..!โ
Basi alipomaliza kuongea akaondoka bila ata kuniaga, lakini muda mfupi nikaona vile vi helicopter vidogo kikija usawa wangu kisha kika sogea chini kabisa alafu akasema mlete hapa ndani nikawaomba vijana wanisaidie kumpakia ndani ya iyo helicopter wakati tunampakia wale vijana wakawa wanasema;
“Yani kama akipona uyu Dada hakika Mimi nakuwa mlokore mpaka kifo maana ntaamini kweli MUNGU wao yu hai na anajibu maombi”
Mi nikamwambia ngoja tuone haina sababu yakujiuliza uliza wakati kunapazuka sasaivi tu.
Ilikuwa ni tayari saa kumi na mbili asubuhi muda uo ulikuwa umewekwa mziki mkubwa sana huku nyimbo ya mwanamziki Mrembo na Mwimbaji maarufu wa nyimbo za kuabudu Tanzania naye sio mwingine ni mwanadada Christina na muda uo ilikuwa ikipigwa nyimbo yake ya:
__CHORUS_
๐ผ๐ถUnajibu maombi unajibu maombi unajibu maombi naku amini BWANA, ร3
__VERSE__
Ezekiel alipougua alikulilia ukamsikia ukamponya nakumuongea miaka naku amini BWANA,
Nami leo naja mbele zako nakulilia utanisikia utaniponya….>>
Ilikuwa ni maporomoko ya watu wakiwa na wagonjwa wao aina mbalimbali wangine vipofu, vilema, wagumba, machongo,viziwi, wenye vifafa, huku asilimia kubwa wakiwa ni wagonjwa wakurogwa huku wengi zaidi wakitolewa mirembe hospital ya vichaa ambapo walikuwa wakiwekewa mkono tu wanapona papo hapo…!!
Muda ulifika na mgonjwa wa kwanza kabisa alikuwa ni mpenzi wangu mpendwa Koga, kwanza nilimsikia yule Pastor Stefansson Mzee Mwenye umri wa miaka 78 ivi akisema;
โAlelujaa Groly to GOD, Alelujaah yesterday I promise you that, today is our last day to bee in Tanzania… I am very sorry because there is a lot of people here who needs help. So let our prayer beginning. โ
Alipomaliza akaanza kutafsri kwa kiswahili jamaa ayekuwa pembeni yake;
“Aleluya Utukufu kwa MUNGU, aleluyahh, Jana niwaahidi kwamba leo ndio itakuwa siku yetu ya mwisho kuwepo Tanzania..Nasikitika kwasababu kuna watu wengi Sana hapa ambao wanahitaji msahada. Basi acha maombezi yaanze nakuendelea…!!”
Sikuamini nikaona kitanda cha Koga kikisukumwa nakusogezwa jilani na Pastor Stefansson, ambaye yeye katoka Canada, akamsogerea huku akiwa haonyeshi kukerwa na ile halufu ya Koga ata kidogo…. Waandishi wa habari za udaku, blogs, na viombo vikubwa kabisa vya habari vilikuwepo pale vikifuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea ila ili la Koga ndio liliwavuta wengi maana walianza kulisikia muda mlefu tangu kuzariwa kwa Punda. Basi Pastor Stefansson akamfunua usoni Koga tayari kwa kuanza kumombea…lakini ile anataka tu kufungua mdomo wake…. Ghafla….!!!
EP 62
Ile Pastor Stefansson kutaka kuweka mkono juu ya mwili wa Koga, mala ghafla Koga akafumbua macho yake huku akiwa kayatonoa..๐จ..!! Pastor Stefansson hakujali akamuwekea mkono ivyo ivyo daah!!
Nilimshuudia koga aliyekuwa anaumwa na hawezi kutembea zaidi ya mwezi sasa, lakini alisimama huku sura yake nzuri yakuvutia kama malaika ikabadirika nakuwa kama zombie๐น…Alikuwa anatisha wahudumu na walinzi wa mkutano wakajaribu kumshika ili wamzuie hasije kumgusa Pastor Stefansson lakini ilikuwa ngumu sana sababu aliwatupa huku na huko kama maembe yaliyooza hali ambayo ilifanya waandishi wa habari wenye roho nyepesi kuanza kutimua mbio..Koga alibadilika kabisa kama nilivyokwambia uso wake ulikuwa Kama jini๐น au shetani basi hali ikawa si hali tena maana ata yule mkalimani wa Kiingereza kuja kiswahili wa Pastor Stefansson alikimbia jukwaa maana Koga alipofungua mdomo wake nilishangaa kuona meno yake mawili ya mbele yakiwa malefu kuliko mangine..basi jukwaa likabaki jeupe japokuwa police walisogea karibu kabisa lakini wachungaji wangine wa kibongo wakasema tafadhali tafadhali ndugu zetu askari naomba msipige Risasi yoyote maana endapo mkifanya ivyo ndio mtamuua kabisa uyo binti alafu ayo mashetani yataondoka zake…!! Koga yeye alikuwa anamkabili tu Pastor Stefansson wale askari wakasogea nakumshika Koga kisha wakafanikiwa kumtia pingu..katika hali isiyokuwa ya kawaida Koga alizikata zile pingu Kama uzi tu kisha akamdaka mmoja nakumng’ata mkono wake ndipo askari mwingine akajibu mapigo kwa kumpiga risasi kwenye paji la uso lakini iliteleza tu ata alama haikubaki…watu walishangaa nakusema kweli ili ni jini Makata kama sio maimuna…!!
Askari wakatoka nduki pale jukwaani akabaki Pastor Stefansson peke yake akainua mikono yake juu muda uo walokore wote waliokuwepo pale walikuwa wakiomba kila aina ya maombi huku wakilia na mikono yao wameielekeza kule jukwaani. Basi wakati Koga akimfuata kwa kasi Pastor Stefansson, yeye alikuwa kainua mikono yake pamoja na uso wake juu. Basi mpaka Koga akamfikia kabisa nakumvaa kwa kumkumbatia huku mdomo wake akiupeleka shingoni tayari kwa kumng’ata…watu wote pale jukwaani hawakuamini kama Pastor Stefansson aliyeponya vipofu walemavu visukari n.k anakuja kushindwa kwa mwanamke tu tena kijana Mdogo Kama Koga.. Walibaki kushika midomo tu huku wangine wakisema yeye si alijifanya YESU WA PILI aya sasa kakumbana na jini makata ilo tuone Kama atachomoka hapo..ilikuwa ni taaruki…!!
Mara ghafla…Pastor Stefansson akawaka moto..๐ฅ..ambao ulimnasa na Koga.. Ikabidi Koga amuachie Pastor Stefansson kisha akaanza kukimbia huku akipiga kelele waaaaahh!! Yaaaaaahh!!
Katika hali yakushangaza Pastor Stefansson akiwa anawaka moto vile vile akashika mike nakuanza kukemea;
“Fireeeeeee..!!๐ฅ Fireeeeeeee..!!๐ฅIn the name of Jesus.. I say Fireeeeeeeeeee….๐ฅ Out..out..lapa papapa..Yaweeeeehhhh!! Out Out Out…Fireeeeeee…๐ฅ I burning you.!!!”
“Motoooo..!! Motoooo..!! Katika jina la Yesu..nasema motoooo…Toka..!! Toka..!! Lapapapapa.. Toka..Toka..!!”
Sikuamini kabisa nilijikuta napiga magoti.. Peke yangu jamaa aliyekuwa karibu Yang naye akapiga magoti basi tukajikuta wote pale uwanjani tumepiga magoti huku tukiogopa maana yule Pastor alikuwa anawaka moto alafu bado anatembea nakuendelea kukemea pepo Kama kawaida. Koga wangu aliwaka moto Kama dakika kadhaa ivi kisha akaondoka chini pale jukwaani, na ndipo nikamuona Pastor Stefansson naye akiacha kuwaka moto…!! Akamsogerea Koga kisha akamwambia kwa kiingereza;
“Stend up please, you’re free now!!”
(Tafadhali inuka, upo huru sasa)
Jamani, Jamani, Jamaaaaaaaaani..sikuamini macho yangu nilipomuona Koga akisimama huku anamelemeta Kama bibi hatusi yani moto wote ule ulimuwakia haukumdhuru kabisa.
Pastor Stefansson akachukua wakati uo waandishi wamesha sogea tena wakati Koga ameshika mike tayari kwa kujibu maswali toka kwa Pastor Stefansson;
“What is your name..?”
(Jina lako nani)
“Naitwa Koga”
Kwa mala ya kwanza nikasikia sauti laini ya Koga ikiwa katika ubora wake Kama nilivyo isikiaga miaka miwili nyuma, Koga alimjibu Pastor kwa sauti nzuri huku akitabasamu..!! Naye Pastor aliendelea kumuuliza maswali mangine kisha akafikia kumwambia kuwa Yesu kamponya je atamlipa nini kwa kumpa Uzima uo bure ndipo nikamuona Koga akishika Mike nakuanza kulia kwanza.. Alilia sana na fundi wa viombo au wengi uwaita DJ, akaweka wimbo wa Dada Jennifer M. ;
“Naliaaa pole, naliaa pole Sana mmh naliiiiaa pole naliaaaa pole Sana.
Mimi nilijiona nimepata kuumbe nimepatikanaeeh, Mimi nilijiona ni mzuri kumbe nina poteaa, nikajifanya nimrembo kumbe naaribikiwa hee.
Mimi nalia pole naliaa pole Sana, hiiii nalia pole mmmmh naliaaaa pole eehiiiheheheheee!!
Koga alilia sana tena sana kiasi kwamba kila mmoja pale uwanjani alitokwa na machozi huku wanawake wakishindwa kujizuia nakujikuta wakilia pamoja na Koga. Basi baada yakutulia ndipo Pastor Stefansson kama kawaida akamuuliza;
“Binti tayari Yesu kakupa nafasi nyingine yakuishi je unataka kufanya nini hapa duniani katika muda huu machache aliokupa..??”
Ndipo Koga akasema huku akimtazama Pastor Stefansson usoni;
“Nataka nimtumikie yeye mpaka siku yangu ya mwisho, na kwakuthibisha ilo naanza na rafiki yangu mpendwa aliyenivumilia katika hali zote na ndio aliyenileta hapa mpaka saizi nimesimama hapa naonekana kama binadamu kumbe tayari nilikuwa ni;
“The walking Died”
(Maiti inayo tembea)
Basi haraka nikasogea mpaka pale juu ya jukwaa, nikamfuata Koga nakumkumbatia lakini niliungua vibaya sana nikamuachia ghafla nakusogea pembeni huku nikimtazama kwa woga..!!๐ฎ Pastor Stefansson huku akitabasamu akasogea karibu kisha akaniwekea mikono kichwani kisha akasema upo tayari sasa maana mwanzo wewe ulikuwa tofauti kabisa na uyu..!!
Basi tukakumbatiana vizuri na Koga wangu kisha nikamsogerea Pastor Stefansson akatuambia;
“Kuweni tayari kesho tunaondoka pamoja kuelekea Canada ili muanze lasmi kazi ya MUNGU, kila kitu mtakikuta huko Ottawa
MUNGU awabariki sana nilifurahi Sana huku nikiondoka zangu pamoja na Koga wangu kurudi nyumbani kwaajili ya maandalizi.
Tukafika kwa Dada yake koga….!!
EP 63
Kila mmoja alipigwa na butwaa hakuamini anacho kiona mbele yake, koga akasema;
” Ni Mimi Dada, ni Mimi Koga Mdogo wako, ila sio koga yule unayemjua wewe bali ni Koga mpya kabisa ambaye ni binti sayuni”
Basi Dada akaja mbio nakumkumbatia Koga Mara ghafla akamuachia huku akisema wewe mbona una moto mwilini mwako;
“Dada sio moto ila guvu za damu ya Yesu ndio zinazo fanya uone kama nina moto mwilini mwangu lakini sivyo kabisa..!!
Basi tukakaa huku nikimwambia Dada kuwa kesho naondoka Mimi na mume wangu Jofu tunaelekea nchini Canada, kwa ajili ya maisha na tutakuwa huko kama Wainjilisti ambao tutakuwa tukiifanya kazi ya MUNGU mpaka pale tutakapo kamilisha kazi yake MUNGU nakwenda kuketi mkono wake wakuume..!!
“Weee Jofu ivi unaelewa anachoongea mkeo, maana anazungumza vitu ambavyo havipo kabisa, maana nasikia sijui Canada mala mkono wakuume wa Baba MUNGU sielewi kabisa ujue, ebu nisaidie wewe..!!”
Nilimshangaa sana Shemeji yangu ananiona Mimi Mjinga sina akili, kabla Jofu hajajibu nikamwambia Dada kuwa inatosha nilicho ongea kimeeleweka uzuri hakuna mtoto hapo. Ndipo Dada akasema huku akionyesha wasiwasi kidogo;
*Kwaiyo Mdogo wangu Koga Ndio unaondoka kwenda Canada kweli..!??”
“Ndio ivyo”
“Mbona ghafla sana Mdogo wangu, Mimi nashukuru umepona nilitaka tule bata Mdogo tufungue ukurasa Mpya wa maisha yetu, sababu ata Baba tayari kafariki kwaiyo nilidhani wewe unaenda kumsimamia Mama kuzipangilia zile Mali kule kijijini..Koga husiende Canada Mdogo wangu..!!”
“Dada Mimi nilisha kufa sawa ndio maana wote mliukimbia mwili wangu, akabaki binadamu mmoja tu Mwenye roho ya ajabu ambaye ni Jofu, lakini yote ayo nimesha wasamehe kwa dhati kabisa kama Mimi alivyo nisamehe Baba yangu Yesu Christo, sasa ujio Wangu huu au kuziliwa kwangu huku mala ya pili ni special kwa ajili ya kazi moja tu hapa duniani ambayo nikuakikisha wewe na familia yangu yote mnaenda mbinguni na iyo kazi ndio ajila yangu. Kwaiyo ukura unaotaka wewe nifungue Mimi tayari nimeshafungua ukurasa Mpya tena wa HOLY BIBLE (Biblia takatifu) kwaheri Dada yangu naomba kesho mnisindikize airport hapa naomba tu process za Passport zikamilike vizuri, ila katika jina la Yesu itawezekana..!!
Basi ilipofika jioni wahudumu walikuja mpaka tunapoishi tukafanya maombi kwenye kile chumba kisha Yule mbwa wetu Nasri alichukuliwa na Dada na jioni iyo iyo tukaondoka mpaka New Africa Hotel ambapo Ndio alikuwa amefikia Pastor Stefansson, tukalala hapo na hasubuhi tulipanda ndege mahalumu iliyotumwa na serikali ya Kenya. Tulifika Kenya na huduma ikaanza, tulifanya maombi mfululizo kama siku tatu tu na safari ikaanza kuelekea Uganda, maana Pastor Stefansson alisema ngoja afanye maombezi East Africa yote kuliko kufanya Tanzania tu na Kenya, basi baada yakumaliza kufanya mombezi katika jiji la Kampala nchini Uganda, tukachukua ndege ya;
AIR CANADIAN WORSHIPโ๏ธ
Tulipopaa tu angani nikamwambia Jofu;
โJofu Nasikitika kukwambia kuwa sirudi tena Tanzania au nyumbani..๐ขโ
Kisha machozi yakaanza kunitoka, kwakuwa tulikuwa tumekaa seat moja basi Jofu akanikumbatia huku akiniambia;
“Upo sahihi kabisa Mama hakuna sababu yakurudi tena nyuma kuna nini cha maana kilicho baki kwanza zaidi ya maasi na maovu yanayofanywa kila siku twende Mama twende tukamtumikie MUNGU ili tuishi maisha ya furaha na amani.!!”
Tulifika salama kabisa nchini Canada na baada ya mwezi mmoja tukiwa chini ya Pastor Stefansson ambaye kwa pale Ottawa yani mji mkuu wa Canada waumini wamempa jina la The Second Jesus (Yesu wa pili) jina ambalo yeye ulikataa katu katu kabisa maana anaamini kuwa Hakuna wakufanana na Yesu.
Basi tulifunga ndoa na siku ya kwanza kufanya mapenzi na Jofu yani toka nipone huwezi amini kabisa maana nilijishangaa kuona kuwa nimerudi kuwa bikra kabisa yani jamani kweli MUNGU mkubwa aisee…mume wangu mwenyewe ambaye ni Jofu alishangaa kabisa akabaki kaduwaa tu baada yakuona damu kibao huku nyuzi nyuzi za uke Wangu zikikatika yani inaonyesha ni bikra original kabisa tena ambaye sijawahi ata kujiosha na vidole.
Tulipomaliza kufanya tukapiga magoti nakumuomba MUNGU atusamehe, maisha yakaendelea pale Canada huku Pastor Stefansson akisafiri nchi mbalimbali pamoja na mume wangu Jofu nashukuru MUNGU maana nguvu za MUNGU zilimmshukia naye akaanza kutoa mapepo nakuwaponya watu wenye magonjwa madogo madogo. Baada ya muda mlefu kidogo nikafanikiwa kupata mtoto wakiume ambaye tulimpa jina Stefano ili awe wajina wa Pastor Stefansson, baada ya miaka mitano nilikuwa tayari nina watoto watatu yani Stefano, Leah, Na Kenan. Bahati nzuri Pastor Stefansson aliitwa na MUNGU ivyo alilala usingizi mzito nakupokelewa mbinguni na Baba yetu…Basi nafasi yake ikachululiwa na mume wangu Jofu. Tulipata taarifa kuwa Mama yangu ni mgonjwa sana..na Mimi sikutaka kabisa ndugu zangu wafe bila kuona nguvu na uwezo wa MUNGU alionifanyia. Basi nikafunga safari ya ghafla Mimi pamoja na familia nzima Kama lilivyokuwa enzi za Pastor Stefansson tukafika mpaka Dar es salama kwa bahati nzuri kumbe Mama alikuwa yupo Hospital ya Agakhan kalazwa anasumbuliwa na kisukari, miguu, pamoja na macho, sawa umri ulikuwa umeenda lakini ikumbukwe kuwa kwa MUNGU hakuna Bibi wala Babu..tukaenda pale pale hospital tukamfanyia maombi akasimama mwenyewe nakutembea mpaka ilipokuwa imepaki gari..!!
Kwa tukio ilo tulipofika tu nyumbani Dada na Shemeji pamoja na mtoto wa Dada Shinje wote wakapiga magoti nakumpa Yesu maisha yao baada ya siku kadhaa ndugu zangu na rafiki zao wote wakampa Yesu maisha yao na jambo la Ajabu nikwamba Munah rafiki yake Jofu alikuwa nchini India akimuuguza Baba yake aliyekuwa akisumbuliwa na moyo, Basi Jofu akampigia Simu rafiki yake Munah nakumwambia kuwa ampe Simu Baba yake ili amfanyie maombi maana hakuna umbali katika maombi, kweli Jofu alifanya ivyo.. Dakika chache tu Jofu ikapiga Simu akidai Baba yake kasimama nakuzitoa mashine zote za oxygen kwakweli ilikuwa ni furaha ilioje Baba yake Munah aliporudi toka India akatoa godauni lake moja liwe kanisa kisha na yeye akawa mkristo pamoja na familia yake yote..!!
Taarifa za Baba yake Munah kuasi uisilamu nakuwa mkristo zilifika Pakistan ambako ndiko chimbuko la ukoo wake kwaiyo jumapili moja tukiwa ibaadani Mimi nilikuwa pamoja mume wangu Jofu tukisibiri tupewe nafasi ili tuwaage maana kesho ndio tulitakiwa kurudi Canada Sasa sijui ni kitu gani maana Jofu aliwaambia watoto wetu waende nje kuleta zawadi ndani ya gari la Baba yake Munah kweli Stefano alienda na wadogo zake wote wawili wakaenda nakuleta briefcase ya ajabu kisha watoto wetu wakaenda tena nje ghafla ulitokea mlipuko mkubwa sana na kanisa lote likashika moto wakati moto unaendelea kuwaka mala nikamuona Jofu akiwa na mabawa akanishika mkono kisha tukaanza kupaa kwenda mbinguni na watu wangine nao ivyo ivyo..!!
Tulifika mbinguni tukamuona Pastor Stefansson akiwa pamoja na Yule mtume wa Yesu Stefanie aliuwawa kwa kupigwa mawe mwaka 106 AD. Tukasogea na kupokelewa huku watu wote wakiimba nakusujudu.
NIKATAZAMA DUNIANI NILIONA MAOVU YOTE YANAYOFANYIKA NIKALIA SANA MIMI KOGA, NILITAMANI NIRUDI KUWACHUKUA NA WATOTO WANGU LAKINI HAIWEZEKANI.
PASTOR STEFANSSON AKAJA NAKUSEMA UMECHELEWA HAUWEZI KUZUIA.
EP 65
TULIPOISHIA..
Ndipo Koga akasema huku akimtazama Pastor Stefansson usoni;
“Nataka nimtumikie yeye mpaka siku yangu ya mwisho, na kwakuthibisha ilo naanza na rafiki yangu mpya aliyenivumilia katika hali zote na ndio aliyenileta hapa mpaka saizi nimesimama hapa naonekana kama binadamu kumbe tayari nilikuwa ni mfu ambaye nasubiri kuzikwa”
“The walking Died”
(Maiti inayo tembea)
Basi Koga alipogusia habari ya rafiki yake wa karibu nikajua moja kwa moja ni Mimi, lakini nilishangaa maana…!!!
ENDELEA NAYO
Basi nikamuona Koga akiangaza angaza macho yake kwenye umati mkubwa wa watu pale Tanganyika Pekars, lakini hakuweza kuniona nadhani nikutokana na pindi nilipokuwa namleta alikuwa hajitambui kabisa kwaiyo hakujua Mimi nipo upande gani.
Basi ikabidi wale wahudumu wamuulize jina la uyo MTU yani Mimi akawaambia na hapo ndipo nikalisikia jina langu kwenye speaker kubwa likitajwa nakunitaka niende mbele.
Jofu, Jofu, rafiki wa Koga, tunakuomba uje mbele. Jofu tunaomba usogee hapa mbele.๐ฃ
Basi haraka nikasogea mpaka pale juu ya jukwaa, nikawa nimesimama pembeni kidogo ya Koga.. Basi Koga akawa ananitazama tu huku akibubujikwa na machozi yakutosha mpaka na Mimi nikashindwa kujizuia nikaanza kutokwa na machozi pia..!! Basi nikamfuata naye akawa ananifuata kisha wote kwa Pamoja tukakumbatiana huku tukilia..!!
Lakini katika hali yakushangaza nilijikuta nikianza kuungua vibaya sana..๐ฅMpaka ikabidi nimuachie ghafla Koga nakusogea pembeni huku nikimtazama kwa woga..!!๐ฎ
Ilo tukio kila mmoja alikuwa akilishuudia, Pastor Stefansson huku akitabasamu akasogea karibu kisha akaniwekea mikono kichwani kisha akasema;
“Kijana upo tayari kumpokea YESU awe bwana na mwokozi wako..??”
“Ndio nipo tayari kabisa”
“Sawa,naomba nifuatishe maneno aya, sema bwana YESU”
“Bwana YESU”
“Naja mbele zako”
“Naja mbele zako”
“Nisamehe Mimi mwenye dhambi”
“Nisamehe Mimi Mwenye dhambi”
“Nifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu, na uniandike kwenye kitabu cha watakatifu.!”
“AMEN”
“Basi sasa upo umefunguliwa nakuwa kiumbe kipya ambaye umepewa mamlaka yakukanya nyoka nakula vitu vyakufisha lakini hautodhulika, sasa waweza kumsalimu tu rafiki maana mwanzo wewe ulikuwa tofauti kabisa na uyu..maana yeye alikuwa ni nuru wakati uo wee ni Giza..!!”
Basi tukakumbatiana vizuri na Koga wangu kisha nikamsogerea Pastor Stefansson akatuambia;
“Kuweni tayari kesho tunaondoka pamoja kuelekea Canada ili muanze lasmi kazi ya MUNGU, kila kitu mtakikuta huko Ottawa
MUNGU awabariki sana!!”
“Kweli Pastor”
“Ndio kijana, maana roho mtakatifu ananishuudia nakunionyesha juu ya utumishi wenu kwa MUNGU hapo baadaye kwaiyo lazima nilisimamie ilo ili mtumike.”
“Tunashukuru sana Pastor.!”
Nilifurahi Sana huku nikiondoka zangu pamoja na Koga wangu kurudi nyumbani kwaajili ya maandalizi. Tulipewa Bible na baadhi ya vitabu vingine, Koga alikuwa akionekana Kama hataki ata kuondoka pale Tanganyika Pekars. Lakini Mimi nilimsihi kuwa anahitaji kuoga na apumzike maana kateseka sana mke wangu.
Tukafika kwa Dada yake koga..Mimi nikapita ndani moja kwa moja ambapo nilimuona Shemeji akiwa na rafiki zake wengine wakanikaribisha huku wakisema nimefika muda mzuri;
“Karibu Shemeji yangu Jofu, Shemeji wa ukweli Shemeji mwenye mapenzi ya dhati, aya niambie mzoga wako ukwapi maana ungekuwa umekuja nao hapa sidhani Kama pangekalika.”
Alivyoongea ivyo chumba chote wakaangua kicheko huku rafiki yao mmoja akisema;
“Lakini jamani sio vizuri ivyo mjue, kumbukeni kuna leo na kesho, alafu pia yule binti ni mwanamke mwenzetu sema ndio ivyo yamemkuta tu, alafu wewe yule ni Mdogo wako inamaana huoni ata aibu.!!”
Nilipoona ivyo sikutaka kusubiri mpaka waongee sana nilichofanya nikumwita tu Koga.
“Koga mpenzi naomba ingia ndani umsalimie Dada yako kwanza.!!”
Wote wakatumbua macho mlangoni kuangalia kama ni kweli au masihala.
Kila mmoja alipigwa na butwaa hakuamini anacho kiona mbele yake, Koga akasema;
“Usinishangae Dada, ni Mimi Koga, ni Mimi Mdogo wako, ila sio yule Koga unayemjua wewe, Mimi ni Koga Mpya kabisa, au waweza kuniita binti sayuni..!!”
Basi Dada akainuka nakuja kwangu, kisha akanikumbatia Kama alivyofanya Jofu pale jukwaani muda ule.!! Mara ghafla akaniachia huku akilalama kwa kusema;
“Uwiiiihh..wee Koga mbona una moto mwilini mwako wewe eeh!! Jamani.. Makubwa.!!”
Basi nikacheka kidogo kisha nikamwambia kwa sauti laini na ya unyenyekevu;
“Dada huu sio moto ila ni NGUVU za damu ya YESU, ndio zinafanya uone Kama nina moto. Na pia Mimi ni nuru na wewe ni giza hatuwezi
Kukaa mahali Pamoja.!!”
Basi wakabaki kunishangaa tu jinsi nilivyo na Mimi nilikuwa nikiwashangaa jinsi walivyo maana nilikuwa nikiwaonea huruma sana.
Nikaenda kuoga niliporudi Dada alikuwa tayari kaanda Chakula na wale rafiki zake walishaondoka, basi tukiwa kwenye Chakula ndipo nikaanza kumwambia Dada juu uponywaji wangu na nikamshuudia juu ya uyu MTU wa Ajabu aitwaye YESU, kuwa ata yeye akimpokea atambadilisha nakumfanya kuwa kiumbe kipya kabisa. Dada alikuwa akinisikiliza kwa umakini sana, na nilipomaliza ndipo Jofu akamwambia;
“Alafu Dada Kama MUNGU akipenda kesho tunaanza safari kuelekea nchini Canada.”
Dada akastaajabu akauliza tena kana kwamba hajasikia nilichomwambia.
“Unasemaje Jofu..!!?”
Ikabidi nimjibu Mimi maana nikaona Kama Jofu akimwambia hamuelewi vizuri.
“Nasema ivi Kama MUNGU akiwa upande wetu kesho tunaaza safari ya kuelekea nchini Canada, Pamoja na Mtumishi wa MUNGU Pastor Stefansson!, na tunaenda wote Mimi na Jofu na tutakuwa huko kimaisha na tutakuwa tukimtumikia MUNGU muda wote Kama wainjilist mpaka pale tutakapo itwa nakupewa malipo yetu au kupewa mavuno ya tulicho kipanda, maana imeandikwa kuwa “Kwa muda usio dhani utavuna ulichopanda, kama umepanda mema hakika utavuna mema.!!”
Nilipomaliza kuongea nikamuona Shemeji akitoka CHUMBANI, sikufikiri kama atakuwepo hapa ndani basi akamgeukia Jofu nakuanza kumwambia kwa mtindo wakuuliza;
“Wee Jofu ivi unaelewa anachozughumza uyu mkeo, maana anaongea vitu ambavyo havipo kabisa maana nasikia Mara Canada Mara sijui kulipwa na MUNGU, kwakweli Mdogo wangu kapona ila nahisi akili zake bado hazipo sawa.!”
Kwanza nilimshangaa Sana Shemeji yangu kwa kuniona Mimi Mjinga na mpuuzi nadhani hajui nani kaniponya, ila kabla Jofu hajamjibu chochote Shemeji nikamkatisha kwa kusema..!!
Nini tena kimetokea jamani
INAENDELEA


